JESTINA 11

 RIWAYA: JESTINA

MTUNZI: Tariq Haji

CONTACT: +255624065911


SEHEMU YA 11


"unajua mke wangu Alwin kabadilika sana siku hizi" aliongea Mr Kelvin kumwambia mkewe, "kivipi mbona mi namuona yupo kawaida tu. "hapana mke wangu mi nakwambia tena Alwin kabadilika sana tokea atoke hospitali ya vichaa" alisitiza Mr Kelvin. "mhh haya lakini mi namuona kawaida tu isipokuwa siku hizi kachangamka sana tafauti na zamani" aliongea mama Alwin huku akiachia tabasamu akionesha kufurahishwa na mabadiliko ya Alwin. Wakati wakiendelea kuongea Alwin aliingia na kuwasalimia, waliitika kwa pamoja na baadae Alwin akaenda zake chumbani kwake.

 


Kwa upande wa inspecta Hans baada ya kutoka kwenye kikao alikwenda nje na kutulia huku akili ikitafakari mengi sana, akiwa dimbwi hilo la mawazo aliskia akiitwa na alipogeuka alikutana na mkuu wake wa kituo inspecta Brandon. "nifuate ofisini" aliongea na kuondoka, bila kusita aliinuka nae akamfuata nyuma mpaka walipofika ofisini. "bwana mdogo chunga kauli zako" hayo ni maneno ya kwanza yaliotoka kinywani mwa inspecta Brandon, "wewe hapa kituoni unaongea vile kama nani" aliendelea kuongea kwa hasira. "samahani mkuu, ule ndio ukweli we unadhani dunia bila haki ipo sawa. Hata waliokufa nao wanataka haki zao, we ulielewa fika kama Matt na wenzake wako hatiani lakini ukaibaitilisha kesi na kumuuzia Alwin. Natamani huo mzimu siku moja ukutembelee na wewe uone machungu ya kudhulumiwa" alijibu inspecta Hans bila woga wowote ule. "sasa unaonekana umeota mapembe si ndio" aliongea inspecta Brandon, "kama ndivyo unavofikiri sawa tena makubwa sana" alijib inspecta Hans na hakusubiri neno jingine kutoka kwa mkuu wake aliondoka maana hata yeye hasira zilishaanza kumpanda. Alimuacha mkuu wake akiwa ni mwenye mawazo tele lakini akaona bora apotezee tu.

 


Kifo cha Jesca kiliwachanganya wengi miongoni ya waliotenda kosa lile, wapo walioomba usiku usiingie maana walijua Jestina hufanya mauaji yake usiku. Lakini kwa vile hatuwezi kuzuia masaa basi muda uliyoyoma na hatimae kiza kikaana kutanda angani, hatiame usiku uliingia lakini kulikua na mvua kali sana iliondamana na ngurumo pamoja na radi. Usiku huo ulivo ulitosha kuwatisha wengi sana, Mark ndo alikuwa akitoka zake mihangaikononi kwake kuelekea nyumbani kwao ghafla akiwa njiani umeme ukazima.

 


Hali hiyoilimshtua kidogo Mark lakini akajipa moyo kuwa ameshaakaribia nyumbani kwao, hivyo basi alianza kukazana huku akiangalia pande zote kama kuna kitu ama mtu anamfuata. Nyumba yao ilikuwa imejitenga kidogo kutoka katika makazi ya wtu wengine, aliacha njia kubwa na kuingia njia ndogo ambayo ilikuwa nampeleka mpaka kwao. Wakati akikazana kwa mbali mbele yake akaona kama mtu kapita mbio. Moyo ulianza kumuenda mbio maana alishaanza kuziona dalili za mauzauza, akiwa anatetemeka ghafla alihisi kama kitu kimepita nyuma yake. Aligeuka kwa kasi lakini hakuona kitu, alipogeuka tena mbele kwa mbali akaona mtu akiwa anakuja upande wake taratibu . Kidogo alipata matumaini na kuanza kukazana kumfata yule mtu. Lakini alivomkaribia mwili ulimsisimka na kuhisi kama hakuwa mtu wa kawaida lakini alipiga moyo konde na kunyongea kwa mendo wa haraka. Ghafla tochi yake ilizima, na ilivowaka alikutana sura ya ajabu sana mbele yake. Aliruka na kuiangusa tochi pembeni, japo kulikuwa na baridi lakini kijasho kilianza kumtoka kwa wingi. "maumivu...." alisikia sauti ikitamka neno hilo kwa sauti a kuning'ona, "leo utahisi maumivu nilioyapata" sauti hiyo iliendelea kuongea huku ikizidi kuwa kali. "unataka nini lakini" aliuliza Mark kwa woga, "nataka roho yako" alijibiwa na wakati huu sauti aliifahamu vizuri sana kama ilikuwa sauti ya Jestina.

 


Aliokota tochi yake na kuanza kukimbia, lakini hakufika mbali alishtukia akichezea kofi zito la uso lililomfanya aanze kuona mawenge kidogo na kuanguka chini. Mark alijua kuwa huo ndio ulikuwa mwisho wake, "nisamehe Jestina" alianza kuomba msamaha kwa kilio huku damu zikimoka mdomoni. "leo unalia mshenzi mkubwa wewe, siku ile ulikuwa ukicheka" Jestina aliongea na kumnyanyua Mark. Sasa alifanikiwa kumuona uso kwa uso, macho yalimtoka Mark asijue nini la kufanya. Wakati akiendelea kutumbua macho alirushwa kwa nguvu, kabla hajakaa sawa alichezea makucha kadhaa ya mgongo na kumfanya apige kelele za maumivu. "nimekoma naomba unisamehe" aliongea huku akisimama, "nikusamehe kweli, hivi unajua ni maumivu kiasi gani niliyapata siku ile" Jestina alijibu na kumtokea Mark mbele na kumkaba, kisha sura yake ilianza kubadilika na kuwa ya kutisha sana huku damu nyingi zikichuruzika kutoka machoni mwake kama machozi. Mabadiliko hayo yaliambatana na harufu kali sana ya kuoza, kwa nguvu alimpiga Mark na chini kiasi cha kushndwa kuinuka. "leo utakiona cha moto mpumbavu mkubwa wewe" aliongea Jestina na kisha akamfungua mdomo Mark na kumtia funza. Yeye alikaa pembeni akimuangalia kwa jinsi funza wanavomteketeza Mark. Hawakuwa funza wa kawaida kwani punde baada ya kutiwa mdomoni walianza kutoboa sehemu mbalimbali za mwili wa Mark na kusababisha maumivu makali sana. Mark alipiga sana kelele lakini hakuna msaada wowote alioupata mpaka mwisho alitulia tuli na kuaga dunia. Jestina alipotea eneo hilo akiacha ujumbe wake wa kawaida. 

 


Asubuhi taarifa ya kwanza ilikuwa ni kifo cha Mark, huku ikisema bado mauaji hayo hajulikani yanasababishwa na nani. Lakini kilichowashtua watu ni kwamba wote waliokufa walikuwa ni marafiki tokea zamani sana, hivo kukaibua maswali mengi sana. Kituo kimoja cha televisheni kiliomba kufanya mahojiano na mwalimu mkuu wa shule ambayo inaaminika kuwa wote waliokufa wamesoma pale.


"habari yako mwalimu"

"nzuri nashkuru"

"kwa jina naitwa Anita ni mwandishi wa habari kutoka J76 news chanel"

"mimi naitwa Anthon Dickson, ni mwalimu mkuu hapa"

"naam mwalim unazungumziaje matukio haya ya mauaji yanayoendelea hapa mjini hasa ukizingatia wote walipoteza maisha mpaka sasa ni wananfunzi wako"

"kwa kweli ni vigumu kueleza"

"kivipi mwalimu"

"unajua ndugu Anita hapa kulitokea kesi kubwa sana ya ubakaji kama utakuwa unakumbuka, ni takriban miaka kumi sasa imepita na inavosemekana kuna wananfunzi wamehusika na tukio hilo"

"unaweza kuwataja"

"hapana siruhusiwi kufanya hivo"

"na kwanini hasa ukawa unahisi kama mauaji yanayofanyika sasa ya uhusiano wowote na kilichotokea miaka kumi nyuma"

"Unajua tulivokuwa wadogo, tulikuwa tukisimuliwa mambo mengi sana ambayo wengi wetu hatuyaamini"

"kama yapi"

"kwa mfano najua utakuwa umesimuliwa kuhusu ulimwengu wa watu waliodhulumiwa"

"ndio lakini hizo ni hadithi za kufikirika tu"

"hapo ndio kwenye utata sasa na hilo ndilo linalotokea saa hivi, baada kufanyika tukio lile kesi ilipelekwa mahakamani lakini cha ajabu ilizimwa haraka na watuhumiwa wakaacha huru, kwa sababu haki haikupatikana, sasa aliedhulumiwa amerudi kuja kuitafuta haki kwa mikono yake kama tunavojua HAKI ISIPOPATIKANA KWA AMANI BASI ITAPATIKANA KWA VITA. Na hii ni vita ambayo hakuna mtu yoyote kati yetu anaeweza kuizua na kama huamini kama mizimu ipo heebu jaribu siku moja kuuwa halafu uachiwe huru uone kama hutokipata walichokipata hawa vijana walikufa"

 


Mwalimu mkuu alimaliza kuongea na kuomba kuondoka akaendelee na majukumu mengine ya kawaida. Na kwa sababu kipindi hicho kilikuwa hewani live kila mtu alishuhudia, "ni bora wafe tu ili watu wajue kama haki ya mtu ni mali", "pumbavu nani atakaa aamini upumbavu ule". "mmmh makubwa mi nlijua ni hadithi tu za kufikirika", hayo ni baadhi ya maneno yaliokuwa yakisemwa na baadhi ya watu kila pahali. Kwa kweli story ilikuwa ni hiyo tu kila kona unayopita, Alwin ni miongoni mwa watu waliokiona kipindi hicho na kufurahia sana majibu ya mwalimu, yalitosha kupeleke ujumbe kwa wote ambao wanacheza na haki za watu. 

 


"jamani hali imezidi kuwa mbaya sasa" Jay aliongea katika kikao kifupi cha dahrura kilichoitisha baada ya kifo cha Mark. "sasa tunafanyaje" aliuliza Monica, "ah hatuna la kufanya, sisi tulitenda uovu huku tukifurahia bila kufikiria ni kiasi gani tulichowaumiza wengine" Jay aliongea akionekana kujuta sasa. "akah! we vipi sasa unajuta nini, mi nasema hapa cha msingi ni kumuua Alwin maana nahisi yeye ndie anetufanyia mchezo huu" alifoka Alex kwa hasira. "sasa umeona ulivokuwa huna akili unataka kurekebisha kosa moja kwa kutenda jingine" Jay alimjibu akionekana kuchukizwa na maneno ya Alex. "mi nlikwambieni huyo boya ni mtoto wa mama" aliongea Alex na kumkejeli Jay, "sawa mi ni mtoto wa mama, lakini mi naona bora tujiandae kufa tu maana hatujui anefuata ni nani" Jay aliongea na kuinuka kisha akaanza kutoka nje, "nenda huko na leo utakufa wewe, Jestina kama unanisikia leo Jay amejianda ukamuue sawa" aliongea Alex na kufanya mzaha.

 


Jay hakujibu kitu,wakati anatoka aliingia unyonge wa ghafla na kupatwa na homa kali sana iliomfanya aanguke barabarani. Wasamaria wema walipiga simu hospitali na punde gari ya kubebea wagonjwa ilifika na kumuawahisha hospitali. Alipofika tu alipatiwa huduma ya kwanza na kupelekwa chumba cha wagonjwa mahututi kutokana na hali yake kuwa mbaya sana. Familia yake ilifka akiwemo mkewe na mwanae wa kike mwenye umri wa miaka minne, lakini hawakuruhuisiwa kumuona kutokana na kuwa hali yake haikuwa nzuri. Hali hiyo ilimtia simanzi mkewe kumuona mumewe yupo katika hali mbaya sana lakini angefanyaje na alitakiwa kusubiri.

 


Walisubiri mpaka jioni lakini hali yake haikuchanganya hico wakaambiwa waondoke na warudi kesho kwa ajili ya kumuangalia walikubaliana na daktaru na kuondoka. Kiza kilianza kuingia lakini bado hali ya Jay haikutengemaa kabisa "kwa kweli tumejaribu kadri ya uwezo wetu sasa ni muda wa kumuachia Mungu atende muujiza" aliongea daktari mmoja na wenzake wakamuunga mkono. Walizima vifaa vyote na kumuhamisha chumba, huko walimuunganisha na mashine ya kupumulia kwa ajili ya msaada maana hata pumzi ilikuwa ni ngumu kuvuta. Baada ya hapo walitoka wote na kumuacha chini ya uangalizi wa manesi. 


ITAENDELEA.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.