2.Istilahi za Ushairi
¶ Istilahi ni maneno yanayotumiwa katika uwanja fulani maalumu;√MASHAIRI YA ARUDHI_ni yale ambayo hutungwa kwa kufuata sheria, kanuni au kaida za utunzi *ARUDHI_ni sheria au kanuni za kimapokeo, jadi au kiutamaduni zinazoongoza utunzi wa mashairi. Arudhi za mashairi ni kama vile uzingatiaji wa vina, idadi fulani ya mishororo, vipande na kadhalika.
√MASHAIRI HURU_ni mashairi ambayo hayazingatii arudhi za kiutunzi ; hukiuka Arudhi au kaida za utunzi wa mashairi na walah hayajifungi kwenye mtindo fulani maalumu wa uandishi.
√FALSAFA YA MWANDISHI_ni msimamo wa mshairi kuhusu suala linalorejelewa katika shairi. Ni maoni yake kuhusu jambo fulani.
√VINA_ni silabi za mwisho katika Kila kipande cha ubeti.
√MSHORORO_ni mstari katika ubeti.
√MIZANI_ni jumla ya silabi katika kila mshororo wa ubeti
√UBETI_ni kifungu cha mishororo kadha
√VIPANDE_ni sehemu ya mshororo iliyogawanyika aghalabu kwa koma(,).
√UKWAPI_ni kipande cha kwanza cha mshororo.
√UTAO_ni kipande cha pili cha mshororo.
√MWANDAMIZI_ni kipande cha tatu cha mshororo.
√UKINGO_ni kipande cha nne cha mshororo.
√MWANZO_ni mshororo wa kwanza katika ubeti.
√MLOTO_ni mshororo wa pili katika ubeti.
√MLEO_mshororo wa tatu katika ubeti.
√KITUO/KIISHIO/KIMALIZIO_ni mshororo wa mwisho katika ubeti.
√KIBWAGIZO_ni mshororo wa mwisho katika ubeti unaorudiwarudiwa katika kila ubeti pia huitwa kikara au kikomo.
√SABILIA_shairi ambalo halina kibwagizo.
√KIANGIKO_ni mshororo wa kwanza unaorudiwarudiwa.
Your Thoughts