KISASI CHANGU
EPISODE 2
Mwandish:Laurent Elpid
..ilipoishia............EPISODE 1
Nilipofika getini mara ilikuja gari nyingine ya bei mbaya huku akishuka mzee wa kihindi naye pia alikuwa na walinzi wake kama ilivyo kuwa kwa Mr. Erickson waliingia ndani ya hoteli ile ilibidi nigeuze na kuanza kuwafuatilia kwa nyuma bila wao kujua ambapo walienda moja kwa moja mpaka kwenye chumba walichokuwa Mr.Erickson na watu wake lakini wakati na mimi nikiwafuatilia kiujanja alitokea yile dada muhudumu nyuma yangu na kunigusa begani, nilipogeuka nilipokea ngumi nzito iliyo nipeleka chini ,nikaanza kuona giza machoni hatimaye sikuweza kujua kilicho endelea tena.....
endelea................
"Pwaaaa!!!!!" ni sauti ya maji baridi niliyo mwagiwa yaliyo nitoa katika usingizi mzito wa kifo , nikajikuta ndani ya chumba kidogo chenye mwanga hafifu nikiwa nime lala chini huku nimefungwa na kamba ngumu na iliyo kazwa vizuri katika mikono na miguu yangu, niliangaza macho yangu pande zote za chumba kile sikuweza kutambua sehemu ulipo mlango katika chumba kile , mara nikasikia sauti nzito ikizungumza nami ambapo niligundua inatokea juu ya chumba kile baada ya kutazama na kuona mlango mdogo mfano wa boksi
"Nina taka kujua wewe ni nani na kwanini ulikuwa unatu fuatilia"ilisema sauti ile wakati huo nami nikaanza kujigeuza vizuri ili niweze kumuona mzungumza lakini kadiri nilivyo zidi kuji vuta ndivyo kamba zile zilivyo zidi kunibana kwa nguvu...
"wala usijaribu kuji nasua katika kamba hizo maana utakavyo endelea utaji sababishia maumivu makali na majeraha"aliniambia mtu yule
"sikuwa nikiwa fuatilia nyinyi jamani nilikuwa na mambo yangu binafsi" nilimwambia
"kwahiyo sisi wajinga mpaka tukukamate wewe na sio wengine nataka uniambie ulikuwa unafanya nini la sivyo utafia huku , laiti ungejua hapa bado hata hujaonja hata lepe la mateso , ungeni eleza mapema nia yako ni ipi na nani alikutuma "aliniambia mwanaume yule, ambapo nilijitahidi kugeuza shingo japo kwa shida nikagundua ni yule mlinzi aliye kuwa akimfuatilia Magret
"hapana ndugu yangu nilikuja pale hotelini kama mteja tu sija wafuatilia nyinyi, yule msichana wa hoteli nilipo mwona nilivutiwa naye nikamwomba namba za simu akanikatalia nikaachana naye sasa kuna kitu nili sahau wakati narudi ndio nikakutana naye akanipiga na kitu kizito kichwani ndio mpaka nilipo jikuta ndani ya chumba hichi, naomba uniamini tu ndugu yangu nitoke hapa sijui chochote kuhusu hili jambo unalo nieleza"nilimwambia njemba yule kwa sauti ya huruma na msisitizo nikijipa matumaini ana weza japo kuni fungua kamba nilozo fungwa nisubiri hitimisho kutoka kwa wenzake
" wewe nahisi hujipendi wewe" aliniambia milinzi yule kisha akabonyeza kitufe fulani alicho kuwa nacho mkononi , nili pigwa shoti ya ajabu na zile kamba za nyaya walizo kuwa wame nifunga nazo , mlinzi yule aliondoka na kuniacha nikiendelea ku ugulia mtetemo wa shoti ile nili tetemeshwa na umeme ule mpaka pale nilipo hisi mapigo ya moyo yame simama hivyo fahamu zili nipotea sikujua kilicho endelea...
Nilikuja kustuka nahisi ulikuwa wakati wa usiku na kujikuta nimekalishwa kwenye kiti katika chumba kingine tofauti na kile huku mikono na miguu yangu vime fugwa na kamba iliyo fangiwa pia kwenye kiti kile , sikuwa na nguo yeyote zaidi ya bukta , ambapo baada ya uwezo wa kuhisi kunirejea vizuri nilianza kuhisi maumivu makali mwili mzima nikajishika nikakutana na majeraha makubwa ya kuchanwa chanwa yakiwa yamekaukiwa damu huku katika mikono na miguu yangu nilipo fungiwa nyaya zile kulikuwa na majeraha makubwa ya kuungua kwa moto yaliyoonesha ngozi nyeupe ya ndani , hakika mwili ulichoka sana huku kiu na njaa vikini andama .....
Nikiwa nime jiinamia kichwa chini kwa kukata tamaa ya maisha mara mlango wa chuma wa chumba kile ulifunguliwa kisha ikawashwa taa yenye mwanga mkali ulio yaumiza macho yangu na kunifanya nione ndani ya chumba kile kulivyo tisha kwa kutapakaa damu iliyo kauka sakafuni huku kukiwa na makabati mbalimbali ya wazi yaliyo jaa vifaa kama nyundo , visu na mikasi ya aina mbalimbali migeledi ya chuma , shoka na vifaa mbalimbali vina vyotumiwa kama silaha za mkononi wakati wa vita...
Mara nikamuona jamaa mmoja kijeba mfupi mwenye sura mbaya na aliye jazia nayeye pia alivaa mavazi meusi akipiga hatua kunifuata huku mkononi ameshika kisu kidogo akitabasamu , aliponifikia alianza kuongea lugha ambayo niliitambua ni kireno akiniambia
" dogo wacha kujitia mjanja we kubali tu kosa na utuambie aliye kutuma, yani hapa bado kabisa sasa ndio nataka tuanze kukupa mateso ukiwa na fahamu ili uyasikie vizuri"aliongea jamaa yule huku akichomoa bangi yake mfukoni na kuanza kuvuta
Muda wote huo sikuweza kuongea chochote zaidi ya kuina misha kichwa changu chini niki wa radhi anifanye chochote maana kama ni matumaini ya kuishi sikuwa nayo..
Baada ya kumaliza kuvuta msokoto wake alinishika kichwa changu huku akitabasamu kwa dharau akiendelea kuniambia kwa kireno kubali tu maana huko tunapo elekea si pazuri hata kidogo , sijui kama utatoka mzima..
Alishika kisu kila na kuanza kuichanja ngozi yangu kama ana menya maganda ambapo alibandua sehemu ya ngozi yangu na kuitupa chini huku damu ikitirika nikilalama kwa maumivu bila ya njemba yule kunionea huruma
Mchezo ule uliendelea mpaka ikafika hatua akawa ameibandua ngozi yote shingoni kwahiyo shingo ilibaki inavuja damu kukionekana ngozi nyeupe ya ndani wakati huo nilihisi maumivu makali yaliyo pitiliza
Jamaa yule akatoa tena kipande kingine cha msokoto na kuanza kuuvuta huku moshi wake akinipulizia usoni , akaendelea kuvuta msokoto ule ambapo sasa aliuvutia pale mdomoni bila kuushika na mkono hivyo akapata nafasi ya kuendelea kunipa mateso
Alafu akatoa ungaunga fulani hivi wa kijani uliokuwa kwenye mfuko maalumu akifungua kwa uangalifu kisha akavaa gloves akachota unga unga ule na kuanza kunipaka shingoni sehemu alizo toa ngozi yangu
Sinto sahau maumivu niliyo hisi siku ile nilipiga ukelele wa nguvu wa maumivu makali ambapo jamaa yaule aliendelea kunipaka akihakikisha ana paka sehemu zote , kwa kweli unga ule sijui ilikuwa kemikali gani maana nilihisi kama nime mwagiwa mafuta ya moto shingoni ,pia nikihisi kama kuna kitu kilikuwa kikini chana chana ngozi yangu
Kwa maumivu niliyo pata nilishindwa kujizuia nikajikuta naachia haja kubwa na ndogo kwenye kiti kile ambapo jamaa yule alianza kunicheka kwa dharau huku sasa akiiwasha simu yake na kuweka live video ambapo sasa nikamuona Mr. Harrison akicheka naye kwa dharau huku akiniambia
"wewe si mjanja sasa ngoja nione ujanja wako utaishia wapi, tuambie nani alikutuma la sivyo tutakubadilishia adhabu ambayo itakuwa mara mia moja ya hii "
Sikuwa hata na uwezo wa kumjibu , nilibaki nikiitazama simu ile machozi yakinitoka tu maana hata nguvu za kulia zilishaniisha hakika maumivu yale yalikuwa makali sana
jamaa aliendelea kunipaka unga unga ule na sasa akianza kuyachubua baadhi ya majeraha niliyo kuwa nayo yaliyo anza kukauka kwa kutumia kisu chake kisha akapaka tena unga ule
maumivu niliyosikia yalinifanya nipige ukelele wa nguvu uliozi poteza fahamu zangu......
Mambo kweli magumu ...nitapona kweli.
Baada ya muda mrefu kupita nilikuja kuzinduka nikajikuta nipo ndani ya chumba cha kisasa chenye hewa safi huku nime zungukwa na kundi la watu ambao baada ya kuwa tazama vizuri nilimuona Mr.Erickson akiwa na walinzi wake wamekaa wakiwa bize kuvuta bangi ambapo baada ya mmoja wa wale walinzi kuona nime rudiwa na fahamu aliwa onyesha wenzake nilipo ambapo Mr Erickson alikuwa wa kwanza kuamka na kunifuata nilipo .
Wakati wote huo nilikuwa katika hali ile ile ya maumivu kama ilivyo kuwa kabla ya kupoteza fahamu, hivyo kusababisha sakafu ya chumba kile kuenea michirizi na matone ya damu lakini siku isikia harufu ya haja kubwa na ndogo ambayo ili nitoka baada ya kupata maumivu yaliyo pitiliza
Alipo nifikia alinishika kidevu changu na kunyanyua kichwa changu na kuni tazama kwa dharau huku akiendelea kuburudika na moshi wa bidhaa haramu ya bangi
"kwa nini upate mateso yote haya wakati kazi ni rahisi tu, kumtaja aliye kutuma"aliniambia Mr. Harison
Niilibaki nime mtumbulia macho yangu yaliyo vimba huku nikiugulia maumivu makali baada ya kuinyanyua shingo yangu na kutonesha madonda ambayo yalianza kupungua maumivu..
" Hutaki kujibu siyo , Fujo hebu toa taarifa walete maji glasi mlja anywe huyu mpuuzi apate nguvu ya kutu eleza kinaga ubaga" alisema Mr. harison
Kidogo mlango wa chumba kile cha kisasa kilicho wekewa mawasiliano ya internet ulifunguliwa akaingia msichana aliye kuwa na asili ya kisomali aka mkabidhi mlinzi niliye sikia akiitwa kwa jina la fujo ambaye alichuku glasi ile ya maji na kuiweka pembeni ya kiti nili kuwa nime kalia
"chukua unywe" aliniambia
Kwa kuwa wakati ule hawakuwa wamenifunga tena niliji kaza kuchukua glasi ile lakini mikono haikuwa na nguvu ili baki kuteteka kutokana na maumivu ya majeraha makubwa nilio kuwa nayo..
Mr. Harrison akaniambia nichukue hayo maji na iwapo nikishidwa hawana budi kuyarudisha , nilijaribu wakati huo nikiwa kama mchekeshaji katika kundi lile la magaidi wakini cheka kwa dharau na dhihaka, lakini haikuwa hivyo kwa msichana yule wa kisomali ,alinitazama kwa huruma jinsi nilivyo hangaika kuya chukua maji yale na alionekana kuto kubaliana na kitendo walicho nifanyia wenzie na kwa kweli kama siyo njaa na kiu kali niliyokuwa nayo nisinge jisumbua na maji yale yaliyo nifanya nionekane kama taira miongoni mwa wana haramu wale..
Baada ya kun'gan'gana kwa muda mrefu na kushindwa niliona bora niachane na maji hayo kwani nilizidi kujiongezea maumivu na kudhalilika mbele ya waalifu wale .
Lakini aliamua kuongea msichana yule akiwaambia sio vizuri walivyo nifanyia kama ni mateso walisha nitesa vya kutosha na walicho hitaji kwa wakati ule ni kumjua aliye nituma hivyo hakukuwa na faida yeyote kuni fanyisha jambo kama lile ambalo yeye alilitafsri kama la kijinga ..
Alinyanyuka Mr. Harrison kwa hasira na kusema
" Sabra naona siku hizi ume kuwa unafikia hatua ya kuni nyanyulia mdomo baba yako tena una bahati sana usinge kuwa damu yangu ninge kufanya kitu mbaya , haya nenda kamnyweshe sasa"alisema Mr. harrison ambapo alinifanya nigundue msichana yule aliitwa Sabra na alikuwa binti yake
Msichana yule ali chukua glasi ile akanipa pole na kuanza kuninywesha maji yale taratibu huku akini tazama kwa huruma , nilikunywa maji yale kwa shida sana kidogo mwili ulipata nguvu japo maumivu yaliendelea kuniandama wakati huo Mr. Erickson na walinzi wake walikuwa bize wakitumia kompyuta moja ambapo nahisi kuna kitu walikuwa wana elekezana
Msichana yule aligeuka na kuwa tazama na kuona hawa waki tuangalia akanipa kifaa fulani kidogo mkononi na kuniambia nikifiche kisi onekane na yeyote , kupitia kifaa hicho atanipa maelekezo ambayo nitatakiwa kuyafuata kama ili kutoka katika ngome ile..
Alimaliza na kutoka ndani ya chumba kile kuniacha pale wakati huo Mr. Harrison walisha maliza walicho kuwa wakikifanya
"haya tuambie sasa nani alikutuma"aliniambia
"mzee sija tumwa na yeyote na wala sijui chochote kinacho endelea , kama mme panga kuniuwa bora mniuwe tu kuliko kunitesa kiasi hiki" nilimjibu kwa jazba kidogo
Alini fuata kwa hasira na kuni piga teke kali la shingoni kulipo kuwa na majeraha ya kupakwa kemikali , nilianguka chini huku niki lalama maumivu ambapo mzee yule aliondoka kwa hasira na kuwaambia vijana wake amepo teza mda wake kwenye kwa mpuuzi kama mimi na akaagiza wanipige wawe zavyo ikiwezekana waniuwe kabisa maana nina waletea kiburi na nime shajua baadhi ya siri zao..
Walinzi wale nao kwa hasira walinifuata na kuanza kuni piga mateke ya nguvu pale chini huku wakini kanyaga tumboni na viatu vyao vikubwa vya kijeshi nililia kwa uchungu niki jiwazia laiti nisinge kuwa na majeraha yale wangekiona cha mtema kuni waliendelea kuni piga mateke mazito pale chini yaliyozidi kunisogeza mpaka nilipo fika katika ukuta wa chumba kile ikiwa bado wana nivurumishia mateke yasiyo hesabika
Katika eneo walilo nifikisha kwa mateke yao mazito kulikuwa na kabati ambayo kwa chini ili kuwa na uwazi , mungu si athumani nilipo tazama vizuri chini ya kabati lile niliona bastola ndogo na kwa kutumia mafunzo niliyo pata ughaibuni niliweza kutambua ilikuwa ime kokiwa vizuri hivyo kadiri walivyo nipiga ndivyo nilivyo zidi kusogea ukutani huku nime unyoosha mkono wangu bila ya wao kutambua dhamira yangu nili vumilia maumivu ya kipigo kile pamoja na majeraha niliyo kuwa nayo nikanyoosha mkono wangu na kukusanya nguvu maana mwili ulinilegea japo nilikunywa maji kidogo waliyo nipa lakini njaa na kipigo cha muda mrefu vilinifanya nikose nguvu za kutosha
Hatimaye mkono uliweza kuishika bastola ile nikajitahidi kuingiza kidole changu katika kiwambo cha bastola ile nika fanikiwa wakati huo walinzi wale watatu waliojazia miili yao waliendelea kuni surubu bila huruma niliutoa mkono wangu uliokuwa umeshikilia bastola chini ya kabati lile haraka na kuanza kuwa fyatulia risasi mfululizo walinzi wale ambao nao kwa taharuki walianza kukimbia hovyo ndani ya chumba kile hivyo nika pata nafasi ya kuwa lenga vizuri maana walijitenga sijui nguvu zile nilizitoa wapi kwa kweli, nilianza na yule mzungu nika mpiga risasi ya kichwa iliyo ingia jichoni ambapo alianguka na kufia pale pale , wale weusi wote niliwa piga mfululizo risasi za tumboni na kifuani nao pia walianguka chini na kupoteza maisha milio ile ya risasi ili sikika na kuonekana sehemu mbalimbali katika ngome kwa ktumia ka
mera zilizo egeshwa ndani ya chumba kila ..
Kundi la walinzi walikoki silaha zao nakuja mbio katika chumba kulipo sikika shambalio la risasi ....
ITAENDELEA
Your Thoughts