JESTINA SEHEMU YA MWISHO

RIWAYA: JESTINA

MTUNZI: Tariq Haji

CONTACT: +255624065911


SEHEMU YA MWISHO


Veronica akiwa kwenye gari yake anarudi kwao, alikuwa amefungulia mziki mzito hiyo ni kwa sababu alikuwa anatoka club kujirusha. Alipoangalia kwenye kioo aliona kama mtu amekaa siti ya nyuma, lakini alipogeuka hakuona kitu. "ah pombe bwana" alijsemea huku akitoa simu yake kwenye begi ili apige, ghafla alihisi kama kagonga kitu. Alisimamisha gari, kwa uoga akashuka kuangalia ni kitu gani. "toba nimegonga mtu" alijisemea baada kugunduwa kuwa aliemgonga ni mtu. Wakati anajishauri afanye nini mara akaanza kumuona akisimama huku akionekana kuvunjikavunjika viuongo, lakini ajabu vilianza kukaa sawa. Baada kuona hivo aliamua kukimbilila kwenye gari, lakini alipojaribu kufungua mlango ulikuwa na loki. Alijaribu milango mingine lakini hali ilikuwa hiyohiyo, "huwezi kunikimbia" alimsikia akiongea, Alipogeuka uso kwa uso na Jestina. "wewe si ushakufa" alijikuta akiropoka, "ndio" alijibu Jestina na kumtandika kofi la uso Veronica. Kisha akaanza kubadilika na kuanza kutisha sana macho yalikuwa meusi yote huku mwili wake ukitanuka na kutoa harufu mbaya sana. Veronica kuona hivo alianza kukimbia hovyo bila kujua wapi anaelekea, "huwezi kunitoroka" Jestina aliongea kwa hasira na kutoweka. 

 


Wakati Veronoca anakimbia ghafla alijikuta akirushwa na kujipigiza katika mti, alitoa yowe la maumivu makali sana huku akijishika mbavuni. "nisamehe Jestina" alianza kulia huku akiomba msamaha, "wewe huna haja ya kusamehewa, wewe ulikuwa unashangilia wakati mwanamke mwenzako anadhalilishwa pumbavu mkubwa wee" alijibu Jestina na kumsigelea na kumtia vidole vya macho kisha akaanza kumpiga makucha. Alimnyanyua na kumpigiza na chini kisha akamnyanyua tena na kumrusha kwa nguvu, moja kwa moja alikwenda kutua kwenye gogo lenye ncha kali lilipenya mgongoni na kutokea mbele na hapo mia zake zikawa zimefika ukingoni, kama kawaida aliacha ujumbe na kutoweka eneo hilo.

 Uwezo aliokuwa nao sasa ulimuwezeshe kuwatokea maadui zake mpaka mchana, lakini hakutaka kutembeza kichapo mchana hivyo aliamua kuendelea na kazi yake nyakati za usiku. Wazazi wa vijana waliouwa waliamua kufanya maandamano na kuitaka serekali iwajibike na vifo vya watoto wao. Walonekana ni wenye hasira sana, "sasa jamani hasira za nini" aliongea waziri mkuu wakati akijaribu kuwapoza. "wewe na serekali yako ni wapuuzi, watoto wetu kila siku wanakufa vifo vya kutatanisha halafu wewe unatuuliza hasira za nini" aliongea mzazi mmoja, macho yake yalikuwa mekundu sana. "au kwa sababu wako wewe hayupo ndio maana unatuona sisi wajinga" mwengine alifoka, "eh yamekuwa hayo tena, basi msijali nawaahidi kuwa muuaji tutamkamata na tutamleta mbele yenu mumuhukumu" aliongea waziri mkuu na kuondoka bila kutaka swali lolote.

 


"dah mnajua leo nimedhalilika sana" aliongea waziri mkuu katika kikao maalum cha dharura, "mwiteni mkuu wa kituo" alitoa agizo. "hilo haliwezekani" alijibu Inspecta Hans nae pia alikuwepo kenye kikao hicho. "kwanini isiwezekane" alifoka waziri mkuu, "kwa sababu Inspecta Brandon yupo hospitaly kalazwa" alijibu inspecta Hans. "unasemaje wewe, sasa yule aliekuwa anakuja nyumbani kwangu tokea juzi ni nani" aliongea waziri mkuu huku akionyesha kuchanganyikiwa, "ndio muheshimiwa, tokea majuzi Inspecta Brandon amelazwa hospitali kuu akiwa amepooza" alijibu inspecta Hans, "na umesema alikuwa anakuja kwako" aliuliza Inspecta Hans. "ndio kwanini atakuwa nani yule" alijibu na kuuliza kwa wakati mmoja, "huyo ndio muuaji mwenyewe" alijibu inspecta Hans na kumfanya waziri ashtuke kidogo na kijasho chembamba kikaanza kumtoka. Bila kuongea jambo aliinuka na kuondoka huku kichwani mwake akiwa na mawazo mengi sana kwa sababu amemueleza mambo mengi sana ambaya alitka kuyafanya kabla ya kumaliza wakati wake kama waziri mkuu.

 


Kwa upande wa Alwin na Miryam mapenzi yalinoga sana, muda mwingi walikuwa pamoja huku wakibadilishana mawazo na hasa wakipanga maisha yao ya ndoa yatakuwaje. Jestina hasira ziliongezeka na kujikuta akitamani kuuwa hata mchana. Alipoona hali imezidi kuwa mbaya aliamua kufunga safari na ya kurudi katika ulimwengu wa watu waliodhulumiwa. "nilitarajia utarudi tu" aliongea malikia baada kumuona Jestina, "tokea nguvu ziongezeka huwa napata hamu ya kuuwa sana" aliongea Jestina. "hio ni dalili ya kuwa muda wako kukaa duniani unakwenda ukingoni" aliongea malikia na kumshangaza Jestina. "unasema nini" aliuliza Jestina, "ndio, mpaka sasa umebakia na siku tano tu" alijibu malikia. "hauwezi kuongezeka muda" aliuliza tena, "haiwezekani hata kidogo, kwa sababu muda wako wakuwepo katika ulmwengu huu pia umekwisha, unatakiwa kuondoka na urudi kwa muumba wako" aliongea malikia na alionekana kama hatanii hata kidogo. Baada ya kusikia hivo aliaga na kuondoka zake. Alirudi duniani hukua akitafakari jinsi ya kuwamaliza waliobakia hasa Matt ambae yupo nje ya mji. Na ukizingatia yeye hawezi kutoka nje mji huo, alihisi kama mpaka ataondoka hatokamilisha kazi yake. Kilichomuuma zaidi ni pale alipokumbuka kuwa Adui yake mkubwa alikuwa hayupo katika mji huo.

**********************************************

 Siku mbili zilipita na mauaji yalizidi sasa, kwa siku aliuwa watu zaidi ya wanne, Watu walizidi kulalamika kutokana na mauaji hayo lakini kumkamata ni jambo ambalo lilkuwa haliwezekani. Alipoona zimebakia siku tatu ndipo likamjia wazo, aliamua kwenda kwa waziri na kumuingia mwilini na kumtia kama ugonjwa hivi. Hali ya waziri ilikuwa mbaya sana, aliwahishwa hospitali kwaajili ya matibabu lakini haikusaidia, Alipoona anakaribia mwisho wake akaamuru Matt apigiwe simu na kupewa taarifa hizo jambo ambalo lilitekelezwa haraka sana. Ndani ya masaa kumi baada kupigiwa simu Matt aliwasili Mashvile na moja kwa moja alikwenda hospitali kwaajili ya kumjulia hali baba yake. Masikini hakujua kama amerudi kuja kukifata kifo chake "vipi hali yako baba" aliuliza "ndio kama unavyoiyona mwanangu" alijibu kwa tabu sana. Mwili wake ulivimba na kupata vidonda vingi sana ambavo vilitoa harufu na damu. Jestiina baada kuona windo lake limerudi alisubiri mpaka usiku na kutoka katika mwili wa waziri mkuu, usiku huo alikwenda kuwamaliza waliobakia ili abakie na Matt tu.

 


Siku iliofuata Matt alikwenda hospitali kumuona baba yake, lakini alipofika alishangaa kuona vidonda vimeanza kupungua na akaambiwa kuwa hali ya mheshimiwa inazidi kuwa nzuri na huenda muda si mrefu akeuhusiwa kurudi nyumbani. Mapenzi yalizidi kunoga kati ya Alwin na Miryam na kutokana na kuwa walikuwa ni watoto wa familia zenye uwezo mkubwa kifedha. Walinunua jumba moja kubwa sana na la kisasa, taratibu walianza kuweka vitu huku wakionekana ni wenye furaha sana. Mtu yeyote aliewaona aliweza kuiona furaha hiyo kupitia macho ya wawili hao. Jestina alikuwa kaishuhudia yote hayo na alionekana kufurahi sana, jioni ya siku hiyo aliwatokea kina Alwin na kuomba kuongea nao.


"najua mupo katika kipindi cha maandalizi ya ndoa lakini naomba dakika kadhaa tu mnisikilize" aliongea Jestina.

"sawa hakuna shida" Alijibu Alwin

"muda wangu wa kukaa katika dunia umekwisha"

"unamaanisha nini" aliuliza Miryam

"namaanisha kuwa muda si mrefu nitawaacha niende nnapostahiki kuwepo

"mbona mapema" aliongea tena Miryam kwa unyonge zaidi

"na vipi kuhusu Matt" aliuliza Alwin

"Matt siku yake ishafika" alijibu Jestina akionekana kupandwa na hasira

"Dah sawa ila tunatamani ungeendelea kuwepo" aliongea Alwin

"Hata mimi pia natamani ingekuwa hivyo lakini ni jambo ambalo haliwezi kutokea kumbuka mimi nilishaakufa muda mrefu sana" aliongea Jestina na kuwaaga "nakwenda kutimiza kilichonileta duniani" aliongea na kutoweka.

 


Kwa bahati nzuri usiku huohuo waziri mkuu aliruhusiwa na kurudi nyumbani, ama kweli siku hiyo illikuwa ni ya furaha sana kwa Matt baada kumuona baba yake akiingia nyumbani. "karibu baba" aliongea Matt na kumkumbatia mzee wake. Walifanya kasherehe kadogo cha kushukuru, usiku huo waliongea mengi sana mpaka waliporidhika kila mtu aliingia chumbani kwake kwaajili ya kupimzika.

 


Matt alikwenda chooni na kujimwagia maji na kurudi chumbani, "home sweet home" alijisemea na kuachia tabasamu. Alipanda kitandani kwaajili ya mapumziko, ghafla hali ya hewa chumbani ikaana kubadilika. Alianza kuhisi kama kuna mtu ndani ya chumba hicho lakini kila alipoangaza huku na kule hakuona mtu akajipa moyo "labda ni mawazo tu". "Matt" aliskia jina likiitwa, alishtuka na kuwasha taa lakini hakuona mtu yoyote, "Matt kwanini" aliskia tena sauti na kwa wakati mshale wa hatari ukagonga kichwani mwake. "mbona hii" sauti kama naijua hivi", "ndio unaijua" yeye alijisemea moyoni lakini lishangaa kujibiwa. "hahaha Matt mpenzi wangu" alisikia kicheko na maneno hayo, alianza kuhisi kuchanganyikiwa. Alikurupuka kitandani na kukimbilia mlangoni lakini cha ajabu hakuona mlango, "unakwenda wapi unadhani" alisikia tena na wakati huu moja kwa moja akaitambua sauti hiyo kuwa ni ya Jestina. "haiwezekani hata kidogo" alisema kwa nguvu kidogo, "kwanini isiwezekane we ulidhani utanifanyiwa unyama ule halafu uendelee kuponda raha za dunia bila kuadhibiwa" alijiu Jestina na kumpitia Matt kwa nyuma,Matt aligeuka lakini hakuona kitu. Alijaribu kila njia kutoka ndani ya chuma chake lakini juhudi zake ziligonga mwamba, alianza kupiga kelele kwa nguvu "hazitakusaidia hizo" aliongea Jestina na kumpitia mbele kwa kasi ya ajabu sana na kupiga kikumbo kilichomtupa huko. "Jestina tafadahali nisamehe" aliongea Matt huku akijifuta damu zilizokuwa zikitoka puani, "wewe mbona hukuniachia nilipokwambia uniache" aliongea Jestina na kupiga kofi zito la mgongo. "nakufaa, Jestina nisamehe mpenzi wangu" yalimtoka maneno hayo Matt bila kutarajia. "nyooo nani mpenzi wako, kweli mtu anaweza kumbaka mpenzi wake na kisha kuwaambia marafiki zake wajisevie" aliongea Jestina na kumtokea mbele katika umbile la kutisha sana. "nakubali nimekosa nisamehe maana hata mungu anasamehe" aliongea Matt huku akipiga magoti akionyesha kuomba msamaha, "leo unamkumbuka mungu wakati unanibaka ulikuwa hujui kama kuna mungu wa kuogopa" alijibu Jestina na kumkaba kooni ghafla akatoweka nae na kutokea katika kaburi lake. "siku ile si ulinifanya kwa nguvu bila mimi kutaka, sasa leo nataka tufanye tena kwa ridhaa yangu" aliongea Jestina na papo hapo nguo zake zikachonyoka mwilini na kumuacha akiwa uchi. Kwa kweli mwili wake ulitisha sana, ulipambwa na vidonda vilivokuwa vinatoka damu na usaha mwingi sana. Pia ulitawaliwa na funza wengi sana kiasi cha kumfanya aonekana kama kaota nyasi mwilini, "sasa ole wako ushindwe kufanya ulichokifanya siku ile" aliongea Jestina huku akimfata Matt ambae wakati huo alikuwa akijaribu kutafuta njia ya kukimbia lakini kutokana na kiza hakufanikiwa. "Jestina nisamehe......nisamehe sitarudia tena" aliendelea kuongea Matt ambae alikuwa akiishika suruali yake ili isivuke lakini wapi ilichojoka katika mazingira ya kutatanisha. "siku ile si uliona raha kunidhalilisha tena kwa kujifanya kidume na kuwaalika wenzako wanifanyie uchafu" alizidi kuongea Jestina wakati huu tayari alikuwa kashamlaza Matt chini. Kila damu zilipomdondokea Matt alipiga kelele kuashiria kuwa alikuwa akipata maumivu makali sana, na kila ilipondokea damu palifoka moshi. Katika hali ya kawaida hata uwe rijali vipi lakini katika hali kama hio uume hauwezi simama. 

 


Jestina aliuangalia uume wa Matt na papo hapo ulisimama na bila kupoteza muda aliukalia. Matt alianza kupiga kelele kwa nguvu huku akijaribu kumtoa lakini wapi ilikuwa ni sawa na kutaka kuuhamisha ukuta. Jestina alinyanyuka huku uume wa Matt ukionekana kuungua sana, alimnyanyua kwa nguvu na kumrusha katika mti. Kabla hajakaa sawa alimnyanyua na kumning'niza katika mti. "nataka uyahisi maumivu nilioyapata mimi wakati ule na pengine utayapata zaidi ya yale" zilitoka kucha ndefu mkononi, zilikuwa zimechongeka sana na zilikuwa ngumu mithili ya chum. Taratibu alizunguka nyuma na kumchoma chini shingo na kuanza kuteremsha mkono chini kama vile anachuna ngozi ya mnyama. Maumivu yalikuwa makali sana kiasi cha kama ingekuwa anafanyiwa na mu wa kawaida angekuwa kashaazimia tayari lakini halikutokea hilo. Matt alipiga kelele sana akiomba msaada lakini wapi hakukuwa na yoyote wa kumsaidia. Jestina aliendelea kumchanja mgongoni mpaka mgongo wote ulirowa damu, baada ya hapo alimgeukia mbele na sura yake ilizidi kuwa mbaya. "kama ungenisikiliza siku ile tusingefika hapa leo" aliongea Jestina huku machozi ya damu yakimtoka. Alimshika kichwa na kumfungua mdomo kisha akamtemea kitu kama makohoo hivi na kumfunga mdomo na pua jambo ambalo lilimfanya ameze bila kutaka. "tutakutana kuzimu huko" aliongea Jestina kutoweka eneo hilo, ghafla Matt alianza kutapika damu nzito ikiamatana usaha pamoja na funza.

 


"Alwin nimekuja hapa kukuaga kwani muda wangu wa kuwepo hapa umekwisha" aliongea Jestina baada kumtokea Alwin, "tutakumis sana kwa kweli" aliongea Alwin huku machozi yakimtoka. "utanisahau tu, nina imani Miryam atakufanya uwe mume bora kabisa" aliongea Jestina huku akianza kutoweka taratibu, "utarudi kama mwanangu" aliongea Alwin huku akipunga mkono. Mwisho kabisa Jestina alitoweka kabisa, "nenda kwa amani Jestina" aliongea Alwin huku akitabasamu. Asubuhi mapema televisheni zote zilitangaza kifo cha Matt ambae alikutwa ametapika mpaka utumbo, habari hiyo ilipelekea waziri mkuu kupata shimikizo la damu lilisababisha kifo chake.

*************************************

 


Mwezi mmoja sasa umepita na hakukuripotiwa mauaji yoyote yale, na hali ya amani ilirudi katika mji wa Mashvile. Harusi ya Alwin na Miryam ndio iliopmba vichwa vya magazeti huku kila mtu akialikwa kuhudguria harusi hiyo.

"bwana Alwin umekubali kuishi na Ms Miryam kama mke wako halali wa ndoa katika dhiki na faraja"

"nimekubali"

"Ms Miryam Alexander umekubali kumpokea bwana Alwin Kelvin kama mume wako halali wa ndoa katika dhiki na faraja"

"nimekubali"

"unaweza kumbusu bibi harusi" 

Hapo Alwin alimsogelea Miryam na kumbusu, ukumbi mzima ulisimama na kuashangilia. Jioni yake ilifanyika sherehe kubwa sana huku watu kadhaa wakuwa wakuhudhuria ghafla hiyo. 


"Alwin mwanangu akirudi nyumbani na kipele tu utawajibika" aliongea Profesa na kugonga glass na Alwin. "ah usijali, hata mbu akimgusa mke wangu atawajibika kama walivowajibika wengine" alijibu Alwin  na kutabasamu kidogo. Sherehe ilimalizika na maharusu hao wakapelekwa nyumbani kwao, usiku huo ulikuwa ni usiku wa pekee kwa wapenda nao hao. Ulikuwa ni kihistoria katika mapenzi yao, mapenzi yalinoga kupita maelezo, baada ya muda walikwenda hospitali na majibu yalikuwa mazuri sana. Tayari Miryam alishaabeba mimba, ilikuwa furaha kubwa sana kwa familia hiyo ya wazazi vijana. Miezi ilikatika na hatimae mwezi wa kijufungua ulifika, na Mungu aliitika kilio chao. Mtoto wao wa kwanza alikuwa ni mwanamke na kama walivyokubaliana walimpa Jina la JESTINA. Baada kuruhusiwa kutoka hospitali, moja kwa moja walikwenda wazazi wa Jestina kwa ajili ya utambulisho rasmi wa Jestina mdogo. 

 


Wazee hao ambao tabasamu lao lilipotea baada kuondokewa na mtoto wao wa pekee lilirudi baada kupewa mtot huyo wambebe. Walishindwa kujizuia, machozi yaliana kuwatiririka kwa furaha, "ama kweli Mungu ndie mjua kila kitu, na hakutokei kitu isipokuwa kuna sababu nyuma yake. Umeona mke wangu Mungu kamchukua Jestina wetu ili amlinde aibu kwa walimwengu lakini angalia sasa ametupa watoto wengine wawili na mjukuu juu" Aliongea Mr Hendrix huku akimwangalia mkewe ambae sura yake baada muda mrefu kupoteza tabasamu sasa limerudi upya. "wanangu mukihitaji msaada wowote ule iwe ni ushauri au jambo lolote lile msisite kutuambia, na msiache kutulea mjukuu wetu tumuone" Aliingea mke wa Mr Hendrix.

******************************************


IN GOD WE TRUST

MWISHO

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.