MTUNZI:BARAKA GEOFREY
+255652089642
JUNE 2015-HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI
Tiiii....tiiii....tiii mlio wa mashine ndani ya chumba cha upasuaji(theatre) ulisikika,madaktari walikuwa bize kumuandaa mtu aliyekuwa amelazwa kwenye kitanda cha chumba hicho
Aliyekuwa anasubiriwa ni kiongozi wa oparesheni hiyo Dr.Austin Meyer daktari bingwa kijana mwenye umri wa takribani miaka 30
Kwa hatua za haraka
Dr.Ausitin alielekea kwenye chumba cha upasuaji
"Mmeshakamilisha maandalizi yote?"
alimuuliza nesi anayehusika na maandalizi
"ndiyo dokta"
"Basi ni vizuri tumwombe Mungu oparesheni ifanikiwe"
Dr.Austin aliingia haraka kwenye chumba cha upasuaji ili kuanza oparesheni mara moja.......
"Nipatie huo mkasi......"alitoa maagizo kwa msaidizi wake
griii.....griii.....mlio wa simu ulimshtua dokta lakini aliupuuzia kwani hakuwa na kawaida ya kupokea simu akiwa anaelekea kuanza shughuli nzito kama hiyo hivyo aliipuuzia
Simu iliita tena kwa mara nyingine,akaamua kuitoa ilk aizime kabisa kuondoa usumbufu.... McDonald lilisomeka jina la mpigaji wa simu hiyo
Dr.Austin alijikuta akishindwa kuikata simu hiyo na kuanza kutetemeka
"I have to take this call"
(natakiwa kupokea hii simu)
aliwaambia madaktari wenzake
"Dr.Austin are you out of your mind how can you......"
"sikiliza Dr.Magesa ni lazima niipokee nakuja sasa hivi" Dr.Austin alisisitiza nakutoka ndani ya chumba hicho
Madaktari wenzake hawakumuelewa kabisa kwani ulikuwa mda wa kuanza oparesheni hiyo ngumu na sio kawaida kwa daktari kama yeye tena kiongozi wa oparesheni kufanya kitendo hicho
"Kijana wangu habari yako, pole kwa kukutoa kwenye oparesheni nzito ya kujaribu kumfufua maiti"
Sauti nzito ya kukwaruza ilisikika kwenye spika ya simu ya Dr.Austin
"Mzee tafadhali naomba uniache....."
"Sikiliza dokta sina mda mwingi wa kuongea na wewe ninachotaka huyo kenge hapo kitandani afe....."
"Unasemaje? hivi wewe una aki......"
" sikia kijana unanijua vizuri, iko hivi hapo mezani ofisini kwako utakuta chupa ya sumu ya Acetamin-220 nenda kamchome huyo mbuzi..."
"Nisikilize McDonald huwezi endelea niendesha unavyotaka ni lazima niokoe maisha yake."
"Hahahahaha usinichekeshe Austin najua mke wako na mwanao wapo Sun beach hotel na huko kuna vijana wangu sasa utachagua kati ya familia yako na huyo mpuuzi hapo theatre bye.."
"We mzee usiguse...ti ti ti...
Dr Austin alijikuta anapika kelele mwenyewe simu ilishakatwa mda mrefu.
Mikono yake illikuwa inatetemeka na moyo wake ulikita kwa spidi ya ajabu kwa mshtuko aliopata
'Mungu wangu nifanye nini mimi' aliwaza
....huyu mzee hana utani ataua familia yangu kweli...
Kwa mwendo wa unyonge Dr Austin aliingia ofisini kwake na kweli aliikuta chupa ya Acetamin-220 mezani, alijiuliza imefikaje na mda gani lakini alikumbuka jinsi mzee huyo alivyo na mtandao mpana hivyo hakushangaa sana. Aliichukua sumu hiyo na kuelekea chumba cha upasuaji
'No I can't do this'
(hapana siwezi fanya hivi)
'lakini yule mzee ni shetani ataua familia yangu'
Bado Dr Austin aliendelea kuwaza, mawazo juu ya mke wake Olivia ambaye ndiye kwanza wana miaka minne ya ndoa alikuwa bado mbichi na mtoto wao mwenye miaka miwili na nusu yaliendelea kumsumbua
'hapana huyu mtu lazima nimuokoe hata kama simjui'
Dr Austin aliingia ndani ya chumba cha upasuaji kwa haraka
"Sikilizeni jamani sitaki maswali yoyote huyu mgonjwa ili tumuokoe anatakiwa kuondolewa hapa sasa hivi la sivyo atauawa kwa hiyo..."
"Dr Austin are you okay?" daktari mwenzake alimuuliza kwa taharuki
"Dr Magesa fanyeni hivyo tafadhali maisha yake yanatafutwa mhamisheni hospitali haraka" alimaliza kwa msisitizo na kutoka akiacha mshangao kwa wenzake...
Dr Austin alitoka nje ya chumba cha upasuaji kama mwendawazimu asijue uelekeo wake alijua kabisa kuwa ameenda kinyume na maagizo ya mzee McDonald na hivyo maisha yake, familia yake na hata huyo mgonjwa yapo hatarini
Aliitoa simu yake na haraka aliitafuta namba ya mkewe na kuipiga
'shit...! mbona hapokei'
Aliipiga tena na mara hii ilipokelewa na akaisikia sauti ya mkewe kipenzi
"Hello my love..." sauti tamu ya mkewe ilisikika
"Olivia nisikilize hivi nnavyoongea jiandae kuondoka nakuja sasa hivi kuwachukua mwandae na Noreen pia"
"Baby mbona sikuelewi si ndio...."
"Olivia sitaki maswali kuna hatari kubwa wewe jiandae nakuja kuwachukua Sasa hivi" Dr Ausin akakata simu
Mkewe alishindwa kuelewa nini kinaendelea kwani hakuwahi kumsikia mmewe akionge nae kwa namna kama ile , siku zote mme wake aliongea nae kwa namna ya kumbembeleza akimuita majina mazuri;baby, sweetheart, my love na mengine yote... pia alikuwa hapo kwa mapumziko na mwanae kipenzi lakini yalikatishwa ghafla
Hakuwa na namna alimheshimu mmewe hivyo alikusanya vitu vyake vichache na kwenda kumfuata mwanae aliyekuwa akicheza na watoto wenzake swimming pool.....
La haula!.....mwanae hakuwepo huko...
"Samahani mwanangu nilimwacha hapa simuoni" alimuuliza msimamizi wa watoto eneo hilo
"Mbona baba yake ameshamchukua"
"Baba yake? amemchukua saa ngapi?" aliuliza kwa hamaki mapigo yake ya moyo yalishabadili uelekeo kwani baba yake ndio kwanza ametoka kuongea naye
"Kama dakika kumi hivi zimepita alienda nae kwenye ile range rover nyeusi kwani kuna tatizo?"
Pasipo kumjibu Olivia aliondoka kwa kasi kuelekea kwenye hiyo range rover nyeusi alishangaa kwani hawakuwa wakimiliki gari kama hilo iweje mmewe awe huko?
Pasipo hata kujiuliza mara mbili mbili alienda moja kwa moja kwenye gari hilo asahau hata kumpigia mmewe simu
Alifika kwenye gari na kujaribu kugonga kioo kwani hakuona chochote sababu vioo vilikuwa 'tinted'
"Mama Noreen tafadhali ingia ndani tunatakiwa kwenda mahali na wewe na mwanao" Olivia alisikia sauti nyuma yake
Olivia aligeuka kwa hamaki na kukutana na pande jibaba la mtu sura yake ilikuwa ya ajabu kama mtu anayetaka kupiga chafya kwa haraka haraka hakujua kama jibaba hilo ni kabila gani wala ni la nchi gani alikuwa ametinga suti nyeusi na kofia nyeusi....
"Wewe ni nani na mwanangu yuko wapi?"
"We mwanamke sitaki maswali mengi timiza nilichokwambia" alijibu mtu huyo huku akifunua kidogo koti lake na kumuonyesha Olivia bastola yake iliyochomekwa kiunoni
Olivia alishtuka na kujikuta ananyong'onyea
"Kwani nimewakosea nini jamani.... "
"Mama nakwambia mara ya mwisho ingia ndani ya gari na sitaki maswali"
Pasipo ubishi Olivia aliingia ndani ya gari kama kondoo anayeenda kuchinjwa alimkuta mwanae anakula 'chocolate' bila stress pembeni yake kukiwa na kijana mweupe aliyevalia suti nyeusi pia na miwani tinted akicheza na mwanae mbele alikiwepo dereva ambaye alikuwa na upara na ndevu kiasi
Yeye na mwanae waliwekwa kati tayari kwa safari kuanza
"Kazi nzuri Antonio" dereva alimwambia jibaba yule
Hapo ndipo Olivia alitambua kuwa jibaba yule anaitwa Antonio
"Nimemchukua kirahisi mpigie bosi mwambie kondoo washachukuliwa atupe maelekezo mengine.." alijibu Antonio kwa majigambo
"Mama mbona unalia? angalia anko Thomas amenipa chocolate na ameniambia anatupeleka hoteli nyingine.." Noreen alimweleza mama yake kwa furaha akimnyooshea kidole kijana yule mweupe
Olivia alishindwa cha kujibu na akajilazimisha kutabasamu ili mwanae asijue kama wametekwa au kuna hatari yoyote
"Bosi tayari tunao tunasubiri maelekezo yako" dereva alikuwa akiongea kwenye simu
"Kazi nzuri Gilbert waleteni zone 3A"
"Sawa bosi...."
Gari iliwashwa na kuelekea mahali ambako Olivia hakupajua, alitamani kuuliza lakini alijionya kwani Antonio alishamkataza kuuliza maswali na kila alipoiona sura yake ilitosha sana kumfanya atulie kama maji mtungini.
"Nipatie simu yako" aliamuru bwana Mwamba
Bila ubishi Olivia alimpa Antonio simu yake, Antonio aliizima na kutoa laini zote na kuzivunja vunja
Walitoka nje ya geti la hoteli pasipo mtu yoyote kugundua kinachoendelea
Dr Austin alitoka nje ya geti la hospitali kama mtu aliyechanganyikiwa aliiona taxi inapita aliipungia mkono
Nipeleke Sun beach hotel"
"Sawa kiongozi"
Aliingia ndani ya taxi kwa haraka
"Kaka na wewe ni daktari wa hapa?" dereva taxi alijaribu kuanzisha mazungimzo ili kumzoea mteja wake
"Fanya haraka uwezavyo tafadhali nataka kufika haraka iwezekanavyo" alitoa maelekezo Dr Austin alionekana kabisa hataki mazungumzo wakati huo
"Sawa kiongozi dakika tano tu tutakuwa tumefika" alijibu dereva na kukanyaga mafuta akichochea mwendo wa gari
Simu ya Dr Austin ilianza kuita kwa fujo..... McDonald lilisomeka jina kwenye kioo cha simu
Dr Austin alijikuta akitetemeka kwa hofu na kushindwa kupokea simu hadi ilipokata...simu iliita tena kwa mara ya pili akaamua kuipokea....
"Hahahahahahahaha" mzee McDonald alicheka kwa kebehi
"Nakuona kijana wangu unajaribu kuwahk eneo la tukio kuchukua maelezo you are so stupid Austin"
"Mzee nakuomba tafadhali uiache familia yangu..." Dr Austin aliongea kwa unyonge
"Ungefanya ninachotaka nisingewagusa lakini umenijaribu, sikia kijana mimi huwa sijaribiwi nadhani unanifahamu vizuri... Sasa usijisumbue kwenda huko kwa sababu tayari ninao na utafanya kile ninachotaka la sivyo usinilaumu"
" Mzee tafadhali sana....."
"Austin nakupa masaa mawili uikamilishe kazi niliyokupa ikizidi hata sekunde moja usinilaumu kwa kitakachotokea rudi hospitali ukammalize yule mshenzi...kazi njema" McDonald alikata simu
'Mungu wangu kwanini mimi lakini" aliwaza Dr Austin
alijuta kumfahamu mzee huyu ambaye mpaka sasa hatujui historia yao
"Bro geuza gari tunarudi Muhimbili" Austin alimueleza dereva taxi
"Ina maana umeahirisha safari?...gharama itaongezeka lakini kiongozi"
"Nimekwambia turudi kwani nimekwambia sina nauli" Austin alijibu kwa hasira
"Samahani kaka nilishangaa tu mama watoto amekuita nini" dereva taxi alijaribu kuchomekea utani kumfurahisha mteja wake lakini Dr Austin hakumjali aliendelea kuzama kwenye mawazo dereva aliona isiwe shida aliendelea na kazi yake kimya kimya
"Tumefika mkuu"
"Kwa hiyo kiasi gani hapa"
"Elfu hamsini bosi wangu"
"Sawa"
Dr Austin alijua kabisa kuwa anapigwa cha juu lakini hakujali alichomoa elfu kumi tano na kumkabidhi bila maswali
Dereva taxi alifurahi kupata pesa hiyo ndefu bila shida yoyote
"Siku nyingine ukiwa na shida mkuu niite namba yangu hii hapa" dereva alimkabidhi kadi yake ya biashara
Dr Austin hata hakuwa na mda naye alivuta hatua ndefu ndefu kuelekea ndani ya jengo la hospitali
'Duh! huyu jamaa sijui ana shida gani' alijiwazia dereva taxi aliamua kuwasha gari lake na kuondoka akimpuuzia
'atajua mwenyewe bwana cha msingi ameniachia pesa iliyotakata' alijikuta akitabasamu kwa mawazo hayo, akaanza kupanga viwanja mbalimbali vya kujirusha siku hiyo
*************
Dr Austin alielekea ofisini kwake na kumuulizia mgonjwa kwa katibu muhtasi wake
"Mh niliona anahamishwa sikujua anakopelekwa labda muulize Dr Magesa" katibu wake alimjibu
Dr Austin alinyoosha moja kwa moja ofisini kwa Dr Magesa ambaye alimuachia jukumu la kusimamia usalama wa mgonjwa yule
"Dr Austin!" Magesa alishtuka kumuona daktari mwenzake pale alimuona kama mzuka uliomuibukia
"Dr Magesa poleni kwa hali niliyowaacha nayo naomba nijue maendeleo ya mgonjwa"
"Austin naomba nieleze kila kitu kinachoendelea maana mambo yanayoendelea hata siyaelewi" Dr Magesa aliuliza kwa udadisi
"Kaka ntakueleza kila kitu usijali lakini kwa sasa naomba uniambie hali ya mgonjwa ikoje na amehamishiwa wapi"
"Ok mda hule wakati unaondoka tukiwa bado tunajiuliza cha kufanya walikuja watu watatu ambao walijitambulisha kuwa wametoka idara ya usalama wa taifa na wamekuja kumhamisha mgonjwa kutokana na sababu za kiusalama...hatukuelewa na wala hatukuwa na nafasi ya kuongea nao vizuri hivyo tulimuandaa mgonjwa kwa ajili ya uhamisho...."
"Subiri......." Dr Austin alimkatisha
"Kwa hiyo hamkujua hata anakohamishiwa?"
"Ndiyo sisi tulimuandaa tu na kumpakia kwenye 'ambulance' waliyokuja nayo ila nakumbuka tu walisema wanaenda naye uwanja ya ndege kwani anapelekwa nje ya nchi" alijibu Dr Magesa
"Ooh my God kwa hiyo...."
"Tulia basi kaka nimalizie...sasa lilichotushangaza kama baada ya dakika kumi hivi walikuja watu wengine wawili nao wakasema wametoka idara ya usalama wa taifa nao pia walikuwa na vitambulisho kama wale wa kwanza, nao walisema wamekuja kumchukua mgonjwa..."
"Duuuuuh!" Dr Austin alipigwa na mshangao
" Sasa sisi hatukuwaelewa tukawaambia mbona wenzao washamchukua walitushangaa na kusema mbona hawakutumwa watu wengine....kwa hiyo walinichukua kwenda kunihoji vizuri hivi unavyoniona ndio nimetoka huko ofisini kwao.."
"Uuuuumph" Dr Austin alijikuta amechoka ghafla
"Mbona sielewi Magesa..."
" Kwani huyo mgonjwa ni nani Austin mbona kama kuna mambo siyaelewi kuhusu yeye?"
"Mimi sielewi kaka ngoja niende" Dr Austin alijibu huku akinyanyuka
"Subiri....naomba nieleze kwanini mda ule ulikiwa namna ile baada ya kupokea simu?"
"Kaka ni mambo mengi yametokea nitakueleza siku nyingine kwa sasa acha niende"
Dr Austin aliondoka zake kinyonge upande mmoja alijiuliza kama McDonald atamuelewa kweli na upande mwingine alifurahi kwani asingeweza kumuua mgonjwa yule asiyemjua
'lakini yupo salama kweli huko aliko?' Dr Austin alijiuliza akili yake ilichoka kabisa
Aliamua aende nyumbani ili ampigie simu McDonald kumjulisha yaliyotokea kwani aliogopa maongezi yake kusikika pale hospitali.
*****************
"Ndiyo kama hivyo mzee wangu nimeshindwa kufanikisha kabisa"
"Kijana sikiliza usinifanye mtoto hata sielewi unayoyaongea, nawatuma vijana wangu waje wakuchukue ili unieleze vizuri wanakuja hapo ndani ya robo saa" simu ilikatwa
Na kweli mda sio mrefu Dr Austin alisikia muungurumo wa gari nje ya geti lake akajua mambo yameiva
Watu wawili walishuka ambao walikiwa ni Antonio na Gilbert
"Dr Austin nadhani unajua kinachoendelea panda kwenye gari tuondoke"
Bila ubishi alipanda kwenye gari na kutulia kimya, gari iliondoka taratibu na kuanza safari hiyo isiyopangwa
"Dokta utatusamehe kidogo kuanzia hapa huruhusiwi kujua tunakoelekea" Antonio alimweleza huku akitoa kitambaa cheusi na kumfunga machoni
Hofu kiasi ilimshika Dr Austin lakini alijikaza kiume...baada ya mda mchache alihisi gari ikisimama kisha geti kufunguliwa na gari ikaingia ndani aliamriwa kushuka naye akatii kwa mwendo wa haraka alielekezwa mpaka kwenye geti la pili na kisha geti la tatu ambapo alifanyiwa ukaguzi kama hana siliha au kifaa chochote hatari
Kina Antonio walimkabidhi kwa wadada wawili ambao walimpeleka kwenye sebule nzuri ya kisasa na kisha kufunguliwa kitambaa chake
"Karibu Dr Austin ukihitaji chochote utabonyeza hicho kitufe cha kijani na sisi tutakusaidia, sijui utatumia kinywaji gani?" mdada mmojawapo alimuuliza kwa ukarimu na upole lakini Dr Austin alimwona kama jini mtoa roho tu
"Asante sihitaji chochote" akajibu kwa mkato
"Sawa bosi atafika baada ya nusu saa kwa mazungumzo na wewe"
"Sawa.."
Dr Austin alibaki hapo akiona mda hauendi kwani alitamani kitu kimoja tu kutoka salama na familia yake.....
Baada ya mda kidogo vijana wanne ambao wote walivalia suti nyeusi waliingia hapo sebuleni na kujipanga kila mmoja kwenye kona ya sebule, dr Austin hakujua nini kinaendelea
Akiwa katika mshangao mzee mmoja mwenye umri takribani miaka 54 mwenye asili ya kizungu aliingia nyuma yake pia walikuwepo vijana wawili waliovalia suti nyeusi ambao kwa haraka walionekana kama walinzi wake
"McDonald!" alinong'ona Dr Austin kwa sauti aliyoweza kuisikia mwenyewe.. alikuwa akimfahamu mzee huyu
"Karibu sana Dr Austin ni kama miaka mitatu sasa hatujaonana" aliongea McDonald akitoa tabasamu.....
ITAENDELEA......
ACETAMIN-220...(02)
MTUNZI:BARAKA GEOFREY
0652089642
Email:hadithizabeka@gmail.com
Facebook:hadithi za beka
ILIPOISHIA......
Nipeleke Sun beach hotel"
"Sawa kiongozi"
Aliingia ndani ya taxi kwa haraka
"Kaka na wewe ni daktari wa hapa?" dereva taxi alijaribu kuanzisha mazungimzo ili kumzoea mteja wake
"Fanya haraka uwezavyo tafadhali nataka kufika haraka iwezekanavyo" alitoa maelekezo Dr Austin alionekana kabisa hataki mazungumzo wakati huo
"Sawa kiongozi dakika tano tu tutakuwa tumefika" alijibu dereva na kukanyaga mafuta akichochea mwendo wa gari
Simu ya Dr Austin ilianza kuita kwa fujo..... McDonald lilisomeka jina kwenye kioo cha simu
Dr Austin alijikuta akitetemeka kwa hofu na kushindwa kupokea simu hadi ilipokata...simu iliita tena kwa mara ya pili akaamua kuipokea....
ENDELEA......
"Hahahahahahahaha" mzee McDonald alicheka kwa kebehi
"Nakuona kijana wangu unajaribu kuwahk eneo la tukio kuchukua maelezo you are so stupid Austin"
"Mzee nakuomba tafadhali uiache familia yangu..." Dr Austin aliongea kwa unyonge
"Ungefanya ninachotaka nisingewagusa lakini umenijaribu, sikia kijana mimi huwa sijaribiwi nadhani unanifahamu vizuri... Sasa usijisumbue kwenda huko kwa sababu tayari ninao na utafanya kile ninachotaka la sivyo usinilaumu"
" Mzee tafadhali sana....."
"Austin nakupa masaa mawili uikamilishe kazi niliyokupa ikizidi hata sekunde moja usinilaumu kwa kitakachotokea rudi hospitali ukammalize yule mshenzi...kazi njema" McDonald alikata simu
'Mungu wangu kwanini mimi lakini" aliwaza Dr Austin
alijuta kumfahamu mzee huyu ambaye mpaka sasa hatujui historia yao
"Bro geuza gari tunarudi Muhimbili" Austin alimueleza dereva taxi
"Ina maana umeahirisha safari?...gharama itaongezeka lakini kiongozi"
"Nimekwambia turudi kwani nimekwambia sina nauli" Austin alijibu kwa hasira
"Samahani kaka nilishangaa tu mama watoto amekuita nini" dereva taxi alijaribu kuchomekea utani kumfurahisha mteja wake lakini Dr Austin hakumjali aliendelea kuzama kwenye mawazo dereva aliona isiwe shida aliendelea na kazi yake kimya kimya
"Tumefika mkuu"
"Kwa hiyo kiasi gani hapa"
"Elfu hamsini bosi wangu"
"Sawa"
Dr Austin alijua kabisa kuwa anapigwa cha juu lakini hakujali alichomoa elfu kumi tano na kumkabidhi bila maswali
Dereva taxi alifurahi kupata pesa hiyo ndefu bila shida yoyote
"Siku nyingine ukiwa na shida mkuu niite namba yangu hii hapa" dereva alimkabidhi kadi yake ya biashara
Dr Austin hata hakuwa na mda naye alivuta hatua ndefu ndefu kuelekea ndani ya jengo la hospitali
'Duh! huyu jamaa sijui ana shida gani' alijiwazia dereva taxi aliamua kuwasha gari lake na kuondoka akimpuuzia
'atajua mwenyewe bwana cha msingi ameniachia pesa iliyotakata' alijikuta akitabasamu kwa mawazo hayo, akaanza kupanga viwanja mbalimbali vya kujirusha siku hiyo
*************
Dr Austin alielekea ofisini kwake na kumuulizia mgonjwa kwa katibu muhtasi wake
"Mh niliona anahamishwa sikujua anakopelekwa labda muulize Dr Magesa" katibu wake alimjibu
Dr Austin alinyoosha moja kwa moja ofisini kwa Dr Magesa ambaye alimuachia jukumu la kusimamia usalama wa mgonjwa yule
"Dr Austin!" Magesa alishtuka kumuona daktari mwenzake pale alimuona kama mzuka uliomuibukia
"Dr Magesa poleni kwa hali niliyowaacha nayo naomba nijue maendeleo ya mgonjwa"
"Austin naomba nieleze kila kitu kinachoendelea maana mambo yanayoendelea hata siyaelewi" Dr Magesa aliuliza kwa udadisi
"Kaka ntakueleza kila kitu usijali lakini kwa sasa naomba uniambie hali ya mgonjwa ikoje na amehamishiwa wapi"
"Ok mda hule wakati unaondoka tukiwa bado tunajiuliza cha kufanya walikuja watu watatu ambao walijitambulisha kuwa wametoka idara ya usalama wa taifa na wamekuja kumhamisha mgonjwa kutokana na sababu za kiusalama...hatukuelewa na wala hatukuwa na nafasi ya kuongea nao vizuri hivyo tulimuandaa mgonjwa kwa ajili ya uhamisho...."
"Subiri......." Dr Austin alimkatisha
"Kwa hiyo hamkujua hata anakohamishiwa?"
"Ndiyo sisi tulimuandaa tu na kumpakia kwenye 'ambulance' waliyokuja nayo ila nakumbuka tu walisema wanaenda naye uwanja ya ndege kwani anapelekwa nje ya nchi" alijibu Dr Magesa
"Ooh my God kwa hiyo...."
"Tulia basi kaka nimalizie...sasa lilichotushangaza kama baada ya dakika kumi hivi walikuja watu wengine wawili nao wakasema wametoka idara ya usalama wa taifa nao pia walikuwa na vitambulisho kama wale wa kwanza, nao walisema wamekuja kumchukua mgonjwa..."
"Duuuuuh!" Dr Austin alipigwa na mshangao
" Sasa sisi hatukuwaelewa tukawaambia mbona wenzao washamchukua walitushangaa na kusema mbona hawakutumwa watu wengine....kwa hiyo walinichukua kwenda kunihoji vizuri hivi unavyoniona ndio nimetoka huko ofisini kwao.."
"Uuuuumph" Dr Austin alijikuta amechoka ghafla
"Mbona sielewi Magesa..."
" Kwani huyo mgonjwa ni nani Austin mbona kama kuna mambo siyaelewi kuhusu yeye?"
"Mimi sielewi kaka ngoja niende" Dr Austin alijibu huku akinyanyuka
"Subiri....naomba nieleze kwanini mda ule ulikiwa namna ile baada ya kupokea simu?"
"Kaka ni mambo mengi yametokea nitakueleza siku nyingine kwa sasa acha niende"
Dr Austin aliondoka zake kinyonge upande mmoja alijiuliza kama McDonald atamuelewa kweli na upande mwingine alifurahi kwani asingeweza kumuua mgonjwa yule asiyemjua
'lakini yupo salama kweli huko aliko?' Dr Austin alijiuliza akili yake ilichoka kabisa
Aliamua aende nyumbani ili ampigie simu McDonald kumjulisha yaliyotokea kwani aliogopa maongezi yake kusikika pale hospitali.
*****************
"Ndiyo kama hivyo mzee wangu nimeshindwa kufanikisha kabisa"
"Kijana sikiliza usinifanye mtoto hata sielewi unayoyaongea, nawatuma vijana wangu waje wakuchukue ili unieleze vizuri wanakuja hapo ndani ya robo saa" simu ilikatwa
Na kweli mda sio mrefu Dr Austin alisikia muungurumo wa gari nje ya geti lake akajua mambo yameiva
Watu wawili walishuka ambao walikiwa ni Antonio na Gilbert
"Dr Austin nadhani unajua kinachoendelea panda kwenye gari tuondoke"
Bila ubishi alipanda kwenye gari na kutulia kimya, gari iliondoka taratibu na kuanza safari hiyo isiyopangwa
"Dokta utatusamehe kidogo kuanzia hapa huruhusiwi kujua tunakoelekea" Antonio alimweleza huku akitoa kitambaa cheusi na kumfunga machoni
Hofu kiasi ilimshika Dr Austin lakini alijikaza kiume...baada ya mda mchache alihisi gari ikisimama kisha geti kufunguliwa na gari ikaingia ndani aliamriwa kushuka naye akatii kwa mwendo wa haraka alielekezwa mpaka kwenye geti la pili na kisha geti la tatu ambapo alifanyiwa ukaguzi kama hana siliha au kifaa chochote hatari
Kina Antonio walimkabidhi kwa wadada wawili ambao walimpeleka kwenye sebule nzuri ya kisasa na kisha kufunguliwa kitambaa chake
"Karibu Dr Austin ukihitaji chochote utabonyeza hicho kitufe cha kijani na sisi tutakusaidia, sijui utatumia kinywaji gani?" mdada mmojawapo alimuuliza kwa ukarimu na upole lakini Dr Austin alimwona kama jini mtoa roho tu
"Asante sihitaji chochote" akajibu kwa mkato
"Sawa bosi atafika baada ya nusu saa kwa mazungumzo na wewe"
"Sawa.."
Dr alibaki hapo akiona mda hauendi kwani alitamani kitu kimoja tu kutoka salama na familia yake.....
Baada ya mda kidogo vijana wanne ambao wote walivalia suti nyeusi waliingia hapo sebuleni na kujipanga kila mmoja kwenye kona ya sebule, dr Austin hakujua nini kinaendelea
Akiwa katika mshangao mzee mmoja mwenye umri takribani miaka 54 mwenye asili ya kizungu aliingia nyuma yake pia walikuwepo vijana wawili waliovalia suti nyeusi ambao kwa haraka walionekana kama walinzi wake
"McDonald!" alinong'ona Dr Austin kwa sauti aliyoweza kuisikia mwenyewe.. alikuwa akimfahamu mzee huyu
"Karibu sana Dr Austin ni kama miaka mitatu sasa hatujaonana" aliongea McDonald akitoa tabasamu...............
Dr Austin hakumjibu kitu ila alimuangalia tu kwa hasira
"Kwanza nikupe pole kwa namna ulivyoletwa kwani ndio utaratibu wa kuja huku sitaki kila mtu apajue by the way nilihama kule nilikokuwa ni mda sasa" mzungu huyo aliendeleza maneno kwa kiswahili fasaha kabisa
"Naombeni mtupishe nina mazungumzo ya faragha kidogo na huyu mtu"McDonald aliwaambia walinzi wake, waliinama kwa heshima na kutoka nje ya sebule
"Okay turudi kwenye jambo letu la msingi, nieleze kwanini hujafanikiwa kazi niliyokupa"
" Ni kama nilivyokwambia kwenye simu...(alimweleza yote aliyoambiwa na Dr Magesa)"
"Hebu subiri Austin umesema usalama wa taifa walikuja mara mbili"
"Ndio lakini ni kama walikuwa hawafahamiani"
"Sasa kijana umeona umesabisha kazi yangu kuwa ngumu unajua ni shida kiasi gani umesababisha?...na mimi sina budi kutimiza nilichokuahidi baada ya masaa mawili"
"Lakini mzee kosa langu ni nini sasa mimi ningefanya nini wakati wameshamchukua"aliuliza Austin akitia huruma
"Hahahahahaha usinichekeshe dokta ulitakiwa kutimiza maagizo 'immediately' baada ya mimi kukupa tu lakini wewe ukajifanya mjanja ukaanza kukimbia...trust me usingekuwa kijana wangu ungekuwa kuzimu saizi umegeuzwa kuni....."
"Mzee naomba uishie mambo ya zamani yalishapita mimi sio kijana wako tena siwezi kuwa karibu na mtu dhalimu kama wewe" alijibu Dr Austin kwa tahamaki
"Pumbavu....kaka kimya panya wewe unathubutu kubishana na mimi....watch your tongue son I can destroy your whole clan right now (angalia ulimi wako kijana naweza kuharibu ukoo wako mzima sasa hivi" McDonald aliongea kwa hasira na tayari alianza kuwa mwekundu
"Basi mzee naomba unisamehe" Austin aliongea kinyonge.....afanyeje sasa tayari amewekwa mkononi
"Sasa ni hivi ilibidi niwaue wote na familia yako lakini bado nina kazi na wewe...."
McDonald alibonyeza kitufe chekundu kilichokuwa chini ya meza na walinzi wake wakaingia haraka
"Mchukueni huyo mkamhifadhi zone 3B hakikisheni haonani na familia yake nitakuwa na kazi naye"
"Sawa bosi" walijibu kwa heshima na kumchukua Austin
Dr Austin alikuwa na hofu sana nini kinafuata lakini alifurahi angalau familia yake bado wapo hai
********************
Huku nyuma McDonald aliitoa simu yake na kumpigia rafiki yake Mr Amos Gamba ambaye alikuwa ni mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa na rafiki yake sana pia alimsaidia kwenye shughuli zake mbalimbali na kumpa taarifa na siri mbali mbali za serikali.....
"Hallow Mr Gamba"
"Naam McDonald habari za siku?"
"Nzuri tu sijui mnaendeleaje huko na usalama wa nchi"
"Aah shida tupu kuna jambo hapa linatuumiza vichwa bwana"
"Poleni Mr Gamba kwa shuguli.....sasa kulikuwa na jambo nahitaji msaada wako kidogo" ukimya wa Mr Gamba ulimaanisga aendelee
"Kuna mtu mmoja alilazwa hapo Muhimbili ilibidi afanyiwe oparesheni....sasa huyo mtu nilikuwa nna shida ya kumuwahisha kuzimu kwani ni mdudu kwenye mambo yangu...lakini nimeambiwa mmemchukua kwa hiyo nilikuwa nahitaji msaada wako asilione jua la kesho amalizwe"
"Uuuuumph..." Mr Gamba alishusha pumzi bila kupenda
"McDonald huyo mtu anahitajika sana kwenye idara yetu kuna siri anayo na tunaihitaji hivyo tunamtafuta kwa udi na uvumba tumtibu ili tumhoji...."
"Mnamtafuta??!....si tayari mmemhamisha hospitali?"
"Mkuu hao waliomchukua hata hatuwafahamu sijui ni watu gani sisi pia tumechanganyikiwa na tunawatafuta....tukipiga hatua yoyote by nitakujulisha"
"Make sure mkimpata anauawa Mr Gamba"
"Sawa McDonald"
"Kesho asubuhi nitakuingizia mzigo kidogo kwenye akaunti yako kwa usumbufu"
"Asante mkuu"
*****************
'Huyu ana shida gani na huyu kijana' alijiwazia Mr Gamba
'Hapana siwezi kumuua huyu kijana nikimpata lazima atibiwe kwa siri nimhoji ndiyo labda auawe'
*****************
Ndege ndogo ya binafsi (private jet) aina ya Cessna Citation CJ2 ilikuwa ikipasua anga......ndani ya ndege kulikuwa kama hospitali ndogo kulikuwa na kitanda ambacho mgonjwa alilazwa na kilikuwa na madaktari wawili wakimhudumia kwa ukaribu
Kwenye chumba kingine cha ndege hiyo kulikuwa watu watatu ambao walimchukua Muhimbili walivua sura za bandia walizozivaa wawili walikuwa ni waarabu na mmoja alikuwa ni miafrika
"The boss have said we are going to land in Nairobi then we will take another flight to Riyadh Saud Arabia....i just remind you we have to make sure this guy arrives safely because he is very important and we should not fail him I think you have understood" (Bosi amesema tutatua Nairobi baada ya hapo tutabadilisha ndege na kuelekea Riyadh Saudi Arabia...tukumbuke jamani tunatakiwa kuhakikisha huyu anafika salama kwani ni muhimu sana kwa bosi na hatutakiwi kumuangusha nadhani tumeelewana) yule mwarabu aliwaambia wengine ambaye alionekana kama ndiye kiongozi
"Sawa sawa" wenzake walimjibu.
Saa nane kamili jioni ndege ilitua Nairobi na baada ya nusu saa walichukua ndege nyingine ambayo iliwapeleka Riyadh Saudi Arabia...saa mbili na nusu ndege iliingia kwenye anga la Saudi Arabia na kutua kwenye kiwanja cha ndege jijini hapo
Baada ya shughuli za kiitifaki kukamilika mgonjwa alipakiwa kwenye gari la wagonjwa na likaondoka kwa kasi likifuatiwa na Audi mbili nyeusi
Baada ya kukatisha mitaa kadhaa waliingia kwenye jumba kubwa la kifahari hapo mgonjwa na walinzi kadhaa waliingia kwenye. helikopta mbili na kuondoka mahali hapo
Helikopta zilitua kwenye kiwanja kidogo cha helikopta ndani ya jumba kubwa la kifahari kwa haraka, mgonjwa alishushwa na kuwekwa kwenye kitanda cha magurudumu na kupelekwa ndani ya jumba hilo.
"Job done boss" (kazi imekamilika bosi) yule mwarabu aliongea kwenye simu na bosi wake
"Good job Faheed I need you right now" (kazi nzuri Faheed nakuhitaji sasa hivi.
"Ok boss I am on my way" (sawa bosi nipo njiani)
*******************
OFISI YA IDARA YA USALAMA WA TAIFA
"Mkuu tumepata taarifa wale watu waliomchukua mgonjwa walimpandisha ndege kuelekea Nairobi" mfanyakazi mmoja wa idara hiyo alimwambia mkuu wake Mr Gamba
"Good niitie Doreen aje hapa mara moja"
"Ndiyo mkuu" binti mmoja mweupe urefu wa wastani aliingia
"Doreen mtafute Allen mwambie afike hapa kesho usiku"
"Lakini mkuu yupo Cape town kwa ile misheni ya......"
"Tell him to abort the mission (mwambie aachane nayo) nitamtuma Gregory akamalizie"
"Sawa mkuu"
Siku iliyofuata jioni kijana mmoja mrefu mwenye weusi wa kung'aa ambaye mda wote alikuwa anatabasamu mwenye sura ya kuvutia ambayo mara nyingi iliwafanya wadada wawe na hali mbaya, alisimama kwa ukakamavu mbele ya meza ya mkuu wake
"Nimefurahi sana umefika kwa wakati kijana wangu....kama unavyojua kazi zetu hazina mapumziko....kuna jambo zito kidogo limetokea na nikaona wewe ndo kijana wangu ninayekukuamini unaweza ukafanya kazi yetu kwa ufasaha....kuna mtu ana taarifa za msingi sana kwetu lakini yupo hoi kitandani na hadi sasa hatujui alipo....kuna watu wasiojulikana waliomchukua Muhimbili na kwa taarifa tulizonazo ni kwamba watu hao walitua naye Nairobi, hivyo unaweza kuanzia hospitali upate chochote na kesho asubuhi utaelekea Nairobi Doreen ameshakukatia tiketi"
"Sawa mkuu nimekuelewa"
"Nataka kazi hiyo ifanyike kwa ufanisi sana can unampata huyo mtu na kumleta hakikisha anakuwa hai sikufundishi jinsi ya kufanya ila nakuamini"
"Sawa mkuu nitafanya hivyo"
"Sawa kazi njema Allen"
"Asante" Allen alijibu na kuondoka ofisini hapo
ENDELEA..........
Allen alikuwa ni kijana mwenye umri wa takribani miaka 35 alitumikia idara ya usalama wa taifa kwa miaka mitano kwa mafanikio makubwa na uaminifu wa hali ya juu na hivyo kuaminiwa sana na viongozi wake....baada ya kuhitimu masomo yake ya kidato cha sita Allen alienda jeshi akiwa na miaka 20 kama sheria ya nchi ilivyomtaka ambako aliunga moja kwa moja hivyo hakwenda chuo.....alipata mafunzo ya jeshi kwa miaka mitatu na wakuu wake waliona uwezo wa tofauti alio nao katika mambo mbalimbali kama kulenga shabaha, mapigano ya ana kwa ana, kujituma, uwezo wa kuongoza wengine na kadhalika hivyo walimpendekeza katika majina ya watu wanaohitajika usalama wa taifa....Allen aliitwa usalama wa taifa na alikubali kujiunga na idara hiyo hapo alipatiwa mafunzo ya idara hiyo kwa mwaka mmoja kuhusiana na uzalendo na mambo kuhusu idara kwa mwaka mmoja baada ya hapo alipelekwa nchini Cuba kwa mafunzo ya kikomandoo kwa miaka minne ambako alikamilisha vyema na kisha kupelekwa Marekani kwa mafunzo ya kijasusi kwa miaka mitatu huko walifundishwa mbinu mbali mbali za kijasusi utundu wa teknolojia na kadhalika....baada ya hapo alielekea nchini China kwa mafunzo zaidi ya mapigano ya ana kwa ana;karate, judo,ti chi na mafunzo ya kininja kwa miaka miwili
Kisha alirejea nchini akiwa jasusi aliyekamilika na wa kiwango cha juu kabisa na kuanza kulitumikia taifa
*****************
"Allen pole naona unapewa majukumu tu hata hupumziki" Doreen alimwambia Allen kwa huruma
"Aah tutafanyeje sasa kazi tumeichagua wenyewe" alijibu Allen akitabasamu
"Mmh haya cha msingi urudi salama tiketi yako ya Nairobi hiyo hapo...utaondoka kesho saa 2 asubuhi na Precision air"
"Sawa asante"
"Make sure you return alive" (hakikisha unarudi salama)
"Sawa mke" Allen alijibu kiutani akitabasamu
"Kwenda huko mme gani wewe hata hutulii nyumbani" Doreen na yeye alitania akimwangalia kwa macho fulani yanayoongea, Allen alicheka tu na kuondoka ofisini hapo
Alitoka nje na kuchukua taxi kuelekea hospitali ya taifa hakupenda kutumia gari lake au gari la ofisi....
******************
"Habari yako dada..." Allen alimsabahi dada wa mapokezi
"Nzuri tu" alijibu dada huyo akiwa bize na tarakilishi yake
"Naitwa inspekta Ramadhani Kibanga kutoka kituo kikuu cha polisi" aliongea Allen akitoa kitambulisho chake feki
"Ahaaa karibu sana sijui nikusaidie nini" dada huyu alijibu kwa adabu zote na safari hii akiacha shughuli yake kwenye tarakilishi
"Jana asubuhi kuna mgonjwa alikuwa anafanyiwa oparesheni na baadaye akahamishwa nahitaji kupata taarifa zake zote na daktari mkuu aliyeshughulikia"
"Sawa kaka...."
Dada huyo alibonyeza tarakilishi yake mara kadhaa na kuanza kutoa taarifa
"Mgonjwa aliwasilishwa juzi usiku na polisi kutoka kituo cha Oysterbay, walisema wamemuokota ufukweni usiku hivyo ashughulikiwe na watakuja kesho ambayo ndiyo jana kwa taratibu zingine kwa hiyo sisi bado hatujamtambua....."
"Na daktari mkuu aliyemsimamia anaitwa Dr Austin Meyer na msaidizi wake alikuwa Dr Jonathan Magesa"
"Oooh asante sana binti...sasa nahitaji kumuona huyo Dr Austin..."
"Mmh alifika jana mchana mara ya mwisho leo hajaripoti kabisa"
"Ooh sawa naomba basi nimuone huyo Dr Magesi sijui"
"Hahahahaha ni Dr Jonathan Magesa bahati nzuri umemkuta yupo shift ya usiku leo"
"Sawa namhitaji"
"Ngoja nikupeleke ofisini kwake.."
"Haina haja bibie mimi mwenyeji nielekeze tu ofisi yake ilipo"
"Sawa panda ghorofa ya nne utanyosha na korido ya upande wako wa kulia kwenye kona kabisa ndiyo kuna ofisi yake"
"Asante mrembo" alijibu Allen huku akimpa noti tano za elfu kumi
"Hiyo utanywea chai"
"Asante" alijibu binti huyo akijichekesha.......mambo ya hela bwana
Allen alifuata maelekezo kuelekea kwa Dr Magesa...
"Habari ya jioni"
"Nzuri tu karibu"
"Naitwa inspekta Ramadhani Kibanga kutoka kituo kikuu cha polisi"
"Sawa karibu nikusaidie nini?" Dr Magesa alijibu akiwa kiunyonge amechoshwa na maswali ya hao wanausalama na mapolisi
"Nimekuja kuchukua maelezo ya mgonjwa ambaye mlimsimamia na Dr Austin"
"Ok jana tulimpokea aliokotwa ufukweni na tulimfanyia vipimo tukagundua ana majeraha mbali mbali haswa alionekana amepigwa kichwani na pia tukagundua ini lake limefeli kutokana na sumu ambayo anayo mwilini.....hivyo tukamfanyia matibabu kidogo na jana asubuhi ndiyo tulikuwa tumfanyie oparesheni kubwa mbili kwanza kuondoa bonge la damu lililoganda kichwani na pili kumuondo sumu mwilini kumfanyia 'liver transplant' ambapo tungepandikiza kipande kidogo cha ini ambalo halijaathirika tukiwa katikati ya oparesheni ndiyo mgonjwa akachukuliwa"
"Ahaaa asante dokta na unaweza niambia kama una taarifa zozote za Dr Austin?"
"Mh hapana mara ya mwisho tulionana nae jana jioni lakini kuna kitu nimejifunza kwake ni kama ana wasiwasi na anajua kidogo jambo linaloendelea"
"Kwanini umesema hivyo?"
"Jana wakati tunataka kuanza oparesheni alipigiwa simu na akabadilika na kutuambia tuahirishe oparesheni kwa usalama wa mgonjwa na baada ya hapo akaondoka hadi nilipoonana nae tena mchana"
"Namhitaji kwa kila namna.....anaishi wapi kwani?"
"Mbezi beach nyumba namba 804B"alijibu Dr Magesa akiisoma kadi ya biashara ya Dr Austin
"Sawa nipe namba yake"
Dr Magesa alimpa namba na Allen alishukuru na kunyanyuka kabla ya kuondoka alikumbuka kitu
"Samahani anaishi na nani?"
"Mke wake, mtoto wao mdogo na house girl wao"
"Sawa asante kwa mara nyingine"
Allen aliondoka zake na kurudi mapokezi...
"Mrembo nitajisikia hatia nikiondoka bila hata kufahamu jina lako.." Allen alimwambia mdada yule akimtizama kwa macho ya kichokozi huku akitabasamu kwa mbali
"Naitwa Rehema mheshimiwa inspekta" alijibu kwa utani akitabasamu
"Ooh nashukuru kukufahamu mwenyeji wangu" na yeye alirudisha tabasamu hapo vishimo vidogo mashavuni vilionekana yaani 'dimpoz' hakujau tu alisababisha shida kiasi kani kwa mdada yule
"Ok acha me niende ila naomba nipate mawasiliano yako Rehema..."
Binti huyo hakujibu kitu alitabasamu tu na kutoa kadi yake ya biashara
"I will call you tonight" (nitakupigia usiku) Allen alimwambia huku akimkonyeza na kuondoka maeneo hayo akimwacha binti wa watu akicheka tu mwenyewe.
****************
Baada ya kutoka hospitali Allen alienda moja kwa moja nyumbani kwa Dr Austin na kumkuta binti tu wa kazi....
"Kwa hiyo umesema mama naye pia hajarejea?"
"Ndiyo aliondoka jana asubuhi na mtoto walienda hotelini na baba kuna watu aliondoka nao jana mchana hajarejea mpaka leo"
"Hao watu unawafahamu au alikuaga anaenda wapi?"
"Hapana kaka sisafahamu pia hakuniaga ni kama alikuwa na haraka sana"
"Sawa asante" Allen aliondoka kwani hakuona cha maana cha kubaki hapo
'Mmh hii kazi sasa....au huyu jamaa naye anahusika ameamua kutoroka na familia yake' alijiwazia Allen......'itajulikana tu hapo hapo'
Allen aliwaza abaki Tanzania kumtafuta Dr Austin au aende Nairobi alibaki njia panda.
'Ngoja niende Nairobi halafu itajulikana huko'
******************
'Anaitwa Allen Jacob ataondoka Dar saa 2 asubuhi kwenda Nairobi na ndege kampuni ya Precision air' ujumbe mfupi ulisomeka kwenye kioo cha Doreen ndani ya application ya WhatsApp
'Sawa asante kwa taarifa tutashughulika naye...mzigo wako utaingia kwenye akaunti yako baada ya saa 1' ujumbe wa Faheed
kutoka Riyadh Saudi Arabia ulimjibu
'Asante' Doreen aliujibu na kufuta jumbe zote
'I am sorry Allen I am just doing my job' (samahani Allen nafanya kazi yangu)
Doreen alijiwazia akitabasamu kwani alijua mda sio mrefu akaunti yake itacheka
*****************
"Bosi nimepata taarifa kutoka Tanzania kuwa kuna kijana ametumwa kufuata nyayo zetu anatua Nairobi kesho"Faheed alimwambia bosi wake
"Hahahahaha nilijua tu watatufuata ndiyo maana nikasema mtue kwanza Nairobi.....sasa waambieni akina Rashid huko Nairobi wammalize mara kesho kabla hajajua chochote"
"Sawa bosi"alijibu kwa utii
Allen alikuwa yupo nyumbani kwake akifanya maandalizi ya kuelekea Nairobi kwani aliamua aende kwanza huko na kisha atarejea Tanzania kushughulika na suala la Dr Austin ambalo aliwaachia ofisini kwake waendelee nalo kwa kiasi baada ya maandalizi alipumzika kwa ajili ya safari kwani alijua kwenye kazi zao unaweza usilale kabisa...lakini hakujua kuwa ugeni wake Nairobi ulishatambulika na tayari mipango kabambe iliandaliwa dhidi yake.
Mapema asubuhi Allen aliamka na kuingia bafuni kujiweka sawa kichwa chake bado kilikuwa kikiwaza sakata hilo it alilonalo.....alipitia ofisini kwao mapema ili kuacha maagizo ya kumtafuta Dr Austin na pia huko alienda kuchukua picha za watu waliosadikika kumchukua mgonjwa yule ambazo zilipigwa na kamera za ulinzi za Muhimbili na uwanja wa ndege
"Mbona umezichana?' Doreen alimuuliza kwa mshangao baada ya Allen kuzichana zile picha
"Nimeshazihifadhi kichwani, haina haja kutembea nazo zitaniharibia kazi" Allen alijibu
"Sawa kazi njema urudi salama" Doreen alimuaga akiweka sura ya huruma ila alijua kinachoendelea
"Nitarudi salama usijali"
"Kitu kingine...utafikia Swiss lenana mount hotel nimebook chumba namba 773"
"Sawa mke ndio maana nakupenda unajua jinsi ya kunijali" alijibu Allen kwa utani na kutabasamu kama kawaida yake
"Hebu nenda huko mme gani wewe kwanza sio type yangu"
"Hee kumbe mwenzagu umeumbwa na kokoto mimi nikajua wote tumeumbwa na udongo" wote walijikuta wakicheka na Allen akaanza kuondoka
"Allen"
"Yes"
"Take care..." (Uwe mwangalifu)
"I will" (nitafanya hivyo)
"Ok" Doreen alijibu akijua kabisa kuwa jamaa anavuta pumzi za mwisho
'Swiss Lenana mount hotel-773' aliandika ujumbe na kumtumia Faheed
******************
MASAA SABA NYUMA-PEMBEZONI MWA MSITU WA ARBEDARE KENYA
"Hakikisha mnakamilisha bila shida yoyote" yalikuwa ni maneno ya mwisho kutoka kwa Faheed akimuelekeza bwana Rashid wa Nairobi kwenye simu
"Sawa kaka"
Pembezoni mwa msitu wa Arbedare kulikuwa na kambi kubwa ya kijeshi iliyoendeshwa kwa siri, kambi hii ilikuwa ikisimamiwa na bwana Rashid mwenye asili ya Iran.....baadhi ya viongozi wa serikali walifahamu uwepo wa kambi hii isiyo rasmi lakini walifunga midomo kwa sababu ya pesa waliyopewa...
Katika kambi hii vijana mbalimbali walikuwa wakipatiwa mafunzo makali ya kijeshi, walikuwepo watu wa asili mbalimbali waafrika, waarabu, wazungu na waasia wachache....
Pia vifaa vizito vya kijeshi vilihifadhiwa kwenye kambi hii....
Bwana Rashid aliwaita vijana wanne kutoka
katika kambi hiyo ndani ya ofisi yake...aliwapatia picha ya Allen na kisha kuwapa maelekezo...
"Pichani ni Allen Jacob jasusi kutoka Tanzania ataingia kesho kuanzia mida ya saa tatu na Precision air tunatakiwa kumkaribisha na kumpumzisha kuzimu kabla hajaleta madhara nadhani tumeelewana"
"Ndiyo" walijibu kwa pamoja
"Mnatakiwa kuondoka usiku huu muelekee Nairobi kumsubiri, mtachukua kila mnachohitaji.....kazi njema sitaki uzembe juu ya hili"
"Sawa mkuu" walijibu na kuondoka tayari kwa safari ya kumkaribisha Allen
*****************
"Abiria fungeni mikanda tafadhali.....tunaelekea kutua"
Ndege ya kampuni ya Precision air ilitikisika kidogo wakati wa kutua na kuzunguka kwenye njia zake (runways) kwenye uwanja wa kimataifa Jomo Kenyatta na kisha kusimama kabisa
Baada ya mda kidogo abiria walianza kushuka
"Khalid kuwa makini kuangalia ndiyo wanashuka" sauti ilimuelekeza kwenye kifaa cha mawasiliano alichovaa
Baada ya kama abiria kumi kushuka Allen alikuwa akishuka kwenye ngazi za ndege hiyo alivaa suti ya ghali na miwani ya jua machoni....miwani hii haikuwa ya kawaida kwani ilikuwa na uwezo wa kupiga picha na kurekodi kukuza picha za vitu vya mbalimbali na kutambua kama mtu amebeba silaha au kitu chochote cha chuma kwa kutumia X-Rays
Kwa macho ya kijasusi aliwaangalia watu wote hapo uwanjani haraka haraka, hakuna aliyemtilia shaka zaidi ya kuwaona watu wachache wenye bastola ambao alijua tu ni maafisa usalama
Alivuta hatua kuelekea jengo la ukaguzi kukamilisha taratibu zote......
"Naomba paspoti yako tafadhali" kijana aliyehusika na uhamiaji alimwomba
Paspoti yake ilimtambulisha kama Jean Mwikiza mfanyabiashara raia wa Congo ambaye alikuwa Tanzania kwa mapumziko na atakuwa hapo Kenya kwa wiki mbili kwa vikao vya kibiashara...
Baada ya kijana yule kujiridhisha na maelezo hayo alipiga muhuri paspoti hiyo na kumruhusu kwenda
"Kwa mwendo wa madaha Allen alitoka nje ya jengo hilo bwana Khalid alikuwa nyuma yake akimfuatilia kwa mbali bila ya yeye kujua nje alilakiwa na madereva taxi wengi
Baada ya kuapatana na mmojawapo alipanda taxi yake
"Umesema nikupeleke......"
"Swiss Lenana mount hotel" Allen alimjibu ilikuwa ni hotel ambayo Doreen alimkodia chumba chumba toka jana
"Sawa mkuu....karibu sana Kenya nadhani ni mara yako ya kwanza kufika"
"Hapana"
"Sawa naitwa Munyemo nitakuwa mwenyeji wako ukipenda" dereva alimwambia akianza kuondoa gari maeneo hayo
"Asante"
Khalid aliingia kwenye gari yao na kuwakuta wenzake watatu
"Itabidi tumfuatilie nadhani....." mmoja wao aliongea
"Hapana hatuwezi kwenda wote mkuu ametuma ujumbe kuwa anafikia Swiss Lenana hotel chumba namba 773 hivyo mimi na Khalid tutamfuatilia, wewe na Jordan muwahi kumsubiri huko nadhani tutammaliza huko hotelini" mwingine alitoa maelezo
"Wazo zuri" mwingine alijibu na kisha waligawana Jordan na mwenzake walishuka na kuingia kwenye gari nyingine na kuchomoka kwa kasi kuwahi hotelini kabla ya Allen kufika na Khalid na mwenzake walianza kumfuatilia kwa mbali wakiacha kama gari tatu kati yao ili wasigundulike
Allen ndani ya taxi aliendelea kuwa makini na usalama japo kuwa hadi mda huo hakuona kitisho chochote cha usalama lakini bado aliendelea kuwa makini
Kupitia vioo vya pembeni vya gari aliliona gari jeusi likiwafuata kwa umbali mrefu mwanzoni alilipuuzia lakini baadae alikuwa na mashaka nalo
"Hebu kata hapo kulia" alimpa maelekezo dereva taxi, ambaye alichepuka kwenye barabara kuu Mombasa road na kuingia Lusaka road na gari hilo liliendelea kuwaungia mkia
"Kata tena hapo" aliendelea kutoa maelekezo
Dereva aliingia Ladhies road bado gari hilo liliendelea kuwafuata, Allen akagundua kuwa wanafuatwa, aliiona pub moja pembeni ya barabara
"Sasa ndugu kuna mtu nahitaji kumuona mara moja simamisha hapo" Allen alimweleza dereva
"Sasa mkuu sasa itakuwaje ukichelewa si........." Alijikuta akinyamaza baada ya Allen kumpa bunda la dola 100
"Ukiona nimechelewa unaweza kwenda" alimjibu akifungua mlango na kuondoka kuelekea ndani ya hiyo pub
Baada ya mda Khalid naye alitoka ndani ya gari na kuanza kumfuta kama mtu ambaye hana shughuli naye, lakini hakujua Allen ameshamsoma
Allen alinyoosha moja kwa moja kwenye vyoo vya pub hiyo na kuingia ndani.... alifurahi kukuta hamna mtu hivyo alitulia pembeni ya mlango akaamua amsubiri jamaa ajichanganye, Khalid naye alimfuata na kufika mlangoni...alijiuliza aingie au amsubiri na hapo akafanya kosa la kuamua kuingia kichwa kichwa....
Alijikuta anavutwa ndani kwa nguvu mara tu alipotokeza, alijikuta anapata ngumi tano za haraka haraka za uso.....akaona nyota nyota, aliamua kuchomoa bastola yake yenye kiwambo cha kuzuia sauti ili ajihami, lakini alichelewa kwani mkono wake ulipigwa teke na Allen akamrukia teke aina ya 'flying kick' lillilomsindikiza ukutani na kumbamiza, alikuwa hoi hakuweza hata kuinuka
"Kumbe mtu mwenyewe mdebwedo hivi halafu unafuata fuata wanaume" Allen alimkebehi
Hakumpa nafasi ya kujibu alimrukia na goti kifuani hapo Khalid alijikuta anatema damu kisha alimvunja shingo, alimvutia ndani ya choo kimoja ili amfungie
"What's going on Khalid" (nini kinaendelea Khalid)
Alisikia sauti kwa mbali kwenye kifaa cha mawasiliano alichovaa Khalid, alijua jamaa yake anaweza kuja kumfuata hivyo alitoka nje haraka kupitia mlango wa nyuma...alipokuwa anaelekea upande wa mbele alimuona mwenzake akishuka kwa pupa na kuingia ndani ya pub...
Allen alipita kwa kujibanza kwenye magari yaliyopo parking na kuliendea gari la kina Khalid
"Hana akili amesahau hata kufunga mlango" Allen aliwaza akitabasamu, aliingia ndani ya gari na kujilaza kimya kwenye siti za nyuma akimsubiri huyo bwege ajichanganye na kurudi garini........
Jamaa aliingia pub na kuanza kumtafuta Khalid, hakumuona Khalid wala Allen.... alichanganyikiwa, baada ya kuwakosa alielekea vyooni huko alishtuka kuona michirizi ya damu ukutani alishtuka na kuchomoa bastola yake haraka kwa uangalifu alifungua choo kimoja kimoja, alipofika mlango wa mwisho alishtuka kumuona mwenzake ametulia chini
'amekufa' alitahamaki
Haraka aliangalia huku na huko kumtafuta adui lakini hakumuona
Alitoka nje ya pub kwa haraka na kuelekea kwenye gari lao
'inabidi nikamjulishe bosi na kina Jordan kuwa tumegundulika' aliwaza kwa haraka aliingia ndani ya gari pasipo tahadhari na kuliwasha
"Tulia hivyo hivyo na ujibu maswali yangu ukijifanya mjanja nakumwaga ubongo" chuma cha baridi kilimgusa na kufuatiwa na sauti ya kibabe
ITAENDELEA USIKOSE SEHEMU IJAYO..........
Tags:
Hadithi za Kijasusi
