KISASI CHANGU UTANGULIZI


KISASI CHANGU

UTANGULIZI

Mwandishi:Laurent Elpid (Mzee baba)


Baada ya kufika Dar es salaam nilipokelewa na mwanajeshi mmoja ambaye alikuwa na cheo cha ukomando ambapo kutokana na kazi niliyotakiwa kuifanya hakuja amevaa kijeshi wala hatukusalimiana kijeshi


        Vilevile hatukuelekea jeshini kama nilivyo tarajia bali alini peleka mpaka kwenye hoteli kubwa ya nyota tano ya kifahari na kuniambia nitakaa pale kwa muda nitakao kuwa nikiifanya kazi , kisha akanikabidhi kadi ya benki ikiwa tayari walisha nifungulia akaunti iliyokuwa na fedha za kutosha 


      Kisha akatoa bastola ndogo, vifaa vya kudukua mawasiliano , kamera pamoja na picha ndogo ya passport akimuonesha mzee wa umri wa makamo 


      "Sasa muheshimiwa kuna kazi ume tumwa uifanye " aliniambia komandoo yule..


  Nilimtizama pima nikimsikiliza kwa makini kujua ni kazi gani haswa nilitakiwa kuikamilisha


       "ulichaguliwa peke yako na kupewa nafasi ya kuweza kupata mafunzo nje ya nchi, si kwamba ilitokea tu ukachaguliwa bali ni juhudi ulizoonesha katika kulitumikia jeshi letu, hivyo sasa baada ya kumaliza mafunzo yako jeshi limeamua kukutuma ukafanye upelelezi juu ya huyu mzee


 (alinionesha picha ya mzee yule) 


   Huyu anaitwa bwana Magula lakini amebadilisha jina kwa sasa anajiita Mr. Erickson anatuhumiwa kufanya biashara mbalimbali haramu kama uuzaji wa madawa ya kulevya, inasemekana ana kikosi cha majambazi ambao huwatumia kufanya ujambazi wa kutumia silaha ndani na nje ya nchi pia anafanya biashara haramu ya kuuza viungo vya binadamu kama moyo, figo, na ini katika mahospitali makubwa yaliyo nchi za Marekani , India , Australia na Uingereza ambapo huvipata viungo hivyo kwa kutumia mbinu ya kuwalaghai watu kisha kuwaingiza kwenye mtego ambapo huwafanyia mauaji ya kutisha na kutoa sehemu mbambali za miili yao na kuziuza kwa bei kubwa ughaibuni


       Tunakupa hii kazi kwa kuwa jeshi la polisi limeshindwa kuifanikisha kwani ndani ya jeshi hilo mzee huyu ana watu wake maalumu ambao humptia taarifa  kuhusu mipango yoyote ya jeshi la polisi na amefikia hatua ya kumlaghai mkuu wa jeshi hilo kwa fedha nyingi ambapo mara nyingi humlinda mzee huyo na kumpatia taarifa juu ya chochote jeshi lilicho panga kufanya juu yake, hivyo mpaka ninavyoongea na wewe sasa mzee huyu ameliweka jeshi la polisi kiganjani mwake na hivyo kufanikiwa kumtia mbaroni kwa kutumia jeshi la polisi ni ndoto


   Sasa tuna kutuma wewe utumie mafunzo yote uliyopata huko ughaibuni ufanikishe uchunguzi na kutipatia ushahidi kamili juu ya mtuhumiwa huyu , tunaimani utaifanya kazi kwa weledi na epuka kurubunika na chochote kwani mzee huyu ana mbinu mbalimbali za kumfanya yeyote awe mpambe wake hivyo na kukabidhi vifaa hivi vitakusaidia katika kazi yako, pia kuna hii miwani inauwezo wa kupiga picha na kuchukua video ambapo wewe unatakiwa ui control kwa kutumia macho yako ..


     Nje kuna gari aina ya range rover sport new model ikiwa na uwezo wa kuzuia risasi kupenya na uwezo wa kuhifadhi silaha na utaweza kuweka mafuta kwenye kituo chochote kwa kutumia hii kadi muhimu kujituma kwakona uaminifu wako kwa jeshi letu tukufu na iwapo lolote litakutatiza usisite kutujulisha"alimaliza komandoo yule


      "naahidi kuifanikisha kazi hii kwa uwezo wngu wote ikiwezekana hata kwa kuutoa uhai wangu"


     nilimjibu komandoo yule tukapigiana salute kisha akatoka na kuniacha hotelini lakini hakufika mbali alirudi na kunigongea mlango


   nikamfungulia


     "kuna kitu nilisahau kukueleza kuhusu mahali anapopatika huyu mzee mara kwa mara anaonekaga maeneo ya Sinza kwenye kiwanda chake cha kuzalisha bidhaa za plastiki wewe anza kumfuatilia taratibu "


     Aliondoka mwanajeshi yule mweusi aliyeonekana kujazia mwili kwa mazoezi japo alivaa shati na suruali ya kawaida ambapo isingekuwa rahisi kumtambua 



      Nami niliweka vifaa nilivyo kabidhiwa mahala salama nikapiga hatua kutoka nje na kweli kama nilivyoambiwa nilikuta gari mpya kabisa aina ya range rover nikiwa katika kulishangaa gari lile nilisikia sauti ya kike ikilitaja jina langu na nilipogeuka nilimwona msichana mrembo amekaa kwenye viti vilivyokuwa nje ya hoteli ile amezishika funguo za gari lile lakini nikabaki na viulizo vipi kalijuaje jina langu na ni nani hasa msichana yule

Hakika alikuwa msichana mzuri nilipiga hatua kumfuata alipo.


     " mambo zako mrembo"nilimsalimu

msichana yule


     "pouwa mzima kaka"alinijibu


     "mi nipo salama tu niambie mamy"nilimjibu


     "jamani na wewe si ukae kwanza  mbona unaonekana unaharaka sana"


     "wala hata mambo mengi tu dada yangu"nilimjibu huku nikikaa

  alinitazama usoni kwa muda kidogo kisha akaniambia


      "kilicho niweka hapa na kufanya nikuite ni kuhusu ile gari ambayo nimeagizwa nikukabidhi na kukupa maelekezo ya jinsi ya kulitumia kwani si kama magari ya kawaida uliyozoea kuendesha, hebu twende pale nikakuoneshe jinsi ya kutumia"aliniambia msichana yule lakini nikamwambia asihangaike kwani gari kama lile lisinge nishinda kuendesha nika mdanganya nilisha endesha mara nyingi gari kama hilo lakini ukweli ni kwamba nilifundishwa kipindi niko mafunzoni nchini Iraq na sikutaka kumwambia msichana yule kwani sikujua hasa alikuwa nani

        "Basi sawa kama unajua funguo hizi hapa gari hilo hapo mi nikuache (good luck) "aliniambia msichana yule na kunyanyuka akitaka kuondoka 


    "jamani mbona unaondoka mapema hivyo hata hatuja juana"nilimwambia


       "ahaa!! mbona wewe mi nakufahamu ila wewe ndo hunifahamu kifupi mi naitwa Magret tutaonana siku nyingine" alinijibu msichana yule na kuanza kupiga hatua akiondoka


     aliniacha mdomo wazi hasa kwa tabia yake ya kutotaka kuwa muwazi na nikabaki najiuliza iweje msichana mrembo kama yule ahusike na mambo ya jeshi na iweje aweze kunifahamu mimi wakati siku ile ilikuwa mara ya kwanza kuonana naye , nilibaki na mtazama msichana yule mrembo na mwendo wake wa madaha kila hatua aliopiga akitoka pale tulipokaa


       Nikiwa bado namtazama msichana yule ghafla ndani ya hotel ile liliingia gari leusi la kifahari aina ya hammer lililo kuwa na vioo vyeusi yaani tinted, lilisimama wakashuka kutoka siti ya nyuma  jamaa watatu waliovaa nguo nyeusi zilizo wabana na kuonyesha miili yao iliyo jaa vizuri mmoja wao alikuwa mzungu wawili walikuwa weusi


     yule mzungu akazunguka upande wa pili na kwenda kufungua mlango wa gari ile ambapo alishuka mzee wa umri wa makamo mnene kiasi na aliyenyoa upara kichwani ambapo baada ya kumuona nilimfananisha na mtu fulani ambaye nilikumbuka alikuwa bwana Magula au Mr. Erickson kama alivyojiita nilistuka nikajiweka tayari kuona kitakachoendelea



***

TANGAZO TANGAZO TANGAZO 

MNAOFUTALIA MALAIKA MWEUSI NAWAPA POLE KWANI HADITHI HIYO HAITOISHA HAPA KWA BLOG WALA KULE FACABOOK KISA MAANA LIKE NI KIDOGO SANA KULINGANISHA NA WANAO SOMA. KAMA KAZI NI MBOVU RUHSA KUMKOSOA MWANDISHI HIVYO NDIVYO WATU HUJENGANA KAMA UNAITAKA WASILIANA NA MTUNZI ALLY MBETU AU SIO. TUENDELEE NA KISASI CHANGU

**

   

   Lakini kilichonishangaza wakati gari lile linafika pale msichana Magret aliendelea kutembea lakini baada ya watu wale kuanza kushuka kutoka kwenye gari ile niliona Magret akionesha kustuka na kubadili uelekeo na sasa alitembea haraka sana na kwa uangalifu bila hata kutazama pembeni 


****

UKISHASOMA LIKE COMMENT PIA SHARE IFIKIE WENGI ZAIDI. SUPPORT IKIWA NDOGO YAANI WASOMAO WENGI HARAFU WANAO LIKE NA KUCOMMENT NI KIDOGO BASI SIMULIZI HII HAITAMALIZWA HAPA.

****



      Mmoja wa wale walinzi wa Mr. Erickson alimuona Magret na kuwashitua wenzake akiwa onesha alipo Magret..


     Mr. Erickson naye aliliona tukio lile na kumuamuru mmoja wa wale walinzi wake amlete haraka mahali pale  msichana yule . Mr Erickson na walinzi wake wawili waliingia ndani ya hoteli ile nami nika jipanga kuwa fuata lakini


     Nilimuona yule mlinzi mweusi mrefu sana naaliye jazia vizuri akitoka na kupiga hatua za haraka akimfuata msichana aliye jitambulisha kwangu kwa jina la Magret


     Sasa nikaanza kujishauri nimfuatile Mr. Erickson au nimfuatilie msichana Magret ambaye ilionekan alikuwa hatarini..


    Mwishowe niliamua nimfuatilie mlinzi aliye tumwa amkamate Magret na kumpeleka nikiamini Mr . Erickson hatoweza kuondoka pale hotelini mpaka atakapo rejea mlinzi wake hivyo itanipa nafasi ya kurudi na kufuatilia  kilicho waleta katika hoteli ile

     

     Nilitoka taratibu nikimfuata mlinzi yule nikijificha ili ikitokea akageuka nyuma  asiweze kuniona, wakati huo msichana Magret aligeuka na kuona mtu anamfuata lakini alifanya kitu kilicho niacha mdomo wazi si mimi tu bali hata mlinzi aliyekuwa ana mfuatilia...

ITAENDELEA...


NI FUPI SANA AISEE!

HAYA BASI IFANYENI NDEFU KWA KULIKE NA KUCOMMENT.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.