DADA MDUNGUWAJI
Episode 2
STORY NA Mbogo Edgar
ILIPOISHIA SEHEMU YA TANO : “yap! natakatuanze safari siku tatu zijazo” hapo Anitha akapiga magoti karibu na ngozi yake ya kulalia, akaifunua akatoa ubao, akifuatia silaha yake SMG, na mwisho akatoa lile beg la ngozi akaliweka juu, kisha akafungua, ndani “ona hii Michael, utapenda twende nayo Tanzania?” aliongea Anitha huku akiwa amelitanuwa lile begi, Michael akachungulia ndani ya beg, alichokiona ndani ya begi nusu Michael azimie : endelea...
kwa mshangao wa furaha, ya likuwa madini ya almas na dhahabu nyingi sana, ni mala dufu ya zile za kwake, tofauti ni kwamba, hizi zilikuwa ni vipande vidogo vidogo, kama punje za maindi, *** kumbe baba yake Anitha alikuwa na uwezo mkubwa kifedha, akiishi mitaa ya vilunga nyuma ya soko kuu la mjini Goma, shuguli zake zilikuwa ni kununua madini nakwenda kuyauza nchi Rwanda, siku waliyopoteana na mwanae Anitha, ilikuwa ni kutokana na vita, anitha alikuwa ametoka shule, akuwakuta ndugu zake nyumbani, kuanzia baba mama na wadogo zake, ata mda mfupi baadae mapigano ya lipoanza, alichukua ilo begi na kuweka nguo zake chache, pasipo kujuwa kuna madini ndani yake, alitembea nalo mpaka alipo fika huku porini ndipo alipo gunduwa uwepo way ale mawe kwenye begi lake, akuwaambia wenzake juu yay ale mawe ya kyng’aa, sababu akujuwa yale mawe yakung’aa yana maana gani, ila alishawai kusikia hadithi yamawe yenye thamani, ndipo alipo chimba shimo ndani ya kibanda chake alicho jengewa na wenzake, na kuliweka beg lake na silaha yake, huku juu yake akifanya kuwa ni sehemu ya kulala, alibaki na sir yake mpaka akaja kutambua umuhimu wake, siku alipo yaona yakitaka kusababisha kifo cha Michael, kule juu alipo pigwa risasi na watanzania wenzake, *****
Michael alimkumbatia Anitha na kumbusu mdomoni, kisha akamwambia “tutaishi maisha mazuri sana tukifika Tanzania, naimani wazazi wako na ndugu zako utawaona tena, na kuwasaidia, ama ulivyo panga” hapo Anitha alifurahi kusikia vile, *** siku yatatu Michael na Anitha walikuwa wamesha jiandaa tayari kwa safari, walibeba chakula, nyama porini ya swala iliyo banikwa na kukauka vizuri, pia maji ya kunywa ya kutosha, Anitha aliwaaga wale watoto wamama mtu mzima pamoja na mama yao, pia akawaaga wale dada zake ambao walimsaidia kufika kule porini, akiwa ahidi kurudi kuwasaidia pindi maisha yake yakiwa mazuri, Michael pia alifanya hivyo, wakiwa wamezifungua silaha zao, na kuzitenganisha vipande vipande, na kuzi weka kwenye begi kubwa, Michael na Anitha waliazimwa Smg na wale wanawake waliobaki, kwa ajiri ya kutembelea msituni kipindi wakitafuta mji ulipo, wao wakibaki na smg moja safari ikaanza wakisindikizwa na wale vijana watatu, ambao wangerudi na siraha, walitembea usiku kucha, wakiwa wamevaa nguo zilizo chakaa Michael ili kufanana na wakzi wa maeneo wanayo pita, alipewa na wenyeji wake, alfajili walitokea kwenye kitongoji cha kanyaluchina, kupitia mirima ya Muja, walikuta vita ikiendelea, upande wa goma mjini, kuanzia bhilele kuelekea Tsake na m’bambilo, na kusababisha upande huu wa kanaluchina kujae watu wanao kimbia vita, wakielekea lutchuru mpaka bunagana, kuingia Rwanda au Uganda, pia wapo walioishia kibumba na kuingia Rwanda, wakitumia usafiri wa magari makubwa ya mizigo ila wengi wao wakitembea kwa miguu au baiskeri za miti, maharufu kama chukudu, lakini walisema mpaka wa Rwanda kutokea kibumba ni vigumu kupita kutokana na vikundi vidogo vya wahasi wa maimai, kukalia maeneo hayo, Michael na Anitha waliagana na wale jamaa zao, huku Michael akiwapatia faranga elfu ishirini wanunue mahitaji yao yakule porini kwenye maduka machache yaliyokuwa wazi pale kanaluchina, wale jamaa walishukuru sana wakiwasisitiza Anitha na Michael, kuwakumbuka pindi watakapo kuwa wamefika na kutulia Tanzania, atimae wakatengana wakiwakabidhi silaha zao, huku wakina Michael wakijichanganya kwenye makundi ya wakimbizi, waliokuwa wamebeba mizigo mikubwa, huku wengine wakiwa na mifugo yao, na safari ikaanza. ****
<
Jioni ya kwanza iliwakuta kibumba, wakipita kibhati Kilima nyoka na minara mitatu, wakapumzika kwa masaa matatu saa nne usiku walibadiri nguo zao na kuvaa nguo za kijeshi, ambazo Michael alikuwa nazo pea mbili, moja akampatia Anitha ambae zilimtosha vyema chini akamvalisha rubber, nazo zilimtosha, wakaanza safari awamu ya pili, tofauti na mchana usiku huu awakutumia barabara, walipitia porini kwa msaada wa ramani waliyokuwanayo, walitembea adi juwa lilipo chomoza wakabadiri nguo tena, na kuvaa zile chakavu kisha wakatokea barabarani na kujiunga na makundi ya wakimbizi, walitembe kwa masaa mawili, wakawa wamefika lutchuru, wakaihacha njia ya kuelekea mbuga ya virunga mpaka ruwindi na butembo, wakaingia kulia kuelekea bunagana, hapo walitumia masaa mawili, kuingia bunagana na kusogea kwenye mpaka wa congo na uganda, hapo wakakuta makundi mengi ya wakimbizi, wakijaribu kuvuka mpaka, ukaguzi ulikuwa mkari, askari wajeshi na polisi wa uganda, walisimamia kuakikisha watu awavuki na silaha au kitu chochote kibaya, wakati mwingine askari hao uwapola vitu vyao vya thamani, hapo Michael akatumia akiri ya kuzaliwa nayo, kwanza akajitoa kwenye kwenye kundi kubwa la wakimbizi yeye na Anitha, akaya fwata magari ya umoja wa mataifa yaliyo kuwa yamepaki pembeni, mengine yakisubiri kuvuka na mengine yakishusha wakimbizi au misaada ya chakula na mavazi, akaongea na dereva wa gari moja ambalo lilikuwa lina taka kuvuka, likirudi toka kupeleka misaada ya chakula na dawa, ****
Nusu saa baadae walivuka wakiwa ndani ya gari la umoja wa mataifa yani UN, na sale za kijeshi, lile gari lili wapeleka mpaka kampala, ambapo walinunua nguo nzuri za kiraia na kuzivaa, wakamlipa yule jamaa wa UN fendha walizo kubaliana kisha yule jamaa akaondoka na gari lake, na wao wakaenda barabara kuu iendayo Kenya mpaka Tanzania, jioni walifanikiwa kupata gari kubwa la mizigo linaloenda bandari ya dar es salaam kuchukuwa mizigo ya misaada ya wakimbizi, siku hiyo walilala mpakani mwa Uganda na Kenya, siku yapili walilala Arusha Tanzania, wakiachana na lile gari kubwa la mizigo, siku hiyo walillala usingizi mzito mzito nusu kifo, kwenye hotel moja ya kawaida tu, siku ya pili wakapanda basi kuelekea dar es salaam, walitumia masaa kumi kufika dar es salaam (enzi hizo barabara haikuwa nzuri sana) moja kwamoja walishukia kimara na kutafuta nyumba ya wageni, wakachukua chumba na kupumzika, japo mida flani walienda kukaa sehemu ya chakula na vinywaji, walipo maliza kula waliagiza vinywaji, Michael akiagiza pombe, na kuanza kunywa huu wakioonyesha uchangamfu, kwa furaha walizokuwa nazo, ni baada ya miezi sita ya kunusulika kifo, akanywa bia, huku Anitha na ye akijarbu kunywa, ambae muda wote alikuwa akitabasamu kama kawaida yake, japo alionekana kuwa mchovu, kutokana na safari yao ngumu yasiku kadhaa, Anitha alishangaa kuona jinsi watanzania wanavyoishi kwa amani na furaha, kule kwao pengine ata siku ya siku kuu usingeona watu wakikaa kwenye bar mpaka saa mbili, usiku
Pombe ilisha mchukua Anitha, japo alikuwa amekunywa kidogo sana, ilikuwa ni mala yake ya kwanza, usiku ule waliutumia vizuri sana kuburudisha miili yao, maana jana yake awakuweza kufanya mapenzi kutokana na uchovu wasafari, *** Asubuhi siku yapili, Michael alimwacha Anitha pale nyumba ya wageni akaanza kuwasaka wabaya wake wakina Masinde, alianzia kwenye kikosi maalumu cha kazi za siri, akaenda na kukaa kwenye mgahawa ulipo jirani na kambi hilo akiangalia wanaoingia na kutoka, pengine angemuona ata mmoja wa askari, ambao alikuwa nao nchini Congo, wakati huo Michael alikuwa amebeba kisu chake kikali cha kijeshi, akiamini kingetosha kutekeleza mauaji, aliyokusudia kwa wabaya wake, kwani alijuwa kati ya adui zake, hakuna ambae angeweza kumzidi uwezo wa kimapigano, Michael alikaa hapo kwa masaa matatu, adi ilipo timia saa nne za asubuhi, lakini hakumwona mtu yoyote kati ya maadui zake, aliogopa kwenda ofisini kwani akujuwa ametolewa taalifa gani na wale wenzake, akapitisha uamuzi wa kwenda kutafuta kibanda cha simu, alipiga simu ikapokelewa “hallow brigade gen Soud hapa, nikusaidie tafadhari” Michael aliitambua sauti ya mkuu wake Soud Hassan, lakini akasita kujitambulisha, “naitwa Sam na mwulizia rafiki yangu Michael Nyati” alidanganya Michael ilikujuwa kama wanafahamu nini juu yake, bahati nzuri brg Soud alifunguka mwanzo mwisho, akimweleza pasipo kujuwa kuwa anaongea na Michael, kuwa Michael ameandikwa kama mtoro jeshini, sababu amewakimbia wenzake wakiwa kwenye kazi nje ya nchi, hivyo akipatikana atoe taharifa ili akakamatwe, pia Michael akaulizia juu ya wale maadui zake akaambiwa walihacha kazi baada tu! ya kurudi toka likizo waliyo pewa baada ya kumaliza mission huko congo, Mchael akarudi hotelini akiwa amejawa na mawazo, ya kuwakosa maadui zake, lakini akuwa na jinsi,**** baada ya kukata simu ambayo alikuwa akiongea na mtu asiye mfahamu aliye jitambulisha kuwa ni rafiki wa kijana mpotevu Michael Fransis Nyati, brig Gen Soud Hassan, alistuka kidogo na kufikilia jambo, kakumbuka jambo moja kuwa ile sauti ya mtu ambae ametoka kuongea nae, ni sauti inayofanana kabisa na sauti ya askari wake Michael Nyati, hapo mzee soudy akagunduwa kuwa kunajambo zito nyuma ya panzia, ambalo lingeleta mahafa kwa siku za hivi karibuni, na kwa jinsi anavyo mjuwa kijana Michael, ni mtu mwenye kutumia akili nyingi sana kwenye mambo yake, hapo bwan Soud akapiga simu nyumbani kwa bwana Masinde ndie pekee ambae alikuwa na namba zake za simu yake ya nyumbani, simu ile ilipokelewa na mtoto wa bwana Masinde, “hallow shikamoo,” ilikuwa ni sauti a mtoto Johnson, mwenemiaka mine, “malahaba John, mpe simu baba niongee nae,” bwana Soud alimfahau sana huyu mtoto, kwakuwa siku zote anavyo piga simu lazima apokee kwanza ndipo ampatie baba yake, ni kweli baada ya sekunde chache bwana masinde akawa amesha shika simu, brg Gen Soud akaongea na bwana Masinde akimsimulia kile alicho kihisi kuwa, ni ni kuongea na kijana ni Michael Nyati, akamwuliza kama kuna jambo lolote lililo jificha juu ya kupotea kwa kijana huyo nchini congo, lakini bwana Masinde ambae kwa sasa, maisha yake yalikuwa mazuri zaidi ya kipindi akiwa mwanajeshi, alikataa kabisa kutokea jamb lolote zaidi ya kijana huyo kutoweka katika namna ya kushangaza, baada ya kukosa alicho tarajia bwana Soud alikata simu na kubaki akivuta picha yakile kitakacho tokea siku za usoni, mwasho wasiku brig gen Soudy akajikuta akitabasamu, huku akijisemea peke yake, “sasa watavuna walicho panda” **** huku nako Michael na Anitha walifaya mipango ya kuuza vipande viwili vya almas, ambapo walijipatia milioni mia tatu, kwa kipindi hicho, nifedha nyingi sana, ambazo ungefananisha na billion tatu kwa sasa, akanunua gari moja aina ya land rover 110 wagon, na vitu vingi sana vya kuwasaidia huko wanakoenda, pia wakanunua pamoja na mavazi yao, safari ya songea kwa wazazi wa Michael ikaanza, wazazi wa Michael awakuwai kupata tahalifa ya kupotea kwa Michael, hivyo awakushangaa kumuona Michael akirudi nyumbani, kilicho wastua nikuja na mwanamke mwenye rafudhi ya congo pia mandevu na nywele nyingi sana, mwisho aliwaambia kuwa, ameamua kuhacha kazi yajeshi, huku akiwataka wazazi wake wasimwambie mtu yoyote, uwepo wake pale songea, wakiulizwa waambiwe awajuwi,
Michaeli alinunua eneo kubwa sana nje yamji, na kujenga nyumba moja kubwa sana yenye gorofa mbili, akiuacha msitu mkubwa ukizunguka nyumba hiyo, alifungua kiwanda cha kutegeneza wine itokanayo na matunda yaasiri, akawaajiri watu, waifanye kazi hiyo, akaongeza magari mengine matatu na trector mbili kwaajili yakilimo akaweka mifugo mingi sana yakila aina, ndani yamiakamiwili alikuwa amesha wasaidia wale rafikizake wacongo, ambao aliwasafirisha kwenda Kinshasa kutoka kule porini nakuwawezesha fedha nyingi zakufanyia bihashara, pia alifanikiwa kuipata familia ya akina Anitha waliyoikuta kwenye kambi ya waimbizi ya ngara Tanzania wakawatoa nakuwasafirisha afrika ya kusini wakimpatia mzee madini baadhi na fedha za kuanzia, wote waliahidi kumtembelea wapatapo nafasi , *****Ilikuwa imesha pita miaka miwili toka tukio la kupigwa risasi Michael kwenye misitu ya congo litokee, ilikuwa ni mwaka 1990 mwezi wa sita, Anitha alijifungua mtoto wakwanza wakike, siku hiyo Michael alikuwa kwenye bechi la hospital ya mkoa wa Ruvuma akijaribu kusoma gazeti la mzalendo, lakini mawazo ayakuwepo pale kabisa, aliwaza jinsi atakavyo mshika mwanae wa kwanza baada ya kutoka chumba cha kujifungulia, Michael akuweza kulisoma lile gazeti kabisa, akalikunja na kulishika mkononi, muda mchache baadae walikuwa wamemaliza taratibu za hospital na kuanza kuelekea nyumbani, tabia yake ya kutabasamu kila mala, bado alikuwa nayo Anitha, ambaye uzuri wake ulizidi mala dufu, na kiswahili chake kilianza kuwa safi, japo kuna maeno bado aliyatamka kwa rafudhi ya ki congo,
Walianza maisha mapya wakiwa baba na mama Jackline, zilisha pita siku saba toka Anitha ajifungue, siku hiyo Michael akiwa anaweka vitu vyake sawa kwenye gari lake 110, akaliona lile gazeti la mzalendo, ambalo alishindwa kulisoma siku ile, ambayo mke wake alikuwa anajifungua, akalichukuwa na kulitazama, macho yake yaligonga kwenye picha moja juu ya ukurasa wa kwanza kabisa wa gazeti hilo, akalishika na kulikunjua vizuri, maana alivutiwa na picha ile, Michael Nyati au baba Jack aliona picha moja ya mchungaji wakanisa flani, akiwa amezungukwa na waumini, sura ya yule mchungaji ndiyo iliyo mvutia Michael, kichwa cha habari kiliandikwa “mch Chilumba kuanza kuponya wagonjwa” Michael akatabasamu, nitabasamu la uchungu, na kuufanya uso wake ufanane na simba anayepiga muhayo, akalichukua gazeti na kuinganalo ndani ya nyumba na kukaa sebuleni, sambamaba na mke wake Anitha, ambae alikuwa amemlaza mtoto kwenye kochi, akaanza kuisoma ile habari kwa kina, aligundua kuwa mteule daraja la pili Chilumba, ambae ni moja kati ya wale askari walio mwacha mstni congo, baada ya kuhacha kazi ameamua kufungua kanisa, maeneo ya buguruni rozana, hapo Michael akamtazama mwanae ambae Jackline alikuwa
amelazwa juu ya kochi, pembeni ya mama yake, akatikisa kichwa kuafiki jambo flani, huku akiachia tabasamu lake kama lile la nje, lililo mshangaza Anitha, “wewe mbona unatabasamu hivyo” aliuliza Anitha kwamshangao, maana akuwai kumwona mume wake akiwa katika hali kama hiyo “wamekwisha, washenzi, atimae nimewakamata” aliongea Michael akimwonyesha picha gazetini, *** “nazani mpaka hapo umeanza kuelewa Denis?” aliliza Jaclene Michael Nyati, ambae ndie mama Fransis, mke wa kijana Denis, huku uso wake ukiwa umetawalliwa na tabasamu, “nimeanza kuelewa, lakini ilikuwaje uwe mama ntilie, wakati baba yako ni mtu mwenye fedha nyingi kiasi hiki?” aliuliza Denis kwa sauti ya chini, akimtazama mkewake kwa umakini huku akili yake ikikataa kuwa mke wake ndie ametekeleza mauwaji hayo ambayo yamelitikisa jiji la dar kwa miaka mingi, “ndio tunakuja huko mume wangu, wala husiwe na haraka” alijibu Jackline kwa sauti laini na tulivu, kisha Jackline Michael Nyati akaendelea, “nazani unakumbuka sikuile tulipo kutana pale pale manzese?” alisema Jack na Denis akakubali kwa kichwa.
Mwaka 2004 mwezi wa saba, saa nne asubuhi mitaa ya manzese, Denis na rafiki yake Mahadhi walikuwa wanawai supu kwenye mgahawa wakaribu na jengo la ofisi yao, iliyopo kwenye jengo la ghorofa nane, linalojulikana kama Mazao building, ambalo limepangishwa na wafanya biashara wengi wengi, ambao waliweka ofisi zao, wakati Denis na Mahadhi wanaingia pale mgahawani, walipishana na watu wengi sana, waliokuwa wanatoka ndani ya mgahawa wakiwawamesha pata kufungua kinywa, “bwana heee! kwa hiyo sehemeji akamaind” aliuliza Denis, wakati wanatembea kuelekea kwenye mgahawa, “moto uliwaka si kidogo, yani leo nataka nirudi mapema kidogo” aliongea Mahadhi akijaribu kuonyesha jinsi gani mke wake alichukia sana usiku uliopita, “tatizo siyo kuchelewa kurudi, tatizo uzinzi” alisema Denis akimsema rafiki yake Mahadhi, lakini ile kutahamaki, Denis alijikuta mkono wake ukigongwa na kitu kizito, nakigumu kama chuma, aligeuka na kutazama kitu hicho kilicho mgonga, hakuona kitu zaidi ya kwamba alikuwa amengonga kibegi kidogo cheusi, kilicho bebwa na mwanamke mmoja, ambae alimwona tokea mgongoni, ambae alitembea atuwa chache kisha yule mwanamke akageuza sura yake na kumtazama kidogo kisha akaendelea nasafari yake, alikuwa ni mzuri wa kuvutia, huku kwenye mkono wake mmoja, yule mwanamke alikuwa amebeba sahani moja iliyo funikwa, alionekana wazi kuwa anafanya kazi kwa mama bupe, huyo mama nimsimamizi wa ule mgahawa, ambao wakina Denis walikuwa wanaenda kupata chochote, Denis alitumia dakika chache kumtazama yule mwanamke, licha ya kumwangalia mgongoni akiwa katika mavazi la kimama ntilie, gauni refu na kanga chakavu aliyo jifunga kiunoni, lakini umbo lake lilionekana wazi jinsi alivyo kaa vizuri, Denis alibaki akimtazama yule dada, akipandisha kwenye jengo ambalo lina gorofa nane la Mazao building, humo ndani wamekodisha watu mbalimbali, ikiwemo ofisi ya kina Denis, inayo jiusisha na utengenezaji wa ramani za majengo na usimamizi wa ujenzi wa majengo makubwa, “hoyaa vipi tena” aliita Mahadhi baada ya kuona mwenzie ameganda
Muda mfupi baadae, walikuwa wame inamia bakuri zao za supu yakuku, wakifakamia, ukumaongezi yakiendelea, “bola mimi kuliko wewe, yani una penda pombe sijuwi zina faida gani kwako” alijitetea Mahadhi kutoka kwenye msimango ya Denis, “mh! bola uzinzi, wakati na pombe una kunywa, alafu nilisahau, basi jana nili piga mtungi mbaya, ile nafika home, si nika lala ndani ya gari” walicheka kwa pamoja wakisaidiwa na watu walio kaa nao karibu, ambao bahadhi yao wana wafahammu sana vjana awa marafiki, “ngoja pate mke, utabadirika tu!” aliongea Mahadhi akimalizia kicheko “Mahadhi hee! kwani wewe ugongi mtungi, tena shemji akiijuwa ile nyumba ndogo yako ya pale jirani yako, sijuwi utambebaje, unabahati simu nimeisahau kwenye gari, ninge kurecord uavyo bwabwaja alfu nimpelekee” wakati wanaendelea kuongea, mala wakasikia ving’ola vya police vikija upande wao, na kupitiliza kwenye jengo la pili, jirani na lile la kwao, kwa umbali wamita mia moja tu!, linaloitwa Kamanga Plaza, kwa mtaa hule palikuwa na majengo mawili tu! marefu, watu walitimua mbio kuelekea kule ambako magari ya polisi yalipoelekea, huku wakipiga kelele, Denis na Mahadhi walimaliza supu zao na kukimbilia kule walikoelekea wenzao, walijichanganya kwenye makundi ya watu ambao walizuiliwa na polisi wasizidi kusogea,
Yalikuwa ni mauaji yametokea, mchungaji maarufu Chilumba ameuwawa kwa risasi, ambayo inasadikiwa imepigwa na mdunguwaji, wazungu wanaita sniper, utumia silaha ya kulengea mbari, inayotumiwa na waduguaji wa kijeshi wenye mafunzo maalumu, polisi wakagundua pengine risasi imetokea upande wa kushoto wajengo lile inamaana kwenye gorofa lenye ofisi za kina Denis, sababu mzee Chilumba alipigwa kupitia dirisha la upende wa kulia wa jengo la KAMANGA PLAZA,
Wakiwa wanaendelea kushangaa juu ya tukio hilo geni kutokea katika jiji la Dar es salaam, Denis na Mahadhi wakamshuhudia polisi mmoja akiongea kwenye redio call “ hallow charle tango, akikisheni kila mtu anaetoka kwenye hilo jengo la Mazao, anasachiwa, na polisi wengine waingie nadani ya jengo, wafanye msako wa nguvu, umenipata over” kisha ikasikika sauti toka kwenye redio call yake “hallow charle papaa, nimekupata, na sasa askari wamesha zuwia mlango mkuu wakutokea, na wengine wameingia ndani wanaedelea na msako, over” kisha yule polisi akaongea tena, “Charle Tango, target ni silaha kubwa yakijeshi, umenipata over?” hapo ikasikika tena sauti toka kwenye redio, “nimekupata vizuri kabisa over” hapo Denis akakumbuka kitu, “mahadhi, ngoja niende kwenye gari nikachukuwe simu yangu, tutafute pozi nitoe lock, maana ofisini apaingiliki tena” aliongea Denis na kuelekea lilipo jengo la Mazao ambalo lina ofisi yao, huku moyoni mwake afurahia tukio hilo, maana atakuwa amepata mda wa kwenda kunywa pombe, Denis alipo lisogelea jengo lile, aliona mlango mkubwa wakuingilia, ukiwa umezungukwa na polisi wengi sana, yeye akaelekea kwenye gari lake kisha akazunguka upande wa siti ya abiria wambele, na kufungua mlango, alafu aka ingiza mkono kwenye mfuko ambao ulikuwepo kwenye ile siti, akaibuka na bia moja ya kopo, akatazamakushoto na kulia bila kuona mtu , akaifungua na kuanza kuinywa ile bia, kwa kuigugumia, yani gudu gudu, alitumia kama sekunde tano hivi mpaka kuishusha ile bia ikiwa nusu, akatazama tena kushoto na kulia akuona mtu, akaiweka tena bia ake mdomoni lakini safari hii kabala ajapiga ata funda mbili, akasikia “paaaaa” ikifwatia na sauti ya vioo kudondoka chini, hapo Denis akastuka na kutazama upande wa kulia wa gari lake, hapo Denis alimwona yule dada mzuri mwenye umbo lakuvutia, mama ntilie akiwa anaishangaa side mirror ya gari lake, (kioo cha kutazamia nyuma) ambacho kilikuwa kimevunjika, na yeye akiwa ndie mvunjaji, na alikivunja bahati mbaya, baada ya kugonga na lile begi lake jeusi , Denis aliuma meno kwa hasira, huku akishika kichwa “samahani ni bahati mbaya” aliongea yule dada mama ntilie kwa sauti nzuri ya upole, lakini Denis alibaki ameduwaa kama aliepigwa na butwaha, “ nibahati mbaya kaka yangu, ni bei gani nikulipe?“ aliongea yule dada akionyesha mwenye wasiwasi sana, lakini kiukweli akufanana na uwezo wakulipa ile side mirror “we! nenda tu dada, si umeshasema ni bahati mbaya” Denis aliongea kwa sauti ya upole sana, bia yake mkononi, huku anazunguka kwenda kutazama palipo vunjika, alikuta kioo chote kipo chini, kanamba kimegongwa na kitu kizito sana, hapo Denis akashangaa na kuinia ,acho kumtazama yule dada, kitu cha kushangaza akumwona tena yule dada mama ntilie
Denis akajaribu kusunguka huku nahuku mahali pale lakini akumwona, akarudi kwenye gari lake akachukuwa simu yake na kumtafuta rafiki yake Mahadhi, kisha akamsimulia juu ya yule dada mrembo mama ntilie mwenye begi dogo jeusi, jinsi alivyo mgonga pale mgahawani na alivyo vunja side mirror, dakika chache zilizopita “yani kaka nimeshindwa la kufanya, ni mtoto wa nguvu, sijawai kuona mama ntilie mzuri kama yule” alimwaga sifa Denis “hahahahaha kweli hicho kitakuwa chombo, mpaka wewe umesema hivyo?, ebu nika kione” aliongea Mahadhi kwa kejeri “ametoweka ghafla, nambaya zaidi sijawai kumwona siku za nyuma” Denis aliongea akionyesha kuchachawa na huyo mwanamke “labda atakuwa mgeni pale kwamama bupe” kweli twende tuka mwangalie mgahawani” waliongea hayo wakiwa wamesimama mbele ya jengo lao, pamoja na wananchi wengine wakishangaa juu ya mauwaji yaliyo tokea, ambapo polisi hawakupata chochote, muuwaji alisha toroka, licha yakuangaika kwa masaa manne wakikagua kila mtu aliekuwepo mle ndani, lilikuja gari la wagonjwa nakubeba mwili wa marehemu, likisindikizwa na magari ya polisi, **** Yule dada mama ntilie alikuwa amesimama kwenye duka moja pembeni ya mgahawa, akijiunga nawatu wengine wengi, walio kuwa wamekaa pale akishangaa tukio la kuuwawa kwa mchungaji maharufu Chilumba, akiwa anatazama polisi wakiondoka eneo lile, mala akamwona kijana alie mvunjia kioo cha gari lake akiwa na mwenzie wakija upande aliopo, huku wakiongea jambo flani kwa msisitizo, wakaingia kwenye mgahawa, awakukaa muda mrefu wakatoka, wakaangalia huku nahuku, kisha waka sogea pale dukani wakasimama kwenye kundi lawatu, jirani kabisa na huyu dada mama ntilie lakini awakumwona, sababu alipowaona wakimsogelea akajificha akijibanza kwa watu wengine, walio kuwa wamesimama eneo lile, na aliwasikia kwa ukaribu wale vijana wawili wamkizungumzia, “ni kitu cha ukweli kaka” aliongea yule aliemvunjia kioo chagari, mwenzie akamwuliza “sasa unamtafuta wanini au unataka akulipe side mirror yako?” “hapana yani ata akitaka gari lote nitampatia, nimzuri huyo mwanamke sija pata kuona” aliongea mwenye kuvunjiwa kioo akifwatiwa nakicheko cha yule mwenzie, “manemno ya yule kijana yalimstua dada mama n’tilie, japo alisha wai kusikia vijana wengi wakitoa ahadi kama zile, juu yake lakini huyu alizidisha, na mbaya zaidi alionekana kuwa yupo makini na anacho kisema, kwamba akuwa na utani “yani wewe kweli pimbi, yule Jen wa ofisini amejipendekeza weeee, umemwacha, alafu eti una angaika kwa mama ntilie, usie mjuwa” waliongea wale vijana wakianza kuondoka eneo lile kuelekea ofisini ambako walitoka masaa manne yaliyopita wakienda kwenye chai, ndipo yule dada mama n’tilie alipo achia tabasamu dogo, huku nayeye akiondoka zake na kuvuka barabara kuelekea upande wa pili, huku moyoni mwake akiwaza tabia yake ya kuchukia wanaume wanaodai kuwa
mwambia anampenda ndie adui yake wakwanza, endelea ...
alipovuka barara, yule dada akanyoosha moja kwa moja, aiingia ndani ya mitaa ya Manzese akiipita bar moja kubwa sana ya Jambo pub, iliyopo mita chache kabisa toka barabarani, akaingia mtaa wapili, na safari yake iaishaia kwenye bar moja yenye guest house, yenye hadhi ya kawaida, inayoitwa Mapambano, akaingia ndani upande wa vyumba, “hoo! dada umerudi, vipi mambo?” alipokelewa kwa shangwe na muhudumu wa vyumba, “safi dada yangu, za tangu jana?” alijibu dada mama ntilie, huku aki mtazama kwa tabasamu yule dada mhudumu, ambae alimpokea siku iliyopita, yani jana jioni, alipo ingia hapa na kuchukua chumba “za tangu jana poa kabisa, sema kuna yule jamaa uliekuwa anakusemesha jana usiku, ukamchunia amenipa ujumbe wako”aliongea yule dada muhudumu wa vyumba “mh! kwani ananifahamu? We! hachana naye” alijibu yule dada mama n’tilie na kuanza kuondoka, kuelekea kwenye chumba chake, “sikia we!dada usipoteze bahati yako, yule mkaka anafedha nyingi, hacha ufala utakufa nanjaa mjini hapa” hapo dada mama n’tilie akasimama nakugeuka nyuma, akarudi alipo yule dada mhudumu “nazani atawewe una itaji hizo fedha, nivyema ukampatia anachoitaji, ili akupatie hizo fedha, wewe mweye shida nazo” aliongea mama ntilie kwa sauti ya chini, akimalizia kwa tabasamu laini, na kuondoka zake kuelekea chumbani kwake, akimwacha yule dada amekunja sura kwa ghazab, akiona kabisa kuwa yule mschana ambae kwamanekano ni mrembo na mzuri wa haja, lakini ni fukara sana, kwa nguo alizo vaa, baada ya kuingia kule chumbani dada mama ntilie, alifunga mlango kwa ufunguo, akaanza kuivua ile kanga yake aliyo jifunga kiunoni, akifwatia lile gauni refu, ambalo siku izi wanaita dela, akabaki na kikaptula kifupi cha jinsi na tishet la rangi nyeusi, ambacho kilikuwa kimemkaa vyema na kutokana na mahips yake na makalio yake makubwa kiasi, akafungua mkanda alio valia kile kikaptula, akiruhusu bastora yenye kiwamba sauti (silence baler) na kisu kikiwa kwenye kifuko chake, alivyo vining’niza kiunoni kwa msaada wa mkanda mgumu wa ngozi, kuweza kutoka na kuweka pembeni, akamalizia kuvua nguo zilizobaki akimalizia ile ndogo kabisa ya ndani, kisha akaingia bafuni akaoga, alipomaliza, akajiweka sawa akavalia gauni lake jingine linalofana na lile la mwanzo, ndani akitanguliza nguo ka mazile alizo vaa mwazo, kikaptula cha jinsi na tishert, akiwa amenig’iniza bastora na kisu, kwenye kaptura ya jinsi ikifichwa na gauni refu, akatoka na kufunga mlango wake kwa nje, kisha akaenda upande wa bar ambapo panauzwa chakula, wakati anakula alikuwa akiangalia tv iliyopo mahari pale, akiwa na watu wengi wakipata chakula pi, na wengine wakinywa pombe, kuna habari ilikuwa ikitangazwa kwenye TV, ni kuhusu mauwaji ya mchungaji mmoja maharufu sana, wakanisa moja la kilokole, lilopo buguruni, mama ntilie alipomaliza kula akainuka na kuanza kurudi ndani, akiwa anaelekea ndani upande wa vyumba, akisindikizwa na macho ya wanaume wakwale, mama ntilie alipo tazama kwenye kona moja pale sehemu ya kupata vinywaji na chakula, alimwona yule mhudumu wa vyumba akiwa na kijana mmoja, alimkumbuka mala moja kuwa, ni yule ambae jana yake alikuwa akimtaka kimapenzi, lakini leo kulikuwa kuna utofauti kdogo, tofauti ni kwamba aliwaona wakiongea huku wakimtazama, na yule mhudumu akionyesha kutahaluki na kusisitiza jambo, yule dada mama n’tilie alitabasamu, kwani alikuwa amesha hisi jambo flani, na kuelekea chumbani kwake, akiwa amehisi kuwa kile kikao si’salama kwake, *****
Huyu dada anaitwa Jackline Michael Nyati, binti mrembo hatari wa mzee Michael Nyati na mke wake Anitha, miaka mingi iliyopita, baadaya Jackline kutimiza miaka mitano Michael alianza kumtengenezea mazingira yakupenda ngumi na sarakasi mwanae mdogo wakike Jackline, ikiwa pamoja na mazoezi ya pumzi na viungo, na kupita kwenye sehemu zenye vikwazo, adi anafikisha miaka kumi akiwa darasa la nne, alikuwa na uwezomkubwa sana wa kupigana, katika shule aliyo kuwa anasoma, akuna mwanafunzi aliweza kumpiga, awe wakike au wakiume, ni kuanzia mwanafunzi wa darasa la kwanza, Jackline mpaka darasa la saba, mpaka anamaliza darasa la saba, baba yake alisha wai kuitwa mala nyingi sana shuleni, akienda kujibu mashitaka ya kupiga wenzake, Jackline aliyafanya hayo akiwa ni mschana, mwenye sura nzuri na ya upole, pia mwili wake ulikuwa wakuvutia, katika kumbu kumbu chache, akiwa kidato cha pili shule ya wanawake songea, kuna siku walienda kushiriki michezo baina ya shule zote za songea mjini, siku hiyo, ilikuwa ina cheza shule ya songea wavulana na ruvuma sekondali, baada ya michezo kumalizika, binti huyu alishika njia ya kuelekea kwao, kumbuka Michael Nyati alijenga nje kidogo ya mji, hivyo ilimlazimu Jackline kutembea kamwendo kidogo kabla ya kufika nyumbani akivuka vichaka na mapori, pasipo kujuwa ili wala lile, jackline alichapa mwendo, kumbe kuna wanafunzi wa shule ya Songea wavulana wa kidato cha nne, walitangulia nakujificha, wakiwa na uakika kuwa Jackline lazima atapita tu! vijana hawa ni Festo, Kadoda na Majaliwa, vijana hawa walikuwa ni wakolofi sana, na walikuwa wanafahamika kwa ukolofi wao, kesinyingi zilisha fika adi polisi, lakini wazazi wao walinde na kuwatoa vijana wao kuwa kesi za wanfunzi zitafikaje polisi, nawakati mwingine kutokana na uwezo wakifedha na madalaka ya wazazi wao polisi walikataa ata kwenda kuwakamata, maana hawakuchelea kupiga simu kwa staff offcer au RPC kulaumu kukamwatwa kwa watoto wao, nale vijana hawa watukutu walikuwa wamepania kumbaka binti huyu, licha ya kusikia kuwa ni hatari, kwenye mapigano lakini wali amini wao watatu ndio bala zaidi kuliko mwanamke mmoja, waliamini wangefanikiwa walichokusudia, kweli bwana dakika chache wali mwona bint akija kwamwendo wa speed japo alikuwa anatembea, lakini alitembea kwa nguvu sana, ndipo walipo jitokeza barabarani, wawili mbele mmoja nyuma, kumbuka sehemu hiyo ina umbali wa kama km tatu toka mtaani na km moja kufika kwao wakina Jackline, "sasa kwahiyali yako, tuingie pitino tumalizane, vinginevyo utajuta kuwa mzuri hivyo" aliongea Kadoda ambae alionekana ni mkorofi kuliko wote, kitu cha kushangaza binti huyu hakuonyesha wasiwasi wowote zaidi alitabasamu na kuwauliza, "hivi nyie, mkisema mkimbie, mtakimbilia wapi hapa?" Wote wakashangaa wakatazama pande zote, wakizani labda kuna mtu mwingine eneo lile ambaye anampa kiburi binti huyu, awakuona ta dalili ya mtu, kwa pupa kisha wakarudisha macho kwa Jackline, "poleni sana, mtakacho kipata leo ladhima kesho mnitafute tena" hapo walishuhudia tabasamu la hajabu ambalo hakuna ata mmoja wao, aliewai kuliona, kiukweli usingeweza kutambua kama huyu binti alikuwa anatabasamu au amekasirika wale vijana watukutu walitulia kwa muda kidogo, wakishangaa lile tabasamu la hajabu, kabla awaja stuka wakamwona Jackline Nyati, akigeuka aliko toka, yani upande wa mjini, ambako alikuwepo mwenzao mmoja ambae ni Majaliwa, kisha akatoka mbio kumfwata Majaliwa, ambae alikuwa aelewi elewi, maana alitalajia kuwa yule binti Jackline, angeanza kuangua kilio cha kuomba msaada, tofauti yake alimwoana, akimjia kwa speed moja ya kimbunga, mpaka Majaliwa ana pata wazo la kwamba kina chofwata ni hatari kwake, alimshuhudia Jackline, akiruka juu na kutuwa karibu yake ikienda sambamba na ngumi nzito iliyo tuwa usoni kwake, na kumfanya aone giza lenye nyota nyingi za kijani, sambamba na maumivu makali, kabla aja kaa sawa, Majaliwa alijikuta akifyetuliwa miguu, yake kwa mtama wa nguvu ulio mfanya ajikut, hewani kwa sekunde kadhaa kabla ya kutuwa chini, na kukandamizwa na teke la usoni, mpaka hapo wakina Festor na Kadoda walijuwa kuwa wanae pambana nae siyo mtu wakawaida, yani ni nitofauti na sura yake nzuri wa kuvutia, Jackline alikuwa ni wanamke katili sana, hapo kadoda na Festor wakanza kukimbia, kuifwata barabara, kuelekea nyumbani kwa kina Jackline, lakini awakupata nafasi ya kukimbia, kwa sababu walishuhudia Jackline akiwajia kwa speed ya hajabu, na kuwa piga kikumbo kikubwa, kilicho wa tupa pembeni, kisha kilicho fwatia hapo, ni kichapo kikubwa sana, ambachoo kilisababisha mzee Michael Nyati aitwe kituo cha polisi akiwa na mwanae, siku ya pili saa nne asubuhi, mzee Nyati aliwasili kituo chapolisi cha wilaya, pembezoni mwa uwanja wa mpila wa maji maji, aliingia ndani akiwa na binti yake binti mrembo sana, akaelekezwa ofisini kwa OCD, OCD Lukaka Nyamakena, alikuwa amekaa kwenye kiti chake mbele ya meza kubwa, yenye vikolokolo vingi, ikiwepo na bendera ya taifa na simu ya mezani, peni makalatasi na mafile mengi, kwenye visehemu vilivyo andikwa IN, OUT na PENDING, mbele yake kulikuwa na watu sita, wanaume wote watau wakiwa ni vijana watu wazima umri ukilingana na wa Michael Nyati, wakionyesha ni watu wenye uwezo kifedha, lakini wasinge mfikia mzee Nyati, pia walionekana vijana watatu wakiwa wamevimba nyuso zao, pia wamefungwa bandeji karibu mwili mzima, wakiwa na magongo ya kutembelea mikononi mwao, mzee Michael Nyati, akiwa na mwanae waliingia na kusalia, "samahani, bwana mkubwa, awaja kuambia kama nina wageni, humu ndani?" aliuliza OCD Nyamakena, kwarafudhii ya kikulya, "nime elekezwa hapo mapokezi, nije kwako moja kwa moja" alijibu kwa sauti ya utulivu, mzee Nyati, "ok! aina ubaya, ujuwe kuna kijana mmoja mwanafunzi, amefanya ualifu hapa, ndio tuna msubiri, aletwe na mzazi wake?, ni kama unavyo ona, yani hapa hawa watoto wameletwa hapa kwa msaada wapolisi, awawezi atakutembea" akatulia kidogo kisha akawaza jambo, OCD akamtazama Jackline, “kwanini msiwe kama mwenzenu huyu, ata kwa mwonekano anaonekana ni mpole sana”, aliongea OCD Nyamakena, kabla ajainua uso wake na kumwuliza mzee Nyati,"ok tatizo nini, au linamuhusu huyu binti yako?" hapo mzee Nyati akajikooza kidogo na kuwatazama wazee wenzake, ambao walionekana wamekunja sura zao kahasira, wakinyesha kuwa, wanahamu ya kumwona mwalifu,alie wachakaza vjiana wao, "samahani kwakuchelwa mzee wangu, mzee mimi ndie mzazi mnae msubiri" wote mle ndani kasolo wale vijana watatu tu, walimtazama mzee Nyati kwa mshangao, na hasira kari, kisha wakamtazama binti yake, "unaona sasa we mzee ulivyo mkolofi, sasa mbona huyo kijana wako umemwacha?, na usije uka niambia kuwa, amekimbia nyumbani" aliongea OCD, akionyesha hasira usoni kwake, "hapana mweshimiwa, nikwamba...." kabla mzee Nyati haja malizia, mzee mmoja kati ya wale wazazi watatu, akadakia kwa jazba, "huyu asicheze na damu yangu, ikiwezekana alela lumande, mpaka kijana wake apatikane" hapo akadakia tena mwingine akionekana mwenye hasira kupita wote, "tena sikubali kabisa, watoto wao wakipigwa ndio wakwanza kukimbilia polisi, nakudai fidia, lakini yeye wakwake anamficha" OCD likaa kimya akiwatazama wale wazazi wakimshambulia kwa maneno mzee Nyati, ambae alikuwa ametulia akiwaangalia wale vijana, huku akitabasamu, akuonyesha wasi wasi, zaidi alionekana kukubali kiwango cha mwanae, katika mapigano, OCD aligunduwa kitu usoni kwa nzee Nyati, "ok! ebu tulieni kwanza," wote wakatulia kutokana na kauli ya OCD "haya we! mzee tueleze umemwacha wapi huyo kijana wako?" huku akionyesha mwenye tabasamu, pasipo wasi wasi wowote, mzee Nyati akaongea huku akimwonesha mwanae Jackline, "mimi nina mtoto mmoja tu!, ambae ni huyu hapa," hapo ukasikika mguno toka kwa wale wazee watatu, wakionyesha kupinga kauli ya mzee Nyati, kwamba zilikuwa ni mbinu zake za kumwokoa mwanae, "mchezo wakitoto huo" mmoja wao aliongea kwa jazba, "unauakika unacho kisema mzee wangu?" aliuliza kwa kwa mshangao OCD, ambae nae aliona mazingaombwe yana karibia kutokea ofisini kwake, "ndiyo mzee wangu" alijibu mzee Nyati kwa sauti ya upole kabisa, "na huyo Jack ..sijuwi Jackson..sijuwi nani, ninani wako?" aliuliza OCD, na wale wazee wote, wakatulia macho wakiyaelekeza kwa mzee Nyati, huku tabasamu likiwa limetawala kwenye nyuso zao, wakizani wamesha mkamata kwa uongo wake, "sina mtu nyumbani kwangu anaitwa Jackson, ila huyu binti yangu anaitwa Jackline,"aliongea Michael Nyati kwa sauti ya upole, kama kwaida tokea ameingia hapa ndani, akiwaacha wale wazee wakodoe macho kwa hasira wakizani wana chezewa mchezo wa kiuni, wakataka kuanza kuongea, lakini Ocd Nyamakena akamtazama yule binti, kisha akawatazama wale vijana, "eti nyie huyo Jack ndie huyu?" wote wakaitikia kwa vichwa, wakionyesha kukubari, maana awakuweza kuongea, midomo yao ilikuwa imevimba sana, hapo OCD alingua kicheko cha kejeli vibaya sana, "nyie manunda, leo mepigwa na huyu binti?" aliongea OCD alafu akaendelea tena kucheka, na kusababisha wale wazazi nao wacheke kicheko cha uchungu, OCD alimwaomba Jackline aeleze ilivyokuwa, naye akaeleza jinsi walivyo mvizia kwa lengo la kumbaka, lakini kilicho wapata ndicho hicho kinacho onekana, "pole kwa usumbufu baba Jack, unaweza kwenda, na mwanao" alisema Ocd akimwambia mzee Nyati, kisha akamwambia Jackline, “wakirudia tena waongezee, wasiweze ata kufika hapa polisi wabakaji hawa" alimaliza pia akawatimua wale wazazi akiwaambia "ebu bebeni hii mizigo yenu, mwende sehemu mnayozani wanaweza kuwasaidia" ****
Hayo nibahadhi ya matukio ya kinyama, aliyo yafanya Jackline na baada ya kumaliza kidato cha nne, alianza kufundishwa namna ya kutumia silaha, kwanza alianza na bastola akifwatia silaha zote za kati, kuanzia SMG(AK47) UZI GUN, MMG, LMG, MIKE GALILY, mwisho akamaliza na Mugnum Snper riffle, yenye uwezo wakumpiga mtu umbali wa km mbili, hii nisilaha ya kudungulia toka mbali, pia licha ya kuwa na uwezo wakutumia mikono na mikuu kupigana, pia aliweza kutumia silihaha za jadi kama kisu na vinginevyo, chochote kilichipo mkononi mwa Jackline kwake uwa ni silaha, mpaka anamaliza kidato cha sita, Jackline alikuwa anambinu elfu moja za kuuwa pasipo kutumia bunduki, hiyo ni kwamikono yake tu! sasa ni week ya tatu yupo hapa dar es salaam, naleo ndiyo siku ambayo, amemdondosha windo lake la kwanza, kati ya sita aliyotumwa kuwamaliza, Siku zote Jack alikumbuka kuwa, baba yake alimsisitiza kutoji usisha na mapenzi, kitu kilicho sababisha, Jackline kuwafanya wanaume ndio maadui zake wa kwanza, pale wanapo jaribu kumtongoza,
Miezi mitatu nyuma ya leo, baba yake alimwita Jackline, na kumweleza jukumu lililopo mbele yake la kulipiza kisasi, akimsimulia tukio lilimtokea mwaka 1988, huko nyilagongo nchini Congo, nibahada ya kufanya uchunguzi nakufahamu wabaya wake wapo hai na shuguli wanazo zifanya akianza na afisa mteule Chilumba, ambae alikuwa mchungaji wa kanisa moja la kilokole mjini dar maeneo ya buguruni, sasa ni mwezi mmoja tangu Jackline alipoingia dar es salaam, kikazi zaidi, moja kwa moja alifikia kwenye nyumba ya wageni hiliyopo karibu na nyumba za polisi mtaa wa rozana, akajifanya muumini wa kanisa la mchungaji Chilumba, aliuzuria mala mbili huku akichunguza ratiba za mchungaji Chilumba, natabia yake, akagundua mchungaji alikuwa anatabia ya kupenda waschana, uwarubuni kwa janja ya maombi, kisha kufanyanao mapenzi, ndipo alipoomba kukutana na mchungaji,
Jackline alipatanafasi ya kukutana na mchungaji, mchungaji Chilumba akaingiwa natamaa, akaomba kukutana na Jackline, ambae alimdanganya mchungaji Chilumba kuwa, anafanyia kazi kwenye ofisi inayojiusisha na utoaji wa mikopo, kwa wakina mama wajasiliamari, zilizopo manzese kwenye jengo la Kamanga plaza, wakapeana miadi siku ile ya jumatatu, saa nne asubuhi wakutane kamanga plaza, ambapo haikuwa kazi ngumu kwa Jackline kumdungua Chilumba kutokea jengo la pili **** Sasa Jackline alikuwa amejilaza kitandani, ndani ya chumba chake alicho kikodi pale Mapambani bar, akachukua simu yake ya kisasa, akabonyeza namba na kupiga, alisubiri kidogo kabla ya kuanza kuongea “kazi tayari baba” aliongea Jackline kwa sauti ya chini “nimeona kwenye tv, kuanzia sasa makini sana, wakati natafuta walipo wengine, nikiwapata nitakujurisha, naiimani nitawapata mapema, maana tumesha wachokoza” Jackline alipo maliza kuongea na baba yake akajilaza tena, hapo yakaanza kumjia mawazo ya yule kijana mlevi, alie mgongea site mirror yake na kumsamehe, ambae alimsikia kwa mdomo wake akidai kuwa yupo tayari, kuonga gari kwa yeye mama n’tilie, Jackiline akajikuta akimchukia sana yule kijana, na baada ya kuwaza wa dadika chache, Jackline akapitiwa na usingizi *** Kituo kikuu cha polisi askari polisi walionekana wakiwa katika pilika pilika za hapa na pale, huko ndani ya ofisi ya mkuu wakitengo cha upelelezi, wakuu walikuwa katika mjadala mzito, juu ya tukio la kuuawa kwa mwanajeshi mstahafu, anaye julikana kama mchungaji Chilumba, baada ya mjadala wa muda mrefu sana, wakatoa mahamuzi kuwa atafutwe inspector Johnson David asimamie hii kesi, maana yeye ni hodari sana, wakuzikabiri kesi kama hizi, Masaa machache baadae Inspector Johnson alikuwa amesha report kituo kikuu, akitokea kigamboni, alikokuwa anafanyia kazi mwanzo, alipewa jukumu la kumtafuta muhuwaji, akikabiziwa magari mawili aina ya land lover defender na askari wapatao kumi wakiwa na silaha aina ya smg, kwaajiri ya kumsaidia, kilicho wastua wakuu wapolisi na selikari, ni kwamba silaha iliyotumika ni kubwa sana, tena ni silaha mahalumu ya kijeshi, utumiwa na wanajeshi mahalumu walio pitia mafunzo mahalumu ya kivita na mauwaji ya siri, taharifa zilipelekwa kwenye makao makuu ya jeshi la ulinzi juu ya kifo cha askari wao mstahafu **** Ilisha timia saa mbili usiku Jackline akiwa amejilaza kitandani alistuliwa na mwanga wataa iliyowashwa mle chumbani kwake, akafumbua macho akakutana na sura za wanaume watatu walio shiba kweli kweli, kila mmoja akiwa na kisu kikubwa mkononi, kati yao akiwepo yule alie kuwa akiongea na mhudumu wa vyumba, kwa hiyo ni yule alie tuma ujumbe wakumtaka kimapenzi, alipoangalia vizuri nyuma yao mlangoni alimwona yule mhudumu wa vyumba, akichungulia, macho yao yalipogongana akamng’ong’a, jitahidini asipige kelele, fanyeni faster” aliongea yule dada mhudumu, kisha akaondoka zake, njemba moja kati ya wale jamaa watatu, alifunga mlango na funguo akiiweka mfukoni, “wakubwa mimi naanza alafu nyie mtamaliza” aliongea yule jamaa ambae alisha mfukuzia Jack toka jana, Jackline aliwaangalia kwa umakini sana, vijana wale watatu, asijuwe wamefunguaje mlango, wakati aliufunga kwa ufunguo, lakini akagundua kosa alilofanya, nikuchomoa funguo kwenye kitasa, ndipo yule mhudumu alipo wapafunguo nyingine wakatumia kuingilia ndani, Jackline alitulia kitandani akiwatazama wageni wake, kwa umakini sana alipapasa kwenye paja lake la kulia na kukigusa kisu chake, hapo Jackline akatabasamu kidogo “karibuni kuzimu,” ilisikika sauti tulivu ya Jackline masikioni mwa wale vijana, ambao waliduwaa wasimwelewe kabisa anacho maanisha huyu dada,ambae bado alikuwepo juu ya kitanda, zaidi walishangaa huyu mwanamke akuonyesha dalili yoyote ya uoga au wasiwasi usoni kwake, hapo walishuhudia tabasamu la hajabu ana, usoni anacho maanisha huyu dada,ambae bado huyu mwanamke akuonyesha dalili yoyote ya uoga au wasiwasi usoni kwake, hapo walishuhudia tabasamu la hajabu
Wakatazamana usoni, kwa mshangao, kila mmoja akizani labda yule dada ni jinni, kutokana na kujiamini kwa kutoa ile kauli, ya karibu kuzimu, **** wakati huo ilisha timia saa tatu za usiku, magari yalikuwa yameanza kupungua barabarani, asa barabar kuu iendayo morogoro, Denis na Mahadhi walikuwa kwenye bar, ya Jambo pub, wakiendelea kunywa pombe, bar hiyo ipo pembeni ya barabara ya morogoro upande wapili, ikitazamana na jengo la ofisi yao (Mazao building) “we! Chapombe muda wakuondoka umewadia” aliongea Mahadhi huku anasimama na kujipapasa mfukoni, akatoa funguo ya gari, “poa kaka, wewe nenda, wacha mimi nimalizie hii ya mwisho, tutaonana kesho” aliongea Denis kwa sauti iliyozidiwa na ulevi, Mahadhi akaanza kuondoka, akielekea kwenye maegesho ya magari, akimwacha rafiki yake akiwa anakata maji, **** yule mhudumu wa vyumba baada ya kuwafungulia wale vijana watatu, mlango wa chumba cha Jackline alirudi mapokezi na kusikilizia, akijuwa kabisa kuwa mwanamke mwenzie ana bakwa na midume mitatu, alivuta picha jinsi tukio la mle ndani linavyotokea, aliona kuwa yule dada mshamba atakuwa ame kamatwa miguu na mikono, akiingiliwa huku analia kimya kimya, baada ya kutishiwa kisu, lakini aikuwa hivyo, maana azikupita ata dakika mbili, aliona ule mlango wachumba cha yule mdada ukifunguliwa, kitendo ambacho akutegemea, alimwona yule dada akitoka akiwa na mabegi yake mawili kama alivyokuja jana jioni, yule dada mhudumu akuelewa kilichotokea, alimwona yole dada akija upande wake, alitamani kukimbia lakini kilichompa moyo nitabasamu usoni kwa yule dada, ambae alipofika pale mapokezi, akamsogelea kabisa, wakawa uso kwa uso wakitenganishwa na meza, “nenda kawafunike mabwana zako” ni kauri iliyo ambatana na kitendo cha ghafla cha mkono mmoja wa yule dada, kumkamata mhudumu wa vyumba na kumvuta kwake, akimtandika kichwa cha nguvu,kilicho lenga katikati ya uso wa wa mhudumu, kilichompeleka chini yule mhudumu, na kumfanya ajishikilie sehemu ya pua iliyoshikwa na maumuvu makali sana, huku akianza kuisi maj maji ya moto yaki mchuruzika sehemu hiyo, alipo jiangalia alikuwa anatoka damu, yule mhudumu akajiinua haraka sana, alipoinuka akumwona tena yule dada, kwa kitendo kile, dada muhudumu akajuwa fika kuwa wale jamaa ndani hawapo salama, akatoka pale mapokezi huku akijishika kwenye pua yake, akizuwia damu, na kwenda kutazama kule chumbani, “kwanini wale jamaa wamemwachilia yule mwanamke”, aliwa za dada mhudumu, wakati akiingia ndani ya chumba kwa fujo, nusu ajikwae kwenye miili ya wale vijana watatu, ikiwa imelala kwenye dimbwi la damu, huku shingo zao zikiwa na majeraha makubwa ya kisu, yule dada mhudumu akapiga kelele zilizo wafanya watu wote walio kuwepo pale bar, wakimbilie kule chumbani, **** Denis alikuwa ameshamaliza bia yake, aliyosema kuwa ni ya mwisho, akanunua katon moja ya bia za kopo na soda nne aina ya cola nazo za kopo, na kuelekea kwenye gari, huku anayumba yumba, ghafla akakoswa koswa na gari la polisi lililokuwa speed, huku likipiga king’ora, Denis akatazama lile gari la polisi likiingia kwenye chochoro za mitaa, akasonya kilevi, na kuendelea na safari yake ya kulifwata gari lake, alipolifikia akazibana kwapani zile soda zilizo kuwa chache kwenye mfuko, huku mkono wa kushoto hukiwa umeshikilia bia, akaanza kufungua mlango wa gari, lake aina ya noah, akiwa anaangaika kulenga tundu la ufunguo kutokana na urevi, ghafla akasukumwa na mtu aliekuwa anapita njia, Denis aliyumba kidogo, huku soda zikimdondoka, yule mtu ambae alikuwa amebeba mabegi mawili, alionyesha busara, akasimama kisha akainama kumsaidia kuokota zile soda, akamkabidhi Denis, “samahani kaka yangu ni bahati mbaya” ilikuwa sauti tamu ya kike, muda wote Denis alikuwa ameganda akimshangaa yule dada, kumbe alisha mtambua, toka akiwa anaokota zile soda za kopo baada ya kuliona lile begi dogo jeusi, ni yule dada mama ntilie, Jackline naye akaduwaa, akamkumbuka huyu kijana “huyu tena” alisema kwa sauti ya kunong’ona **** wakati huo polisi walisha fika eneo la tukio, pale Mapambano bar and guest house, kwanza walizunguka eneo lote, na kuanza kukagua eneo zima ndani na nje, huku wakiwazuwia watu kutoka na kuingia eneo hilo, waliwaita wahudumu, kwa ajili ya kuwachukua maelezo, walipo muhoji yule dada mhudumu wavyumba, aliwaambia kuwa muuwajia ni mwanamke, akiwaeleza jinsi alivyo na mavazi yake, na mizigi aliyobeba, “yani ametoka sasa hivi”, haraka sana polisi waligawana, wengine wakabaki pale mapambano bar na wengine wakatoka nje wakijaribu kufwatilia huyo mwanamke alikoelekea, wakiwa kwa miguu, walielekea kule aliko elekea Jackline, njiani waliangalia kwa umakini kla waliepisha nae, wakifwata maelekezo ya dada mhudumu. ***** Jackline Michael Nyati alimtazama kwa umakini, yule kijana aliemvunjia kioo cha gari mchana wa siku ile, huku mapigo yake ya moyo, yakienda mbio, akamwona yule mkaka akiyumba yumba kwa ulevi, “we.. we! Mwanamke mbona ninabahati sana nawewe,” Jackline alitamani kucheka lakini akajizuwia “ebu.. ebu.. nisaidie kufungua mlango wagari, maana mikono yangu imelegea ghafla baada ya kukuona” aliongea kilevi yule kijana, akimnyooshea funguo zagari Jackline, hapo Jackline akaona huyu kijana analeta mazowea, akataka amtwange japo kichwa kisha aondoke zake, lakini wakati anajiandaa, aliwaona polisi wanne wakija upande wake huku wakiangalia kila mtu wanae pishana nae, akakumbuka alipishana na polisi wakati anatoka Mapambano bar, lakini sasa wapo kwa mguu tena atua chache toka pale alipo, hapo Jackline akaidaka funguo ya gari toka kwenye mikono ya yule kaka, na kufungua mlango wadereva, kisha aka fungua mlango wa dereva kabla hajazunguka na kufungua mlango wanyuma na kuingia haraka sana na kisha kuufunga, akimwacha yule kijana mlevi Denis akimshangaa, Jackline akaomba sana huyu mlevi asilopoke neno lolote “kumbe unataka rift” alionge Denis kwa sauti ya kilevi, huku anazirushia bia na soda kwenye kiti cha jirani yani cha abiria wa mbele, wakatihuo wale police walikuwa wanakatiza pale walipo, wakiwa makini na silaha zao mikononi, yule kijana mlevi aliingia kwenye gari, kisha akakaa kwenye kiti cha dereva, akawasha gari na kuingiza gia ya kuondokea, akaikamata barabara kuu ya morogoro, safari ya kuelekea nje ya mji ikaanza, “sasa.. we!..mdada una elekea wapi?” Denis alikumbuka kama yupo na mtu mle ndani ya gari, “niondoe maeneo haya, maana mama ninaye kaa naye, amewatuma watu wanataka wanibake” aliongea Jackline kwa sauti ya uoga wa kuigiza, iliyo changanyika na wasiwasi ya kweli, maana aliofia mwendo mkali wa gari lile, na jinsi dereva mwenyewe alivyokuwa amelewa “mh! huyo mama ni ndugu yako?” aliuliza Denis akionyesha dailili ya huruma, lakini katika hali ya ulevi “hapana mimi nimekuja juzi toka Songea, nimekuja kutafuta maisha, ndo nimefikia kwake” Jackline alicheza na akili ya Denis “loooh! Kwa hiyo sasa hivi, auna pakukaa?” aliuliza Denis huku akizidi kukanyaga mafuta, wakati huo alikuwa akipita ubungo mataa “ndiyo sina pakukaa, ila usijari nita pata tu!” aliongea Jackline huku wasiwasi ikizidi, kutokana na mwendo wa kijana huyu mlevi “dada yangu usijari, utafikia kwangu utakaa kama kwako” maneno hayo yaliupasua moyo wa Jackline, hapo haraka sana mawazo mawili yakamjia kichwani, moja ni kwamba, huyu kijana amesha mtamani, kwake mwanamume anaye mtamani ni adui yake, pili huyu kijana amememuokoa kwa polisi, pia anaweza kuwa msaada kwake, kwa sababu amesha fanya amuwaji nyumba ya kulala wageni, hivyo polisi wanaweza kuanzisha msako mkubwa kwenye nyumba zote za wageni, ikawa rahisi kumstukia au kukamatwa kabisa, hivyo akikaa kwa huyu mlevi itakuwa nafuu kwake, lakini itakuwaje endapo atataka kitumbua, “mkeo je?, si’ataniuwa?” aliongea Jackline akimtega Denis ambae bado alikuwa amjuwi jina, “haaa wapi? mkeee atoke wapi?” aliongea Denis kwasauti kubwa ya kilevi, iliyomfanya Jackline acheke kwa sauti ya chini, sasa wasiwasi wakufika salama ulipungua baada ya kuona yule kijana mlevi yupo makini sana na uendeshaji wa gari lake, sasa walikuwa anaingia mbezi mwisho, ndipo Denis akatafuta sehemu nzuri karibu na bar, akaparki gari, Jackline akamtazama kwa umakini sana, akujuwa yule kijana mlevi anataka kufanya nini, Denis akamgeukia Jackline, ambae alikuwa amekaa seat ya nyuma, huku akiachia tabasamu lake la kilevi, hapo Jackline akaona kuna dalili ya kujeruhi mtu au kuuwa kabisa, maana alihisi kuwa huyu kijana mlevi ameingiwa na tamaa ya kimwili, itaendelea............
JE? DENIS ANATAKA KUFANYA NINI, ENDELEA KUFWATILIA #DADA_MDUNGUAJI INAYOKUJIA
Your Thoughts