SIKU ISIYO NA JINA SEHEMU YA SABA

 SIKU ISIYO NA JINA

Na: Emmanuel Charo

WhatsApp: +254796273110


Sehemu ya Saba


Ilipoishia


"Eti eee" Nuru alisema na kumsogelea raisi na kumtazama Kwa macho yake

"Umekosea sana raisi, umesahau mimi ni nani. Na wewe nakwambia omba miungu yako nisitoke hai ndani hapa"

"Unajiamini nini binti, sema Manu yuko wapi maana wewe ulimtorosha, tukimpata Manu pia nanyi mtamzika Mzee wenu mkiwa na amani maana yake muuaji atakuwa mbele za sheria"

"Raisi nisikilize, acha kupoteza muda wako mwambie Henessa na timu yake wamtafute muuaji. Manu si muuaji"

Raisi alibaki kinywa wazi



Endelea

*********

Ngamba na Ngombo walifuata uelekeo wa kidole cha Ngube wote walipigwa na butwaa.

Walipokuwa Angel na Abdul viti vilikuwa vitupu na hakukuwa na dalili za hao watu wawili

"Yote ni sababu ya simulizi zako zisizo kichwa wala miguu" Ngamba alimtupia lawama Ngube

"Nishasema mimi sioni sababu ya sisi tukosane mwanzo wa hii kazi" alisema Ngube kisha na kuendelea

"Nyie mnaichukulia nyepesi hii kazi lakini sivyo mjue kumlinda yule binti inahusiana moja Kwa moja na kesi ya Frankoo Sari. Chakufanya sasa ni kujua yule binti kaelekea wapi" 

"Hebu tuwe makini basi wenzangu" aliingilia kati Ngombo.

"Hii inaashiria tulivyozembea Kwa muda huu mfupi tu" aliendelea kuongea Ngombo


******


Baada ya siku Tatu


Moscow, Urusi

Mrembo Angel alikuwa sako Kwa bako na kijana huyu barobaro katika jiji kuu la Urusi; Moscow

Maskioni alieka headphone kubwa zenye nembo ya boomplay Kwa mbali alikuwa akisikiliza wimbo wa mwanadada Sia unaoenda Kwa jina 'elastic heart'

Wimbo huu ulimrejesha mbali sana walipokuwa na mvutano katika mahusiano yake na Manu.

Hakuna mwanadamu aliyekamilika katika ulimwengu huu waliyatengeneza na yakapita, leo hii Manu kawa muuaji, pole pole hisia zake zinahama kutoka Kwa Manu na Kwa Kasi ya ajabu anajikuta anavutwa na Abdul. Japo Angel anaamini kupitia Abdul huenda Manu akanusurika kutoka Kwa janga linalomkabili.

Mbinu anayotumia ndio hatarishi Kwa penzi lake.

"Urusi huku karibu malaika wangu" Abdul alimwambia Angel

"Nimekaribia natumai nitapumzika"

"Hata ukitaka naweza kukufanyia mpango upate uraia wa huku"

Angel alicheka Kwa kauli hiyo

"Kweli unadhani ni utani"

"Kile kibabu hakiezi kubali mke wa muuaji kuwa raia wake"

"Wewe sasa si mke wa muuaji tena"

"Unaamana gani"

"Angel ni mke wa polisi, hahaha"

Angel alimukodolea macho Abdul Kwa kauli hiyo, anakumbuka moja ya kauli za Manu alizokwambia. kauli hiyo ni ngumu kuamini

'kama kuna binti mwenye bahati ulimwengu huu ni wewe, ndoto ya kila mwanamke awe na mume mwaminifu, uaminifu huo ni kuwa na mke mmoja. Amini Manu ni mmoja ya wanaume hao, Manu kwako ni wa Kwanza na atakuwa wa mwisho. Nikukupoteza maana yake Manu hatawahi kuingia kwenye mahusiano amini' 

Alikumbuka hayo yote na kujikuta miguu ina mlegea na kukosa nguvu pumzi zilianza kumutoka Kwa shida.

Abdul aliliona hilo na akamuwahi kabla ya kuanguka


******

"Yuko Urusi sasa na Mpenzi wako" Romeo aliongea hayo na kumrushia picha Manu.

Manu alitazama picha ile na kutoa mnong'ono

"Abdul"

"Ndio Abdul huyo akidhamiria jambo lake harudi nyuma, nawaza sijui alimkula yule mrembo wako mara ngapi" kisha Romeo alicheka.

Pichani alikuwa Abdul amemupakata Angel, pozi lile lilikuwa na dalili zote za mahaba mazito. Manu alifikicha macho yake haamini anachokiona

'Namuamini Angel, najua anafanya haya yote sababu yangu' aliwaza

"Una lolote la kusema" 

"Ni muda wa Angel kujua ukweli" 

"Unadhani hilo ni sahihi, akiwa mikononi mwa Abdul"

"Hakuna namna navyojua Abdul bado hajalala na Angel ndio maana hadi sasa Angel anapumua, anachotaka ni kumuulia Angel ardhi ya Urusi, unadhani Angel akifa Urusi Nani muuaji?"

"Kuwa makini, Abdul unamfahamu vizuri"

"Usijali, najua"


Manu haamini kama Abdul amefanikiwa kuwa karibu na Angel

'duh! Abdul nilidhani tuliyamaliza kumbe bado'

'Angel usilolijua ni usiku wa giza Abdul ni kiumbe hatari sana tafadhali mama kuwa mwangalifu usidiriki kumvulia chupi huyo mtu, oooh my God nasema vitu hata hasikii' aliwaza Manu

'hamna njia nyengine sasa ni muda wa kumtumia jini Sukubi, sijui kama atakubali huyu naye'

Kwa uharaka alitoa simu yake na kumtumia ujumbe Mike Gonard 

'jaribu kutumia yule jini Sukubi'

'ni hatari dogo'

'jaribu, Angel yuko mikononi mwa mwehu'

'usijali analindwa na Risasi Tatu huyo'

'bro yuko mikononi mwa Abdul'

'Abdul ndio nani huyo'

'fanya kumtuma utajua baada ya ametoka mikononi mwake'

'huwaamini Risasi Tatu ama'

'bro ungejua moto wa huyo kiumbe anaitwa Abdul, ungehofu hata kumtuma huyo jini, nakushauri wambie hao Risasi Tatu wasitishe zoezi lao maana ni hatari kwao'

'haiwezi wapi Urusi hadi hivi tunaongea'

'wambie wasitishe zoezi la kumfuatilia huyo mtu'

'duh! Sawa acha niwafahamishe'

'fanya hivyo hii misheni ni nzito hawawezi kile kiumbe'

'ni sawa lakini misheni si kudili na huyo kiumbe bali ni kumlinda Angel'

'Abdul atawamaliza akigundua anafuatiliwa'


*******

Risasi Tatu walikuwa unyo unyo na gari iliyokuwa inamkimbiza Angel kuelekea hospital 


Itaendelea 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.