RIWAYA: JESTINA
MTUNZI: Tariq Haji
CONTACT: +255624065911
SEHEMU YA 13.
tumefanikiwa kupata camera sehemu ya tukio" aliongea polisi mmoja na kumkabidhi Inspector Hans ile camera. Na yeye bila kuchelewa aliunganisha na computer yake na kuanza kuangalia, ilionyesha Alex akitoka chooni na alipofika kitandani alijirusha lakini hakuonekana mtu mwengine katika kitanda hicho. Lakini ghafla alichomoka kitandani na kujigonga ukutani kisha akaonekana kama akiomba msamaha lakini ghafla alipiga kelele na damu kuanza kumtoka. Waliendelea kuangalia video hiyo mpaka walipoona anachukua kioo na kuanza kujikata wenyewe mpaka akaanguka chini na ghafla akaanza kutoka damu shingoni kama ishara kuwa amekachinjwa, yakatokea maandishi ukutani
"AMELIPA". Hapo camera ikaingia chenga na kuzima kabisa,askari wengi waliotizama ile video walishtuka sana hasa pale yalipotokea maandshi ukutani.
"mi si niliwaambia kama mauaji haya hayafanywi na mtu wa kawaida" aliongea Inspecta Hans na kuwaangalia wenzake "sasa mmeamini kama kuna mizimu duniani" aliendelea kuongea lakini alionesha kama kushtuka kidogo na kuamua kurudia kuingalia tena kwa mara ya pili lakini kwa makini zaidi, ndipo akagundua kama shape ya mschana kama iliokuwa inaakisi mwanga. Wenzake walimshangaa na kumuuliza mbona anaangalia tena. "hebu angalieni kwa makini hiyo video kwa mbali sana utaona kama shape ya mschana" aliwaambia na wote wakaikodolea macho ndipo wengi wakagundua kile alichokisema Inspecta Hans.
Alwin akiwa kwao alifutwa na askari kuombwa aende kituoni kwa ajili ya majadiliano, alikubali bila kinyongo na kuondoka nao. walifika kituoni na kuanza mazungumzo.
"kijana hebu tueleze kuhusiana na Jestina"
"mimi sina la kueleza"
"tunaomba msaada wako maana mauaji yamezidi na yantupa sifa mbaya kama kitengo cha polisi"
"sasa mimi niwaambie nini wakati kesi yake ilifikishwa kwenu miaka kumi iliopita lakini mkajifanya wababe kuipindisha sheria, kwa kupewa pesa mkanibambikia mimi"
"tusaidie basi tuweze kumdhibiti"
"hahaha mna kichaa kweli nyinyi, kiufupi mumechelewa sana amerudi mwenyewe kuja kuiweka sawa sheria na nyinyi hakuna mnaloweza kufanya kilichobaki nyie kaeni tu musubiri kukusanya miili ya atakao waua"
"kijana unajifanya jeuri si ndio" inpecta Brandon alifoka
"tena wewe haswaa umo katika list yangu" Alwin aliongea maneno hayo na ghafla alianza kubadilika na kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Naam walilipata jibu kumbe hakuwa Alwin bali alikuwa ni mwenyewe Jestina na aliamua kufanya hivo kumpa onyo Inspecta Brandon na polisi wengine juu ya mpango wa kupenda pesa na kupindisha sheria. Kushuhudia hivo Inspecta Brandon alianguka chini na kupoteza fahamu.
"mimi niliwaambia mkaniona namtetea Alwin, sikusema tu ila yalishaanikuta ndio maana nikawaambia haitasaidia hata kama mtamkamata Alwin kwa sababu Jestina ndie anaejibu ukimwita Alwin" aliongea Inspecta Hans, "unamaanisha nini kusema hivyo" aliuliza askari mwingine. "namaanisha kuwa Jestina anatumia sura ya Alwin, hivyo basi hata ukimhoji utaishia kukipata kama kilichompta Inspecta Brandon muda mfupi uliopita" aliposema hivo ndio wakakumbuka kama mkuu wao ameanguka, haraka walimbeba na kumuwahisha hosptali.
******************************
Ndege ilitua uwanja wa Mashvile, miongon mwa abiria walioshuka alikuwemo binti mmoja mrembo sana. Hakuwa mwengine isipokuwa ni mtoto wa Profesa Alexander Harison, Miryam. Baada ya miaka mingi sasa ndio anarudi nyumbani akitoka kuchukua masters katika udaktari akiwa kama daktari bingwa saikolojia. Alitoka nje ya uwanja na kuonana na baba yake mzazi "karibu nyumbani mwanangu" profesa aliongea huku akitanua mikono kama ishara ya kutaka kumkumbatia mwanae. Miryam kwa furaha aliruka na kumkumbatia baba yake.
"umekuwa mkubwa mwanangu" aliongea profesa, "ah kawaida tu baba" Miryam alijibu na kuachia tabasamu na kuufanya uzuri wake uonekane vilivyo. "mie ningapata mtoto kama yule pia nisingefikiria kuoa mke mwengine", "dah yule mtoto ni mkali kupindukia kiasi profesa ampe kila anachotak", "sasa wewe unadhani acheze zawadi kama ile kutoka kwa muumba, kama angekuwa mwanangu angetaka hata dunia ningempa". Hayo ni maneo yalikuwa yakisemwa na walinzi walipokuwa wakimpokea mtoto wa bosi wao.
Waliingia kwenye gari na safari ikaanza, msafara huo ulikuwa ni zaidi ya ule wa raisi, ulikuwa na gari kumi zote aina Rolls royce nyeusi zikisindikizwa na pikipiki tatu mbele na tatu nyuma. Kwa kweli profesa alimpenda sana mwanae kiasi kwamba hakujali anatumia kiasi gani cha fedha kumhudumia tu. Alimpa kila alichotaka na hakusita kumwambia "WEWE NI LULU YA MAISHA YANGU". Mapenzi yake kwa mtoto wake hayakuwa na hayakufanana na chochote. Ila alijua ipo siku itabidi amkabidhi kwa mtu mwengine ili amlee, akimaanisha kuwa ipo siku mwanae pekee ataolewa na kuondoka nyumbani. Na kila alipoifikiria siku hiyo alihisi kama nusu na robo ya maisha yake atakua kayatoa, kuna baadhi ya wakati alijikuta akibubujikwa na machozi lakini angefanyaje na ndio mfumo wa maisha ulivo.
Walifika nyumbani na kupokewa kwa shangwe kubwa hasa ukizingatia anapokuwepo Miryam katika nyumba hio kila siku ni skukuu. Maana binti huyo kajaaliwa upendo wa hali ya juu sana kiasi kwamba wafanyakazi wote walikuwa wawazi katika kuongea nae, Ni mschana ambae hakujiona kwa uzuri wake na utajiri aliokuwa nao bali aliishi na watu wote kama sehemu ya familia yake. "Afadhali amerudi", "nakwambia huyu mtoto ni baraka ndani ya nyumba hii", "hata leo profesa aseme hana mshahara wa kutulipa basi mie nitafanya kazi bure ilimradi niwe karibu tu na Miryam". wafanyakazi wa kike hawakuwa nyuma katika kummwagia sifa binti huyo wa profesa maana aliuteka moyo wa kila mtu alikuwa ndani ya nyumba yao.
Kutokana na machofu ya safari, Miryam alioga na kupumzika. Upande wa Alwin alikuwa hafahamu chochote kuhusiana na ujio wa Miryam na hata profesa alikubaliana na mwanae kuwa asimwambie chochote.
Sasa kutokana na kilichoonekana kwenye kamera askari wote waliamini kama kuzuia mauaji hayo ni sawa na kuzuia mawimbi baharini. Kila asakri aliamua kushughulika na mambo yake pasi na kuwaza tena njia za kumkamata muuaji, walijisemea "muache auwe tutakwena kukusanya mizoga". Jestina akiwa chumbani kwa Alwin ghafla hali ya hewa ilibadilika ghafla na kutoweka bila yeye mwenyewe kutaka, funga fungua alijikuta yupo kule katika ulimwengu wa waliodhulumiwa. "karibu tena Jestina" aliongea yule malkia, "mbona umenirudisha huku wakati sijamaliza kazi yangu" aliongea akionekana kuchukia kidogo. "kuna jambo nataka nikueleze kwanza ndio utarudi tena katika ulimwengu wa kibinaadamu" baada kusikia hivo kidogo akapoa. "Muda wako wa kukaa huko unakaribia kuisha" aliongea malikia na kumshtuwa kidogo Jestina, "si umenambia muda wangu utakwisha mpaka pale nitakapo wamaliza wote" aliongea Jestina kwa sintofahamu. "ndio, ilikuwa iwe hivyo lakini muda si mrefu utaanza kukutana na kikwazo" alijibu malikia, "na hicho kikwazo kitakufanya upumgukiwe nguvu za kuishi katika ulimwengu wa kibinaadamu", "nambie ni kikwazo gani hicho nikakiondoe mapema" aliaongea Jestina huku akianza kubadilika kwa hasira. "hutoweza kukiondoa hata uwe na nguvu kiasi gani hata mimi pia sikuweza kukiondoa wakati wangu" alijibu malikia akionesha ugumu wa kukiondoa kikwazo hicho. "basi nambie kikwazo chenyewe ni kipi" aliomba sasa Jestina, "MIRYAM" malikia alijibu huku akitetemeka.
"ah kumbe huyo tu" aliongea Jestina kwa dharau kidogo, "hiyo ni kutokana na mapenzi mazito aliokuwa nayo juu ya Alwin na jambo ambalo wewe hulijui ni kwamba Alwin anampenda sana Miryam japo hajawahi kumuona tokea azinduke, ila kwa sasa Miryam amerudi kutoka masomoni na akianza tu kuwasiliana na Alwin mapenzi yao yatamea tena jambo ambalo litamfanya Alwin aanze kusahau mambo mengine ikiwemo kisasi anachokusaidia kukikamilisha" aliongea malikia na hapo Jestina aliishiwa ujanja.
"lakini kuna kitu unaweza kukifanya ili kuendelea kubakia ulimwengu wa kibinaadamu" aliongea malikia, "kitu gani hicho". "usiwaingilia katika mapenzi yao wala usijaribu kumsogelea Miryam kwa ubaya maana katika ulimwengu hakuna vita kubwa kama ya mapenzi, pia hayohayo mapenzi ni amani ya kutosha" aliongea malikia. "sasa umesema wakianza kukutana mimi nitapoteza nguvu zangu" aliuliza Jestina, "utaweza kuwa nazo ikiwa Alwin atamueleza Miryam juu ya uwepo wa mzimu wako na kama atakubali bila kinyongo na kuamini kama ni kweli basi hapo utakuwa umeshinda maana hata nguvu zako zitaongezeka kwa sababu utakuwa na watu wawili ambao walikupenda sana kipindi cha uhai wako japo mwenyewe hukulifahamu hilo" alimaliza kuongea Malikia na kabla Jestina hajajibu chochote alitoweka na kurudi katika ulimwengu wa binaadamu. Alimkuta Alwin kalala fofofo, alisogea mpaka pembeni yake na kukaa. Alimuangalia kwa muda sana kisha akajilaumu kwa kumpa wakati mgumu sana kipindi cha uhai wake japo alimuonyesha ni kiasi alimpenda na kumjali, lakini kutokana na wivu wake wakimasomo hakutaka kumkubalia bali aliamua kumtesa kwa kutoka na mwanaume mwengine ambae baadae aliamua kumfanyi ukatili wa hali ya juu sana. Machozi yalianza kumtoka na kujikuta ni mwanamke asie na shukurania hata kidogo. Pia alikumbuka kipindi akiwa na urafiki na Miryam mschana ambae walitokea kupendana sana kutoka na tabia zao kuendana sana japo kiakili hakuwa na akili kama yeye "ama kweli kuwa na akili nyingi si kuwa na maarifa" alijisemea moyoni huku akihisi maumivu makali ya usaliti aliowatendea wawili hao pasi na kumthamini sana. Ila angefanyaje na ndio mambo yashaatokea hata kama angetaka kuyarekebisha isingewezekana maana tayari alishaaga dunia.
*****************************
Usiku uliingia huku maandalizi ya sherehe kubwa ya yakifanyika, ilikuwa ni sherehe ya kumkaribisha Miryam. Alwin akiwa kwao aliskia akiitwa na mama yake na aliposhuka alikutana na mtu asie mfahamu. Alikuwa na briefcase mkononi, "Mr Alwin huu ni mzigo wako" aliongea na kumkabidhi kisha bila kuongea kitu yeye aliondoka. Alwin alirudi chumbani kuufungua mzigo huo, alishangaa kuona kuna suti ya rangi ya maziwa au crem, viatu, tai nyekundu pamoja na funguo ya usafir. Pembeni kulikuwa na barua ndogo iliosema hivi.
ITAENDELEA
Your Thoughts