DADA MDUNGUAJI
EPISODE 15
FINAL EPISODE
STORY NA Mbogo Edgar
Ilipoishia episode 14 : “simama hapo hapo Jack, ukipiga atuwa moja tu! nakufyetua” ilisikika sauti kali ya insp, ambae alikuwa ameunyoosha mkono wake wenye bastora, kumwelekezea Jackline, ambae alitulia kidogo na kushika kitasa cha mlango, na kufungua mlango, hapo ikasikika, endelea ........
‘kacha!’ ikiashiria kuwa, insp aliminya trigger (yani kifyetulio) pasipo kutoka risasi, kumbe wakati huo mke wake ambae wakati anakuja mume wake, alimsikia na kutulia kitandani, akijuwa kuwa ni kawaida mue wake kujisevia chakula, hivyo akuwa na sababu ya kujiinua kitandani, pia akaona mume wake akitoka nje, na kuagana nawenzake, kisha akurudi ndani huku magari ya polisi yakiondoka, na dakika chache baadae, akashangaa kusikia maongezi ya chini chini, akaza ni sauti ya TV, lakini baadae akasikia jina la mume wake likitajwa, hapo akainuka taratibu na kusogelea mlango, na kusikiliza maongzi yote, akijuwa kuwa mume wake alikuja na mgeni wakike, pengine na polisi mwenzie, ambayo mwishoni yaliishia kwa mume wake, kupiga kelele za kumtishia mgeni wake, hapo mama Bitty akafungua mlango taratibu, na kumwona mume wake akiwa amemwonyeshea bastora mwanamke ambae ni nesi, pia akamwona mume wake akijaribu kufyetua risasi pasipo mafanikio, akamwona akijaribu mala kadhaa, kuminya kiyetulio, ‘kacha! kacha!” huku yule dada akiufungua mlango bila wasiwasi wowote, na mlango ukafunguka, kisha yule dada akageuka huku anatabasamu, akamkumbuka kuwa anaitwa Jackline, aliwai kuja pale nyumbani kwao miezi sita nyuma, mama Bitte akiwa katika mshangao, akamwona yule mwanamke mwenye sura na shepu nzuri, anaingiza mkono mfukoni, na kutoa kimkebe cha risasi, “Johnson nilijuwa na wewe lazima utarudia kosa la baba yako, kulipiza jema kwa mabaya, bado ujaona wema wangu kwako?” aliuliza Jackline akimtazama insp kwamacho ya tabasamu, insp alibaki akiitazama ile bastora mikononi mwake, “ok! najuwa ujuwi thamani yako ila mama bitty na Bitty ndio wanao juwa thamani yako” alisema Jackline, kisha akamtazama mke wa insp aliekuwa amesimama kwenye mlango wa kuingilia chumbani kwao, “samahani dada, leo nimekuja kimya kimya, tutaongea siku nyingine” alisema Jackline, na kumsanua insp kuwa mke wake alikuwa pale sebuleni, hivyo akageuka faster kumtazama nyuma yake, ni kweli insp akamwona mke wake akimtazama kwa macho ya mshangao yenye maswali mengi sana, akishindwa kumjibu Jackline, wanandoa hawa walitazama kwa sekunde kadhaa, alafu wakakumbuka kuwa walikuwa na mgeni mle ndani, hivyo wakatazama mlango wa kutokea nje, wakaona akuna mtu, zaidi walikiona kimkebe cha risasi pekee, kikiwa sakafuni, “insp akachomoka mbio na kufwata ule mkebe warisasi (magazine) akaipachika kwenye bastora yake kisha akatoka nje, kwa tahadhari kubwa, akuona dalili ya mtu yoyote, zaidi kwambali kama mita sabini hivi, akaona gari likiondoka taratibu, insp akarudi ndani, na kukaa na mkewake, akianza kumsimulia mkasa mzima, kuanzia mwanzo, yani mwaka 1988, mpaka leo kifo kilivyo mkuta baba yake, hapo mama Bitte akanza kuangua kili cha chini chini, ambacho kilipanda kila baada ya dakika kadhaa, ***** siku ya pili asubuhi, nyumbani kwa mzee Masinde, walionekana watu wengi sana, huku matulubai yakiwa yame fungwa, na viti vingi vya plastic vikiwemo chini ya mhema hayo, ambapo ukiachilia askari polisi, wengi waliokuwa wanaonekana kushughulikia swala hilo, pia watu wakawaida walionekana wakisogea eneo hilo, ambalo pia ulisika music wa uzuni uzuni, kuashilia kuwa kulikuwa na maombolezo ya msiba, mmoja wa waombolezaji alikuwa mzee Soud Hassan na mke wake, wali tembea moja kwa moja, mpaka alipokuwa amekaa insp Johnson na mke wake, na mtoto wao Bitty, “pole sana kijana” alisema mzee Soud, huku akimpa mkono insp Johnson, “wamesha muuwa! wamsha muuwa” alisema insp kwa sauti ilio jawa na uchungu mwingi sana, ikiambatana nakilio cha kwikwi, huku mke wake akiendelea kububujikwa na machozi, “usijari Johnson, tutakuwa bega kwa bega kumzika baba yako, chamsingi jikaze umzike baba yako” alisema mzee Soud huku akivuta kiti na kukaa karibu na insp Johnson, wakati huo mke wake akikaa karibu na mama Bitte, “nashukuru mzee wangu, ninge fwata ushauri wako, pengine baba yasingemkuta” aliendelea kulalamika insp, “kijana huu sio wakati wake, jikaze usiongee kisicho stahili kusikilizwa, na watu wengine” insp akatulia kidogo na kufuta machozi kwa kitambaa chake, “vipi mama yupo hapa au alisafiri?” aliuliza mzee Soud, na insp akasema kuwa mama yake yupo musoma, na amesha julishwa juu ya swala hilo, hivyo, yeye atakuwa kule kwaajili ya kupokea mwili wa maaehemu ambao utasafirishwa kesho, saa nne, **** insp Khamis ndie aliekabidhiwa jukumu la kufwatilia kesi hii ambae inaonekana ime mshinda mwamba insp mwenzie Johnson, akipewa msaidizi, Kachelo Daniel, wakiamini nsp Johnson alishindwa kufanikisha upelelezi, kutokana na kuficha bahadhii ya mambo ambayo pengine baba yake na wenzie waliyafanya na kugeukana, nakusababisha kutoana roho, baada ya kukabidiwa jukumu hilo, insp Khamis aka kutana na Kachelo Danny, na kuanza kujadiliana juu ya wapi wataanzia, waliangalia record za mwanzo ambazo zilionyesha kuwa marehu sita kati ya wengi walio uwawa walikuwa ni askari wastaafu, na ambao walionyesha kuwa ndio walengwa, na vifo vyao vilighalimu maisha ya wengine pia, wakina insp Kahamis na kachero Denis, aua Danny kama wenzake wanavyo mwita, waliendelea kupitia record za uchunguzi ulio fanywa na insp Johnson, na kugundua kuwa, wanaweza kupata mambo mengi zaidi iwapo wata enda makao makuu ya jeshi, maana lengo lao ni kufahamu waliobakia kuuwawa, ambao historia zitakuwa zina fanana, na wale ambao tayari, walisha poteza maisha, nusu saa baadae walikuwa tayari wamesha fika makao makuu ya kikosi cha operation za siri, na kukutana na brig Gen Eric Gigi, ambae aliwapokea na kuwapa ushirikiano polisi wale wawili, kisha aka wakabisi wa afisa mteule Mathayo Ngimba , ambae aliwapeleka kwene ofisi ya kutunzia nyaraka za zamani, wakapewa jarida (file) la mwaka 1988, ambalo lilikuwa lime andikwa private Michael Francsis Nyati, likiwa lime gongwa mhuri mwekundu, limefungwa, ***** saa sita mchana mkuu wa kitengo cha upelelezi, aliingia ofisi kwa CGP, ambae alikuwa anapokea simu kila mala toka kwa waziri na raisi, ambao walikuwa wanaitaji kujuwa atua iliyo fikiwa, katika msako wa muuwaji anae semekana kuwa ni mwanamke, “ndio C.Cid” kunajipya, yani hapa mpaka kazi naiona chungu” alisema CGP baada ya kumwona mkuu waupelelezi akiingia ofisini kwake, “jipya lipo afande” alisema mzee huyu ambae amkononi mwake alikuwa ameshika makaratasi manne yenye maelezo, “ok! itisha mkutano na wanadhimu wote, ilikusomewa hiyo report” ***** nusu saa baadae wanadhimu wote walikuwa ndani ya ukumbi wa mikutano, wakisomewa report ya uchunguzi toka kwa insp Khamis, na kachero Daniel, iliyo somwa na mkuu wakitengo cha upelelezi, “kati ya askari saba walio enda nchini kongo kwa kazi mahalumu, walirudi sita, mmoja wakisema alipotea huko huko, inafaamika kama missing in action, sababu aikujulikana kuwa amekufa au ame tekwa au ametoroka, ama vinginevyo, askari aliepotea ndie hiyo ambae tulipata habari zake kuwa ameuwawa kaika kajibizano na polisi, miezi tisa iliyo pita, anaitwa Michael Fransis Nyati, ambae Jeshi lina kili uwezo wake mkubwa katik uwanja wa vita, imebainisha, uikiachilia kufudhu vizuri katika mafunzo yake ya mwanzo, ya kujiunga na jeshi, pia alipata mafunzo makubwa ya hali ya juu sana katika VIP protector, na mafunzo ya udunguaji, pia askari huyu alisha wai kuwaokoa askari wenzie, wakiwemo marehemu awa askari wastaafu, ziada inasema kuwa, Michael Nyati ni askari makini sana, ambae mawazo na mipango yake ya kimapigano, ilisaidia kufanikisha kazi nyingi sana, za kimapigano, kwa jinsi hiyo mpaka hapo Michael Nyati ambae tuna juwa kuwa ni marehemu, tayari ame kamilisha kazi yake,” alimaliza Chief Cid, “kwahiyo niwazi huyoo bwana Nyati bado mzima?” aliuliza CGP, kwa hasira yakukata tamaha, hapo wote wakatazamana, lakini Chie Cid akajibu, “ndio afande sababu ndie alie muuwa mzee Masinde usiku wajana, akishirikiana na mkewake alie mtorosha binti yao ambae alie kuwa amekamatwa na insp Johnson” hapo CGP, akaachia kicheko kikari sana huku anainuka “CID, fanya mjumuhisho wamwisho, niwapelekee reprt yao” alisema CGP huku akipotelea nje ya ukumbi wa mikutano, na kuwaacha wanadhimu wakitazamana kwa mshangao, **** report ili mfikia waziri na raisi ambao licha ya kuilewa ikaagizwa, paawe na miezi sita ya matazamio na uchunguzi wakina, juu ya swala hili, **** siku yapili insp Johnson na familia yake, wakitumia magari ya polisi, alisafirisha mwili wa baba yake kuelekea kwao musoma, huku mzee Soud akisimamia mazishi, kwa msaada wa jeshi la polisi, ata baada ya kumaliza kuzika walikaa week mbili zaidi, kisha wakarudi dar, ambako Johnson alienda kureport kazini, ambako aliwakilisha uchunguzi wake mwanzo mwisho, bila kuficha chochote, akieleza kama alivyo elezwa na baba yake, akiitimisha kwakusema kuwa, mpaka hapo muuwaji alikuwa ameshafunga hesabu yake, maelezo ya insp yakawekwa kwenye file lakesi ya mauwaji mfurulizo ya mwanamke mdunguwaji, pia akaruhusiwa kuendelea kkufanya uchunguzi wa swala hili, akishirikiana na insp Khamis na Kachero Daniel, ***** uchunguzi ulianza mala moja, siku zikiendelea kusogea, huku Johnson katikati ya uchunguzi alipewa mapumziko, ambapo alisafiri week mbili kwenda kisiwani zanzibar, ambako alienda na familia yake mapumzikoni, akarudi na kujiunga na wenzake, kuendelea na uchunguzi, mpaka miezi sita mbele, pasipo kuambulia chochote, pamoja na ukimya mkubwa wakuto kupatikana mauwaji ya aina yoyote yaliyo ashilia kuwa yamefanywa na Jackline Nyati, ndipo jeshi la polisi, lilipo amua kufunga jarada la kesi hiyo, lakini pasipo kupata ufumbuzi, ***** siyo kwamba insp Johnson akujuwa alipo kuwepo mzee Nyati na familia yake, alijuwa sana na alisha wai kukutana na Jackline mala mbili baada ya kuanza tena uchunguzi, mala ya kwanza Zanzibar, maeneo ya gome kongwe, kila mmoja kiwa na familia yake, wakiwa mapumzikoni, kiukweli wali salimiana huku Jackline na mama Bitte wakichanga mkiana ungesema ni marafiki atujuwi kama ni kutoka moyoni au vipi, baada ya hapo kila mmoja akaendelea na safari yake, mala ya pili ilikuwa ni week mojatu mbele, walikutana maeneo ya mbezi kwenye hospital ya doctor Stella, ambapo yeye alimpeleka mke wake ambae alikuwa anadalili za ujauzito, akuweza kufanya lolote wala kutoa taalifa kwa wenzake, ni sababu aligundua kuwa Jackline, alikuwa mwema sana kwake, maana alikuwa ana uwezo wa kummaliza yeye na familia yake, lakini ata alipogundua kuwa yeye yupo tayari kumuuwa, Jackline alimsamehe, na kuondoka zake, Johnson alijikuta akianza kumchukulia Jackline kama mtu mwema alie lazimika kufanya aliyo yafanya, baada kwa uchungu wa baba yake, kama alivyi upata yeye baada ya kuondokewa na baba yake, **** ukweli nikwamba Denis na mkewake, ambao wanaishi songea kwenye nyumba yao kubwa waliyo jengewa na mzee Nyati, huku wakisimamia kampuni yao kubwa ya usanifu wa majengo, pia kiwanda cha kutengeneza viatu na mikanda ya ngozi za ng’ombe, nacho pia waliandaliwa na mzee Nyati, ikiwa ni moja ya mpango wake wa maisha ya mwanae Jackline mume wake Denis na mtoto wao France, ni pamoja na kuwanunulia magari kumi na nane, kwaajili ya kutembelea na kampuni yao, na kabala ya yote kwanza walienda mapumziko Zanzibar, ambako walikaa wee moja na nusu, wakirudi dar es salaam, ni baada ya Jackline hali yake kubadirika kidogo, ata huvyo walipofika dar, pamoja na kumkabidhi mahadhi nyumba kwaajili ya usalama wa nyumba, pia walienda hospital kwa doctor Stella, kuchunguza afya ya Jackline ambae alionyesha dalilizote za ujauzito, ambapo alibainika kuwa anamimba ya miezi miwili, na siku hiyo alikutana na insp Johnson, akiwa na mke wake pia, mzee Nyati ameshapoa machungu yake, kila siku anacheza na mke wake pamoja na mjukuu wake, huku akimsubiri mjukuu wapili, **** MWISHO **** mpaka hapo tume fikia mwisho wa story yetu hii ya dada mdunguaji, asanteni sana wadau kwa kuwa pamoja na mimi mwanzo mpaka mwisho wa story hii, asnateni kwa like zenu, na comment, asanteni kwa walio kuwa wana share, pia asanteni wale mliokuwa mna soma bila kulike, wala ku comment, nakaribisha maoni na ushauri, in box ruksa, N.B jiandae kwa hadithi nyingine,
Your Thoughts