JESTINA 14

RIWAYA: JESTINA

MTUNZI: Tariq Haji

CONTACT: +255624065911


SEHEMU YA 14


Usiku uliingia huku maandalizi ya sherehe kubwa ya yakifanyika, ilikuwa ni sherehe ya kumkaribisha Miryam. Alwin akiwa kwao aliskia akiitwa na mama yake na aliposhuka alikutana na mtu asie mfahamu. Alikuwa na briefcase mkononi, "Mr Alwin huu ni mzigo wako" aliongea na kumkabidhi kisha bila kuongea kitu yeye aliondoka. Alwin alirudi chumbani kuufungua mzigo huo, alishangaa kuona kuna suti ya rangi ya maziwa au crem, viatu, tai nyekundu pamoja na funguo ya usafir. Pembeni kulikuwa na barua ndogo iliosema hivi.

 


"jiandae uje nyumbani kwangu by Profesa", yeye akiitwa na profesa huwa hafikirii mara mbili, aliingia chooni na kujimwagia maji. Alipomaliza alitinga suti alioletewa na kuning'iniza tai shingoni, alivaa viatu na kuchukua funguo lakini alipaongalia vizuri aliona saa moja matata sana na yeye bila kuchelewa aliitia mkononi na kuhakikisha kuwa amechukua kila kilicho ndani ya briefcase hilo. Alipojiridhisha yuko sawa alitoka chumbani kwake na kuelekea nje, aliwaaga wazazi wake na kutoka. Nje huko alikutana na gari moja ya bei mbaya aina ya Buggtti supersport vitesse ya rangi ya maziwa. Hakuuliza alibonyeza kitufe na kutoa loki, aliingia kwenye gari na safari ya kuelekea kwa profesa ilianza, kwa mwendo wa umakini zaidi alitumia dakika kama saba hivi kufika mjengoni kwa profesa.

  


Alishuka gari na kumkabidhi funguo mlinzi aende akaiweke maegesho, "na sasa anaingia mgeni rasmi wa kwanza Mr Alwin Kelvin" MC alitangaza na ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe. "mmh jamani huyu kapendezaje", "wee jifanye mwendawazimu tu mali ya watu hiyo shosti". "sasa kwani mimi jiwe" hayo ni maneno waliokuwa wakiongea waschana wawili ambao walivutiwa sana ujio wa Alwin. 

 


Basi aliekezwa meza kuu na kuambiwa akae kwenye kiti, "profesa kuna nini mbona unafanya sherehe" aliuliza Alwin "mambo matamu hayataki haraka" alijibu Profesa na hapo Alwin alielewa kuwa anatakiwa asiulize tena maswali. "na sasa tumkairbishe mgeni rasmi mwengine ambae pia ndie mlengwa mkuu wa sherehe hii Ms Miryam Alexander Harison" MC alitangaza tena na kuwafanya watu wachizike kwa makelele. Alwin alijikuta akitumbua macho kama mjusi aliebanwa na mlango huku akihisi hata moyo wake ulipunguza kasi ya mapigo, bila kujitmbua alijikuta akisemama na kuelekea kwenye ngazi ambapo Miryam alikuwa anashuka, hakuna aliemuuliza watu wote walitengeza njia ili apite bila kikwazo. "kwa kweli umependeza sana" alisema maneno hayo huku akimpa mkono Miryam, "asante hata wewe umependeza pia" alijibu Miryam. walitembea wawili hao huku wameshikana mikono utadhani ni mfalme na malkia wake mpaka kwenye meza.

**************************

 


Kimbembe kilikuwa kwa Patrick amabe alikuwa anapambana kutetea maisha yake, "Jestina najua nimekukosea naomba unisamehe", "ulikuwa na muda mwingi wa kutubu lakini hukufikiria hilo" Jestina aliongea kwa hasira mpaka radi zikawa zinapiga. Lakini ghafla alianza kupotea bila mpango, Patrick alipoona adui yake anapoteza muelekeo akaamua kutoka nduki. "Alwin nakuomba subiri japo kidogo nimalizane na huyu kwanza" aliongea katika moyo wake, na papo hapo akatoweka na kumtokea Patrick kwa mbele, bila kuchelewa alimpiga kucha za koromeo na kumuulia mbali. Alimpa kifo cha haraka makusudi ili asije akapoteza nguvu kabisa, Patrick alianguka chini kama mzigo huku damu nyingi zikimtoka shingoni. Taratibu Jestina alianza kutoweka kama vile unavofuta mchoro wa penseli kwa ufutio, nguvu zilinza kumuisha na kuanza kusikia maumivu makali sana. Aliona njia peke ya kujinusuru na kutoweka kabisa ni kwenda alipo Alwin na kumueleza yanayomkuta. Kwa nguvu zake kidogo zilizobakia alifanikiwa kutoweka na kutokea nyumbani kwa profesa. Na moja kwa moja alitokea mbele ya Alwin lakini alishangaa na kuona hata Alwin alikuwa hamuoni tena.

 


Alijaribu sana kumtokea mbele yake lakini hali ilikuwa ileile, kwa wakati ule Alwin alisahau kila kitu kiasi cha kuwa akili yake ilikuwa ikiutathmini uzuri wa Miryam tu. Baada kuona haonekani mbele ya Alwin, akaona njia pekee ya kuongea na Alwin ni kwa kutumia mwili wa mtu mwengine, alizunguka ndani ya ukumbi huo mpaka alipopata mtu wa kumtumia. Hapo aliuingia mwili huo na kuelekea alipo Alwin, "Alwin tunaweza kuongea kidogo" aliongea na kumfanya Alwin kugeuka lakini hakushughulika sana kwa sababu mwanamke aliemuita wala yeye hamjui. Alijaribu kumuita tena lakini haliilikuwa ni ile ile ndipo akaamua kumgusa mkononi, hapo Alwin alizinduka na kumgeukia kwasababu mwili wake ulikuwa wa baridi haswaa. 

 


"Jestina unafanya nini hapa" aliuliza kwa sauti ya chini, "Alwin nakuomba nisikilize kwa makini sana" Jestina aliongea na kumvuta pembeni na kumueleza kila kitu. Alwin alishtuka kidogo baada kusikia vile, "subiri nikamwite Miryam" aliongea na kuondoka. "Miryam tunaweza kwenda kuongea varanda" nae Miryam hakukataa waliongozana mpaka varanda na kuanza kumueleza kila kitu, mwanzo Miryam alionekana kusita. "najua utakuwa huamini, subiri ni nimwite lakini nakuomba usipige kelele" aliongea Alwin baada kuona Miryam anakuwa mgumu kumuelewa. "Jestina jitokeze mbele yake ili akuone". Ghafla Jestina akatokea mbele ya Miryam "Mungu wangu, hivi ni kweli au nasinzia" yaliomtoka maneno hayo bila kujitambua. "Miryam nakuomba unisamehe kwa yale yote nlokukosea kwa sasa naomba unikubali kama rafiki yako kwa mara nyingine tena" aliongea Jestina huku akijitahidi asibadilike.

 


"Jestina mimi nilishaasahau hasa kama tuligombana mimi na wewe, siku ile nilitaka ufahamu tu kama ulikuwa ukiwaumiza watu wasio na hatia" Aliongea Miryam huku akimsogelea, "kama alivyoniambia Alwin kuwa umerudi kuja kuwalipisha waliokutenda basi mim niko pamoja na wewe" aliongea na hapo alikuwa karibu yake sana, aliamua kumshika mkono ili ajiridhishe kama kweli aliokuwa mbele yake. Alpomshika tu Jestina alitoweka na kumfanya Miryam ashangae kidogo "wow! Alwin its fantastic" aliongea huku akimkubatia Alwin kwa nguvu, "kama sheria ilishindwa kumpatia rafiki yangu haki yake basi mimi niko pamoja na nyinyi katika kuwateketeza wale wote waliohusika na kifo chake" Miryam aliongea lakini sauti yake ilikuwa imebadilika kidogo, Alwin alijitoa na kumwangalia "mbona unalia sasa" aliuliza kwa mshangao. "Alwin najua ulikuwa ukidhani namchukia sana Jestina, ukweli ni kwamba nilikuwa nampenda sana na ndio maana sikutaka apotee" aliongea Miryam kwa kwikwi. "usijali mpenzi wale wote waliohusika na kifo chake watalipa kwa maisha yao" Aliongea Alwin na kwa mara ya kwanza alimvuta Miryam na kukutanisha midomo yao au kama wanavyosema wengine "ROMANCE".

 


Kwa upande wa Jestina huo ulikuwa ni msimu mpya, maana alihisi mwili wake umepata uhai tena. Nguvu zake ziliongezeka mara dufu, wakati alizidi kutisha kiasi kwamba akikutokea tu kama unariho nyepesi basi unaweza kuaga dunia. Mvua ilianza kunyesha na radi zikawa zinapiga kwa nguvu sana hadi umeme ukazimika, "hahaha mlobakia jiandaeni" aliongea na kutoweka kisha hali ikarudi kuwa kawaida na umeme ukarudi. 

 


Alwin na Miryam walirudi uwanjani huku wakiwa wameshikana viunoni, moja kwa moja mpaka meza kuu. "Profesa" Alwin aliita kwa sauti ya chini, "sema Alwin" alijibu profesa huku akimuangalia. "nataka kukuibia kitu"


"wewe mtoto we, kitu gani hicho"


"ni kitu unachokipenda sana katika maisha yako" Profesa aliposikia hivyo akaelewa Alwin anamaanisha nini. Alisimama na kuelekea kwa MC kisha akachukua kipaza sauti na kuomba watu wamsikilize. "mabibi na mabwana naomba muniazime masikio yenu kwa dakika chache, ule muda niliokuwa nikiusubiria kwa hamu umefika, hatimae Mungu ameitika maombi yangu. Nawaomba wageni rasmi wasogee hapa jukwaani" aliongea na Alwin na Miryam wakainuka na kuelekea jukwaani. "napenda kumtambulisha kwenu rasmi Mr Alwin Kelvin ni mkwe wangu wangu kuanzia sasa" aliongea na ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe "hongera kijana na karibu katika familia" aliongea tena na kukumbatiana na Alwin kisha akairudisha mike kwa MC na kumwambia aendelee na ratiba.

 


Wakati wakiendelea na sherehe, aliingia mwanamke mwengine aliekuwa mzuri kupita maelezo. Vidume vyote vilianza kutokwa na mate ya kumtamani mwanamke huyo ambae alivaa nguo iliong'ara sana. Alitembea taratibu mpaka alipo Alwin na Miryam "hongereani sana" aliongea na hapo Alwin akashtuka baada kusikia sauti hiyo maana aliifahamu vilivyo kama ilikuwa ni sauti ya Jestina. "duh umebadilika" alikuta akiongea, "Jestina" Miryam aliita. "ndio mwenyewe" Jestina alijibu, Miryam alishindwa kujizuia na kumkumbatia bila kujali kama ule ni mzimu. Marafiki hao watatu waliongea na kufurahi sana, waliongea kama walivyokuwa wakiongea kipindi kabla hawajagombana. "Jestina nina ombi moja kwako" alikuwa Miryam, "lipo tena" aliuliza Jestina "ombi langu ni Matt, naomba umpe kifo chechenye maumivu makali sana" aliongea Miryam na kumfanya Jestina atabasamu kisha akajibu "usijali maana huyo dawa yako ipo kuzimu naipika".

 


"na mimi nina ombi moja" mara Alwin aliingilia, "haya lipi hilo" aliuliza Jestina. "nikipata mtoto wa kike nitamwita Jestina" aliongea na kutabasamu, "ah hilo si umwambie Miryam" alijibu Jestina, "mimi nimekubali" Miryam alijibu kisha wote wakacheka. "jamani muda wangu wa kuondoka umefika kwa hio tutaonana kesho" aliongea Jestina na wote walikubaliana. Alipiga hatua tatu ghafla umeme ukazima na uliporudi hakuonekana tena.

**************************************

 


Veronica akiwa kwenye gari yake anarudi kwao, alikuwa amefungulia mziki mzito hiyo ni kwa sababu alikuwa anatoka club kujirusha. Alipoangalia kwenye kioo aliona kama mtu amekaa siti ya nyuma, lakini alipogeuka hakuona kitu. "ah pombe bwana" alijsemea huku akitoa simu yake kwenye begi ili apige, ghafla alihisi kama kagonga kitu. Alisimamisha gari, kwa uoga akashuka kuangalia ni kitu gani. "toba nimegonga mtu" alijisemea baada kugunduwa kuwa aliemgonga ni mtu. Wakati anajishauri afanye nini mara akaanza kumuona akisimama huku akionekana kuvunjikavunjika viuongo, lakini ajabu vilianza kukaa sawa. Baada kuona hivo aliamua kukimbilila kwenye gari, lakini alipojaribu kufungua mlango ulikuwa na loki. Alijaribu milango mingine lakini hali ilikuwa hiyohiyo, "huwezi kunikimbia" alimsikia akiongea, Alipogeuka uso kwa uso na Jestina. "wewe si ushakufa" alijikuta akiropoka, "ndio" alijibu Jestina na kumtandika kofi la uso Veronica. Kisha akaanza kubadilika na kuanza kutisha sana macho yalikuwa meusi yote huku mwili wake ukitanuka na kutoa harufu mbaya sana. Veronica kuona hivo alianza kukimbia hovyo bila kujua wapi anaelekea, "huwezi kunitoroka" Jestina aliongea kwa hasira na kutoweka. 


ITAENDELEA.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.