A REJECT KAYUMBA 2024.
NA: Emmanuel Charo.
WhatsApp +25496273110
SEHEMU YA PILI.
Baba Takisha nilikwambia huyu mtoto hasomi na wala hata hajakanyaga lango la chuo ukadhani ni utani" alilonga mama Rahim
"Oooh Baba Takisha, Takisha mwanao kitinda mimba husikii wewe kila siku Baba Takisha koma" ndio kauli ilomtoka Mzee Karim
"Afadhali hivyo kuliko lile jambazi, mwanao jambazi Karim nitamutia ndani yule amesahau mamake nani hadi anatuongopea hapa" alifoka mama Rahim
"Miezi tisa ulimbeba tumboni, uko tayari mtoto wako aozee jela eti mama Rahim"
"Koma usiniite na jina la jambazi niite na jina la kipenzi changu Takisha au Kassim lakini si Yule mwehu"
Alimaanisha alichozungumza kisha aliinuka mama huyu japo umri umesonga lakini umbo lake maridadi halijapwaya kamwe.
*****
Baada ya wiki
Tanga, Tanzania.
"Maneno mawili tu! Yakabadilisha kila kitu na labda si muda sahihi ya kuyasema maneno hayo. Lakini acha niseme hivi naichukia kalamu Sana"
Rahim alihitimisha maneno hayo na kumtazama bwana huyu anyejiita Mr Shuu mzawa wa Korea kusini.
Kisha aliendelea,
"Mbona ulimuua Abdul" mara hii Rahim aliikunja sura yake na kuuma Meno Kwa hasira
Mr Shuu alitoa cheko haswa lililojaa bezo ndani yake
"Rahim hii vita huiwezi kijana" sauti nzito ilitokezea mlango wa nyuma wa chumba kile mkabala wa kiti cha Mr Shuu.
"Wewe ni nani" Rahim aliuliza swali hilo lakini bila hata kuambiwa mtu huyu alifanana na Mr Shuu Kwa kiwango kikubwa.
"Niite Mr Shii au kiwembe" pia akahitimisha kauli yake na kicheko
"Rahim unataka kujua Kwa nini tulimuua Abdul" aliuliza Mr Shii
"Ndio maana nipo hapa"
"Rahisi tu hivyo bam'dogo" alitia usemi Mr Shuu.
"Kama unataka ukweli kamuulize mama yako, akikwambia rudi hapa kijana"
raundi hii Mr Shuu aliongea Kwa msisitizo na lile tabasamu lake liliyeyuka usoni mwake.
"Ni kama sijakuelewa mama yangu vipi"
"Mama yako anayo majibu ya maswali yako" alitia neno Mr Shuu
"Ok na Manu Yuko wapi, maana Abdul aliniahidi kunipeleka aliko, na Abdul akauwawa usiku wa kuamkia safari yetu"
"Hilo nalo jibu, acha nikwambie hivi kijana" Mr Shii alinong'ona
"Mama yako hakutaka wewe ukakutane na Manu pia anajua wakati wote huu huendi shule"
Rahim alijiinamia na kukosa la kusema.
Mr Shuu alichukua simu yake na kufinya namba kadhaa.
****
Trrr! Trrrr!
Simu ya mama Rahim ilikiriza, alichukua ki uvivu na kuiweka sikioni
"Unalijua hili mtoto wako tuko naye huku Tanzania"
"Rahim, Rahim mtoto ana balaa huyo"
"Na ni kama anajua unahusika na kifo cha Abdul"
"Mmmh ni kama hajui nini kinaendelea, mpe simu"
"Mama sikudhani unaeza kuwa mnyama kiasi hicho"
"Rahim mwanangu, hata ingekuwa wewe upo kwenye hii nafasi yangu hayo ndio maamuzi ungechukua"
Rahim alishangazwa na upole wa mama yake
"Hata kama mama, lakini mbona uamuzi uwe kuua mtu, tena mtu muhimu kwangu mama eee!"
"Rudi nyumbani Baba tuje tuyaongee na ujue picha halisi mwanangu"
"Sirudi tena Kenya Mama kwaheri"
tii tii
Simu ilikatika
****
"Rahim tena sio shogangu"
"Ni yeye hasa itakuwa nani zaidi yake"
"Shogangu mbona unaona kiza ingali mwanga bado upo wewe"
"Unamaana gani Naomi"
"Hivi Esther....'
" Koma Almas mimi sio Esther tena'
Kimwana huyu machozi yalokuwa yakimdondoka yalikauka kwa ghafla baada ya rafiki yake kumuita Esther
"Dah kumbe unaitwa nani Shoga, jina uloitwa na wazazi wako unalikana kisa mwanaume, Makubwa!"
"Ndo ivyo shoga kuanzia sasa niite Nusraty"
"Mmmmh"
Naomi aliishia kuguna tu!
"Heri mimi na Abdul wangu tuh!" Alinena Almas na kufuta machozi yalioanza kumdondoka
"Almas mmh ni miaka mingapi ishapita bila kumuona Abdul hivi unadhani bado yuko hai kweli na hata kama yuko hai unadhani anakuwaza kweli?" Alimalizia na swali binti Nusraty
"Najua Abdul hawezi kunisahau"
"Hebu fungua macho na wewe, mapenzi yenu yalikuwa ya kitoto na sasa ushakuwa mtu mzima hali kadhalika Abdul, penzi lenu halikuwa komavu eti hivi sasa Abdul akukumbuke dah! shoga umepotea aisee"
Almas alitoka pale mbio bila kuangalia nyuma
************
Virax January 2016
Hekaheka za kufungua shule zilipamba moto Kenya yote, wazazi walihaha kutafuta hela walizozimaliza kwa sherehe disemba hadi akiba.
Mwezi wa januari pesa huadimika na kupelekea wanafunzi kuenda shule kuchelewa kila mwanzo wa muhula wa kwanza na wazazi kuahidi kubadilika mwaka unaofuata ahadi ambayo ni deni ambalo halijawahi kulipwa.
Hali hii ya kuenda shule kuchelewa kila mwanzo wa mwaka ni tofauti kwa kijana huyu mdogo anayeenda kwa jina Abdul Razak anayeelekea darasa la saba, anatamani pia yeye abaki nyumbani angalau kwa wiki lakini wazazi wake ni baadhi ya binadamu wenye nidhamu ya pesa, wao humuwahisha mtoto wao siku ya kwanza wiki ya kwanza na hili humukera sana Kijana huyu.
Asubuhi ya leo hali ilikuwa tofauti kwa Abdul alichangamka kiasi cha kuwashangaza wazazi wake. Uchangamfu alionao haukulingana na siku ya leo, siku ya kwanza ya kufungua shule na Abdul anaonekana kuchangamka isivyo kawaida.
wazazi wake walijisemea mtoto wetu amekuwa.
Abdul hakujuwa furaha ile ingeyeyuka tu pindi atakapofika shuleni. kwa mara ya kwanza pia rafiki zake waliwahi kufika shule
Aliingia ndani ya darasa lao mpya darasa la saba na kuona rafiki zake wote hilo liliongeza furaha yake lakini hakuiona nywila ya maisha yake kama alivyoipa jina hilo la msimbo.
Nywila ya maisha yake inaenda kwa jina la Almas chotara wa kiyemen mamake mkenya jamii ya wamijikenda babake mwarabu mzawa wa yemen
Hakika Almas Alibarikiwa kila idara, wanasema kizuri kina kasoro lakini kwa huyu Almas Abdul hakuiona kamwe.
aliyazungusha macho yake kote darasani lakA REJECT KAYUMBA 2024.

aliyazungusha macho yake kote darasani lakini hakukuwa na dalili ya Almas hata harufu yake.
Baada ya mwezi
..........
ITAENDELEAini hakukuwa na dalili ya Almas hata harufu yake.
Baada ya mwezi
..........
ITAENDELEA