NAISMA 2
Mtunzi: Zamrata mbwana
No: +255698095257
Hatimae ni muda wakuondoka Nyumbani na kila mfanya kazi alijiandaa kuondoka zake Naisma alikuwa nje ya Ofisi akimsubili Lamek
"Vipi shosti mbona umesimama Kama trafki !? Kulikoni ?
Novo aliuliza kabla ajajibu ilikuja Gari ya Lamek
"Oooh ! Ni Lamek !
"Mh !
Novo aliguna uku akiwangalia na Hapo Hapo Tina alikuja na Naisma alienda kumkumbatia Lameck
"Enhe ! Novo si unaona 👉 walivyo pendezana ! Alafu oooh Haidary ! Yani wenye wivu wajinyonge mwaka huu !
Tina alimaliza kusema Ivo na kuondoka Novo Alichukia na aliwapita Lamek Pamoja na Naisma Kama ajawaona
"Yani huyu rafiki ako Novo ata simuelewagi Kama anakachuki fulani na Mimi uyu !
"Aah! Achana naye ! Ana Mambo yake tu kichwani !
Naisma aliongea uku akishuka mikono ya Lamek
"Twende tutafute sehemu mzuli baby tuongee !
Naisma akimwambia Lamek
"Mh ! Unajua ! Baby saizi nipo bize Sana Ivo tutafute siku nyingine !
"Sawa Basi nisindikize hata Nyumbani !
"Jamani si nimekwambia nipo bize mbona uelewi Naisma !
"Du! Yani Lamek atasikuelewi sikumbili izi umebadilika Sana ! Na Nyumbani wananiuliza kuhusu wewe na wewe umenibadilikia !
"Bhna achana na Mimi ! Ushaanza habari zako
Lamek aliongea Ivo nakupanda Ndani ya Gari nakuondoka zake !
"Mungu wangu ! Lamek ! Lamek !
Naisma aliita lakini Lamek akutaka atakugeuka na Naisma alichuchumaa nakuanza kulia kwa uchungu. Gafla alishangaa akipewa leso alipokea nakuanza kufuta machozi . Aliinua sura iliamuone aliempa leso na hakuamini macho yake alipomuona Haidary Frut
"Haidary !!!!
"Aaaa!!!! Kho ! Kho !
Haidary Frut akua na lakuongea zaidi alijikoholesha
"Shika Leso yako ! Nasitaki mazoea na watu Kama Wewe ! Sijakwambia naupungufu wa Vitamini A !
Haidary Frut alinyong'onyea na kuchukua Leso yake kwa huzuni na Naisma alipiga hatua na kupanda kwenye Gari lake nakuondoka zake
...................................
Siku iliyofata Naisma alienda kazini na alivyofika alishangaa kukuta uwa zuri likiwa mezani kwake Ndani ya Ofisi 💐
Akiwa anashangaa shangaa akaona na kadi iliyo andikwa
I LOVE YOU NAISMA💌
Aliisoma huku akitabasamu mda huo huo walikuja Rafiki zake Novo berry na Tina
"Oh! Kulikoni shosti ! Mbona makopa kopa !
"Yani amuwezi amini Lamek ameamua kunifanyia suprise ! Jamani Kumbe nilikua namfikiria vibaya bure ! Kumbe ananipenda tu !
"Unauhakika gani ? Kama ni Lamek alietuma Ayo maua !
Novo aliongea uku akimuangalia Naisma usoni!
"Oooh !!!! Novo berry Hilo ndo jibu Best !
Naisma alijibu kwa kulinga nakuchukua Simu nakumpigia mpenzi wake Lamek
"Asante !!! Baby jamani !!!!!
"Asante !!???? Ya Nini !?
"Khe! Kwani ujanitumia maua ! Saizi Asubuhi hii?
"Aaaa ! Naisma sijuiata unazungumzia Nini ni msumbufu tu !
Lamek alikata Simu na kumuacha Naisma ambaye alibaki na bumbuwazi na aliweka Loud speaker . Wenzie walibaki wakimuangalia uku vicheko vikiwa vimewabana na kilamtu alizuga na Naisma aligundua ilo nakuwatolea macho
"Nasema tokeniiii !
..............................
Lamek akiwa na mpenzi wake Warda huku mahaba Moto Moto na leo walikuwepo kwenye fukwe za bahari wakipiga picha za mahaba.
"Baby Lamek siku si nyingi nataka tuandae party na univeshe pete yakutoka uarabuni ya gharama nataka nitikise vichwa vya udaku kwa kutrend ukizingatia wewe ni maarufu baby !
"M.m.m.m sa.wa..
🍊🍊🍊🍊🍊🍊🍊🍊🍊🍊
Hatimae jioni ilifika na Naisma alijiandaa kuondoka kutwa mzima hakuona Simu ya Lamek na siku iyo alipanga aende kwa Lameck wakaongee vizuri na aliwaomba Rafiki zake Novo pamoja na Tina wamsindikize . Walipanda kwenye Gari na walifika Hadi kwenye Nyumba waligonga hodi na walikalibishwa Hadi sebleni
"Kalibuni !
"Asante !
"Mh ! Niwasaidie Nini ?
"Samahani Dada hii nyumba alikuwa anakaa kaka mmoja anaeitwa Lamek ! Sijui amehama maana alikuwa msela tu
Ooh! Apana ajahama yupo !
"Wewe ni Nani yake !!!
Novo alidakia na kumuuliza Warda
"Oooh ! Mimi ni mpenzi wake !
"Tobaaaaa !!! 🤭 !
Mda huo huo Naisma alichenji moyo ulimuenda mbio kijasho chembamba kilimtoka
"Ngoja niwaitieni ! Baby baby Lamek !!!!!
Sauti iyo ilipasua moja kwa moja Ndani ya moyo wa Naisma ambae mapigo ya moyo yalianza kwenda kwa Kasi uku kijasho chembamba kikianza kimtoka
Lamek Alitoka akiwa kavalia taulo
"Tobaaa !!! Mtoto mwanahizaya uyu muone 👌
Aliongea Novo berry huku akisimama nakujishika kiuno.Lamek hakuamini macho yake baada ya kumuona Naisma yupo pale
"Na.na.na.aa
"Lamek ! Wewe ndo wakunifanyia ivi Mimi ? Umekosa Nini kwangu ?
"Ni.mi.i
"Eee ! Nyie akina Nani? Mbona siwaeleweni ? Mmekuja nakuanza kumshambulia Baby Wangu !
"Ni hivi uyo unae muita baby wako! Na Rafiki etu nae ni Baby wake na aliahidi atamuoa siku si nyingi !
Tina alimjibu Warda ambaye alibaki kushangaa
"Khe ! Yani Lamek kujitaidi kote kukuhudumia ! Leo ndo unanifanyia haya ! Kukupa pesa zote zile ,kukupangia nyumba bado unaniona Mimi mpumbavu Lamek !!! ?
Warda aliongea uku machozi ya kimtoka
"Sawa ! Isiwe mie ndo chanzo cha kuwagombanisheni ! Kwaheri Lamek ! Asante kwa maumivu haya !
Naisma aliongea maneno hayo uku alianza kulia kwa kwikwi nakukimbilia nje ya Nyumba
"Yani wewe Lamek ! Wewe wakumchanganya shoga etu na mshangazi ! Kama ! Loh ! Umtakii kheri ! Rafiki etu ! Yani mie ndo Novo berry nisikuone ! Yani nisikuone kabisa kalibu na Naisma kuanzia Leo ! Utajuta nakwambia !
"Basi Novo tuondoke !
"Embu subiri ! Tina imeniuma Sana Naisma Anampenda Sana uyu jamaa sio amfanyie haya !
"Sasa utafanyaje? Nando kashayafanya !
"Au nimuashe ata ngumi ! Izi Zalau !!!
"A.a.aaaa
Lamek alikimbilia chumbani Baada ya kusikia Novo anataka kumpiga.Tina alimvuta Novo nakuondoka zao
"Unakimbilia uko chumbani kwako ? Yani hakikisha ukitoka unatoka na begi lako tu kila kitu nilicho kununulia Mimi kiache umu umu !
"Jamani ! Baby usinifanyie Ivo ! Ngoja nikuelezee vizuri !
"Yani sitaki ! Masihara kumbe sikuzote unaniongopea nasema ! Tokaaa!
🍉🍉🍉🍉🍉
Novo berry pamoja na Tina walifika nje lakini hawakumkuta Naisma wala Gari yake na walivyotaka kumpigia wote Simu zao zilizima chaji
Naisma alienda kwao na kuwaacha Rafiki zake . Aliludi kwao uku akiwa analia adi ndugu zake wakabaki na mshangao . Naisma alikimbilia moja kwa moja chumbani na kujifungia mlango
Wazazi Wake walipigwa na butwaa mda huo huo walikuja malafiki zake Novo pamoja na Tina nakuwaelezea jinsi ulivyo kuwa na Baba yake Naisma Mzee Kazumali alikasirika Sana
"Kuanzia Leo sitaki kusikia habari za Lamek Ndani ya Nyumba yangu !
Mzee Kazumali aliongea kwa sauti Adi mwanae Naisma alisikia chumbani na Alitoka uku akiwa analia na kumkumbatia Baba yake
"Usilie mwanangu utampata mwengine Alie Bora kuliko uyo Lamek!
"Sawa Baba !
🍊🍊🍊🍊🍊
Siku kazaa zilipita na Naisma alikuwa bado anamaumivu yakumfunia mpenzi wake Lamek
Akiwa amekaa Ofsini hana ili wala lile alishangaa kuona maua ya kiletwa alikuwa kayabeba Novo berry uku akiwa na Tabasamu Pana
"Novo berry !!! Umeniletea zawadi ya maua !!!!
",Apana sijakuletea mie Bali nimeagizwa !
"Umeagizwa na Nani ? Na Lamek ?
"Kha ! Yani Naisma usitake kunitibua ! Yote aliokufanyia bado unapata Nguvu ya kumtaja uyo mtu !!
"Sasa kakutuma Nani ? Au ndo wasikuile ?
"Enhe ! Kumbe unaakili eee !!! Uyo uyo
"Mmh ! Anaitwa Nani ? Au ni Boss gani ? Au mtu maarufu maana ana supls ! Atali
Naisma alisema uku akitabasamu
"Basi kamuite !
"Kweli ?
"Ndiyo ! Au mtaje
"Apana kwa kumtaja Apana Siwezi kumtaja !
"Sawa ! Mwambie aje nikutane nae !
"Sawa!
Novo alienda kumpanga uyo mtu anaeleta maua kwa Naisma na baada ya mda alikuwa kashafika mapokezi kwaajili ya kwenda kuonana na Naisma lakinialikuwa na wasi wasi Sana alikuwa ajiamini
Mda huo huo aliingia mzee Kazumali na macho ya Mzee Kazumali na huyo kijana ambae si mwingine Bali ni Haidary Frut yaligongana
"Shikamoo Mzee !
"Malhaba !
Wafanyakazi wote walimsalimia mzee Kazumali. Mzee Kazumali alimuliza Yule Dada wamapokezi " Yule kijana ni Nani ?
"Sijajua Boss . Novo ndo anajua Mana ndoamekuja nae ! "Sawa!
Baada ya mda kidogo Yule kijana aliondoka.
"Enhe Novo kunakijana alikaa Apo na nimesikia wewe ndo unamjua enhe ! Ninani !?
"Ee.ee.e kijana yupi Tena !
"Novo yule kijana ulieingia nae mda ule alivaa shati jeusi !
Alidakia Dada wamapokezi nakumfanya Novo abaki kimya na kukodoa macho tu asijue cha kusema
"Mbona ivo Novo au kuna kitu unanificha !
"Amna Mzee tatizo ni stori ndefu !
"Okay ! Anza kunihadithia !
"Ni hivi Yule kijana ambae ukiniona Pale anaitwa Haidary Frut (...............)
Novo alimsimulia Baba yake Naisma ambae alikuwa anakalibia kustafu na alimuachia majukumu ya Ofisi mwanae Naisma lakini ilitakiwa aolewe kwanza Naisma ndo akabiziwe Rasmi kampuni
"Okay ! Nimekuelewa vizuli Novo unamaanisha Yule kijana Anampenda Sana Binti yangu Naisma ?
"Ndiyo Mzee ila ni fukara adi anashindwa kujiamini !
"Sawa !
🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺
Mda wa kazi uliisha na Naisma akimwambia Novo uyo mtu aliemletea maua akutane nae ufukweni na Naisma alifika na Alisubili Sana huku akiangalia saa yake ya mkononi na kuamua kuondoka ile anageuka tu . Haidary Frut uyo apo uso kwa uso
"Mambo !!
Haidary Frut alimsalimia Naisma uku akiachia Tabasamu Pana usoni mwake lililofanya azidi kuonekana Handsome zaidi
Kabla ajajibu Naisma Simu yake ya mkononi iliita na Novo berry ndo aliekuwa anapiga
"Enhe ! Novo nilikuwa nakumpigia ilinikuulize mtu mwenyewe mbona sijamuona mpaka saizi ! Mimi naondoka zangu !
"Anha ! Ujamuona Haidary Frut Apo ?
"Haidary Frut unamaana ? Yani unamaanisha mtu mwenyewe ndo Haidary Frut ?
"Eeh !
"Yani ! Hallo hallo !!!!
Novo berry alijibu Ivo na kukataa simu.
"Mh ! Embu Nicheke kwanza ! Kwaiyo wewe ndo uliekuwa unanitumia tumia vile viua vyako vya miambili miambili ?
"Samahani ! Naisma Mimi sijakuitia kuhusu Ayo maua Bali kuna kitu nataka nikwambie ! Kama utojali nakuomba !
"Enhe ongea fasta maana mda ushaenda ! Nataka niwai Home ! Now !
Naisma aliongea Ivo nakuwasha Simu yake na kuangalia saa
"Mh naomba tutafute sehemu mzuri tukae ndo tuongee vizuri !
Naisma alianza kumkata jicho Haidary Frut lakini haidary hakuogopa aliendelea kumkazia macho na yeye Adi Naisma akaona aibu nakuangalia pembeni
"Ongea apa apa nakusikia !
"Okay ! Ni hivi Naisma nimetokea kupenda Tena Sana nakuomba uwe mpenzi wangu I love you !
"Mh umemaliza ?
"Aaah ! Ndo Ivo Nakupenda Naisma nipo tayari kukuoa !
"Hahahaha ! Hii Kali ya mwaka ! Jamani Naisma kupendwa na muuza matunda ! Wewe Kaka Naomba usiendelee kunambia upuuzi wako ! Kwaheli
Naisma aliongea uku akipiga hatua nakuondoka zake . Haidary Frut alimshika Naisma mkono na kumvuta kifuani kwake Kama wanacheza songi la kihindi
!Paaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!
Kilikuwa ni kibao kilichosikika baada ya Naisma kumzaba Haidary Frut . Ambae bado alikuwa kamshikilia Naisma Adi watu waliokuwa kalibu Yao waliwageukia nakuanza kuwaangalia
" Niache ! Nakwambia niachilie niondoke ! Au wewe ni chizi Nini ?
" Ndiyo ! Kweli Mimi ni chizi ! Tena kwaajili yako ! Nakupenda mwenzio Naisma nihurumie Siwezi kuwa na furaha bila Wewe !
Haidary Frut aliongea ivyo na kupiga magoti uku machozi yakimtoka 😭 nakumuangalia usoni Naisma . Ambae kwake aliona Kama kelo
"Nihurumie Naisma Nakupenda nipe nafasi hata kidogo Basi! Hatakama Sina elimu hiyo sio sababu ya kushindwa kueleza hisia zangu kwako I love you Naisma !!
"Hahahaha ! Mungu Wangu ! Wewe iyangalie vizuri hii sura ! Ukome tena ukome ! Uone kama kituo cha polisi sawa! Koma!
Naisma aliongea Ivo na kumsukumiza Haidary na kuondoka zake
"Pole " "pole" "pole we Kaka jamani!
"Jamani natamani ningepata mwanaume Kama uyu Kaka anamapenzi ya zati Sana lakini Yule Dada hapendeki wenzie tunalilia bahati Kama izo !
Yalikuwa ni maneno ya mdada ambae na yeye aliangalia tukio zima na wengine walimpa Pole Haidary Frut
Haidary Frut aliinuka na kujikung'uta michanga ambayo ilimgandia uku akiwa analia kwa uchungu aliinua shati lake na kujifuta machozi uku akitembea kama mgonjwa nakuelekea kwake
🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
"Usiende bhna ! Novo please ! Utaalibu !
Ni sauti ya Tina.kumbe walikuwa wamejibanza pembeni yote yalikuwa ya kuendelea Kati ya Naisma na Haidary Frut walikuwa wanayangalia
"Yani Tina ujui tu! Navyojisikia Ndani ya moyo wangu ! Uyu shoga ako amezidi Sasa . Sio kwa kumzalilisha vile Haidary wawatu !
"Mh ! Embu tuondoke Novo jamani ! Awatakiwi watuone Kama tupo apa !
Kidogo Simu ya Novo berry iliita na Haidary Frut ndo aliekuwa anapiga
"Hallo ! Novo
"Enhe!
"Naisma amenikataa Yani !
Kabla Novo ajajibu alimsikia Haidary Frut akilia upande wa pili na akakata Simu
"Ospuuu! Hatali
Kidogo Simu yake iliita Tena na Naisma ndo alikuwa anapiga safali hii
"Du ! Sijui nisipokee !
"Mh ! Pokea tu Novo utafanyaje sasa !
"Mh ! Aya
🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
" Yani Novo nakwambia kabisa Ukome ! Tena Ukome kunikutanisha na kutaka taka Kama kile alafu kinanitia tia aibu Mimi kinajiliza liza tu!
Novo berry hakujibu kitu na kukata Simu
"Umeona Tina ? Shoga yako alivyo na Zalau enhe !
"Achana naye Novo kwani wewe mgeni na Naisma! Tuondoke bhna
🌿☘️
Naisma aliludi kwao na moja kwa moja alienda chumbani kwake na kumkuta mdogo wake Jasmini akiwa anamnyonyesha mwanae
Walisalimiana na Naisma alijilaza kitandani kwake
"Hahahaha ! Nicheke mie jamani duniani Kuna Mambo eti!
"Mh ! Mambo gani Tena? Dada angu !
"Yani kalibu na kazini kwetu kuna mkaka anaitwa Haidary Frut anauza matunda Basi (......)
Naisma alimuhadithia yote mdogo wake Jasmini kuhusu Haidary Frut
" Mh ! Ila Dada inaonesha uyo Kaka anamapenzi ya dhati na wewe kabisa na sio mbabaishaji Kama Yule Lamek !
"Enhe eti unasemaje ? Unamaana gani ?
"Namasnisha mkubalie tu ! Kazi au umaskini wake isiwe kikwazo cha wewe kumkataa , Kama anakupenda mkubalie na wewe utajikuta unampenda badae tu !
"Msiuuuuu ! Embu usiniletee ujinga wako . Nilijua unaakili kumbe una ata kidogo ! Embu usiniwangie ndo Mana shule ukashindwa !
"Haijalishi ! Dada Mimi lazima nikwambie ukweli ! Wewe ni Dada yangu na usitumie mazaifu yangu kunisema ! Utamkumbuka uyo kaka wewe kataa kataa utakuta mwali si wako !
Naisma hakujibu chochote aliinuka na kutoka zake nje
ITAENDELEA...
NAISMA!
ReplyDeleteYour Thoughts