JESTINA 5

RIWAYA: JESTINA

MTUNZI: Tariq Haji

CONTACT: +255624065911


SEHEMU YA TANO


Siku ya mashindano ya magenius kwa ngazi ya kitaifa ilifika na matokeo yalikuwa kama yalivotarajiwa na wengi. Alwin na Jestina waliiwakilisha shule yao vizuri huku wakiibuka na alama nyingi sana. Walirudi college na kupokewa kwa shangwe "mashindano ya kimataifa yatakuwa mwezi ujao hivo naomba mujiandae vizuri ili mtusaidie kurudisha sifa ya college yetu" mwalimu mkuu aliongea wakati alipowaita ofisini kwaaajili ya kuwapongeza. "usijali mwalimu, tutajitahidi na kuhakikisha jina la college hii linakuwa zuri kama la zamani. Baada ya maongezi hayo walitoka na kuelekea nje, huko Jestina alipokewa na MAtt na Alwin alipokewa na mtoto Miryam.  Maisha yalindelea huku maandalizi kwa ajili ya fainali yakipamba moto. Hatimae siku iliokuwa ikisubiriwa kwa hamu ilifika, Jestina na Alwin walisafiri kuelekea nchini England maana huko ndipo fainali zilipokuwa zinafanyika. Watu wote wa Mashvile walikusanyika katika nyumba za ibada kuwaombea makinda hao ushindi wa kishindo.

 


"habari zenu mabibi na mabwana, karibuni katika THE  WORLD ULTIMATE GENIUS CHALLENGE. Mgeni rasmi atakuwa profesa Alexander Harison mtu mwenye uwezo mkubwa wa akili kuliko watu wote duniani mpaka sasa. Kwa ujumla mwaka huu timu zitakuwa hamsini na mchezo utakuwa na jumla ya mizunguko mitatu" MC alindelea kutangaza huku akiwekwa mbwembwe nyingi. "Jestina, huu ndio wakati tulikuwa tukijiandaa nao" Alwin alimwambia Jestina huku akimuangalia kwa makini. Wakati huu walizieka pembeni tafauti zao, "lakini mi naogopa" Jestina alijibu kwa sauti ya kutetemeka. "sasa unaogopa nini, usiwe na hofu kombe mara hii linakwenda nyumbani" Alwin alimjibu huku akimshika mkono. 

 


Mashindano yalianza huku kila timu ikijitahidi kubakia mpaka mzunguko wa pili, lakini ni kawaida ya mchezo wengine kuwa wasindikizaji tu. Maunguko wa kwanza uliisha zikiwa zimebakia timu ishirini na tano tu na nafasi ya kina Alwin ilikuwa ni ya ishirini jambo ambalo lilimtia wasiwasi Alwin. "Jestina una nini lakini mbona ulikuwa unakosa maswali kizembe" Alwin alimwambia wakiwa mapumziko. "hata sijui kwa kweli" alijibu, "sasa ukiendelea kuwa hivyo tutatolewa mzunguko wa pili" Alwin aliongea na kumsisitiza arudi katika hali yake ya kawaida.

 


 Kengele ya mzunguko wa pili ililia na washindani wote wakaingia ulingoni, mzunguko huo ulikuwa na maswali magumu sana na yalihitaji uwezo mkubwa sana wa kufikiri. Kwa upande wa Alwin kazi haikuwa ngumu sana kwa sababu alitrain akili yake katika kiwango kikubwa cha kufikiri. Lakini kwa upande wa Jestina mambo yalikuwa magumu sana, hii ilitokana kila alipojaribu kufikiri mawazo ya Matt yaliingilia kati. Mzunguko wa pili ulikwesha na kwa bahati walipenya japo waliponea chupuchupu kutoka. Walikuwa katika nafasi ya tano katika timu tano zilizopita, kiufupi walishika mkia.

 


"Jestina, Jestina una nini lakini" Alwin alimlalamikia, "ukiendele kuwa hivo basi ushindi utatupitia mbali" aliendelea kuongea. Mapumziko yalikwisha na muda wa kurudi uwanjani ulifikia lakini hali ya Jestina ilibadlika ghafla na wakati wanatoka alidondoka chini na kupoteza fahamu. Watu wa huduma ya kwanza walimuwahi na kumpeleka katika chumba cha huduma ya kwanza. Na kwa bahati mbaya sana majibu yalikuja vibaya, Jestina asingeweza kushiriki mzunguko huo kutokana na kuwa akili yake imechoka sana. Sasa maamuzi yalibakia kwa Alwin ima aendelee kupambana peke yake au akubali kuachia mzunguko huo. "yaani nitoke kote huko mpaka hapa halafu niachie kirahirahisi hivi" alijsemea moyoni "litakalokuwa na liwe kombe linakwenda Mashvile". 

 


Aliingia uwanjani akiwa peke yake. "sasa ni ule mzunguko wa akili nyingi, mabibi mabwana si mwengine bali ni THE ULTIMATE BRAIN STORMING CHALLENGE, mzunguko huu ni wa hatari hivyo tunaomba machela ziwe karibu na watu wa huduma ya kwanza msiwe mbali na ukumbi maana ni shiiiiida" MC alizidi kuweka vikombwelezo vingi. "mzunguko huu utakuwa na swali moja tu na kila timu itakuwa na nusu saa tu kumaliza mchezo, itaanza timu kutoka London" waliingia vijana hao walikuwa wamevaa miwani mikubwa, honi ililia na kuanza mchezo huo. Mchezo ulindelea "na sasa timu ya mwisho kuingia uwanjani ni kutoka Mashvile" Alwin aliingia peke yake na kuwafanya watu wote washangae.

********************

 Mlango ulifunguliwa na kuingia kijana mmoja huku akipiga kelele "nimemuona, jamani nimemuona na anakuja kuniuwa". "oya tulia kwanza, shusha pumzi na ukae kwenye kiti" aliongea mwenzake, "haya tuambie huyo uliemuona ni nani na kwanini anakuja kukuuwa" aliulizwa, "jamani acheni utani nimemuona tena anatisha sana, najuta kwanini nilifanya vile","tuambie basi nani huyo unaemsema"

 


Upande wa Alwin watu walizidi kushangaa maana walielewa kuwa jaribio hilo la mwisho mtu mmoja hawezi hata siku moja kushinda akiwa peke yake. "Alwin Kelvin inabidi uingie makubaliano kwamba lolote litakalotokea jumuiya ilioandaa mashindano haya haitahusika", "ndio nimekubali lolote litakalotokea litakuwa ni juu yangu" Alijibu Alwin kwa kujiamini. "Una dakika thalathni kuipanga ramani hii na muda wako unaanza sasa", honi ililia na dakika zikaanza.

  


Alwin aliangalia fumbo hilo ambalo kwa akili ya kawaida tu ungedhani michoro tu ya kitoto, "ikiwa watu wawili wanatumia dakika ishirini na tano zaidi kutatu fumbo kama hili, mimi natakiwa nitumie chini ya hapo kwa sababu niko peke yangu na hakuna wa kupingana na mawazo yangu" alijisemea mwenyewe huku akiendelea kuliangalia fumbo hilo. Baada kuridhika alitoa kalamu na karatasi na kuanza kazi, tayari dakika tatu zilishakatika. Kitu kimoja ambacho wengi hawakukijua juu yake ni kwamba ameifanya akili yake kufanya kazi kasi mara tatu zaidi kuliko computer, alianza kuandika namba namba nyingi huku akizikata kwa kuzipiga michoro. kila baada sekunde tano aliandika namba na kukata namba, wengi walimuona kama kijana anaepoteza muda kjaribu kutafuta umaarufu kwa kujaribu kujibu fumbo hilo peke yake wakati anajua kuwa hatoshinda.

 


 "profesa mi naona anapoteza muda huyu kijana" mmoja kati ya watu waliokaa karibu na profesa Alexander Harison aliropokwa. "Huyu kijana atashinda tena atatumia dakika ishirini tu" Alijibu profesa huku akiwa hamuangalii mtu huyo, lakini ukweli alichukizwa na swali hilo. Dakika saba zilishakata huku Alwin akiendelea kuandika namba tu, kumbuka hapo yuko peke yake. Zilipotimia dakika kumi alibadilisha mfumo na kutumia mfumo wa matrix, kazi iliendelea huku watu wengi wakitegemea atashindwa kumaliza. Kutokana na kufikiria sana mishipa ya fahamu iliopita pembeni ya kichwa ilianza kuvimba na haukupita muda alianza kutoka damu za pua. Lakini wala alikuwa hajui hasa kama anachuruzika damu, MC alitaka kumwambia ache lakini Prof Alexander Harison alimpa ishara amuache kwani kumshtua pale kungepelekea kupasuka kwa mishipa hiyo.

  


Dakika kumi na tano zilikata na Alwin alianz kutabasamu baada hesabu zake kwenda kama alivyotaka. Alianza kuipanga ramani hiyo huku akiangalia saa iliokuwa ikimwambia kuwa zilibaki dakika kumi na tatu.

Aliongeza kasi ya kupanga ramani hiyo huku akihisi maumivu makali ya kichwa, Prof Alexander aliligundua hilo baada kumuangalia usoni. Aliinuka alipo kaa na kushuka kuelekea kwenye jukwaa alipo Alwin huku akiangalia saa yake ambayo ilimwabia bado dakika moja tu kutimia dakika ishirini. Alifika na kusimama nyuma yake na ilipotimia tu dakika ishirini Alwin aliinua mikono kuashiria alishamliza kupanga na hapo hapo Profesa akamgusa kwenye shingo kidogo na kumminya, alianguka na kupoteza fahamu. Kisha akatoa ishara watu wa huduma ya kwanza wafanye kazi yao na kuwaambia wamtundukie dripu ya damu pamoja na maji ya glucose, pia aliwaambia baada dakika tano atazinduka. Alirudi kwenye kiti chake na kutulia, dakika tano baadae Alwin alizinduka na kuruka kwa furaha. Watoa huduma wote walishangaa kumuona vile, walimtuliza na baada ya dripu kuisha alinyanyuka na kurudi ukumbini. "jamani makofi kwa mshindi wetu wa shindano hili gumu ALWIN KELVIN" MC alitangaza na watu wote walipiga makofi. "ndugu Alwin umepata nafasi ya kufanya mawasiliano na profesa Alexander Harison hapahapa ukumbini" aliendelea kutangaza na kumuelekeza kwenye kiti na majadiliano yakaanza.


Prof : Pole kijana kwa kazi nzito

Alwin: asante profesa

Prof: Tunaomba utuambie uwezo wako wa akili

Alwin: 176 IQ capacity

Prof: unajua kama leo umevunja rikodi ya mtu mkubwa sana

Alwin: hapana sijui

Prof: Hongera Alwin kwa kuvunja rikodi yangu, mimi nilimaliza ndani ya dakika ishirin na sekunde moja.

Alwin: Ah asante lakini wewe utabaki kuwa kama ulivo

Prof: na pia hongera kwa kujinyakulia cheo cha uprofesa katika hesabu hasa kwenye Matrix

 


Ukumbi mzima walishangaa kusikia maneno hayo kutoka kwa profesa huyo, mjadala ulikwisha kwa namna hiyo huku Alwin akinyakua tuzo tatu moja kama mshindi, ya pili ya kuvunja rikodi na ya tatu cheo cha uprofesa. Katika vyombo vyote vya habari, habari ilikuwa ni hiyo tu "KIJANA ALIEVUNJA RIKODI YA PROFESA ALEXANDER HARISON". Walipumzika siku hiyo na siku ya pili walipamnda ndege na kurudi Mashvile, walipokewa kwa shangwe hasa Alwin ambae alionekana shujaa wa sehemu hiyo. 

 


Kama njia ya kutoa shukrani college iliamua kupanga safari kwa ajili ya Alwin na Jestina, ilikuwa ni safari ya kuelekea Mashvile National Park. Wanafunzi walifurahi sana kwa sababu kwa mwaka huo ilikuwa ni safari ya kwanza.

****************************

 


"hawezi kunifanya mimi nionekane bwege kiasi chote hichi, tokea tuingie katika mahusiano hajawahi kunipa penzi" Matt alikuwa akiongea peke yake huku akionekana mwenye hasira sana "lakini subiri atatoa tu, anadhani mi kaka yake". Siku ya safari ilifika na mapema asubuhi wanafunzi waliondoka na kuelekea Mashvile National Park (M.N.P), walifka saa sita mchana kwa sababu kulikuwa mbali sana. Muda mwingi Alwin alikuwa na Miryam na walionekana kufurahi sana, upande wa Jestina alikuwa hana amani kabisa hasa baada kugundua kuwa aliingia woga na kukubali kudhalilishwa na Alwin ambae kwa alivyotafsiri yeye ni kwamba "sina haja ya kuwa na mwenza kama wewe hata peke yangu naweza kushinda". Hivyo ndivyo alivokuwa akitafisiri Jestina, basi walindelea kufurahia safari hiyo huku wakitembezwa maeneo mbali mbali, jioni lipofika walikwenda kuogelea katika mto.


MZIGO HUU, UTAENDELEA KESHO

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.