Acetamin 220 (05)

 ACETAMIN-220...(5)

MTUNZI:BARAKA GEOFREY

0652089642

TAHADHARI:Majina na matukio yote kenye simulizi hii ni ya kutungwa tu kwa ajili ya kufikisha ujumbe.


ILIPOISHIA..........

Austin alipelekwa kulelewa huko ili alelewe, asomeshwe na atimize ndoto zake kwa mara ya kwanza ilikuwa vigumu sana kwa Austin kujichanganya na wenzake kwani tukio la kifo cha mama yake na kuchukuliwa mdogo wake lilimuathiri vibaya kisaikolojia lakini baadae alijikuta akisahau na kurudi katika hali ya kawaida

"Austin ukiwa mkubwa unatamani kuwa nani?" mlezi mmoja aliyeitwa sister Magreth alimuuliza

"Nataka kuwa daktari bingwa ili nitibu wengine"

"Sawa mtangulize Mungu siku moja utafikia malengo yako"

ENDELEA............

Austin aliendelea kukua na alikuwa ni kijana mpole mwenye akili nyingi sana walezi wake na watu wengine walimshangaa sana Austin kwa akili zake, aliendelea kuweka juhudi kwenye masomo yake alimaliza kidato cha nne kwa daraja la kwanza la pointi nane na pia alikuwa mwanafunzi bora kwenye somo la Chemistry na Biology baada ya hapo alijiunga kidato cha tano mchepuo wa PCB alimaliza kidato cha sita akipata daraja la kwanza la pointi tatu na alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi kumi bora waliofanya vizuri alijiunga na chuo kikuu cha Havard nchini Uingereza kusomea masomo ya udaktari kwa kwa ufadhili wa mtu mmoja ambaye hakumjua alisomea udaktari kwa miaka sita na kisha kusomea zaidi kwenye masuala ya ini (hepatologist) kwa miaka mitatu


                    ******************

Aaron alichukuliwa na wale wanamgambo wa Al qaeda na kusafirishwa pamoja na watoto wadogo wengine mpaka Peshawar Pakistan yaliko makao makuu ya kundi hilo

Al qaeda walikuwa wakichukua watoto wadogo ili kuwafundisha na kuwafanya kuwa wanajeshi wao wengine walipewa mafundisho maalum ya kutoogopa kifo ili watumike baadae kama watu wa kujitoa mhanga kwaajili ya mashambulio ya kigaidi duniani kote

"Wewe unaitwa nani?" mtu mmoja mwenye umri wa makamo mwenye asili ya kiafrika aliyekuwa na ndevu nyingi alimuuliza kwa lugha ya kiingereza

"Aaron Meyer" alijibu mtoto huyo kiuoga sana

"Kuanzia leo utaitwa Ayman al-Zawahiri sawa?" Aliuliza mtu huyo akimuangalia kwa macho makali

"Sawa" alijibu Aaron akiinama chini

"Niangalie machoni" Aaron aliinua macho yake na kumuangalia machoni mtu huyo mwenye macho ya kikatili sana, mtu huyo alimuangalia kwa karibu dakika mbili na Aaron hakukwepesha macho yake

Tabasamu lilichanua kwenye macho ya mtu huyo 'Mpambanaji' aliwaza mtu yule mwenye madevu

Mtu yule alikuwa na kazi ya kumsaili kila aliyeingizwa kambini hapo na kuamua aingie sehemu gani


"Mahmoud" aliita mtu yule

"Mpeleke huyu kwenye kikosi ni mpambanaji huyu" alitoa maelezo bwana yule na hapo Aaron alichukuliwa na kupelekwa chumba cha kubadilishia nguo pasipo kujali umri wake wa miaka mitano alivalishwa gwanda na kupewa mtutu wa AK47 ambao alikuwa akiuona tu kwenye televisheni kisha akapelekwa kwenye uwanja mkubwa huko alikuta watoto wengi wa asili mbalimbali walikuwepo waafrika,waasia,wazungu, na wahindi walikuwa wamekaa uwanjani eneo hilo na wametulia kimya kila mmoja alishikiliia mtutu wake na walivaa gwanda za kundi la Al qaeda, Aaron alielekezwa sehemu ya kukaa na alikuwa akitoa machozi kwa hofu na kumkumbuka mama yake na kaka yake Austin


Baada ya mda mfupi mtu mmoja mrefu mwarabu aliingia eneo hilo alikuwa amefuga ndevu nyingi nyeupe na alijifunga kilemba kichwani alifuatiwa na watu wengine kadhaa akiwepo yule aliyemsaili Aaron

Watoto wote pale walisimama kwa heshima na kunyanyua silaha zao juu, Aaron hakuelewa na yeye alifuatisha tu...walikaa tena chini baada ya kutoa heshima zao


"Wewe njoo hapa" mtu yule mwarabu alimwita mtoto mmoja wa kizungu kwa kiarabu akimnyooshea kidole na mtu yule aliyewasaili kina Aaron akatafsiri kwa kiingereza, mtoto yule alisogea mbele akitetemeka

"Kwanini unalia?" Alimuuliza akimkazia macho

"I want my mother back" alijibu mtoto yule akiendelea kulia, na ghafla mwarabu yule alimtandika risasi kichwani na mtoto yule akafa pale pale

"Mpambanaji anayemuwaza mama yake hahitajiki hapa" alizungumza mwarabu yule kwa sauti na hapo Aaron alijikuta akifuta machozi yake yote na kutulia kimya

"Tupo hapa kwa ajili ya kuitafuta haki na amani ya kweli duniani..." alianza kuhutubia mwarabu yule kwa sauti


"Hakuna haki pasipo kuitafuta....madhalimu wa dunia hii wanaiendesha dunia wanavyotaka, wanaingiza mambo ya kishenzi kwenye ulimwengu huu na kuleta machukizo mbele za Mwenyezi Mungu, wanakandamiza mataifa masikini na kuwawekea vikwazo ili wafuate matakwa yao ya kidhalimu hatupo tayari kwa hilo na hivyo tupo hapa kupambania amani ya kweli..." Aliweka kituo mtu yule akimsubiri mtafsiri wake atafsiri kwa kiingereza

"Amani ya kweli haipatikani mpaka damu imwagike na tupo tayari kumwaga damu kwa ajili ya haki na amani ya kweli" mtu yule alimaliza na kuondoka mahali pale akifuatiwa na wenzake kadhaa, haikujalisha lugha zilizoongelewa zimeeleweka au la ila alikuwa tayari amefungua rasmi mafunzo ya ugaidi kwa watoto wale wadogo wasioelewa jema wala baya walikabidhiwa kwa wakufunzi wao tayari kuanza mafunzo, kambi ilikuwa katikati ya msitu ulioitwa Ziarat, mahali hapo palikuwa na ulinzi mkali sana


Mafunzo yalianza rasmi siku iliyofuata...walikurupushwa saa 10 usiku na kupelekwa uwanjani hapo walifanya mazoezi ya kuweka viungo sawa kisha walianza kukimbia katikati ya msitu kwa mda wa karibu masaa manne, watoto wengi walizimia na wawili walipoteza maisha katika zoezi hilo la ufunguzi, hakuna aliyejali ilikuwa ni kazi kazi


Ratiba ilikuwa ngumu na mazoezi pia yalikuwa ni mazito sana kwa watoto wale pia ukatili ulikuwa mkubwa kambini hapo, kwao kuona mtu anauawa kwa kupigwa risasi au kuchinjwa kama kuku lilikiwa jambo la kawaida na kadri siku zilivyozidi kwenda roho ya kinyama ilianza kuwaingia taratibu


Kwa miaka minne mfululizo mafunzo makali ya kijeshi yaliendelea tayari watoto wengi walishakata tamaa ya kurudi kwao na wengine walisahau kabisa akili zao zote zilihamia hapo na walijua hayo ndio maisha yao, kwa miaka hiyo waliyofundushwa walikuwa wameiva haswa na walikuwa ni wanajeshi kamili japo walikuwa bado ni wadogo na walianza kutumwa kenye mission mbalimbali


Siku moja wakiwa uwanjani kwa ajili ya kupewa matangazo mbalimbali mkuu wao aliita majina ya watoto wanne na Aaron alikuwepo, walienda kwenye ofisi maalum na huko walikuta vijana wengine wanne wakubwa kuliko wao wenye umri wa takribani miaka 20


"Nyie mmechaguliwa kwenda kumsindikiza mkuu wetu Abd al-Uzza kutoka Islamabad international airport kesho kutwa mpaka hapa kambini hivyo mkajiandae" mkuu wao aliwaeleza ambaye ndiye aliyempokea Aaron siku ya kwanza aliitwa Abdel Fattah

"Sawa mkuu" walijibu kwa pamoja na kila mtu alirudi kwenye shughuli yake


Abd al-Uzza alikuwa ni mmoja wa wafadhili wakubwa wa Al qaeda na makundi mengine ya kigaidi alikuwa ni tajiri mkubwa sana aliyeishi nchini Saudi Arabia alimiliki visima vingi vya mafuta ambavyo vilikuwa ni chanzo cha utajiri wake mkubwa sana aliheshimika sana ukanda wote wa mashariki ya kati pia katika nchi zote za kiarabu kama mfanyabiashara na uhusika wake wa makundi ya kigaidi ulikuwa ni siri kubwa.

Mataifa yenye nguvu duniani hususani Marekani waliitamani sana biashara ya mafuta iliyokuwa ikifanyika mashariki ya kati ambayo kwa wakati huo ilishikiliwa na bwana Abd al-Uzza hivyo walianza kumuwekea vikwazo mbalimbali kisiri ili aanguke kibiashara na wao kushikilia biashara hiyo, hivyo bwana Abd aliamua kuvifadhili vikundi mbalimbali vya kigaidi kwa siri ikiwemo Al qaeda vilivyokuwa vikipambana na serikali ya Marekani na alikuwa na safari ya kuelekea nchini Pakistan kuangalia maendeleo ya kundi la Al qaeda na pia kuchagua baadhi ya vijana mahiri arudi nao Saudi Arabia kwa kazi maalum


Asubuhi ya siku ya kumpokea bwana Abd al-Uzza vijana wote waliochaguliwa walikuwa tayari na waliondoka asubuhi mapema kuelekea uwanja wa kimataifa wa Islamabad walivalia kiraia na waliondoka na msafara magari manne ya kifahari ya kipindi hicho Audi A4 waliambatana pia na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa Al qaeda.. I


                     ***************

WASHINGTON D.C MAKAO MAKUU YA FBI (Federal Bureau of investigation)

"Sir we have got information Abd al-Uzza will land on Islamabad international airport tommorow at twelve o'clock afternoon" (Mkuu tumepata habari Abd al-Uzza atatua uwanja wa kimataifa wa Islamabad saa sita mchana) sauti ilisikika kwenye simu ya mkurugenzi wa shirika hilo la kiusalama Mr Giovanni Alex na kisha simu ilikatika, tabasamu lilichanua usoni mwa Mr Giovanni 'hatimaye anayenisumbua kichwa amepatikana' aliwaza na kisha aliingia kwenye mtandao wa Skype na kuanza kuongea na Jordan mmoja wa majasusi wa shirika hilo aliyeko nchini Pakistan akimpa maelekezo ya kuhakikisha kwa kushirikiana na wenzake bwana Abd anauawa haraka iwezekanavyo.


                    ***************

Gari zaidi ya 20 aina ya Audi A4 nyeusi gari zilizotamba mwanzoni mwa karne ya 21 zilikuwa zikitoka uwanja wa ndege, ulikuwa ni msafara wa bwana Abd al-Uzza ndani yake pia zilikuwepo gari nne za kina Aaron kutoka kambini kuhakikisha ulinzi

Bwana Abd al-Uzza alikuwa ndio ametokea nchini Saudi Arabia yalipo makazi yake msafara huo ulikuwa ukielekea ikulu katika makazi ya rais Pervez Musharraf kwa maongezi mbalimbali ya kibiashara.

Katika muda wote huo hawakujua kuwa majasusi makini kutoka CIA walikuwa wakifuatilia kwa making

Aliingia ikulu na kupokelewa vizuri na rais huko waliongea masuala mbalimbali juu ya biashara na uwekezaji wa mafuta nchini humo, mikataba mbalimbali ilisainiwa na kikao hicho kilihitimishwa baada ya masaa mawili, bwana Abd al-Uzza aliendelea na mizunguko mbalimbali kwa mda wa saa moja na baadae msafara wake ulielekea Peshawar yaliko makao makuu ya Al qaeda mda huu msafara wake ulipungua yalibaki magari sita tu manne kutoka kambini na mawili yaliyobeba walinzi wake binafsi na baadhi ya watu alioambatana nao kutoka Saudi Arabia

Juu ya ghorofa refu lililoko maeneo ya Chughal Pura alilala mwanaume mmoja makini aliyevaa suti nyeusi jicho lake likiwa katika darubini ya bunduki ya kudungulia (sniper riffle) aina ya Barrett M82 ambayo ni moja ya bunduki za kudungulia zenye nguvu zaidi, mdunguaji huyu alikuwa makini sana akiangalia eneo la barabarani ambapo msafara utapita

"They will be there in ten minutes get ready, soon after explosion he will be shifted to another car you have to shoot him on the spot" (watakuwa hapo baada ya dakika kumi kaa tayari, punde baada ya mlipuko atahamishiwa kwenye gari nyingine unatakiwa kumuua mara moja) sauti ilimpa maelekezo kupitia kifaa chake alichovaa sikioni

Msafara wa magari uliwasili eneo hilo na ghafla kombora lililofyatuliwa kutoka kwenye RPG (rocket propeller gun) lilipiga gari iliyokuwa katikati ya msafara na kusababisha mlipuko mkubwa na gari ile ilipaishwa juu ikichakazwa vibaya sana

Taharuki kubwa ilitokea eneo hilo bwana Abd alishindwa kubaki kwenye gari alishuka na kwa haraka walinzi wote kwenye gari zingine walishuka na kumzingira wakikitoa silaha zao na kutafuta upande kombora lilipotokea kwa wakati huo mdunguaji alikuwa amekijaza kifua cha bwana Abd al-Uzza kwenye shabaha 'go to hell' (nenda kuzimu) alijisemea na kisha kubonyeza kifyatulio na risasi moja ilichomoka kumwendea bwana Abd al-Uzza

itaendelea 

Jaba Zulma

Siyumbi

Your Thoughts

Previous Post Next Post

Contact Form