SIKU ISIYO NA JINA SEHEMU YA TATU

Emmanuel Lee
By -
1

 SIKU ISIYO NA JINA

Na: EMMANUEL CHARO

WhatsApp: +254796273110


Sehemu ya tatu


Ilipoishia 

Alivuta pumzi ndefu baada ya kukaaa kwenye gari lakini kuna kitu kilikuwa kinamkera kwenye ile laptop yake, ule ujumbe wa "try the new feature" mara hii alipiga try

"Wow!" Ukemi ulimtoka

Maana kwenye skrini ilitokea ile boti waliyopanda msichana yule na Manu.

Boti ilipunguza mwendo na kusimama, Angel alitazama Kwa makini japo alikuwa hasikii wanachoongea lakini ni kama walikuwa na ugomvi fulani, Yule msichana ghafla alimsukuma Manu ndani ya maji kisha akaiondoa boti ile kwa kasi. Angel alishangaa. Boti ile ilipotea mahali pale na kubaki maji yanayochezacheza, machozi yalimdondoka.

Ghafla Manu aliibuka mahala pale na kuanza kuogelea kuelekea magharibi ghafla kulitokea boti nyengine kubwa kuliko Ile ya msichana aliyemurusha Manu ndani ya maji.

Pia hii nayo iliendeshwa na msichana.

Ilisimama karibu na Manu kisha yule msichana akamsaidia kupanda boti ile.

Angel alishangaa baada tu ya Manu kueka mguu mmoja ndani ya boti laptop yake iliandika 'Signal Lost'


Endelea


"Mkuu Hadi sasa hakuna boti imepita, inayofanana na maelezo yako" 

"Haiwezekani, Abdul amehakikisha uelekeo wao ulikuwa kaskazini, mbona wasipite hapo"

"Hadi sasa ni masaa mawili yamepita na hakuna watu kama hao wamepitia hapa hata kama mwendo wao ulikuwa wa kinyonga wanafaa muda huu wawe washapita "

"Ok ni sawa tumerudi sufuri tena, hadi sasa hakuna pingamizi Manu si mtu wa kawaida hivyo tuwe macho"

"Mkuu acha wasiwasi mtu aliyemtorosha Manu ndio si wa kawaida yule binti hana dogo yule"

"Ok fanya Urudi kituoni basi"

Yalikuwa mazungumzo ya Mafaa Henessa na kijana wake Hezron Wazir.


****

Angel aliendelea kutumbulia macho laptop yake asijuwe la kufanya. Aliamua kurudi nyumbani Kwa rafiki yake.

Joan alimpokea Kwa furaha lakini hata mwenzake alionekana kuchoka.

"Kwema shosti"

"Hivi Joan mie na upungufu gani eee hebu nambie basi" Angel aliongea katika kwikwikwi za kilio 

"Kunani umemfumania nini? Wanaume ndivyo walivyo"

"inamaana ulikuwa ukijua muda wote huo"

"Kuhusu nini labda" aliuliza Joan

"Hebu nieleze nini kimekukuta huko, maana hata sikuelewi shosti" alisema Joan


Angel alianza mosi hadi mwisho kile alishuhudia lakini hakusema alimuona Abdul akiwa na bastola.

'heri niolewe na jambazi kuliko muuaji na msaliti kama yule, ama jambazi ni muuaji pia ama' aliwaza Angel

"Acha nipumzike maana wueeh! Kesho nitarudi Siaya"

"Pole Shosti lakini usiache kumfuatilia labda ni changamoto ya muda tu hiyo lakini atarejea hewani" Joan aliongea Kwa sauti ya kutia moyo.


******


"Brudah umefikaje fikaje uku aiseee" aliropoka Manu, aliyemuona mahali pale hakutarajia hasa wakati kama huu, anafaa awe nchini Kenya akitekeleza majukumu ya kitaifa.

"Hata salamu kaka, umuzima weye" kauli hii ilitokea Kwa kijana mrefu wa wastani, mwenye mwili wenye afya. Alikuwa na macho meupe na nywele za nyeusi zenye kung'aa, na tabasamu la kuvutia ambalo lilimfanya aonekane mchangamfu sana. Nyuma yake aliambatana na msichana mrembo kwa njia ya pekee. Alikuwa na macho meupe ya kuvutia ambayo yalikuwa kama nyota kwenye anga la usiku, na nywele ndefu na laini zenye rangi ya kahawia ambazo zilionekana kama shanga zenye kung'aa. Uso wake ulikuwa na tabasamu lenye upole ambalo lilileta furaha kwa kila mtu aliyezungumza naye.

Manu alibaki kumtumbulia macho mrembo yule

"Ndiye shemeji nini?" Aliuliza Manu badala ya kujibu salamu

"Yaani hadi salamu umekatalia hivyo eee" alihamaki kijana huyu

"Si hivyo Adrian nashangaa uzuri wa shemeji hapo, si Kwa uzuri huo aisee ndio maana mwafulani pale chuo aling'ang'ana weee kumbe chombo hicho duh hapo utaanzaje hasa..."

"Bro unataka kumwaga mtama kwenye kuku wengi cheza chini kaka"

"Hamna shida bro. Uwepo wako hapa inamaana watu wa Dabaso ward hawana kiongozi"

"Nimekuja tu kumsalimia tu shemeji yako hapa, halafu ni rudi"

"Mchezo mchezo tu sasa wewe ni MCA aisee kweli ni tuishi kwenye ndoto zetu, hivi Romeo yuko wapi yeye ndiye mwenye majibu ya maswali yangu"

"Romeo yuko Japan" sauti nyororo na yakuvutia ilimtoka binti aliyekuwa nyuma ya Adrian 

"Duh! Sasa nimejua Kwa nini..." 

"Kaka ee tuchat " Adrian  alimkata kalima Manu


"Inaonekana wewe ni mwenyeji hapa" aliuliza Adrian

"Si wenyeji tu hapa ni nyumbani , karibu nyumbani ndugu" 

"Nikuulize hivi hapa ni wapi" Manu alimtazama Adrian na kuachia kicheko hafifu

"pia mimi sijui hapa ni wapi"

"Maajabu hayo, unapaita nyumbani na hujui ni wapi"

"Ok hapa ni nyumbani" alijibu 

"Hutaki kunijibu pia Pendo hataki kunijibu, kila mtu hapa ndani hataki kunijibu hili swali ni nini mnaficha"

"Kabla ni kujibu, kwa nini uko hapa?"

"Sijui Kwa nini niko hapa" 

"Na ulifikajefikaje hapa?"

"Nilijikuta tu niko hapa"

"Umekaa hapa siku ngapi"

"Wiki sasa sijui hali ya wazazi wangu wala wananchi, hofu yangu ni kupoteza nafasi hii niliyonayo"

"Na shemeji mlikuja pamoja"

"Hapana, nilimkuta hapa hadi sasa mimi kuwa mtulivu ni yeye"


"Hadi natoka Kenya sikuona taarifa ya kupotea kwako..."

"Inamaana gani ukisema ulipotoka Kenya kwani hapa si ndani ya Kenya" aliuliza Kwa mshangao Adrian

"Kutokuwa Kwa taarifa ya upotevu wako kuna ukakasi"

"Wewe ni Emmanuel ninaye mjua au wewe ni mwengine? Nambie ukweli wewe ni nani"


Manu alitoa simu yake na kumuonyesha kilichokuwa kikiendelea ndani ya Bunge la kaunti ya kilifi, hakuamini alichoona.

"Hii ndio sababu ya kutokuwa taarifa ya wewe kupotea"

Adrian alikaa kwenye sakafu haamini anachoona.


****

Taarifa hii ilivuma kwa kasi sana, muwakilishi wadi ya Dabaso kilifi kaunti Adrian Sirya alijitokeza waziwazi na kumtetea Emmanuel Charo anayeshukiwa Kwa mauaji ya aliyekuwa mkuu wa idara ya ujasusi nchini, ambaye hadi sasa hajulikani alipo. Adrian alisema anajua wote waliohusika na mauaji ya Frankoo Sari.


"Acheni upuuzi nyinyi, acheni kumuandama Manu mnajua fika hahusiki na mauaji yale nawapa wiki moja msafishe jina lake, baada ya hapo nitayatoa hadharani majina ya wote walio husika na kifo cha mpendwa wetu, Frankoo Sari ni. Ni nao ushahidi na wengi ni vigogo"

Muwakilishi wadi huyu aliongea bila uwoga.

Wananchi wengi walishangazwa na ujasiri wa Adrian. kesi hii ya mauaji ya Frankoo Sari ni kama itachukua mkondo mpya baada ya kauli ya muwakilishi wadi wa Dabaso; Adrian Sirya 


*****

"Yule ni nani" aliuliza Adrian

"Adrian Sirya Maitha muwakilishi wadi ya Dabaso" alimujibu Manu

"Unajua fika mimi ndio Adrian nakuomba nambie yule ni nani"

 Adrian alichanganyikiwa baada ya kuona mtu waliofanana Kwa kila kitu hadi sauti alitoa hotuba ndani ya bunge la kaunti ya kilifi.

Kila atakacho muuliza Manu hapati jibu linalomuridhisha , alijiuliza kama ashawahi kumkosea kigogo yeyote serikalini lakini hakumbuki chochote. Anachokumbuka ni kuwatumikia 

Wakazi wa Dabaso vilivyo. Haamini na hakuwahi fikiria itafika siku kama hii maishani mwake.


Itaendelea


Post a Comment

1Comments

Your Thoughts

  1. Nice one though kuchangnykiwa kiasiπŸ˜‚πŸ˜‚

    ReplyDelete
Post a Comment