A REJECT KAYUMBA 2024.
NA: Emmanuel Charo.
WhatsApp+25496273110
KIONJO
"Ni kauli gani mwanangu unazozungumza, huna hata soni haya mwogope mola wako alekuumba kama kutuheshimu sisi wazazi wako umeshindwa"
"Baba ni mwaka wa pili huu nateseka, niseme mara ngapi udaktari si uwezi mimi"
kauli hii ilitoka Kwa kijana huyu aliyekuwa amekaa akitazamana na wazazi wake wawili chini ya muembe wakiwa wamekalia mkeka uliotengenezwa na majani ya mkoma. Aliendelea
"Nahisi kabisa shetani ananielekeza kwenye njia sawa lakini huyu Mungu wenu hanipendi mimi, Mungu Mungu kitu gani ndio maana shetani ametawala dunia"
"Eee mola muumba mbingu na nchi msamehe mtoto wangu maana hajui asemalo" alizungumza mama yake.
"Rahim kijana wangu nini kimekukumba hadi unafikia kutoa kauli za kufuru namna hiyo" alizungumza kwa upole Baba yake
"Iko wapi ile elimu yako, si ni wewe uliyekuwa ukijitapa mtaani kote hakuna anayekufika elimu yako ya madrasa, hivi si ni wewe?" Baba yake alimalizia na swali.
"Baba, mbona ukasisitiza ni somee udaktari ilihali nilikuweka wazi si utaki udaktari mimi, kama wewe ni daktari haikuwa lazima mimi niwe daktari"
Rahim alifoka
"Ona sasa kila mtihani nina feli kisa? Mimi sio daktari, mwaka wa pili sasa haina haja Mzee uendelee kupoteza hela yako kwangu. Mimi na udaktari basi, I am not a Doctor full stop"
Kwa upole Rahim aliinuka pale mkekani, aste aste guu mosi guu pili alijipata kwenye mabirika ya kutayarisha chumvi yanayomilikiwa na kampuni inayoenda kwa jina Ken salt.
Alitazama jinsi ndege wanavyofurahia kushika samaki wadogo Kwa kiasi fulani alitamami awe ndege wale maana ana amini hawapitii shida anazopitia yeye.
Rahim ni kifungua mimba Kwa familia hii ya Mzee Karim Abdullah Razak na mke wake Yusra Nuit Bilah wenye asili ya warabu wa Yemen.
Hadi sasa familia hii ina jumla ya watoto wa tatu ikiwa Rahim kama kifungua mimba, akifuatwa Kwa ukaribu na kijana mwengine anayeenda Kwa jina Kassim na wakabarikiwa mtoto mmoja wa kike, malaika haswa na wakampa jina Takisha ambalo Kwa kiarabu ina maana kuwa ndie mtoto pendwa zaidi ndani ya familia ile.
Familia ya Mzee Karim ni ya wenye navyo Baba mtu ni daktari maalumu wa moyo na alidumu kwenye taaluma hiyo Kwa muda wa miaka ishirini na tano ndipo akaamua kutundika daluga zake akiamini kifungua mimba wake atachukua pale alipoachia, pia haachi kutoa msaada popote pale anapohitajika. Mama Yusra yeye ni mwana usalama wa taifa japo miaka imesonga lakini mchango wake bado unahitajika kwenye usalama wa taifa Kwa ujumla Kwa upande wake yeye hataki hata kidogo mtoto wake yeyote akanyage guu lake upande ule japo mtoto wake wa kike anaonyesha nia ya kuingia upande huo.
Ni watu wa chache sana wanaotambua kuwa mama huyu yuko hiyo sekta maana wengi humuona na kapu la samaki kila asubuhi pale Gongoni sokoni akiuza nalo hilo hushangaza wengi maana si Boma analotoka na biashara afanyayo, wengi husema anaona haya kuwa mke tegemezi.
Kweli usilolijua ni usiku wa Giza.
Rahim bado alikuwa akikodelea macho wale ndege, huku mawazo tenge yakitawala kichwa chake, akiunda mazungumzo kwenye akili yake na kujichekea tu kama zuzu au tahira chambilecho ndugu zetu Watanzania kama si msukule.
'Dhana ni mbaya sana, nalo tumaini humualika izrael' aliwaza
'natamani siku zirudi nyuma ili niepuke siku ile' ndege waliokuwa mbele yake walianza kufifia na kuwaona Kwa umbali alihisi vitu moto vikitambaa mashavuni mwake, alipeleka kiganja chake cha kulia kwenye shavu lake la kushoto, machozi!
'sasa nalia nini, niliyakoroga sina budi kuyanywa'
'sasa hata nitaanzia wapi kumwambia ukweli Baba kuwa ndani ya hiyo miaka miwili sikuwa na soma hata' aliwaza, machozi yaliendelea kutiririka.
'mtihani wa maisha, dah niliisoma hadithi hiyo kumbe kweli'
*****
"Baba Takisha nilikwambia huyu mtoto hasomi na wala hata hajakanyaga lango la chuo ukadhani ni utani" alilonga mama Rahim
"Oooh Baba Takisha, Takisha mwanao kitinda mimba husikii wewe kila siku Baba Takisha koma" ndio kauli ilomtoka Mzee Karim
"Afadhali hivyo kuliko lile jambazi, mwanao jambazi Karim nitamutia ndani yule amesahau mamake nani hadi anatuongopea hapa" alifoka mama Rahim
"Miezi tisa ulimbeba tumboni, uko tayari mtoto wako aozee jela eti mama Rahim"
"Koma usiniite na jina la jambazi niite na jina la kipenzi chamgu Takisha au Kassim lakini si Yule mwehu"
Alimaanisha alichozungumza kisha aliinuka mama huyu japo umri umesonga lakini umbo lake maridadi halijapwaya kwame.
*****
Tanga, Tanzania.
Itaendelea....
Mwanzo fit
ReplyDeleteYour Thoughts