NGOJA NILEWE 10(MWISHO)

Emmanuel Lee
By -
0

 NGOJA NILEWE  10 (MWISHO)


MTUNZI: Mbogo Edgar


WHATSAPP +255743632247 


ILIPOISHIA 9


alipiga kelele George, huku anatafuta maji, ya kunywa, ata alipoyapata, na kuyanywa, lakini aikusaidia kupunguza uchungu nkubwa ulio kuwepo kwenye chakula kile, “mamaweeeeee Adija umeniwekea nini” alilia George, kama mtoto mdogo, mdomo wazi, uchungu mkubwa na mkali ulijaa mdomoni, koo lake lilikuwa linawaka moto, kwa kitu kikali kama pili pili, hukuulimi na midomo yake ikihisi uchungu kali, zaidi ya mchunga au shubiri, Adija alimpatia kikopo cha sukari ambacho kilikuwana sukari kidogo, aliyo ibakiza Seba. ,…… . ENDELEA……..


Lakini alipo inwia, bado nayo ilikuwa na uchungu kama vile amekula kitu kile kile, ambacho niwazi kilikuwa kime changanywa kwenye chakula, alicholetwa, “Adija umeniwekea nini kwenye chakula, mbona unataka kuniwa weweee” alisema George, kwa sauti ya juu, sambamba na kilio, kuona hivyo Adija ambae akuelewa kwanini imekuwa vile, akachukuwa bakuri lake na kuondoka nalo mbio mbio, ata alipokaribia barabara akaanza kuwaona wapangaji wengine wakike na wakiume wakitoka na kukifwata chumba cha George ambae bado alikuwa apiga kelele za uchungu na maumivu.


Adija alikimbia mbio mbio huku akivurumisha lile bakuri porini, na kukimbilia nyumbani kwao, ambako ila anaingia ndani anawakuta maboss zake wakiwa wana msubiri sebuleni, hakika alishtuka sana, kwa kujuwa wazi uwa tayari kila kitu kipo adharani, kwamba mtindo wake wakubeba chakula na kwenda kwa wanaumeusiku umegundulika, “Adija kesho unaenda kwenu, kazi yako imeishia hapa” alisema Boss wakiume, kisha bila kuongea lolote wakamweleza akalale, na kesho ajiandae kwa safari.


Kumbe awa maboss walisha gundua mchezo wa Adija, toka week iliyopita, ambapo waliamua kuvunga, huku wakitafuta dawa ya kukomesha tabia ya Adija, ambayo waliipata na kuchukuwa maamuzi ya kuchanganya vitu vyote vichungu, wakachuja na maji yake wakichanganya na pili pili kali sana, alafu waka vizia chakula ambacho kimewekwa pembeni na Adija, na kuchanganya mkorogo huo, kisha wakasubiria matokeo yake, ambayo aikupita ata dakika kumi na tano, wakamwona Adija anakua mbio mbio.


Siku ya pili wakati Adija anaondoka kuelekea kijijini kwao, huku Geroge, akiwa amelala hoi bin tahabani, aeleweki, siyo kwaajili ya mavutu aliyokula pekee, ambayo bado yalikuwa yana mkwanguo kuanzia mdomoni mpaka kooni, ambayo alikuwa anatamani dumbukize mswaki kooni ilisugue kwanguvu, hii ilizidishwa na njaa ya toka juzi usiku, “naomba mkamwambie kaka yangu pale kwa Vanesa, aje anichukuwe anipeleke hosptal, alisema George kwa tabu sana, “samahani George, unaweza kutaja ndugu mwingine yoyote, maana kwa ulicho mfanyia yule jamaa, sizani kama ata kusaidia” alisema mmoja kati ya wapangaji wenzake, “nyie mwambieni tu” alisisitiza George, na hapo majilani zake waka weka mtego, na kumvizia Seba, wakati anaenda kazini, wakamsimamisha na kumweleza kilicho mkuta ndugu yake.


Seba akaweka gari pembeni, akamwomba mke wake amsubiri kidogo, nae akaenda mpaka chumbani kwa George, ambako alimkuta amelala huku uso umemvimba kweli kweli, “vipi kaka nasikia umeniita” alisema Seba, akimtazama George alie lala kitandani, “Seba namba unipeleke hospita, nimelishwa vitu vichungu, alafu ninanjaa, sijala toka juzi” alisema George, bila aibu yoyote, “mh! George, umesahau nilivyo kuambia kwamba nimejifunza, umewezaje, kupata ujasiri wa kuniita na kunieleza shida yako, kama nilikusaidia mwanzo, na ukanifanyie vile itakuwaje safari nyingine?” ukweli swali ilo George akuweza kulijibu, na baada ya kuona kimya, Seba akatoka nje na kumwita yule alie mwita, mimi nasafiri kesho kuelekea Dar, naombeni muuze hiyo tv yake, na deki, tumieni kumpeleka hospita, inayobakia itumike kama anauri ya kuelekea kijijini kamataki achaneni nae” alisema Seba, kisha akaondoka zake.


Ayakupita masaa mawili kabla wateja awakapatikana, wakanunua TV na Deck, na kumpeleka George hospital, siku ya tatu alipopata mafuu, akafunga kitanda na godoro lake, safari ya kijijini ikaiva, moja kwa moja akamsimulia mama yake kilicho tokea na mikausho ya Seba, “mwanangu tumechokwa, ata mama yake sasa hivi, anidekezi kama zamani, nilivyokuwa na mnyayasa weee, lakini akipata kitu ananiletea, sasa hivi bati bati” alisema mama George, huku akimsisitiza kijana wake, kuto kulala mika kwawatu jambo kama ilo.***********


Babu aliwai kiniambia kuwa, FISI afugiki, ukiona FISI anafugwa, basi ujuwe ushirikina umetumika, maana utamfuga na kumpa chakula, lakini akipata nafasi lazima ata ondoka zake, kwenda kutafuta mizoga na kuiba mifugo ya watu, kama alivyozowea, msemo huo unatimia kwa bwana Daniel.


Iilikuwa ni baada kumaliza fedha yote aliyoipata, kupitia mnada wa vitu ambavyo akujuwa ata bei yake, vitu ambavyo alishirikiana na mpenzi wake wasiku nyingi sana, Adellah, pamoja na dada yake Sophia, Daniel sasa akubakiza ata senti moja ya dawa, akiwa ametapanya mari na makahaba, ila pia pombe ziliusika kwa kiasi kikubwa, sasa Daniel alikuwa ameshauza mpaka nguo zile zenye uafadhari, asa zile za Sebastian, alizobakia nazo kwa lengo la kuzivaa, Daniel akuwa na kitu wala akuwa na la kufanya, akaanza tena kulala sehemu zenye uafadhari wakulala, pasipo kujari ni kwenye kibanda cha watu au kwenye kituo cha dala dala, siku zote akiombea mpenzi wake Adellah, apate tena mwanaume mwingine wakamtaperi, lakini licha kuwaza hayo, akuwai kufikilia mwanamke huyo mwenye watoto wake anaishi vipi huko aliko.


Lakini kunamsemo pia unasema kuwa, kipaji akimtupi mtu, na kwakuwa Daniel alikuwa na uzoefu wa maswala ya WTK yani Wizi, Taperi na Kabaji, na tayari alikuwa na uzoefu wa mika zaidi ya sita katika kazi hiyo ambayo imemweka mjini zadi ya miaka nane, akaona isiwe tabu awezi kulala na njaa wakati anatahaluma hiyo, ya kipekee, ambayo unawashiriki wachache sana.


Kwamaana hiyo Daniel akarudi mitaa yake ya mbezi mitaa mbayo alikuwa ameizowea sana, pamoja na chochoro zake, ili iwe lahisi kwake kukimbia atakapotokea anakimbizwa, na wale wanachi wenye hasira kali, na pia ingekuwa lahisi kwake kujiegesha kwenye ile stendi ya dala dala, ambapo nikama watu awaishagi hivi.*******


 Naaam Daniel alianza maisha aliyo yazowea, maisha ya kujitafutia kwa kutumia WTK, huku akikutana na baadhi ya vijana aliowai kuwa nao pale kijiweni miaka hiyo, huku wengine wengi wakiwa ni wageni mitaa ile, maisha yale kwa upande wake yalikuwa malahisi, aliaendelea kukaba na kuiba, huku akizidi kuchakaa, bahati nzuri kwake, aliendelea kupata starehe yake ya pombe, wakati huo alikuwa anakunywa pombe flani ilikuwa na jina linalofanana na neno kitabu, kwa kiingeleza au neno elfu moja, kwalugha ya mtaani, ila lazima uanze na neno chi, ni pombe ya kienyeji, lakini ilitengenezwa kiwandani.


Siku moja mida ya jioni, Daniel akiwa amenywa kopo sita za pombe, moja likiwa lina uzwa shilingi hamsini, na amesha vuta puli nne za bangi, akaamua aendezake stendi, ambako alikuwa anafanya kazi za wizi, huku akisingizia kuwa anapiga debe, ukweli ata selewi kilicho mkuta huyu doctor mwenye Phd ya WTK, akafanya kosa kubwa kama ili, maana akiwa pale stendi amesimama, anasikilizia utendaji kazi wa pombe na bangi kichwani mwake, mala likaingia dala dala la kutokea kaliakoo, lililokuwa linaenda kibamba, likashusha abiria kadhaa, mmoja wa abiria hao, alikuwa nimama mmoja mtu mzima, ambae mala tu baada ya kushuka, akafungua pochi yake, yenye noti za blue za elfu kumi kumi.

Macho yakamtoka bwana Daniel, akaikazia macho ile pochi ya mama mtumzima, ambae sasa alikuwa anapekuwa kutafuta shilingi mia hamsini, ya kulipia nauri, lakini kabla ajaipata tayari bwana Daniel alisha ikwapua ile pochi, na kujaribu kukimbia, “jamani mwiziiiiii” alipiga kelele yule mama, huku akimdaka mkono Daniel, na kuichukuwa ilepochi, wakati huo huo, Daniel ambae kutokana na vitu alivyokuwa ametumia, muda mchache uliopita, akikataa matokeo ya kunyang’nywa ile pochi, ambayo alimini kuwa akiipata leo lazima akanywe bia, akageuka na kutaka kumnyang’anya tena yule mama, ile pochi yake, lilikuwa kosa kubwa sana kwake.


Maana alishtuka aki akifyetuliwa mtama mmoja wanguvu, akapaa hewani na kujibwaga chini, fumba na kumbua, alishangaa kundi la watu likiwa limesha mzunguka, huku kila mmoja akiwa nakipigio chake, akuna ata ammoja alie mpiga ngumi, ilikuwa mawe na magongo, ungesema wanauwa chatu au mnyama mmoja mkubwa wa kutisha, hapo ndipo Daniel alipogudua kuwa, alifanya tukio mchana wa juakali, lakini aliku amesha chelewa, maana asingweza kukimbia wala kujitetea kwa lolote, wakatihuo huo anamshtukia kitu kizito kikitua kwenye mkono wake wakushoto, na lilikuwa ni jiwe kubwa sana, ambalo lisingefaa ata kujengewa msingi wa nyuma, kutokana na ukubwa wake, ile anajigeuza ashike mkono wake, tayari gongo mfano wa mwichi, lilitua kwenye paja lake la kulia, napo ikasikika kaah! Kuashiria kuwa mfupa umesha vunjwa, “mamaaaaaaaa!!!” hii ilimkolea bwana Daniel, ambae sasa aliona wazi kuwa anapoteza maisha.


Kipigo kiliendelea huku maumivu makali yakiushika mwili wake, wazi kabisa Daniel aliona kuwa anaenda kupoteza maisha, taratibu akamkumbuka Adellah na watoto wake, ikamjia Sura ya Sebastian, na wengine alio wai kuwaibia, huku giza likianza kunda usoni mwake, na huo ndio wakati alio ona watu wakianza kutawanyika, “polisi, jamani polisi” walisema baadhi, na hapo Daniel akawaona polisi wakiwa wanamzunguka pale chini alipokuwa amelala, damu zimemjaa usoni, zinamuuza macho yake kutokana na chumvu nyingi iliypo damuni, Seba anajiona kuwa sasa yupo kwenye mikono salama, ata kama atakufa, asi kitapatikakana cha kwenye kuzika, na wakatihuo giza likafunika uso wake, japo aliendelea kusikia maonezi ya mwisho, “anapoteza fahamu huyu, tumkimbize tumbi” walikuwa ni polisi walio ongea hivyo, wakitaja jina la hospital ya tumbi.********


Miezi miwili mbele, ujauzito wa Vanesa ukiwa na miezi saba, Seba na Vanesa wakuwa dar es salaam, katika moja safari zao, wakiwa wametembelea biashara zao, tumbo la Vanesa lilikuwa linaonekana wazi wazi kuwa alikuwa mjamzito, ambapo siku ile ya ijumaa, ikiwa siku ya pili toka waingie hapa dar, nakufikia kwenye nyumba ya Sebastian, ile ile ya kibamba kwa mangi, nyumba ambayo Vaanesa aliinunu kwaajili ya wfanyakazi wake, ambapo baada ya kujuwa kuwa ni nyumba ya Seba akaodnoa wafanyakazi na kumkabidhi Seba hati za nyumba yake.


Mida ya saa saba wakiwa wanatoka kibaha kwa mfipa, waliona wapitie panama, wakapate nyamachoma, kabila awajaenda nyumbani kupata wine na nyama choma, “alafu ulinambia hapa ulikuwa na rafiki yako, uendi kumsalimia?” aliuliza Vanesa, ambae ujauzito wake ulipenda sana nyama za mbuzi, “ni kweli bwana sito kuwa muungwana, kama sitoenda kumsalimia” alisema Sebastian wakiwa wamekaa kwenye viti vya bar ile kubwa ya panama, enzi hizo kabla aijavunjwa ulikuwa ukipita barabarani ndani ya busy, unasikia harufu ya nyama choma.


Naam, ile kukaa tu, akaja mhudumu wajikoni, maana mida kama hii, wateja wengi uwa ni wachakula, alafu kinywaji kingefwata, “niwahudume chakula gani?” aliuliza yule mhudumu mala baada ya kusalimia, “nao wakaagiza vyakula walivyo itaji, kisha Vanesa akaagiza kwa mhudumu yule yule, “samahani dada, niitie mhudumu wa vinywaji” alisema Vnesa, na yule dada akaondoka zake, akielekea mapokezi ambako kulikuwa na wahudumu wawili, walikuwa wamekaa kwenye viti virefu, wanapiga soga, “dada Jeni nyie kaeni tu, boss akute mteja amekaa vile, alafu anaitaji huduma” alisema yule dada nakuondoka zake, “hivi kunawateja mbona siku waona” alisema mmoja akimweleza mwenzie, “mimi nimewaona sana, wamekuja na gari lile pale, nilijuwa wanakuja kula” alisema mwingine, yule alie itwa Jeni, huku anaonyesha gari aina ya Nissan Patrol, lililosimama kwenye maegesho ya bar ile, likiwa pake yake, basi mimi siku waona kabisaaaaa” alisema yule mwanamke mwingine, huku anawatazama wateja wale, ambao ni mwanamke na mwanaume, mwanaume akiwa amekaa kwa kumgeuziamgongo, ikiwa nivigumu kuiona sura yake, na mwanamke akiwa ametazama upande wao, “mdada mzuri yule, alafu mimba imempenda wala aija mwaribu” alisema mwanamke huyu mwenzie na Jen, “Sophi nenda basi kawasikilize, akija mteja mwingine nitainuka mimi” alisema Jen.


Bila kujiuliza mala mbili, yule mwingine, ambae tunamwona kuwa ni Sophia, yani dada yake Adella, anashuka kwenye kiti kirefu na kuelekea moja kwa moja mpaka walipo wateja, wale wawili mwanamke na mwanaume, nakasimama pembeni ya yule mwanaume, ambae akuweza kumtazama usoni, sababu alikuwa ubavuni mwake, “karibu” alisema Sophia, huku akimkazia macho Vanesa, “asante, unamaji ya baridi kiasi” aliuliza Vanesa, “yapo, ni shilingi mia hamsini” alisema Sophia, lete mawili” alisema Sebastian, huku anatoa wallet yake na kuifungua, macho ya Sophia yakiwa kama paka lilao tazama samaki kwenye chungu, alitazama kwenye ile wallet ya Seba, ambae mpaka dakika hii alikuwa ajamtazama usoni, akaona minoti mingi ya elfu kumi kumi mpyaaaaa, wakati huo zikiitwa blue blue.


Sophia anawaza kama yule kijana, asingekuwa amekuja na mke wake, basi angefanya kila linalowezekana, kumshawishi kijana huyu, akamnyandue, ili angalau apate japo elfu kumi moja tu, ambayo kwa hakika ingemsaidia ata week mbili, yeye na mdogo wake, ambae wote kwa pamoja wapo kwenye shida kubwa sana, “sina fedha dogo, labda utampatia wajikonipia akate na fedha yake” alisema Seba huku ananyoosha mkono wake, sambamba na kugeuza uso wake kumtazama Sophia.


Naaaam Sophia anajikuja akitoa macho kwa mshangao, kumtazama Sebastian, ambae pia alimtazama Sophia, lakini pasipo mshangao wowote, “kumbe ni wewe, yani muda wote huu sikuwa nime kutambua” alisema Sebastian kwa sauti ya kawaida tu, usingezania kuwa kuna kitu kiliwai kutokea kati ya wawili awa, “jamaniiiii, ni wewe kweli Seba, umewezaje ku……. ku…… au wewe ni ndugu yake Seba?” aliuliza Sophia kwa sauti yenye mshangao namshtuko mkubwa, “nimimi, vipi uamini kuwa aisha yanabadirika Sophia” alijibu Sebastian, kwa sauti tulivu ya kawaida tu, kama akuna jambo zito kati yao, “hivi nyie wawili mna fahamiana?” aliuliza Vanesa ambae muda wote alikuwa anawatazama tu wawili awa, “ndiyo mke wangu, nazani unakumbuka niliwai kukueleza kuhusu Adellah, sasa huyu ndie dada yake anaitwa Sophia” alijibu Sebastian kwa sauti flani hivi, ungesema akuwa, alikuwa amekumbushia wakati mgumu sana katika maisha yake, “hooooo! kumbe, nimefurahi kumfahamu” alisema Vanesa huku akimtazama Sophia kwa mala nyingine, akamwona Sophia anaachia tabasamu la kibwege, “basi ngoja niwahudumie, alafu tutaongea” alisema Sophia ambae ni wazi aliona kuwa Seba, amesha sahau kila kitu, na kwa ule moyo wake waupendo, alisha samehe kila kitu, akuwa na kinyongo chochote.


Sophia alichukuwa ela mkononi kwa Seba, na kuelekea mapokezi ambako alichukuwa maji chupa mbili na pia akaenda jikoni, na kumpatia fedha yule mwanamke mhudumu wa chakula, akimpa na maelekezo ya mgawanyo wailefedha, kama seba alivyo sema, kisha akapeleka maji kwenye meza ya Sena na mke wake, huku wakati wote wa mzunguko Sophia alikuwa anawaza, namna ya kumshawishi Sebastian awe karibu na Adellah, pengine wanaweza kurudiana na kuwa mpenzi wake wasiri, na yeye akafaidika kwa ilo, “jamani shemeji ata kuja kuangalia watoto wanaendelea, vibaya hivyo?” aliuliza Sophia, huku anaweka maji mezani, pasipo chemembe ya aibu au kujishtukia, kwa yale yaliyotokea, ilimshangaza sana Seba ata Vanesa pia alishangaa, “he! kumbe ulizaa na Adellah, au ni watoto gani anawazungumzia?” aliuliza Vanesa, kwasauti tulivu nyololo, huku anachukuwa maji na kupeleka mdomoni, “sina hakika, ila nazani kuna watoto nilisimulia habari zao” alisema Sebastian ambe pia aliongea katika hali ya kawaida tu.


Sophia alishajuwa ni hadithi gani aliyo isimulia Seba kwa mke wake mpya, ambae uzuri wake, ata kama hukoo wa wakina Sophia, wangeitana wanawake wote, na kuchambua, kila mwenye kitu ambacho anaamini katika mwili wake ni kizuri kuliko kingine, yani huyu anatoa mdomo, mwingine anasema meneo yake ndiyo mazuri anachangia, huyu anasema mimi na macho ya kulembua, anachangia, sijuwimwenye makalio makubwa, hips, nywele maziwa, pengine ata kitumbua, lakini wasinge mfikia mwanamke huyu aliekuwa mbele yake, “lakini watoto wale ni malaika, na ukichukulia wanakuchukulia kama baba yao” kauri ile iliwafanya Seba na Vanesa watazamane kwamshangao, maana katika kumbu kumbu zao, Seba mala ya mwisho kuwa baba wa Saimon, ni wakati mtoto huyu, akiwa anatimiza miezi nane, kiasi kwamba ata kuongea alikuwa bado, “ata hivyo Adellah akisikia nimekuona ata furahi sana, yani anakukumbuka sana” alisema Sophia, huku akiwa bado amesima pembeni yao.


Vanesa na Seba, nikama waliambizana kuwa watulivu, maana ata walipotamani kucheka walichekea matumboni mwao, “sawa basi mimi naenda, ila siku nyingine ukija nitamwita aje akusalimie” alisema Sophia, ambae nashindwa kumwelewa, kama ni kumwona Sebastian zoba au mjinga, maana akuonyesha kujutia kile walicho mfanyia, nae akaondoka zake, akiwaacha wapenzi wawili wakiletewa chakula na kuanza kukifakamia taratiiiiiib, huku wanakumbushana maongezu ya Sohpia na kucheka kwa pamoja.


Ata walipo maliza kula na kuondoka zao, Sophia aliwakimbilia na kuwaaga, nao wakaondoka zao wakishika uelekeo wa kibamba kwa mangi, ambako walimtembelea baraka pale gengeni, kiukweli baraka akuamini alicho kiona, siyo tu mwonekano wa Seba, ila pia ata mwonekano wa mke wa Seba, “sasa kaka hapo umeopoa” alisema baraka, huku akimtazama Vanesa ambae alikuwa amechoka, anaona uvivu kushuka toka kwenye gari, “hoooo boss afadhari umekuja, nazani leo nitakunywa bia” ilisikika sauti ya Side mkaa, Seba aligeuka na kumtazama Side alie jichekesha kama chizi, kisha akapotezea, lakini wa baraka ilikuwa ngumu, “kwahiyo na wewe unataka ununuliwe bia, siuje atakwangu nikununulie bwana” alisema Baraka kwa sauti ya kejeli, hapo Sophia ambae aliona wazi kuwa Seba akuitaji mazowea na yeye, akakausha kimya kabisa, “Seba alimwachia baraka shilingi laki moja, na kuondoka zake kuelekea kwa mangi nyumbani kwake.*******


Naaam! mida ya saa moja za jioni, kama siyo usiku, kama ambavyo tungeita kutokan na giza lililotanda, anaonekana Adellah, akiwa na sinia lale lenye chana nne za ndizi na machunywa ishilini, alilo liweka kichwani, huku mtoto mdogo akiwa mgongoni, na mwingine mdogo wa miaka miwili anatembea mwenyewe, ungeweza kuona jinsi mtoto alivyo choka, kwa kutembea, ni wazi mama yake akuwa na mtu wakumwachia mtoto huko nyumbani, hivyo ilimlazimu kuzunguka nao mtaani, wakati akifanya biashara hii ya matunda, Sophia alikuwa amesha tembea kilomita zaidi ya tatu, pasipo mafanikio katika biashara yake, aliona wazi kuwa Saimon alikuwa na njaa kali, maana toka alipokula kitumbua kimoja na maji saa tano asubuhi, “ni kosa langu ili, bila ujinga wangu leo hii mngekuwa na baba bora ambae angewapatia maisha mazuri” alisema Adelah kwa sauti ya chini, ailiyoenda sambamba na tonye la chozi toka kwenye jicho lake la kulia, analiwai analifuta, lakini jicho lakushoto nalo, chozi linachungulia kabisa, anapotaka kulifuta ana kijikuta anapeleka mkono puani, ambako kulikuwa na maji mepesi yaliyo kuwa yanataka kudondoka, “Daniel kokote uliko ulahaniwe shetani wewe” alijilalamisha peke yake Adellah, huku anaendelea kutembea.


Adellah alitembea weeeee, lakini akukuwa natamteja mmoja alie nunua matunda yake, ukweli asinge kubari kurudi nyumbani katika hali kama ile, watoto wange kula nini, nilazima angepata japo ela kidogo watoto wake wakale, hii ilimkumbusha miaka mitatu iliyopita, siku ambayo ilifanana sana na hii, ambapo dada yake na watoto, walikuwa awajala toka siku iliyopita, nae akaenda kwa Baraka kuomba wakopeshwe, ambapo akufanikiwa na baada yake akapewa fedha buleee, na Sebastian, kijana ambae siyo tu alimsaidia yeye peke yake, ila pia alimsaidia dada yake na wazazi wao.


Kwakumbu kumbu hii, Adellah anajikuta anajichukia yeye mwenye, anamchukia Daniel, anamchukia dada yake Sophia, kwa ushauri na kile walicho kifanya mpaka kumwalibia maisha mwanaume ambae alimwonyesha upendo wa kweli, tena wa hali ya juu, upendo ambao, ata yule ambae alijuwa ndie mpenzi wake wa maisha, akuweza kumwonyesha ata nusu yake, zaidi ya maumivu na usariti.


Adellah aliendelea kuwaza huku akiendelea kutembea, na sasa alibadiri mtaa na kuelekea kwamangi ambako alijikuta anaibukia kwenye ile nyumba ambayo waliiuza, nyumba ambayo ilikuwa ni nyumba ya Sebastian, ambayo alipoina tu alijikuta anatokwa machozi, tena alizidi kutokwa na machozi mala baada ya kuliona gari limesimama nje yake, gari ambalo lilimkumbusha lile gari ambalo waliliuza, yani gari la Seba.


Dakika nusu saa baadae tayari Adellah, alikuwa kwenye kitanda cha hospital akilejewa na fahamu zake, na kujikuta akiwa amezungukwa na manesi, “wanangu wapo wapi” aliuliza Adellah, mala baada ya kuona watoto wake awapo, “wameenda kula hapo canteen na wale waliokuleta” alijibiwa Adellah, na mmoja kati yale ma nurse waliokuwa wanampahuduma, “kwani hapa nimefikaje ala moja hii, na upo wapi Seba” alisema Adellah, kama vile aamini kilicho tokea, “weeee! ebu tulia bwana, tena unabahati waliokuleta walikuwa na moyo wa huruma, mwingine angekumwagia maji uzinduke” alisema Nurse mmoja kwa sauti ya ukali, wakati huo huo akaingia nurse mmoaja akiwa na sahani yenye chakula, “ebu kula hii upate nguvu” alisema yule nurse ambae ni mtu mzima hivi.


Adellah, ambae sasa alikuwa anawaza namna yakuomba msamaha kwa Seba, ainuka na kukaa kwenye kitanda hicho kisha akaanza kula, na kabla aja piga ata tonge tano, mala akaingia Sophia nakujitambulisha kuwa ni dada wa mgonjwa, sekunde chache baadae wale wauguzi wakatawanyika, na kuwaachia wao wawili, “dada nimemwona Seba” alisema Adellah, huku anatokwa machozi, dada mtu akakosa la kijibu au kuongea akabakia ametazama chini, “dada najuta mimi, bola ata nisingemleta tena Danile maishani mwangu, aya yasingetokea, pengine Simon angekuwa amaisha mazuri” alizidi kulalamika Adellah, huku anaangua kilio cha chini chini, “sasa Adellah tutafanyaje na wakati yamesha tokea?” aliuliza Sophia ambae moyoni alikuwa na uhakika kuwa Seba akuwa na kinyongo nao, “dada inauma, nilibahatika mimi nikachezea bahati” alizidi kulala mika Adellah, “ebu tulia kwanza Adellah, huu sio wakati wakulia peke yako, tunza machozi umlilie Seba, nauhakika ata kusamehe, baada ya hapo utamshawishi kama kipindikile akusamehe mrudiane ata kwa siri” alisema Sophia, kwa sauti ya kumsihi mdogo wake, “labda #UNGOJE_NILEWE, hakika kusamehe ni kawaida yangu, yangu lakini siyo kurudiana na Adellah, au kuwa karibu na nyie, watu ambao wema kwenu ni upuuzi” ilisikika sauti ya Sebastian, toka upande wa mlangoni, wote wakatazama mlangoni.


Naam kwa macho yao wakawaona Seba, Vanesa Samuel na mdogo wake, pamoja na kijana baraka, “kweli nyie wapuuzi sana, kwahiyo bado mnatamaa ya kuwa Adellah ata ruana na Seba, wakati unamwona anamke wake tena ni mzuri kama nini” alisema baraka, kwa sauti ya kusimanga, huku wote wawili wakiwa wameinamisha vichwa chini, kwa aibu, “lakini shemeji umwoni Adellah anavyo jutia alicho kifanya” alisema Sophia kwa sauti ya kubembeleza, “anajutia alichofanyiwa na Daniel anajutia alicho nifanyia mimi, kwanza tuyaache ayo mambo, mimi nilimleta huyu nimesha hapa hospital nayo kuja kuongea habari ambazo azikuwepo” alisema Sebastian, kwa sauti yakawaida tu, ungesema kuwa alikuwa amaanishi anacho kisema, “hapana shemeji Adellah, nakupenda na anajutia alichokifanya , anaikuita msikilize mwenzio” alisema Sophia, kwa sauti ya kubembeleza, huku Adellah mwenyewe akidakia, “seba kumbuka penzi letu lilibarikiwa na mama yako, ebu kumbuka alivyo nipenda na kunichukulia kama binti yake, naomba unisamahe ata kama atuto rudiana basi tuwe kama ndugu” alisema Adelllah, sauti yake ambayo iliambatana na kilio cha chini chini.


Uweli hali ya Adellah, ambae siyo tu sura na mwili wake ata alivyokuwa anaongea na kulia, vilitia huruma, lakini hii yote nikama alijitakia yeye mwenyewe, “Adellah, nilisha jitoa kwako nilivyoweza, ukweli siyo kwamba nilikupenda sana kama ninavyo mpenda mke wangu, ila niliamua kusihi na wewe, sababu niliamua kukusaidia, na kikubwa zaidi niliamini Samuel ni mwanangu, kwa hiyo kwa sasa akuna kinacho nirudisha kwako, na mbaya zaidi nimegundua kuwa wewe ukuja kwangu sababu unanipenda, ila ulikuja kwangu, sababu ulikuwa unatafuta mtu wa kukulelea mimba, uliyokuwa umepewa na Daniel, kwa hiyo auna cha kujutia wala auna ulichopoteza kwangu, sababu maleno yako yalitimia na ulipoona unaempenda amerudi kwako, ukaamua kuniangamiza kabisa ukishirikiana na dada yako nayule mzazi mwenzio, kwa jinsi hiyo Adellah ata ukirudi kwangu na ukapatana tena na mzazi wenzio, mtakuja kuniuwa kabisa, ili mchukuwe kila nilicho nacho” alisema Sebastian, safari hii akionyesha msisitizo wa kile alicho kisema, na hapo Adellah akainua uso wake na kumtazama Sebastian, sijuwi kwanini alifanya vile.


Maana Adellah aliganda akimtazama Sebastian, kwa dakika moja nzima, kisha akaamishia uso wake kwa Vanesa, “dada naomba uniachie Seba, najuwa jinsi alivyo nipenda, ata kama sikuwa na upendo wakweli, lakini sasa hivi ninampenda kiukweli, nimegundua yeye alikuwa anipenda kweli” alisema Adellah, huku machozi yanamtililika, “mh! dada, labda nikueleze kitu, Seba alisha kuwa wangu kabla ata ujamjuwa, hivyo nisawa na kusema kwamba, alikuwa amepotea na sasa amerudi kwao” alisema Vanesa, kabla ajamgeukia Seba, mume wangu, hivi unakumbuka tumeacha nini jikoni, tunapaswa kuondoka” alisema Vanesa, na kabla awajaondoka, akaingia Nurse, “hooo kumbe wote mpo humu ndani, aya mchukueni mgonjwa wenu mkakae hapo nje mkamilishe malipo, ili muondoke nae, aumwichochote zaidi ya mshtuko na njaa aliyo kuwa nayo” alisema yule nurse, akisisitiza kuwa kuna mgonjwa mwingine anatakiwa kuja kulazwa pale.


Kiunyonge sana, Adellah aliinuka toka kitandani, nakuongozana na wakina Seba na dada yake kutka nje, huku wakina Samuel wakiwa na Vanesa, kisha wakafanya taratibu za malipo, ambazo zilikamilishwa na seba mwenyewe, maana ndio walio mleta mgonjwa, kisha wakaanza safari ya kuondoka pale tumbi hospita.


Wakati wanatoka nje ya uzio wa hospital, mala wakasikia mtu akiwaomba msaada, “majani msaada ndugu zangu sina uwezo, sijala toka asubuhi” ilikuwa ni sauti ya kinyonge, sauti ambayo ilimtia huruma kila mmoja, kiasi kwamba Seba akafungua wallet yake na kutaka kutoa fedha, kumpatia mgnjwa huyo ambae alikuwa ameondolewa mguu wa kulia na mkono wa kushoto, huku wengine wakiwa wamsha pita kasoro Baraka alie mshika mkono, “bro wema utakuponza, unataka kumsaidia huyu mshenzi, ebu achana nae aendelee kula joto ya jiwe” alisema Baraka na kumshangaza kila mmoja, ata wale waliokuwa wametangulia, yani Vanesa na wakina Adellah, kiasi cha kusimama na kugeuka nyuma kuwatazama wakina Seba, “kwani unamfahamu huyu jamaa” aliuliza Seba kwa mshangao, wali ambalo ata wakina Vanesa na wakina Sophia, walitamani kuuliza, “umjuwi huyu taperi, si ndio yule Daniel alie uza nyumba yako” alisema Baraka na hapo Sebastian alie shtushwa na jina lile, akageuza uso wake kumtazama mgonjwa huyu kwa macho ya kuto kuamini, “Daniel” Sebastian alikuta akinong,ona, alijikuta akinong’ona 


Sebastian alijikuta akitoa macho kwa mshangao, “Daniel, vipi tena ulipata hajari” aliuliza Sebastian kwa sauti ya mshangao na kuto kuamini, huku wakina Adellah wakirudi kwa haraka pale walipokuwa wakina Seba, wakati huo Daniel akiwa ametoa macho kwa mshangao, kama vile akuamini kuwa huyu ndie yule Sebastian alie msababishia anguko kubwa, “kaka kipigo hicho, huyu jamaa aliiba pale mbezi mchana kweupe, watu wakamtengeneza” alisema mlinzi wa hospital alie kuwa getini, “naukome mbwa wewe bora ata wange kuuwa kabisa” alisema Adellah, huku akivulumisha kofi moja kali lililotuwa usoni kwa Daniel, “waap!” nacho kikalia “paaah!” ni wazi Daniel alipatwa na maumivu makali sana, mama Sam nisamehe mke wangu ni shetani tu alinipitia, aikuwa kwa akili yangu” alisema Daniel kwa kulalamika.


Hapo yakaanza maongezi mengine kabisa ya kuombana msamaha, kuona hivyo Seba akawashtua baraka na Vanesa, nao wakaondoka zao, wakiwaacha peke yao, wanaendelea na kuombana msamaha, “Adellah tuondoke bwana, ona sasa wakina Seba wametuacha, tunalazimika kutumia ela yatu kama nauli, alisema Sophia, huku anawachukuwa watoto na kuongoza kwenye kituo cha dala dala, wakati huo barabara ile ndiyo ilikuwa barabara kuu, na magari mengi yalikuwa yanapita. Hivyo wakaondoka zao wakimwacha Daniel pale pale hospital.


Naaam miezi mitatu mbele Adellah akiwa amesha kubari matokeo, alipata nauri kwa msaada wa dada yake, nauri ambayo ilitosha kupanda magari ya mizigo, na kurudi Lungwe, akimwacha dada yake, ambae sasa aliendelea kufanya kazi, huku akitumia kitumbua chake, kama njia ya ziada ya kujipatia fedha, kule kijijini Adellah, alinooshewa kidole na kila mtu, ata mabinti wadogo, wa miaka kimi na kumi na moja walihapa kuto kuiga mfano wa Adellah, ambae sasa aligeuka kuwa ubao wa mafunzo ya wanawake wangine, “usije kuwa kama Adellah” ndio msemo ambao angeambiwa binti au mwanamke ambae alionekana kuwa na mwenendo mbaya, au alikuwa anatarajia kusafiri nje ya lungwe.


Daniel baada ya kuachiwa pale hospital akuwa na sehemu ya kwenda, zaidi alikuwa anashinda pale stenfi stendi maili moja, akiomba misaada kwa raia wema, na wakati wmingine kupiga debe, akuwa na uwezo wa kutumia WTK, maana siyo tu kuogopakifo, au kujifunza kwa kile kilicho mtokea, ila pia, ni sababu, akuwa na uwezo kuiba wala kukimbia.


Songea nako, mambo yalikuwa moto moto, uzalendo ulimshinda George, ambae akujuwa kulima wala kuchoma mkaa, na kuamua kwenda kuomba msamaha kwa Seba, maana alikuwa anaitaji msaada wake, kwa hali na mali, ili angalau aishi maisha mazuri, “George, wewe ni kaka yangu hiyo aitokaa ifutike, niwe mzima au nimekufa, utabakia kuwa kaka yangu, ninauwezo wa kukujengea nyumba mjini, lakini kwa somo ulilonipa siwezi aya nitakusaidia kukununulia vitu na kukupangia chumba” alisema Sebastian ambae, akuna alie mlahumu, maana licha ya kusitisha msaada na huduma kwa mama yake mkubwa na George, lakini aliwa endelea kuwa hudumia Joyce na Ester, ambao ni watoto wa mama yake mkubwa, yani wadogo zake George, ambae sasa amrudi mjini, na kupata kazi ya kusafisha mazingira kwenye nyumba ya mzee Willison, yani baba yake Malaika, yule wa kwenye BIBI HARUSI MTARAJIWA.


Wakati huo bwana Philipo ambae aliamia bagamoyo, anaendelea na biashara ya duka, pale karibu na stand, watoto wake wawili wanaendelea kusoma vizuri, bado ajaowa maana ajaamini kama atakae muoa ata mwacha salama, yasije kumkuta kama yaliyowakuta wengine, japo juzi juzi ametoka kumwona Sebastian akiwa kwenye gazeti la mfanyakazi, akiwa amefunga ndoa na mmilikiwa kapumpuni ya V SUN OIL, “ama kweli nimeamini kuwa, mwenye bahati abahatishi” alisema Philipo, huku anatabasamu peke yake.


Naaam mpaka tunamaliza adithi yetu, tayari Vanesa alisha jifungua watoto mapacha, wakike na wakime, na sasa wanaishi kwenye nyumba kubwa ya ghorofa mbili, iliyopo mtaa wa songea club, wanaishi vizuri kwa raha na starehe, huku mama Seba nae akiaminia mjini mtaa wa mahenge, ambako sasa anaishi maisha mazuri ya kifahari, japo alishutumiwa na baadhi ya watu kwakukoto kumsamehe dada yake huku na yeye akisisitiza kuwa “mimi binafsi sina ugomvi na dada yangu nashangaa anakuja kuomba msamaha” lakini licha ya kusema hivyo alisha wafungia vioo, akuna msaada wala huduma, ila ndugu wengine na majilani, waliendelea kupata msaada kama kawaida, wakiwepo Joyce na Ester, wadada yake.


MWISHO.gao, kama vile akuamini kuwa huyu ndie yule Sebastian alie msababishia anguko kubwa, “kaka kipigo hicho, huyu jamaa aliiba pale mbezi mchana kweupe, watu wakamtengeneza” alisema mlinzi wa hospital alie kuwa getini, “naukome mbwa wewe bora ata wange kuuwa kabisa” alisema Adellah, huku akivulumisha kofi moja kali lililotuwa usoni kwa Daniel, “waap!” nacho kikalia “paaah!” ni wazi Daniel alipatwa na maumivu makali sana, mama Sam nisamehe mke wangu ni shetani tu alinipitia, aikuwa kwa akili yangu” alisema Daniel kwa kulalamika.


Hapo yakaanza maongezi mengine kabisa ya kuombana msamaha, kuona hivyo Seba akawashtua baraka na Vanesa, nao wakaondoka zao, wakiwaacha peke yao, wanaendelea na kuombana msamaha, “Adellah tuondoke bwana, ona sasa wakina Seba wametuacha, tunalazimika kutumia ela yatu kama nauli, alisema Sophia, huku anawachukuwa watoto na kuongoza kwenye kituo cha dala dala, wakati huo barabara ile ndiyo ilikuwa barabara kuu, na magari mengi yalikuwa yanapita. Hivyo wakaondoka zao wakimwacha Daniel pale pale hospital.


Naaam miezi mitatu mbele Adellah akiwa amesha kubari matokeo, alipata nauri kwa msaada wa dada yake, nauri ambayo ilitosha kupanda magari ya mizigo, na kurudi Lungwe, akimwacha dada yake, ambae sasa aliendelea kufanya kazi, huku akitumia kitumbua chake, kama njia ya ziada ya kujipatia fedha, kule kijijini Adellah, alinooshewa kidole na kila mtu, ata mabinti wadogo, wa miaka kimi na kumi na moja walihapa kuto kuiga mfano wa Adellah, ambae sasa aligeuka kuwa ubao wa mafunzo ya wanawake wangine, “usije kuwa kama Adellah” ndio msemo ambao angeambiwa binti au mwanamke ambae alionekana kuwa na mwenendo mbaya, au alikuwa anatarajia kusafiri nje ya lungwe.


Daniel baada ya kuachiwa pale hospital akuwa na sehemu ya kwenda, zaidi alikuwa anashinda pale stenfi stendi maili moja, akiomba misaada kwa raia wema, na wakati wmingine kupiga debe, akuwa na uwezo wa kutumia WTK, maana siyo tu kuogopakifo, au kujifunza kwa kile kilicho mtokea, ila pia, ni sababu, akuwa na uwezo kuiba wala kukimbia.


Songea nako, mambo yalikuwa moto moto, uzalendo ulimshinda George, ambae akujuwa kulima wala kuchoma mkaa, na kuamua kwenda kuomba msamaha kwa Seba, maana alikuwa anaitaji msaada wake, kwa hali na mali, ili angalau aishi maisha mazuri, “George, wewe ni kaka yangu hiyo aitokaa ifutike, niwe mzima au nimekufa, utabakia kuwa kaka yangu, ninauwezo wa kukujengea nyumba mjini, lakini kwa somo ulilonipa siwezi aya nitakusaidia kukununulia vitu na kukupangia chumba” alisema Sebastian ambae, akuna alie mlahumu, maana licha ya kusitisha msaada na huduma kwa mama yake mkubwa na George, lakini aliwa endelea kuwa hudumia Joyce na Ester, ambao ni watoto wa mama yake mkubwa, yani wadogo zake George, ambae sasa amrudi mjini, na kupata kazi ya kusafisha mazingira kwenye nyumba ya mzee Willison, yani baba yake Malaika, yule wa kwenye BIBI HARUSI MTARAJIWA.


Wakati huo bwana Philipo ambae aliamia bagamoyo, anaendelea na biashara ya duka, pale karibu na stand, watoto wake wawili wanaendelea kusoma vizuri, bado ajaowa maana ajaamini kama atakae muoa ata mwacha salama, yasije kumkuta kama yaliyowakuta wengine, japo juzi juzi ametoka kumwona Sebastian akiwa kwenye gazeti la mfanyakazi, akiwa amefunga ndoa na mmilikiwa kapumpuni ya V SUN OIL, “ama kweli nimeamini kuwa, mwenye bahati abahatishi” alisema Philipo, huku anatabasamu peke yake.


Naaam mpaka tunamaliza adithi yetu, tayari Vanesa alisha jifungua watoto mapacha, wakike na wakime, na sasa wanaishi kwenye nyumba kubwa ya ghorofa mbili, iliyopo mtaa wa songea club, wanaishi vizuri kwa raha na starehe, huku mama Seba nae akiaminia mjini mtaa wa mahenge, ambako sasa anaishi maisha mazuri ya kifahari, japo alishutumiwa na baadhi ya watu kwakukoto kumsamehe dada yake huku na yeye akisisitiza kuwa “mimi binafsi sina ugomvi na dada yangu nashangaa anakuja kuomba msamaha” lakini licha ya kusema hivyo alisha wafungia vioo, akuna msaada wala huduma, ila ndugu wengine na majilani, waliendelea kupata msaada kama kawaida, wakiwepo Joyce na Ester, wadada yake.


MWISHO.

Post a Comment

0Comments

Your Thoughts

Post a Comment (0)