MALAIKA MWEUSI EPISODE 9

Emmanuel Lee
By -
0

 HADITHI: MALAIKA MWEUSI

EPISODE 9

MTUNZI: Ally Mbetu ‘DrAmbe’

SIMU: 0713 646500


ILIPOISHIA: EPISODE 8

“ Hapana ..wapo waliokula njama ya kuua vitendea kazi, wengine kuuza silaha na mwingine aliyeuawa wiki iliyopita alitaka kumbaka mhuduma wa kambi.”

“Vizuri unataka kunieleza mauaji ya Doctor Ray mmeyafanya kwa sababu gani?” 

“Ni hivi dada hili kundi tulielezwa ni watu waliojitenga kutoka kwenye kundi moja kubwa linaloongozwa na mzungu mmoja anayefahamika kwa jina la Father Gin, lakini si Father hasa bali ni mkuu wa majasusi.

SASA ENDELEA...


“Walijitenga, walijiondoa baada ya kuona kazi wanayoifanya ni kubwa na ya kuhatarisha maisha yao, lakini malipo yao ni madogo wanamnufaisha mtu mmoja Father Gin. Hapo ndipo baadhi walipoamua kujitenga na kkutangaza wamechana na kikundi kile na kuanzisha  mtandao wao wa kuuza damu na madawa ya kulevya.

“Lakini soko upande wao lilikuwa zito hivyo waliamua kutumia hila pale damu iliyopelekwa ya troni 50 kuzunguka na kuchukua pesa kupitia mkuu wa ujasusi wa ujerumani ambaye ndiye hawara yake Marry White.

“Mpango wake ulifanikiwa na likawa pigo kwa Father Gin pale alipoletewa taarifa kuwa damu yote aliyopeleka ni chafu kwa hiyo imemwagwa.Pesa zile ndizo zilizokiimarisha kikundi cha Marry White ndipo alipojenga kituo kikubwa cha kulelea watoto na vingine anajenga mikoani na kununua mitambo ya kisasa ya kunyonyea damu, matanuri ya kuchomea miili ya watu, matawi mengine yako nchini Kenya, Rwanda,Kongo na Afrika kusini.

Pia kanunua eneo ambalo ukienda vibaya utajua ni makaburi kumbe sio, ni maghala ya kuhifadhia madawa ya kulevya ipo maeneo yaleyale ya kambini Arusha. Pesa zile ndizo zilizompa jeuri kubwa Marry White ilifikia hatua ya kupenyeza mamluki kwenye kikundi cha Father Gin ambao walimpa siri zote zinazoendelea juu ya mpango wa kumsaka Marry White na wenzie watatu walio jiengua kwenye kikundi.

Taarifa zile ndizo zilizo mfanya Marry White aunde kikosi cha kukabiliana na Father Gin hapo wote tuliokuwepo tuliingia mafunzoni kwa ajili ya kukabiliana na Father Gin  tuliokuwepo tuliingia mafunzoni kwa ajili ya kukabiliana na adui mazoezi yetu yalikuwa ya miezi sita.”

“Umesema mpango wenu wa kukusanya watoto kwa ajili ya vuno la damu na ngozi una miezi sita sasa mlifanyaje kazi mbili kwa wakati mmoja?”

“Sikukueleza mwanzoni, ni hivi tulipokusanywa baada ya semina ndipo zilipofika taarifa za kusakwa Marry White hapo ndipo mafunzo yalipoanza mara moja. Kwa miezi sita, baada ya kukamilika mafunzo wakati huo kambini tulikuwa na watoto mia moja na majengo zaidi yalikuwa yakiendelea kujengwa.

“Ndipo tulipoanza kazi rasmi ya kukusanya watoto japo ilikuwa kazi kwani vituo vingi Father Gin alikuwa amevihodhi. Baada ya hila za Marry White kumuharibia biashara zake ambazo zilisimama hapo ndipo alipopata nguvu ya kukusanya watoto kwa kasi vituo vingine walipokataa tuliwapa pesa ndipo siku moja Marry White alituita na kutueleza kumeandaliwa watu wamsake. Kumbuka ni siri iliyovuja toka kwenye kundi la Father Gin tulielewa jinsi tutavyokabiliana hivyo kazi ya kuwaua haikuwa nzito tuliwaua kiurahisi sana.

“Wewe umeisha ua wangapi?”

“  Watatu.”

“Unaweza kutumia silaha gani?”

“Bunduki na bastola ya aina yoyote.”

“Wote uliwaua kwa risasi au nini?”

“Mmoja kwa kisu , wengine kwa sumu na risasi.”

“Katika watu wa Father Gin umeua wangapi?” 

“Wote watatu.”

“Uliwaulia wapi?”

“Hapohapo ni hawa wa mwisho mwisho ambao niliwaingilia ndani mwao siku wanayo jiandaa na safari.” 

“Mmh, vizuri endelea.”

“Basi tulijua kazi imekwisha tukawa tunaendelea na kazi zetu. Siku moja Marry White hakuwa kwenye hali ya kawaida  tulijua kuna jambo, siku hiyo alionekana mtu mwenye mashaka mengi.  Ndipo alipotueleza habari zako kuwa umerudi kutoka mafunzoni kwenye chuo cha ujasusi ambacho ndicho alichosoma Marry White yeye alisoma kwa miezi  minane wewe mwaka mzima na kutuambia jinsi gani ulivyo hatari.

“Hapo ndipo tulipopewa jukumu la kukuua ila jukumu hilo walipewa kina Zone, Marry White anawaamini wameshafanya vizuri kazi zote za nyuma walizotumwa, na jana tuliingia jioni kwa ajili ya kutekeleza kazi hii leo.”

“Sawa mlinifuata mimi na Doctor Ray kwa sababu ndiye aliyekutafuta vilevile hata wewe ukifa atawatafuta wengine na ndiye waliyemtumia ili upatikane kutokana na ukaribu wenu.”

  “Umeniambia umepitia mafunzo ya mapigano kwa miezi sita iweje kofi moja likuzidi nguvu na kulegeza hivyo?”

“Tangu niingie kazi hii sijawahi kupigwa na mtu vilevile nilihisi nimepigwa na ubao ulionifanya nisikie kizunguzungu.”

“Ooh, pole sana sasa ni hivi wewe ndiye utayenisaidia kuwakomboa hawa watoto na kukomesha biashara hii.”

“Mmh, Dada itakuwa ngumu lazima Marry White atajua hivyo nitakabiliwa na kifo cha kutisha.”

“Wewe ndiye atayenisaidia kuwaangamiza Marry White na wenzie,” nilimpa moyo.

“Kukusaidia kivipi?”

“Kunipa taarifa kutoka kwenye kikundi chenu ambazo zitanisaidia kuifanya kazi yangu kwa wepesi elewa Kallo mimi sina ugomvi na nyingi bali Marry White na washirika wake pamoja na Father Gin.”

“Father Gin si ndio bosi wako?”

“Elewa kazi yangu si kutoa roho za viumbe bali kuokoa roho za viumbe wasio na hatia nina imani kwa uwezo wa Mungu nitawashinda Father Gin na Marry White.”

Kauli yangu ile yenye msisitizo ilimfanya Kallo ajae ujasiri na kuniahidi:

“Da Thereza na kuahidi nitashirikiana nawe hadi tone la mwisho la damu yangu.”

Tulikumbatiana na kupigana  migongoni kupeana mioyo ya utendaji, mara simu ya Lallo iliita aliiangalia na kuseama kwa hofu.

“Nani?”

“Marry White.”

“Mungu vile ni ghafla hujapanga maneno mweleze ndio unarudi kutoka kukusanya watoto,” nilimwelekeza cha kusema.

“Haloo Sister Marry White.”

“Ee’he Kallo shughuli imefikia wapi halafu mbona simu za Marc na Zome zinaita tu hazipokelewi? Sijui wamefikia wapi katika kumuua Thereza unajua Kallo moyo wangu umeingia hofu?”

“Kwa nini Sister?”

Hata sielewi nimejikuta namuogopa Thereza japo sijaona uwezo wake  huenda kishanitia hasara.”

“Hasara! Una maana gani?”

“Yaani kawaua Marc na Zone.”

“Mmh ! Sidhani.”

“We umeshawasiliana nao?”

“Ni kama nusu saa walinijulisha wameshamuua Doctor Ray na wanamsubiri Thereza ambaye walijulishwa yupo njiani kuelekea Kibaha na walinihakikishia kazi yao itakuwa nyepesi tofauti na walivyo fikiria.”

“Kwa sasa umeshawasiliana nao?”

“Hata mimi simu zao zinaita hazipokelewe sijui kuna nini?”

“Lazima kutakuwa na tatizo mtume John na Puchu wawafuatilie.”

“Sawa mimi ndio naelekea hotelini.”

“Fanya hivyo haraka unijulishe moyo wangu umeingiwa hofu lazima kuna hatari.”

“Sawa bosi.”

“Vipi nawe kazi yako imefikia wapi?”

Kwangu imekwenda vizuri sana na jioni tunarudi.”

“Hesabu imetimia?”

“Imetimia nimepata wote mia mbili.”

“Vizuri sana kazi yako nzuri Kallo, imenifurahisha lazima nikuongezee mshahara mkubwa.”

"Sawa bosi nitashukuru.”

"Kazi njema natarajia tutaonana Arusha usiku tuna kikao kingine..Kallo,” alimwita. “Unasemaje sister Marry White.”

“Huwezi amini ile 'Issue imejibu imewahi tofauti na tulivyotarajia.”

“Eehe..lete raha.”

“Saini ya Father Gin tumeipata na yale makaratasi yalikuwa yanatuumiza kichwa huwezi amini kikao cha leo kilikuwa kuzuri kuliko tulivyotarajia mengine tukionana jioni tutaongea mengi...kazi njema ila wasisitize Puchu na John wafuatilie mara moja.”

“ Sawa bosi.”

“ Kazi njema.”

“Nawe pia,” simu ilikatwa alinigeukia na kuniuliza:

“ Sasa da’ Thereza nitamweleza nini tena?”

“Usiwe na wasi nitakufundisha cha kumueleza la muhimu tuondoke humu ndani ili twende sehemu yenye usalama, chukua vitu vyote muhimu.”

Kallo alichukua vitu vyake vyote tukaondoka eneo la tukio mara moja, nilikwenda naye hadi moja ya ofisi yangu na kuingia naye ndani. Niligundua Kallo bado hakuwa na imani nami alijua nimempeleka ili nimuue.

“Kallo nina imani hii ni sehemu iliyo salama hivyo tunaweza kuongea vizuri zaidi vile vile jisikie upo huru we urafiki yangu hebu nieleze ni mpango gani unaohusiana na saini Father Gin?” nilimuuliza kwa upole.

“Kama nilivyokueleza mwanzo kuhusu kundi la Marry White baada ya kujitenga hawakujitenga bali dhamira yao kubwa ni kumtia adabu Father Gin kwa kuhakikisha wanaziba njia zote za kumuingizia na kuchukua zile pesa za mauzo kwa kuiba disc yenye mikataba ya malipo na kufuta kumbukumbu zote kwenye computer.

Baada ya kufanikiwa kuziiba zile disc walikuwa wakitafuta saini na profoma invoice za Father Gin ili kumpiga pigo takatifu.”

Nilishtuka kusikia pigo takatifu na kuona mpango huo unafanana kabisa na operesheni ya Father Gin.

“Eeeh, nina imani pigo hilo litamchanganya trion 150 si mchezo.”

“Umesema kuna mamruki kwenye kikundi cha Father Gin walio chini ya Marry White ni wangapi?”

“Huwezi kuamini ni wote kumi na tano unaowaona ndio wanaomla kisogo na kujifanya wapo pamoja naye, kama ungebahatika kukiona kikao cha leo Arusha ungechanganyikiwa yaani aliyepungua ni Father Gin tu.

“Mmh, hizi habari nzito, ina maana maisha yangu yapo mikononi mwao?”

“Ni kweli lakini nilioyaona leo nimeshawahi kuyaona kwenye sinema na kujua ni uongo kumbe yapo kweli, dada unatisha wacha Marry White akuhofie.”

 Mara simu alilia, ilikuwa ya Marry White, kabla ya kupokea aliniuliza amjibu nini. Nilimwewleza amjibu kuwa amekuta mayaji ya kutisha hotelini ya wenzake wote ila yeye amefanikiwa kutoroka. Kallo alimweleza kama nilivyo mwambia aseme.

  Nilisikia Marry White akipiga meza upande wa pili kwa hasira:

"Unanisikia Kallo.”

"Ndiyo sister." 

“Ni hivi mambo yamesha haribika hivyo basi simamisha kazi zote za kukusa watoto njoo haraka Arusha ili tujipange upya hili ni pigo takatifu. Jitahidi utoke salana maana sina imani tena na Thereza anaweza nawe kukumalizia mbali jitahidi utoke salama kwani sasa hivi upo wapi?”

“Nipo sehemu nina imani ni salama japo siamini sana.”

“Vipi ulipoingia hotelini ulibahatika kuchukua vitu muhimu?”

“Huwezi amini sikukuta kitu chochote.”

“Ooh, Mungu wangu.” Marry White aliongea sauti ya kukata tamaa.

“Sasa ndio itakuwaje?” Kallo aliuliza.

“Kwa sasa hivi siwezi kuongea lolote nimechanganyikiwa mengi tutaongea ukifika ila ninaapa nitamshikisha adabu mshenzi huyu nitamtafuna mbichi,” Marry White alisema kwa hasira.

“Kwa hiyo unaniambia niende kwenye vituo nikawataarifu?”

“We  wee..we..acha kabisa  unaweza kukutana naye nasema acha kazi zote rudi mara moja.”

Ilionyesha ni jinsi gani Marry White anavyoniogopa lakini hicho hakikuwa kigezo cha kunifanya nitembee kifua mbele la muhimu lilikuwa kuwatokomeza wazandiki wale washenzi mamumiani wenye maumbile ya kibinadamu lakini mioyo yao zaidi ya ukatili wa mnyama.

Vilevile nilimshukuru Mungu ningeweza kuokoa watoto mia mbili bila jasho kwani kusitisha kuwachukkua watoto mia mbili kulinifanya niokoe watoto elfu mbili na mia tatu.

Nimemtupia macho Kallo ambaye alionyesha ni jinsi gani nilivyo mtu wa ajabu. Alinitazama macho ya mtu kuniuliza swali, hilo nililigundua.

“Sema tu Kallo usiniogope wewe sasa hivi si rafiki tena ni ndugu ambaye nakuona tumetoka tumbo moja najua unaswali uliza.”

“Sasa da’ Thereza utaniruhusu niende Arusha?” 

“Hiyo ndiyo dhamira yangu kuu, ya wewe kwenda Arusha ili nipate habari za kule ambazo zitanipa urahisi wa kurahishisha shughuli yangu.

“Tutawasiliana vipi wakati huo tunaweza kuwa na Marry White?” Kallo aliniuliza swali muhimu.

“Ina maana hata kulala mnalala wote?”

“Hapana.”

“Basi muda utaokuwa peke yako ndio wakati muafaka wa kuwasiliana vilevile kuna chombo nitakiweka kwenye simu yako kitasaidia kukamata maongezi yote ya simu zinazotoka na zinazoingia. Nina imani utanisadia , lakini Kallo ukinigeuka sisemi ila shuguli yangu unaijua, sijui utajificha wapi labda nife lakini kama ningali hai nitakutia mikononi. Huyo bosi wako ninakupa wiki nitamtia mikonini si yeye hata Father Gin,” nilitoa mkwara mzito nikiwa sitanii.

“Mmh, dada umepania.”

“Unajua Kallo, Mungu namwita wa ajabu kwa sababu haya mafunzo niliyopata japo wamenipa wao lakini ndiyo silaha ya kuuangamiza udhalimu wao unaoendelea labda nife leo lakini Mungu atanilinda na kuushinda udhalimu wao.”

"Da’ Thereza maneno yako yamenipa ushupavu na ushujaa moyoni nami nitakuwa nawe bega kwa bega sitakwenda kinyume na yote tuliyoahidiana.”

“Nimekuamini usiniangushe.”

“Sitakuangusha.”

“Nina imani tutashinda.”

Tulipeana mikono na kushikana kwa nguvu kuonyesha jinsi gani tulivyoungana mioyo yetu kuutokomeza udhalimu. Nilichukua simu yake na kuweka chombo maalum cha kukamata mawasiliano.

Kallo unavyokuwa upo na Marry White mkiongea utabonyeza kwenye kidude hiki utaona neno hili baada ya kujiandika simu itarudia katika hali ya kawaida hapo utakuwa umeungana na mimi kwenye mazungumzo yenu.”

“Sawa usihofu mambo yataenda kama yalivyo pangwa.”

“Basi wewe wahi Arusha una hela?”

“Ninazo.”

Nilimsindikiza Kallo hadi sehemu walikopaki gari lililowaleta, kwa vile John ndiye aliyekuwa dereva ilibidi aendeshe mwenyewe.  Kabla ya kuondoka aliniuliza swali.

“Sasa da Therza suala la watoto litakuwaje?”

“Hiyo kazi niachie nitakujulisha ulinieleza pale kambini ulinzi ukoje?”

“Ulinzi pale si mkubwa sana.”

“Una maana gani kusema si mkubwa sana?”

“Walinzi hawazidi watano, unajua wanajiamini kwa vile hakuna kitu cha kuchukuliwa zaidi ya watoto tena mwanzo kambi ilikuwa na walinzi wawili tu, watatu wameongezwa baada ya kufungwa ile mitambo ya kunyonyea damu na matanuru ya kuchomea watu.”

“ Asante kuna wahudumu wangapi?”

“Wako kumi.”

“En’he na mkutano umesema unaanza saa ngapi?”

“ Saa nne usiku.”

“Wana sehemu nyingine au ni ileile?”

“Ni ile ile, vipi utakuja?”

“Mmh..sidhani,lazima nijipange kwa leo waache wafanye mkutano wao ili kitakachofuata au ajenda ya mkutano utanijulisha ili nijipange vizuri.”

“Lakini dada si unajua jumatatu ndio inaanza kazi ya unyonyaji wa damu na uchunaji wa ngozi, ukichelewa utakuta tayari wameshateketezwa kama nilivyo kueleza damu inatakiwa haraka na leo pamoja na mkutano kuna wageni wanaokuja kuingia mkataba wa ngozi za binaadamu ambazo huzitumia kuvushia dawa za kulevya.

“Nitajitahidi lakini ondoka ukiwa na tumaini kuwa hawatadhuriwa na mtu yeyote.” 

“Sawa dada wacha niwahi.”

 Nilimuacha Kallo aondoke najua moyo wake wake ulitawaliwa na wasiwasi juu ya mpango tuliopanga wa kuwakomboa watoto.  Pamoja na kumuamini lakini haikuwa lazima kila nilichokifikiria kukifanya basi lazima nimweleze. Huwezi kumuamini mtu kwa asilimia mia hata awe ndugu yako wa damu.


                                                             ****

Niliamua kujipanga vilivyo ili majira ya saa moja usiku niivamie kambi ya Marry 

White kuwaokoa watoto kisha niwahi mkutano wao wa Arusha mjini majira ya saa nne usiku. Najua kwa akili ya kibinadamu haiwezekani lakini tuwe pamoja. 

Baada ya kujipanga nilichukua mlinzi mmojammoja mwenye uwezo wa kutumia chombo cha moto katika kila kitega uchumi changu. Pale nilikuwa nimeajili askari mgambo na askari waliofukuzwa kazi mdiyo walikuwa walinzi wa miradi yangu.

Baada ya kuwakusanya na kuwapa semina ya robo saa ambayo haikuhitaji swali zaidi ya kutekelezwa. Niliwaeleza wao kazi yao kubwa ni kuwalinda watoto kama nitafanikiwa kuwatorosha kwenye kambi.

Hakukuwa na mjadala zaidi ya kuingia ndani ya Nissan Patrol, walikuwa tisa na mimi wa kumi. Kila mmoja nilimpa silaha nzito kwa ajili ya kujihami panapo tokea tatizo.  Japo nilikkuwa na uhakika shughuli itakuwa nyepesi isiyo na madhara. 

Tuliingia wote na safari ilianza ilikuwa ni majira ya saa nane alasiri. Nilikimbiza gari kiasi kama ajali ingetokea au tairi la mbele kupasuka hakuna ambaye angepona.

Tuliwasili maeneo ya njia panda ya kuingia kambini  ilikuwa vigumu mtu kuitilia mashaka gari letu.

Tuliteremka wote na kumuacha mtu mmoja alinde gari tuliingia porini tuliizunguka ile kambi kilichonifurahisha askari wangu walikuwa makini sana tofauti na nilivyo wafikiria. Tulikwenda kwa mtindo wa kuvamia kambi ilionyesha ni jinsi gani walivyo iva kijeshi.

Tulitembea porini mwendo wa nusu saa, wakati huo giza lilikuwa linazidi kutanda  Nilipoangalia saa yangu ilionyesha ni saa mbili kasoro, taa za majengo zilitujulisha tumebakiza hatua chache.

Tulipobakiza kama hatua mia mbili niliwaomba wanisubiri na wakae tayari kutoa msaada japo sikujua uwezo wao. Nilitembea kwa mwendo wa paka kwenye mawindo hadi nyuma ya jengo. Eneo la nyuma lilikuwa linawaka taa kali iliofanya eneo ilionekana vizuri.

 Nilikuwa sina ujanja niliokota jiwe na kulirusha ambalo liliipiga ile taa na kuizima eneo lote la nyuma likawa giza. Nilisikia mtu akiongea kumbe hakuwa mbali na mimi, nilimuona akinipita huku akivuta sigara.

“ Hii taa sijui imefanya nini tena?” alijisemeza.

Nilitumia uzembe wa yule mlinzi kwa kumnyatia na kumtia kabali mithili ya kicheche na kuku na kumvutia kichakani nilikowaacha wanajeshi wangu, nilipofika nilimuachia baada ya kumsachi na kumkuta ana simu, sigara bhangi, kondom na magazini iliyokuwa imejaa risasi na bastola pia iliyojaa risasi.

Nilipomwachia alianza kukohoa, maana kabali ilikua si mchezo. Japo mtoto wa kike nilikuwa nimeshupaa, nilimuuliza swali:

''Unamjua Thereza?”

 "Thereza yupi?”

"Yule mliyepewa habari zake na Marry White?”

“ Sijawahi kumuona ‘live’ ila nimemuona kwenye picha.” 

Niliwasha taa ya tochi na kujimulika usoni na kumweleza:

"Ndio mimi.”

"Ooh! Mungu wangu nimekwisha.”

“Wala hujaisha, ukiwa mkweli utapona ila ukileta uongo wowote utakuwa mgeni wa kuzimu.”

“Sawa dada, uliza swali lolote nitakujibu,” aliingia woga. 

“Hapa kambini mpo wangapi?”

“Sisi askari au wote kwa ujumla?”

 “Askari.”

“Tuko watano.”

 "Wenzako wako wapi?”

 “Hapa kambini tupo watatu.”

“Wengine wako wapi?”

 “Wamekwenda mjini kwa wanawake zao.”

“Na wenzako wawili wako wapi?”

“Wapo ofisini wanacheza game."

“Mbona mmekuwa wazembe kiasi hicho?”

“Dada yangu tunalinda nini?”

“ Tutaongozana na wewe hadi kwa wenzako na ukileta utani au ujanjaujanja mwili wako nitatengeneza chujio la nazi kwa risasi,” nilimpa mkwara mzito.

Tuliongozana hadi kwenye ofisi moja ndani tulisikia sauti ya mlio wa game kwenye komputa na watu wakicheka kuonesha kuna  mtu kamfunga mwenzake.

Nilimsukumia ndani, ile hali iliwashtua walipotaka kuwahi silaha zao nilimuwahi mmoja na kitako cha bunduki kwenye taya lililomfanya apige kelele za maumivu.

Mmoja alijifanya mjanja kuchupa kupitia dirishani, mlio wa risasi wa mmoja wa askari wangu zilizompata mgongoni na kumtoa roho.

Tulitoka na yule askari aliyebaki hadi kwenye vyumba vya wahudumu ambao nao tuliwaweka chini ya ulinzi. Tuliwaamsha vijana wote waliokuwa wamelala na kuwakusanya sehemu moja kisha tuliwahesabu walikusanya wote sehemu moja kisha tuliwahesabu walikuwa ni walewale elfu mbili na mia tatu idadi niliopewa na Kallo.

Baada ya kuwakusanya nilizungukia mitambo ya kunyonyea damu na matanuru ya kuchomea miili ya watu ilikuwa ni mitambo ya kisasa inayoonyesha kugharimu mamilioni ya dola.

Nilitega kila kona mabomu kambi nzima wakati huo msafara ulielekea msituni askari wangu waliwazunguka wale watoto na wahudumu. Nikiwa namalizia kutega mabomu mara nilikuta nimetokea kwenye ofisi iliyo kuwa na mitambo na komputa ilionyesha ndiyo ofisi ya Marry White kwa juu ya meza kulikuwa na picha yake ndogo.

Nikiwa natafakari ninzie wapi mara nilisikia breki za gari nje ya jengo na sauti ya miguu ilielekea kule kwenye ofisi mara nilisikia mlango ukifunguliwa nilijificha chooni. Taa za ofisi ziliwashwa nilisikia watu wakiongea:

"We tafuta disk mimi naangalia kwenye kompyuta.”

Nilifungua mlango taratibu wa choo  na  kuchungulia niliwashuhudia mwanamume wa shoka wanne wenye mavazi ya kijeshi wakifungua komputa na kusoma vitu, mwingine alifungua droo na kutoa disk nyingi na kusoma moja moja alisema:

  "Hii hapa nimeipata."

 "Achana nayo hata mimi nishaipata kwenye faili wacha nimtumie moja kwa moja kwenye e-mail yake sister Marry White.”

Saa yangu ilionyesha bado dakika tano mabomu yalipuke na kuiteketeza kambi yote lakini sikuwa na ujanja. Ili kuokoa maisha yangu ilikuwa  lazima nijitoe muhanga la sivyo ningekufa kifo kibaya na dhamira yangu kupotea. Niliamua kusubiri dakia mbili labda watatoka. 

Nilipoangalia saa ilinionyesha bado dakika mbili mabomu yalipuke, muda ulivyozidi kukatika nikajua sina ujanja maana watu walio ofisini si watu wa mchezo walionekana ni watu kazi kama ningeingia kichwa kichwa ningeishia mikononi mwao. Mbaya zaidi nilimuona mtu mmoja macho yake yametazama mlango wa choo kama vile ameona kitu au amehisi kitu. 

Kitu kilichoniweka katika kipindi kigumu cha kuweza kujitoa mule chooni muda nao ulizidi kukatika. Niliwasikia wakiongea mmoja alisema.

 "Oooh, afadhali imekwenda.”alisema mmoja. 

“Ina maana hii CD haina umuhimu tena?”

"Haina  ila mwanangu mambo yakijipa tutaukata.”

"Yajipe mara ngapi wiki ijayo Sister Marry White ana kwenda kuchukua mavumba (pesa) Italia.”

 “Unakumbuka alituahidi kila mtu bilioni ishirini?”

“Si utani mwanangu lazima wanijue mi nani," mmoja alijigamba.

"Ulisema billion 150?”

"Unacheza! Trillion 150."

 Taarifa ile ilinipata picha nyingine akilini mwangu juu ya mpango wa Sister Marry White ya kwenda Italia kuchukua trillion 150. Pesa ambayo ilikuwa ikimchanganya akili Father Gin.

 Pamoja na kunifungua akili lakini maneno yao hayakuwa na umuhimu kwangu zaidi ya uhai wangu na maongezi yao yalizidi kula muda. Sasa ilionyesha bado sekunde sabini yaani dakika moja na sekunde kumi mabomu niliyoyatega yalipuke.  Nilijikuta mwili wote unalowa jasho kwa hofu ya kufa kwa mabomu. Niliamua liwalo na liwe kama kula bora waniue wao kuliko kufa kikondoo namna ile.

Vilevile bado hofu ilinitawala huenda pakatokea mapigano yatayochukua muda utaofanya mabomu yalipuke wakati bado tunapigana. Lakini niliona uoga wangu ndio utakaosababisha nife kifo cha kikondoo na haikuwa sifa yetu. 

Niliamua liwalo na liwe wazo lililoniijia ni kuipiga risasi taa na kukurupuka kuelekea mlangoni kama nitakosea mlango. Mungu ndiye anayejua na ndiye niliyemkabidhi uhai wangu.  

Kabla sijatoka juu ya choo kulikuwa na ki-uwazi kidogo kilichoonyesha siku za nyuma kulikuwa na kiyoyozi (Air Condition).  Japo tundu lilikuwa dogo kwa mafunzo yangu nilikuwa na imani nitapita tu.

Kwa haraka bila kuchelea niliuparamia ukuta kama paka hadi kwenye lile tundu lilikuwa dogo kwa mafunzo yangu nilikuwa na imani nitapita tu. Nilijipenya mithili ya paka na kujikuta ninafanikiwa kupita na kutoka nje ya jengo.

Wakati huo mwili wote ulikuwa unanivuja jasho kama mtu niliyenyeshewa mvua usiombe jasho la uoga, huwa linatoka mfululizo na kufanya nguo zote zitote. Asikwambie mtu maisha matamu hasa pale unapoona uhai unataka kutoka huku unaona. Nilipotua chini nilikuta zimebakia sekunde arobaini mabomu yalipuke.

Nilitimua mbio kuelekea msituni huku nikiangalia saa yangu, zilipobakia sekunde tano nilijirusha na kujilaza  chini. Baada ya muda mfupi kitu kilikubali, mabomu yalilipuka kwa mpigo na kulitetemesha eneo lote linaloizunguka kambi ya Marry White.

Wale vijana wa Marry White nao wote waliteketea pamoja na mitambo yake ya kunyonyea damu, nilijua lazima litakuwa pigo lingine la mwaka "PT yaani pigo takatifu.

Baada ya milipuko kutulia nilinyanyuka kuelekea kwa wanajeshi wangu na kundi la watoto na wahudumu. Niliwakuta bado wote wamelala chini. Nilipofika niliwaamuru wote wanyanyuke.

Tuliendelia na safari kuitafuta barabara kuu tulipokaribia barabarani, niliwaamuru askari wangu wawalinde wale watoto na wahudumu mpaka pale magari yatapofika kuwachukua.

Niliwapigia simu kwa ajili ya kuleta magari zaidi ya ishirini ya kuwasomba watoto wote kuwarudisha Dar es salaam. Niliwaachia jukumu kuwa magari yakifika tu basi wawapakie wote na kurudi nao Dar es salaam.  Vile vile niliwapa maelekezo ya kuwasambaza vipi watoto kwenye vituo vyangu ili wapate mapumziko mazuri.

Baada ya kukabidhi majukumu nilikimbilia kwenye gari muda ulionyesha saa tatu za usiku hivyo usiku hivyo ilikuwa imebakiza saa moja ili kuwahi mkutano wa Marry White na watu wake pamoja na hao wakala kulikuwa na ugeni wa kuingia mkataba wa kununua ngozi za binadamu.

Nilipofika kwenye gari, nilimkuta mlinzi amelala mpaka anakoroma, nilishangaa ulinzi wa kizembe namna ile.  Kwa hali ile lazima adui anajitawala atakavyo mbaya zaidi anakoroma ile kumrahisishia kujua amelala  kwani ameshajulishwa kwa mkoromo wa usingizi “kuwa njoo mimi mwenzio sijitambui.”

Nilimshtua nusra akurupuke nilimtuliza.  

"Vipi mbona unalala kama uko msibani?”

 “Aaah! Aaah..samahani sister."

"Mimi.”

“Samahani, adui utamwambia samahani itakusaidia nini?  Kuwa makini bwana tupo shughulini," nilimtaadhalisha.

''Sawa sister nitakuwa makini."

Alijibu huku akipiga miayo na kujinyoosha na mkono mmoja ukifikicha macho.

"Sasa ni hivi wewe utaungana na wenzako kuwalinda wale watoto kisha nijulishe, una simu?”

 "Ndiyo sister."

"Piga namba hizi ifikapo saa tano kamili, atayepokea mwambie kambi yote imeteketea kwa moto hakuna kilicho baki, sawa?”

 "Sawa sister."

"Usiniangushe na kutegemia wewe."

"Sasa hivi niko makini sana."

"Ok, tutaonana wacha niwahi, magari yakifika wapandisheni watoto tutaonana Dar." 

Niliingia kwenye gari na safari ya Arusha mjini ilianza mara moja. Niliwasili Arusha mjini baada ya robo saa. Nilitafuta eneo nililo elekezwa nilikuwa na imani Kallo alikuwa upande wangu. 

Eneo lilikuwa lilelile kwenye maeneo ya mtaa wa sokoine, lilikuwa jengo la kisasa la ghorofa nne, mzigo ulikuwa palepale  nilipomuagiza Kallo auweke, nilimweleza kama sitakwenda baada ya muda fulani auchukue.  

Ilikuwa ni sare wanayovaa wahudumu wa mkutano ule niliuchukua ule mzigo na kuufungua ndani. Nilikuta sare na kijikaratasi kilichoandikwa.

Sare hiyo ni kwa ajili ya vinywaji vya wageni hivyo ukivaa ingia chumba namba 103 hapo utamkuta mkuu wa ugawaji ataye kupa utaratibu

 Niliingia hadi hotelini na kuingia hadi hotelini na kuingia chooni nilibadili nguo na kuvaa sare ya muhudumu wa vinywaji. Nilitembea taratibu kuelekea ukumbi wa mkutano uliokuwa ghorofa la pili.

Jamaa mmoja mwenye suti nzito iliyomkaa vizuri mwilini alinishua:

 ''We vipi una fanya nini huku? Wahi ukumbi wa mikutano wageni wako njiani.”

 Nilichepua mwendo kupanda ngazi hadi ghorofa la pili niliinga chumba namba 103, Nilimkuta mzee mmoja aliponiona aliniuza:

"We nimekupaga  wapi?”

 "Bado.''

"Basi we utakuwa upande wa kuwapa maji wageni kwa hivyo chukua chupa za maji weka kila kitu sawa pamoja na glasi fanya haraka wageni wako njiani." 

Nilielekea ukumbini nilipoingia nilikuta kikao kinaendelea, meza ya kati alikuwepo mwanamke mmoja aliyekuwa mweupe kidogo kama albino mboni za macho yake zilikuwa bluu alikuwa mwanamke mzuri.

Nilijua huyu ndiye Marry White alikuwa amezungukwa na watu waliovaa suti nzito nyeusi walikuwa kumi na wanne, kwa hiyo walikuwa kumi na tano. Niliangalia sura zao. Mmh! Nilizidi kuamini maneno ya Kallo wote waliokuwemo ni walewale washirika wa Father Gin tofauti ni watu wanne yaani Marry White na washirika wake watatu ambao wote picha zao nilikuwazo.

Kwa vile walikuwa mbali kidogo nami sikuweza kusikia walichokiongea, nilichomoa simu yangu ndogo kama kalamu yenye kamera na uwezo wa kuchukua picha za video.

Nilianza kusambaza chupa za maji, macho yangu yaliangalia kwenye meza ya mkutano wa Marry White na washirika wake niligundua baadhi ya chupa zilikuwa zimeishiwa na kinywaji japo haikuwa idara yangu.

Nilikwenda hadi kwenye meza yao na kuanza kukusanya chupa wakati huo kamera ilizidi kupiga picha na kuchukua matukio. Niliwasogelea karibu wao waliendelea na mkutano wao bila kunigundua.  Nilipokuwa na uhakika picha yangu nilipokuwa na uhakika picha yangu nimeichukua vizuri niliondoka pale mezani na kurudisha chupa.

"We vipi hiyo si kazi yako, glasi umeishasambaza?” mkuu wa vinywaji aliniuliza.

"Bado."

 "Ona sasa kazi yako hujaimaliza unaingilia kazi nyingine isiyokuhusu, haya sambaza glasi haraka."

Nilizibeba glasi na kuzisambaza,  mara nilishangaa kuwaona wote wakinyanyuka na kutoka nje kwa pamoja baada ya dakika tano walirudi wakiwa wameongozana na msafara wa watu saba walikuwa ni waarabu saba wenye kanzu nyeupe na vilemba vyeupe.


Kila mmoja alichukua sehemu yake muda ule walihama kwenye ile meza yao kuu ya mkutano na kuhamia meza nyingine wote walikaa pamoja. Baada ya wageni kukaa, Marry White alisimama na kuwakaribisha wageni.  Wakati huo wahudumu wote tulitolewa ukumbini. 

 Kwa vile nilikuwa nimeshaweka kinasa sauti chini ya meza niliweza kuyasikia yote waliyozungumza. Wakati huo nilikuwa nikielekea nje ya jengo niliteremka ngazi hadi chini. Nilikwenda hadi choo nilichobadili nguo nilivaa nguo zangu na kuziacha zile za uhudumu mulemule chooni.

Niliyasikiliza maongezi yao, nilimsikia Marry White akisema:  

"Karibuni sana, tena mmekuja wakati mwafaka, jumapili tutakuwa tumeshakusanya ngozi za binaadamu elfu tatu ambazo nina imani mtaondoka nazo."

"Kwa hiyo bei ni ileile?”

"Hapana kutokana na gharama za mitambo ya kisasa kila ngozi mtaongeza dola 5000."

“Sawa hamna tatizo wacha tulipie ngozi zote 3000 na zingine tutazipata lini kwani tuna uhaba wa ngozi?"

"Sawa," mara nilisikia sauti ya makaratasi baada ya kama dakika ishirini nilisikia sauti ya Marry White ikisema:

"Hela, ipo sawa jiandaeni tu, vipi mnaondoka au mnasubiri mwondoke nazo?"

"Tunasubiri kwani sasa hivi tuna safari ya kutembelea mbuga za Tanzania za sehemu zote za kitalii maana wengi wamesifia uzuri wa mbuga na maziwa na kisiwa cha Zanzibar.”

“Ooh! Itakuwa vizuri nitakupeni mtu wa kukutembezeni nitatoa ofa kama wageni wangu."

 "Tutashukuru sana.”

Mara nilisikia simu ikiita nilipoangalia saa yangu ilionyesha ni saa tano na dakika tano,

Nilijua lazima atakuwa yule mlinzi niliyemwachia maagizo. Nilisikia Marry White akiita:

 "Hallo unasemaje?  Acha utani...  Usiniambie, ooh Mungu wangu," nilijua kimenuka.

"Vipi kuna nini bosi?" walimuuliza.

"Ee.. eeti lambi ya watoto yote imelipuliwa.”

 "Haiwezekani.. haiwezekani... Si rahisi huo ni utani tu bosi," mtu mmoja alipinga.

 "Hapana lazima twende eneo la tukio."

Walinyanyuka niliwaona wakiingia kwenye magari yao na safari ya kuelekea eneo la tukio ilianza na kusababisha kikao kuvunjwa.

Muda kidogo walitoka wale Waarabu saba na kuingia kwenye 'Hiace' na kuondoka.

 Nilikimbilia ndani nilikutana na Kallo akiwa amepigwa na butwaa.

 "Ha! sister Thereza ndo unafika?”

"Eeeh... kwani vipi?”

"Nasikia kuna tukio limetokea kambi ya watoto imelipuliwa nasikia hakuna kilichobakia ina maana hata watoto walinzi na wahudumu wote wamefariki,” Kallo aliongea huku akilia.  

Nilitaka kucheka lakini nikabana kicheko changu.

 "Kallo zile hela wamewahi kuondoka nazo?"

"Hela zipi da Thereza?"

 "Za manunuzi ya ngozi."

"Sijui lolote."

"Hebu twende kwenye meza ya mkutano."

Niliongozana na Kallo hadi kwenye ile meza tulikula fuko la pesa lipo pale pale chini ya meza. Niliingiza mkono na kutoa bando la pesa zilikuwa dola tupu.

"Ha!" Kalo alishangaa.

"Usishangae mdogo wangu hili ndilo jasho letu sasa zibebe unifuate."

Niliweka lile fuko kwenye gari langu, mara simu ya Kallo ililia alipokea:

"Haloo Kallo huwezi kuamini kambi yote imelipuliwa sijui ni mshenzi gani huyu lazima atakuwa Thereza akishirikiana na Father Gin.. Kallo..Kalo unanisikia nitawafundisha adabu labda sio mimi Marry White naapa watajuta kuzaliwa hawawezi  kunitia hasara kiasi hiki subiri nirudi Italia watanijua mimi nami nitawatafuta mimi mwenyewe na kuwaua kwa mkono wangu.”

Ilikuwa sauti ya kilio ya Marry White baada ya kushuhudia jinsi nilivyo isambaratisha kambi yake vilevile alijua na watoto wote wameuawa.

"Sasa ndio itakuwaje?" Kallo aliuliza.

''Tunakuja sasa hivi tutajua la kufanya,” Marry White alikata simu.

"Umenieleza wageni wale, Waarabu wamefikia wapi?"

 "Ngurudoto."

"Ok , wacha niwahi Dar tutawasiliana usiwe na wasi kila kitu kipo sawa na hii hela tutagawana sawa japo sijui ni kiasi gani.” 

 Niliagana na Kallo nilielekea hoteli ya Ngurudoto kuwafuatilia wale Waarabu, sikutaka ajue chochote juu ya mipango yangu. Niliwasili maeneo ya hoteli ya Ngurudoto na kuliegesha gari langu kwenye maegesho. Niliteremka na kuelekea mapokezi.

Nilimuuliza mhudumu wa mapokezi ambaye aliyeonekana kusinzia, saa yangu ilinionyesha ni saa sita kasoro.  Nilimuuliza sehemu walipo wageni wale Waarabu alinijulisha wapo chumba namba 099 na 100. Niliagana naye nilimuacha akiendelea akiendeleza usingizi wake, baada ya kuondoka nilimuona akilalia kaunta kabisa.  Nilikwenda hadi chumba namba 099 na kugonga wakati huo nilikuwa nimeshikilia bastolaaliyefungua nilimwekea kifuani na kumsukumia ndani.

Niliwakuta wakicheza karata usiku ule huku wakinywa kahawa iliyokuwa kwenye chupa kubwa ya chai.

Aliyenifungulia mlango nilimuamuru arudi nyuma kwa wenzake, mmoja alitaka kuchukua bastola nilimkemea kwa sauti kali kwa kumwambia akifanya ujanja wowote basi atakuwa mgeni wa kuzimu niliwaomba wanijibu maswali yangu.

“Ninyi ni akina nani mmekuja kufanya nini?”

"Sisi ni watalii tumekuja kutalii."

" Mkutano mliofanya nusu saa, mliingia mkataba wa nini na jasusi Marry White na kundi lake?”

Swali langu liliwashtua wote niliwaona wanatazamana.

 "Mbona hamnijibu,  mnajifanya watalii kumbe mna mchezo mchafu? Basi leo ndipo mwanzo na mwisho wenu," nilisema kwa sauti kali.

Niliifuata ile chupa ya chai yenye kahawa na kuimiminia unga wa sumu na kuwalazimisha wote wanywe. Wa kwanza alikuwa mbishi alitaka kupimana ubavu na mimi.  Ngumi aliyorusha niliona nilimpiga mapigo manne ya mfululizo yaliyomvunja taya na damu kumtoka kwa wingi.

Waliobaki walikunywa kikombe kimoja kimoja na yule niliyemjeruhi naye alikunywa.  Ndani ya dakika tano wote walikuwa wageni wa kuzimu, nilijisemea moyoni:

"Washenzi kama ninyi hukumu yenu ni hii.”

“Nilifanya upekuzi wa vyumba vyote walivyopanga na kukuta pesa nyingi mchanganyiko yeni, dola na pesa za Kitanzania niliziweka kwenye mfuko mmoja na kutokomea zangu.

                                                                  ****

Niliwasili Dar  saa kumi usiku sikulala nilikwenda moja kwa moja kwenye vituo vyangu vya kulelea watoto na kukuta wote wamefika salama.  Niliwapa asante wote nilioshiriki nao kwenye operesheni ile dola 1,000 kila mmoja.Nilirudi nyumbani na kupumzika kabla ya kulala nilimshukkuru Mungu kuweza kunifanikishia operesheni Pigo Takatifu PT, Baada ya kuoga nilijilaza.

 Mlio wa simu ulinishtua saa ya mezani ilinionyesha tayari kumekucha ilikuwa ni saa mbili kasoro asubuhi. Nilipoangalia namba ilikuwa inatoka kwa Kallo.

  "Eehe Kallo leta habari."

 "Da’ Thereza kazi yako nimeisikia.”

"Ipi hiyo?"

 "Ya Ngurudoto, umezidi kumchanganya Marry White, nusu aingie wazimu."

"Hiyo ndogo,”  ilibidi nimweleze na ukweli wa kazi ya kambi ya Marry White.

"Aisee usiniambie kumbe wapo hai, sasa da’ Thereza ni hivi Marry  White anaondoka jioni ya leo kufuata zile pesa Italia.”

"Unasema kweli?"

"Ndio mapigo uliyo mpiga yamemchanganya hivyo anafuata pesa alipe kisasi."

“Sasa sijui itakuwaje?"

"Nitaifanyia kazi."

Taarifa ya Kallo ilinivunja nguvu kwani kutokana na shuguli ya siku tatu isiyo na mapunziko nilihitaji muda wa kupumzika ili nipate muda wa kujipanga vizuri.

Lakini nilikuwa sina jinsi sababu maji niliisha yavulia nguo sikuwa na budi kuyaoga. Ilibidi niamke ili nijue nitawezaje kumawahi Marry White asichukue zile hela.

Niliamka na kuoga harakaharaka na kumpigia simu Father Gin ili aniandalie safari ya Ujerumani jioni  ya siku ile.

"Vipi umeshaaanza kazi au vipi?"

"Nimeona nifanye uchunguzi kwanza kule kwenye donge nono ambalo nina imani ndio roho yako,” nilimdanganya Father Gin sikupenda ajue kinachoendelea.

"Ni kweli kabisa Thereza ukiweza kunifanikishia kuzipata hizo hela zangu zawadi nitayokupa ni ya ajabu ambayo hujaitegemea katika maisha yako yote."

Baada ya kauyli ile nilichekea moyoni na kujisemea:

“ Zawadi ya ajabu ndio hiyo ya kifo, nilimuona mtu anayejiona amevaa kumbe anatembea uchi siri zake zote zilikuwa mkononi mwangu. Vilevile nilimuonea huruma kutokana mpango kabambe wa kumteketeza na kummaliza ulioandaliwa na wenzake wanao mla mgongo bila kujijua.

"Sasa Father uhakika wa safari nitaupata saa ngapi?"

"Muda si mrefu ila we jiandae na safari vilevile kama kuna msaada wowote unaoutaka kwangu usisite njoo uchukue. Thereza wewe ndiye ninayekutegemea baada ya kifo cha Dakta Ray.”

"Hamna tatizo, halafu Father nilikuwa naomba leo kabla sijaondoka unipeleke kwenye kambi ya wale vijana, ili nikirudi niianze kazi mara moja, " nilitaka kuua ndege wawili kwa jiwe moja.

"Hamna tatizo, basi acha nishughulikie suala lako la usafiri kisha tuongozane."

"Sawa Father.”

Baada ya kukata simu nilikumbuka kuna mzigo wa pesa niliokuja nao, nilichukua mfuko na kuzihesabu  zile hela nilizotoa Arusha kwenye mfuko wa mauzo wa ngozi za binadamu.  Kulikuwa na dola laki nne na nusu na zile nilizochukua kule hotelini zilikuwa dola laki saba na ishirini na nne elfu.Nilitenga na kuchukua dola laki mbili na nusu ni kamwekea Kallo.

  Nilichukua ramani yangu ya mji wa Dusseldorf Ujerumani, niliangalia jinsi eneo analoishi yule mkuu wa uwakala wa kununua ngozi na damu na dawa za kulevya, Ilionyesha anakaa mtaa wa Ost-strabe

 Hoteli iliyopo karibu na mtaa ule ni HOLIDAN INN DUSSELDOF CITY ENTR-KONIGSA,  iliyo barabara ya Harold Strabe. 

Mazingira yalinionyesha kama hakutakuwa na tatizo lolote nitaweza kuingia katika chumba cha huyo mkuu bila tatizo.  Nikiwa bado napanga kete zangu ili nishinde mchezo japo nilijua ni wa hatari kwani kosa langu lolote litagharimu maisha yangu, Mara simu yangu iliita, niliiangalia namba ilikuwa ya Father Gin.

 "Haloo Father lete habari.”

"Mambo yamekwenda vizuri safari ipo,  kama sasa hivi upo tayari njoo mara moja nikupeleke kwenye ile kambi ili upate muda wa kujiandaa na safari yako ya Ujerumani."

"Sawa nakuja."

Kwa vile nilikuwa nimeshajiandaa nilitoka kama kawaida yangu kwa kuruka ukuta na kutokea mtaa wa nyuma na kukodi gari hadi kanisani. Nilipokewa mapokezi na wasichana waliovaa mavazi ya utawa. Mabinti walipendeza kwa mtu yoyote angewaona angejua ni watumishi wa bwana kumbe ni miongoni mwa kundi la mashetani wanyonya damu.




Waliponiona walinikaribisha kwa heshima na upole:

"Bwana asifiwe."

"Ameni.”'

 "Karibu sana mtumishi."

"Asante."

 "We  ndio Thereza?"

"Ndio mimi."

"Ooh vizuri, Father amesema ukifika upite moja kwa moja.”

"Asante nashukuru."

Niliingia moja kwa moja hadi kwenye sebule bahati ndio wakati huo Father Gin alikuwa anatoka ofisini kwake.

 "Ooh! Thereza karibu sana.”

“Asante Father.”

"Pata kinywaji ili tuondoke."

"Hapana Father nipo tayari."

''Ok, tunaweza kwenda.”

Niliongozana na Father Gin hadi kwenye gari Toyota Land Cruser V8 ya rangi nyeusi yenye vioo vilivyowekewa kivuli (tinted) nyeusi.

Niliongozana na Father Gin kwenye gari tulikuwa wawili, tulielekea barabara ya Kilwa baada ya ukimya mfupi Father Gin aliuvunja.

"Thereza ukifanikisha operesheni kuna mpango ambao nina imani utaniingizia pesa nyingi.”

"Upi huo?" nilimdodosa bila kujua.

"Nataka kupandikiza ugonjwa na dawa nitauza mimi."

"Utafanya vipi?”

"Unajua Thereza siku zote mtu akipanga kitu si kukurupuka hili nimelipanga muda mrefu na kama si upuuzi wa Marry White na wenzake ungekuwa umeanza ni hivi nimetengeneza virusi ambavyo nimevirutubisha kwenye mwili wa binaadamu ambao utaleta ugonjwa wa ajabu ambao dawa yake haitapatikana popote ila kwetu.

"Na tutauza kwa bei nafuu kwani wengi watanunua kwa ajili ya kinga hapo tutakusanya mamilioni ya pesa si Tanzania tu hata majirani lazima watanunua kwa ajili ya kinga.''

"Mmh! Sawa sasa unatarajia kuufanya lini huo mpango?”

"Baada ya operesheni hii."

Wakati huo tulikuwa tumefika Chamazi tuliacha barabara kubwa na kuingia kushoto, tulikwenda mwendo wa robo saa ndipo tulipofika kambi ya Father Gin. Ilikuwa imejengwa vizuri tofauti na ya Marry White. Ukifika utasema ni chuo cha dini jinsi wahudumu wake walivyovaa sare zao za utawa. Asilimia kubwa ya sehemu za Father Gin  wafanyakazi wake wengi ni wanawake.

Nilipokelewa kwa heshima kama vile ni watumishi wa Bwana wa kweli lakini kumbe nyoyo zao zimeshabadilishwa na shetani anayejiita Father. Lakini Mungu hamfichi mnafiki nilijua  ipo siku siri yake itakuwa hadharani kama si mimi basi yupo mwingine atayetokea kwa uwezo wa Mungu.

  Alinitembeza kambi yote ambayo ilikuwa kubwa, iliyokuwa na vijana elfu nne. Pia alinitembeza kwenye kambi yote kwenye mitambo ya kunyonyea damu matanuru ya kuchomea watu.

Mitambo ya Father Gin ilikuwa mingi ila iliyoanza kuchakaa tofauti na ya Marry White.  Niliiangalia mandhari ya mule ndani na eneo lote.  Vilevile ulinzi ulikuwa dhaifu ilitokana kuvuli chao cha utumishi wa dini. Udhaifu huo nilijua ndio utaonisaidia kuwakomboa vijana ambao walionekana wana afya njema wanaoyafurahia maisha kumbe ni zao la damu na ngozi.

"Thereza umeona mali ilivyopendeza? Wewe tu, watoto wanazidi kunipa hasara wanakula tu kama mchwa kila siku napoteza si chini ya laki tano."

 Sio siri moyo uliuma kusikia eti mtu anawaita wanaadamu wenzake mali. Nilijikuta nahama kimawazo niliijiwa na picha ya ajabu pale nilipojiona kama nitakufa basi watoto wote walio kwenye vituo vya kulelea watoto wa mitaani, yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ndio watakuwa vuno la kuwaingizia pesa madhalimu hawa. Hata Father Gin aliponiita nilikuwa mbali:

“Vipi Thereza una mawazo gani? Inavyoonekana hatuko pamoja.”

"Ni kweli Father."

 "Unawaza nini?”

 "Kuhusu safari yangu, nilimdanganya.

”Utashinda nakuamini."

Tulirudi mjini na kuagana na Father Gin baada ya kuniongezea vitendea kazi vya hali ya juu. Nilipita sehemu niliyomweka Kalekwa alelewe.  Hali yake ilikuwa inaendelea vizuri, nilirudi hadi nyumbani na kujiandaa na safari ya Ujerumani.

                                                               ****

Majira ya saa moja na nusu nilikuwa ndani ya shirika la ndege la Swiss Airways majira ya saa mbili kasoro ndege iliondoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere.  Nilikuwa na mengi kuhusu safari yangu nilijiuliza uwezo wa watu ninaokwenda kupambana nao. Wasiwasi  wangu ulikuwa juu ya uwezo wa jasusi mkuu kuwa ni mkubwa.  

Niliwasili mji wa Dusseldort.  Ujerumani majira ya saa tatu usiku siku ya pili.  Uwanja wa ndege ulikuwa na pilikapilia polisi walikuwa wengi na msako ulikuwa mkubwa kutokana na tishio la kigaidi.

Ilibidi wageni tuchelewe kwa saa mbili, upekuzi wao tuliruhusiwa kutoka uwanja wa ndege wa Rhein Ruhr Flughfeh Dusseldort. Flughfeh Dusseldort.

Nilikodi gari hadi hoteli ya Holiday in Dusseldof City CNTR-Kowegsa iliyopo barabara ya HoroldsstraBe.  Nilipofika nilichukua chumba na kuweka vitu vyangu nilijikoki vitu muhimu na kutoka. Mji wa Dusseldof ulikuwa na pilika pilika kila mtu alikuwa na shughuli zake hakuna aliyekuwa na habari na mwenzake.

Nilitembea kwa miguu kutoka mtaa wa Horold straBe kwa mwendo wa kuharakisha kidogo, usiku ule hali ya hewa ilikuwa ya baridi.

Nilitembea hadi njia panda ya Horold straBe na Ost-straBe nilikata kushoto na kuanza kuitafuta nyumba anayoishi Mr Michael, jasusi wakala mkuu vile nilipata historia yake ni trionea anayetikisa kwa utajiri.

Nyumba niliiona niliipita na kwenda kwa mbele kwenye mtaa wa mbele kwenye mtaa wa Stein-str nilikata kushoto hadi kwenye mtaa kipande ambao unarudi hadi mtaa wa Harold. Niliufuata ule mtaa wa tahadhari kubwa na kuangalia labda kuna mtu ananifuatilia lakini hakuwepo. 

 Nilivuka kama nyumba sita na kuingia kwenye uchochoto mmoja kama ramani ilivyonionyesha. Nilikwenda hadi nyuma ya jengo alilopanga Mr Michael.

Niliangalia kulia na kushoto lakini hapakuwa na kitu cha kunitilia hapakua na kitu cha kunitilia wasiwasi.

Nilitoa glovu zenye makucha na viatu vyake maalum kwa kupandia ukuta na miamba na kuvaa mikononi na miguuni, nikaanza kuukwea ukuta hadi ghorofa la tatu. Sehemu nilijiingiza hadi ndani ya bafu. Hakukuwa  na mtu mlango pia ulikuwa haukufungwa.

Nilisikia watu wakizungumza, nilichungulia taratibu, na kuwaona watu wawili mzee mmoja wa makamo mwenye tumbo kubwa na kichwani vinywele kidogo lakini sehemu kubwa ya kichwa ni upara.

Alikuwa na mwanamke ambaye si mwingine ila Marry White walikuwa kwenye Computer. Mara waliacha walichokuwa wakikifanya kwenye Computer na kuanza kupapasana kimahaba mara niliona wakishikana mkono na kuondoka pale. Kutokana na hali niliyowaona nayo nilijua wamekwenda chumbani kurusha roho.

Nilisubiri kwa muda kisha nilinyata kuwafuatilia, nilipofika nilikiona chumba na mihemo ya watu walio kwenye dimbwi la mahaba ilisikika. Nilirudi hadi kwenye Computer nilikuta ndio zile pesa zinataka kuhamishiwa kwenye akaunti ya Marry White, lakini bado hazijatumwa. alikuwa ndio anaingiza namba za akaunti ya Marry White. Mara simu ya Marry White iliyokuwa juu ya meza ililia nilijikuta napagawa kwani  nilikuwa nimefuta  namba za akaunti ya Marry White ili niingize zangu. Nilijikuta nimetaharuki nilijiuliza nirudi chooni au nijifiche chini ya meza ile.

Ndani nilimsikia Marry White akimuomba samahani Mr Michael ili atoke kusikiliza simu.  Niliamua kujificha chini ya meza, Marry White mara alitoka chumbani akiwa hana kitu mwilini, yaani mtupu, si unajua alikuwa kwenye rusha roho.

Alitoka akiwa hana wasiwasi alijiamini kwa kiasi kikubwa akijua sitaweza kuwepo eneo lilie. Niliamini kama ningemuibukia mbele ya uso wake lazima angekufa kwa mshtuko. Alitoka hadi kwenye meza ile ya Computer na kuchukkua simu yake iliyokuwa bado inaita:

"Haloo Jimmy kuna habari gani?”

"Vipi umefika salama?"

 "Aah hilo si la kuuliza,  nimefika salama ni sekunde chache nakamilisha mambo yote nikirudi ni chereko chereko."

“Ndicho tunachokisubiri sio siri sister, huyu malaya katutia hasara lazima nimchune ngozi kwa mikono yangu siku tutapomtia mikononi.”

“Hana ujanja ngoma yake ya kitoto haikeshi, nikirudi ajue amekwisha na huyo hawara yake shetani Gin."

"Jimmy vipi kuna jipya maana simu inaonyesha si ya kawaida?"

"Ni kweli sister."

"Ee’he, kuna nini tena?"

"Habari za mtandao zinasema Thereza ameonekana jioni ya jana anasafiri kwa shirika la ndege la Swiss Airways hatujui amekwenda wapi."

"Mmh! Mna uhakika na mnachosema?"

"Ndio maana tukakutaarifu isije kuwa anakufuatilia."

"Mmh! Sidhani, lakini nitafanyia kazi hata hivyo kishachelewa pesa yote nimeshaidhibiti hilo lisikutie wasi.”

"Hapana dada yule msichana ni hatari kwani maisha yako vilevile ni muhimu."

"Nashukuru kwa taarifa yako nitakuwa makini kuanzia sasa."

"Sawa sister ni hayo, kama kuna mengine nitakujulisha, sijui unarudi lini?"

"Kazi imemalizika, nisubiri nini narudi usiku huu huu.”

"Ok sister kazi njema.”

"Asante,” Marry White alikata simu wakati huo Mr michael alikuwa akiunguruma ndani kwa uchu kama fisi aliyenyang'anywa mfupa.

 "Sweet fanya haraka bwana simu gani mwaka mzima?”

"Nakuja darling si unajua napata habari za  Tanzania, nipo kwa ajili yako ushindwe wewe tu."

Marry White aliirudisha ile simu juu ya meza  na kurudi chumbani kuendeleza kurusha roho na Mr Michael. Kwa upande wangu kila kilichokuwa kikifanyika nilijua ni uwezo wa Mungu.  Marry White hakushtuka chochote wala hakuwa na wazo lolote la mabadiliko kwenye Computer japo alikuwa anatazamana nayo.

Aliporudi chumbani kuendeleza  'uchafu' wao nami nilichukua nafasi ile kufanya kilichonileta. Niliingiza namba za akaunti yangu na kuzituma zile pesa trion 150 bila pingamizi ziliingia kwenye akaunti yangu.

Nilichokifanya ni kuiunguza program ya Computa kufuta ushahidi niliweka kinasa sauti chini ya meza ya Computer ili kunasa mazungumzo yao wataporudi kutoka kwenye uchafu wao.

Nilitoka kwa kupitia njia niliyoingilia ni kuwaacha wapo juu ya kilele cha mahaba kila mtu akimwagia sifa mwenziwe. Nilipitia dirisha la bafuni na kutoka nje niliteremka ukuta ule mpaka chini.  Wakati nafika chini nilishtukia mwanga mkali wa tochi, alikuwa mmoja wa askari wa doria.

"Haloo unatoka wapi?”

"Najisaidia afande."

"Usinichezee yaani unajisaidia juu ya nyumba za watu?"

“Watu?" nilijifamnya kushangaa.

Wakati huo alikuwa ameshanifikia karibu na kuanza kunipekua mikono ikiwa juu.

Nilijua ishakuwa noma, nilitulia nikipanga jinsi ya kujitoa mikononi mwa yule mnoko.

Vitu nilivyokuwa navyo sikuwa na tofauti na gaidi lazima ingehusishwa moja kwa moja na ugaidi. 



Aliponieleza nigeuke ili aendelee kunipekua nilitumia nafasi ile kusogea mbele kidogo na kugeuka na teke jepesi lililompata shingoni na kumpotezea fahamu. Nilimvuta pembeni na kumlaza pale uchochoroni. Harakaharaka nilirudi hotelini kupitia ule mtaa mfupi hadi mtaa wa Horold streBc.

Nilichepua mwendo hadi hotelini ambapo nilichukua mzigo wangu na kuondoka usiku ule ule.  Bahati nzuri nilipata nafasi ya ndege iliyokuwa ikiishia Oman. Niliingia kwenye ndege moyo ukiwa bado si wangu.

Nilijiuliza nitatoka salama kweli? Nikiwa nimo kwenye ndege ya Gull Air nimetulia kwenye kiti changu head phone zikiwa maskioni niliwasikia Marry White na Mr Michael:

 "Haloo sweet hii computer imefanya nini mbona imezima?"

“Nikuulize wewe.”

"Nitajuaje wakati tulikuwa wote?"

"Ooh..aisee huwezi amini computer imeungua.”

"Acha utani Mr Michael!”

"Ni kweli si unaona vipimo?”

"Haiwezekani! Basi washa nyingine.”

“Kumbukumbu zote zilikuwa humu, haijawahi kutokea lazima umenichezea akili Marry White.”

"Sikuelewi Mr Michael."

"Marry White nieleze ukweli nani amefanya hivi?”

"Usinichanganye Mr Michael unataka kunitapeli?"

"Hebu ngoja."

Baada ya kama dakika saba nilimsikia Mr Michael akisema:

"Marry White unanifanya mimi ni mtoto?"

 "Kivipi?”

"Unaona hii.. pesa zote trion 150 zimehamishwa! kibaya zaidi mmeniulia na computer yangu muhimu kama roho yangu ni vitu vingapi vimepotea?"

"Usinichanganye, usiniletee ujanja pesa yangu utaitoa tena safari hii si kwa kuihamisha bali unanipa mkononi.” Nilisikia sauti ya Marry White.

"Unacheza binti yaani ujanja uliomfanyia Father Gin ndio umenigeuzia mimi?  Hapa utachemsha kwanza toka humu ndani, ushanitia hasara kubwa.”

"Humu ndani sitoki mpaka umenipa hela yangu la sivyo nitakuua kama nilivyo muua mkeo."

"Binti mtu mzima atishiwi nyau kabla hujaniua utakufa wewe."

Dakika tatu baadae nilisikia sauti za mapigano na vilio vya maumivu, vilivyodumu zaidi ya dakika kumi..mara nilisikia sauti ya muhemo ya Marry White:

"We firauni huu ni mtambo mzito hao vijana wako sita hawatoshi labda ungekuja na jeshi zima..sasa nasema hivi nataka hela yangu au nakufumua ubongo," nilimsikia akihesabu:

Moja mbili tatu..tatu tatu shiti," nilisikia mlio wa bastola ikimaanisha Marry White kamuua Mr Michael.

"Huwezi kuniletea utapeli nikuache," sauti ya Marry White ilitamba.

Palitokea utulivu wa muda wakati huo ndege ilikuwa hewani mara nilimsikia akisema:

"Oooh..afadhali wacha niondoke na hizi hundi za Mr Michael zitapunguza maumivu, si siri mbona mwaka huu wangu sijui ni nani aliyefanya nchezo huu mchafu au Thereza? ..Inawezekana ni njama Mr Michael kunihadaa kimapenzi ili anidhulumu lakini kwa nini sikufanya nilicho kifuata na kujiingiza kwenye mapenzi na kuvuruga kila kitu? Acha niondoke niwahi ndege sehemu hii sasa hivi haifai."

Mara nilisikia sauti ya mlango kufungwa kuanzia hapo sikusikia kitu chochote nilijua Marry White ameshaondoka.

Nilimshukuru kazi yangu ilikwenda vizuri bila kumwaga damu, vilevile kupunguzana wao kwa wao nina imani mzizi mkuu Mr Michael ulisha ng'oka matawi Marry White na Father Gin watakuwa wepesi.

Nilipofika Oman niliunganisha ndege hadi nyumbani Tanzania, nilipofika nilikwenda kwangu moja kwa moja nilikuwa nimechoka kupita kiasi. Nilipofika nyumbani nilioga na kujilaza hata bila kula. Usingizi ulichukua masaa manane bila kugeuka.  Nilijipa mapumziko ya wiki nzima bila kujishughulisha na chochote zaidi ya kumchukua mdogo wangu Kalekwa kuwa naye muda wote wa mapumziko na afya yake iliendelea vizuri.

Baada ya wiki, nikiwa nimetulia mara nilipata simu toka kwa Kallo:

"Vipi Kallo?"

 "Da Teddy ni hivi, sasa hivi huku watu wamepagawa baada ya kuzikosa trioni 150 japo wameambulia trion 10 kutokana na hundi alizozichukua Marry kwa Mr Michael na una taarifa kama wakala mkuu Mr Michael aliuawa na Marry White?"

"Hata sijui..kwani nini?" nilijifanya sijui kitu.

"Anasema eti amemzidi akili lakini maelezo yao yanakulenga huenda ni wewe hivyo mkakati uliopangwa utafikiri Marekani walivyo mkamata Saadam Husein da’ Teddy kuwa makini ni watu waliotumwa si watu wa mchezo.”

"Usiwe na wasi mdogo wangu na kwa taarifa yako trioni zote 150 nimezichukua."

"Acha utani da Teddy!”

"Mi na wewe hatuna utani ni hivi sasa ndio naingia kazini rasmi, japo wananitafuta moto utawawakia, usihofu ndugu yangu asante kwa taarifa yako muhimu."

 "Kweli we kiboko!”

"Tumeombe Mungu turuke salama ili uje uishi maisha ya peponi."

''Na dua zetu Mungu atazipokea.”

"Ameni,” nilikata simu.

Wazo lilinijia niende kwa msaidizi wa Father Gin  yeye mwenyewe anapokuwa yupo nje. Alikuwa mama wa makamo mwenye sura ya upole, uso wake ulijengeka huruma sikuwahi kumkuta akiwa na furaha.  Sikujua  kwa sababu gani, mwanzoni nilijua huenda dini imemuingia hata kauli zake ni za kukujaza moyo ili usiwe mnyonge.

Lakini kumbe alikuwa na sura ya shilingi yenye pande mbili upande mmoja mtu mpole mwema na mkarimu  lakini  upange wa pili alikuwa msaidizi mkuu wa jasusi Father Gin.  Sikuelewa yule mama alikuwepo sehemu inayomchukiza mwenyezi Mungu kwa  kupenda kwake, njaa au ni vitisho kama alivyopata Kallo na wenzake ndio vimefanya awepo pale. 

Nilijua ningepitia kwa mama huyo aliyefahamika kama mama Monika mwenye miaka 58-60 ningepata maelezo mengi kuhusu Father Gin ambayo yangenisaidia kumteketeza kirahisi lakini pia kujua mradi wake na maabara yake aliyorutubisha virusi vya ugonjwa ili niharibu mpango wake. Niliamini dawa ni kumvamia mama Monika nyumbani kwake.  

Niligundua kwamba nyumba yake ilikuwa mulemule ndani ya kambi ya Kimanzichana. Niliamini kwanza uvamizi wangu isingemshtua mtu yeyote kwani wengi wangejua mimi ni mtu wao. Nilipanga siku ile majira ya saa kumi na mbili nimfuate nyumbani kwake muda huo huwa amepumzika kwa ajili ya kazi ya kutwa nzima.

Majira ya saa kumi na mbili jioni niliruka ukuta kama kawaida yangu na kutokea upande wa pili. Kutokana na msongamano wa magari na utundu wa dereva tulifika  Mbagala rangi tatu saa kumi na mbili na nusu. Tulipovuka Vikindu nilishangaa kuona gari letu limezingirwa na magari zaidi ya matano.

 Tulitulia bila kuteremka garini lakini nilikaa mkao wa shari kwani nilijua nipo msambweni. Mara aliteremka mwanaume mmoja mwenye mwili mkubwa wa mazoezi na kuja kwenye gari letu.  

Alifungua mlango na kumtoa dereva kwa kumtupa nje, alinifuata na kunishika  kunivuta nje. Alinibeba juujuu hadi kwenye uwazi na kunitupa chini, nilibakia nikishangaa nikijua nimepatikana ni yale niliyoelezwa na Kallo.  Nikiwa bado nipo chini nilipotupwa mara liliingia Benzi moja jeusi.

Lilisimama katikati ya magari yaliyokuwapo pale, mtu mmoja mwenye mwili mkubwa uliojengeka kimazoezi aliyevalia fulana iliyombana barabara mwilini alikwenda kufungua mlango.

Aliteremka Marry White alisimama nje ya Benzi na kuliegemea kisha  alinifuata pale chini nilipokuwa. Alinishika uso wangu na kuunyanyua kisha alisema:

"Hongera sana."

"Asante," nilijibu kwa jeuri.

"Umejitahidi, lakini nilijua ngoma yako ya kitoto  haikeshi na kweli haikukesha sasa ndio utanijua mimi ni nani..huyo hawara yako shetani Gin ananijua mimi nani?”  sikumjibu kitu nilimwangalia tu.

"Yaani bosi aliyekuwa anatusumbua hivi ni huyu?” aliuliza yule baunsa aliyenitoa kwenye gari.

"Ni huyu.”

 "Hata mimi nashangaa basi ndio ameshaingia kwenye moto wa gesi, atabakia majivu.” Kallo alikuwa miongoni mwa watu waliokuwepo pale alimuona aliniangalia kwa uso wa huruma kwa kuamini ule ulikuwa mwisho wangu.

"Jamani shughuli yote uwanja wa damu au sio?” alisema Marry White.

"Ndiyooo,” waliitikia wote.

"Lakini hawezi kuondoka hivi hivi kama mwari yeye si mjuzi wa kupigana, George vipi upo tayari?”

"Ndiyo bosi, nampasua kifua.”

"Haya kazi kwako,” George alijianda kunishikisha adabu.

Nikajua pale maisha yangu yako hatarini kupona ni vigumu, nilitumia nafasi ile kuondoka na watu watakaojipendekeza.  Nilipomuona yule mwenye mwili mkubwa anakuja nilinyanyuka.

Kama kawaida alipotaka kunipiga teke nilimpisha kidogo na kupiga teke la mchongoko kwenye sehemu zake na siri, alipiga kelele za maumivu. Nilijua pigo lile lilimtosha, alikuwa akilia huku akigaagaa chini kwa maumivu. Wa pili yeye nilimmaliza kwa teke la kuzunguka yeye alipiga la juu mimi nikausomba  mguu wake chini na kummalizia na kifuti kilichomvunja shingo yake.

Kuona hivyo ndipo walipokuja wengi hapo kwa kweli nilipigana kufa ama kupona.  Katika watu kumi na tano nilifanikiwa kuwaua saba lakini nilipigika sana. Ndipo Marry White alipowaamuru waniache akavua nguo zake na kubakia na 'skin tight' iliyombana vyema na kuanza upya mpambano.

Mwanzo tulipigana vilivyo kila mtu alionyesha uwezo wake, lakini kwa vile nilikuwa nimepigana kwa kipindi kirefu nilikuwa nimechoka sana.  Hali ile ilimpa nafasi Marry White kunipa kipigo mpaka nikapoteza fahamu.

ITAENDELEA

Post a Comment

0Comments

Your Thoughts

Post a Comment (0)