SIKU ISIYO NA JINA SEHEMU YA NNE

 


SIKU ISIYO NA JINA

Na: EMMANUEL CHARO

WhatsApp: +254796273110


Sehemu ya Nne


Ilipoishia 

*****

"Yule ni nani" aliuliza Adrian

"Adrian Sirya Maitha muwakilishi wadi ya Dabaso" alimujibu Manu

"Unajua fika mimi ndio Adrian nakuomba nambie yule ni nani"

 Adrian alichanganyikiwa baada ya kuona mtu waliofanana Kwa kila kitu hadi sauti alitoa hotuba ndani ya bunge la kaunti ya kilifi.

Kila atakacho muuliza Manu hapati jibu linalomuridhisha , alijiuliza kama ashawahi kumkosea kigogo yeyote serikalini lakini hakumbuki chochote. Anachokumbuka ni kuwatumikia 

Wakazi wa Dabaso vilivyo. Haamini na hakuwahi fikiria itafika siku kama hii maishani mwake.


Endelea


Adrian alishtuliwa na king'ora, aliangalia mule chumbani na akijipata peke yake hakujua Manu ameelekea wapi. King'ora kiliiendelea kupiga kelele hali iliyomkera.

Pendo mke wake kipenzi aliingia ghafla chumbani mule huku akihema

"Kipenzi hebu inuka mkuu ashafika wewe unaendelea tu kukaa hapo, harakisha basi"

"Si inuki hadi unambie tuko wapi?"

"Mwisho masihara yatakuponza, nilikwambia sijui mimi labda utamuuliza mkuu wa hapa analo jibu, hivyo inuka twende"


Adrian aliinuka kinyonge akisaidiwa ni mke wake , pendo alimuuongoza kupitia korido nyembamba ambayo wiki nzima aliyokuwa pale hakuwahi kuiona, korido ile ilikuwa hao wawili tu

"hivi wengine wako wapi" aliuliza Adrian

"wako chumba cha mkutano"

"Sehemu hii imenichosha haina tofauti na jela hujui ni mchana wala usiku"

"Kuwa na subra mume wangu mambo yakikaa sawa tutarudi nyumbani, tumuombe mungu"

"Ulipatana nao wapi hawa watu, pia nilishangaa kumuona Manu huku"

"Ni stori ndefu mume wangu nitakuhadithia tukitoka salama mahali hapa"

"Unanitisha ujue, inaonekana unajua ukweli Kwa nini niko hapa lakini hutaki kuniambia mpaka sasa sikuamini hata kidogo" Adrian aliongea huku alimkata jicho la hasira mke wake

"Haya yote uliyataka wewe" Pendo alijibu machozi yalianza kumtiririka.


Walifika mwisho wa ile korido, Pendo aligusagusa ule ukuta maajabu ulijifungua na kutokea ngazi zilizoelekea chini 

"Nifuate" aliamrisha Pendo

Kadri walivyokuwa wakishuka zile ngazi Adrian aligundua kando ya zile kuta kilikuwa na maji, sifa kubwa ya zile kuta zilitengenezwa na kioo, aliendelea kushangaa uzuri wa zile ngazi.

Walitokezea katika Chumba hicho kilikuwa kimeundwa kwa umakini wa hali ya juu, kikitumia teknolojia ya hali ya juu na ubunifu wa usanifu. Wakati unapochukua hatua ndani yake, ilikuwa kana kwamba ulikuwa ukitembea katika ulimwengu mwingine.


Kuta zake zilikuwa zimejengwa na vioo vya kisasa na vitu vya kuvutia, na taa zilizong'aa zilionyesha  washiriki wote waliokuwa katika hali ya utulivu na umakini. Viti vyake vilikuwa vizuri sana kwa faraja na vifaa vya kisasa vya teknolojia

Samaki walionekana wakiogelea Kwa furaha kupitia kuta zile.


"Inamaana tuko baharini" alimuliza Pendo aliyekuwa kando yake lakini hakujibiwa aligeuza shingo yake upande wa kushoto hakumuona Mke wake akarudisha shingo yake kulia hakuna mtu 

'mmh kaenda wapi huyu' alijiuliza, alirusha macho yake mbele alimuona mke wake amekaa Kwa utulivu.

Wote waliokaa pale waligeuza shingo zao na kumtazama yeye aliyekuwa ameganda mlangoni akishangaa uzuri wa chumba kile 


"Bwana Adrian kiti hicho kinakusubri wewe" aliongea mwanaume mwenye  misuli thabiti na inayoonekana vizuri bila shaka alikuwa mtu wa kufanya mazoezi ya viungo

Ilikuwa mara ya kwanza kumuona mwanaume huyu

Adrian alitembea aste aste hadi pale kwenye kiti.

'labda huyu ndiye mkuu' aliwaza 

Alijibwaga kwenye kiti kile 

"Mmmh!"  Aliguna alipokalia kiti kile alijishika faraja kiti kilikuwa laini kupitiliza alisahau yote na kupata faraja ya ghafla

'wachawi hawa' kisha alivuta pumzi Kwa nguvu

"Tufanye utambulisho tukimsubiria Mkuu wetu; Romeo"

"Duh" alitoa ukemi Adrian

"Jina langu ni Khumalo Thembi, natokea Africa kusini hapa Mimi ni mkufunzi wa karate" aliongea mwanaume huyo

akaendelea 

"hivyo tuanzie kwako bwana Adrian 

"Niseme nini tena ikiwa mnajua jina langu"

"Hata hawa wananijua, utaratibu uko hivyo. Tunakusikiliza"

"Ok Langu jina ni Adrian Maitha wavivu wakutamka hilo jina huniita Eddy, natokea nchini Kenya hapa sijui ni wapi wala niko hapa nafanya nini, nyinyi ni wapu..."

"Hiyo inatosha" alisema Khumalo

"Eeeh tuendelee" Khumalo akaashiria alipokuwa amekaa mke wa Eddy

"Naitwa Pendo, Natokea Kenya"

"Naitwa Nirrah" alisema Mrembo mmoja chotara nakutia nukta.

"Unatokea wapi" Eddy aliuliza maana mrembo huyu hakuonyesha dalili za kusema anakotokea.

"Haya kuhusu"

"Kila mmoja hapa ame..."

"Mwengine tafadhali" Khumalo alimkata kalima Adrian 

"Manu hapa kwa sasa niko urusi"

Eddy alishangaa utambulisho ule wa rafiki yake, ulaini wa kile kiti ulianza kupotea. Alitaka kuuliza swali lakini kinywa chake kilikuwa kizito kutamka neno.

Alishangazwa zaidi pale utambulisho ulisemekana umeisha ilihali bado kulikuwa na watu watano bado hawajajitambulisha.


"Acha niwe mvivu, mheshimiwa Eddy najua Una maswali mengi lakini maswali yako bwana mkubwa Romeo atayajibu, lakini sahau kujua hapa ni wapi"

Khumalo aliyasema hayo na kumgeukia Manu 

"Muonyeshe mazingira ya hapa pia itakuwa vyema akiliona jua. Tukutane hapa Romeo akifika"


******

Mombasa Apparel


Mike Gonard alikuwa amekamilisha kazi yake, muda huu alikuwa akiweka mazingira sawa Kwa watakao kuja baada yake.

Ulikuwa mwendo wa saa nane za mchana.

Alimaliza kueka kila kitu sawa kisha huyo akaanza kutambaa pole pole akielekea lango kuu la kampuni hili la Mombasa Apparel linalotengeneza nguo.

Alishtushwa na mtetemo wa simu yake, aliitoa kutoka Kwa mfuko wa  jeans jina anayepiga lilisomeka "Lavinia" Gonard alisonya na kukata na kutaka kuirudisha mfukoni simu yake lakini ikapigwa tena, wakati huu mpigaji hakuwa Lavinia bali jina lilisomeka "Romeo"  Gonard aliachia tabasamu pana

Kisha akapokea

"Niambie mwana" alianza kuongea Gonard

"Safi ndugu hali yako" alijibu Romeo

"Mie pia mzima, haya nambie"

"Kuna kazi nataka uitekeleze, lakini hatuwezi kuongelea Kwa simu"

"Ok ni sawa acha nifike nyumbani, maana sasa ndio natoka job"

"Safi mwana pia nitaiingia chimbo usiku huu"

"Ok fit" alihitimisha Gonard


'Itakuwa kazi gani hiyo' alijiuliza

'hope sikuchukua uhai wa mtu this round'

Gonard alijipata amefika kwenye chumba alichopanga, haraka haraka alifikia laptop yake na kuiwasha Kwa speed ile ile alitafuta app inayoitwa Jaba Planet kisha ili load Kwa uharaka na akakutana na ujumbe unaosomeka 

'm'linde shemeji yako'

Gonard akatuma ujumbe pia

'shemeji yupi'

'wa Siaya'

'ok' Mike Alishusha pumzi Kwa nguvu

'anaingiaje kwenye hili sakata naye' bila shaka Manu ashamwambia tayari' aliwaza Mike

'huyu dogo sijui shida yake nini, nilimwambia hisia kando kama upo kazini ona sasa amemueka Shemeji katika hatari' kisha akajikuna kichwa

'hadi agizo limetoka kwa Romeo maanake yuko katika hatari kubwa'

'sijui niwatumie akina Ngube ama'

'nimekumbuka Sukubi aliniambia kama nataka msaada nimwambie, mmmh lakini jini lile acha tu niwatumie Risasi Tatu' 

Mike akajibwaga kwenye kitanda chake

'hope yataisha very soon, itafika siku ya hatima ya haya yote angalau nasi tuishi kama wengine.

'lakini naona huu ni muda mwafaka wa kumtumia SUKUBI aliwaza.


******

Ramallah, Palestina


Ramallah iko katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Ukingo wa Magharibi ni eneo la Palestina, na ndiyo mji mkuu wa Utawala wa Palestina.

Henessa alionekana kwa umbali akitembea aste aste katikati mwa mji huu akielekea katika kingo za mto Jordan alionekana mtu mwenye wasiwasi na wakati wote alikuwa anageuza kichwa chake kushoto kulia hata kuangalia nyuma kuona kama kuna mtu anamfuatilia.

Ilimchukua takribani dakika ishirini hadi kufikia ukingo wa mto Jordan hapo alipatana na kijana mmoja machachari aliyejitambulisha Kwa Jina moja Rami.

"Niite Henessa itapendeza zaidi"

"Usiwaze buda" Henessa alishangazwa na lafudhi ya kijana huyu maana aliongea kama mtu aliyeishi Nairobi Kwa miaka mingi

"Nipe changu niende"

Rami alitoa kalamu kwenye kaptula yake na kumkabithi, kusema kweli kalamu ile ilifanana na ile aliyokabidhiwa  Angel na Joan

"Nipe changu niende" alisema Rami, Henessa aliingiza mkono wake kwenye suti yake na kuchomoka na bahasha akampa Rami 

" Buda upo vizuri sasa kalamu hiyo Itakuelekeza hadi alipo Emmanuel, muwe na tahadhari Manu naye mjua mimi si kiumbe cha kawaida naeza sema ni jini haswa kumbuka nywila ni AlMaS∅∅½' " Rami alinena hayo na kuondoka eneo lile.


Henessa alitaka kumuuliza maswali lakini hakupewa muda huo. Aliiangalia kalamu aliyopewa na kuachia kicheko kichungu.

'kutoka Kenya hadi huku nafuata kalamu dah! Siamini hata'

Aliwaza Henessa na yeye akaondoka sehemu ile.

Alirudi moja Kwa moja Kwa chumba cha hoteli, ndani ya hoteli maarufu pale Ramallah, Movenpick Hotel Ramallah hoteli hii inajulikana kwa huduma zake bora.

Alichomoa kimfuniko cha kalamu ile na kukutana na kitu kama chip, aliichomeka kwenye laptop yake na ilipoitisha nywila akaweka kama alivyoagizwa.

'NO SIGNAL'  ukisomeka ujumbe pale kwenye skrini ya laptop

"Aaaaghrrrrr" alinguruma na kuirisha chini laptop ile

'wakora hawa' alijisemesha.


Kuliingia ujumbe Kwa simu yake 

"Ukikuletea NO SIGNAL jua Manu yuko katika himaya Yao au anatumia usafiri wa umoja wao"

Alijaribu kuujibu ujumbe ule lakini haikuwezekana

'hivi Emmanuel ni nani?" ...


Itaendelea 


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.