SIKU ISIYO NA JINA SEHEMU YA TANO

SIKU ISIYO NA JINA

Na: EMMANUEL CHARO

WhatsApp: +254796273110


Sehemu ya Tano


Ilipoishia 

kutoka Kenya hadi huku nafuata kalamu dah! Siamini hata'

Aliwaza Henessa na yeye akaondoka sehemu ile.

Alirudi moja Kwa moja Kwa chumba cha hoteli, ndani ya hoteli maarufu pale Ramallah, Movenpick Hotel Ramallah hoteli hii inajulikana kwa huduma zake bora.

Alichomoa kimfuniko cha kalamu ile na kukutana na kitu kama chip, aliichomeka kwenye laptop yake na ilipoitisha nywila akaweka kama alivyoagizwa.

'NO SIGNAL'  ukisomeka ujumbe pale kwenye skrini ya laptop

"Aaaaghrrrrr" alinguruma na kuirisha chini laptop ile

'wakora hawa' alijisemesha.


Kuliingia ujumbe Kwa simu yake 

"Ukikuletea NO SIGNAL jua Manu yuko katika himaya Yao au anatumia usafiri wa umoja wao"

Alijaribu kuujibu ujumbe ule lakini haikuwezekana

'hivi Emmanuel ni nani?" ...


Endelea


Sehemu ISIYO NA JINA:

"Nifuate" Manu alimuamrisha Adrian. 

Adrian alianza kumfuata pole pole kutoka katika kile chumba na akagundua mwendo wa Manu ulikuwa wa kinyonge, haukuwa mwendo wa mtu timamu au mzima kiufupi hakuwa sawa. Aliamua tu kunyamaza na kumfuata kimya kimya.

Adrian alishangaa walipotokezea maana pande zote walikuwa wamezungukwa na maji

"Usijisumbue Adrian hata mimi sijui hapa ni wapi" alisema Manu 

"Najua wataka kuuliza tuko wapi, swali ambalo natumai toka ufike huku hujapata jibu wala usitarajie kupata jibu"

"Nishakata tamaa enyewe. Haupo sawa bro, nimeangalia tembea yako hapana nini mbaya?" Aliuliza Adrian 

Manu aliachia kicheko cha kulazimisha na kuendelea kutumbulia macho maji yaliyowazunguka 

"Inaonekana pia wewe wamekulazimisha kukaa hapa, achana na Ile ringa yako oooh hapa ni nyumbani" Adrian alisema hayo huku akimalizia kauli hiyo Kwa kumuiga anavyoongea Manu.


Manu alimtazama rafiki yake huyo na kutikisa kichwa chake ishara ya kumstikia kisha akalonga

"Ni kweli sipo sawa sikufikiria maishani mwangu nitapitia haya ninayopitia" alimeza mate na kuendelea

"Nakuwaweka wasio stahili katika mkasa huu"

Manu alitoa picha toka Kwa mfuko wa ile track suit yake

"Huyu ndiye ananipa wasiwasi, sijui hali yake wala anavyonichukulia muda huu" alimkabidhi picha ile Adrian.

Adrian aliiangalia kwa nukta kadhaa

"Huyu ni nani, simtambui" Adrian alisema hayo baada ya kuiangalia picha ile

Manu alimtazama Kwa mshangao

"Haupo sawa rafiki yangu ikiwa humtambui huyu basi umechizi" kisha akaachia kicheko.

"Twende ndani" Manu alisema na kuanza kuteremka kuelekea chini


*****

Mama Ngina Drive, Mombasa


Angel alikuwa amejiinamia anawaza ni pepo gani aliyemuingia Manu hadi akawa muuaji, maisha yake chuoni haya kuonyesha hata chembe ya utovu wa nidhamu.

'oooh siamini hata, na yule msichana ni nani, na huyu Abdul naye mmmh' aliwaza

Mawazo yake yalikatizwa na mlio toka Kwa simu yake 

"Live"

Ulisomeka ujumbe huo haraka haraka alitoa laptop yake na kuiwasha 

Moja Kwa moja alienda kwa program ya kalamu 

Moyo ulimuenda mbio, kwenye skrini pale walitokea vijana wawili anaowafahamu: Manu na Adrian.

'Adrian naye yumo, inawezekanaje kahutubia bunge si kitambo'

Alishangazwa na mazingira Yale, walikuwa wamezingirwa na maji alijaribu kujua location ya pale walipo lakini ujumbe ulijitokeza Kwenye laptop

"unknown" 

'duh' aliguna mrembo huyu

Angel alimuona Manu akitoa kitu mfukoni mwake na kukitazama Kwa muda Kisha kumpa Adrian.

Kisha wakaanza kuteremka kuelekea chini na picha zikajizima ghafla 

"No signal" ulitokea ujumbe huu uliomkera mno, kisha kukatokea ujumbe mwengine pale ambao mwanzo wake ulimkanganya na mwisho wake ukamchanganya zaidi kama si kumvuruga

'&#x2764 Angel stay safe usiamini ulimwengu niamini mimi, bado nipo Urusi, &#x2764 see you soon'

'&#x2764 hii namba ina maana gani ama ndio location' aliwaza

'kasema bado yupo Urusi, mmmh Kwa ivyo yule ni nani ama pale ni Urusi'

'Manu mbona kunitesa hivi jamani' aliongea Kwa sauti hafifu mrembo huyu

'haikuwa rahisi kukupata sasa hivi wataka kuniponyoka' Angel alijiongelesha na kujifuta machozi

'Joan haezi nisaidia, au ni muelezee Abdul mkasa huu huenda akanisaidia dunia hii hujui mwokozi wako ni yupi'


Angel alitafuta namba ya Abdul na kumtumia ujumbe kuwa amkute Mama Ngina

Angel alivuta taswira ya Abdul, urefu wake, tabasamu lake na mwili wake uliojengeka vyema vilimpa mrembo huyu tabasamu angavu.

'ni mhandsome lakini. But siezi msaliti Manu, acha nimueleze huenda akawa msaada kwangu.'


*****

Mtwapa, Kenya

Kijana Mike Gonard alikuwa amejituliza kwenye Kona ya mgahawa maarufu mjini mtwapa Neptune Beach Resort alivyoonekana ni kama alikuwa akimsubiri mtu mahala pale

Alijiweka bize na simu yake pia hakuwacha kutupa macho yake kwenye milango ya kuingilia mahala pale.

'mbona wanachelewa hawa' alijiongelesha

'oooh ndio hao' alisema Mike na kuinuka alipokuwa amekaa na kutanua mikono yake na kuwakumbatia jamaa walioibuka mahala pale ghafla kama mizimu.

Njemba tatu zilichukuwa viti na kukaa karibu na Mike.

"Let's have a walk" Mike aliwambia jamaa wale na kuinuka na kuelekea nje

Mike alitoa Picha mfukoni mwa kaptula yake na kumkabidhi mmoja wa wale jamaa

"Mlindeni" alisema Mike

Aliyekabidhiwa picha ile aliitazama Kwa umakini na kumpatia mwenzake pia vile vile akaitazama Kwa nukta kadhaa na kumkabidhi aliyebaki.

Huyu wa mwisho aliitazama Kwa nukta kadhaa na kuigeuza na kuingalia nyuma pia, huko nyuma alipatana na nambari hii 

'&#128274'

"Mumeona hii ama" aliwauliza wenzake na kuwaonyesha nambari ile

"Hongera Ngamba, nambari hiyo ndiyo itawaongoza Hadi alipo" alisema Mike 

"Risasi Tatu ni weledi katika kazi hizi msiniangushe wangwana" alisema Mike na kurudi ndani na kuwaacha jamaa wale pale nje.


"Nadhani mushaielewa nambari hii" Ngamba aliwauliza wenzake

"Mie ni shaielewa labda Ngube apo" alijibu mmoja

"Mnajua mambo na minamba Mie ombwe" Ngube alisema

"Ngombo hebu mueleze ili sote tuwe sawa kabla hatujaanza kazi hino" Ngamba aliamuru ni kama ndiye kiongozi wa watu hawa wanaoenda Kwa Jina Risasi Tatu


********

Henessa alishtuliwa na mlio uliotolewa na laptop yake, haraka haraka aliizoazoa toka pale chini hakuamini baada ya kuona kidoti chekundu kikiwa katika mwendo mkali.

Aliaagalia location na kukuta inasoma 'Saint Basil, Moscow'

"Inawezekanaje jamani" alisema Henessa na kujiinamia kitandani pale

"Mtu huyu ni mwanga huyu si Kwa mwendo huu pia ni usiku isitoshe" aliendelea kujisemesha Henessa

'try the new feature' ujumbe huu ulijitokeza, Henessa bila kujiuliza mara mbili aliminya batani ya try. Baada tu ya kubonyeza pale Kwa skrini kulitokea kiumbe kikitembea kwa hatua za kimya katika anga ya mstari wa machweo ndani ya jiji la Moscow. Nguo zake za kujikinga na giza zilijificha kati ya vivuli vya majengo. Alitembea kwa kujiamini, macho yake yakiangaza kwa umakini, na kila hatua ikichukuliwa kwa ustadi wa hali ya juu.

Ghafla, alisimama mbele ya Kanisa la Mtakatifu Basil, alionyesha utulivu.Kwa ustadi wa haraka, alipanda juu ya dari la kanisa kama vile kivuli kisichoonekana.

"Ninja" ulimtoka mguno huo Henessa

Kama vile kiumbe yule anajua anatazamwa, Kwa utaratibu alitoa kinyago kilichomfunika uso 

"Ni yeye kumbe ni ninja huyu" alinguruma Henessa

"Sasa mbona bado yuko Urusi ama ni video hii ili kunipoteza maboya hawa" Henessa alirudisha macho yake Kwa ile laptop

Aliona kiumbe yule akifingua moja ya ubao wa dari na kutokeza ngazi inayoelekea chini na Manu alipoeka mguu mmoja kwenye ngazi zile ujumbe 'signal Lost' ulijitokeza kwenye laptop.

Henessa alitoa kalamu na kuandika 

'Saint Basil' 

"Kwa hivyo Saint Basil ni moja ya ngome ya Manu na watu wake" aliwaza 

"Lakini hainingii akilini eti Urusi , na Ile speed mmmh" alijisemesha Henessa

"Inabidi kuelekea Urusi, hatuna budi" alisema na kuandika ujumbe kwenye simu yake.


*********

"Eti wewe ni polisi"

"Naam mimi ni polisi wa kupambana na wahalifu"

"Sasa utanisaidiaje ili Manu aiepuke kesi hii" Angel aliongea na Kwa mbali macho yako yakianza kulowa machozi

"Angel, hustahili kupitia haya mrembo kama wewe wasaa huu ni uwe unakula tu bata na sikulialia"

"Ndio maana naomba unisaidie Kwa vile umesema wewe ni polisi, Abdul plz" 

"Nisikilize Angel Kwa kufanya haya takuwa nimevunja misimamo yangu ya kazi lakini Kwa mrembo kama wewe sioni shida ni kivunja miiko hiyo" Alisema Abdul na kugandisha macho yake Kwa kifua cha mrembo huyu kilichosimama dede. Alimeza mate na kuendelea

"Manu hawezi kuepuka kesi hii maana ushahidi upo tena wa kutosha" Abdul aligusagusa simu yake na kumpa Angel simu Ile ajionee picha za Manu. Angel hakuamini kumuona Manu akiwa ameloa damu huku akiwa amemushika Frankoo Sari anayeonekena amepoteza uhai.

Mara ujumbe uliingia simuni mwa Abdul ikiwa bado simu iko na Angel, aliusoma ujumbe ule Kwa ufasaha

'mshenzi kashaenda Urusi, tukutane Urusi baada ya siku tatu' alipomaliza alimurudishia simu yake

"Kwa kukuonyesha picha hizo nimevunja taratibu za Kazi yangu Angel" alipiga funda la maji ya dafu na kuendelea

"Manu si mwanaume anayekufaa Angel, ona sasa alikudanganya kumbe yeye ni muuaji najua unapitia wakati mgumu nipo hapa Kwa ajili yako" Abdul ilimtoka kauli hii na kuinuka na kuenda kumuinua Angel na kumkumbatia, Angel alijiachilia kifuani mwa Abdul, alijisikia faraja kitu alichokikosa Kwa muda mrefu.


Tukio lile lilionekana na wengi waliokuwa mahali pale, wengine waliwaonea wivu wawili hawa na kutamani kuwa kama wao kwani kumbatio lile liliashiria watu waliokuwa kwenye penzi zito.

Baadhi ya waliona tukio lile walikuwa wanachama wa Risasi Tatu; Ngamba, Ngombo na Ngube. Haijulikani walifika mahali pale saa ngapi.


"Hivi yule jamaa ni nani" aliuliza Ngombo

"ngoja nimpige picha tutafahamu si kitambo" alijibu Ngube na kutoa kamera yake yenye uwezo wa kupiga picha safi, alisubiri wawili hawa kuachiliana ndipo akampiga picha Abdul na kuunganisha kamera Ile na saa yake Kwa kupitia waya mwembamba na kubofya batani ndogo zilizoko kwenye saa

"Jina lake anaitwa Abdul Aziz mzaliwa wa kaunti ya Lamu kazi yake ni Mwanapolisi ni mmoja wanao fuatilia mauaji ya Frankoo Sari" alihitimisha Ngube

"Acha tuone mwisho wake ni upi" alisema Ngamba

"Bora hakuna madhara kwa Angel" alitia usemi Ngombo

"Tuwe macho" akasema Ngube


Itaendelea




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.