KILIO CHA VALENTINE
_______________
Tarehe kumi na nne ya mwezi wa pili mwaka 2024 ilikuwa ni siku muhimu na ya kuvutia sana kwa vijana wawili wapenzi Abdul na Nasra waliokuwa wanafunzi katika chuo kikuu cha udaktari, Ugunja kaunti ya Siaya. Si tuu kwa kuwa ilikuwa ni siku ya wapendanao duniani kwote lakini siku hiyo ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya wapenzi hao.Wakiwa na furaha ya kuadhimisha siku hiyo kwa pamoja kwa mara ya pili kwani mara ya kwanza ilikuwa mwaka uliopita wakiwa si wapenzi ingawa tukio hilo liliwaunganisha na kuwafanya wawe wapenzi.
Baada ya sherehe hiyo kufanyika kwenye ukumbi mdogo uliokuwa ng’ambo ya Dunga beach jijini Kisumu , Abdul na Nasra waliachana na rafiki zao na kuelekea nyumbani ama tuseme vyumbani kwao walikokuwa wamepanga.Walipoachana na rafiki zao waliopanda daladala ama kutembea kwenda kwao kwa miguu kama walivyofanya akina Nasra, walikumbatiana na kupena mabusu kabla ya kuendelea na safari yao kuelekea chumba walichopanga kwenye nyumba za wageni mjini humo almaarufu guesthouse huku wakiwa wameshikana mikono kimahaba.
Kitu ambacho hawakukijua ama walikijua na kukisahau ama kukipuuza kutokana na vipombe walivyorashia vinywani mwao kuitoa ile aibu ya kusherekea na kuchangamka kunogesha sherehe yao iliyofana kutokana kuwa katika siku ambayo kwa waanzilishi ilikuwa ni ya wapendanao ila kwa sie wanamapokeo ni siku ya zinaa na ngono.Walipita kwenye kichaka kidogo kilichokuwa kikikaribia kona ya ukuta wa wa ile guesthouse na kuwakuta watu watatu waliokuwa wamekaa kwenye mawe wawili upande huu mmoja upande wa pili wa barabara ile iliyokuwa na majani mabichi yaliyonyeshewa na kimvua kidogo kilichokuwa kimenyesha jioni ya siku ile, kichaka kilichojulikana kwa uhatari wake kutokana na uwepo wa mateja labda mtaa huu Una wahuni kama kisauni tu kama si Florida huko likoni
Ilikuwa ni saa saba usiku, na akili zao zikawaambia kuwa wale walikuuwa ni wavuta bangi tuu walioamua kuutumia usiku ule kwa kuwa na kitu wakipendacho, bangi.
Naam hawakukosea watatu wale walikuwa wakivuta bangi na walianza kuzivuta muda mrefu tangu kile kimvua kilipoacha kunyesha na sasa walikuwa wamependana na bangi na bangi ilikuwa imeuzidi upendo wao na kuziteka akili zao.Walitenda akili zilivyowaambia na kwa bahati mbaya kila mmoja alizifuata, huyu alipowaza kuimba pambio waliimba wote, huyu alipowaza kulia walilia wote na mengine mengi waliyoyatoa waliyafanya kwa umoja wao.
Sauti za wapenzi wale wakiimbiana nyimbo za mapenzi na kucheka kimahaba kutoka mbali ziliwafanya watulie kuwasikiliza, ulikuwa ni wimbo mmoja wa Preston Pablo aliokuwa akiuimba Abdul ndio uliomfanya Nasra ajikute ajisahau kabisa kama walikuwa barabarani kwenye usiku ule uliokuwa na giza zito.Joto la huba lilijidhihirisha kupitia kiganja kilichofumbatiwa na kile cha mpenziwe.
‘’Simameni’’Sauti nzito ya kilevi iliyojaa amri ilisikika kutoka kwa mmoja wa wale waliokaa upande mmoja wa barabara wawili.
‘’Habari zenu mabraza’’
‘’Shikamooni’’ Sauti zao zilisikika kwa zamu huku Nasra akionekana mwenye uoga.
Nywele zilimsimama kwa woga akizidi kujisogeza kwenye mwili wa mpenziwe ambaye naye alianza kuiona ile hatari waliyokuwa wameisogelea.
‘’Kaeni’’ Sauti ilitoka upande wa pili wa ile barabara.
Waligwaya, na hilo ndilo walilolitaka wale wavuta bangi kwani waliwavamia na kuwaweka kwenye himaya yao, wawili wakimdhibiti Abdul na mmoja akimdhibiti Nasra aliyekuwa akiomba msamaha kwa wale wahuni ambao hawakutaka kumsikia wa kumjali zaidi ya kumtaka anyamaze.
Waliwaongoza hadi kwenye kichaka kikubwa kilichokuwa kilimani ambako huko walikutana na wahuni wengine ambao wao walikuwa wabwia unga.Hapo wakalazimishwa kuvuta bangi kitu ambacho Abdul hakukikubali na kutaka kupambana nao kitu ambacho kilikuwa kosa kubwa sana kwani aliwafanya wale mabwana wachane na mpenziwe na kuanza kumpiga.
‘’Nasra kimbia’’ alimwambia mpenziwe huku akiendelea kupokea kipigo kizito kutoka kwa wale mateja na wavuta bangi wenye nguvu lakini kabla Nasra hajafanikiwa kuunyanyua mguu akimbie kutokana na hofu na ule upendo aliokuwa nao kwa mpenziwe alikamatwa na mmoja wa wale wavuta bangi wenye nguvu na kudhibitiwa kikamilifu akishuhudia kitu kilichomuumiza moyo wake.
Kitu ambacho hakuweza kustahimili kukitazama kwani mpenziwe alivuliwa suruali yake na kuingiliwa kimwili na vijana wawili wavuta bangi waliowakuta pale barabarani na wakawaleta pale.
Alifumba macho asiuone ule unyama lakini masikio yake yalizisikia sauti za kilio cha maumivu alichokitoa mpenziwe huku maneno ya kashfa , dhihaka na ya kukolea utamu kutoka kwa wale vijana wawili waokuwa wakipokezana kwa zamu yakimuumiza nafsi yake na kujikuta akitokwa na machozi na kilio ambacho kilizuiwa na yule mvutaji aliyemdhibiti kwa kumziba mdomo wake.
Dakika ishirini za mateso na maumivu ya mwili na akili kwa wapenzi wale wawili zilikuwa kama muongo wa mateso mfululizo.Waliachiwa na kutakiwa kukimbia bila kugeuka huku wale walevi wa bangi na unga walipotelea kilimani wakikimbia na kucheka vicheko vilivyozidi kuzikata nyoyo za wapenzi wale ambao sasa badala ya mwanaume kumsaidia mwanamke safari hii mwanamke akawa akimsaidia mpenziwe kutembea kwani alikuwa akishindwa kutembea vyema.
Waliofika walipopanga , Nasra akachemsha maji na kumwogesha akimkanda.Baada ya hapo akampa dawa ya kutuliza maumivu iliyopunguza maumivu ya mwili lakini nafsi zao ziliumia sana kuliko hata maumivu ya mwili.
Asubuhi na mapema waliaanza safar ya kurudi ugunja
ajabu taarifa za Nasra kuwa na homa ambayo wengi walijua ilitokana na uchovu wa kushereheka usiku uliopita.Walifanya siri ya wawili , siri iliyowaumiza peke yao kwani walijua kuvuja kwa siri hiyo ni aibu na mateso ya nafsi zao.
Walifanikiwa kuifanya siri hiyo ikadumu hadi pale Nasra alipopona na kuendelea na masomo kama kawaida .Kupona kwa Nasra kulikuwa faraja kwao ingawa ile aibu haikukoma mioyoni mwao lakini ambacho hawakukijua kupona kwake ulikuwa ni mwanzo wa aibu nyingine kubwa iliyotisha.
Wiki mbili baada ya kupona Abdul alitamani tunda, tunda alilolipenda akalila na kulitamani zaidi kabla ya tukio lile la aibu lakini siku walipoamua kulila tunda ilikuwa ni msiba mwingine kwani Nasra akahakikisha kile alichokuwa akikiwaza wakati akijiuguza.Aliwaza kwani licha ya kushikwa na kuguswa hapa na pale katika kuugua kwake alijikuta akili ikishtuka lakini mwili uligoma, siku zote uligoma katika usiri lakini siku ile uligoma kwenye usiri wa wawili ambao walianza kuuzoea ingawa usiri huo kwa Nasra ulikuwa ni kama utumwa kwake kwani alijua lazima kulikuwa na siku ambayo usiri huo utapotea hasa siku akija kumkosea mwenye siri yake.
Tofauti na alivyotegemea jambo lile lilimuumiza na kuonesha kumuumiza sana Abdul ambaye licha ya kuona kwa macho yake, hakuwa tayari kukubaliana na hali ile na kuwa mvumilivu akijaribu kila siku kwa mwezi mzima, kimya miezi miwili kimya mitatu hadi mwaka ulipoisha bado mwili wa Nasra ulikataa kufanya kile akili yake ilitaka.
Hadi walipohitimu Abdul aliondoka akiwa mnyonge na mwenye hofu sana, kitu ambacho kwa Nasra ni kama alikuwa amekisahau, alijiweka mbali na Abdul na kumtaka atafute mwanaume asiye na tatizo kama lake.Nasra hakutaka kukubalina na jambo hilo akitaka kumsaidia mpenziwe kwa kutafuta tiba hospitalini jambo ambalo Abdul hakulitaka akimwambia kuwa ule ulikuwa ni mwisho wake kuwa mwanaume sahihi kwani hakukuwa na matarajio ya kupona.
MWISHO
Your Thoughts