RISASI TATU EPISODE 1

 ****𝘀𝗶𝗺𝘂𝗹𝗶𝘇𝗶 𝘆𝗮 𝗸𝗶𝗷𝗮𝘀𝘂𝘀𝗶****


***𝗥𝗜𝗦𝗔𝗦𝗜 𝗧𝗔𝗧𝗨***


𝗠𝘁𝘂𝗻𝘇𝗶:𝗠𝗶𝗸𝗲 𝗚𝗼𝗻𝗮𝗿𝗱


 EPISODE 1                                        


   Imepita miaka mingi tangia Boss wa kikosi cha kijambazi kinachojulikana ulimwenguni kote kama Risasi tatu kuipea dunia mkono wa buriani.Mwaka huu wa 2099 Risasi tatu wamepanga kufanya tukio kubwa zaidi kuliko lile  lililofanyika mwaka wa 1999,tukio ambalo lilisababisha kifo cha boss kamanda wa kikosi cha Risasi tatu.


Risasi tatu ni kikosi cha majangili watatu,sababu kuu ya kujiita Risasi tatu ni kuwa wenyewe ni watatu,wako na bastola tatu na kila bastola hujazwa risasi tatu waendapo kufanya kazi yao kwenye maeneo matatu husika...ama kweli vichaa hawa.


...Kwenye meza iliyo pembeni mwa Club fulani mjini Mtwapa kaskazini mwa mji wa Mombasa  kaketi baro baro fulani lenye miraba minne,lililotutumuka misuli si haba...yes a sturdily built person.Jitu hilo lilikuwa limetulia tu kwenye kiti mara simu ya mkononi aina ya Smartphone iliita...jamaa yule aliiangalia kisha akatoa tabasamu zito kisha akaipokea.


Alipokea simu ile kisha..


"Nambie Ngamba..nadhani kila kitu kiko salama upande wako'' jamaa huyo aliuliza mwenye alikuwa akiongea naye.Aliporidhika na majibu ya mwenzake walikatiza mawasiliano hayo.


Hazikuisha hata dakika mbili simu iliita tena..kama kawaida jamaa huyo aliipokea...aliyepiga mara ya pili pia alimtambua vile vile.


"Upande wangu uko salama nasubiri muda mwafaka kazi ianze"

"OK Ngombo tutazidi kuwasiliana" simu ilikatika baada ya maungumzo ya wawili hao.


Kuna jambo linaenda kutendeka...watatu hao wakitengana ujue fika kuwa kuna jambo kubwa liko karibu kutendeka.Wakati huo ilikuwa ilkikaribia saa tano usiku hivi na kila mmoja katika watatu hao alikuwa sehemu tofauti tofauti.


Ngube alikuwa kakita kambi kwenye Club fulani mjini Mtwapa,hili ni lile lililopigiwa simu na wale wenzake wawili.Ngamba alikuwa kakita kambi kwenye ua wa jumba la bwenyenye fulani huko Nyali.Naye Ngombo alikuwa sehemu fiche akiangalia na kumulika kila kitu kilichotendeka kwenye jumba alilokuwa Ngamba.Sehemu aliyokuwa ilikuwa ya siri mno...ilikuwa fiche.. hakuna aliyejuwa isipokuwa wale wenzake wawili.


....mchana kabla ya usiku huo kulikuwa na mkutano wa kisiasa wa Mheshimiwa Chinjaua.Chinjaua ni mwanasiasa aliyejulikana kote nchini kwa siasa yake..akiongea jambo hakuna aliyepaswa kulipinga...ikitukia utoe upingamizi wowote basi litakukuta jina lake.


Mkutanoni walikuwepo wale watatu Ngamba..Ngombo na Ngube.Kila mmoja alikuwa pembe tofauti tofauti za uwanja ule.


"Chinjaua eeeee!"

"Chinjaua aaaaah"

"Sasa wananchi wenzangu ningependa kuwajuza kuwa..mkinipatia nafasi ya kuwa kiongozi wenu nitahakikisha ya kwamba..nitapoteza janga la njaa linaloikumba nchi yetu" mwanasiasa huyo aliendelea kuboboja sera zake.


"Nikisema njaa mnasema Chinjaua"

"Njaaaaa!"ilisikika sauti nzito ya mwanasiasa huyo ikifuatiliwa na sauti   za  wananchi waliokuwa wakishangilia.


"Chinjauaaaaa!"


Ilikuwa ikikaribia saa kumi jioni ndipo mwanasiasa huyo alihitimisha mkutano huo.

"Asanteni sana nduguzanguni kwa muda wenu sina budi kuwaaga na kuwaacha..naenda kwa mkutano mwengine kule Malindi, nimesubiriwa mno" Mheshimiwa aliongezea,


"Kabla niende ningependa kuwapea maji ya kunywa,angalau muitoe kiu mliyokuwa nayo tangia asubuhi hadi hivi sasa."

"Nitamkabidhi mmoja wenu millioni moja mtagawana,huu ni mwanzo tu!" Mheshimiwa Chinjaua alichukuwa briefcase na kuinyosha juu ili kila mmoja aione.Aliikabidhi kwa jamaa fulani aliyekuwa mbele kwenye umati huo. Mmmh jamaa huyo alikuwa ni Ngube  mfuasi mkubwa wa risasi tatu. 


Takriban saa kumi na mbili jioni Mheshimiwa Chinjaua  na walinzi wake na baadhi ya wanasiasa wenzake waliokuja pamoja..walipanda ndege waliokuja nayo ..ndani ya dakika tano waliacha vumbi tu uwanjani pale na kelele nyingi za wananchi walioshinda njaa. Wananchi hao walianza kuvutana huku na huku kila mmoja akitaka hela iliyoachwa na Chinjaua.Mfarakano ulizidi na kuwa vurugu pale ambapo mwenye kupewa briefcase ya hela kukosekana,haikujulikana kaenda wapi wala hakuna hata mmoja aliyemuona alivyotoka pale.Maskini! watu walipigana, wakaumizana na  mwisho wa kuisha kila mmoja akarudi kwake mikono mitupu.


...Nje  ya Club aliyokuwa Ngube kuna gari fulani jeusi aina  ya Toyota liliegeshwa na hakuna mtu alitoka kwenye gari hiyo.Ngube aliinama  chini ya meza na kuitoa briefcase na kutoka nje ya Club hiyo..kwa wakati huo hakuna aliyejali ndani mle.kila  mmoja alikuwa  bize na lake.Kuna walio cheza..wengine waliendelea kubugia kila aina ya  vileo wasijue kile kilichokuwa kikiendelea.


Ngube aliufungua mlango wa nyuma wa  gari  na kujitosa  ndani na kuipakata briefcase aliyokuwa  nayo.Aliufunga  mlango kisha gari hiyo ikang'oa nanga.Ndani ya gari  hiyo mlikuwa  na watu watatu wala Ngube hakutoa hata chembe ya salamu.Kwa wakati huo barabara kuu ya Mombasa- Malindi ilikuwa clear kwa  maana haikuwa  na msongamano wowote ule..hali iliyofanya Toyota  hiyo kubugunya masafa  kwa  kasi bila  wasiwasi wowote ule.


"Ok Mr.Ngube nadhani umefanya kila kitu kama  tulivyoagana," iliroroma  sauti mojawapo ya wale watatu waliokuwa kwenye gari  hilo.


"Wala usitie shaka wala baridi Mheshimiwa..kila kitu kimeenda sawia na  hakuna hata senti  moja iliyopotea,niliwaacha wakipigana tu"Ngube  alijibu.

"Ngube ni zaidi ya Mandonga mtu  kazi...wakati wote haupaswi kuwa  na wasiwasi", Ngube  aliendelea  kuporoja porojo zake.


"Ha ha haaa! Mheshimiwa alipasua kicheko   kisha..


"Bwanaee usinikumbushe alivyofanywa Mandonga mtu kazi kule jijini Nairobi ,alikuwa na  mbwembwe sana yule...mara ooh kasema amekuja na ndondi aina ya sugunyo ..asili ya ndondi hiyo eti ni Ukraine...lakini mwisho wa  siku  akapoteza mchezo wenyewe"

"Lakini nakuaminia Mr.Ngube...hongera sana,"Mheshimiwa Chinjaua alihitimisha maongezi hayo huku akiichukuwa briefcase na kuhakikisha hela zote zilikuwemo.


 Ndani ya  mwendo wa  lisaa...hatimaye gari lilifika nyali..liliingia kwenye jumba lililokuwa  kama kasri.Alishuka Mheshimiwa Chinjaua mkononi kaishika briefcase , bibi yake na Mr.Ngube.Dereva alibaki ndani ya  gari..alilipeleka nyuma ya jumba hilo kulipokuwa maegesho.


"Simameni hapo hapo mlipofika!...wekeni kila kitu chini na mnyoshe  mikono yenu juu"

 Ilisikika sauti nzito  ikiamuru...kisha tu!  tu!  tu!......

ITAENDELEA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.