NGOJA NILEWE 2

NGOJA NILEWE 2

MTUNZI: Mbogo Edgar

WHATSAPP 0743632247 


ILIPOISHIA 1: “jamani, huyu kaka anahatari” alijisemea Venesa kimoyo moyo, “angenibaka usiku sijuwi kama ninge umia” aliwaza Vanesa huku anatabasamu peke yake, “sema tu nashukuru ni mstaarab” alijisema Vanesa huku anageuka kutazama upande wa vyumbani, ambako sasa palisikika vishindo vikija sebuleni, “samahani dada yangu, sikufunga mlango, yani sikuwa na wazo kama bado hupo hapa, nilijuwa umesha ondoka” alisema Sebastian, ambae sasa alikuwa amevaa truck na tishert, chini alivaa viatu vya wazi, yani sendo, “nilienda nyumbani, lakini nimekuta wameniibia, ela yangu ya nauri” alisema Vanesa kwa sauti ambayo ilikuwa inakaribia kuangua kilio. ,…… . ENDELEA……..


Sebastian akatazama sanduku la Vanesa, nakuona jinsi lilivyo vunjwa sehemu ile ya kufuri, yenye namba za siri, “dah! Pole sana, sasa unafanyaje?” aliuliza Sebastian, na hapo mwana dada huyu akaeleza shida yake kwa Sebastian, “naomba niweke mizigo yangu hapa, niazime elfu moja, nikanunue card nipige simu kwa baba, anitumie nauri nyingine, alisema Vanesa, na hapo Sebastian akakubaliana nae moja kwa moja, “akunashida, na kuhusu card ninayo hapa inaunity hamsini, najuwa uwezi kumaliza” alisema Sebastian na hapo kidogo Vanesa akatabasamu.********


Naam! Vanesa aliondoka nyumbani kwa Sebastian, akiwa ameacha mizogo yake pale, alijuwa fika kuwa, lazima siku ile angelala kwa kijana huyu, sababu lazima fedha angetumiwa baadae muda ukiwa umeshaenda sana, ata hivyo alipanga akapige simu kwanza kisha ndio arudi kuja kuoga, kabla ajaenda mjini kuchukuwa fedha, atakazo tumiwa.


Sijuwi ni nani alie semaga kuwa, mipango siyo matumizi, maana ni neno la kweli kabisaaa, ebu angalia, Vanesa alipoenda kupiga simu, ilipokelewa na dada yao wakazi huko nyumbani kwao, na mbaya Zaidi ni kwamba, alipowaulizia wazazi wake, alielezwa kuwa wametembelea shamba lao lililoo nje ya mji, na kikawaida wanapofanya safari kama hiyo, uwa wanatumia week end nzima, kwahiyo wangerudi jumapili jioni, na muda huo lazima watakuwa wamesha chelewa muda wa kutuma fedha hivyo lazima yeye angetumiwa, kesho kutwa jumatatu, na kusafiri juma nne, “kwahiyo sikuzote nitakaa kwa huyu kaka jamani” alijiuliza Vanesa akiwa njiani anarudi nyumbani wa Sebastian, “sasa navile nilivyo lala jana usiku nikilala tena vile sinitakuta amesha ingiz….” Aliwaza mwana dada huyu, ambae alijiwazia njia nzima, mpaka anaingia nyumbani kwa Sebastian, akiwa na sura ya uzuni, na kumkuta mwenyeji wake, anaandaa supu ya kuku, aliyotoka kuinunua kwenye kimgahawa cha jilani.


Vanesa alimsumulia Sebastian kilicho tokea, kwa sauti ya kukata tamaa, maana juma pili ndiyo siku ambayo angeweza kuwasilina na wazazi wake, wazo ni kwamba ataishije kwa siku hizi mbili, hapa jijini dar es salaam, “usijari dada yangu, sitapenda nikuona ukiwa katika hali hii, nita kupatia fedha, unazo itaji, uweze kufika nyumbani kwa wazazi wako” alisema Sebastian, ambae kiukweli alijaliwa moyo wa kusaidia wenzake, kwasauti iliyojaa urafiki kubwa.


Ukweli Vanesa akuamini alicho kisikia, japo kwa upande mwingine alihisi kuwa, kijana huyu, anaweza kuwa anafanya vile kwa nia ya kupata bumunda, yani kitumbua, au kile kitu kinachofanan na jina la samaki mkubwa mwenye upanga wa baharini, yani samaki papa, “jamani kaka yangu, asante sana, basi utanipa anuani yako ya poster, nikipata ela nikurudishie” alisema Vanesa, kwasauti yenye kujawa na furaha kubwa, “hapana dada yangu, una aja ya kuchukuwa anuani yangu, nakusaidia tu, wala usiwe na wasi wasi” alisema Sebastian, na hapo Vanesa alianza kuhisi mapigo ya moyo yanaenda mbio, kwamba leo lazima akeshe na mwiko chunguni, aki kwa kujuwa kuwa msaada wa kijana huyu, aukuwa na lengo la kurudishiwa, ila ni lengo la kuonja kitumbua chake, “kwanini kaka, nitakurudishia wala usiwe na wasi wasi, wazazi wangu wanauwezo wakulipa ela hiyo, hisitoshe na mimi naenda kusimamia biashara yangu” alisema Vanesa, ambae ni mwanafunzi wa chuo cha biashara na usimamizi wa fedha, “dada ebu achana na hizo, mimi nimeamua kukusaidia tu uwezi kujuwa kesho utanisaidia nini, alafu isitoshe natumia fedha ngapi kununua wine kila week end, ebu kaa hapo tupate supu uwai ndege” alisema Sebastian, na kumshangaza zaidi Vanesa, ambae alitegemea kuambiwa, kuwa alale hapa kwa usiku mmoja ili alipie fedha atakayopewa, ambayo isngepungua elfu sitini.*******


Naam! mwanadada Vanesa anaingia bafuni kuoga, huku bado ana aamini kama kweli msaada aliopewa, ni wabule, “hivi akitaka nita wezaje kukataa?” anawaza Vanesa huku anaoga, kichwani mwake anahisi muda wowote angemwona kijana wetu akiingia bafuni na kudai kitumbua, “yani wakina Stellah, sito kuja kuwasamehe ata kidogo, yani wanasababisha leo nafanywa kwaajili ya ela” aliwaza Vanesa, ambae mpaka anamaliza kuoga , akumwona yule jamaa akiingia bafuni wala chumbani, “pengine alikuwa anasubiri nimalize kuoga” aliwaza Vanesa, ambae akuamini macho yake, maana mpaka anamaliza kuvaa nguo ya mwisho, kijana alikuwa ametulia zake sebuleni.


 Vanesa anatoka chumbani akiwa amesha jiandaa kwa safari, huku anawaza kuwa, muda wowote atadaiwa malipo ya msaada aliopewa, maana ata yeye alifahamu uzuri allionao, ambao unatamanisha watu wanaume wengi sana, ukiachialia wanaume wa shuleni chuoni ata walimu, pia walikuwepo ata wanaume watu wazima, ambao wengine ni marafiki wakaribu wa wazazi wake, na wengine ni waume wa shamngazi zake au waume wa mama zake wadogo, lakini ilikuwa tofauti kwa kijana huyu, ambae kiukweli yeye kwa  lakini mpaka dakika hii, kijana Sebastian wala aonyeshi ata dalili ya kumwuliza jina, au kuuliza anaelekea mkoa gani, na kwamba akimwitaji ata mpataje.


Muda wa kuondoka unapofika, Sebastian anampatia fedha Vanesa na kumsindikiza mpaka kivukoni, ambako anamkodia taxi, wanaagana, pasipo kuitaji chochote toka kwake, ilimshangaza sana Vanase ambae anakaa na mwanaume masaa zaidi ya kumi na mbili, pasipo kutongozwa, “asante sana kaka yangu, asante kwa msasaada wako, asante kwa usiku wa jana, umenitunzia heshima, naamini akuna jema linaloenda bule, hipo siku mungu ata kulipa, na ninaomba akulipe kwa kwa kuitia mimi mwenyewe” alisema Vanesa wakati wanaagana, na kuondoka zake, huku kichwani akijiuliza kwamba huyu kijana ni mstaarabu, au anamatatizo katika uanaume wake.********


Naaaam hiii ilichukuwa miezi minne kwa Sebastian kumsahau mwanamke huyu, nae kuendelea kuishi kama alivyokuwa akifanya mwanzo, anafanya kazi week nzima, kisha week end anatulia nyumbani na wine yake na nyama choma, huku mala kwa mala akimsaidia mama yake, ambae kwa sasa alikuwa na maisha mazuri, japo siyo kama mwanzo, lakini alikuwa katika hali ya mwonekano wa mama mwenye mtotowake anafanya kazi.


Yaap miezi sita baadae, Sebastian anapata nyumba huko kibamba kwa mangi, nyumba ambayo ilikuwa inauzwa na mfanyakazi mmoja wa serikali, alie amishiwa mkoani shinyanga, bahati nzuri, bei yake ilikuwa lahisi kidogo, million moja, na lakini moja naelfu hamsini, kwa msaada wa mmilikiwa wa kiwanda, Sebastian akapewa fedha alizo takiwa kulipwa kodi ya mezi sita, ambayo kiasi chake ni laki mbili kwa mwezi, ikiwa na jumla ya million moja na lakimbili, ambayo alitumia kununulia nyumba na kukodi gari la hamisha mizigo, kuelekea kibamba kwa mangi, ambako alianza maisha mapya, na katika nyumba yake kubwa ya vyumba vinnei.

Yaap miezi sita baadae, Sebastian anapata nyumba huko kibamba kwa mangi, nyumba ambayo ilikuwa inauzwa na mfanyakazi mmoja wa serikali, alie amishiwa mkoani shinyanga, bahati nzuri, bei yake ilikuwa lahisi kidogo, million moja, na lakini moja naelfu hamsini, kwa msaada wa mmilikiwa wa kiwanda, Sebastian akapewa fedha alizo takiwa kulipwa kodi ya mezi sita, ambayo kiasi chake ni laki mbili kwa mwezi, ikiwa na jumla ya million moja na lakimbili, ambayo alitumia kununulia nyumba na kukodi gari la hamisha mizigo, kuelekea kibamba kwa mangi, ambako alianza maisha mapya, na katika nyumba yake kubwa ya vyumba vinne. . ,…… . ENDELEA……..


Changamoto iliyo fwatia ni usafiri, ambayo aliimaliza miezi mitatu baadae, kwakununua gari dogo aina ya Suzuki escudo, toka kwa mtu ambae alikuwa na uitaji wa fedha, hapo safari za kigamboni zikawa lahisi sana kwake, huku maisha yakiendelea kumyookea kwa kile alicho kiamini kuwa, Baraka na maombi ya mama yake, ambae mala zote alikuwa aachi kumkumbuka kwa kumtumia fedha, na maitaji mbali mbali, japo akusahau ndugu, kama vile mama yake mkubwa, na watoto wake, yani wakina George.


Lakini licha ya hayo yote, Sebastian alizidi kujipenda, kama ilivyo tabia yake toka udogoni, kitu ambacho kilifanya wanawake wa mtaa huo, waanze kujipitisha mbele yake, huku wakifanya mbwe mbwe za kila namna, ilikijana wetu aingie mtegoni, kwa lengo la kumpata kimapenzi kijana huyu, ambae akuiacha ile ratiba yake ya week end, yani kunywa pombe siku za ijumaa na jumamosi, huku akichoma nyama kama ilivyo kawaida yake.*******


Naaam ilikuwa ijumaa moja, mida ya saa mbili usiku, mitaa ya kibamba kwa mangi, maeneo ya magengeni, anaonekana mwanadada mmoja mwenye umbo la wastani, yani siyo mnene sana wala uwezi kumwita mwembamba, ila kitu ambacho unawezza kusema ni mzuri wa kuvutia, japo alionekana kuwa katika mazingira ya kawaida, yani mavazi yake yalimtambulisha kuwa, alikuwa na maisha ya chini, japo alikuwa msafi, akiwa amesimama kiunyonge, mbele ya genge moja, kati ya mmengi ya sokoni hapo, linalo uza mboga mboga na vyakula, yani kama vile ndizi za aina mbali mbali, viazi mvilingo, nyanya vitunguu karoti oho, na vitu kama hivyo, “kaka Baraka, yani nyumbani hatuna chochote cha kula, shemeji amesema kesho akirudi kazini takupishia ela yako” alisema yule dada kwa sauti ya kubembeleza, inayotia huruma, “sikia shemeji, Philipo mimi namjuwa, mala kibao amesha sema hivyo alafu anapiga kimya, mpaka sasa namdai elfu alobaini, alafu unataka niongeze tena deni” alisema kijana alie kaa kwenye mauzio ya lile genge, alie itwa Baraka, “jamani kaka yangu, namba utusaidie, yani toka tumekunywa uji asubuhi, atuja la chochote” alisema yule mwanamke kwa sauti ile ile yenye kutia huruma.


Naam wakati wanaendelea na maongezi yale ambayo kiukweli aya kuwa na matumaini ya kufanikiwa, mala kuna mtu akaingilia maongezi yao, “Baraka ebu nihudumie, alafu tuone tunamsaidiaje huyu dada” ilikuwa ni sauti ya kiume toka pembeni ya yule dada, wote wakageuka, wanamwona kijana alie valia katula ya kaki, na tishert jepesi, huku miguuni akiwa amevalia sendo za ngozi, ukweli ni kwamba, dada huyu amfahamu kabisa kijana huyu, “karibu braza seba, naona leo umerudi mapema” alisema Baraka, ambae ni wazi anamfahamu kijana huyu, siunajuwa tena atuna cha ngoja huko mjini” alisema yule kijana ambae ndie Sebastian, huku anasogea karibu na meza ya biashara, pasipo kumtazama yule mwanamke, “haaaa! bro siuseme mambo ya week end yanaanza” alisema Baraka, kwa sauti yenye utani, “kama kawaida, lazima tuiweke sawa week end” alisema Sebastian, huku huku anatazama tazama kwenye meza iliyojaa bidhaa.


Wakati maongezi ya Baraka na Sebastian yanaendelea, yule mwanamke alikuwa anamtazama Sebastian kwa macho ya kumtathmini au kujadiri, kwamba ni nani na anataka amsaidie kivipi, “kwahiyo kama kawaida mzuzu au leo umebadiri pigo” aliuliza Baraka huku anachukuwa mfuko, “kama kawaida, sema leo niwekee na vitu vya kachumbali, yani limao, nyanya, pili pili na vutunguu” alisema Sebastian ambae mpaka hapo akuwa amemtazama huyu dada usoni, japo dada alikuwa anamtazama sana Seba.


Mwanamke yule anamtazama yule kijana, ambae mwonekano wake, ni mtu alie lizika na maisha yake, na kwamba akuwa na shida ndogo ndogo, ila katika maongezi yake, akuonyesha kuwa na dalili ya malingo, wala majigambo, ata Baraka anapo maliza kumfungashia mazaga yake, kijana anatoa noti moja ya elfu mbili, ambayo inalipia zile ndizi na vitu vingine vyote, na mia mbili hamsini ikabakia, mwanamke huyu anatamani kama vile angepewa ile chenji, ili anunue kitu kitakacho wafaa yeye na ndugu zake huko nyumbani, “vipi bro  leo ujaja na gari?” aliuliza Baraka, “haaa kaka, yani hapa tu, nije na gari?” anauliza Sebastian, kwa namna ya  kuona kama Baraka anamwona mpenda magari, lakini ilikuwa katika utani, wote wanacheka.


Seba anageuka kwa kutaka kuondoka, lakini anamwona yule dada akiwa bado amesimama, “hoooo! nilimsahau dada” alisema Sebastian, huku anatoa wallet yake toka mfukoni, na kuifungua, kisha anatoa noti mbili za elfu mbili mbili, na kumpatia yule dada, ambae anatoa macho kwa mshangao, anatazama yule kaka, kama kweli anampatia ile fedha, au anatania, anaomwona kuwa ni kweli anampatia, dada anamtazama Seba usoni, kuona kama ni kweli anatoa msaada au anamacho yenye tamaa juu yake ndio maana ametoa fedha ile, ambayo kwa kipindi kile cha miaka ya tisini, ilikuwa ni fedha kubwa kidogo, “asante sana kaka yangu, ubarikiwe sana, kaka yangu” alisema yule dada huku anapokea ile fedha, ubarikiwe na wewe dada yangu” alisema Sebastian kisha akaaga na kuondoka zake, huku yule dada namsindikiza kwa macho, mpaka alipotoweka, nayeye akaanza kutembea kuelekea upande wa madukani, “Adellah, mbona unaondoka sasa, unaona mambo yako, ukiwa na shida unakuja kwangu, ikiwa na ela unaenda kwingine” alisema Baraka kwa kulalamika, lakini yule mwanamke akumjari kabisa, zaidi mawazo yake yalikuwa ni kwenda kununua mchele mafuta na samaki, kisha arudi kuja kununua nyanya na viungo vingine, ili usiku huu, wakale chakula kizito kidogo, tofauti na viazi alivyotaka kuazima kwa Baraka, alinunua maandazi manne na kulila moja, huku mengine matatu, akiyafunga vizuri kwaajili ya kuyapeleka nyumbani, ili wenzake wakapooze njaa, wakati wanaangaika mapishi, kisha akaanza kutembea kurudu nyumbani, huku njia nzima akiwa aamini kilichotokea usiku ule, alijikuta anampenda ghafla kijana yule.*********


Huyo anaitwa Adellah, ni mtoto wa tatu wa mzee Mwakafwila, anamwezi wapili sasa, toka afike hapa jijini Dar es salaam, akitokea wilaya ya Lungwe mashaliki, ambayo sasa hivi inaitwa busokero, kijiji cha Lufilyo, huko mkoani Mbeya, akiwa amekuja kwa dada yake Sophia, alie olewa na kijana Philipo Mazengo, mwenyeji wa mkoa wa Dodoma


Itaendelea


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.