ACETAMIN-220...(02)
MTUNZI:BARAKA GEOFREY
+255652089642
ILIPOISHIA..........
Haraka aliangalia huku na huko kumtafuta adui lakini hakumuona
Alitoka nje ya pub kwa haraka na kuelekea kwenye gari lao
'inabidi nikamjulishe bosi na kina Jordan kuwa tumegundulika' aliwaza kwa haraka aliingia ndani ya gari pasipo tahadhari na kuliwasha
"Tulia hivyo hivyo na ujibu maswali yangu ukijifanya mjanja nakumwaga ubongo" chuma cha baridi kilimgusa na kufuatiwa na sauti ya kibabe
ENDELEA........
Bwana yule alijilaumu kwa kuingia mtegoni kirahisi kama nyumbu, alishindwa cha kufanya...watu wa nje walishindwa kujua kinachoendelea kwani vioo vya gari vilikuwa 'tinted'
"Nyie Ni kina nani na kwanini mnanifuatilia" aliuliza Allen kitemi
"Nani kakwambia tunakufuatilia mimi nina mambo yangu bwana" jamaa yule alijibu kijeuri
"Bila shaka umeona kilichompata mwenzako sitaki kurudia swali"
"Mwenzangu yupi we mwendawazimu nini"
Allen alijua jamaa hawezi kutoa ushirikiano hivyo alimpiga na kitako cha bastola kwa nguvu chini ya kisogo na hapo jamaa alipoteza fahamu
'Atasema tu ngoja nipate sehemu ya kuongea naye vizuri..' aliwaza
Alimvuta jamaa kwenye siti ya nyuma kumfunga mikono kwa pingu ambazo aliziona humo kwenye gari...alimpekua kama atamkuta na chochote cha maana....hakupata kingine zaidi ya simu ya mkononi.....aliipekua haraka na akakutana na ujumbe uliomshtua 'Swiss Lenana mount hotel-773' ulisomeka ujumbe huo alipoangalia alieutuma alikutana na jina la Rashid......
'Mh kumbe hawa washenzi wana taarifa zangu' aliwaza
Kwa haraka alijua kuna watu watakuwa wanamsubiri hotelini, alizima simu ya bwana Rashid na kisha kuitoa simu yake na kuipiga.....
"Bosco"
"Nambie kaka umeshaingia Nairobi?" upande wa pili uliuliza
"Ndiyo..."
"Sawa kaka nakuja hapo hotelini sasa hivi..."
"Sasa kuna wageni wasio rasmi huko fanya hivi pitia hapo hotelini kawachore bila kuwashtua wapo chumba namba 773 kisha njoo na gari hapa Senator pub kuna mtu ninaye nataka ahifadhiwe kisha nikaongee na hao wageni"
"Sawa nipe dakika chache nitakuwa hapo"
Bosco alikuwa ni mtanzania jasusi wa idara ya usalama wa taifa ambaye alikuwepo Kenya kwa kazi maalum nchini Kenya alikuwa akijihusisha na biashara ya vifaa vya umeme alikuwa na duka kubwa jijini Nairobi na matawi Mombasa na Eldoret na alifahamika kama George Kimaro....wengi walimfahamu kama mfanyabiashara tu kutoka Tanzania
Allen aliwasiliana nae kabla hajaja Nairobi ili amwandalie mazingira ya kazi yake
Bosco alibandika ndevu za bandia na kuvaa kofia kubwa na miwani na kisha alielekea hotelini Swiss Lenana na kwenda moja kwa moja mapokezi.....
"Habari yako" alimsalimu kijana wa mapokezi
"Nzuri karibu sana"
"Asante...... nahitaji chumba first class"
Kijana yule alibonyeza tarakilishi yake kwa mda kidogo
"Kipo chumba namba 787 floor vya nne"
"Sawa"
Bosco alitoa taarifa zake za uongo na kukodi chumba hicho, kijana alimsindikiza mpaka chumba chake na kumuaga akimpatia maelekezo machache na kadi ya mlango wake
"Asante sana"
"Karibu sana ukihitaji msaada wowote utatupigia"
Mara baada ya kijana yule kuondoka Bosco alitoka nje ya chumba chake na kupita koridoni alizisoma namba za vyumba haraka haraka na kuelekea mlango wa chumba namba 773 kupitia chini ya mlango aliingiza kifaa kidogo kama punje ya harage ambayo ilikuwa ni kamera ya kisasa yenye uwezo mkubwa bila kwa namna ambayo asingewashtua waliopo ndani, aliondoka mahali hapo na kurudi mapokezi
"Kijana nimesahau mzigo wangu narejea baada ya mda mfupi" alimuaga kijana wa mapokezi
"Sawa kaka hamna shida"
Bosco alielekea kwenye gari lake na kuwasha tablet ambayo iliunganishwa na ile kamera....aliangalia kona zote za chumba na aliwaona watu wawili mmoja alikuwa amejibanza nyuma ya kabati na mwingine alikuwa pembeni ya mlango.... alitabasamu kidogo na kuwasha gari kumfuata Allen Senator pub
**************
Baada ya mda mfupi gari nyekundu aina ya Toyota auris iliingia kwenye parking ya Senator pub.....
"Sogeza gari hapa karibu na Harrier nyeusi" Allen alimpa maelekezo Bosco kwenye simu
Kwa pamoja walimhamishia yule jamaa kwenye gari la Bosco bila kuonekana
"Sasa wewe nenda ukamhifadhi mahali salama mimi naenda kushughulika na wale wa hotelini then utakuja kunichukua hapo"
"Sawa kaka kazi njema" alijibu Bosco alimkabidhi ile tablet
***************
"Mbona kina Khalid hawapatikani?" Jordan alimuuliza mwenzake kupitia kifaa cha mawasiliano
"Sijui tusubiri dakika 15 kama itakuwa bado kimya itabidi tuondoke kwani inawezekana kuna hatari" mwenzake alimjibu, na wote walitulia kimya kusubiri windo lao
Allen aliwasili hotelini na kuelekea mapokezi
"Habari kijana"
"Salama karibu Swiss Lenana mount hotel"
"Asante naitwa Jean Mukiza chumba changu kimeshalipiwa"
"Oh sawa ni namba 773?"
"Ndiyo"
"Karibu sana" kijana alichukua mkoba wa Allen akitaka kumpeleka
"Usijali nitaenda mwenyewe mimi sio mgeni mahali hapa" alimzuia
"Hamna shida mkuu"
Allen alipanda lift kuelekea chumba chake ambacho kilikuwa floor ya nne kupitia tablet aliyopewa aliwasoma jamaa jinsi walivyokaa......alifika mlangoni alitizama huku na huko akavaa gloves zake kuzuia kuacha alama za vidole kisha akafungua mlango kwa kadi aliyopewa na kutulia kidogo...aliishika bastola aina ya berreta M9 yake vizuri yenye kiwambo cha kuzuia sauti na ghafla aliupiga mlango teke la nguvu ukambamiza Jordan aliyetoa mguno hafifu bwana maumivu wa kisha aliingia sarakasi maridadi na kufyatua risasi mbili zilizompata yule jamaa wa nyuma ya kabati kifuani na bila kuomba maji aliaga dunia
Jordan aliyekuwa pembeni ya mlango alipagawa kwa tukio hilo la ghafla na kuanza kurusha risasi bila mpangilio ambazo ziliishia kuchimba ukuta....kisu kilichorushwa na Allen kilimpata sawa sawa mkononi na alijikuta akiitupa bastola yake chini akiugulia maumivu
Pasipo kupoteza mda Allen alimchapa risasi moja ya kichwa na habari yake ikaishia hapo
'sio mimi aliyewatuma ndio amewaua' Allen alijisemea aliokota kamera ndogo iliyotegwa na Bosco kisha aliufunga mlango wa chumba kama hakuna kilichotokea na kushuka kwa ngazi mpaka floor ya chini alipita upande tofauti na mapokezi na kutokea jikoni
"Vipi bwana mkubwa mpaka huku?" mpishi mmoja wa jikoni alimuuliza
"Aah....nimekuja kuweka order ya chakula"
"Si ungepiga tu simu mapokezi wangetupa order"
"Oh sikujua"
"Sawa mkuu tukuandalie nini"
"Ugali na samaki na juice ya pera"
"Tukuletee chumba namba ngapi?"
"Hamna haja nileteeni tu kule bustanini nipunge upepo"
"Sawa mkuu"
Mpishi yule alipoondoka tu eneo hilo Allen aliangalia huku na huko akaruka dirisha na kujikuta chumba cha kubadilishia mavazi wapishi.....hapo alivaa nguo mojawapo juu ya nguo zake na akapita tena dirishani na kutokea upande wa nyuma wa bustani... 'bro njoo unichukue hapa Milimani road' alituma ujumbe mfupi kwa Bosco na kisha aliivuta kofia yake usoni na kuuruka ukuta wa hoteli aliambaa na ukuta mpaka barabarani aliiona gari ya Bosco na akajitoma ndani
"Vipi kaka umefanikiwa"
"Aah watu wenyewe warembo tu wale"
"Hahahahaha nakujua Allen huwa hukosei sasa kifuatacho....."
"Tunaenda kwa yule jamaa yetu nina mahojiano naye"
"Poa kaka twende nimemuweka nyumbani..."
"Kuna usalama kweli?"
"Ndiyo tena mkubwa tu si unajua kazi zetu hizi"
"Sawa....una vifaa hapo nyumbani?"
"Vifaa gani"
"Vya kuwafanya mabubu waongee"
"Hahahahaha usijali kaka ushindwe wewe tu" Bosco alijibu na safari ilianza kuelekea nyumbani kwake Thika pembeni kidogo ya mji
Walifika nyumbani baada ya takribani dakika 20 nyumba kubwa nzuri ya kisasa ilikuwa mbele yao, Bosco alibonyeza rimoti yake na geti lilifunguka, gari iliingizwa ndani na wote walishuka
Bosco aliweka alama yake ya kidole na mlango wa kuingia ndani ulifunguka
"Katibu Allen" alimkaribisha mgeni wake
"Asante kaka kumbe una jumba zuri hivi" aliuliza akitabasamu kama kawaida yake
"Kawaida tu mzee..."
"Kwa hiyo ukimleta mtoto hapa hachomoki" Allen alitania
"Aah siku hizi nimeokoka bwana" wote wakicheka
"Nadhani tuingie kazini sasa" Allen alisema
"Poa" Bosco alimwongoza Allen mpaka chumbani kwake ambapo alienda na kuitoa picha iliyokuwa ukutani chini kulikuwa na kitufe chekundu alikibonyeza na mara kabati la chumbani lilisogea pembeni
Kulikuwa na mlango wa Siri Bosco aliingiza nywila na kuweka alama zake za vidole mlango ulifinguka na ngazi zilizoshuka chini zilionekana
"Aisee kumbe umejipanga hivi bro"
Bosco hakujibu alitabasamu tu.... walishuka ngazi na kuingia kwenye ofisi nzuri
"Hapa ndiyo ofisini" Bosco alitoa maelezo na kisha kuufungua mlango ambao uliwapeleka kwenye chumba kingine
Walipoingia Allen alimwona yule bwana aliyemteka amefungwa vizuri kwenye kiti...alitabasamu na kuikubali kazi ya Bosco...alikuwa bado amepoteza fahamu.. Allen alichukua maji ya baridi na kummwagia usoni bwana yule alikurupuka kama mtu aliyekuwa anaota ndoto ya kutisha...Allen alivuta kiti na kukaa mbele yake alimuangalia na kutabasamu kwa dharau
"Mda wa kulala umeisha mkuu" mtu yule alimtumbulia tu macho
"Nadhani tuliongea kidogo kwenye gari lakini ulikuwa mbishi kidogo sasa nimekuja tuongee vizuri tu kirafiki lakini ukitaka nibadilike sitasita kufanya hivyo" Allen alitoa maelezo mafupi
"Ok tuendelee tulipoishia nyie ni kina nani na kwanini mnanifuatilia?" alimalizia swali lakini mtu yule aliendelea tu kumuangalia
"Hujasikia au?" Aliendelea tu kumshangaa
Allen kwa hasira alimchomeka kwa nguvu kisu kwenye paja
"Aaaaaaaaaaaaargh" bwana yule alipiga ukunga wa maumivu
"Hahahahaha kumbe unaongea nilijua wewe bubu haya jibu maswali yangu au tuendelee?"
Bwana yule alikaa kimya tu akimuangalia kwa hasira...."Bosco naona mtoto mbishi hebu nipatie hiyo koleo nimng'oe jino moja moja"
Allen alishika koleo hiyo tayari kwa kazi lakini alishangaa kumuona jamaa akikakamaa na kisha kutulia kimya
Alimfungua mdomo kwa nguvu na hapo aliona jamaa anamalizia kumeza kidonge cha sumu
'Shiiit...stupid' aling'aka kwa hasira
Ilikuwa ni bora jamaa yule afe kuliko kutoa siri
"Duh kazi ipo kaka" Bosco alimwambia Allen
"Hawa ni kina nani"
"sijui lakini inawezekana ni magaidi wa Al shabaab huwa ndio wanajiua kwa staili hiyo wakikamatwa huwa wanakuwa na vidonge vya sumu wanatembea navyo" Bosco alitoa maelezo
"Hapana haiwezekani...magaidi wanahusikaje kwenye hili suala"
"Huwezi jua kaka tuendelee maana hata mimi sielewi kabisa kwanza najiuliza hawa watu wamejuaje uwepo wako Nairobi wakati ilikuwa ni siri"
"Hata mimi nashangaa hata chumba ninachofikia walifahamu pia"
"Mh sasa sijui tutaanzia wapi" Bosco aliuliza
"Nadhani uwanja wa ndege ni pazuri kuanzia uchunguzi tukaangalie kama jamaa ni kweli walitua Nairobi na ikiwezekana kufuatilia walipoelekea"
"Wazo zuri bro nadhani tuanze kesho"
"No Bosco we have no time, tunaenda sasa hivi"
"Poa ngoja niwacheki watu wangu pale Jomo Kenyatta watufanyie mpango"
"Sawa tuondoke basi"
"Mbona haraka nyingi tulia basi niwaambie tusijeharibu"
"Yani hujui tu Bosco kuna mambo nimeacha Tanzania hayajakaa sawa ndiyo maana nataka tumalizane na haya mapema"
"Sawa lakini tusikurupuke tutaharibu kazi"
ITAENDELEA USIKOSE SEHEMU IJAYO
