JESTINA 4

Emmanuel Lee
By -
0

RIWAYA: JESTINA

MTUNZI: Tariq Haji

CONTACT: +255624065911


SEHEMU YA NNE.


Ukweli Miryam anampenda sana Alwin lakini baada kugundua kuwa Alwin ametokea kumpenda Jestina hakutaka aingilie kati na badala yake aliomba kuwa rafiki wa Alwin na Jestina ombi ambalo lilipokewa kwa mikono miwili na marafiki hao. Miryam ni mtoto wa tatu katika familia nambari moja kwa utajiri katika mji wa Mashvile, ni mschana mrefu mwenye asili ya kivenezuela na weupe wa kungaa. Kichwa chake kilipambwa na nywele za kimanga zilizonyooka kama nguo iliopigwa pasi, Kwa bahati mbaya yeye ndie mtoto pekee alieyepona katika ajali ya moto ulioteketeza nyumba yao akiwemo mama yake pamoja na kaka na dada yake. Kwa sasa anaishi na baba tu ambae kwake ndie baba na ndie mama.

  


Wanaume wengi walijaribu bahati yao kwa lengo la kula vya bure lakini waliambulia pakavu, na hakukuwa na kitu cha kumlaghai maana kama gari yeye binafsi ana miliki gari kumi tena tafauti na pia ni za bei mbaya. Kama vito kila siku anavaa vipya, kiufupi hakuna anachokosa kwao hivyo wengi walishindwa kumkamata ndege huyo. Siku ya pili mapema Alwin aliwasili college na kuendelea na ratiba zake kama kawaida bila kusahau kumpa salamu best yake Jestina ambae hakuijali kabisa. Hata hivyo alijisemea moyoyni "mimi wajibu wangu ni kukupa salamu tu, kujibu hiyo ni juu yako" japo aliumia kwa upande mwengine lakini alijikaza kiume tu.

******************************

 "Alwin, Alwin, wewe Alwin si nakuita" Miryam aliita mara kadhaa lakini Alwin hakuskia mpaka pale alipomtingisha. "eh, samahani nilikuwa sipo kabisa hapa" aliongea Alwin huku akilazimisha tabasamu kitu ambacho Miryam alikishtukia mapema. Lakini alielewa nini cha kufanya hasa anapomkuta Alwin katika hali hiyo, "unajua kawaida yetu watu kama sisi tunapokutana na jambo ambalo ni gumu kulitatua basi njia pekee ya kutusaidia ni kutupa swali" aliakumbuka maneno hayo ambayo aliambiwa na Alwin siku za nyuma. Basi alifungua begi lake na kutoa kitu kama kiboxi kidogo na kumkabidhi. "nisaidie kufungua hicho kiboxi nimepewa na baba lakini mimi kimenishida" aliongea Miryam kwa sauti ndogo sana. Alwin alikiangalia kidogo kisha akamuangalia Miryam "lakini mbona hiki kimepangika vizuri tu".

 


 "Baba kanambia ikiwa hizo picha zitapangika basi kitafunguka chenyewe" alijibu Miryam. Hapo sasa Alwin alikiangaliwa kwa umakini na kugundua picha zote zilikuwa sawa lakini kulikuwa na tofauti ndogo katika kila picha. Tofauti hio ndio funguo wa kufungua kibox hicho, alimpa Miryam kibox na kumwambia azipangue zile picha kisha yeye akafunga macho. Alizipangua zote na kumwabia "tayari". 

 


Alwin alifungua macho na kuanza kuzipanga zile picha upya. Kila baada dakika moja aliandika namba kwenye karatasi mpaka zilipotimia sita akatoa pumzi kwa nguvu na kumuangalia Miryam ambae alikuwa amekodowa macho utadhani mjusi aliebanwa na mlango. Kisha Alwin alianza kuvipanga vipande vya zile picha na kila baada ya mizunguko sita aliahamisha kipande kimoja na kukiingiza upande wa pili wa kiboxi hicho mpaka ilipotimia mizunguko thalathini na sita, aliandika namba hiyo na kuigawa mara tatu na kundika kumi na mbili. Alinza tena kukipanga na kila alipofika mizunguko kumi na mbili alihama upande mpaka ilipotimia mara kumi na mbili.

  


Baada ya hapo akaivunja kumi na mbili mara nne na kupata tatu, kisha akaanza tena kuzipainga lakini mara hii alidili na mstari wa tatu tu. Na kila baada kupanga vipande vitatu alihama upande na mwisho alikamilisha zoezi hilo. Kumbe zile picha zilikuwa na maandishi yalioadikiwa "HAPPY FRIENDSHIP DAY ALWIN", na ghafla kilifunguka na ndani kulikuwa na funguo ilioandikwa "SPECIAL FOR ALWIN". Miryam alimuangalia Alwin kwa makini kisha akamwambia "unakumbuka siku niliokwambia nikipasi kuingia mwaka wa tatu college nitakupa zawadi", "ndio nakumbuka" Alwin alijibu kwa sintofahamu. "nifate" Miryam aliongea na kuinuka na kuondoka na Alwin alinyanyuka haraka na kumfata.

 


Wakati wanatembea Miryam alito simu yake na kupiga "uleteni mzigo wangu" kisha akakata, walipofika barabarani. Miryam alionesha ishara ya kusimama na ghafla ikaja gari kubwa aina ya scania na kusimama mbele yao ikiwa imebeba kontena. Milango ya kontena ilifunguliwa na kushushwa pikipiki moja nyeupe kama zile za mashindano. Katika pipa la mafuta iliandikwa "SPECIAL FOR ALWIN", Alwin alibakia ametoa macho tu maana alipanga atengenezesha pikipiki kama hiyo akishapata kazi yake. "umejuaje kama nilikuwa napanga kutengeneza pikipiki ya aina yangu peke yangu" hilo lilikuwa ni swali la kwanza kutoka kinywani mwa Alwin, "siku ile ulionambia nikachukua kitabu katika begi lako nilikuta picha ya pikipiki hii ulioichora na kuandika chini MY FUTURE RIDE.

  


Namimi nikaona kwanini nisikuapatie zawadi hii kama fadhila za msaada wako mkubwa katika masomo yangu. Ndipo nikaipiga picha pamoja na vifaa vyote ulivovichora kisha nikampelekea baba yangu na kumwambia anitengenezee, aliponiuliza ni kwanini nataka itengezwe nikamjibu kuwa hii itakuwa zawadi kwa mtu aliefanikisha mimi kupasi japo nilikuwa mzito kwenye masomo. Hapo akanambia nimueleze wewe ni nani na mimi nikamwambia kila kitu, basi alisafiri kuelekea ujerumani kwa ajili ya kazi hii tu. Kwa vile wewe ni genius akaamua kutengeneza kiboxi hichi na kuweka funguo na kunambia kuwa mwenye uwezo wa kufungua kiboxi hichi ni mtu mwenye IQ kati kati ya 165 na kuendelea juu. Na ameweza kukidizaini hicho kibox kwa mfumo wa hesabu" aliongea Miryam na kumshangaza Alwin, "basi kama baba yako ndie aliekitengeneza koboxi hici bila shaka na yeye ni kama mimi" Alwin aliongea.

 


"hujakosea mwanangu ila mimi nimekuzidi sana" iliskiaka sauti ikitokea nyuma yao. Alikuwa ni baba yake Miryam " mimi nina 197 IQ capacity na ndie niliendaa mashindano ya magenius" alijib Mr Alexander Harison, hilo ndio jina lake nainasemekana ndie mwenye uwezo mkubwa wa akili kuliko watu wote duniani. "mimi na wewe tutaonana kwenye fainali za mashindano haya na nakutakia siku njema" alimaliza kuongea na hapo hapo ikaja gari, aliingia na kuondoka. Alwin hakuamini macho yake kama mtu aliemuona mbele yake ndie mtu ambae alikuwa akimkubali tokea udogoni kwake. Siku hiyo ilikuwa ni ya furaha sana kwa Alwin alijikuta kwa muda akisahau machungu yote na maumivu aliyoyapata kutoka kwa Jestina.

 


Alwin alijikuta akimkumbatia Miryam kumbatio ambalo kwa wengi lilitafsiri kuwa ni upendo. Kwa mara ya kwanza Miryam alijikuta akilihisi joto la mwanaume huyo ambae alitokea kumpenda kupita maelezo. Mkumbatio huo ulidumu kwa dakika kama mbili hivi, kisha wakaachiana huku Miryam akiangalia chini kwwa aibu. "asante sana Miryam kwa zawadi yako nzuri" Aliongea Alwin huku machozi kwa mbali yakilowanisha macho yake. "usijali Alwin hivyo ndivyo marafiki wanavotakiwa kuwa" alijibu Miryam na kutoa kitambaa chake na kumfuta machozi ambayo tayari yalishaanza kulowanisha mashavu ya Alwin.

  


Yote hayo yalifanyika huku Jestina akishuhudia kila kitu, lakini hata hivyo alipotezea na kuondoka eneo hilo. "ah halafu nimesahau subri na mimi nikupe zawadi yako" Alwin aliongea na kufungua begi lake na kutoa kitu mfano kama wa simu. "hiki kifaa nimekiteneza mwenyewe na nimekiprogram na maswali mengi sana ambayo yatakusaidia ikiwa utahitaji msaada na sitokuwa karibu" Aliongea na kumkabidhi kifaa kile. Miryam alirukaruka kama kidege huku meno yote thalathini na mbili yakiwa nje. Baada ya hapo kila mtu aliondoka na Alwin aliltafuta Jestina ili ampe zawadi ya siku ya marafiki duniani lakini alichokutana nacho huko kilikuwa kinyume maana Jestina alitoa maneno machafu huku akimwita Miryam malaya. Hakumaliza kuongea alichezea kibao kizito kutoka kwa Alwin na kumfanya ayumbe kidogo kabla ya kuzuiwa na bwana wake Matt "umeniacha bila chaguo Jestina ila kukufunga mdomo na nikwambie kitu huna haki ya kumuita Miryam majina machafu kama hayo. Nimejaribu sana kukueleza lakini inaonekana Matt anakutia kiburi sana" Alwin aliongea na wakati huu alivimba kwa hasira.

 


"We dogo sikia nikwambie, kama unataka kupimana uzito pimana na saizi yako na sio kukimbilia waschana" Matt aliongea huku akimsukuma Alwin. "Na wewe mwanaume mpumbavu usie na akili, kwa muonekano tu hata kurusha jiwe huwezi achilia mbali kukunja ngumi. Kama unadhani kuwashusha sketi wanawake ni uanaume basi umebugi na nikwambie kitu kama kweli unaweza ndondi tuzame uwanjani nikuonesha kama mwanaume hasifiwi kuchungulia wanawake" yalitoka maneno hayo kinywani mwa Alwin na kushangza umati mzima maana huyo hakuwa Alwin aliezoeleka hapo college. Basi Matt alitaka kumjaribu Alwin japo Jestina alijaribu kumzuia lakini ilishindakana. 

 


Jestina alimfahamu vizuri sana Alwin anakuaje hasa pale anapojaribu kuwalinda wale anaowajali sana. Basi kwa kutaka kuonyesha kama yeye ni kidume alianza kumsukum Alwin ambae kwa wakati huo alikuwa akitetemeka kwa hasira, alipomsukuma mara ya tatu Alwin alijibu mashambulizi kwa kumpiga ngumi mbili kwa wakati mmoja kwenye mabega yote mawili. Bila kutaka Matt alijikuta akikibetua kifua chake huku mikono ikikosa ushirikiano na mwili, hapo Alwin alimtandika ngumi nzito ya kifua iliotuwa kwenye chembe na kumfanya Acheuke damu na bila kutarajia alidondoka chini na kupoteza fahamu. "huu ni mfano tu, nikuskie unamtovukia tena adabu Miryam na akiinuka huyo basha wako mwambie akae mbali na mimi" aliongea Alwin na kugeuka, alikwenda mpaka lipo Miryam na kumwambia waondoke.

 


Siku ya mashindano ya magenius kwa ngazi ya kitaifa ilifika na matokeo yalikuwa kama yalivotarajiwa na wengi. Alwin na Jestina waliiwakilisha shule yao vizuri huku wakiibuka na alama nyingi sana. Walirudi college na kupokewa kwa shangwe "mashindano ya kimataifa yatakuwa mwezi ujao hivo naomba mujiandae vizuri ili mtusaidie kurudisha sifa ya college yetu" mwalimu mkuu aliongea wakati alipowaita ofisini kwaaajili ya kuwapongeza. "usijali mwalimu, tutajitahidi na kuhakikisha jina la college hii linakuwa zuri kama la zamani. Baada ya maongezi hayo walitoka na kuelekea nje, huko Jestina alipokewa na MAtt na Alwin alipokewa na mtoto Miryam.  Maisha yalindelea huku maandalizi kwa ajili ya fainali yakipamba moto. Hatimae siku iliokuwa ikisubiriwa kwa hamu ilifika, Jestina na Alwin walisafiri kuelekea nchini England maana huko ndipo fainali zilipokuwa zinafanyika. Watu wote wa Mashvile walikusanyika katika nyumba za ibada kuwaombea makinda hao ushindi wa kishindo.


WAJUA NINI KITATOKEA?

ITAENDELEA.

Post a Comment

0Comments

Your Thoughts

Post a Comment (0)