Mzabibu

Emmanuel Lee
By -
0

Sungura kazikosa zabibu, lakini mzabibu na miti mingine iliyo uzunguka mzabibu inabaki vinywa wazi, japo kazikosa zabibu yale matusi na majigambo ya sungura hayaonekani kamwe.

Zile za 'ooh zabibu zimeoza, sijui zabibu mbichi zabibu zenyewe si tamu. Sungura alikuwa mtulivu tu hakutukana na wala kujaribu tena kutunda tena zabibu zile.


Hali ya utulivu ile ilifanya miti ukiwemo mzabibu kumfuata Sungura kwa upole kama alivyoonyesha utulivu Sungura bila shaka mpole mfuate kwa upole ukitaka majibu.

'Kwenye vitabu vya hadithi na simulizi sungura alirusha matusi na kuongea yake yote pale alipozikosa zabibu lakini wewe mbona hata neno moja hukulitoa?' muembe uliuliza

Sungura aliingalia miti mingine pale na kusema

'kabla ya kumjibu muembe je kuna swali lengine, mzabibu nawe una lolote la kuuliza'

'koh koh!' mpesheni ulisafisha koo na kusema 

'inashangaza sana aisee au wewe si sungura?'

mzabibu nao ukasema

'Sungura alionyesha juhudi ya kuzipata zabibu kusema kweli alijaribu si mara moja wala mara mbili lakini wewe hata huonyeshi juhudi ya kuzipata zabibu ulijaribu mara moja tu na kuachia hapo, bidii hulipa' 


'Na nyie wengine hamna la kusema au'

Sungura aliuliza ile miti mengine miti ile haikusema chochote bali iliendelea tu ku ufurahia upepo mwanana uliokuwa ukipeperusha majani yao.


Sungura alianza kusema 

'matarajio humualika iziraili, unataka kufa basi tarajia kitu fulani toka kwa fulani; muda si mrefu utaitwa marehemu. Mimi sikutaka kuitwa marehemu mapema hivyo kisa Sungura akisikosa zabibu lazima matusi la hasha Sungura huyu aliyeko mbele yenu ni tofauti sana na huyo mliyemsoma kwenye vitabu.' alimeza mate kisha na kuendelea

'Mzabibu nikuulize mimi ndiye sungura wa kwanza kuzitaka zabibu zako? je ningezipata ina maana mimi ndio ningekuwa sungura wa kwanza kuzila zabibu hizo?

Mzabibu ulibaki kimya kufuatia swali hilo la ghafla toka kwa sungura.

'Mnaona sikuwa hana jibu aidha ana haya kuliongea jibu lake hapa maana hakuna atakeye amini jibu hilo'


Sikuona haja ya kuporomosha matusi kwani mzabibu uliona raha kunichezea kunionyesha zabibu zikiwa chini chini tu lakini nilivyo jaribu kuzitunda basi mzabibu ulijikunjua kwa madaha na kuenda juu na kunitazama kwa bezo, sijutaka kuendelea kuzitaka zabibu zake nilijiondoa kimya kimya tu.

Na wala sioni haja ya kusema zimeoza, ningejuta ingekuwa mimi ndio sungura wa kwanza kuzitaka na kuzikosa zabibu zake lakini kama nikivyomuuliza swali na kushindwa kutoa jibu.

Ukweli ni kwamba tuseme amekataa Sungura mimi kuzitunda Zabibu zake labda ni kwa kuwa kuna sungura aliwahi kula zabibu zake kisha akatorokea kwa mzabibu mwingine kisa kashajua utamu wa zabibu hizo labda pia sungura kaamua kula maembe kama si machungwa na mananasi.


Mwisho ni kuwa Sungura hawako sawa hasa wa karne hii ya ishirini na moja.

pia ukweli ni zabibu hizo hazitooza bila kiumbe mwengine atakeye konga roho yako mzabibu na kujirudisha chini na kula zabibu zako huo ndio ukweli na labda ni miongoni mwetu hapa.

Post a Comment

0Comments

Your Thoughts

Post a Comment (0)