TUMPE JINA GANI?

 TUMPE JINA GANI?


Tunasaka jina lake, kiumbe ale mgeni,

mie pia na mamake, twayatathimini

yapo majina ya kike, ya leo na zamani,

nishauri kwenye jina, tumuite tumudeke.


Sanura au Sunira, majina tuloyapanga,

Samira au Subira, lipi jema manyakanga?

Zuena, Zena, Zera, au Zuhura wa Tanga?

Nishauri kwenye jina, Zubeida na Zahira.


Tamara hata Tamira, Talia na Tamrina,

vipi Lena na Laura, Leyla hata Liana,

nambie kuhusu Lara, Tiana na Tatiana,

Nishauri kwenye jina, Lamania au Lina?


Tanasha au Natasha, Maisura na Melissa,

vipi Aisha na Asha, Faiza ama Hamissa,

Maria, Mima, na Masha, Naima ama Farissa,

Nishauri kwenye jina, Talisa au Vanessa?


Ninasihi kwa Ashura, Asinati na Latifa,

Naomba pia Shakira, Aliya hata Hanifa,

Kayla ama Debora, Noelina na Shanifa,

Nishauri kwenye jina, Nadia au Shalifa?


Sijasahau Munira, Maya,Muna na Rukiya,

Sonia Siena, Sara, Maimuna na Radhiya,

vipi Rita na Tahira, Amrina na Raniya,

Nishauri kwenye jina, Mira, Amira, na Miya.


Vipi kuhusu Jamila, Julia na Juliana?

ama Cindy na Sheila, Zuberi na Rujiana?

Cinderella na Shamila, Aziza na Severina,

Nishauri kwenye jina, Amina ama Asina.


Nambieni Rwaida, Rehema ama Tamima,

Epifania na Roda, Safarina na Salima,

Jessica au Saida, Angelina na Neema,

Nishauri kwenye jina, Malia ama Halima?


Niaje pia Habida, Farashuu na Habiba,

Raya, Nirrah na Ida, Hidaya hata Haiba,

Tumuite Zenaida, Lulu, Rubi ama Huba?

Nishauri kwenye jina, Vumilia ama Huda?


Mwisho nafukiza udi, haliudi kwenye Kona,

nakumbuka Waridi, Fauziya na Zarina,

vipi pendo na Zawadi, Khadija pia Fena?

Nishauri kwenye jina, Sabaha au Fiona?

       ©️2019

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Your Thoughts