Siku Isiyo na Jina 9

SIKU ISIYO NA JINA
Na: Emmanuel Charo 
WhatsApp: +254796273110

SEHEMU YA 9
Ilipoishia sehemu ya 8

"Unaiona hii" Abdul alimuonyesha kalamu Angel, Angel alishangaa kuona kalamu aliyokabidhiwa ni Joan ipo mikononi mwa Abdul, hakuamini kwa Kasi ya ajabu aliinuka na kuufikia mkoba wake na kufurukuta cha kushangaza akaikuta kalamu ile ipo salama salimini.
"Wow the show is about to begin" alisema Abdul baada ya kuona Angel pia yuko na ile kalamu.

Endelea

Sehemu ya tisa

"Kumbe uko nayo pia wewe"
Angel alibaki kimya na kurudi pale alipokuwa amekaa
"Tuache haya ya kalamu, kilichobaki ni ufahamu ukweli, ukweli ambao wewe utaniamini uhakika lakini, Manu hataweza kuelewa. Hivyo Angel nikimaliza mkasa huu ikiwa Manu hajafika hapa na kuniua fanya hima umueleze ukweli 
"Umesema sitaamini na nitajutia kumfahamu Manu, wewe tena unasema nitaamini!"
"Yap Manu ananitazama kama adui wake, yeye anajua upande tu mmoja bahati ilikuwa upande wangu nikafahamu pande zote mbili za mtu anaitwa Romeo"
"Romeo ndio nani?"
"Utamujua na huyo ndio utamuchukia ikiwa una akili timamu"
"Umeongea mengi ambayo hayana mantiki hebu nambie Manu ni nani pia mmmh lakini anza na wewe. Wewe ni nani?
"Usijali utajua mimi ni nani"

Abdul anaanza kumusumulia Angel.

"Mwaka ni elfu mbili kumi na tisa nchini Japan. Mwaka huo ndio maisha halisi yake pia yangu yaliisha. Acha nikwambie hivi 
'Ni siku ya mwisho ya uhalisia maishani mwake, ni siku ya mwisho kuishi katika maisha ya ulimwengu huru na kuishi kwenye ulimwengu wa ndoto. Kila siku akilala au kufanya jambo lolote anadhani atazinduka na kukuta siku ni ya ishirini na tano mwezi ni wa oktoba mwaka wa elfu mbili na kumi na Tisa, na aendelee na maisha yake ya kawaida.
Lakini sivyo siku zinaenda lakini kwake ni kama ndoto haamini kila jambo linalofanyika mbele ya macho yake Yuko katika ulimwengu wake kivyake akiwa anamatarajio ipo siku atazinduka na kujikuta yuko siku ile; siku hiyo si nyingine bali ni siku ya ishirini na tano mwezi ni wa kumi mwaka wa elfu mbili kumi na tisa.
Ni ndoto yake kuwa ndoto hiyo itaisha'

Ndoto yake ya kuamka kuishi kawaida ni yeye kujuwa hasa adui anayepigana naye. Hicho ndicho kitu Manu hajui adui yake hasa ni nani?
"Unazunguka sana Abdul"
"Acha papara mrembo"
"Muongo huwa na maneno mengi, unaniongopea?"
"Mimi na Manu tulikuwa marafiki wa kufa kuzikana"
Abdul alisema huku akimuangalia Angel kisha alishusha pumzi ndefu. Nakuanza kumusumulia Angel.

Ilimuchukua saa tatu, hadi anamalizia kueleza upande wake Abdul. 
Abdul alikuwa ameinamisha kichwa akisubiri neno toka Kwa Angel lakini ukimya ulitawala, alinua kichwa chake lakini Kwa umbali wa sentimita mbili tu utosi wake uligusana na kitu kigumu na baridi
'bastola' aliwaza 
"Abdul ni mwaka wa ngapi unanifutilia?" Aliuliza swali Angel
Alijaribu kujiinua lakini Angel aligandamiza ile bastola kichwani mwake
"Inaonekana unajua mengi kunihusu lakini mbona hata robo hujaifikia" kisha Angel aliangua kicheko cha kebehi.
Abdul alibaki kimya, akipiga hesabu jinsi ya kujinasua
Angel naye alitawala upande wa kuzungumza, kwa mara ya kwanza alishika upande wa upini wa kisu hiki.
"Ama ni yule kiumbe zaifu anayejifanya Ninja ndio kakutuma unipeleleze?"

Ghafla Abdul aliinuka na kuupiga teke mkono uliokamata bastola na kubingirika akielekea mlangoni, aliufikia mlango na kuupapasa mfuko wa shati lake akagundua ufunguo hana, aligeuka 
"Dah!" Ulimtoka ukemi
Angel alikuwa amesimama amekamata bastola kama si Yule aliepigwa teke zito, vilivyo huku mkono mwengine ukiizungusha funguo Kwa madaha
"Unaitafuta hii" alimuonyesha ile funguo
Angel alimurushia funguo ile Abdul 
Abdul hakugundua janja ya kurushiwa funguo ile macho yake aliyaelekeza Kwa funguo ile hadi funguo inamfikia Angel pia alikuwa mbele yake. Hakuamini macho yake ndani ya nukta tano Abdul alikuwa amefungwa kamba mwili mzima

'Hivi huyu bastola kaitoa wapi, hizi kamba nazo duh acha ni sikurupuke maana yuko makini tofauti nilivyoelezwa' aliwaza Abdul
'mbona hata sikutegemea haya, mbona pia mwili wangu umekuwa dhaifu kiasi hiki itakuwa ni mwanga huyu msichana si bure'
'dah Abdul mie nimeshikwa kike tena na mwanamke'
'itakuwa Manu amemfunza mbinu hizi maana kila kitu anachofanya hakuna tofauti anavyofanya Manu akiwa mbele ya adui wake'
'lakini Manu naye inaonekana hajatambua upande wa pili wa huyu anayemuita malaika'
'ndio maana akaniuliza kama Manu amenituma'
'lakini dah mbona ajiingize upande huo msichana mrembo kama huyu duh! Kweli dunia imefika mwisho maana hizi ndio dalili dunia kuisha'
'namuonea huruma Manu maana hata nikamwambia hatoniamini hata kunisikiza hawezi'
Abdul aliwaza hayo yote 
Aliamua kuvunja ukimya 
"Angel jitoe Kwa hiyo cult ndugu yangu, you are a girl and you I'll remain to be" 
"Kaa kimya msenge wewe" 
'dah kumbe anaweza kutoa kauli chafu kama hii' 

******
"Hivi, huyu ndio Abdul tulo onywa tusimfuatilie atatua" Ngamba aliuliza wale wenzake 
Watatu hawa walikuwa wamejituliza chumbani mwao ndani ya hoteli ile ile waliofikia akina Abdul.
Ngube alitumia mwanya wa kutegesha kamera chumba cha Abdul walipotoka kwenda punga upepo, hivyo yote yaliyotokea waliyaona kasoro tu sauti.
"Hadi mimi nimeshangaa" alitia neno Ngombo
"Nyie acheni tu, kinachonishangaza ni huyu kiumbe wa kike alivyo mwepesi mmh! Hebu tazameni alivyomfunga kamba huyu mwehu" alisema Ngube na kurudia pale Angel alivyomfunga kamba Abdul Kwa Kasi ya ajabu
"Kweli hili nalo linatia shaka, shetani hapa si Abdul ni huyu dada" Ngube akaendelea kunena
"Tukumbuke maagizo, kazi yetu ni kuhakikisha huyu msichana yuko salama" Ngamba alihitimisha hayo na kuwataza wenzake

"Akijitokeza hapa aanze kutuvamia utamuacha tu afanye mashambulio" Ngube alihoji kwa hasira 
"Hata siwezi kuwavamia mpo vizuri kufuata maagizo" ni sauti nyororo isiyokera bali kufurahisha wengi hasa wanaume ilitokea karibu na dirisha ya chumba cha Risasi Tatu ikufuatiwa na mvunjiko wa dirisha hilo.
Mbele yao alisimama Angel.
"Karibu uketi" bila wasiwasi wala tashwishi Ngamba alimukaribisha Mwanadada huyu.
"Ngube acha wasiwasi ndugu siwezi wadhuru" Angel alimrembulia macho Ngube 
"Inaonekana unatujua vyema Mwanadada" alisema Ngombo
"Sikuwajua tu navyowafahamu mimi ni zaidi mnavyojijua nyinyi wenyewe"
"Inapendeza sisi tunakujua Kwa jina moja tu Angel, ambalo si jina lako halisi huwa hatuna utaratibu wa kufukunyua yasiyotuhusu." Ngamba alisema na wakati wote alionyesha utulivu
"Tusingechukua pesa ya bure, tungejua tuliyeambiwa tumulinde ana uwezo wake binafsi tena wa hali ya juu" 
"Kabsa ndugu huwa hatuna roho ya kuwazulumu"

Ngube alitazama dirisha lililokuwa limevunjika, hakuamini dirisha lilikuwa imara na halikuonyesha dalili kuwa limevunjika.
Alitaka kuwaonyesha wenzake alichokiona lakini alishangaa zaidi kuona mrembo Angel hayuko mahali pale.
Risasi Tatu walihaha

"Au tunaota?" aliuliza Ngamba 
"Hawezekani au Abdul anatuchezea ujue tulipewa onyo Kali sana tusitishe kumfuatilia hicho kiumbe" kama kawaida yake alilalamika Ngube
Ngombo alibaki kimya tu huku akihema Kwa Kasi mara ameliangalia dirisha mara anaangalia alipokuwa amesimama Angel.
"Huyu msichana atakuwa jini" alisema Ngube
******

Itaendelea

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyo sukubi kaanza kazi yake.
    Mwendelezo mwandishi nataka kujua Angel halisi Yuko wapi

    ReplyDelete
  2. Risasi Tatu waoga kweli

    ReplyDelete

Your Thoughts