NYANZO(Swahili girl) 01
MTUNZI : Director Chii
Kila mtu ana namna yake anavyo yaelelezea MAPENZI,
ila kiupande wangu ukiniuliza kuhusu Mapenzi,nitacheka,kisha nitakujibu kuwa "MAPENZI NI UCHIZI"
Unajua kwa nini?
Ilikuwa ni siku ya ijumaa,mapema tu nilitoka ofisini ili kuwahi masjid.
Kwa kuwa nyumbani nilihisi mbali,na nilinuia kuswali siku hiyo,nikaamua kuingia mtaa flani ili niiwahi swala.
Yalikuwa ni majira ya mvua.
Nikiwa njiani katika mtaa huo nilio ingia,kuelekea msikitini,kwa mbele niliona kundi moja kubwa la watu waliokuwa wakija upande wangu huku wakiwa wanakifata kigoma kilichokuwa kikipigwa.
Lilikuwa ni kundi kubwa la kina dada walio vaa sare ya vijora wakicheza na kukata mauno barabarani huku wakitembea kuja upande ninao tokea.
Nilipunguza mwendo na kutembea taratibu na kwa umakini zaidi,kwani kulikuwa pia na kundi kubwa la watoto waliokuwa wakiifata burudani hiyo.
Ostadh imani ikanishuka,taratibu nikiwa napishana nao,nikajikuta nashusha kioo na kuangalia burudani hiyo iliyokuwa ikiendelea mtaani hapo.
Kwa bahati mbaya kabla sijapishana nao wote,nilikanyaga kishimo flani cha maji na kuwamwagia wadada flani wawili waliokuwa nyuma kabisa wakitembea taratibu kuufata huo msafala.
Nilisimama ili kuomba radhi,wadada wale waligeuka na kunifata.
Kabla sijasema chochote,mmoja akiwa amekunja sura ,mkono mmoja kiunoni,na mwengine kashikilia dera lake,huku akijitingisha matako yake,aliniuliza.
"Hivi kaka hujatuona au?"
nikajibu
"Bahati mbaya jamani,mnisamehe"
Yule dada aliyeniuliza aliniangalia,kisha akanipotezea na kugeuka ili waendelee na safari yao.
Mwezake akasonya,na kujibu
"Yani watu wengine bwana,we unamuachaje aondoke hivi hivi,wakati kashatuchafua."
Akajibu
"Asa si ameshaomba samahani,ulitaka nini tena?
Hebu twende huko"
Wakati tunaendelea na ule mjadala, ghafla akaja kijana mmoja ambaye pia alikuwa akiufata msafala huo.
"Oya we Mama mtu,vipi hapo"
Yule dada mwengine,ambaye hakuitaka samahani yangu,alimjibu yule jamaa.
"Huyu jamaa kapita hapa katuona halafu katumwagia maji maksudi"
"We dada wewe..."
Nilijikuta napata gadhabu ghafla na kumjibu kwa kumkazia macho yule dada.
Jamaa,akasogea karibu yangu zaidi.
"Kwa hiyo mjomba,umetumwagia maji na kigari chako cha mkopo hichi,halafu unatuletea dharau au sio"
Nikajibu
"Amna mwanangu,mbona nmewaomba samahani lakini"
"Kaka hebu nenda zako,achana nao machizi hawa,watakuharibia tu siku"
Aliniambia yule dada wa kwanza.
Jamaa akageuka,nikasikia mlio wa kofi kubwa na zito.
Kutizama vizuri,ni yule dada aliyekuwa akinitetea ndiye aliyepigwa.
"We malaya unaniita mimi Chizi,
Kwanza muda wote nakutafuta kati kule,kumbe unatongozwa huku"
Nikajikuta napatwa na huruma na kumjibu
"Oya broh,sio hivyo bwana,huyu dada me wala sifahamiani nae"
Yule mwengine akajibu.
"Kweli Razaki,huyu kaka hatumjui,katumwagia maji tu ndo tulikuwa tunagombana nae"
Razaki akanigeukia,
"Haya mjomba,umemmwagia demu wangu tope halafu ndo kashapendeza hivyo,tunafanyaje sasa?"
Nikaona isiwe shida,kwanza nikiitizama tu sura ya Mjomba Razaki,inajielezea kabisa ni mtu wa namna gani,kutokana na ngeu/alama/makovu mbali mbali yaliyokuwa usoni mwake,na kwa vile kweli nilitenda kosa,nikaona nitoe shilingi elfu 30 ili kumaliza msala huo niendelee na safari yangu.
Jamaa alizipokea zile pesa na kuzitia zote mfukoni,kisha akawaamrisha wale wadada waondoke.
"Hii we Razaki,kwani maji umemwagiwa wewe?"
Aliuliza yule dada mwengine.
Razaki aligeuka na kumtizama tu bila ya kumjibu kitu,wakaogopa na kuondoka yeye pamoja na rafiki yake.
Wakati na mimi nataka kuondoka,nikamuona yule jamaa(Razaki) ameinama,kisha akazoa maji kwa kibati kilichokuwa kando kidogo na kunimwagia.
"Siku nyengine kuwa makini mjomba"
Kisha akaondoka,akiwafata nyuma wale wadada.
Nilipatwa na hasira,ila sikuwa na cha kufanya,nilibaki nikisonya tu,ukizingatia ni mtaa ambao siufahamu.
Nikaamua kuendelea na safari.
Nilifika hadi msikitini,kanzu yangu ikiwa na matope kidogo ambayo nilimwagiwa na yule jamaa,nilijisafisha ili kuendelea na ibada.
Ikiwa ni jioni tayari,baada ya kufika nyumbani na kutulia,nilitoa simu ili kumtafuta mpenzi wangu Nasrah,kumjulia hali na kumsimulia siku yangu jinsi ilivyokuwa.
Ni mwaka wa pili sasa kwenye mahusiano yangu na Nasrah.
Kwa kuwa nilimpenda na nilitamani kumuoa,nilikuwa tayari kwa lolote na nilibadisha dini kwa ajili yake.
Nilinyanyua Simu na kumpigia.
Simu ikaita,ila haikufanikiwa kupokelewa.
Nikajaribu tena,simu ikaita kisha ikapokelewa.
Baada ya simu kupokelewa,Kwa mbwembwe mwenyewe nikaanza
"Hellow baby?"
Nilishtuka kusikia sauti ya kiume kwenye simu ikiniuliza.
"Unasemaje wewe,
Nani baby wako?"
Nilikata simu chap,nikihisi labda nmekosea namba.
Lakini sikuwa nimekosea,ilikuwa ni namba ya mpenzi wangu Nasrah.
Nikaona nijaribu tena kupiga.
Simu ikaita mara ya kwanza bila kupokelewa, nikajaribu tena kupiga,simu ikawa inaita,sekunde kadhaa ikakatwa,kisha nikasikia mtoa huduma kwa wateja akisema
"No unayoipigia,inatumika kwa sasa, tafadhali jaribu tena baadae"
Nikaanza kuwa na hofu,nikajaribu tena.
"Namba unayoipigia,haipatikani kwa sasa,tafadhali jaribu tena baadae"Mtoa huduma kwa wateja.
Hofu kubwa moyoni na hasira zikanijaa,nikasema nijaribu tena mara ya mwisho kupiga,lakini kweli ilikuwa haipatikani.
Ni mida ya saa 4 za usiku.
Mawazo yakiwa mbali,nikiendelea kutafakari ni nani aliyepokea simu ya mpenzi wangu Nasrah usiku huu,pia nikiwa nafikiria kwa nini alinikatia simu na kuizima.
Simu inaita,kutizama jina ni TONNY,rafiki yangu na msaidizi wangu Kazini.
Nikapokea na kuzungumza nae,
Tonny,
"Yo Broh,mambo vipi?"
•"Safi broh,niaje?"
nikajibu,kisha akaniuliza
Tonny
"Wapi hiyo kaka?
•"nimepoa home hivi kaka,vipi?"
Tonny
"Anhaa..
"Vipi ndugu yangu?"nikauliza.
Tonny
"Ah,nmekutana na Shem sehem flani,nikahisi utakuwepo nae pia"
•"Umekutana nae wapi"
Kabla hajanijibu,simu yake ikakata.
Kwa kuwa hatukumaliza mazungumzo,na ameniambia amekutana na Nasrah,nikapata shauku ya kumpigia tena.
Baada ya kupiga,nae pia simu yake ikawa inatumika,nikasubiri kwa dakika kadhaa,kisha nikajaribu tena,akapokea.
Kutokana na kelele za sehemu aliyokuwepo,nikamsikia kwa mbali tu akinijibu.
Tonny
"Oya kakaa..,ntakupgia mwanangu,au tutaonana kesho ofisini.
"Poa,usilewe sana sasa,kesho ukazingua kwenye interview"
Nikamsikia akicheka kisha akanijibu.
Tonny
"Usiwaze kaka"
Akacheka,kisha akakata simu.
Lakini kiupande wangu amani ndo ilizidi kutoweka,baada ya kuniambia kuwa amekutana na Mpenzi wangu Nasrah,na wakati huo yeye kanipigia simu akiwa kwenye kelele za mziki.
Niliwaza,Kwahiyo Nasrah ameamua kutoka leo bila kuniambia?
Na ameenda na nani?
Na Kwa nini simu yake alipokea mwanaume?
Nikaona vyema nijaribu kupiga tena labda nitampata,lakini bado simu yake ilikuwa haipatikani.
Nilienda kuwaza,
na kwa nini kazima simu?
Usingizi ukanichukua palepale nikibaki na maswali kichwani yasiyokuwa na majibu.
Kesho yake mapema asubuhi niliamkaa bado nikiwa namfikiria Nasrah,Huku nikiwa najiandaa kuwahi ofisi kwa ajili ya kwenda kuwafanyia watu interview,nikajaribu tena kuipiga simu yake,ikawa inaita,ila haikupokelewa.
Wasi wasi ukanizidi,lakini nilijipa moyo na kuamua kuacha kumtafuta kwa wakati ule,ili asinivuruge zaidi nikiwa ofisini.
Nilipofika ofisini,nikakutana na baadhi ya watu waliofika kwa ajili ya kufanya interview.
Kwa kuwa nilikuwa nasubiriwa mimi,niliingia ofisini haraka na kujiandaa tayari kwa ajili ya interview.
Kutokana na nafasi ya kazi tuliyoitangaza,watu kadhaa waliingia na kuwahoji kumtafuta yule ambaye atafaa katika nafasi iliyotolewa.
Wakati naendelea na kazi,akaingia dada mmoja ambaye ni kati ya wale wawili nilio wamwagia maji siku ya jana.
Alikuwa ni yule mdada ambaye alikuwa akinikandia sana kwa yule jamaa wao(Razaki),alishtuka sana kuniona,na kwa aibu alitaka kutoka nje.
Nikamzui.
"Unaenda wapi sasa?"
Akageuka,kwa aibu akarudi na kukaa kwenye kiti.
"Vipi unanikumbuka"
"Ndio"akajibu
"Tulionana wapi?"
Akabaki kimya akiniangalia kwa aibu,
"Rafiki yako yuko wapi?"
"Yupo nje na yeye anasubiri interview"
Akajibu kwa sauti ya chini.
Nikajikuta nacheka,kisha nikawasha TV,kuangalia wageni wote waliopo nje wanaosubiri interview,kupitia camera zilizopo ofisini.
Kweli nilimuona yule binti,na nikatoa maagizo kwa mlinzi amlete ndani
"Kweli milima haikutani ila binadamu tunakutana"
Ni kauli ya kwanza kuwaambia baada ya yule dada mwengine pia kuingia ofisini kwangu.
Wote wawili wakiwa wamesimama mbele yangu huku wakiniangalia kwa aibu,nikamuuliza yule mdada wa pili ambaye ameletwa na mlinzi.
"Eti dada,unanikumbuka?"
Akajibu
"Ndio"
"Vizuri"
Wewe unaitwa nani?"
Nikageuka kumuuliza yule wa kwanza.
"Naitwa SADA"
"Na wewe?"nikamuuliza yule wa pili.
"Naitwa NYANZO"akajibu
"Nyanzo!?"
Nikauliza kwa mshangao,maana ni jina geni kwangu.
"Ndio"akajibu
"Unajina zuri"
Nikamsifia kwa kumkejeli,akatabasamu.
Nikawatizama,kisha nikiendelea
"Sasa nyie interview yenu itakuwa nyepesi tu.
Nitauliza swali moja,kisha kila mtu atanijibu kiupande wake,
atakaye nijibu vizuri nitampa nafasi ya kazi.
Sawa?"nikauliza
Walikubali,kisha wakajibu
"Sawa"
"Haya swali langu ni
nini maana ya Samahani?"
Aibu ilionekana kuzidi kuwatanda usoni,kwa sekunde kadhaa.
Bila kupatiwa jibu,walibaki wakiangaliana na kila mtu akifikiria cha kunijibu.
"Hakuna mwenye jibu?"niliuliza
Nyanzo akajibu
"Mimi hapa ntajibu"
"Enhe,endelea"
"Msamaha ni kauli au vitendo anavyo fanya mkosaji kwa mtu aliyemtendea kosa,ili kusafisha makosa yake na kumaliza tofauti kati yake na aliye mkosea"
Nyanzo akajibu
Nikamtazamaa..,kisha nikamwambie arude.
"Hebu rudia"
Akarudia jibu lake kama alivyo lisema mara ya kwanza,ila kabla hajamaliza,mlango ukagongwa,nikamwambie asubiri,nikaruhusu aliyebisha hodi kuingia.
Alikuwa ni Nasrah,kipenzi cha moyo wangu,kama kawaida yake ostadhat wangu,ndani ya abaya katoto ka-zanzibari,nikikaona tu,me roho Paaahh....!!!!.
Kwa uchangamfu,alinifata na kunikumbati,kisha akaniuliza kama anaweza kukaa kunisubiri.
Nikasahau yote ya jana,nikaruhusu asubiri,kisha nikaendelea na interview
Nikarudia tena swali kwa Nyanzo,
"Enhe,umesema nini maana ya Msamaha?"
Nasrah alionekana kushtuka swali nililo uliza,mana hakuelewa linahusiana nini na kazi,akawa anamtizama Nyanzo akiwa ananijibu.
Nyanzo akarudia tena jibu lake.
Nikajikuta huruma inaniingia kwa jinsi alivyo kuwa akiongea kwa adabu na kwa upole kama anakiri kile alichokifanya.
Nikiwa nimebaki namtaza,Nasrah akauliza
"Babe,am sorry,naweza kuuliza?"
Nikaruhusu aulize
"Kwa nini umewauliza hivyo Babe?"
Sikumjibu,bali niliwapa mtihani wale wadada wajibu wao hilo swali.
"Swali la nyongeza,jibu wewe hapo".
Nikamchagua Sada kujibu swali.
Sada akaelezea kwa kifupi kile kilichotekea.
Nasraha akashtuka,kisha akauliza
"Hee..!
wamefata nini hapa kwahiyo?"
Nikamjibu
"Wamwkuja kufanya interview"
"Nyie wakina dada,
kazi mshakosa,
Haya tokeni"
Akasimama na kuwafokea kwa hasira.
Nilimtizama,nilifurahi kumuona mpenzi wangu akinisimamia na kunipambania,niliona upendo mkubwa uliopo ndani yake,kwa jinsi alivyo badilika na kuwa Chui kwa wale wadada.
Niliwaza,nikaona pia sio kizuri alicho kifanya kwasababu ni ofisini.
Sikumaliza mazungumzo na wale wadada,sababu walifukuzwa.
Kabla ya kuingia mtu mwengine,nikamuomba Nasrah anisubiri nje ili asivuruge utaratibu.
Alikubali.
Akiwa anatoka,nilimuita,akageuka,nikamtizama huku nikifikiri kidogo,kisha nikamuuliza.
Ulikuwa wapi jana?"
Hakuogopa wala hakuwa na wasi wasi.
Alinijibu
"Maliza kazi kwanza Babe,tutaongea."
Sikumuelewa kabisaa....,alizidi kunichanganya kutokana na kunionyesha kuwa hakukosea.
Nikapotezea,nikisubiri anijibu baadae.
Baada ya zoezi kumalizika,nikakutana na Tonny,nikataka kuzungumza nae kuhusu simu ya jana,ila aliniomba tuzungumze wakati mwengine,kwani alikuwa amechoka.
Sikutilia maanani,nikapotezea.
Nasra alikuwa ametangulia ndani ya gari akinisubiri tuondoke.
Nikiwa naingia ndani ya gari,mlinzi aliniita,akanikabidhi barua flani,akaniambia inatoka kwa mmoja kati ya wale mabinti wawili.
Nikachukua na kuingia nayo ndani ya gari,na kuondoka.
Tukiwa njiani kuelekea nyumbani kwangu,nikaanzisha mada
"Hukunijibu swali langu."
Alinitizama kama amesahau,kisha akaniuliza.
"Swali gani tena Babe?"
Sikupenda,nikakaa kimya sikumjibu,nikaendelea kuendesha gari.
Akaniita.
"Babe?"
Nikageuka kuona ananiambia nini
Hakusema kitu,sura yake ilibadilika,nilimuona akinuna,kisha akageuka kuangalia mbele.
Sikumuelewa kwa kweli,akanifanya nianze kujihisi mwenye makosa.
Nilijakaza,kisha nikamuuliza,huku nmemkazia macho
"Ulikuwa wapi jana?"
Zilikuwa ni nyakati za jioni,wakati tukielekea nyumbani mimi na mpenzi wangu Sarah.
Tulipokuwa njiani,nilihitaji kufahamu kuwa alikuwa wapi jana,nikarudia tena kumuuliza swali.
"Ulikuwa wapi jana?"
Hakunijibu kwa haraka,alinikazia macho na kulitaja jina langu.
"SAM"
Yes,Naitwa Samwel.
Nina umri wa miaka 28.
Ni kijana niliyesoma,na ni mmiliki wa Kampuni ya magari kutoka Japan.
Miaka 2 nyuma,tulialika wageni mbali mbali kwa ajili ya kusherehekea nasi siku ya uzinduzi wa kampuni yetu.
Kwa kuwa ilikuwa ni kipindi cha Ramadhani,tuliifanya sherehe yetu jioni,na kufturu pamoja na wageni walio hudhuria.
Moja kati ya wageni wale,alikuwa ni MZEE MOHAMED,baba wa mpenzi wangu Nasrah,akiwa ameambata na Binti yake ambaye ni NASRAH.
Mimi pamoja na mzee Mohamed tulifahamiana siku chache kabla,kwani alikuwa ni mteja wangu tangu nilipokuwa nmeajiriwa katika kampuni nyengine ambayo pia inajihusisha na kuuza magari.
Tulipata bahati ya kuzungumza kidogo,na alinisifia sana kutokana na mafanikio niliyo yapata.
Aliniambia
"Ucheshi,uchangamfu wako na jinsi unavyojua kuongea na wateja,
ndio siraha yako ya ushindi,
Usiache kuwa mtiifu na kuwaheshimu wateja,utafika mbali zaidi kijana wangu"
Alinipa mkono na kunikumbatia kwa pongezi
Tulizungumza na kuyafanya hayo yote huku Nasrah akiwa pembeni anasikia.
Ilikuwa ndo mara yetu ya kwanza kuonana,mimi na Nasrah.
Nikamtania Mzee Mohamed.
"Hujanitambulisha baba Mkwe"
Niliongea hayo huku nikiwa namtazama Nasrah usoni,nilimuona akiinama kwa aibu na kutabasamu.
Mzee Mohamed alinijibu.
"Ah weeeh...
Samwel hawezi kuwa Mkwe wangu,nikwambie kabisaa...
Ungekuwa Juma,au Abdallah au Salum,ningekufikiria.
Nadhani hapo umenielewa kijana?"
Tukacheka
Nikabaini kuwa Nasrah alikuwa akiniangalia kwa kuibia.
Baba yake alimshika mkono na kumsogeza karibu.
"Huyu ni binti yangu bwana,anaitwa Nasrah,
Nasrah..
Huyu ni Bwana Samwel,rafiki yangu sana huyu
Or,you can call him SAM"
Mzee alitutambulisha,na alikuwa akionyesha ni jinsi gani anavyo nikubali kwa jinsi alivyokuwa akinishika Bega.
Niliziona point kadhaa nilizo chukua kwa Nasrah.
Macho yake yaliongea kwa jinsi alivyokuwa akinitazama,tabasamu na aibu yake havikuficha aliyokuwa akiyawaza.
Tulipeana mikono na kusalimiana.
Tuliganda sekunde kadhaa tumeshikana mikono huku tukitizamana.
"Nmeshakwambia kijana,
Mimi siwataki wakina Sam hapa,nawataka wakina Mohamed kama mimi au Yussuf"
Alituachanisha mikono huku akiendelezea utani.
Kisha nikawaaga na kwenda kusalimiana na wageni wengine,lakini akili ikiwa imebaki kwa Nasrah.
Nilitamani nipate tena wasaa wa kuongea naw hata kidogo,ila nilikuwa nikimuogopa mzee Mohamed.
Shughuli ilifana,tulizindua kampuni kisha tukapata iftari pamoja na wageni wetu.
Wakati pirika za hapa na pale zikiendelea,nilimuona Nasrah akielekea Maliwatoni.
Nilijifanya kuwa nibenwa na haja pia, nilisimama na kuelekea Maliwatoni.
Nilimkuta Nasrah akiwa anatoka,kwa kuwa nilishaelewa kwamba ninapoint zangu kadhaa kwa mtoto,nikatumia nafasi.
Nilikutana nae akiwa anatoka,
Nilisimama mbele yake nikimtazama,kwa ishara ya macho alinielewa nini kilinipeleka kule.
Tulibaki tukitizama bila kusemeshana,sekunde kadhaa niliendelea kutembea kuelekea Maliwatoni,na yeye akiwa anatoka.
Nilisimama mbele yake tena na sikumpisha.
Alinielewa,akasimama pia na kutizama chini huku akicheka.
"Nasrah eeh"
Nilimuita.
Alinyanyua macho na kunitizama,huku akiwa bado na aibu.
"Nipo tayari kuwa ABDALLAH kwanzia leo,kwa ajili yako kama utanikubalia"
Ni mfupi kidogo kwangu,na ni hatua moja tu mbele yake nilisimama,niliuona ushindi,kwa vile nilivyokuwa nmekazia macho na yeye alivyokuwa akiona aibu kunitizama.
Hakujibu,ila nilimuona akifurahi.
Tukasikia michakacho ya mtu akija upande ule.
Nikawahi haraka kuingia chooni.
Nikasikia akiulizwa.
"Ulikuwa unaongea na nani hapa?"
Hakuwa mwengine,bali ni mzee Mohamed.
Sikumsikia Nasrah akijibu,ila nilimsikia mzee akiuliza tena.
"Yuko wapi uliyekuwa unaongea nae"
Nikachungulia sehem ndogo iliyokuwa ikionyesha njee,nikamuona Nasrah akionyesha ishara kwangu mimi.
"Mama yangu,nitamwambia nini huyu Mzee wa kipemba anielewe,na alishanikanya.
Nilichungulia tena nikamuona mzee ameshafika mlangoni.
"Mama yangu"
Nilijisema hivyo mikono ikiwa kichwani.
Kimuonekano ni mrefu kiasi na mnene.
Ni kama jitu flani la miraba minne ukimuona akiwa ndani ya suti yake.
Akitembea tu,lazima usikie kishindo kutokana na uzito alio nao,pamoja na mwondoko wake na viatu vyake anavyo vaa.
Hajazeeka sana,ila ni mzee wa makamu.
Akiongea utasema ni Simba wa kizanzibari ana nguruma kutokana na uzito wa sauti yake na lafudhi yake ya kipemba.
Ni sifa zake Mzee Mohamed,na ndo huyu hapa ananifata.
"Mama yangu,
Nimeisha"
Nilijisemea mikono ikiwa kichwani nikihesabu vishindo vya hatua zake wakati ananifata.
Mwili wote ulikufa ganzi.
Macho yalinitoka na kijasho kwa mbali nikisubiri kitakacho nikuta.
Huyu hapa mzee Mohamed,anataka kufungua mlango.
"Baa..."
Sio kishindo cha mlango,ni sauti ya Nasrah,alikuwa akimuita mzee wake,badala kuita "Baba"yeye kazoea kuita "Ba.." kutokana na athari ya lafudhi ya lugha yao.
Nilikaa kimyaa sekunde kadha kusikilizia.
Mlango haukufunguliwa,nilimsikia Nasrah akiwa amemfata Mzee wake mpaka pale jirani na mlango na kumwambia.
"Simu yako inaita."
Siku sikia tena chochote kwa sekunde kadhaa.
Siku sikia tena kishindo cha mzee Mohamed,wala sikumsikia Nasrah.
Nikachungulia kuona nini kinaendelea,nikawaona bado wapo pale mbele ya mlango.
Nilimuona Nasra akimpatia simu Mzee wake.
Mzee alipokea simu na kuanza kuitumia pale pale mbele ya mlango.
"Eeh Mungu baba,naomba niokoe hapa"
Nilitamani mzee ageuke aondoka,nilibana pu.. huku nikisali.
Nikachungulia tena,nikamuona kaweka simu sikioni anampigia mtu flani.
Simu ilipokolewa
"Naam Shekh,Assalam Aleykum"
Akatoka pale maliwatoni na kwenda kuongea vizuri na sim sehemu nyengine..
Siku poteza muda,chap nilitoka bila hata kuongea na Nasrah,nikampita kama simjui na kurudi nilipokuwa nmekaa.
Nilinusurika hivyo siku hiyo,nilimshukuru sana Mungu kwa kuniokoa na kuapia kuwa sito rudia tena.
Kila mara nilikuwa nikihisi mzee Mohamed ananitizama ile siku,sikutamani tena hata kumuona binti yake ili lisinikute jambo.
Ulipita mwezi bila kumuona wala kusikia tena kuhusu Nasrah,tangu siku ile ya sherehe.
Alinivutia kiukweli,na nahisi nilimaanisha kile nilicho sema,kuwa
"Ningekuwa tayari kuitwa Abdallah,kama angekubali kuwa na mimi"
Kwa sababu ya uzuri wake,ni kama Malaika flani hivi ukimuona,hasa akiwa katika mavazi yake ya kiislam.
"Ndo hivyo tena,hakuwa bahati yangu"
Niliwaza hivyo.
Siku moja nikiwa zangu bize ofisini, secretary aliniambia kuna mgeni anahitaji kuzungumza na mimi.
Niliruhusu aingie.
Nilikuwa bize nikipitia nyaraka flani ofisini.
Nilihisi mtu kaingia ofisini,nilimkaribisha bila kumtazama na kumfahamu ni nani,huku nikiwa bize na zile nyaraka.
"Ah,samahani kidogo Boss,kuna karatasi naangalia hapa mara moja,kisha tuongee".
Mgeni hakujibu kitu,na wala hakukaa.
Nilishtuka, nilinyanyua macho na kumtizama.
Kumbe alikuwa ni Nasrah.
Nilisimama kwa haraka na kwa mshangao.
"Nasrah"
Nilimuita huku nikiwa nmesimama nmeshika karatasi zangu mkononi
Alinitizama huku akitabasamu.
Sikujua amefata nini.
niliwasha Tv,na kuangalia pande zote za ofisi kupitia camera zilizopo kumtafuta Mzee Mohamed labda walikuja wote,lakini sikumuona.
"Ah,karibu ukae Nasra"
Nilimkaribisha.
"Hapana, me sikai.
Nilipita tu kukusalimia.
Hatukuongea mengi siku hiyo,aliniachia mawasiliano yake akaondoka.
Tulianza kwa kuwasiliana kwenye simu mimi na Nasrah,nilimueleza hisia zangu akaelewa.
Akakubali kuwa wangu,na tukaahidiana ndoa.
Mara kadhaa alikuwa akija nyumbani kwangu tukapika,tukala,na tukala tena.
Ni mwezi wa tano sasa tangu nimebadili dini na kuwa Muislamu,ni kwa ajili yake.
Ni katika kutimiza lengo langu la kumuoa.
Jana usiku,simu yake ilipokelewa na mwanaume,kisha ikawa haipatikani.
Sijui atanidanganya nini leo,ngoja nimsikilize.
"We Sam"
"Nakusikiliza"
Aliniita tena nikamjibu.
"Inamana we huijui sauti ya baba?"
"Mhhh!"
niliguna kimoyo kimoyo.
"Utoto gani tena anataka kuniletea?"
Niliwaza.
"Naijua?"
Nilimjibu.
"Ujue jana ulinichoma nyumbani"
Alianza kujitetea.
"Wakati unapiga,simu alikuwa nayo Mzee,
Si unajua nilivyo save jina lako,akapata wasi akapokea.
Wewe moja kwa moja ukaanza na mahaba yako,ukaniita babe,akasikia.
Ndo mana alikuuliza nani Babe wako?
Uzuri tu Ma alikuwa karibu akampokonya simu akakata,wakaanza kugombana wao kuwa kwa nini amepokea simu yangu.
Hiyo ndo ilikuwa pona yangu"
Kama kweli vile anachokisema,mana alishawahi kuniambia niwe makini ninapo mpigia.
Lakiniii..,ile sauti haikuwa ya mzee Mohamed,hivyo ndivyo nnavyokumbuka.
"Yani nahisi ningekuwa karibu yake ningekoma"
Alimalizia hivyo.
Nilibaki kimya tu,sikuweza kupinga.
"Nmeshakwambia mara nyingi sana Babe,ukinipigia sikilizia kwanza,ona ulicho fanya jana".
Sikuona dalili ya uwoga machoni mwake,kitu ambacho kilininyima nafasi ya kumuweka kwenye makosa.
Nilitaka kuamini,lakini bado nilikuwa na maswali.
"Ok,am sorry"
Nilimuomba samahani.
Akakaa kimyaa.
Nikamuuliza tena,
"Na kwanini ulinikatia simu,kisha ikawa haipatikani"
"Khe...Wewe..!?
Ulitaka nifanyeje sasa,nipokee simu yako mbele ya mzee Mudi?"
Alinijibu kwa kunifokea.
Sikumjibu,nikawa mnyonge kama Pilton
"Ndo mana nikakuzimia simu"
Alisonya na kugeuka mbele ya gari.
Kiupande flani nilimuamini,kiupande flani sikuamini.
Nikamkumbuka TONNY.
Nikasema nitafahamu tu ukweli.
Tulifika mpaka kwangu,tukaombana radhi yakaisha.
Tukafanya mapenzi,tukalala.
Siku hiyo haikuchangamka kama siku zingine,sababu nilikuwa na chembe chembe za wasi juu yake.
Weekend ile nzima alishinda kwangu.
Kisha aliondoka na kwenda kwa Untie yake.
Mara zote huaga hivyo kwao,kuwa anaenda kwa Untie yake akiwa anakuja kwangu.
Nikamtext Tonny.
"Yo broh,kesho tuongee basi ofisini kuhusu juzi"
Akanijibu
"Sawa"
Jumatatu nikakutana kweli na Tonny Ofisini.
Nilikuwa na shauku ya kutaka kujua ukweli,alimuona wapi Nasrah ile ijumaa.
Nilimuuliza.
"Enhe,nipange mwanangu."
ITAENDELEA...
Your Thoughts