PENDO LAKO SUZAN
Pendo lako Suzana, Linanijaza furaha
unanipenda ja mwana, kwa mamaye nafuraha,
Jadi nayona ja jana,, u'vyokuwa na madaha,
Pendo lako Suzana, talinyonya hadi kifo.
Talinyonya hadi kifo, nahidi sitokuacha
takukumbata ja pillo , mpaka ifike macha
'lifanya tumbo lako, libebe watoto pacha
Pendo lako suzana, lanitia uwazimu
Lanitia uwazimu, mwana wa Mkamba
nilokujia ilimu, Luo naacha Mimba
Ugunja sio Kisumu, napaona Kama Pemba
Pendo lako suzana, limenipofua macho
Limenipofua macho, mpaka mbele sioni
kibe nimelala nacho, nimetafuta sioni
'me'ndika kuta za choo, Jina lako Suu zani
Pendo lako suzana, ndilo 'menitoa Chonyi.
Ndilo 'menitoa Chonyi, nahisi Mungu kapanga
nitakulinda kwa Usunyi, kwa manati na Upanga
'tanizalia Akinyi , babaye akiwa Chonga
Pendo lako suzana, nipe hadi uzeeni
Nipe hadi uzeeni, nikunywe yako maziwa
juu ata paka uzeeni, hunyweshwa hata maziwa
nami nakusihi jamani, 'sininyime 'go maziwa
pendo lako suzana, lanikosesha usemi.
Lanikosesha usemi, yanibidi nitamatishe
wajua wewe na mimi, hata tujijumulishe
'takula chakula "yummy", tuachane tsalakushe
pendo lako suzana 💋💋❣️❣️ only God knows.
Created by
Chonga@254✌️
Your Thoughts