MALAIKA MWEUSI EPISODE 5

Emmanuel Lee
By -
0

 HADITHI: MALAIKA MWEUSI

MTUNZI: Ally Mbetu ‘DrAmbe’

SIMU: 0713 646500.


EPISODE 5


ILIPOISHIA: episode 4

Nilimshika na kumgeuza ambapo alipiga kelele kutokana na maumivu. Maskini mama yangu aliteseka..sijui wanadamu wengine kwa nini Mungu aliwaumba katika hali ya ubinadamu kwa nini asiwaumbe wanyama nilimchukia sana baba sijui nimfananishe na kitu gani,” Malaika alisema kwa uchungu mkubwa japo jambo lile lilitokea muda mrefu. 

SASA ENDELEA...


Aliendelea kuhadithi kisa kilichokuwa sawa na kuchubua ndonda lilipona. Baada kumgeuza huku moyo wangu ukiwa katika maumivu makali  nilimpa moyo mama yangu.

 ''Ooh pole sana mama yangu taratibu.” 

Nilimgeuza mama alilalia mgongo kisha akaniita tena 

“Mwanangu Tereza.”

  ''Abee mama'' 

“Kila nikikuangalia moyo wangu unaniuma.''

''Una maana gani mama?’

“ Mwanangu najua utapata shida utaishi maisha ya tabu hata ile dhamira yako siamini kama itatimia''

“ Mama...mbona leo sikuelewi, una maanisha nini?”

''Ni vigumu kunielewa kwa vile bado mdogo akili yako ni changa ndiyo maana nakuonea huruma” 

“ Unanionea huruma kwa lipi?”

  “Mwanangu nakuacha kama kinda la ndege ambalo mama yake amekufa kutokana na mvua kubwa yenye upepo mkali iliyozoa kiota chake na kuua wazazi wote na kubaki kinda lisilojua lolote.”

“ Mama unataka kwenda wapi kama mateso ya baba yamekushinda basi tuondoke wote sitakubali kubaki kuendelea kupigwa na baba. “

Kauli yangu  ilimfanya mama acheke kicheko ambacho sikukielewa kilikuwa ni kicheko cha mtu aliye jikatia tamaa ya kuendelea kuishi.

''Tereza mwanangu.''

''Abee mama.” 

  “Leo nataka kukupa siri moja sipendi kufa nayo moyoni nina imani Mungu atanihukumu.”

''Siri gani mama yangu?”

Mama aliushika mkono wangu na kuunyanyua kisha alianza kunisimulia.

“Miaka 15 iliyopita mimi mama yako nilikuwa mtawa kwenye kanisa kuu mjini nimekuwa pale kwa zaidi ya miaka mitano nikimtumikia Mungu.

Siku moja niliporudi nyumbani kumjulia hali bibi yako ambaye ni mama yangu, kwa kuwa vijijini kuna shida ya maji niliamua kufuata maji kisimani. Kisima hikihiki tulichokitumia miaka ya nyuma kabla ya kujengwa baadhi ya nyumba kulikuwa na pori.

Wakati natoka kisimani kuchota maji ile navuka tu lile pori walitokea wanaume watatu ambao ni vijana wa pale kijijini ambao nilikuwa nimesoma nao na kucheza nao lakini siku hiyo walikuwa na roho ya kishetani  kwa kunivamia na kunivuta kichakani ambapo walinibaka kwa zamu.”

“Aah! Mamaa!” Nilishtuka sana kusikia habari ile japo moyo uliniuma nilitulia nijue mwisho wake.

“Kitendo kile kwa kweli kilinidhalilisha sana na kunitia dosari katika maisha yangu ya utawa lakini sikutaka kumweleza mtu na wale wote walionitendea kitendo kile niliwasamehe, kwani sisi tumefundishwa kusamehe saba mara sabini kwa kuwa walionibaka hawakujua walitendalo.

“Nilirudi hadi nyumbani nikiwa na siri yangu moyoni niliogopa kumwambia mtu kwani niliona aibu. Baada ya kumaliza mapumziko yangu nilirudi Parokiani kuendelea na huduma na siri yangu moyoni.  Siku zilibadilika na hali yangu ya kimaumbile nayo ilibadilika ilibidi nipelekwe hospitali ambapo nilipopimwa niligundulika ni mjamzito.

“Hapakuwa na jinsi, kanisa ilibidi linitenge na kuondolewa baada ya kuonekana nilivunja masharti kufanya ngono nje ya utaratibu za utawa. Nirudi tena kijijini kuanza maisha mapya, hiyo mimba ndio uliyozaliwa wewe,”  habari hizi zilinishitua sana na kujua kumbe sina baba ujauzito wangu uliingia baada ya mama yangu kubakwa.

“Waliokubaka kwani bado wapo hapa kijijini?” nilimuuliza mama.

'"'Eehe wapo mbona huwa naongea nao walishakuja kuniomba msamaha nami niliwasamehe.”

  “Aah! Mama hao si watu wa kuwasamehe ningekuwa na uwezo ningewaulia mbali,” nilisema kwa hasira japo nilikuwa binti mdogo.

”Aah, mwanangu jifunze kusamehe ili hata bwana Mungu naye akusamehe usipende kulipiza kisasi.”

“'Ni ngumu, ni akina nani hao?”

Mama alinitajia kwa majina, kumbe ni watu ambao nilikuwa nawaheshimu sana  kumbe ni mashetani ipo siku yao,” nilijikuta nikisema kwa hasira.

“Mama kwa nini mungu aliumba wanaume si bora angeumba dunia na jinsia moja. Mama wanaume wote angewageuza wanyama kama nyati, kiboko na hata fisi.”  ''Hapana sio wote wanaume wana roho mbaya wapo wenye roho nzuri na pia wapo wanawake wenye roho mbaya kuliko hata wanaume.”

''Hapana...hapana...hakuna mwanaume mwenye roho nzuri yaani mama naapa sitawapenda wanaume mpaka nimeingia makaburini nina imani ni kundi la mashetani yaliyohasi ingekuwa amri yangu ingekuwa dunia ya jinsia moja...na huyo shetani mwingine alikujuaje?”

“Mwanangu lekebishe kauli yako, baba yako usimwite shetani,” mama alinionya.

“Tena mkubwa wa mashetani binadamu gani asiyekuwa na huruma ndio maana nilikuwa najiuliza muda mrefu baba gani asiyekuwa na mapenzi ya familia yake?”

''Yule baba yako tulikutana nae hapahapa kijijini kwa kweli katika siku za mwanzo alikuwa ni mtu mzuri sana, lakini kumbe upole wake ulikuwa wa kuniteka kimawazo kumbe ni chui aliyevaa ngozi ya kondoo...alianza kubadilika na  kunipiga hasa baada ya bibi yako kufariki, ulevi ukawa ndio sehemu ya maisha yake.”

“Alizidi kubadilika na kunipiga,  yeye ndio aliyenitia ubovu huu wa mwili kwa kipigo hata meno yeye ndiye aliyeningoa kutokana na kipigo.”

“Sasa mama bado mtu huyo unamtetea labda sio mimi nitakapokua mkubwa nimkute amekufa la sivyo lazima nitalipa kisasi,” nilisema kwa uchungu.

“'Hapana mwanangu usifanye hivyo, la muhimu ni kuomba kwa Mungu usome kwa bidii kwani huo ndio mtaji wako utaokutoa kwenye dimbwi la umaskini.”

“Mama ninakuahidi nitasoma kwa bidii ili siku moja niwe hakimu au polisi ili niwashikishe adabu wote wenye tabia ya kuwanyanyasa wanawake'.”

“Mungu atasikia maombi yako lakini chonde usilipe kisasi,” mama alizidi kunionya,  alitulia kidogo kisha alianza kuhema kama mwenye pumu, kitu kilichonitisha.”  ''Tereza...mwanangu nipe...maji,” mama alisema kwa shida, nilimletea maji wakati huo  alikuwa akiongea kwa sauti iliyoanza kufifia.

''Maskini mwanangu...Mungu nilindie mwanangu,” hakuendelea tena alinyamaza kimya,nilimuita:

 ''Mama...mama.” hakunijibu zaidi ya kunitazama, alitabasamu lakini tabasamu lake liliishia kati alitulia tuli, nilimuita lakini hakunijibu.

Ile hali ilinitisha ilinibidi nitoke nje niombe msaada wa majirani, nilishangaa wakati natoka nje baada ya muda ndipo nilipotambua mama yangu alikuwa amekufa. Siku hiyo nililia sana hadi nikapoteza fahamu. Sio siri mama yangu nilikuwa nampenda sana lilikuwa pigo zito maishani mwangu.

Baada ya mazishi ya mama niliendelea kukaa na baba ambaye nilifahamu kuwa si baba yangu mzazi ila ni wakufikia, nilikuwa sina jinsi lakini ukweli nilimchukia sijui nimfananishe na kitu gani. Si yeye tu hata wanaume wote duniani niliwachukia sana licha ya mama kunikataza  nisilipe kisasi.  Kisasi changu ni kusoma kwa bidii ili siku moja niwe askari wa cheo cha juu  au hakimu ambaye nitawashikisha adabu wote wanaonyanyasa wanawake.

Baada ya msiba wa mama kidogo nyumbani alirudi katika hali ya utulivu, niliendelea kusoma kwa bidii na darasani nilifanya vizuri mtihani wangu wa darasa la tano. Nikiwa darasa la tano mwaka mmoja baada ya kifo cha mama alikuja mama mmoja hivi.

Nilimsikia baba yangu akisema:

“Tena huyo ndio anarudi,” nilipofika niliwasalimia na kisha kuingia ndani, nikiwa nabadili nguo baba aliniita.

"Thereza."

”Abee baba, nabadili nguo."

"Fanya haraka kidogo.”

Baada ya kubadili nguo nilitoka nje.

"Abee baba."

"Thereza mwangu huyu mama hapa anataka akuchukue akupeleke mjini.”

“Na shule baba?”

“Aah! Utasomea huko huko.”

Nilishindwa kukataa hata nguo za kubadili sikubeba niliingia ndani ya gari na kuletwa jijini kwa mara ya kwanza. Mawazo yangu nilijua nakuja kusoma kumbe kufanywa mfanyakazi wa ndani nilipomuuliza mama alinijibu kuhusu kusoma jibu alilonipa ndio lilinimaliza kabisa ndoto yangu ya kuwa afisa wa jeshi au hakimu ilizimika.

Alijibu kuwa yule baba wangu wa kambo amemuuzia kwani alipofika pale kijijni kutafuta mtumishi wa ndani alinitoa mimi, roho iliniuma nilipojua nimeuzwa kama mbuzi.

 Kuanzi hapo nikawa mtumishi wa ndani ya nyumba hiyo kwa kweli nilifanyishwa kazi kama mbwa sikuwa na mapumziko. Kitu kilichonifanya nimshangae mama huyu ambaye hakuonyesha hata huruma kwanza umri wangu haukuwa wa kufanya kazi pili kazi zilikuwa nzito ambazo zilinizidi uwezo.

 Miaka miwili ilikatika nami nikazoea kazi za sulubu siku moja nilivamiwa chumbani kwangu na baba ambaye alinibaka na kunitishia endapo nitasema nitajuta kuzaliwa. Japo aliniumiza ilibidi niwe mpole sikumweleza mtu nilikumbuka yale yote ambayo yalimtokea mama yangu. 

Roho iliniuma nilimkumbuka mama yangu siku hiyo nililia sana kitu kilichomshtua mama mwenye nyumba. Usiku wa siku iliyofuata ilikuwa kama wameambizana mtoto wa mwenye nyumba naye alinibaka, Mchezo ule ukawa wa kila siku kunibaka. Mwisho hali ile niliizoea nikawa sigomi tena akifika baba sawa au  mtoto wa mwenye nyumba  walinikuta tayari nawasubiri.

 Nafikiri  walikuwa hawajuani siku zote penzi halina siri siku moja tulifumaniwa na mama mwenye nyumba mbona siku hiyo ilikuwa kasheshe. Pamoja na kujitetea kuwa nililazimishwa lakini hawakunielewa siku hiyo alichonifanya mama yule nina imani akitanitoka akilini mwangu.

Alinifunga kwa kamba na kunichoma katika mapaja yangu kwa pasi na kunipaka pili pili sehemu za siri kisha kunipa kipigo cha mbwa. 

                                                     ******

Baada ya mateso makali nilifukuzwa pale nyumbani tena ukiwa ni usiku huku mvua   kubwa ikinyesha. Yaani ulikuwa ukatili wa hali ya juu, kubakwa nibakwe  niteswe na kipigo juu.

 Nililala kwenye jumba moja bovu hadi asubuhi ambapo niliokotwa na wasamali wema na kupelekwa hospital ambapo sehemu zangu za siri zilikuwa hazitamaniki, mapaja na ngozi yote ilikuwa imebanduka. Kabla ya matibabu kwanza nilipelekwa kituo cha polisi na kupewa PF3 ndipo nilipopata matibabu.

Nilimshukuru Mungu nilipata msamalia mwema mmoja ambaye alisema atanisimamia kuhakikisha wahusika wote wanatiwa hatihani. Katika muda wote niliokuwa pale hospitali alinihudumia kama mdogo wake na baada ya kupata nafuu alinichukua hadi nyumbani kwake.

Kisha aliifungulia mashtaka ile familia kwa unyanyasaji wa kijinsia na ubakaiji. Siku moja wakati anarudi nyumbani yule dada ambaye kitaaluma alikuwa mwanasheria wa kujitegemea alinieleza kuwa ameamua kujitoa katika kesi yangu kwa kuhofia usalama wa maisha yake.

Alinipa nauli ili  nirudi nyumbani kwetu iringa katika wilaya ya Makete kwani kama ningeendelea kukaa pale basi maisha yake yangekuwa hatarini. Kutokana na vitisho ilibidi niondoke siku ileile usiku na kulala kwenye nyumba ya wageni karibu na stendi ya mabasi Ubungo. 

Kama kawaida asubuhi nilidamkia kituo cha basi, lakini mwaka wa mkosi ni mkosi tu nikiwa nataka kukata tiketi nilipogundua pesa yangu ya nauli ilikuwa nimeibiwa. Niliangua kilio pale kituo cha basi lakini hakuna mtu hata mtu  mmoja aliyenijali.

 Wapo walionisaidia pesa ya chakula tu na hata jioni ilipoingia ilibidi nilale palepale kituoni hadi asubuhi. Nilijifikiria sana nirudi tena kwa yule dada ili nimweleze masahibu yaliyonikuta, lakini aliyonieleza jana yake yaliniogopesha kuhofia usalama wa maisha yake.

Niliamua kuingia mjini na kuomba msaada kwa wasamalia wema, siku hiyo  Mungu aliniangazia kwani mpaka jioni nilikuwa nimepata laki moja na arobaini elfu. Hapo tamaa ikanipata nikaona nisifanye haraka kuondoka niendelee kuombaomba hata nikirudi nyumbani niwe na pesa nyingi za kufungulia miradi ya kujiendeleza kimaisha.

Jioni ile nilipanga chumba cha gesti moja ya uswahilini na kulipokucha nikaendelea kuchangisha mchango wa hiyari. Siku hiyo mambo hayakuwa mazuri sana nilipata elfu sitini. Kama kawaida yangu jioni nilirudi kwenye chumba changu na kulala hadi asubuhi.

Kulipo pambazuka kama kawaida yangu kiguu na njia, nakumbuka siku moja nilikutana na mtu mmoja ambaye nilimuomba pesa zaidi ya mara tatu. Hapo sasa niliona naanza kuchanganya mambo niliamua kukaa kona moja sehemu ya Mtaa ya barabarani maeneo ya Faya nakufanya hapo ni makazi yangu ya kudumu.

Niliamua kutafuta nguo zilizochakaa ili nionekane kweli ni chokoraa na shukuru kipindi kile cha mzee ruksa watu walikuwa wakitoa pesa zao bila ya ubahiri. Ndani ya mwezi mmoja nilipata pesa nyingi kiasi cha kufuta wazo la kurudi nyumbani sikuwa na neno niliamua kupanga chumba na kununua vitu vya ndani.

Kuanzia hapo ikawa ni kawaida yangu ifikapo jioni kujichanganya katika majumba ya starehe ilikuwa ni vigumu kunitambua kwani mchana nilikuwa chokoraa niliyenyoa upara wenye kuonyesha kidonda kikubwa lakini usiku hubadili nguo na kuvaa nguo nusu uchi za kichangudoa na kichwani nilivaa wigi la nguvu. Nashukuru Mungu aliniumba nikiwa na umbo la kuvutia ndio maana hata baba na mtoto wake walishindwa kujizuia na kuamua kunibaka.

 Nikiwa viwanjani nilipata marafiki waliosifia figa yangu kuwa endapo nitafuatana nao lazima wazungu wajichanganye siwezi kukosa dola mia tano mpaka elfu kwa mara moja. Kutokana na malengo yangu nilikubali kuifanya kazi ile kwa muda kisha niachane  nayo.

Kuanzia hapo nikawa na kazi mbili asubuhi nakuwa ombaomba na usiku naruka viwanjani kama kawaida. Utafikiri nilikuwa nimejifukiza dawa wanaume walikuwa wakinifuata kama malkia wa nyuki hoteli zangu zilikuwa za kitalii tu sio za uswahilini.

Kutokana na kitendo cha mimi kuwazidi  kete baadhi ya rafiki zangu kiliwaudhi na walifanya kunifanyia njama. Shoga yangu mmoja alinipeleka kwa rafiki yake mmoja anayekuwa akisoma chuo kikuu ili tukamtembelee kumbe walikuwa wamepanga nibakwe na wanafunzi zaidi ya kumi  ili wanikomoe .

Bila ya kujua niliongozana na rafiki yangu yule  tulipofika chuo kikuuu niliingia katika chumba kimoja cha yule shoga yake mara aliniomba nimsubiri kumbe walikuwa wamewafuata wale wanafunzi wa kiume  mara waliingia vijana wa kiume kama kumi walinishika kwa nguvu na kunibaka. Kutokana kuwa sijawahi kufanya mapenzi zaidi ya mwanume mmoja nilizidiwa nguvu na kupoteza fahamu nilipozinduka nilijikuta nipo hospitali nikiwa katika hali mbaya.

Wanieleza kuwa walinikuta ufukweni nikiwa mtupu kama nilivyozaliwa  baada ya kuokotwa na askari wa doria ambao walinileta hospitali. Kila nilivyowaeleza hawakukubali walidai kuwa mimi ni changudoa uliyataka  mwenyewe. Niliruhusiwa kutoka hospital baada ya wiki tatu.

Nilipotoka hospitali hali yangu haikuwa nzuri sehemu zangu za siri zilikuwa zimeharibika vibaya na zilikuwa zikitoa harufu  mbaya kama mzoga uliokufa kwa ajali.

 Kwa vile nilikuwa na pesa za kutosha nilikwenda kwenye hospitali ya Mjerumani ambaye huduma zake zinasifika.

Hospitali yenyewe ipo Kibaha, Pwani, nilikutana na yule mzungu  ambaye alinichukua vipimo baada ya muda alinijulisha kuwa vipimo tayari  nakuniita kwenye chumba ambacho kilikuwa na mitambo ya kisasa.

Alinilaza kitandani ambapo aliniambia nipanue miguu yangu, alikuwa amevaa gloves na kunichunguza sehemu zangu za siri na kisha aliandika kwenye karatasi kabla hajaniruhusu kuvaa nguo zangu. Tulirudi hadi ofisini kwake na kunihoji  sababu zilipelekea nipate ugonjwa huo.

 Nilimweleza yote bila ya kumficha kitu, alitikisa kichwa na kusema:

“Ugonjwa huu  auhusiani na kubakwa bali ni vimelea ambavyo vimepandikizwa. Katika hospitali za kawaida usingepona kwani sehemu zako za siri zingeoza kabisa na hatimaye utumbo pia mwisho wake ungekufa.”


Post a Comment

0Comments

Your Thoughts

Post a Comment (0)