DADA MDUNGUAJI EPISODE 10

DADA MDUNGUAJI


EPISODE 10


STORY NA Mbogo Edgar


whatsaap 075621102


ILIPOISHIA EPISODE 9 : ila amenifurahisha sana alikoifadhi simu na zile risasi” aliongea mama Jackline wote wakacheka, na mda huo huo wakaliona gari la Denis lina ingia kwa fujo, nakusimama mbele ya jengo lile walilo kuwepo wao, wakamwona akishuka na kusogea walipo kuwepo wao, huku anatoa simu yake n kupiga, mala mama Jack akaona simu ya Jackline, iliyo kuwa mikononi mwa mama Jackline, ikianza kuita, Denis akaonekana kuutambua mlio wa simu ya mke wake, akamtazama mama Jack,  endelea .........

 Akamtazama mama Jackline, akijaribu kukumbuka kuwa alisha wai kumwona wapi mama huyu, kisha akamtazama mzee Nyati, nae sura yake aikuwa ngeni sana, “samahani jamani, nyie ndio mlio msaidia mke wangu?” aliuliza Denis pasipo kusalimia, wazee awa wakatazamana, kisha mama Jackline akamtazama Denis, “wewe ndie mume wayule dada mjamzito?” aliuliza mzee Nyati, “ndio ni mimi aliniaga anakwenda kununua dawa, nikashangaa mnanipigia simu mnaniambia mpo huku” aliongea Denis ambae pombe ilisha pungua kichwani mwake, basi kijana wacha sisi tukuache hapa, umsubiri mkeo, ilaombi moja kijana” aliongea mzee Nyati, akimtazama Denis, “aina tatizo mzee wangu, kiasi gani nikulipe?” aliongea Denis, akitoa pochi yake toka mfukoni, “hapa kijana, sina maana ya fedha, ninaombi moja tu!” aliongea mze Nyati, huku akitabasamu kidogo na kumtazama mke wake, “ok! aina tatizo mzee wangu nakusikiliza” aliongea Denis, pasipo kujuwa kuwa waliopo mbele yao ni wakwe zake, “asante kwa kunipa nafasi ya kunisikiliza” alisema mzee Nyati, akajikooza kidogo, kisha akaendelea, “mimi na mke wangu tumefurahi sana kukutana na familia yako, mkeo ametueleza kuwa, huyu anaezaliwa ndie mtoto wenu wa kwanza, kama aouto jari naomba jambo moja, kamatazaliwa mtoto wakiume mwite Fransis, na kamani wakike mwite Rufina” alimaliza kuongea mzee Nyati, nakuttulia akimtazama mkwe wake, “haaa! usijari mzee wangu, tena mke wangu atafurahi sana, sababu babu yake mzaa baba anaitwa Fransis, ila ilo la rufina sija juwa” aliongea Denis kwa uchangamfu sana, wote kwa pamoja wakionekana wenye furaha wakendelea na maongezi, huku wakina mzee Nyati wakisahau kama walisha aga, ***** akiwa nyumbani kwake Kinyelezi, mzee Masinde aliegahili kabisa ata kwenda kwe taflija, baada ya wale polisi wawili kumchelewesha, kwa maswali ya kipuuzi, alikuwa sebuleni kwake akinywa pombe kali kwa fujo, huku mda wote akitukana matusi ya nguoni, kiasi cha kumshangaza ata mke wake, ambae alishindwa kuhoji kitu, kutokana na maelewano mabaya ya mda mrefu yaliyo ikosesha amani familia hii, wakati akiedelea kunung’unika na kutukana ovyo, mala mzee Masinde akasikia simu yake inaita, akaichukuwa toka mezani na kutazama mpigaji, “watakuwa wamesha maliza” alijisemea mzee Masinde huku anapokea simu na kuiweka sikioni, “nimbie bwana Mwijage, Taflija imeendaje?”  aliongea Mzee Masinde, ambae alitambua kuwa mzee mwenzake tayari amesha toka kwenye Taflija kutokana na kusikia utulivu, wa eneo alilokuwepo Mwijage kuwa tulivu ikiashilia kuwa yupo kwenye gari, “kaka sijuwi unabahati gani? maana kilicho tokea hapa cosovo, nizaidi ya matukio yote ya liyo wapata wenzetu” aliongea Mwijage, akiwa katika hali flani ya taaluki, “unataka kusema nini Mwijage,?” aliuliza mzee Masinde katika hali ya wasi wasi, hapo mwijage akamsimulia mzee Masinde jinsi ilivyo kuwa, akimweleza tokea walipo mwona mzee Nyati, akija mbele kuchangia shilingi million moja, pia akmweleza jinsi walivyo pokea taalifa ya kuuwawa kwa Alex alie kuwa amee nda chooni, pamoja na walinzi wake watatu, hivyo akamweleza kuwa yeye binafsi anamshukuru sana mwane, insp Johnson, kwa kumpatia ulinzi na kumpakiza kwenye gari, kisha yeye pamoja na mlinzi mmoja alienae, kuelekea nyumbani, “kwahiyo umemwona Nyati live?” aliuliza Masinde kwa mshangao, uliotawaliwa na wasi wasi, tena anaonekana yupo vizuri, siyo wa wasiwasi, ni mtu mwenye fedha zake” aliongea Mwijage, ambae alionekana kukata tamaha, ya kukwepa mtego huu wa Nyati, “kwa hiyo Michael Nyati yupo hapa dar es salaam?” aliuliza Masinde kwa sauti ya uoga zaidi, “yani dah! kama mzim vile sijuwi kwanini ukumtandika risasi ya kichwa yule mshenzi?” aliongea Mwijage, “ok! mwijage tume baki wawili, ebu tukae chini tujuwe lakufanya, chamsingi tutulie majumbani ketu, huku tuna panga jambo la kufanya” aliongea mzee Masinde, na wawilihao wakakubaliana kisha wakakata simu, “sina ujanja, ina bidi nimshirikishe mwanangu katika jambo hili” aliwaza mzee Masinde, huku akiinua grass iliyo jaa pome kali, “pumzika kwa amani shujaa” kisha akagugumia hiyo grass iliyo jaa pombe kali, na kuishusha ikiwa ainakitu, huku amekunja sura yake kwa uchungu wa pombe hiyo, hapo mzee Masinde akaonekana uwaza jambo flani kwadakika kadhaa, kisha akatabasamu, huku anajisemea peke yake, “Johnson ana akili nyingi sana” ****saa saba usiku, ndio wakati ambao Johnson mwenyewe, alikuwa anaingia nyumbani kwake mbezi beach, akitokea Cosovo Hotel, akiwa amesha angaika kukagua watu wote waliokuwepo pale hotelini, pasipo kujali ni mlemavu au mtazamaji, pia wapangaji wa mle hotelini akikagua chumba kimoja adi kingine, pasipo mafanikio, “huyu mzee anambinu nyingi kali sana, kuna kila sababu ya kumsaidia baba, ata kwa kukiuka miiko ya jeshi, vinginevyo nita mpoteza” aliwaza Johnson, wakati anavua nguo ili kuingia bafuni, kiukweli licha ya kuwa baba yake alikuwa na tabia zinazo ashilia uvunjaji wa sharia za nchi, lakini baba yake huyo alisha mfanyia mambo mengi sana ya kimaisha, ukiachilia kumsomesha na kumsaidia kupata kazi aliyo kuwa anaipenda ya polisi, pia kumjengea hii nyumba anayo ishi sasa huku mbezi bichi, ae mnunulia gari zuri aina ya Nissan patrol isitoshe mzee Masinde akujali kama mwanae anakazi, yeye alimpatia kisi kikubwa cha fedha mala kwa mala, “nazani mzee Soud atanielekeza namna ya kumpata mzee Nyati” **** Denis akiwa mekaa pale nje na wakina mzee Nyati, mala wakamwona nesi mmoja akitoka nje na kuwa uliza, “nyie ndio mlie mleta, dada mzazi usiku huu?” “ndio ndio ndio sisi, mimi ni mume wake” wakwanza kuitikia alikuwa Denis huku anainuka toka kwenye benchi, alilokuwa amekaa pamoja na wakina mzee Nyati na mke wake, “hongera sana kaka,mkeo kajifungua salama, mtoto wa kiume, japo ailuhusiwi kwa usiku huu, lakini nawapeni mda mfupi mka mtazame” hapo Denis na wakina mzee Nyati wali ruka kwa furaha kubwa sana, wakaongozana na yule nesi mpaka kwenye hodi ya wazazi, chumba cha VIP, “mnaenda wapi nyie, kwani huu ndio mda wakutazama wagonjwa?” ilikuwa ni sauti kavu ya kike, toka kwa mwanamke alie valia kama yule nesi mwingine, huku amekunja sura, iliyo mfanya azidi kuwa mbaya wa sura, japo kwa matazamo ni mwanamke mwenye miaka selathini na tatu, ambae sasa alikuwa ameziba mlango akiwazuwia wasiingie, watu awa watatu wakabaki wame simama wakimtazama Jackline, ambae alikuwa busy anamkagua mtoto alie lazwa kitandani, **** ndani ya chumba kutembelea mahabusu, wa kituo kikuu cha polisi, Jackline ambae alikuwa ameilaza mikono yake iliyo fungwa kwa pingu za minyololo mapajani kwa Denis, akiendela kumwelezea kuwa yeye ni muuwaji na kwanini alifanya hivyo, alitulia kidogo na kumtazama Denis usoni, maana alimwona kama alikuwa anajambo alilotaka kuuliza, “ndio maana huyu mzee alilipia hile ward ya VIP, nayule ness ambae tulisikia amekutwa bafuni amekufa, je ulimuuwa pia?” aliuliza Denis, ambae mpaka hapo alisha anza kumwogopa mke wake, 


 “Ndio nilimuuwa mimi, tena siyo peke yake, alikuwa na watu wengine wawili, nazani unakumbuka alichowafanyia usiku pale mlipo luhusiwa kuja kuniona ndani” aliuliza Jackline akimtazama Denis usoni, nakugundua kuwa, mume wake huyo alikuwa na wasi wasi sana juu yake, “ndio alitudai lushwa, nazani ata wewe ulimsikia” aliongea Denis ambae licha y kuujuwa ukweli kuhusu mke wake kuwa muuaji, lakini alikubari kuwa mke wake aliuwa kwa sababu, “ndio nilisikia kila kitu, sasa kama hilo alitoshi, alitaka ufanya kitu ambacho, kama ange fanikiwa nisinge sahau katika maisha yangu” aliongea Jackline huku anatabasamu, “alifanya nini tena?” aliuliza Denis kwa shahuku, “mume wangu kuwa mpole nikusimulie” **** baada ya wakina Denis na wazazi wa Jackline, kumpatia shilingi elfu kumi, yule nesi alie wazuwia mlangoni, akawa luhusu kuingia ndani ya chumba cha VIP, alicho kuwemo Jackline na mwanae, ambacho kipo kwenye gholofa ya pili, na yule nesi alie waleta akaondoka zake, wakati huo huo akaingia kijana mmoja alie valia koti jeupe, ni doctor, akasimama nje ya chumba kile akiongea jambo na yule nesi alie chukuwa elfu kumi kwa kina Denis, “Denis mme wangu, tume pata mtoto wa kiume, aliongea Jackline akimkumbatia Denis, ambae alionekana kuwa nafuraha kubwa sana, “tuta mwita Fransis, jina la babu yako, pia huyu mzee aliekusaidia na yeye anaitwa ameomba tumwite jina hilo, hapo Jackline akamtazama baba yake, macho yao yaka gongana, mzee Nyati akafinya jicho, “nashukuru sana mume wangu, kwa kunipa kipambele” Jackline pia aliwashukuru wale wazee wawili mtu na mke wake kwa kutumia mdawao kumsaidia, huku moyoni alishukuru uwepo wa wazazi wake katika eneo la tukio, na kumshuhudia mjukuu wao, pasipo Denis kujuwa lolote, juu ya wazee wale, wakati wanaendelea kuongea, Jackline aliweza kuwaona nesi mkorofi na yule doctor, wakisistizana jambo flani huku yule docor wakiume akisistiza mda kwa kuonyesha ishara ya kugusa kwakidole chake, karibu na nyuma ya kiganja chake, kisha yule doctor akaondoka na yule nesi akaingia mle chumbani, “haya jamani mda ume waishia naomba muondoke mama apumzike” aliongea yule mama ambae auwa na sura ya kirafiki na ukarimu, “haya dada nesi tunaondoka zetu, wacha tuagane na mgonjwa” aliongea Denis akionyesha kuwa anahamu ya kuendelea kuongea na mke wake, ila kwa upande wa Jackline akaona kuna ishara ya kuwa na hatari mahali pale, baada ya kuagana na wakina Denis, Jackline akaongea kwa lugha moja ya kificho, “sijuwi kama nitalala vizuri, yaningekuwa na moder 99, ningelala vizuri sana,” “ndio kinywaji gani hicho mke wangu?” aliuliza kwa mshangao Denis, pasipo kujuwa kuwa alie ambaiwa amesha elewa, “hahaha mumewangu kwa vinywaji, siyo kinywaji ni mafuta yay a dawa ya mbu” hapo wote wakacheka sana, kisha wakatoka nje ya chumba huku mama Jackline akiipenyeza bastora kwenye shuka, pamoja na kikasha cha risasi na kiwambo cha kuzuwia sauti, pasipo Denis na yule nesi kuona, wakina Denis waliondoka zao, huku akimwachia simu yake na Jackline akimsisitiza kesho kuwai asubuhi pamoja na chai au uji, na kumwacha yule nesi akiwa amesimama nje ya chumba, kile alichokuwepo Jackline  na mwane, Jackline aliiweka vizuri Bastora yake, huku anaendelea kumtazama yule nesi, ambae sasa likuwa ameshika simu yake, akabonyeza ndamba kadhaa kisha akaiweka sikioni, akutimia ata sekunde tano, yule nesi akaongea neo moja tu , “tayari” kisha akakata simu na kuingia kwenye chumba alicho kuwepo Jackline, safari hii aionekana mwenye tabasamu, japo lilikuwa la kulazimisha, “samahani dada japo chumba chako ni VIP, lakini kuna mzazi mwingine analetwa na Doctor, ametoka kujifungua, tunaomba apumzike kidogo hapa, wakati tuna mtafutia kitanda” aliongea yule nesi ambae alionyesha dalili zote za mashaka mashaka, “ok! hakuna tatizo si kwamda tu, maana kitanda chenyewe ni kidogo,” aliongea Jackline huku akizidi kumsoma huyu Nesi, “kitanda siyo tatizo maana mta kaapembeni kidogo watoto mta walaza kitandani, nazani aita dhukuwa nusu saa, kabla ajahama” aliongea yulenesi kisha akatoka nje, hapo Jackline akaichukuwa bastora yake na kupakia kimkebe cha risasi, kisha aka funga bomba la kuzuwia sauti, akaiweka chini ya dogoro, baada ya hapo haraka sana aka nyofoa kiuzi kwenye shuka la hospital na kumfunga mwanae kwenye kidole kimoja cha mguu wa kushoto, ile ana mfunika vizuri mwane alie kuwa amepitiwa na usingizi, akaingia yule nesi, akiwa amebeba kitoto kilicho funikwa mwili mzima, kwa ngu zilizo fanana na zile alizo funikwa france mtoto wa Jackline, akiongozana na binti mmoja alijitanda kanga mwili mzima, “karibu na hongera sana” alisema Jackline huku akiwa meachia tabasamu languvu sana, “asante sana dada” aliongea yule dada, akiachia tabasamu, lakini lilioneka ni la kulazimisha, lililo jaa wasi wasi, yule nesi alimlaza yule mtoto, aliie ingia nae pembeni ya mtoto wa Jackline, kitanda kikipatikana, atakuja doctor kukuchukuwa” aliongea yule nesi na kutoka nje, akiwaacha Jackline na yule dada mwingine wakianza kupiga story, huku watoto wao wakiwa wamelala, Jackline mda wote wamaongezi yao, alijaraibu mkumtazama kwaumakini sana huyu dada ambae aligunduwa kuwa ndani ya kanga chini alivaa suluali ya jinsi, “mh! mzazi jinsi” aliwaza Jackline huku anamtazama yule dada, kisha akamtazama mtoto alikuwa ametulia kimya, huku akaviligishiwa nguo mwilimzima kisi cha kuto kuonekana sura, “eti dada mbona ume mfunika sana huyu mtoto, si atakosa hewa?” aliuliza Jackline, na yule dada akaanza kujiumauma kujibu, lakini hapo hapo akaingia yule nesi, akiwa ameshiaka file mkononi mwake, “Jackline Michael, ndio nani kati yenu?” aliuliza yule nesi akisoma kwenye lile file, “ni mimi hapa” aliitikia Jackline, “ok nifwate” aliongea yule nesi na kuanza kutoka nje, jackline akainuka na kutaka kumbeba mwane, “mwache mtoto apumzike” alisema yule nesi ambae alisha kuwa ametoka nje ya kile chumba na kusimama nje ya mlango, Jackline akamwacha mwane na kumfwata nesi, ambae alielekea moja kwamoja mpaka kwenye meza moja kubwa sana nje y ail;e ward aliyo kuwepo Jackline, wakiwa wanakaribia ile meza wakapisha na yule doctor wakiume, alie onekana mida ile wakina mzee Nyati wakiwa kwenye chumba alichokuwa amelazwa, yule doctor aliwapita kidogo kisha akasimama, “samahani Nesi, naenda kumwamisha yule mzazi, maana tayari tumesha pata kitanda kingine,” aliongea yule doctor, kwa sauti ya unyenyekevu, “swa fanya haraka maana chumba chenyewe tume dandia tu!” aliongea yule nesi, na kumshangaza sana Jackline, kwani yeye anajuwa anae paswa kutumwa ni huyu nesi, na sie yule doctor ambae anaonekana kuto kufahamu nafasi yake yakazi, Jackline akamwona yule Doctor akielekea kule walikotokea wao, lakini akujari sana, akaendelea kumfwata nesi, ambae alienda na kusimama wenye ile meza, inayo tumika kama ofisi katika ile ward, kisha yule nesi akaonekana kufanya jambo flani la makusudi, lakumchelewesha Jackline, maana alianza kushughulisha kwa kupekua mallla huku mala huku, akitumia dakika kumi nzima, mala ikasikika sms kiingia kwenye simu ya nesi, ambae aliusoma ule ujumbe, kisha akamtazama Jackline, “haya dada weka hapa sahihi yako” aliongea yule nesi, akimwonyesha sehemu ya kuweka sahihi, kwenye form moja iliyopokwenye lile file alilokuwa nalo mkononi, alipokuja kumchukuwa Jackline ule chumbani, hapo Jackline akajuwa kuna namna, kwanini asinge mpa awe sahihi kule chumbani, Jackline aliwaza huku anaweka sahihi haraka haraka, kisha akamrudishia peni yake Nesi, “umesha maliza wai ukamtazame mwanao, yupo peke yake” aliongea yule nesi, akijifanya yupo busy na shughuli zake, hapo Jackline akatembea haraka haraka, kuwai chumbani kwake, alipoingia mle ndani ya chumba, Jackline akakutana na mambo tofauti na alivyo yaacha, kwanza kabisa akumkuta yule dada na mwane, pili alikuta mwae ame funikwa mwili mzima tofauti na walivyokuwa amemfunika yeye, akawai na kumfunua yule mtoto, kwanza aikutana na arufu flani kali ya marashi, ambayo akuwai kumpulizia mwanae, akamfunua miguu, akuona ile nyuzi aliyo mfunga kwenye kidole, pia mtoto alikuwa amekakamaa, akionyesha alikuwa amesha fariki mda mrefu uliopita, “mama yangu France kaibiwa” aliongea Jackline, huku akichana shuka na kujifunga kiunoni, mfano wa chupi flani, au kamawalivyo kuwwa wanavaa watu wa zamani, akavaa gauni lake alilikuwa amevaa wakati analetwa hospital, akachukuwa bastora yak echini ya godoro na kuikuki, kisha akaivuligia kwa kipande cha shuka, mwisho akachukuwa simu yake nakutoka nje ya kile chumba, mbio mbio, akaelekea kwenye ile ofisi aliyo mwacha yule nesi, ambae sasa alikuwa anahesabu fungu kubwa la fedha, “wewe unaenda wapi?” aliuliza yule nesi kwa sauti ya kibabeuku akatoka nyuma ya meza kumzuwia, akizani anapitiliza kwenda nje, huk akiziacha zile fedha pamoja na simu mezani, “wala usiwe na wasi wasi, nakuja kwako, nimeibiwa mtoto” aliongea Jackine kwa sauti ambayo usinge zani kuwa anatatizo kama hilo, “weee, unauakika ebu acha kusingizia watu mtoto ulie mkuta kiatandani ndie wakwako” alibwabwaja yule nesi, “dada naongea kwamala ya mwisho, yule doctor na yule dada wapo wapi?” aliongea Jackline safari hii akishindwa kuvumilia na kuonyesha hasira, “we binti unakichaa cha uzazi ngija niwa ite walinzi waku...” aliongea yule nesi huku akichukuwa simu yake toka mezani, alaki akuwai atakumalizia ata maneno yake, kwani alikatinzwa kwa ngumi nzito ya usoni, iliyotuwa katikati yam domo wa yule nesi, na kumrusha nyuma ya meza, kabla yule nesi hajapiga kelele, Jackline akaruja meza na kumuwai yule nesi, ambae alisha juwa kuwa leo ameingia cha kiume, “dada umekosea kuniibia mtoto, aliongea Jackline akiushindilia mguu wake mzima mzima shingoni kwa yule nesi na kubaki amekanyaga hapo hapo, akaichukuwa simu ya yule nesi, ambae alikuwa anaangaika kutafuta pumzi, kutokana na mguu wa Jackline kukita na kushindilia shingoni kwake, Jackline abonyeza simu ya yule nesi akatazama kwenu ukumbi wa sms, akaona iona sms ya mwisho imeandikwa ‘mtoe hapo njiani, sisi tupite’ hapo Jackline akaipiga ile namba, ikaita kidogo tu! na kupokelewa, “ndio tuna tka kwenye jengo ili, vipi kuna ishu?” iliongea sauti ya kiume, hapo Jackline akakata simu, na kumtazama yule nesi, ambae alikuwa anaonyesha ishara ya kuomba samaha, akishindwa kutoa sauti huku macho yame mtoka kweli kweli, “ufai kuishi shetani we” aliongea Jackline na huku akiuinua mguu wake, na kuushusha shingoni kwa yule nesi, nakufwatiwa na mlio wa kuvunjika kwa mti mkavu, ambao ulimfanyanesi yule aanze kutupa tupa miguu kama mtu mwenye ugonjwa wakifafa, huku damu ziki mtoka mdomoni na puani, ulimi na macho yame mtoka,  Jackline akaiacha simu ya nesi, na kuondoka maali pale kuelekea chini gholofa ya chini, huku akisikia simu ya nesi ikianza kuita, Jackline wakati anashuka ngazi kwa tahadhari,  lile basotra yake aliyo iviligishia shuka ikiwa mkononi, alitazama mlango wa kutokea nje na kuwaona wale watu wawili, yani yule doctor na yule mwanamke wakianza kutembea kuelekea nje kabisa, “washenzi nyie mme kwisha” aliongea Jackline kwa suti ya chini kidogo


 hapo Jackline akapandisha tena juu, mpaka kwenye meza ya yule Nesi, ambae sasa alikuwa amesha tulia, kakata roho, aka chukuwa lile file, ambalo alielekezwa aweke ashihi yake, akaliweka kwenye ile nguo aliyo jifunga ndani **** kwa upande wa Doctor fake na mzazi wake wauongo, baada ya kupiga simu kwa nesi ale wasaidia kupaa mtoto wa kutolea kafara, kwa kisi cha million tano, bila kupokelewa simu hiyo, wakaendelea kutembea kuelekea kwenye maegesho ya magari, wakizani labda simu ilijipiga yenyewe, ukweli ni kwamba huyu kijana Anson na na mwana dada Nuru, ni watu wanao jusisha na shuguli za uchimbaji wa madini huko tunduru mpakani na Msumbuji, na baada yakuona kuwa diri zao aziendi sawa, ndipo walipo enda kwa mganga wao kutafuta suluhisho, na mganga akawaambia kuwa wapeleke mtoto mchanga, kwa ajili ya kusafishia nyota zao, na shaliti kubwa nikwamba, mtoto huyo lazima awe mzima, na sio aliekufa, hapo wawili hao wakamtafuta nesi huyu wanae mfahamu toka siku nyingi, na alisha wai kuwasaidia mala moja, lakini ilikuwa ni kupata mtoto mfu, lakini safari hii waliambiwa wapeleke mtoto mzima ili akauwawe kule kule, kwa mganga, na walifanikiwa kuiba mtoto na sasa wakiwa na uakika, walikuwa wanaelekea kwenye gari lao aina ya Toyota stalet, walipo lifikia wakaingia ndani ya gari lao na kuliwasha, kisha wakaanza kutoka nje akilifwata geti kubwa la kutokea nje, bahati nzuri kwenye gate lakutokea hapakuwa na na upekuzi mkubwa, walirudisha card ya maegesho ya gari, na wakaruhusiwa kupita, “yew, tumefanikiwa” alishangilia Nuru kwa sauti kubwa, baada yakuliacha gate kwa atuwa kadhaa, iliyo mstua mtoto France, ambae alistuka na kuanza kulia, lakini ghafla wakashngaa kumwona mschana mmoja akiwa amesimama kati kati ya barabara, Amson akakanyaga breck kwanguvu sana na kusimama, wote wakamtazama yule mwanamke ambae alikuwa ameshika kitu kilicho viligiwa na kipande cha nguo nyeupe, huku mwonekano wake kama mtu hasie na akili timamu, utokana na nywele zake kuwa timu timu, na miguuni hakuwa na viatu, licha ya kunusulika kugongwa lakini chakushangaza yule mwanamke alikuwa ame achia tabasamu ambalo utazani, ni tabasamu la mjumbe wa kuzimu, hapo Anson akashuka toka kwenye gari kwa hasira kali sana, “we mbwa koko, ebu pisha hapo kabla sija kupasua pasua” aliongea Amson, akimsogelea kwa kasi yule mwanamke, ambae bado alikuwa amesimama mbele ya gari, lakini tabasamu likiwa limesha yeyuka usoni mwake, “nimechoka kuuwa, naomba uni patie mwanangu” alisema mwanamke huyu kwa sauti kari ya chini chini, hapo Amsoni akamkumbuka, huyu dada kuwa ndie yule walie mwibia mtoto, Nuru nae aliekuwa amekaa siti ya nyuma, alisha mtambua mwanamke huyu,  hapo Amsoni akaona kimesha nuka, swala ni kuingia kwenye gari na kumgongelea mbali, kisha waondoke zao, hapo Amson akageuka na kurudi kwenye gari, lakini hakuwai kuufikia mlango wa gari hilo, akastuka amesha shikwa bega, na yule mwanamke, kisha kwa itendo cha haraka sana yule mwana mke aka mvuta nyuma Amsoni, aliejibwaga chini, hapo yule mwanamke aka zima gari na kuchomoa funguo ya gari hilo, Amsoni akajiinua haraka na kumfwata Jackline Michael Nyati, kwa lengo la kumtandika ngumi, lakini kwa wepesi wa haraka sana, Jackline alimkwepa na kusababisha Amson, ajibamize kwenye gari lake, wakati wote ilisikika sauti ya mtoto France akilia, “sikia kaka, mpaka sasa  kifo chako kitakuwa cha maumivu makali sana” aliongea Jackline kwa suti ambayo kama ungesikia ungezani anatania, lakini Amsoni kama asie amini maneno aliyo ongea Jackline, alijaribu kurusha tena ngumi, lakini sarari hii Jackline akumkwepa kama mwanzo, akatumia mkono hule hule alioshikia funguo na kuupeleka usoni kwa Amsoni, na kutuwa kwenye usawa wa jicho lake la kushoto, ambapo Amsoni alihisi kitu kwenye mcha butu kikipenya kwenye jicho lake, na kusababisha maumivu makali, na ghafla jicho ilo lika tandwa na giza, “mama na kufaaaa” alipiga yowe Amson, huku akiinama na kuziba jicho lake, lililo tobolewa na funguo ya gari, “nime kwambia leo utakufa kwa machungu” aliongea Jackline huku aki mwinua Amson aliekuwa ameinama kashikilia jicho lake la kushoto, na kumvutia mlango wa nyuma wagari, kisha akaufungua, “dada samahani na omba usini uwe mtoto wako huyu hapa, aliongea Nuru, kwa sauti ya uoga iliyo tawaliwa na kilio cha uoga, “lakini Jackline kama vile hakusikia ali mnyooshe mkono wake wakulia ulio kamatia bastora iliyo viligiwa kipande cha shuka, akamwelekea mdomoni na kuizamisha kwenye mdomo wa mwanamke huyu, “tafadhari dada yangu tusamehe, usi mwu..” Ansoni hakumalizia maneno yake, alishuhudia mwanamke wake akifumuliwa kichwa na ubongo uki tokea kisogoni, na kutapakaa wenye kioo cha nyuma cha gari hilo, “sijawai kukutana na mwanamke katiri kama wewe” aliongea Amson, akijaribu kufurukuta, ili akimbie, lakini mkono imara wa Jackline ulikuwa umemkamata vyema, “sidhani kama dunia itaniesabia kuwa mimi ni katili, kwa kuwauwa nyie wakatili kuliko mimi” aliongea Jackline akimwinamisha Amson, kwa kumkandamiza chini, kisha akaiweka bastora yake kwenye mgongo wa kijana huyu karibu na iuno kisha akafyetua risasi moja iliyopenya kwenye sehemu hiyo ya mwili wa kijana huyu, “mama nakufaaa” alipiga yowe la uchungu kijana Amson, ambae alijuwa kuwa ameingia coo cha kike, “wamaume uwaga analia kimya kimya” aliongea Jackline huku aki mwongezea Amson risasi ya pega, nakumfanya Amsoni alie nakuongea kama mtoto anae adhibiwa kwa kukuwa ana iba mboga, “nisamehe mama yangu, nishetani tu! alinipitia, aikuwa hakili yangu” kelele za Amsoni zili wafikia walizi wa geti la kutokea muhimbili Hospital, ambao walipiga simu kituo simu kituo cha polisi kilichopo mle ndani ya Hospitali hii kubwa ya taifa, Jackline akaendelea na kazi yake, akamwongeza risasi ya kwenye goti, “haaaa tafadhari nimalizie we mwanamke shetani” aliongea Amson kwasauti iliyo jaa uchungu mkubwa, akisahau ushetani wake, akiuona wa Jackline, “usiJali nita kuuwa tu! lakini nataka ufe taratibu” alionga Jackline huku akimshika yule kijana mwizi wa mtoto, nakumwinua, kisha akaushindilia ule funguo ya gari shingoni mwake, na kuizamisha yote wenye koo, ikigota kwenye kishikio, nakusababisha damu ziruke kama kuna bomba lenye kasi kubwa ya maji limetoboka, “krooo kroooh kwoooh!” ali lalamika  kwa mikoromo ya hajabu, iliyo ashilia kuwa jamaa anaelekea kukata roho, Jackline Nyati akamchukuwa mwane, kisha akaanza kutembea kuelekea upande wa diamond jubilee, akiliacha gari na wenye gari pale pale huku funguo ya gari, ikiwa shingoni kwa Amson, baada ya kuakikisha amesha fika mbali, Jackiline akachumoa simu yake sehemu alipo iweka, ikiwa ni kwenye nguo aliyo jiviligishia ndani, bahadhi ya makabila wanaita chikwinda, akapiga simu kwa baba yake, na kumsimulia kilichotokea, nakumwomba msaada wa kuja kumchukuwa, baada ya kutembea atuwa chake Jackline, aliinua gauni lake na kuifadhi simu yake huku akichomoa lile file alilo lichukuwa mezani kwa yule nesi, mwizi wa watoto, ***** wakati huo Denis alikuwa sebuleni kwake, akinywa bia nyingi sana, akionekana ni mwenye furaha kubwa sana usiku ule, huku akimpigia simu rafiki yake mahadhi, ambae leo alikuwa amewai nyumbani kwake mapema sana, ni baada ya kukasirishwa, na kitendo cha jana kuzinguliwa na Janeth, Denis akamwelezea Mahadhi juu ya wake, kujifungua mtoto wa kiume, wakapanga wataenda pamoja saa sita mchana, kumtazama, wakati huo Denis akipanga kuwai saa kumi nambili za asubuhi, lakini wakati anaendelea kunywa pombe, akaona simu ya mke wake kiliita, “wewe bado ujalala tu?” aliuliza Denis baada ya kupokea simu ya mke wake, “nili taka niakikishe kaa hupo nyumbani au bar” alitania Jackline alie onyesha kuwa, yupo sehemu tulivu sana, “haaah! sina ujanja huo nipo tu nyumbani, vipi anaendeleaje mtoto, au kamelala” aliongea Denis, huku huku akicheka cheka, ni wazi alijawa na furaha kubwa sana, “kamelala, ila amesema hacha kunywa pombe sasa ulale” aliongea Jackline, akimtania mume wake, waliongea mengi, Jackline akimweleza Denis kuwa, yeye ameomba uamishiwa hosptali ya Matumaini, ya Doctor stellah, kutokana na huduma ya kule kutokuwa nzuri, kwake na kwa mtoto, “sasa usiku huu luksa amekupa nani usiku huu?” aliuliza Denis kwa mshangao, “wame niachia tu wakaniambia niseme nilizalia nyumbani” hapo Jackline, akamsisitiza Denis kuwa kesho akija aseme hivyo, kuwa alizalia nyumbani, **** siku ya pili magazeti mendi na maredio bila kusahau television, zote zilitangaza kuhusu mauwaji yaliyotokea cosovo Hotel, watu walionekana wakiwa wamesimama vikundi vikundi, wakijadiri swala hilo, ata waliopo maofisini, viwandani maskoni ata wanafunzi mashuleni walikuwa wakizungumzia swala hilo,  saa mbili asubuhi, insp Johnson akiwa ofisini kwake, anajiandaa kwenda kupokea taalifa ya uchunguzi, wa mauwaji ya mzee Alex na walinzi wake watatu, alipokea talifa ya mauwaji yaliyotokea jana  usiku Hospital ya mwimbili ndani ya hodi ya wazazi, na nje ya hospital hiyo, hapo Insp akona nibora awai huko hospital, kupata maelezo yakina, juu ya mauwaji hayo, nusu saa baadae insp Johnson akiwa na askari wake saba, alifika hospital ya muhimbili na kukutana na askari wa zamu, aliekuwepo jana usiku, mwenye cheo cha koplo, maelezo yake yalikuwa ni mafupi tu! kuwa jana akiwa amekaa pale kituoni na wenzake wawili, wakapokea simu toka kwenye gate kuu la kutokea magari, kuwa kuna gari lime simama, ila inasikika sauti ya mtu ana piga kelele na kuomba msamaha, samba mba na sauti ya mtoto mchanga, ndipo wao walipoenda na kukuta vijana wawili wakike na wakiume wakiwa wame uwawa, “tukapiga simu kituo cha polisi salendar bridge, wakaja polisi wa doria, na kuukagua mwili wa marehemu wote wawili, kisha wakaingiza ndani miili, nakwenda kuifadhiwa sehemu usika” aliendelea kusimulia yule Coplo wa polisi, akisema kuwa saa nane usiku walipokea taalifa nyingine, toka chumba cha wazazi, kwamba kunanesi amekutwa ameuwawa, kwenye sehemu ya ofisi ya ward hiyo ya wazazi, walicho fanya wao ni kumhoji nesi mwenzie, ambae alikuwa jengo la chini, upande wa mapokezi, alicho eleza mwenzie, ni kwamba,  mala ya mwisho aimwona mwenzie akiongea na watu watatu waliokuwa wame mleta mwanamke kujifungua, kisha yule nesi akaanza kuongea na mtu mwingine ambae ni doctor, lakini alikili kuwa yule doctor akuwai kumwona pale kwenye jengo la wazazi, baadae akawaona wale watu watau wakitoka na kuondoka zao, wakiwa na magari mawili tofauti, “nusu saa baadae nikiwa nasinzia nikasikia mlio wasimu, nikachungulia nikamwona yule kaka aliekuwa amevaa koti la doctor, akiwa amesha livua, yupo na mwanamke mmoja hivi wame beba mtoto mkoni, yule kaka akaongea na simu, akisema ‘ndio tuna toka kwenye jengo ili, vipi kuna ishu?” alisimulia nesi yule, akielezea tukio alivyo liona yeye, akaendela kusimulia kuwa baada yahapo akuwajali tena, maana aliowaona waktoka nje ya jengo hilo, la wazazi kisha wakapotelea kwenye magari, na dakika mbili baadae akawaona wakito, nesi yule alieleza kuwa saa saba usiku alipandisha ghlofa ya pili ili amstue mwenzie awapatie wagonjwa dawa, ndipo alipo mkuta ame sha uwawa, kitu cha kushangaza apakuwa na report yoyote ya kuonekana fedha, pia yule polisi akaeleza kuwa, tukio jingine ambalo hakuweza kulitambua vizuri, kuna mwanamke mmoja amekimbia na kuacha maiti ya mwanae kitandani, na mbaya zaidi hakuna kumbu kumbu yoyote, iliyo andikwa juu ya mwanake kulazwa chumba hicho ch VIP, pia yule koplo alimkabidhi  insp Johnson simu tatu za maremu wote,  “ok! naomba vipimo na harama za vidole katika miili ya maehemu” aliongea insp Johnson, ambae alionekana kuchanganyikiwa na tukio hilo ambalo mpaka hapo ni tukio moja, 


 Haraka sana akaitwa mkaguzi wa halama za vidole, ambae aliliport kwa insp Johnson David, akiwa na file mokononi mwake, pamoja na kifuko chenye vichwa kadhaa vya risasi, baada ya kusalimia kijeshi, yule mtaalamu wa ukaguzi wa miili ya malehemu, akaanza kumsomea insp matokeo ya uchunguzi, ambayo yalionyesha kuwa licha ya marehemu hawa wawili yani Amson na Nuru, kuuwawa kwa risasi lakini pia zimekutwa halama za vidole kwenye mwili wa Amson, ni Alama zina zo fanana na zile ambazo zimesha wai kukutwa kwa marehemu Kileo na wengine, “pia afande tumegundua kuwa risasi zilizo tumika ni za siraha aina ya pistor mic gurlily moder 99, toka England, yenye uzingo wa mm 5.5,” hapokwa haraka insp Johnson akavuta kumbu kumbu, juu ya siraha hiyo, ambayo iliingia nchini mwaka 1999, lakini aikuruhusiwa kuuzwa, wala kutumiwa na raia yoyote, akawaida, wala vyombo vya usalama, zaidi ya jeshi la ulinzi , tena kwaajili ya VIP protection, “nandio risasi zilizotumika kwenye tukio la Cosovor Hotel,” mpaka hapo insp alikuwa amesha  changanyikiwa, “inawezekanaje?” alijiuliza insp, “inamaana wanausika na huu mkasa?” kiukweli ni maswali yaliyokosa majibu, insp akakumbua kitu, akachukuwa simu ya kwanza ambayo iliwekwa kibadiko cha plast na kuandikwa kijana no 1, ikimaanisha ni Amson, akaingiza namba ya simu ya baba yake, akitegemea ilngetokea jina la baba yake, lakini aikuwa hivyo, akafanya hivyo kwenye simu ya pili, nayo ikawa hivyo hivyo, lakini ya tatu ambayo iliandikwa nesi, ilileta mafanikio kidogo, japo siyo aliyo yategemea, insp alibaada ya kukosa jina la baba yake, akaonelea atazame sehemu za meseji, ni kweli sms yakwanza tu katika simu ya nesi iliandikwa hivi, ‘tayari mtoe tupite’ akatazama mda ilikuwa yapata saa sita za usiku, akaanza kufwatilia sms nyingine, akitazama zilizo tumwa na kupokelewa, aliona sms nyingi zilizo ashilia kuwa kuna mpango ulikuwa unaendelea kati ya nesi na huyo mtu aliekuwa anawasiliana nae, ambae alimsevu kwa jina la, mtoto, maana alikuta sms moja iliyo msisitiza huyo mtu awai hapo hospital, kuwa kuna uwezekano wa kufanikiwa, ndipo insp alipo pata hamu zaidi ya kuipekua ile simu, atimae akaikuta sms iliyo tumwa siku iliyopita, ‘naomba msaada wako kama wakipindi kile, ila safari hii anaitajika mzima kabisa’ kengere ya tahadhari ika gonga kichwani kwa insp akaichukuwa ile namba ya simu iliyo andikwa kwa jina la mtoto, akaiandika kwenye simu yake kisha akaipiga, lakini akashangaa simu moja wapo kati ya alizo zishika ikaanza kuita, akaitazama ni kijana no1, akaikata ya kwake ili apokee kwanza ile, lakini bahati mbaya na ile ikakatika, akaipiga tena, na ile ikaita, hapo insp akatazama namba ya simu iliyo kuwa ina piga kwenye simu a marehemu, akagundua kuwa ni namba yake, kwa hiyo hii namba ni ya simu hii, inamaana aina ubishi kuwa nesi na awa wawili walikuwa na mpango mchafu juu ya kuiba mtoto?” aliongea insp Johnson kisha akamtazama yule dada nesi, ambae alikuwa anatetemeka kwa uoga, “wewe nesi nifwate” aliongea insp huku anainuka na nakutuka nje, akifwatiwa na dada nesi, waliongozana mpaka nje ya jengo, wakasogea pembeni kidogo, sehemu ambayo insp aliiona kuwa ni tulivu, “dada naomba upunguze wasi wasi, nachoitaji ni majibu machache tu ya maswali mepesi nitakayo kuuliza” aliongea insp Johnson na yule nesi akaitikia kwa kichwa akionyesha kuelewa alicho ambiwa na insp Johnson, “unasema uli waona watu wawili wakitoka hapa hospital,” aliuliza imsp Johnson, “ndio niliwaona, tena mala yakwanza yule kijana nilimwona anangea na Nesi” aliongea nesi huyu, huku hali ya uoga bado ime mganda, “je uli mwona dada mjamzito alie letwa usiku?” aliuliza insp akimtazama nesi, kwa umakini kuangalia majibu yake kama ni ya ukweli, “nilimwona na mimi nilishiriki wakati anajifungua” aljibu Nesi, akionyesha kuwa na uakika wa kitu anachoongea, “ok! kuna watu walimleta au alikuja mwenyewe?” aliuliza tena insp akiamini kuwa nesi huyu anampatia majibu ya uakika, ni kweli yule nesi alimweleza jinsi wakina mzee Nyati walivyo mleta, huyo mdada, wakijitambulisha ni wasamalia wema walio mkuta dada huyu anatafuta usafiri wa kujia hospital, na baadae akaja mume wa yule dada, na yeye ndie alie waruhusu waka mwone baada ya kujfungua, ila akika sana akarudi kwenye sehemu yake ya kazi na kumwacha marehemu nesi akiendele kumsimamia ward ile maana ili muusu moja kwamoja, “unaweza kukumbuka hao wasamalia walivaaje” aliuliza insp, hapo yule dada akaonekana kuvuta kumbu kumbu, kisha akaoneka kushindwa kuvuta kumbukumbu sahihi, “kiukweli yule baba kama sikosei, alivalia suti nyeusi, lakini yule mama alivalia nguo iliyotengenezwa kwa kitenge, sina uakika ni kutoka nchi gani, nilivutiwa nacho” aliongea Nesi, huku tayari mda mrefi Insp alikuwa amesha pata jibu, kuwa mzee Nyati ndie aliekuwepo pale Hosptal, usiku ule, na pengine yule mwanae Jackline, ndie aieletwa kujifungua, maana insp alijumlisha na tukio la kuuwawa kwa daktari wa magonjwa ya kina mama, Joseph Ndilane, pia kutokea kwa tukio jingine, siku hiyo hiyo kwenye hospital ya Dr Stellah, ambayo ni maalufu kwa maswala ya uzazi, “ok! Jackline amejifungua, na walitaka kumwibia mtoto, pasipo kumjuwa kuwa ni hatari” aliwaza insp huku anatabasamu, tabasamu lililo fwatiwa na kicheko kikubwa, **** Denis baada ya utoka hospital kwend kupeleka chai na nguo za mke wake, ambazo nyingi zilikuwa ni kanga na vitenge, akaelekea azini kuomba ruksa kwaajili ya kumwangalia na kumhudumia mke wake, alie jifungua, baada ya kupewa mapumziko ya week mbili, Denis akaondoka zake na kwenda kaliakoo, ambakp alifanya manunuzi ya nguo na vifaa vya mtoto, mda wote Denis alionekana kuwa mwenye furaha iliyo pitiliza, Deis akwa kaliakoo akasikia habari ya kutokea kwa mauwaji ya bwana Alex na walinzi wake, pale Cosovor, na pia habari nyingine ni ya kuuwawa nesi jana usiku, hospital ya muhimbili, lakini Denis akaliicukulia kama story ya kawaida ambayo amesha sikia mala nyingi sana, akaendelea na shughuli zake, ***** wakati Denis yupo kaliakoo mzee Nyati na mke wake walikuwa Matumaini Hospital, wakijadiliana jambo na mtoto wao, wazo la mama Jackline lilikuwa ni kwamba, Jackline na mwanae France waende Songea, ili mzazi akapate mda wa kupata huduma anzo stahili, kabla ya kulejea kumalizia kazi, ni kweli wakakubarina hivyo, kwamba wakina mzee Nyati waondoke na Jackline, ikapangwa mipango ya jinsi ya kumshawishi Denis akubari swla hilo, ndipo hapo, mzee Nyati alipo piga simu kwa Denis, “hallow baba, hongereni sana, wenzio ametutaalifu kuwa amejifungua salama” aliongea mzee Nyati, kwa namana ile ile ambayo Denis utambua kuwa baba mkwe wake ni mzee fukara wa huko kijijini, “samahani mzee, yani nilitingwa kidogo kuwajulisha, ni kweli amejfungua mtoto wa kiume tume mwita France” aliongea Denis, huku akikumbuka kuwa akuwai kuwajulisha wazee hao juu ya mbinti yao kujifungua, “umemkumbuka babu yenu, safi sana, lakini inabidi huyo ajae haraka sana ili aweze kufanyiwa huduma anazo stahili, maana huko mjini mpo wenyewe tu, alafu ndio mala yake ya kwanza kujifungua” aliongea mzee Nyati, na Denis hakuwa na pingamizi, akapanga kwenda kumjulisha mke wake juu ya safari hiyo muhimu, **** saa sita mchana, insp Johnson aliikuwa njiani anaenda igamboni mji mwema kwa mzee Soud, akiwa na lengo moja tu, kupajuwa nyumbani kwa mzee Nyati, kwa kisingizio cha kwenda kuongea nae, kumbe lengo lake likiwa ni kumvamia na kundi kubwa la askari kisha wammiminie risasi na kumpoteza kabisa, wakidai alijaribu kupambana na polii akiamini ndio utakuwa mwisho wa mauwaji na kwamba baba yake anakuwa ameepuka kifo, wakati anapanga hayo insp Johnson alijuwa fika kuwa lazima atumie hakili nyingi sana kuzunumza na mzee Soud ili akubari kumwelekeza nyumbani kwa mzee Nyati, na kisingizio kikubwa ni kuwa anaenda kuongea nae kutafuta .

 Nusu saa baadae insp Johnson alikuwa nyumbani kwa mzee Soud akiongea nae juu ya wazo lake la kukutana na mzee Nyati, “sikia Johnson, swala lako ni zuri sana na lina faa kumaliza huu mgogoro, lakini je una uakika kuwa, unania ya kuongea na bwana Nyati?” aliuliza mzee Soud huku akitabasamu, kisi cha insp kujistukia juu ya ule mpango wake wa kwenda kuvamia kwa mzee Nyati, “yesi mzee mpango wangu niuo, sababu ata wewe uliwai kusema kuwa, ndio njia pekee ya kumaliza tatizo hili, ila ikitokea kuwa tukishindwa kuelewana, nitatumia plan B” aliongea insp na hapo mze Soud alicheka kidogo, “vipi mzee mbona unacheka kuna tatizo, mbona unacheka?” aliuliza insp huku akionyesha mshangao kidogo, “sijajuwa hiyo plan B, lakini usi jali” aliongea mzee Soud huku akisimama na kueleka kwenye kabati, akachukuwa kalamu ya wino, na karatasi, akarudi mezani, na kuanza kuandika, kwenye lile karatasi, “hii ni namba ya simu ya mtu atakae kuwa mwenyeji wako” aliongea mzee Soud huku akiendelea kuandika, na hapo anime andika jina la mtaa, ambao ata mimi nilipoenda Songea, nilikutana na mtu huyo, na akanielekeza kwa bwana Nyati”  aliendelea kuongea mzee Soud huku akimkabidhi ile karatasi insp Johnson, ambae alilipokea na kulitazama kidogo, kisha akaliweka mfukoni, kisha akamtazama mzee Soud, “kuna lolote unataka unieleza au naweza kuondoka?” aliuliza insp Johnson, “tatizo lipo, nakuomba usije kujaribu kufanya jambo lingine lakipuuzi, maana ukijaribu kufanya kitu kingine chochote cha kipuuzi, utasababisha damu nyingi sana kumwagika, na mmoja wawatu watakao mwaga damu utakuwa wewe” aliongea mzee Soud hapo alikuwa akionea kwa umakini sana, akionyesha jambo analo ongea ni muhimu kulizingatia, “inamaana anauwezo wa kupambana na kombania ya polisi wa kutuliza ghasia?” swali hilo la Johnson lilimfanya mzee Soud acheke kidogo, usifikilie kumzibiti Nyati, kwa nguvu hiyo ndogo ya kijeshi” aliongea mzee Soud huku akiendelea ucheka, “nazani mzee Soud umeanza kusahau muhundo wa kivita, sija sema section, nimezungumzia kombania, na maanisha watu zaidi ya themanini” aliongea insp Johnson, akiwa na uakika mzee Soud akumwelewa mwanzo, “inawezekana wewe ndie ujanielewa vizuri, na inawezekana pia uja mfahamu vizuri mtu ane itwa Michael Francis Nyati” maneno hayo ya mzee Soud yalimstua kidogo insp Johnson, “inawezikanaje?” aliuliza insp kionyesha kuto kumwamini mzee Soud, “achilia kombania ya polisi, aliwai kuwaokoa watu sita wakiwepo baba yako na hao marehemu, katika kambi kubwa la jeshi, lenye silaha nzito, alitumia saa moja tu!” mpaka hapo insp Johnson alijikuta akisisimkwa na mwili wake, akatulia kidogo na kupitisha mawazo kichwani mwake, “mh! inawezekanaje, askari mmoja, kambi zima, hapana huyu mzee anajaribu kunitisha, ili nisiende kumkamata huyu mshenzi” aliwaza insp akisahau kuwa toka mwanzo wa upelelezi wake amekuwa akisaidiwa sana na mzee huyu, insp Johnson akukaa sana akaaga na kuondoka zake, akimwakikishia mzee Soud, kuwa lengo lake ni kufanya mazugumzo na sio kupambana na mzee Nyati, safari ya bwana Johnson ili kuwa ni ofisini kwake, kituo kikuu, kwenda kuonana na mkuu wakitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai, leo week end alikuwa ofisini kutokana na matukio ya mauwaji mfurulizo yaliyotokea usiku,  ***** saa nane mchana Denis alikuwa anamchukuwa mke wake kutoka hospital ya Matumaini kwa Dr Stellah, shangazi yake Jayden, (#shangazi anataka) na kuelekea nyumbani tayari kuandaa safari ambayo mwisho wasiku, walipanga waende wote wawili kwamba Denis mwenye ndie ampeleke, japo ilikuwa ni ngumu sana kwa Jackline kukubaliana na Denis swala hilo, lakini Denis alikuwa king’ang’anizi akitoa sababu za msingi ambazo Jackline alishindwa kutoa sababu za kukataa, kupelekwa na mume wake, ambae alisema kuwa kutokana na mtoto kuwa na umri mchanga sana, si vyema kusafiri nae kwenye basi, “lakini mume wangu aita kuwa vyema kwa wew kufika nyumbani kwetu, sababu bado uja peleka barua na kujitambulisha kuwa ni mchumba wangu, yani kwetu tuna sharia kali sana kwetu” aliongea Jackline, kwa sauti ya upole na upendo wa hali ya juu, “dah! sijuwi itakuwaje lakii siyo lazima nifike nyumbani kwenu, naweza kuishia ata sehemu nyingine kisha tukaomba mtu akupeleke” alitoa ushauri Denis, “ebu subir niongee na baba kisha nita kupa jibu, kama ata kurhusu ufike nyumbani au uishie sehemu nyingine” aliongea Jackline ambae alikuwa anafahamu kuwa wazazi wake walitegemea wasafari nae kesho yake, **** insp Johnso ambae alionekana na pilika nyingi sana, alienda ofisini kwa mkuu wa upelelezi, licha ya kumpa report ya vifo vya mzee Alex na wale wa Muhimbili, pia alimweleza mpango wake wa kwenda Songea, alimweleza kuwa anaenda kumkatama mzee mmoja anaeitwa Michael Nyati,  kuwa anamshuku mtu huyo, kuusika na mauwaji yaliyotokea jana usiku Cosovo Hoel, akisema kuwa sababu huyu mzee licha ya kutoweka baada ya tukio, pia ni asakari aliekuwa ana tafutwa na jeshi la ulinzi, baada ya kutoroka akiwa na silaha za kijeshi, insp aliomba apatiwe silaha na askari ili aweze kumkamata mshukiwa huyu, wa mauji yaliyotokea Cosovo, baada ya kueleza mpango wake, mkuu wa upelelezi alikubari mpango huo, na alimsisitiza insp kuwa mpango huo uwe wasiri, akamweleza kuwa wataanza maandalizi jumatatu, waliagana huku mzee huyu akionyesha kulizika na mpango wa insp Johnson, na aliombea ufanikiwe maana muuwaji huyu, alikuwa analizalilisha jeshi la polisi, na serikali kwa umla, hapo insp Johnson akaondoka zake, kuelekea nyumbani kwake akipanga kesho mapema kukutana na baba yake, akimwacha mkuu wa upelelezi akiwa ofisini kwake akipitisha mawazo kichwani mwake, mkuu huyu wa pelelezi alijaribu kuvuta kumbukumbu za mauwaji, yaliyofanywa na muuwaji huyu, ambae baadhi ya matukio yanaomyesha kuwa ni mwanamke, lakini anae tajwa ni mwanaume, “lakini huyu mtu anaonyesha kuwa anauwa waalifu” hapo mzee huyu mwenye nyota nyingi mabegani, aliwaza hayo huku akikumbuka mauwaji ya mchungaji chilumba, ambae aliuwawa guest House pale Kmamnga Plaza, “mchungaji na guest wapi na wapi?” aliendelea kukumbuka mauwaji ya vijana watatu, wenye visu, ndani ya chumba kilicho pangwa na mwanamke, “haya sasa na awa nao sijuwi walikuwa wana iba mtoto wa nini?, lakini kwanini yeye afanye kazi hiyo ya kuuwa waarifu?” ilo ndio lilikuwa swali la msingi, mwasho wa siku afande huyu akamaliza kwa kusema kwa sauti yachini na kusimama, “muuwaji wa wauliwa wote waalifu” mkuu wa upelelezi, akatoka nje na kuondoka zake, **** tayari Jackline alisha mpigia simu baba yake, na kumweleza ung’ang’anizi wa mume wake, kuwa anataka ampeleke mwenye Songea, hapo mzee Nyati kwakutumia hakili akajuwa kuwa endapo wata endelea kuzuwia Denis asiende Songea, watamfanya amtilie mashaka mtoto wao na kuanza kumfwatilia kwa ukaribu, kwania ya kupafahamu kwao na wazazi wao, pengine waliofia Denis anaweza kuzani Jackline anampango wa kuto kumtambulisha kwao, na kuachana nae katika siku za mbele, hivyo walikubari kuwa kijana huyu aende Songea, ila mzee Nyati akapanga ya kwake, ili Denis asifahamu ukweli juu ya familia yao, **** siku ya pili safari ilianza mapema sana, gari aina ya Toyota noah lili sheheni mizigo, ambayo mingi ilikuwa ni zawadi kwa baba na mama, Jackline akiwa ameacha zana zake amesha zihifadhi vizuri, sababu pale nyumbani walimwacha kijana mmoja ndugu wa boss wake Denis, alinde nyumba, safri aikuwa na tatizo lolote, japo ilikuwa ni a mwendo wa taratibu sana, kiasi chakuwa fanya wachelewe kufika Songea, ambapo waliingia saa saba usiku, wakapitiliza na kuelekea kijijini kwa kina Jackline, ambako ni pembeni ya mji, huko walipokelewa na mzee mmoja wa makamo, alie jitambulisha kuwa ni baba yake Jackline, pamoja na kijana mmoja, usiku ule Denis akuweza kuona mazingila ya kijiji kile, ila asubuhi siku ya pili Denis alijikuta akiamka toka kwenye nyumba ya udongo, yenye ukubwa wa wastani, iliyo zungukwa na migomba ya ndizi, na mazao mengine ya msimu kama mboga mboga mboga na nafaka, jilani hapakuwa na nyumba nyingine zaidi aliweza kuona kitu kama mtaa mdogo, ulio zungusiwa uzio mkubwa sana katikati ya msitu, alipo uliza akaambiwa kuwa ile ni nyumba ya tajiri mmoja wapale mkoani, asubuhi ile pale nyumbani, zaidi ya Jackline na yeye mwenyewe palikuwa na binti mmoja mdogo kidogo, alie valia kama wakazi wengine wa vijijini hapa Tanzania, tunavyo zowea kuwaona wakivaa, kwa kipindi kile) “baba na mama wapo wapi?, alafu na yule kijana alie tupokea jana usiku, pia simwoni” aliuliza Denis, “waliondoka jana usiku, awa ruhusiwi kukaa pamoja na wewe, mpaka utakapo jitambulisha, hivyo awata rudi mpaka uondoke” aliongea Jackline wakati huo walikuwa wana kunywa uji na na viazi vitamu, “aina tatizo wacha niende nikafanye utaratibu wa kuwajulisha ndugu zangu ili waje walete barua, maana sasa itakuwa kasheshe, unajuwa nimeshindwa kuwa kabidhi zawadi zao” wawili awa waliongea mengi sana, wakijadiliana swala hilo, japo upande wa Jackline alisisitiza kuwa, Denis asifanye lolote, mpaka yeye atakapo rudi Dar, ***** siku hiyo ya jumapili, Insp Johnson aliamka mapema sana akiwa na mke wake, wakaenda kanisani, na baada ya kumaliza ibada, wakaenda nyumbani, kwa wazazi wa insp Johnson, huko kinyelezi mwisho, bahati ilikuwa upande wa Johnson, maana walimkuta mzee Masinde ndio kwanza anapata supu, aliyoandaliwana mke wake, ni baada ya mzee huyu leo hii kuamka akiwa amekosa nguvu za mwili, maana siku iliyopita akuweza kupata muda na hamu ya kula, kutokana na kunywa pombe kali nyingi sana, baada ya kusalimiana, mke wa insp Johnson akaenda upande wa jikoni, akikaa na mama mkwe wake, na Johnson akabakia na baba yake, ambae kumtazamo, alionekana kukata tamaa, pale sebuleni, insp alimweleza baba, kuwa ame pewa uamisho wa muda kwenda Songea, kumchunguza Michael Nyati, “mwanangu sikiliza unachotaka kukifanyani kitu cha hatari sana, nakuomba kataa hiyo safari” aliongea mzee Masinde kwa msisitizo, “kwa nini baba, lazima huyu mtu akatwe na ikiwezekana amalizwe kabisa, maana ni hatari sana kwako,” hapo yakaanza majadiliano, huku mzee Masinde akisisitiza kuwa Nyati siyo mtu mzuri, ata kidogo, endapo atagunduwa kuwa anafwatiliwa, ni wazi kuwa atapoteza maisha ya Johnson, baada ya majadiliano ya mda mrefu wakakubariana kuwa, litakapo kuja jukumu la kumkamata mzee Nyati, basi Johnson akae mbali na eneo la tukio, ***** mpaka juwa linazama jumapili ile, Jackline na Denis, walisha kubariana kuwa siku inayo fwata Denis arudi Dar, ilikuwapa nafasi wazee waje wamwone mjukuu wao, na kweli siku ya pili ambayo ni jumatatu Denis aiondoka mapema sana, toka Songea, akiwa meshindwa kukaa na kuongea na wazazi wa Jackline, kutokana taratibu za kimila za wakina Jackline, ***** huku nako siku saa mbili na nusu mkuu wa kitengo cha upelelezi alikuwa ofisini kwa General of Polisi (GOP) akimweleza juu ya mpango wa kwenda zingila na kumkamata Michael Nyati, huku mkuu wakitengo cha upelelezi akimweleza GOP jinsi wanavyo muusisha mzee huyo na matukio ya mauwaji, yanayo endelea ndani ya jiji la dar, mkuu wa jeshi la polisi hakuwa na kipinga mizi juu ya jambo hilo, aka mpa kibari cha kuandaa askari na silaha, kwaajili ya zoezi hilo la kumtianguvuni mzee huyo hatari sana, ***** kazi ya maandalizi ilitumia siku saba, wakichuliwa askari polisi stini, toka mikoa mitatu, Mbeya Lindi na Mtwara, wakichaguliwa skari wenye uwezo mkubwa sana kimapigano, taalifa ilitumwa kwa kamanda wapolisi mkoa wa Ruvuma, akielezwa kuwa kuna askari polisi wata ingia mkoani kwake kwa kazi maalumu, na kwamba wasi buguziwe,wakwanza kufika Songea alikuwa ni insp Johnson na PC Busungu, ambao walitangulia kwaajili ya kwenda ufanya uchunguzi, baada ya kufika Songea  moja kwa moja insp Johnson alienda kwenye mtaa ulio andikwa kwenye namba ya simu aliyopewa na mzee Soud, insp akiwa kwenye mtaa wa Lizombe, mtaa wenye maduka makubwa sana, akapiga ile namba ya simu aliyopewa na mzee Soud, “hellow unaongea na felister, nikusaidie tafadhari” ilikuwa nisauti tamu ya kike iliyo mfanya Johnson asisimkwe kidogo, kabla ajamkumbuka yule mwanamke hatari sana, alie wi kumshuhudia akitembeza mkong’oto “na itwa Vasco, nipo   mtaa wa Lizombe, naitaji kukuonana na wewe” aliongea insp Johnson ambae alikuwa jirani kabisa na Pc Busungu, 


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.