Acetamin 220 (06)



ACETAMIN-220...(06)

MTUNZI:BARAKA GEOFREY

0652089642


TAHADHARI:Majina na matukio yote kwenye simulizi hii ni ya kutungwa tu kwa ajili ya kufikisha ujumbe.


ILIPOISHIA..........

Msafara wa magari uliwasili eneo hilo na ghafla kombora lililofyatuliwa kutoka kwenye RPG (rocket propeller gun) lilipiga gari iliyokuwa katikati ya msafara na kusababisha mlipuko mkubwa na gari ile ilipaishwa juu ikichakazwa vibaya sana

Taharuki kubwa ilitokea eneo hilo bwana Abd alishindwa kubaki kwenye gari alishuka na kwa haraka walinzi wote kwenye gari zingine walishuka na kumzingira wakikitoa silaha zao na kutafuta upande kombora lilipotokea kwa wakati huo mdunguaji alikuwa amekijaza kifua cha bwana Abd al-Uzza kwenye shabaha 'go to hell' (nenda kuzimu) alijisemea na kisha kubonyeza kifyatulio na risasi moja ilichomoka kumwendea bwana Abd al-Uzza

ENDELEA..............

Katika harakati za kutafuta kombora lilipotokea Aaron aliona kitu kikin'gaa juu ya ghorofa mara moja alitambua kuwa ni sniper riffle....kitendo cha haraka alijirusha kwa nguvu kumwelekea bwana Abd al-Uzza na kumdondosha kwa nguvu chini ni wakati ambao mdunguaji yule aliachia risasi hivyo ilimkosa bwana Abd na kumpata mmoja wa walinzi 'shiiit' mdunguaji yule alilaani kwa kuikosa shabaha yake na pia alijua amefahamika alipo

Kwa haraka alitambaa kuelekea upande mwingine wa ghorofa huku risasi nyingi zilimiminika upande wake, baadhi ya walinzi walikimbia kupandisha juu ya ghorofa lile na wengine walimuingiza bwana Abd kwenye gari na kutimka eneo hilo kwa kasi

Mdunguaji yule aliingia ndani ya ghorofa na kuvaa juba kubwa jeusi lilomfunika mpaka usoni alishuka kwa kutumia lift mpaka chini ya ghorofa hilo alipishana njiani na walinzi wa bwana Abd waliokuwa katika haraka ya kupanda juu ya ghorofa kumkamata lakini hawakumtambua, alienda moja kwa moja kwenye gari jeupe humo aliwakuta wenzake mwanaume mmoja aliyeshika RPG na mdada mwingine

"Mission failed" aliwaambia wenzake waliopo humo ndani

"Harry you are a professional sniper how could you miss the target we have failed CIA and the whole nation" (Harry wewe ni mdunguaji mahiri umewezaje kukosa shabaha tumeifelisha CIA na taifa lote kwa ujumla) mwenzake mmoja alimwambia kwa hasira

"I didn't missed the target but someone rescued that bastard" (sikukosa shabaha ila kuna mtu alimuokoa yule mwanaharamu)

Baada ya hapo gari yao iliondoka kwa kasi na kupotea eneo hilo


                        ****************

Gari iliyombeba bwana Abd na gari mbili zilizobeba walinzi waliosalia zilikuwa njiani kuelekea msitu wa Ziarat ilipo kambi ya wanamgambo wa Al qaeda safari haikuahirishwa licha ya shambulio lilotokea..


Majira ya saa 10 jioni bwana Abd al-Uzza alipokelewa kambini na viongozi wa hapo na kisha kuanza kuzungushwa maeneo mbalimbali, maghala ya silaha na vifaa vingine vya kivita, sehemu mbalimbali za mafunzo na kadhalika kisha vijana wote walikusanywa uwanjani kwa ajili ya kukutana na mtu huyo mzito


Alitoa hotuba fupi ya kuwatia hamasa ya kupambana na kisha vijana 50 waliokuwa na uwezo wa hali ya juu waliitwa ili bwana Abd achague wachache kwa shughuli yake maalum

"Kwanza niitie wale vijana walionipokea uwanja wa ndege" alimpa agizo mmoja wa wakuu wa kambi hiyo, na vijana wanne waliletwa mbele yake watatu walikufa kwa mlipuko na mmoja alikuwa amekwenda kumsaka mdunguaji

"Njoo hapa kijana" alimwita Aaron, alimkumbuka kuwa ni yule aliyemuokoa asipigwe risasi

"Unaitwa nani?"

"Ayman al-Zawahiri" alijibu kikamavu, bwana Abd alikaangalia hako katoto na kutabasamu kwani alikuwa na mambo makubwa kuliko umri wake

"Huogopi risasi?" Alimuuliza

"Siogopi"

"Huogopi kufa"

"Tumezaliwa ili tufe na kila mmoja atakufa hivyo siogopi" alijibu Aaron au al-Zahawiri kama alivyoitwa kambini hapo

Bwana Abd alitabasamu na kisha kumgeukia mmoja wa wakuu wa kambi

"Huyu kijana anafaa sana nitaondoka naye" alisema na kisha alichagua wengine wanne wa umri tofauti na waliamriwa waende kujiandaa kwa safari ya kwenda Saudi Arabia na bwana Abd al-Uzza

  

Kikao kizito kilifanyika kati ya bwana Abd al-Uzza na viongozi wa juu wa kambi hiyo kikubwa ilikuwa ni kuwakabidhi kiwango kikubwa cha pesa na pia kupanga mikakati ya jinsi ya kuingiza silaha nzito nchini humo pia bwana Abd alisisitiza mashambulio makali yaendelee dhidi ya serikali ya Marekani

Majira ya saa 1 usiku kikao kiliisha na bwana Abd aliondoka kambini hapo kwa Helikopta

na kwenda kupumzika hotelini Pearl Continental Hotel Peshawar huko hotelini alikuwa na kikao kifupi pamoja na wafanyabiashara wenzake wakubwa wa nchini Pakistan na kisha akapumzika kwa safari ya kesho.


 ********************

SIKU ILIYOFUATA SAA MBILI ASUBUHI

Msafara wa magari kumi ulitoka Pearl Continental Hotel Peshawar

kuelekea Islamabad international airport ulikuwa umembeba bwana Abd al-Uzza pamoja na baadhi ya wapambe wake, ilikuwa ni siku ambayo anarudi kwenye makazi yake Saudi Arabia, saa moja baadae ndege ya shirika la Qatar airways iliyombeba Abd al-Uzza ilikuwa angani kuelekea Saudi Arabia

hakuongozana na vijana kutoka kambini Ziarat kwani alijua anaweza kuhisiwa kujihusisha na mambo ya kigaidi hivyo wao waliondoka na ndege ya saa sita mchana kuelekea Saudi Arabia


SAA RIYADH - SAUDI ARABIA SAA 12 JIONI

Ndege ya shirika la Qatar airways ilitua uwanja wa ndege wa Riyadh na vijana watano kutoka Pakistan walishuka hawakuongozana na kila mmoja alivalia kivyake, pia passport zao ziliwatambulisha kama wenyeji wa Saudi Arabia ambao walikuwa Pakistan kwa shughuli mbalimbali

Kila mmoja alimwona mtu aliyeshika bango lililoandikwa jina lake na alimfuata waliingia kwenye magari tofauti tofauti na kila moja lilishika njia yake kuelekea mahali wasipopajua

 

Gari zile zilizowabeba kina Aaron ziliingia kwa mda tofauti tofauti ndani ya jumba moja kubwa la kifahari lililopo jijini hapo Riyadh na kisha kila mmoja alipokelewa na mhudumu wa nyumba hiyo na kupelekwa moja kwa moja kwenye sebule mojawapo ya jumba hilo

Sebule hiyo ilikiwa ni ya kifahari kweli kweli samani za sebule hiyo zilinakshiwa kwa dhahabu safi na pia kulikuwa na sanamu mbalimbali za dhahabu.....vijana wale walistaajabu kuwa kumbe kuna watu wafaidi maisha kiasi hicho duniani

"Saa mbili usiku mtakuwa na kikao na bosi hivyo kwa sasa mnaweza kupata vinywaji na kupumzika kwa mda" mhudumu huyo aliwaelekeza kwa ukarimu

"Sawa" walijibu kwa pamoja na kisha kila mmoja alipatiwa kinywaji alichohitaji.....sekunde zilisonga kutimiza dakika, na dakika zilikwenda kutimiza lisaa,la kwanza kisha la pili yakatimia na mda wa kikao ulikuwa umewadia

Vijana walielekezwa mpaka kwenye lift na kupanda ghorofa kadhaa kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano

Baada ya mda mfupi bwana Abd al-Uzza aliingia akiambatana na wenzake kadhaa ndani ya chumba hicho, wote walisimama wima kwa heshima kumkaribisha mkuu wao

"Natumaini wote ni wazima" alianza kuongea bwana Abd kwa lugha ya kiarabu ambayo haikuwapa shida vijana wale kwani walijifunza na kuimudu vilivyo wakiwa kambini

"Natumaini sikukosea kuwateua kuwa kati ya vijana bora kabisa mtakaohusika katika shughuli zangu muhimu" aliweka kituo kwa mda


"Macho yenu yanasanifu ushujaa na kiu ya kuitafuta haki na amani ya kweli ulimwenguni na hii haiwezi timia bila kupambana na kutawala, nia yetu ya dhati ya kuitafuta haki haitatimia kwa kuitawala Pakistan tu au Asia tu bali ulimwengu wote, kila kilichonyang'anywa lazima kirejeshwe" aliongea bwana huyo akizisoma sura za vijana hao na kuona wazi kuwa amewaacha njia panda


"Mtaondoka kuelekea kwenye mafunzo zaidi na baada ya hapo mtaelewa vizuri shughuli niliyowaitia lakini kubwa na kuhakikisha udhalimu unatokomezwa duniani kote" alimalizia bwana yule na kuondoka akifuatiwa na wenzake, huku akiwaacha vijana wale katika sintofahamu kubwa wasielewe walichoitiwa, wakiwa katika mshangao huo mwanaume mmoja mwenye asili ya kijapan aliingia na kuwaeleza wamfuate, walinyanyuka na kuanza kumfuata mwanaume huyo waliingia kwenye lift na kushuka mpaka chini ya jumba hilo na hapo waliingia ndani ya gari mbili na kuliacha jumba hilo walienda mwendo wa nusu saa na huko waliingia nyumba nyingine ila ilikuwa ndogo kuliko ile ya kwanza na yenye ulinzi mdogo zaidi pia haikuwa nzuri na ya kifahari kama kule walikotoka, mwanaume yule aliwaongoza mpaka kwenye mlango wa chumba kimoja na kuwaambia warudi nyuma kidogo

"Your identification code please" sauti ya kike iliuliza kutoka kwenye mlango ule

"SHOOTER 008" alisema maneno hayo na mlango ukafunguka aliingia ndani ya chumba kile cha ofisi na vijana wale walimfuata alibonyeza kitufe chekundu kilichopo chini ya meza na meza ilisogea pembeni ngazi zilizoshuka chini zilionekana na walizifuata meza ikirudi mahali pake.....walikuta milango kadhaa na walienda kwenye mlango ulioandikwa 003 aliufungua na mwanamke mmoja mzungu aliyevaa koti la kidaktari alikuwemo ndani

"Nimeshawaleta" alimwambia mwanamke yule

"Sawa wengine wasubiri nje abaki mmoja" alitoa maelekezo na wote walitolewa akabaki Aaron tu

"Lala hapo kitandani" mwanamke yule alitoa maelekezo

"Unataka kufanya nini?" Aaron aliuliza

"I don't want many questions kid" (wewe mtoto sitaki maswali mengi) alimwambia, Aaron aliendelea tu kumtumbulia macho hakuwa tayari kufanya kitu bila kujua makusudi yake

"Kama hutaki toka nje" mwanamke yule alimwambia, Aaron alijishauri kwa dakika chache na kulala kitandani, Mmama yule alivuta dawa fulani kwenye bomba la sindano na kumchoma mkononi na hapo Aaron alianza kuona giza kisha alipoteza fahamu, mwanamke yule alimvua nguo zote na kisha aliwasha vifaa vilivyopo mle ndani na mara mwanga mkali ukaanza kummulika Aaron kisha kompyuta iliyopo pembeni ilianza kuuonyesha mwili vizuri baada ya kumchunguza kwa dakika kadhaa mwanamke yule alitingisha kichwa kuonesha kuridhika na kisha alibonyeza vitufe kadhaa kwenye vifaa vyake na sindano moja ndefu ilichomoka kutoka kwenye moja ya vifaa vyake na ilizama kwenye bega la Aaron kwa sekunde kadhaa na kisha kuchomoka, mama yule alitabasamu kwani zoezi la kumpandikiza kijana yule 'microchip' lilikamilika


Microchip ni chip ndogo sana mithili ya punje ya mchele ambayo hupandikizwa kwa mtu ili kuwezesha aweze kupatikana akiwa mahali popote na pia huwa na taarifa za msingi za mtu huyo...

Aaron alitolewa nje ya chumba hicho akiwa amepoteza fahamu na kisha vijana wengine pia waliitwa na kufanyiwa kitu kilekile kwa zamu


Masaa mawili baadae Aaron alizinduka na kujikuta kitandani ndani ya chumba tofauti na alichokuwa mwanzoni, alijihisi mchovu na maumivu kidogo kwenye bega lake la kushoto akiwa bado anatafakari ni kitu gani kimetokea na wenzake wako wapi mwanaume yule mwenye asili ya kijapan aliingia na kumuamuru amfuate....alimfuata mpaka nje ya nyumba na Aaron aligundua kuwa ilikuwa ni tofauti na ile waliyoletwa mwanzoni alielekezwa mpaka kwenye kiwanja kidogo cha helikopta (helipad) na hapo alipandishwa kwenye helikopta, alitamani sana kuuliza swali ajue anapelekwa wapi lakini aliamua kutulia kimya, helikopta iliwashwa na rubani na ikaanza kuzungusha mapangaboi yake kwa kasi ikitimua vumbi la kutosha eneo lile kisha ikanyanyuka na kuondoka eneo lile mpaka mda huo hakujua wenzake walipo

Helikopta ilipasua anga kwa dakika kadhaa mpaka bandari ya Dammam iliyopo mashariki kabisa mwa mji wa Riyadh kwenye ghuba ya Persia.....bwana mdogo alishushwa na kupandishwa kwenye nyambizi moja ndogo ya kisasa humo aliwakuta vijana wengine kama kumi tofauti kabisa na alitoka nao Pakistan safari ya yule mwanaume mjapan iliishia pale, nyambizi iliyakata maji kwa kasi na kuibuka kwenye pwani ya India jiji la Mumbai...Aaron alisafirishwa mpaka jiji la New Delhi kwa ndege na kisha alipandishwa ndege mpaka jiji la New York Marekani

ITAENDELEA USIKOSE SEHEMU IJAYO

Jaba Zulma

Siyumbi

Your Thoughts

Previous Post Next Post

Contact Form