SIKU ISIYO NA JINA SEHEMU YA SITA

SIKU ISIYO NA JINA

NA: Emmanuel Charo

WhatsApp: +254796273110


Sehemu ya sita 


Ilipoishia


"Hivi yule jamaa ni nani" aliuliza Ngombo

"ngoja nimpige picha tutafahamu si kitambo" alijibu Ngube na kutoa kamera yake yenye uwezo wa kupiga picha safi, alisubiri wawili hawa kuachiliana ndipo akampiga picha Abdul na kuunganisha kamera Ile na saa yake Kwa kupitia waya mwembamba na kubofya batani ndogo zilizoko kwenye saa

"Jina lake anaitwa Abdul Aziz mzaliwa wa kaunti ya Lamu kazi yake ni Mwanapolisi ni mmoja wanao fuatilia mauaji ya Frankoo Sari" alihitimisha Ngube

"Acha tuone mwisho wake ni upi" alisema Ngamba

"Bora hakuna madhara kwa Angel" alitia usemi Ngombo

"Tuwe macho" akasema Ngube


Endelea


"Angel unahitaji muda wa kupumzika, na sehemu nzuri ya wewe kupumzika ni ukiwa mbali ya Kenya" Abdul alinena baada ya kumbatio lile, akavuta kiti chake na kukaa pembeni ya mrembo huyu.

Abdul aliona haitoshi hiyo akaamua kumvuta Angel toka kwenye kiti chake na kumpakata.

"Hiyo itakusaidia kutomuwaza Yule muuaji" Abdul alitawala kikao kile huku Angel akiwa kimya tu

"Sijuia unanielewa malaika wangu" aliuliza

Angel bado alikuwa kimya 

"Angel mbona kimya sana mammy"

"Kifo pekee ndiyo kitanifanya ni simuwaze" Angel alivunja ukimya wake

"Noo usiseme hivyo unayo nafasi ya kumsahau Yule muuaji"

"Hapo ulipo Una bastola, ni sekunde tu inatosha kuchukua uhai wangu" 

"Acha utani, basi unajua Urusi wewe" Abdul alimwambia huku akitabasamu, alipeleka mkono wake wa kushoto na kuzichezea nywele laini za kipusa huyu

Angel alimuamuangalia bila kusema neno

"Ukimya nao ni jibu, ndani ya hizi siku tatu nataka nikupeleke Urusi"

"Ulimwengu unajua Manu yupo Urusi, umesema kum'sahau ni niwe mbali naye. Mbona sasa nimfuate Urusi" Angel alijiinua pale mapajani mwa Abdul na kuvuta kiti chake kisha akakaaa akitazamana naye.

"Manu yupo hapa Kenya amejificha tu, labda nikuibie siri muuaji wako hakuwahi kwenda Urusi wala haijui harufu ya Urusi"


'&#x2764 Angel stay safe usiamini ulimwengu niamini mimi, bado nipo Urusi, &#x2764 see you soon' Angel alikumbuka ujumbe huu na kutabasamu

'inamaana nikienda Urusi nitamuona kipenzi changu. Na Abdul naye ana kila dalili za kunitaka, ooh my God na nimejiachilia naye kweli labda kuwe na mtu anatupiga picha amuonyeshe Manu si ataniacha mimi ooh no , lakini inabidi hivyo ' aliwaza 

"Tabasamu lako angavu, niamini mimi nilopewa kumsaka muuaji Yule" 

Angel alibaki kimya, naye Abdul aliendelea kuongea

"Uhakika ni tutampata tu na hataamini"

Kuna lengine au ni hayo mauaji?" ilibidi Angel amuulize maana anapotamka jina la Manu huonyesha hasira na chuki machoni mwake

Abdul alitabasamu na kumjibu

"Kama polisi, hatuhurumii muuaji, avunjaye sheria hivyo acha sheria ichukue mkondo wake. Isingekuwa sheria Manu angekuwa marehemu" alitinia nukta.

Abdul alisimama na kumzunguka Angel mara tatu na akasimama nyuma yake, alipeleka mkono wake shingoni mwa Angel na kuinua kichwa chake, na yeye akainama na kupeleka kichwa chake uelekeo wa shingo ya Angel na kuanza kumbusu, pole pole hadi Kwa shavu la kushoto.

Angel alimsukuma baada ya uelekeo wake kuubadilisha kuelekea Kwa kinywa chake

"Pleaseeee stop it. I'll be all yours tukifika Urusi" Kwa sauti legevu isiyokera masikio ya wanaume bali kukosha roho za wengi ilimtoka malaika huyu kama Abdul anavyomuita

Abdul alibaki amekodoa macho haamini kauli ile imetoka Kwa mrembo huyo.


Vitendo vyote walivyovifanya wawili hawa, vilionwa na wana Risasi Tatu.

"Inabidi tujue yule mrembo ni Nani" Ngamba aliwambia wenzake.

"Na Mike ana majibu yote, maana hawa wanaonekana ni wapenzi wa muda mrefu tu" alizidi kuongea Ngamba

"Ni kweli maana bila hata haya watu wazima wanafanya yale hadharani" Ngube naye alitia neno

"Tulikaa muda mrefu bila kufanya kazi hizi" akasema Ngombo, wenzake walimungalia na kutikisa vichwa vyao ishara ya kukubaliana naye

"Mnasahau Abdul ni polisi anayeongoza oparesheni ya kumsaka mwana; Manu. Kitu hapa si kumjua sana huyu mrembo bali ni tujue huyu Abdul ni nani hasa. Bila shaka huyu mrembo ni Mpenzi wake Manu. Navyowaza ni kuwa Abdul anataka kumtumia mrembo yule kumpata Manu" alimeza mate na kuwaangalia wenzake kama anaongea wanaelewa. 

"Mmmh akili zetu nazo zililala hata hazifikiriii" Ngamba na Ngube Kwa pamoja waliongea hayo.

"Ulimwengu unajua Manu yupo Urusi, Wakenya tumeaminishwa Manu yupo Kenya, hatujui Abdul anaamini nini, nachoamini mimi ni kuwa Abdul anaamini anavyoaamini yule msichana." Ngombo Kwa mara nyingine tena aliwataza wenzake.

"Si mbaya unavyosema lakini kusema kweli tuache kuumiza vichwa vyetu sijui Abdul ni nani wala yule mrembo. Kazi yetu ni moja tu ya kumlinda yule binti basi" Ngamba alisema Kwa ukali kidogo

"Haina maana tunaanza kazi halafu tukwazane, hiyo sio sifa ya Risasi Tatu" Ngombo alisema

"Yote niliyosema sikuwa na ubaya lakini kazi yetu itakuwa rahisi tukimjua kwa undani Abdul" 

"Lakini Ngombo si nimesema Abdul ni polisi na anafuatilia kesi ya mauaji ya Frankoo Sari" Ngube naye alionyeshwa kukerwa na kauli za Ngombo

"Ndugu zangu kufanikiwa Kwa kazi yetu hii ambayo hatujui itatupeleka wapi wala kuisha lini ni kumtazama Abdul Kwa jicho la tatu, na tuache kumuangalia kama polisi wa kawaida" 

Ngamba alitoa kicheko kwa kauli hii

"Usinambie eti Abdul ni jasusi, nishakuona mwana Acha wasiwasi. Angekuwa jasusi mtandao wetu ungem'tambua kitambo tu"

"Yap Abdul ni jasusi aliyekubuhu, mtandao wetu unatambua tu kile wananchi wa kawaida wanajua naona mumesahau hilo. Tofauti yetu na wananchi ni kuwa sisi tufahamu ukweli hata akiwa amevaa raia haijalishi ni mara ya Kwanza kukutana ama la, halafu kuna wananchi wanaojua ukweli watakapo muona akiwa amevaa sare"

Mara hii kauli hii iliwagonga vichwa vyao

"Asemaya Ngombo ni kweli, sasa tufanye kazi kama Risasi Tatu" alitoa neno Ngamba


"Kazi tumeianza vibaya oneni kule"

Ngube aliwambia wenzake na kunyosha kidole kuelekea sehemu walipo Abdul na Angel.


********

Mariakani Barracks, Kenya


Raisi Willy Baro alifanya ziara ya ghafla katika kambi hii ya wanajeshi.

Wanajeshi watabaki kuwa wanajeshi. hope mnaelewa.

Moja Kwa moja aliingia katika chumba fulani pale kambini.

"Karibu mheshimiwa Raisi" alinena binti mmoja mle chumbani

"Thank you, Nuru pole sana Kwa yalokukuta na amini Henessa na timu yake bado wanamtafuta yule kijana"

"Nishapoa Mheshimiwa Raisi, nachoomba ni ruhusa yako tumpuzishe Baba huku wakiendelea kumtafuta"

"Binti nasikitika sana lakini wewe hukuwa unampenda baba yako hata chembe"

"Mbona useme hivyo mheshimiwa raisi" aliuliza Nuru

"Mapenzi yako yote yako Kwa yule muuaji"

"Sikuelewi mheshimiwa raisi"

"Hunielewi sio, niliambiwa Binti ya Frankoo Sari haelewi chochote, alikuwa hamuelewi babake. Nuru kuna mtu mmoja humuelewa hadi akipiga mluzi huelewa amesema nini, na mtu huyo ni Emmanuel"

"Bado sikuelewi mheshimiwa raisi"

"Na mimi si huyo mtu anaitwa Manu, Mimi ni raisi wa jamhuri ya Kenya"


Nuru ilimbidi kukaa kimya maana hakuelewa kauli za mheshimiwa raisi Willy Baro.

Ni ni siku ya Nne tangu alipoletwa katika kambi ile ya jeshi toka kaunti ya Kiambu na kufungiwa chumbani mule.

Hakuelezwa sababu za yeye kuzuiliwa, hadi leo hii anatembelewa na raisi.

Uwepo wa raisi mahala pale ulimpa matumaini ya kutoka katika kizuizi maana yeye ni mfanya kazi wa ikulu upande wa usalama pia kupatana idhini toka kwa raisi kumzika baba yake. Matumaini yalififia baada ya raisi kuanza kutoa kauli asizozielewa.

"Pia wakanambia Nuru ni binti jeuri, atakujibu mwishowe atakaa kimya. Kiumbe kinachoitwa Manu ndiye hanyamaziwi na binti Kwa jina Nuru"

"Mheshimiwa Raisi unataka nini, ni wewe ndio ulitoa agizo nizuiliwe hapa"

"Ni mimi" 

Nuru alimtumbulia macho raisi, kisha akatabasamu

"Sasa nimeamini" akasema

Raisi alishangazwa na kauli ile

"Umesema nini"

"Nimesema nimeamini, na nilifanya maamuzi ya kweli. Labda raisi niseme umesahau mimi ni nani"

"Nuru binti ya muuza Siri za nchi" 

"Ni sawa, so unataka nini toka kwangu" raundi hii Nuru alivaa Sura ya kazi

"Manu yuko wapi" 

Nuru aliachia kicheko kikubwa na kupigapiga makofi 

"Hilo andika umenoa Raisi, sitatoa kauli ya wapi alipo"

"Kwa siku Nne umeishi vizuri hapa ndani labda nikuhakikishie usiposema hutatoka hai katika kuta hizi"


"Eti eee" Nuru alisema na kumsogelea raisi na kumtazama Kwa macho yake

"Umekosea sana raisi, umesahau mimi ni nani. Na wewe nakwambia omba miungu yako nisitoke hai ndani hapa"

"Unajiamini nini binti, sema Manu yuko wapi maana wewe ulimtorosha, tukimpata Manu pia nanyi mtamzika Mzee wenu mkiwa na amani maana yake muuaji atakuwa mbele za sheria"

"Raisi nisikilize, acha kupoteza muda wako mwambie Henessa na timu yake wamtafute muuaji. Manu si muuaji"

Raisi alibaki kinywa wazi



Tukutane Urusi wadau........ 





 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.