JESTINA 12

RIWAYA: JESTINA

MTUNZI: Tariq Haji

CONTACT: 0624065911


SEHEMU YA 12.


Walisubiri mpaka jioni lakini hali yake haikuchanganya hico wakaambiwa waondoke na warudi kesho kwa ajili ya kumuangalia walikubaliana na daktaru na kuondoka. Kiza kilianza kuingia lakini bado hali ya Jay haikutengemaa kabisa "kwa kweli tumejaribu kadri ya uwezo wetu sasa ni muda wa kumuachia Mungu atende muujiza" aliongea daktari mmoja na wenzake wakamuunga mkono. Walizima vifaa vyote na kumuhamisha chumba, huko walimuunganisha na mashine ya kupumulia kwa ajili ya msaada maana hata pumzi ilikuwa ni ngumu kuvuta. Baada ya hapo walitoka wote na kumuacha chini ya uangalizi wa manesi. 

 


"Jay.....amka" alisikia sauti ikimuamsha huku akitingishwa, kwa uvivu alifungua macho na mbele yake alikuwa Jestina amesimama akiwa na sura yake ya kawaida, sio ile ya kutisha. "najua umekuja kulipiza" aliongea Jay huku akiitoa mashine ya kupumulia, "lakini nina ombi moja tu kwako, naomba uniache mpaka kesho angalau nimuone mwanangu kwa mara ya mwisho kabla ya kuaga dunia" aliongea Jay kwa masikitiko makubwa. "kwanini ulikubali kushuhudia unyama ule" aliuliza Jestina huku uso wake ukianza kubadilika na kuwa wa kutisha. "kwa kweli siku ile sikutegemea kama kungetokea tukio kama lile" alijibu Jay kiunyonge, "lakini wakati linafanyika ulikuwa na uwezo wa kuzuia lisifanyika" aliongea Jestina akizidi kutisha. "hilo ndio linalonijutisha mpaka leo" aliongea Jay huku machozi yakianza kumtoka, "najua kama nimekukosea na niko tayari kulipa kwa nilolitenda, lakini naomba unipe siku moja tu japo nimuone mwanangu na mke wangu kisha njoo unimalize" Aliendelea kuongea Jay huku kilio kikipamba moto, alijaribu kujifuta lakini aliposusha mkono Jestina alikuwa kashaatoweka. "asante kwa kunikubalia ombi langu" aliongea huku akijiweka vizuri kitandani na kuendelea kulala.

 


 Asubuhi mapema familia yake ilifika kumuona, "nini kimekusibu baba Sophia" aliongea mkewe huku akimuangalia kwa huruma, "hata mimi mwenyewe sijui, homa tu ilinishika ghafla" alijibu huku akilazimisha kutabasamu. "pole mume wangu" aliongea mkewe kumpiga busu katika paji la uso, "pole dady utapona" sauti ya Sophia iliskika huku akimpa pipi baba yake. Sophia alikuwa kafanana sana na baba yake, na alimpenda sana. "Sophia baby njoo nkwambie kitu" Jay alimuita mwanae na kumnong'oneza kitu, Sophia alitabasamu na kumrukia baba yake kisha akasema " wewe ni baba mzuri kuliko wote". Muda wa kutizama wagonjwa uliisha na familia yake iliaga na kuondoka huku wakiahidi kurudi kesho yake kwa ajili ya taratibu za kwenda nae nyumbani. Aliagana nao huku machozi yakimtoka maana alielewa hiyo ilikuwa ni siku yake ya mwisho duniani. Kutokana na hali yake kuimarika mashine za msaada wa kupumua ziliondolewa na kupelekwa chumba cha wagonjwa wa kawaida tu. Aliendelea kupata matibabu madogomadogo, lakini akilini mwake alikuwa akiwaona kama madaktari wanatwangaa maji kwenye kinu maana usiku wa siku hiyo ni usiku wa kifo chake.

 


Usiku hatimae ulifika na Jay alikuwa tayari kwaajili ya kufa tu maana alielewa kabisa ni aina gani ya mauaji anayofanya Jestina. "Jay, naona uko tayari kwa adhabu yako" alimsikia Jestina akimwambia wakati akiwa amepumzika. "ndio niko tayari kwa chochote" alijibu Jay huku akitetemeka, "Kwa vile umelitambua kosa lako na kulijutia, mimi sikuja hapa kukuuwa maana kwanza una mke anaekuthamini sana na pili una mtoto ambae bado anahitaji malezi yako na upendo wako kama baba yake" aliongea Jestina na kujitokeza mbele ya Jay akiwa katika umbile la kibinaadamu "lakini nataka ufanye kitu kimoja, usijaribu kutoa ushahidi kokote pale na pia nakupa siku tatu uondoke Mashvile na familia yako yote, nenda mbali sana na uwe baba mwema kwa mwanao na pia mume mwema kwa mkeo. Na jengine asijue hata mmoja miongoni mwa marafiki zako waliohusika na kifo changu. Mimi nimekusamehe na nakutakia maisha mema na yenye amani tele lakini kumbuka ukitovukwa adabu nitakurudia" alimaliza kuongea Jestina na kuoweka. Jay hakuamini kama kasamehewa maana alielewa kabisa kuwa Jestina alikuwa hataki masihara, alilala usingizi mzuri huku akijiapiza kufanya yote aliyoambiwa.

*******************

 Mapema siku ya iliyofuata familia yake ilifika na taratibu za kutoka hospitali zikafanyika, baada ya kufika kwake alimueleza mkewe kuwa anataka kuhama Mashvile kwani amepata kazi nzuri nchini Italy. Aliwaeleza pia wazazi wake swala hilo na kwa vile yeye ndie aliekuwa analisha familia hakuna aliempinga, maandalizi ya safari yalifanyika kimya kimya bila hata rafiki yake mmoja kujua. Jioni yalikuwa yamekamilika na wote waliondoka mjini Mashvile "nakuahidi Jestina nitatekeleza yote ualionambia" aliongea maneno hayo kimoyomoyo wakati analipita bango liliandikwa KWA HERI MASHVILE. 

 


"Oya Alex mtu wangu mbona tokea jana sijamsikia Jay" Patrick alimuuliza Alex ambae alikuwa bize akijaribu kumchora mwanadada mmoja ambe alionekana kudance vizuri sana, "ah mara mwisho niliskia kalazawa hospitali, lakini nahisi Jestina atakua kashampitia tayari" alijibu Alex na kuinuka kulekea katika ulingo wa kudance lakini nia na madhumuni yake ilikuwa ni kwa ajili ya yule mschana. "habari yako mrembo"

"safi tu"

"Mimi naitwa Alex sijui mwenzangu"

"ahaa mimi naitwa Jessie"

"jina lako zuri, tunaweza tukasogea pembeni tukaongea mawili matatu"


"hamna shida"

basi walisogea mpaka counter na Alex akaagiza vinywaji kisha wakaanza kuongea, waliongea sana mwisho walionekana kukubaliana "oya Patrick wacha mi nitoke na shemeji yako" Alex alimuita Patrick na kumwambia, "oya mwanangu mtoto huyo mkali, kama vipi tupige tungo" Patrick alimnong'oneza Alex. "tulia mtu wangu mi naenda nae geto nikimaliza kula asali na kutwangia na wewe uje kuonja mtu wangu" aliongea na wakakubaliana.

 


Patrick alirudi kwenye dance floor huku Alex akiondoka na Jessie, "tunaenda wapi sasa" aliuliza Jessie, "ah nyumbani kwangu si mbali na hapa" alijibu Alex na kuzungusha mkono wake kwenye nyonga ya binti huyo. Mwendo ulikwa wa dakika tano tu hatimae walifika geto na kumkaribisha ndani. "kaa kitandani hapo nakuja" aliongea Alex na kuingia chooni, kumbe alikwenda kutega camera ili ajirikodi anavomkuna mrembo huyo. Alirudi na kumkuta tayari ameshavua nguo na kubakia mtupu, tamaa ya ngono ilimpanda Alex kujikuta anamvamia lakini kabla hajafikisha mdomo wake kwenye midomo ya mrembo huyo alijikuta akirushwa kwa nguvu.

 


Ghafla mrembo huyo alianza kubadilika, naam hakuwa mwengine isipokuwa Jestina. "wewe hujabadilika hata kidogo" aliongea kwa nguvu sana, "yaani bado wewe na yule mshenzi mwenzako mlikuwa mnafikiri kupiga mtungo" aliendele kuongea huku akimsogelea. "Jestina nisamehe" alianza kuomba msamaha, "umechelewa sana" alijibu Jestina na kupiga kofi la uso akimwachia alama za kucha. Alex aliweweseka lakini alipofungua macho hakumuona ila ghafla akamtokea kwa nyuma na kumchana mgongoni. Alex alipiga yowe la kuomba msaada lakini wapi hakuna lolote lilisikilikana nje ya chumba hicho. Jestina akatoweka tena na kumtokea mbel yake ila hakumgusa alimuangalia tu usoni na Alex mwenyewe akaokota kipande cha kioo na kunaza kujichana. Alipiga kelele kwa maumivu lakini alishindwa kujizuia mwisho alianguka chini, hapo Jestina alimsogelea na kumpiga kucha za shingo na kulitoa koromeo, aliacha ujumbe na kutoweka huku Alex akiwa chini akijaribu kuvuta pumzi ambayo haikua na pakupita mpaka mwisho akakata roho. Patrick baada kuona Alex hapigi simu aliamu kutoka na kumfata geto.

 


Kwa mwendo wa haraka Patrick alifka geto kwa Alex na kukuta mlango umefungwa lakini kila alipojaribu kugonga haukufunguliwa. Alisubiri kama dakika kumi kumi hivi ila bado kulikuwa kimya, mwisho alikumbuka kuwa ana ufunguo mwengine wa mlango huo lakinialipojaribu kuingiza kwenye kitasa uligoma hiyo ilikuwa ni ishara kuwa kulikua na ufunguo mwingine kwa ndani. Baada kuona jitihada zake zimegonga mwamba aliamua kutoa simu yake na kuandika ujmbe "poa mshkaji wangu tumekubaliana vipi na wewe unafanya nini, mbona mimi nikipata kama hivo tunapiga mtungo safi ila haina noma" aliutuma na kuondoka. Aliondoka na kuelekea nyumbani kwao, baada kufika alivua nguo zake na kwenda kujimwagia maji. Alimaliza na kutoka kurudi chumbani na hapo ndipo aliposhtuka kidogo maana suruali yake chini ilikuwa imeganda damu. Alitahidi kutafuta ni sehemu gani ameumia lakini hakuiona ndipo machale yakamcheza lakini akapotezea na kuingia kitandani. 

 


Asubuhi mapema aliwahi kuamka nakwenda geto kwa Alex, alipofika alishtuka sana baada kuona michirizi ya damu ikitokea ndani ya chumba hicho. Alipiga kelele na watu wakaja kwa pamoja walisaidiana kuvunjia mlango na hapo ndipo wakakutana na mwili wa Alex umelela sakafuni huku ukiwa umetapakaa damu. Bila kuchelewa walipiga simu polisi na kutoa taarifa, ila alichokifanya Patrick ni kuchukua simu ya Alex na kuufuta ujumbe aliomtumia ili asije akaonekana yupo hatiani. Haukupita muda polisi walifika eneo la tukio na kuanza kufanya uchunguzi na katik tafuta yao walifanikiwa kuipata camera alioitega Alex na kuichukua kama sehemu moja ya ushahidi wao. Walimaliza kufanya uchunguzi na taratibu nyingine zikafuata ikiwa ni pamoja na kuupeleka mwili wa Alex hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi. 

 


"tumefanikiwa kupata camera sehemu ya tukio" aliongea polisi mmoja na kumkabidhi Inspector Hans ile camera. Na yeye bila kuchelewa aliunganisha na computer yake na kuanza kuangalia, ilionyesha Alex akitoka chooni na alipofika kitandani alijirusha lakini hakuonekana mtu mwengine katika kitanda hicho. Lakini ghafla alichomoka kitandani na kujigonga ukutani kisha akaonekana kama akiomba msamaha lakini ghafla alipiga kelele na damu kuanza kumtoka. Waliendelea kuangalia video hiyo mpaka walipoona anachukua kioo na kuanza kujikata wenyewe mpaka akaanguka chini na ghafla akaanza kutoka damu shingoni kama ishara kuwa amekachinjwa, yakatokea maandishi ukutani "AMELIPA". Hapo camera ikaingia chenga na kuzima kabisa,askari wengi waliotizama ile video walishtuka sana hasa pale yalipotokea maandshi ukutani. 


ITAENDELEA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.