STORY NA Mbogo Edgar
Whatsapp 0743632247 (kwamatumizi ya ofisi tu)
ILIPOISHIA SEHEMU YA EPISODE 7 : “zaidi ya salama, siunajuwa mimi zaidi ya kikosi cha makomadoo” alijibu Jackline kwa kujiamini, “hacha utani mwanangu, atakama ni komadoo sijuwi kitu gani, lakini kumbuka, ukali wote wakiu lakini mbele ya maji uonekana mjinga, namaanisha umeziona sikuzako, maana sielewi jinsi unavyo hema sielewi elewi” hapo Jackline akatulia kidogo na kushusha pumzi kwa nguvu, ENDELEA .......
Kisha kwa sauti ya upole na unyonge akasema “sijaziona mama” hapo Jackline alimsikia mama yake akitoa mguno wakicheko, “nilijuwa tu! maana tokea tulipo ongea asubuhi, nilihisi aupo sawa, hen! niambie ina mda gani?” aliuliza mama Jackline, inamiezi mitatu” alijibu Jackline kwa sauti iliyo ashilia uoga, “umesha anza klinic?” aliuliza mama Jackline, “hapana bado sijaanza” alijibu Jackline, ***** kiukweli usiku huo ulikuwa ni mjadala wa hiyo mimba ya Jackline, wakati baba yake akisema hiyo mimba ikatolewe, huku mama yake alisema hisitolewe, mabishano yaliisha saa saba usiku, wakikubaliana kuwa Jackline ailee hile mimba mpaka atakapo jifungua, ikiwa pamoja na kupumzisha mauwaji ya maadui zao, mwisho mama Jackline akampigia simu mwanae na kumsisitiza kuwamakini wakati wakuilea hiyo mimba, na kaanza klinic mala moja, ila katika majina yake, asijiandike kuwa n Jacklin Nyati, aandike Jackline Francis, ***** siku ya pili asubuhi na mapema isnp Johnson alijihimu, kwenye gereza la ukonga, na kukutana na mkuu wa gerezaakaomba kuonana na mfungwa mmoja anaeitwa Majaliwa, bwana jela akamwita askari anaeusika na kkujwa mfungwa flani yupo selo gani na anakosa gani, akamkabidhi insp Johnson amsaidie kuongea na huyo mfungwa alie fungwa kwa kosa la kuiba mbuzi wanane, mda mfupi baadae,insp Johnson alikuwa ndani ya chumba cha kuongea na wafungwa, akiwa amekaa kwa kutazama na Majaliwa, wakitenganishwa na meza kubwa “mimi naitwa insp Johnson, najuwa wewe unaitwa Majaliwa” aliongea Johnson huku akimtazaa kwa umakini kijana Majaliwa, ambae alikuwa ametulia akimtazama insp kwa macho ya udadisi, maana akujuwa shida ya polisi yule mwenye nyota tatu, “nikweli afande naitwa Majaliwa, sijuwi nikusaidie nini muheshimiwa, maana kifungo changu kinakaribia kuisha, sijuwi kama kana kunakosa jingine nililifanya?” aliuliza Majaliwa huku, akijitaidi kuficha mapengo yake, yaliyo tapakaa mdomoni“bwana Majaliwa kabla atujaaza kuongea, natamani kujuwa hayo makovu na mapengo ume yapataje pataje?” aliongea insp Johnson akijizuwia kucheka, kwani alithibitisha maneno ya yule askari sajenti, kwamba Majaliwa amepondeka usoni, kwanza kabisa Majaliwa alianza kwa kuachia kicheko, “ni mambo ya ujana haya afande achana nayo” aliongea Majaliwa, ambae leo hii kupiga mluzi ilikuwa ni kazi ngumu kwake, “ulifumaniwa nini?, alafu unasema mambo ya ujana, wakati sasa ndio kijana” aliuliza insp Johnson kwa sauti inayojenga urafiki, “afande bwana, story yenyewe ni ya aibu, nilipigwa na demu mmoja hivi, kipindi hicho tupo shuleni” alisimulia Majaliwa, akimsimulia insp Johnson, jinsi sikuile ilivyo kuwa, Majaliwa alieleza kila kitu, kuhusu siku ile akiwa na rafki zake, Kadoda na Festor, wakimvizia binti mrembo sana, aliekuwa anajifanya mgumu wa kukubari wanaume, lakini kilicho wakuta awakutegemea kukipata kutoka kwa mschana kama yule, (soma kuanzia sehemu ya 8) insp Johnson akuwa na haja ya kusikiliza marudio ya story ile, “ok! unalikumbuka jina la huyo mwanamke alie wavuruga, na anafanya kazi gani siku hizi?” aliuliza insp Johnson akijifanya kuvutiwa na ile story, ambayo aliamua kuifwatilia baada ya kusikia kuwa imetokea Songea, “mala ya mwisho yule demu nilimwona akiwa anasoma form six, baada ya hapo niliamia mtwara, sija mwona tena yule mwanamke anaitwa Jackline, ni mtoto wa mzee mmoja hivi, anaitwa Nyati” aliongea Majaliwa, na kumfanya astuke kidogobaada ya kusikia jina la Nyati, “unauakika kuwa huyo binti ni mtoto wa mzee Nyati na ilo ndilo jina lake?” aliuliza insp kwa namna ya kuitaji uakika, “nawafahamu vizuri sana wakina Jackline, tena mama yake anaongea rafudhi ya kikongo hivi” aliongea Majaliwa akionyesha msisitizo, kuwa anauakika na anacho kisema, insp akaingiza mkono mfukoni kwake na kutoa karatasi moja lililo kunjwa vizuri kabisa, akalikunjuwa na umwonyesha Majaliwa, “he! uana mchongo gan na huyu demu, unayo mpaka picha yake?” alistuka sana Majaliwa baada ya kuiona picha ya Jackline, kwenye lile karatasi, “nili wai kukutana nae mwaka moja ulio pita nimetokea kumpenda sana huyu mwananmke nataka nifike kwao nikatoe mahali,” alidanganya insp, “mh! sijuwi, kwajinsi navyo mjuwa huu demu inajibi ujipange kweli kweli” aliongea Majaliwa akionyesha kuwa aikuwa kazi ndogo kumpata Jackline, “kwani baba yake anafanya kazi gani?” aliuliza insp Johnson, “kwakweli yule mze ni mfanya biashara wakawaida tu, japo anaonekana ni tajiri sana” aliongea Majaliwa, “we unazani huyu Jackline alifundishwa nanani kupigana?” aliuliza Johnson, ambae sasa alikuwa amesha pata mwanga wakujuwa mengi juu ya muuwaji anae wamaliza wakina mzee Masinde baba yake, “kwakweli akuna mwenye uakika, japo kuwa wengi wanahisi kuwa anafundishwa na baba yake, maana nilwai kusikia kuwa yule mzee aliwai kuwa askari jeshi” mpaka hapo insp Johnson alikuwa amesha pata uakika wa kile anacho kitafuta, hapo akawaza, “nikienda kwa mzee Soud na kuweleza niliyo yasikia, laima tutapata ufumbuzi” **** mpaka kufika saa mbili asubuhi Denis alikuwa haja zinduka, na alisha mwaga mkojo lita kumi, kiasi cha kumfwanya Jackline ahisi mume wake ata ishiwa maji mwilini, saa tatu na nusu ndio mda ambao wakina mahadhi, walisimamisha gari nje ya nyumba ya Denis, baada ya kuona kuwa na leo akuja kzini, awakupiga simu kuwajulisha ujio wao, sababu Mahadhi alijuwa kuwa Denis asinge kubaliana na ujio huo, japo ilikuwa ni ngumu sana kwa Jackline, lakini alimtambua Mahadhi, aliwa karibisha ndani, na kuwaeleza kuwa Denis usiku wa juzi, alirudi nyumani hapo akiwa amelewa sana, akasimamisha gari na kulala hapo hapo nje ya nyumba, mpaka yeye aipo mbeba na kumwamishia ndani, ambako amelala toka juzi mpaka leo ajaamka, wakina Mahadhi na bosi wake walikaa pale mpaka Denis alipo zinduka saa tano, **** saa moja jioni baada ya kuaga mwili wa askari Kessy uliosafirishwa kwenda kwao singida, insp Johnson akwenda nyumbani kwake, alinyoosha kigamboni kwa mzee Soud, ambapo alitumia lisaa limoja na nusu kufika, “poleni kwa msiba wa askari mwenzenu” alisema mzee Soud baada ya insp kumsimulia juu ya matukio ya juzii na jana, “lakini kwanini amja tangaza, maana leo tena nimesikia tukio la kuokotwa watu wawili, huko kisopwa,” aliuliza mzee Soud, “sidhani kama ingekuwa vyema kutangaza lile tukio, la askari wetu, ila kuhusu hao wawili na mimi nimesikia juu juu nikiwa msibani, ila inasemekana marehemu wametambuliwa, kuwa ni matapeli wakubwa sana waliokuwa wana tafutwa na jeshi la polisi kwa mda mrefu sana” alisema Johnson ambae bado alikuwa ndani ya sale za kazi, “ok! bwana Johnson, nazani umekuja na jambo jipya,
Aliongea mzee Soud, huku ajikijiweka sawa, “nikweli mzee wangu nimekuja na jambo jipya,” aliongea Johnson huk akitowa karaqtasi lake lenye picha ya Jackline, aliyo ipata siku ile pale Full Dose pub, akampatia mzee Soud, “huyu ndie muuwaji wetu, japo aija sibitishwa, anaitwa Jackline Nyati, ni binti hatari sana, mwenye uwezo mkubwa sana wa kimapigano yakutumia mikono, na silaha” mzee Soud Hassan, alitazama ile picha kwa dakika kadhaa, kisha akampatia Johnson.
“tena atakuwa na hakili kuliko baba yake” aliongea mzee Soud, akimtaazama insp Johnson, “kwahiyo mzee wangu aina siri tena, kuwa Michael Nyati yupo hai, na ndie muusika wa mauwaji haya” aliongea insp huku analikunja lie karatasi na kuliweka mfukono mwake, “juu ya uhusika wake nilisha juwa miezi sita, baada ya kupotea kwake, na kuhusu kuusika na mauwaji hilo ata wewe ulisha lifahamu mapema sana, ata baba yako analifahamu” alijibu mzee huyo kwa uakika kabisa, “ilo ni kweli mzee Soud, mimi nilikuwa na wazo moja” aliongea Johnson.
“wazo jingine zaidi ya kumshawishi mzee wako aseme chanzo ayayote ili tujuwe na mna ya kuyamaliza?” aliuliza mzee Soud, ambae siku zote aliamini kuna jambo ambalo wakina maaasinde walimfanyia Nyati, ndio maana ame amua kuchukuwa maamuzi mazito ya kutoa roho zao, “hilo mzee wangu nime shindwa kabisa, nili waza kulishilikisha jeshi la ulinzi, kumtia nguvuni bwana Michael Fransis Nyati, hiyo itasaidia kummtuliza mwanae Jackline, asiendelee na mauwaji” aliongea Johnson, kwa umakini wa hali ya juu.
“mh! kivipi tena?” aliuliza kwa mshangao mzee Soud Hassan, “nakumbuka uliwai kuniambia kuwa, bwana Nyati anaesabika kuwa ni mtoro jeshini, kwa hiyo akionekana, lazima atakamatwa kwa kuli uni jeshi” aliongea bwana Johnson huku akitabasamu, akiamini mbinu yake itafanikiwa, “hili ni wazo zuri, lakini limesha pitwa na wakati,” aliongea mzee Soud, huku akiaachia kicheko kidogo, “kivipi mzee mbona sikuelewi, maana taratibu zina sema utoro jeshini, ni kosa la usaliti” ilikuwa sauti ya mshangao, ya insp Johnson ambae alianza kumtilia mashaka mzee Soud, pengine anausika kwa namna moja au nyingine.
“labda nikukumbushe bwana Johnson, jeshi litamweesabu utoro askari yeyote kwa miezi kumi nambili, adi ishilini na nne, kish lita mfuta kwenye nguvu ya jeshi, na kuto kuesabika katika idadi ya wanajeshi nchini, kwahiyo jeshi lilisha mfuta bwana Nyati, miaka mingi iliyo pita, pengine ata wewe ulikuwa ujaanza shule ya msingi” hapo Johnson akachoka kwa majibu ya liyo nyooka toka kwa mzee Soud.
“kwahiyo mzee akuna tena njia nyingine ya kufanya, ili kumaliza ili tatizo?” aliuliza mzee Johnson ambae kiukweli alionekana anaitaji msaada waharaka sana, juu ya swala hili, “njia nyingine zaidi ya kumshawishi baba yako aeleze ukweli, ili tukae meza moja na Nyati tuyamalize, ni njia hatari sana, zitakazo poteza roho za watu wengi zaidi” alisema mzee huyu ambae utumia busara mda wote, “yani hilo swala lina kuwa ngumu sana kwa baba, sijuwi wali mfanya nini huyu bwana Nyati?” aliongea Johnson, kisha wote wakatulia kwa dakika kadhaa, kama wanawaza jambo flani.
“sikia kijana baba yako na yeye ni binadamu, kumbuka ladhima kuna jambo ambalo walimfanyia Nyati na kulidanganya jeshi, hivyo anaofia kuwa, endapo ata sema ukweli ladhima ataadhibiwa kwamujibu wa sharia, hivyo awezi kusema ukweli” alitulia kidogo mzee Soud, Johnson akiwa bado amemkazia macho, akimsikliza kwa umakini, “chakufanya mlinde baba yako, na wenzake watatu waliobakia, ongeza askari kanzu wakutosha kwaajili ya upelelezi, chagua askari wenye uwezo mkubwa wa kimapigano, nazani utaweza kujaribu kufikia malengo” alishauli mzee Soud.****
Leo mzee Masinde na wenzake wa wili, yani Alex na Kaijage, wali endelea kushinda majumbani mwao wakiwasiliana kwa njia ya simu, “nasikia yule muuwaji leo amechinja askari” ilikuwa sms toka kwa mzee Masinde.
“hivi mna fahamu kuwa huyo muuwaji ni wakike?” aliuliza mzee Alex, “siyo mwanamke sema binti mrembo” aliongezea mzee Masinde, “inakuwaje binti mrembo kama huyo awe muuwaji hivyo?” aliuliza mzee Kaijage, “kwani urembo ni inshu?, hivi unajuwa kuwa kuwa ata israel ni malaika, na akuna malaika mwenye sura mbaya” hapo wote waka tuma sms za kucheka “hahahahahahahaha” kisha bwana Alex, akaandija sms, “bwana Masinde, ebu ongea na vijana, waendelee kumsaka huyo kahaba” kisha akaituma kwa wote wawili, ndivyo walivyo fanya siku zote katika kuwasiliana, licha ya kuwatuma vijana wao kuendelea na uchunguzi wa kina juu ya adui yao.
lakini sikuzilienda bila mafanikio, na wao kuendelea kujifungia ndani ya majumba yao, wakienda kuwasiliana kwa simu zao, huku siku moja moja waki kutana kwa mda mfupi, na kuondoka zao mala moja, wakilindwa na vijana wao ambao sasa walisha pungua na kubakia sita, pasipo kujuwa kuwa, kuna sakari polisi watatu akiwemo PC Busungu na wenzake, walio ongezwa kuwa fwatilia wakina mzee Masinde na wenzake, walikuwa wana wafwatilia kwenye nyendo zao zote, asa kwa siku moja moja ambazo walikuwa wana kutana, japo kazi ilikuwa ngumu sana kwao, maana mda mwingi wazee awa walishinda ndani ya majumba yao makubwa yenye uzio waukuta mkubwa, nakuwa fanya wao washinde wakizurula maeneo hayo, bila kupata jambo la msingi, litakalo wasaidia kufanikisha kazi yao, ya uchunguzi.
wakati huku bwana Johnson alipoona miezi mitatu imepita bila kutokea mauwaji ya aina yoyote, na bila kupata taalifa yoyote ya kumsaidia, akaona bola awa pumzshe askari wake, ambao waliacha kuwafwatilia wakina mzee Masinde ambao anao walishaanza kudharau uwepo wa muuwaji karibu yao, nakuanza kutembea bila wasi wasi, wakitumia ulizi wa wale vijana wao sita wakigawana wawili wawili.****
Upande wapili nako, mambo yalikuwa moto, miezi sita ya ujauzito, ilikuwa juma nne asubuhi, Jackline Michael nyati, alikuwa ametulia sebuleni kwake, tumbo limetangulia na kuonekana wazi wazi, kwa ukubwa wake, mala kwa mala kilichezea chezea, na kusikilizia mtoto akicheza, hapo anatabasamu kidogo, kisha anaendelea kuchezea tumbo lake, ni michezo yake ya kila siku anapokuwa peke yake kama hivi, huku macho kwenye Tv, na kutuma sms kwa mume wake, wakipeana maneno ya kimahaba, unge sema nio wame kutana.*****
Denis mida hii alikuwa pamoja na Mahadhi wanaelekea kwenye supu, kwenye mgahawa wa mama bupe, wakati wana karibia kwenye mgahawa huoo ambao ulikuwa umefulika watu, huku wana piga story zao, kama kawaida Mahadhi alikuwa akisimulia jinsijana alivyo weza kukutana na mtoto wa jirani yake na kumwingizia dudu, “mwanangu mtoto mtamu yule, yani aee nipa vitu ambavyo ni tofauti na umri wake,” aliongea Mahadhi akisifia utamu aliopewa na huyo binti, “saa wewe ulipo mtongoza ulitaka ukamfundishe au ulitaka akakupe mambo?” alijibu Denis ambae siku za hivi karibuni alionekana kuto kupenda tabia ya mwenzie ya kuendekeza ngono mseto.
“habari yako kaka Denis” wote walistushwa na sauti tamu sana yakike, ikitokea nyuma yao, iliyo wafanya wageuke kumtazama mmiliki wa sauti hiyo, naam wote wali shangazwa, ka kile walicho kiona mbele yao, alisimama binti mmoja mrembo sana mwele umbo la wastani na urefu wa kueleweka, mweusi wa kung’aa, akiwa ameachia tabasamu lililo dumu na kupendeza kwenye midomo yake y wastani yenye lips pana za kuchongoka, nakuruhusu meno yake meupe kuonekana kidogo.
“safi dada yangu tuna fahamiana sijuwi?” aliuliza Denis akimtazama yule dada hulu akiachia tabasamu la ujirani, “hapana kaka yangu, ilanime pata kuku fahamu kwa kupitia kazi ulizo zifanya” aliongea yule dada kwa sauti ile ile tamu ya kuamsha dudu, ambae alikuwa amevalia suluali ya kitambaa chepesi cha suti nyeusi na shati la brue, ameninginiza mkoba mweusi na chini alivalia viatu vyeusi, vya chini, (flat shoes) vya kudumbukiza.
“ok! dada yangu, umekuja kiofisi au kimatembezi maana sisi tunaelekea kupata chochote?” aliongea Denis, akionyesha uchangamfu, “ninashida moja ya kikazi, lakini nilitaka tuifanye nje ya ofisi, kama auto jali” aliongea yule dada ambae kila kitu chake kizuri, kuanzaia nywele mpaka macho na pua zilizo pamba uzo wake wa mduara wa yai, Denis akamtazama Mahadhhi ambae alikuwa bado ame duwaa, akiamshangaa yule mwanake, pengine ata mazungumzo yale akuyasikia, “ok! aina noma tena nipo na huyu mwenzanu, nazani akita aribikakitu” aliongea Denis, huku akimpiga bega Madha kwa nguvu, ili kumstua maana alimwona jinsi alivyo kuwa ameduwaa.
“nashukuru sana kaka yangu maana nina itaji mchoro wa jengo moja kubwa la biashara, lenye ukumbi wa mikutano na ofisi sita, kama auto jali nionyeshe sample za michoro ya majengo hayo,” hapo Denis aka mtazama Mahadhi, akamwona bado ame duwaa, akatazama tena yule mwanake, “ok! panga siku uje, ili uangalie maana sija beba mchoro wowote, mpaka nipande ofisini” alisema Denis, lakini yule dada akaonekana kuto kukubariana na Denis
“sito kuwa na siku nyingine kesho nasafiri, kuelekea mkoani boss wangu anaitaji niende na mchoro huo” aliongea yule dada akionyesha msisitizo wa kuondoka na huo mchoro, “ok wacha nipande nika chukue, sijuwi utanisubiri wapi?” aliongea Denis, safari hii akumtazama Mahadhi, maana alimwona rafiki yake huyo, yupo mbari sana kimawazo, “hapana husiangaike sana, kaka Denis, unaweza kuendelea na ratiba zako, ila nikuachie namba ya simu, utanipigia ili tukutane, kama autojali utanikuta Green Hotel pale Ubungo,” aliongea yule dada ambae alionekana kuwa ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa wakifedha, au kazi nzuri sana.
“ok! sawa aina shida, dada yangu inaoneana hupo pazuri sana, kama umefikia pale” aliongea Denis wakacheka kidogo, kicheko kilicho sababisha uzuri wa yule mwanamke kuongezeka maladufu, “hahahaha hapana bwana mbona kawaida tu, aya kaka yangu baadae basi” aliongea yule dada mrembo na kuanza kuondoka, akiwaacha wawili awa wakimshangaa, lakini baada ya kutembea kidogo yule dada akasimama na kugeuka.
“hooo!kaka Denis, nime sahau kitu sijuwi kwanini uni kumbushi” aliongea yule dada, akiwafwata wakina Denis pale walipo kuwa bado wame simama, huku akipekua pekua mkoba wake mdogo , akatoa kad yenye namba za simu na kiasi cha fedha kama lakimoja hivi, akamkabidhi Denis, “hiyo ni namba yangu ya simu, na hizi fedha zitakusaidia kuweka mafuta ya gari,” Denis akapokea zile fedha huku anashangaa, fedha zote hizi dada yangu, wakati atakazi ynyewe bado?” alisema Denis akizitazama zile fedha, kisha akamtazama yule dada, ambae na yeye alikuwa anamtazama, kwa macho ya ushawishi na tabasamu la kivivu,
“usijari huo ni mwanzo tu!, ukija hotelini uta furahi zaidi,” aliongea yule dada kwa sauti laini na tamu zaidi ya ile ya mwanzo, kia akaanza uondoka, “hooo! kunakitu kingine nilisahau, ujuwe unanichanganya sana kaka Denis, wewe ni mtanashati sana” aliongea yule dada akisimama tena na kumgeukia Denis, kisha akaongea kwa sauti ya chini na yakunong’ona, “jitaidi uje peke yako, maana huyu mwenzio simuamini”
ITAENDELEA...
Your Thoughts