Mvua

 Yashampiga sasa, na mvua imem'nyea hana budi kuisifia lakini bado kinywa chake kizito kumwaga sifa hizo. Ataanzaje! Hasa.

Sifa za mvua alifanya tu kuzisikia, vile hulowanisha watu na kuwatetemesha kwa baridi kali kunao waliotabasamu na kusema mvua ni baraka, kunao waliangua kilio maana iliwapiga wakiwa hawana matarajio hayo; Uongo!

Mbona useme mvua ilikupiga bila matarajio ndio Uongo huo, maana kabla ya mvua kunyesha mawingu meusi hutanda dalili hiyo labda hawa ni wale wa kusema ni mara ngapi tumeona mawingu hayo na hakukunyesha. Yaliyowakuta hawakuamini.

Kijana huyu sasa mvua imem'nyea lakini anaona sifa za mvua alizopewa na kuzisikia ni uongo mtupu, yeye aliamini mvua ni baraka hivyo kunyeshewa ingekuwa ahueni kwake lakini mvua ilompiga ilikuwa ya mawe hivyo iliacha maumivu mwilini mwake yaliyopenya hadi moyoni na kuutawala ubongo wake hivyo ikawa ngumu ya kusahau maumivu hayo.

Kila akitaka kunyanyua kinywa chake kuutangazia ulimwengu alichokutana nacho hujikuta mzito sana mwishowe anabaki kimya, mbona iwe hivyo, yote hayo yanamtokea Kwa sababu yeye ni ung'ong'o na moyo wake ulitua kwa binti aliyeng'atwa na nyoka pia binti huyu alipigwa na mvua ya mawe ilihali upande wake wa kuume kulikuwa na mwavuli ulioshikwa imara na 'nyoka' aliyemuona kama malaika na ukatumika kumkinga binti mwenzake shogake hasa. Mbona sasa binti huyu asishtuke kuuona ung'ong'o? Kupitia binti huyu kijana huyu naye anaionja ladha ya mvua ya mawe huku akiona dunia imepinduka juu chini. Hiyo ndio mvua inayowapiga walimwengu. Matarajio humualika iziraili.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Your Thoughts