CHUO KIKUU 1

 

CHUO KIKUU
SEHEMU YA KWANZA (1)

MTUNZI: Emmanuel Charo.
WhatsApp: +254796273110
Facebook: www.facebook.com/jbsonsmedia
website: jabaplanet.blogspot.com
Tiktok: Emmanuel_Bloodstone


2023
Tanga, Tanzania


Ni mara ya kumi kuikodolea macho simu yangu, nikisoma ujumbe ule ule. Sikuamini hata kidogo.
Ndio maana guu mosi guu pili nikajitoa nyumbani kuja hapa fukwe za ziwa maarufu Afrika ziwa Tanganyika. Ilikuwa ni muda wa machweo na wavuvi wengi walikuwa bize kutayarisha nyavu zao kwani wengi wao waliobobea kwenye hizo anga huvua usiku.
Kwa mara nyingine tena nikisoma ujumbe ulionieka roho juu.
'Mpendwa tungependa kukujulisha, umefanikiwa kujinyakulia nafasi ya kusomea udaktari ndani ya chuo bora barani Afrika. Fika chuoni baada ya wiki mbili utakapopata ujumbe huu. Karibu katika safari ya udaktari. Wako mpendwa Hezron Wazir'
Ilikuwa ni raha sana upande wangu, chuo nilichopata nafasi kinapatikana nchini Kenya ndani jiji la Mombasa kinaenda Kwa Jina la Virax University kusema kweli jina hilo sio dogo kwenye ulimwengu wa sayansi na teknolojia.


Wazazi wangu habari sijawambia mpaka muda huu nikiwa kwenye fukwe hizi, upande wao zitakuwa na hisia tofauti za furaha kwa muda mchache kisha nyuso zao zigubikwe na simanzi, mbona iwe hivyo? Andamana nami,,,

Labda nijitambulishe Kwanza ndio ujue Kwa nini wazazi wangu watakuwa na hisia mseto nitakapo wapasha habari hizi.
Abdul Maalim ndio jina langu, kifungua mimba wa Mzee Razak Maalim na Bi Nusrat Bihaye nilezaliwa Miaka kumi na tisa iliyopita, hayo ndio majina ya wazazi wangu niliokuwa nikisikia majirani wakiwaita. Nikiwa na wadogo zangu watatu kitinda mimba akiwa mvulana aliyepewa jina Asaad Maalim, akiwa na umri wa miaka saba walionifuatia walikuwa pacha wa kike nao wakapewa majina Latifa na Hanifa. Warembo hao wenye umri wa miaka kumi na nne.
Familia ndogo hiyo ya watu sita ilimtoa jasho Baba yangu ila alihakikisha watoto wake sisi tunaishi maisha mazuri. Kazi yake kama ilivyo wengi ya wakazi wa pembezoni mwa ziwa Tanganyika ni uvuvi naye mama yangu akijughulisha na biashara ndogo ya kibanda cha chakula akiwa maarufu kwa kutengeza mitai.


Nikiwa nimemaliza kidato cha sita na kufaulu mtihani wangu vyema na kupita combi ya PCB wengi walinishauri nifanye udaktari hasa ndani ya vyuo vilivyoko nje ya Tanzania kama nataka kupata elimu iliyo bora, inashangaza kwa nini nje ya Tanzania? Na wengi wao ni walimu wangu wa sekomdari. Nami sikuwa na budi kufanya hivyo
Nami nilifanya hivyo nilituma maombi Kwa vyuo vitatu nchini Kenya bila kuwaatarifu wazazi wangu hata wadogo zangu pia. Kwani ningepata pingamizi maana hali halisi ya nyumbani hairuhusu mie kusoma nje ya Tanzania.

Kama nilivyotangulia kusema ilikuwa raha isiyo kifani upande wangu niliwaza
'hivi nitaenda Kwa ndege ama kwa gari'
'najua itakuwa ngumu kwa wazazi wangu lakini ni wajibu wao kunipa elimu'.
Jua sasa lilkuwa jekundu na lilianzwa kumezwa na maji ya ziwa Tanganyika nami nilianza kurudi nyumbani polepole
Wakati huu wadogo zangu wote walikuwa likizo ya mwezi wa Tatu hivyo nyumba ilichangamka kiana yake hasa dada zangu walivyowasumbufu furaha iliyoje nawaza jinsi watakavyo ni miss nikienda zangu Kenya.  Pia na mimi nitawamiss sana najua watakavyo pokea habari hii 'kilio'

Kabla ya kuwajulisha wazazi wangu kuhusu habari hii niliamua kumwambia mwalimu wangu wa somo la bayolojia  maana huyu ndiye alinisisitiza kama nataka kuwa daktari bora basi nisomee udaktari nje ya nchi, sikuuliza sana kwa nini maana hata Tanzania kuna vyuo bora vinavyo toa elimu bora kwenye udaktari. Niliamini aliyekutangulia aliona mengi. Sababu ya mimi kukataa aliutumbulia mbali na kusema wewe pita tu mtihani na wafadhili watajitokeza pia wewe msomaji bila shaka sababu umeijua.
Lakini cha kushangaza hadi muda huu sijaona mfadhili aliyejitokeza, dah huzuni.
Nikampigia simu mwalimu wangu anayeenda Kwa jina Nassoro
"Shikamoo mwalimu" kama kawaida nikaitanguliza salamu hii ya jadi.
"Marahaba daktari wangu, unaendeleaje na familia"
"Eti daktari, acha hizo bwana sote tuko salama"
"Vizuri natumai uliufanyia kazi ushauri wangu"
"Ni kweli mwalimu na nimepata nafasi ndani ya Virax University, mpaka sasa siamini kusema kweli"
"Hongera yako, Tanzania ni bai bai nenda utie bidii"
"Lakini kuna shida kama ujuavyo hali yetu nyumbani sidhani kama nitafanikiwa, maana inafaa ndani ya hizi wiki mbili niende nisajiliwe"
"Usitie shaka nilikwambia pita mtihani na wenye nazo watajitokeza"
"Tuamini Hilo halipo ni mwezi wa ngapi sasa tangu majibu yalipotoka na hakuna hata dalili ya hao unaowaita wafadhili
"Usikate tamaa kijana wangu, nafasi uliyopata ndio mwanzo wa milango yako kufunguka amini hivyo. Wazazi wako wanasemaje kwani?"
"Habari hii haijawafikia, wewe ndio mtu wa kwanza kukwambia"
"Ni vyema uwajulishe mapema kijana wangu"
"Sawa kwa heri, mwalimu"

Kama kawaida yake mwalimu huyu hakosi kunitia moyo.
Nilikaza mwendo kiasi maana kigiza kilikuwa kimeanza kuingia,
Wadogo zangu walinipokea Kwa shangwe sana isivyo kawaida
"Kaka eti tunaenda Kenya",  Hanifa alinirushia swali hilo lililonishangaza
"Nani kakwambia"
"Baba yetu amesema tunahamia Kenya"
Hili lilinishangaza zaidi
"Yuko wapi baba"
"Ameenda kuvua"

Itaendelea...

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.