BAHARI ZA USHAIRI

Emmanuel Lee
By -
0
USHAIRI

3.Bahari Za Ushairi

¶ Mashairi yanaweza kuanishwa katika bahari mbali mbali kutokana ifuatavyo;

(a).mpangilio wa vina
(b).mpangilio wa maneno katika mshororo
(c).idadi ya vipande
(d).idadi ya mizani au urari wa mizani
(e).idadi ya mishororo

a.Bahari kutokana na mpangilio wa vina

√ Vina vinaweza kuwa msingi wa kueka mashairi katika bahari mbalimbali.
√ Kuzingatia vina tunapata bahari zifuatazo za mashairi;

¡) Mtiririko _ni shairi ambalo lina vina viwili, vina vya kati na vya mwisho/ndani na vya nje ambavyo havibadiliki. Yaani vina vya kati na vya nje vinafanana katika shairi zima

mfano.1
Mawazo mtu huwaza, ndivyo kiunadamu,
kwani hutofautiza , mnyama na binadamu
kiumbe hutunduwaza, ndipo mambo yakatimu.

Mawazo anayeiza, huyo si mtu timamu
kutaka jifaniza, na jidude maharamu
kwenenda jisukumiza, kila kwa upande ja beramu

Mawazo sefukuza, mimi kunitakadamu
mno nakupendeza, ndiwe unayenikimu
bali unapofuliza, huenda kani hujumu.

mfano.2
sikizeni natamka, jambo menifika
Nawaombeni pulika, si bure natika
mesikiya yalofika, hayajafichikika
ni ndoa inafika, nayo yatishika.

Ajmaina tulicheka, ndoa liposhika
na ghaya likaramka, mbio lipolika
hasidi wapoitika, pete wakavika
nchi hapo ilitulika, sime wakazizika.

¡¡). Ukara_ni shairi ambalo lina vina vya kati vyenye urari ilhali vya nje vikawa vinabadilika badikika ama ; vina vya nje viwe na urari kisha vya ndani vikabadilika badilika

mfano.1
Nina hili la kujua, mkaniweke dhahiri,
Utata mkautatua, mkanipeni na fasiri,
Ni jambo lanisumbua, lanikera kifikiri,
Anacho ni waziri, au waziri ni wa-siri?

Ni nini ameficha, kama waziri ni wa-siri?
Ni anachokicha, asijiweke dhahiri,
Wazimu umemchacha, kwa wajutofikiri?
Augua nini waziri, au ana bawasiri?

Mfano.2

NYAMA NJE NGOZI NDANI
Hicho ni kitu nasema, maarufu duniani,
Si kikubwa chake kima, si kidogo wastani,
Tena ni kitu cha nyama, kina ladha mdomoni,
Nyama nje ngozi ndani, kitu gani wajuzi?

Post a Comment

0Comments

Your Thoughts

Post a Comment (0)