NAISMA
SEHEMU YA KWANZA
Mtunzi: zamrata mbwana
No:+255698095257
NAISMA ni binti wa kiislamu ambae amelelewa kwenye Dini sana kwao wamezaliwa wawili yeye na mdogo wake anaeitwa Jasmini ambae amezalia nyumbani. Yani amepata mimba nakuzaa bila yakuolewa na alikatisha masomo yake alishindwa kuendelea na chuo .
Hivyo Basi Naisma alikuwa yeye peke ake ndo alie maliza chuo na kusimamia kampuni ya baba yake ilioitwa KIU ambayo ilijishugulisha na uzalishaji wa bidhaa ambazo walisambaza ndani na nje ya mikoa na kufika hadi inchi jirani nakupelekea kuwa maarufu Sana
Naisma anaendelea kufanya kazi katika kampuni ya Baba yake mzee Kazumali, na hapo mzee Kazumali anamuona binti yake kaelekea Yani anaweza kuongoza kampuni na anamua kumpandisha cheo awe kiongozi mkuu Yani yeye apumzike amuachie Naisma lakini anashindwa kukamilisha kwa sababu mwanae ajaolewa na anatakiwa ambae anandoa tayari.....
Naisma japo ni Binti mrembo wa kuvutia lakini hakuwai kuletewa barua ya uchumba hata ya bahati mbaya.kitendo kilicho waumiza Sana wazazi Wake wote wawili haswa mzee kazumali ambae ni Baba yake mzazi Naisma aliona mambo ayaendi
Haidary Frut ni kijana ambae anauza matunda ng'ambo ya barabara ya kampuni ya KIU ambayo ni ya kina Naisma ..
Haidary Frut akiwa anaendelea na biashara yake mida ya Asubuhi Mara akaona Gari limekuja kupaki karibia na meza yake ya matunda
Gafla moyo Wake ulilipuka "Paaaa!!!! Baada yakumuona Binti mzuri akishuka kwenye ilo Gari si mwingine Bali alikuwa Naisma kazumali . Alishuka ndani ya Gari na pocho lake na kuelekea kwenye meza ya matunda ya Haidary Frut .
"Ooh! Mambo mrembo? Karibu"
"Asante ! Samahani Kaka Mimi nahitaji machungwa mana nimejikuta nimeyamisi asubui asubui leo !
Naisma aliongea uku akichagua machungwa nakumpa Haidary ammenye . Haidary alifanya ivyo nakumpatia Naisma ambae akalipa ela nakuweka pochi yake pale kwenye meza nakuanza kuyala Yale machungwa baada ya mda kidogo alimaliza nakuondoka zake Naisma
Naisma alifika kazini na kuwasalimia wafanyakazi wengine ambao waliwai kufika kabla yake.
Wafanyakazi walikuwa wengi tu lakini wawili tu ndo walikuwa lafiki zake na Amewazoea ambao ni Tina na mkaka mmoja ambae alijiita Novo Berry ambae alipenda Sana mambo ya kike ya umbea umbea na kuchambana lakini Tina hakuwa na mambo mengi alikuwa kawaida tu
"Oooh !!! Boss Naisma !
"Oooh ! Novo ,Tina Wow !
Naisma aliwakumbatia Rafiki zake
"Mbona umechelewa shosti , Novo alimuliza Naisma
"Aaah! Nimechelewa Apo nje kwenye matunda !
"Wapi kwa Haidary Fruts ,!?..
"Sijui ata jina lake Yule Kaka sijui ndo anaitwa ivo !
"Atakuwa ndo uyo uyo bhna
"Aaah mda unazidi kwenda jamani badae tutaonana !
"Sawa !!
Naisma alielekea Ofsini kwake yani kwenye chumba chake cha kufanyia kazi zake
Nakuanza shuguli zake za Ofsini alifanya kwa mda na alitaka kuangalia saa kwenye simu yake
Ndipo aliposhangaa pochi vake haioni "Mungu ! Wangu pochi yangu !
Naisma alinuka nakutafuta sehemu zote za Ofsini na alienda kwenye Gari pia hakuona na alianza kulizia Hapo kazini kama kuna mtu kaokota Rafiki zake Novo pamoja na Tina walimsaidia kutafuta lakini hawakufanikiwa
Haidary Fruts wakati anaendelea na kuuza matunda alishtuka kuona pochi ya yule Dada Naisma na kuliweka vizuli uku akiamini kuwa angeludi kulichukua
Naisma alikata tamaa ya kupata pochi lake hakuwa na wazo kabisa Kama aliliacha kwa Haidary Fruts .
Mda wa kuludi nyumbani ulifika na kila mfanya kazi wa KIU alijiandaa kuludi nyumbani "Pole Nai ! Baazi ya wafanyakazi wenzie walimpa pole kitendo kilicho mfanya azidi kujisikia vibaya
Novo pamoja walikuja kumuaga Rafiki Yao kwajili ya kuondoka
Walitoka nje ya ofisi walivuka barabara
"Enhe ! Twende tukanunue matunda kwa Haidary Fruts !
Novo berry aliongea uku akiongoza kwa Haidary Fruts
"Jamani Novo ! Tutachelewa !
"Mh ! Tina acha kujishauwa ndo kwanza saa 12 kasoro mbona tunatokaga adi saa 1 na nusu apa !
Walishafika kwa Haidary Fruts na walimkuta anamenya menya machungwa
"Oooh ! I do Fruts !
"Novoo ! Nambie mshikaji wangu !!
"Poa tu ! Naona mishe zinaenda ! Embu tukatie matunda !
Novo pamoja na Tina walichagua matunda na kuanza kula uku wakipiga stori
"Da ! Nimekumbuka mshikaji wangu! Novo Kuna Dada mrembo alikuja Asubuhi kununua matunda kwa bahati mbaya amesahau pochi yake !
"Pochiiiiii !!!!! Ipo wapi ?
Novo pamoja na Tina waliuliza kwa pamoja
"Khe mbona mmeshtuka hili apa !
"Ooh ! Ni la Naisma ! Nov..khe ! Yupo wapi !
Mda huo huo Novo alishavuka barabara Zamani kwenda kumuita Naisma . Baada ya dakika kazaa Novo pamoja na Naisma walifika huku wakiwa wanahema
"Haya nipe pochi yangu upesi ! Mwizi kubwa we !
Naisma alisema kwa hasila mno na kuwafanya wenzie washangae haswa Haidary Fruts
"Mh ! Dada samahani kwani Novo amekufikishiaje Taarifa ?
"Ivyo ivyo unavyojua wewe ! Na mimi ndo najua !
Naisma alijibu uku akimuangalia Haidary Fruts kwa Zalau
"Mh ! Naisma usinigombanishe na majirani zangu! . Novo alijibu uku akimuangalia Haidary Fruts
"Nipe pochi yangu upesi we ! Usinitole tole macho hapa !
"Sawa! Dada pochi yako hi yapa
Haidary Fruts alitoa pochi na kumkabizi Naisma . Naisma alikagua na alikuta vitu vyake vipo vile vile
"Oh! Bahati yako vitu vyangu vimetimia vyote ! Cha kukusaidia tu ! Ukome kuwachukulia wateja mapochi siku nyingine !
"Mh! Ok!
Haidary Fruts akutaka kugombana na Naisma alitikia tu uku akimuangalia usoni
"Oh ! Mungu wangu ! Yani Rafiki angu Naisma sikuzote ujui kuongea kabisa ! Yani bado ushukuru umempata pochi yako ndo kwanza unatoa maneno machafu ! Ushukuru tu umempata uyu kaka mstarabu angekuwa mwengine asinge kupa !
Novo alimchana Rafiki yake Naisma hapo hapo mbele ya Haidary Fruts
"Nitolee mie !
Naisma alijibu na kuondoka zake bila ya kuaga . Na kuwacha wenzie wakimshangaa
Naisma alitoka hapo akiwa na hasila aliludi Ofsini lakini alipofika Ofsini aliachia Tabasamu baada ya kumuona mpenzi wake anaeitwa Lamek
"Wow mpenzi !
Walikumbatiana kwa furaha ....
Naisma aliachia Tabasamu baada va kumuona mchumba ake Lamek na kukumbatiana nakuongozana kwenye Gari ya Naisma na Lamek alimpeleka Naisma adi kwao na kumuacha nje ya Geti na baadae Lamek aliondoka. Uwo ndo ulikuwa utaratibu wao wa kila siku kati ya Naisma na mchumba ake Lamek
Naisma aliagana na mchumba ake Lamek na kuingia ndani alivyofika sebleni alikutana na wazazi Wake wote wawili Baba na Mama yake pamoja na mdogo wake Jasmini
Shikamoo ? Baba na Mama
"Marahaba ! Ujambo !
"Sijambo !
"Za kazini !
"Mzuri tu !
"Mambo Jasmini !
"Poa ! Dada shikamoo ?
"Marahaba !
Naisma alianza kupiga hatua kuelekea chumbani
"Samahani Binti yangu Naisma namazungumzo na wewe !
Naisma aliludi na kukaa kwenye kiti kimya kwaajili yakumsikiliza Baba yake
"Naisma mwanangu huyo kijana ambae upo nae lini atakuletea barua ya posa hapa Nyumbani ? Uoni kama anakupotezea mda tu ! Na sio muoaji ? !!!
"Baba! Lamek kasema atanioa bado anajipanga kwanza !
"Lini ? Hadi lini ataendelea uko kujipanga ? Mwaka wa pili huu au unataka na wewe uzalie Nyumbani Kama mdogo wako Jasmini ?
Baba Naisma aliongea kwa hasira huku akipiga meza Hadi wote walishtuka . Nakumfanya Naisma kukaa kimya uku akiwa kainamia chini.
"Basi mmewangu inatosha !
Mama Naisma ilibidi aingilie Kati ilikumtuliza mumewe na mumewe akaenda chumbani na yeye alimfata sebleni akabaki Naisma na Jasmini
"Samahani Dada ivi unazani Lamek atabadili Dini na kukuoa wewe ! ?
" Ndiyo kwanini asifanye ivo na wakati ananipenda Sana !
"Mh ! Kwa mie mdogo wake atasilioni ilo kwa Lamek , kwa ushaurii wangu we tafuta tu ! Mwanaume mwengine atakae weza kukuoa na sio uyo ! Hakuna muoaji apo !
" Samahi Jasmini tena uishie apo apo we ! Mtoto Lamek ndo mwanaume nilie mpenda Mimi na ndo atakae nioa ! Nimemaliza ! Kwanza sijaomba ushaurii wako kitu mnachojua umeshindwa kumaliza chuo na umezalia nyumbani ! Kama ungekuwa unajua mahesabu ya ndoa vizuri saizi ungekuwa kwa mumeo "?
"Dada Mimi sawa nimekosea nakubali sitaki pia na wewe ukosee Dada angu ! Usije ukapigwa na kitu kizito Lamek nani ? Asiyemjua ni mwanaume wa kuuza sura mitandaoni hakuna muoaji pale !
"Eeeee!!! Tutaona pale atakapo nioa Lamek wangu wanafki Sura zitakavyo washuka !
"Sawa ! Tutaona na kwamnavyomjua uyo Lamek akikuoa niite Mbwa ! Nakaa Pale !
Naisma aliishia tu kumuangalia tu mdogo wake Jasmini na kumuona kamuaribia siku alitoka sebleni na kuelekea chumbani. Ambako alikuwa ana lala na Jasmini lakini vitanda tofauti na alimkuta mtoto wa Jasmini amelala ambae.
Naisma alichukua simu yake nakumpigia mpenzi wake Lamek
"Hello my love !
Naisma alipokelewa na sauti ya Lamek ambayo ilimsisimua na kusahau shida zake zote
"Samahani my love kesho tunaweza kuonana nikitoka kazini !
"Oooh ! Kipenzi natoa wapi ? Jeuri ya kukukatalia !
"Sawa love ! Usiku mwema ! Mmwaaaaaa !
Lamek ni kijana Handsome pia anaumbile la kuvutia pia ni mtu wa mtandaoni Sana huwa anashuti nyimbo mbali mbali za wasanii huwa wanamuita na baadae hulipwa. Pia huitwa kwenye maonesho ya nguo za kiume yani ni ni Model.
Haidary Frut ni kijana Handsome pia ni mpole pia mwenye kujali Sana. Ni kijana anaeendesha maisha yake kupitia biashara yake ya matunda na amepanga.
Haidary Frut aliludi kwake na kwenda kula mgahawani na kuludi akaoga na kutaka kulala Gafla alikuja lafiki yake anaeitwa Fahadi ambae alizoeana nae nakuwa Kama ndugu ila Fahadi alikuwa mvulana mdogo kidogo tofauti na Haidary Frut.pia Fahadi bado anakaa kwao na huwa anakuja kulala kwa Haidary Frut siku moja moja .Alimkuta Haidary Frut anataka kulala
"Aaah ! I do braza wangu !
"Oooh! Fahadi mdogo wangu afazari umekuja ! Yani unazingua na wewe mda mwengine ! Kwanini usiamie tu !
"Aaah ! Niamie tena Kaka sikuakija Mwajuma Ndala ndefu je ?
"Da ! We acha tu mdogo wangu ! Mwajuma si kanikataa mwenzio !
"Khe ! Unasema kweli bro !
"Kweli Fahadi siku iyo kaja ndo kaja kunambia kuwa anataka kuolewa na mtu mwingine ! Nikambembeleza Sana nimuoe kanambia awezi kuolewa na Mimi muuza matunda ni aibu kwake !
"Du !!! Bro ndo ilivyokuwa Pole Sana ! Atamimi nimesikia tetesi izo pia Kama anataka kuolewa!lakini usiwaze Sana utampata mzuri zaidi yake ,! Kwanza Yule akuwa mwanamke sahihi kwako mpenda vigoma kila wiki sale vijora na vitambaa alikuwa anakukudisha nyuma tu kimaendeleo utampata mwengine tu achana naye !
"Sawa ila yalionikuta kazini leo natamani ungekuwepo mdogo wangu !
"Yapi Tena ? !!!!
"Leo Asubuhi alikuja mdada mrembo (........….)
Haidary Frut alimuadisia Fahadi yote yaliyotokea Kati ya yeye na Naisma
"Du ! Ndo ilivyokuwa hivyo ! Pole Sana .
"Ila toka nilivyomuona Yule Dada nimetokea kumpenda hatari ! Kaningia moja kwa moja kwenye moyo ikiwezekana nimuoe kabisa !
"Hahahaha ! Haidary bhna usitake kunifurahisha Kama kakukataa Mwajuma muuza sambusa atakukubali Naisma Boss Kama yule ! Watu Kama wale wanakuwa na wanaume wenye hazi zao ! Wanawake wazuli utaishia kuwaita shemeji tu !.
"Tatizo moyo umependa Fahadi mdogo wangu !
"Uwo moyo wako ! Unawazimu kaupigishe mswaki ulale !
…….............
Naisma alienda kazini siku iliyofata na alimaliza mapema na jioni alikuja Lamek kumfata na wakatoka wakaenda ufukweni mwa bahari .
"Mh ! Nakusikiliza mpenzi wangu ! Naisma ulicho niitia
"Lamek wazazi wangu wananisumbua wananiambia niolewe kila siku sina mwanaume mwengine mnaempenda zaidi yako wewe ! Lamek je ? Upo tayari kubadili Dini na kunioa ?
Lamek alikuwa kanyamaza kimya kwa mda huku akimuangalia Naisma usoni lile Tabasamu lake Gafla lilipotea .....
"Lamek upota tayari kubadili Dini iliunioe mbona unijibu mpenzi wangu ? !!!!
"M.m.m m. Ndi .ndi.ndiyo mpenzi nitafanya Ivo unavyotaka !
"Waoooo!!!!! Baby mmwaaa
Naisma alifurahi Sana alivyokubali mpenzi Wake Lamek kuwa atamuoa japo Lamek alionekana uitikiaji wake wa mashaka Sana
Naisma aliludi kwao akiwa na furaha Sana alimkuta mdogo wake Jasmini akiwa kamkumbatia mwanae alifika na kumchukua mtoto wa Jasmini na kumkumbtia
"Ma mkubwa ! Mmwaaaaaa
"Khe! Dada mbona unaonekana mwenye furaha Sana ? !!!!!!!
"Uwezi amini mdogo wangu Lamek yupo tayari kubadili Dini na kunioa !!!
"We !!!!!!!!! Lamek ndo kasema Ivo ? Dada
"Ndiyo !!!!!
"Weeeeee !!!!!
"Waoooo mdogo wangu njo nikukumbatie
Naisma alimkumbatia mdogo wake. Mda huo huo walikuja wazazi wao Mama na Baba yao
"Khe ! Mbona mnafuraha Sana ! Kuna nini?
"Baba Lamek amekubali kubadili Dini na kumuoa Dada Naisma !
"Khe ! Kumbe je ? Nitaarifa za kweli izo Binti yangu ? Naisma
"Ndiyo Baba nikweli
"Oooh Hongera Binti yangu ni habari njema izo afanye upesi alete iyo barua !!
Furaha ilitawala umo ndani Sana kwa Naisma alikuwa Kama anijiona siku anayovaa shela
.........................................................
Upande wa Haidary Frut aliamka yeye na mdogo wake Fahadi . Fahadi alikuwa wa kwanza kwenda chooni kuoga iliwajiandae waende kwenye kazi Yao ya kuuza matunda .
Haidary Frut akiwa kalala mlango uligongwa kwa Nguvu Adi Haidary Frut alikulupuka usingizini akiwa na Bukta tu
"Kalibu pita !
Haidary Frut hakuamini macho yake baada ya kumuona X wake Mwajuma "Paaaaa!!!!!
"Mwajuma mpenzi wangu ! Karibu nilijua tu ! Uwezi kuniacha ungekuja tu !
"We!!! Ukome 👌mpenzi wako Nani !! ? Nimekwambia nakutaka mie ? Mguu huu nimekuja kuchukua kitenge changu pamoja na kanga angu ! Na siokuja kuangalia uwo uso wako mbaya !
"Mwajuma mpenzi wangu! Mie Bado Nakupenda na nipo tayari kukuoa !
"Hahahaha ! 😅 Nicheke kwanza
Haidary Frut alipiga magoti na kumuomba Mwajuma wawe tena wa penzi . Uku machozi ya kimtoka
"Niambie Mwajuma nini kikubwa nilicho kufanyia Hadi unihukumu ivi ? Mbona kila kitu ulichoniomba nilikupa sare za kwenye vigoma nilikukatia hela ya saluni nilikupa ! Kubandika kope, Ela ya matumizi na vigoma zote nilikupa !!
"Bhna ! Wewe muuza matunda ni aibu kwangu ! Kuolewa na muuza matunda Mwajuma mtu maarufu eti niolewe na Haidary muuza matunda ! Mie mwenyewe muuza miguu ya kuku ! Wewe unauza matunda bora ya uyu daleva wa Tax !
"Tatizo sina elimu Mimi ya kutafuta kazi ya Mana! Nilisoma hadi kidato cha nne na Bibi yangu hakuwa na uwezo wa kunisomesha japo nilifaulu vizuli wazazi wangu walifsriki toka nipo mdogo sana ndo Bibi akanilea Sina ndugu yeyote Yule ! Wewe ndo nakutegemea tuanzishe familia ! 😭
"Msiuuuuu! Nipishe mie !
Mwajuma alimsukuma Haidary Frut ambae alimshika Mwajuma miguu . Alichukua kitenge chake na kanga yake na Alitoka nje ambako alikutana na Fahadi uso kwa uso na Mwajuma alomsonya Fahadi na kuondoka zake
Fahadi alingia ndani nakumkuta kaka ake Haidary akiwa chini analia.
"Pole Kaka yangu !
"Fahadi Mwajuma kanambia Mimi maskini muuza matunda tu ! Yani sina thamani yakuwa nae !!!
"Apana ! Yani yule Demu nilitamani nimpige makofi Hana adabu hata kidogo !
"Ndo Ivo utampata mwengine tu ! Atakae kupenda kaka angu yule Demu alikuwa miyeyusho tu ! Kila siku anaomba ela ya sale za vijora tu! Kwenye vigoma bola aende zake tu ! Na aliemuoa kapata asala !!!!
"Da ! Ila inauma mshikaji wangu usiombe yakukute Mambo aya !
"Aaaaaah si umkubalie tu yule muuza sambusa !!!!!
"Nani ? Salma ?
"Ndiyo au unaonaje ? !!!
"Aaa! Fahadi bhna ! Nimetoka kwa muuza miguu ya kuku, leo niende kwa muuza sambusa atakama nanyota ya punda sio kiivyo !
"Wewe unachofanya ni kumkomesha tu ! Mwajuma
...............................................
Asubuhi na mapema Naisma alimka na kupata Chai ya Asubuhi na kujiandaa kwa jili yakwenda kazini na Alifika kazini . Alivyofika Getini akakutana na Rafiki zake Novo pamoja na Tina
"Waoooo !!!!!!!
Walikumbatiana kwa Pamoja
"Khe ! Shosti mbona unaonekana mwenye furaha Sana !
Novo aliuliza uku akimuangalia Naisma usoni.Naisma ambae alishindwa kuzuia Tabasamu lake
"Yani mnafuraha kweli wala sio masiara Rafiki zangu !
"Mh ! Ipi iyo shosti !
"Mhh! Ni hivi Lamek amekubali kubadili Dini na kunioa !
"weweweeeee!
Tina alinza kupiga kelele uku akimkumbatia shoga ake Naisma .
"Eti Nini ? !!! Ni masikio yangu ! Ama naota ! Au maskio yangu mabovu ?
Novo alisema hivyo uku akiacha kuchezea simu ilibidi Tina ajibu yeye
"Ni hivi 👌hapa 👉shosti wetu anatarajia kufunga ndoa na Lamek siku si nyingi !!
"Eeeh !!! Mungu wangu ! Tarifa hizo we umezitoa wapi Naisma ?
"Mwenyewe kwa kinywa chake ndo kanitamkia !!!!
"Mh usiwe umemlazimisha akubali maana Lamek mwenyewe !
"Enhe! Ushanza Novo Berry usitake kumtoa Naisma kwenye Mod yake
"Ooh na anapiga! Lamek , Hello mpenzi !
Naisma aliongea uku akipandisha ngazi gorofa ya juu kuelekea Ofsini kwake uku akimuacha Tina pamoja na Novo
...................................
Hatimae mda wa lunch ulifika Naisma aliwafata Rafiki zake Novo pamoja na Tina kwajili yakwenda kula chakula cha mchana kabla hawajaenda kula Novo aliwataka Naisma na Tina wamsindikize kwa Haidary Frut kununua Ndizi
" Kha ! Haidary Frut sindo alioniibiaga pochi yangu uyo ?
"Apana Naisma ! Hakuona alikuifazia tu nakuomba twendeni bhna !
"Mh ! Sawa
Naisma alikubali nakuongozana Adi kwa Haidary Frut . Haidary Frut akiwa bize nakumenya machungwa yeye na mdogo wake Fahadi "Paaaaa!!!!! Moyo wake ulishtuka baada ya kumuona Naisma
"Mambo Haidary Frut
"Po.po poa !
Novo alimsalimia Haidary Frut
"Ona kule 👉 Haidary,Naisma anakuja
Fahadi alimwambia Haidary Frut uku waliendelea kumenya matunda
"Habari zenu ! Jamani !
"Safi tu!
Novo alisalimia waliitikia wakina Haidary
"Mambo ! Mrembo Naisma
"Msiiuuuuuuu!!!
Haidary Frut alimsalimia Naisma na aliambulia sonyo Adi Haidary Frut akajikata mkononi
"Yalaaa !!! "
"Kaka Haidary Pole !
Fahadi alisema ivo uku akichukua leso na kumpa Kaka yake Haidary
"Niko sawa yote ni kwaajili ya Naisma sijui kwanini ananichukia ivi "
Naisma alimkazia macho Haidary . Lakini haidary hakuogopa aliendelea kumkazia macho pia Naisma adi akaona aibu nakuangalia pembeni
" Waoooo ! Inapendeza ! Ni hivi Haidary Frut amejikata na kisu kisa lafiki angu Naisma kampa jibu baya ! Oooh mzani umekaaje apo mmm !!!!
Tina aliongea uku akila chungwa
"Mmmh !!!!
Novo berry aliishia kuguna tu
"Embu nyie watu ? Hamjamaliza tu kununua Ayo matunda Mimi naondoka zangu !!!!
Naisma alisema ivo kwa hasila uku akiwangalia Rafiki zake
"Oooh tayari Haidary nifungie izo Ndizi Apo 🍌 "
Novo aliongea uku akiwa anatafuna Ndizi zingine mdomoni upesi upesi akachukua na kuondoka
Haidary Frut alianza kuugulia maumivu baada ya kuona wakina Naisma wameondoka
"Yalaaaa !
"Khe ! Hahahaha Kaka pole
........,............
Naisma aliludi Ofsini baada ya kumaliza lunch akiwa na hasila mno . Mda wakuondoka alikuja mpenzi wake Lamek Kama kawaida yake nakumsindikiza . Naisma alifurahi Sana
Lamek baada ya kumsindikiza Naisma alirudi kwake .
Akiwa anakaribia Nyumbani kwake alipopanga Nyumba mzima
🏠 Alishangaa kuona taa ikiwa inawaka alishtuka nakuwaza au mwizi kaingia alianza kupiga hatua kwakukazana alingia ndani Gafla
"Honey !!!!!!!!!!!!!!!!
Alishtushwa na sauti ya Warda ambae ndo mpenzi wake aliekuwa nae kwa mda mrefu kabla ya Naisma.
Ila Warda alikuwa anafanyakazi marekani kwenye kampuni aliajiliwa uko alikuwa analudi mala moja moja Tanzania ata Apo alipokuwa anakaa Lamek na kumleta Naisma kulikua kwa uyo Warda ndo alipanga yeye nakulipa Kodi
"wa.wa.Warda . !!!!!!!!!!!
Lamek alibaki na mshangao wa Hari ya juu baada yakumuona mpenzi wake Warda
"Waoooo ! My Love I miss you !!!!
Warda alimkumbatia Lamek ambae alikuwa amesimama tu asijue anzie wapi
"Oooh ! Baby mbona upo unafuraha Nini shida ?
"Aaaa! Mimi !
"Come baby I'm looking you
Warda aliongea kingreza chake kiswahili aliona shida kutumia mala kwa mala kwani marekani alizoea kuongea Sana lugha ya kingreza .Walikaa kwenye Sofa uku Warda akimuangalia Lamek
"Mh! Tell me ! My love
"Mh ! Amna nimefurahi tu ! Kukuona mpenzi wangu
"Oooh ! I'm happy ! But Hongera kwakuwa maarufu zaidi mpenzi wangu ! Na nimekuletea nguo ambayo wanavaa masupa staa wa marekani ni milioni mbili kwa bei ya kitanzani !
"Waoooo!!!! Baby kweli ?
"Ndiyo Haney! Na kesho mtakufanyia shopping kila kitu ambacho hakipo ndani !!!
"Jamani Asante Warda wangu !
Lamek alimkumbatia Wa
Your Thoughts