KISASI CHANGU
Laurent.Elpid
EPISODE 3
.ilipoishia..........
Kundi la walinzi walikoki silaha zao nakuja mbio katika chumba kulipo sikika shambalio la risasi ....
endelea.........
#UKISOMA USIACHE KULIKE NA KUTOA MAONI YAKO.
Nilipo hakikisha wameanguka chini na kupoteza maisha, wana haramu wale nilihisi nguvu kuniisha mwilini kutokana na nguvu nilizo tumia kuhakikisha silaha ile inakaa mkononi mwangu vizuri ili niweze kuwa shambulia ,
taratibu nikaiachia silaha ile na kulala chali pale sakafuni wakati huo nilisikia vishindo vya miguu vikifuata mlango wa chumba kile, nilijisemea kimoyomoyo liwalo na liwe maana kama ni ujanja sikuwa nao tena mwili ulichoka na kuandamwa na majeraha makubwa yaliyo kuwa na maumivu yasiyo pimika .
Ghafla mlango wa chumba kile ulifunguliwa , sikutaka hata kugeuka nimuone aliyeingia moyoni nilisha jitoa na kuwa tayari kwa lolote ikiwezekana hata kifo, nilifumba macho yangu na kulala kwa tumbo nikitazama sehemu za ukutani huku mapigo ya moyo yakinienda mbio, mtu yule alianza kupiga hatua za haraka nikisikia sauti ya viatu vyake iliyoonesha vilikuwa vya kike , alinifikia na kunishika begani akini nyanyua
"kaka nyanyuka haraka wanakuja" alikuwa msichana Sabra akiniambia huku akionekana kuwa na hofu sana
Nilijaribu kunyanyuka nikashindwa kabisa nikamuomba aniache tu asijiingize kwenye matatizo na baba yake, lakini katika hali iliyo nishangaza msichana yule alinipa mgongo na kunitaka nipande , nilijaribu kupinga nikimtaka aniache maana nilisha kata tamaa ya kuendelea kuishi lakini msichana yule haraka alini beba na kuniweka mgongoni mwake kama afanyavyo mama kwa mtoto mdogo..
Alitoka pale chumbani huku akikimbia ukisikika mlio wa viatu vyake kodo!!kodo!!! wakati huo nime jishikiza mgongoni kwa msichana yule lakini nikishangazwa na moyo wa ukarimu aliokuwa nao , kwa mtu kama mimi ambaye wakati ule nilikuwa kama adui yao.
Alizidi kutembea mpaka tukafika nje ya jumba lile kubwa , mara mbele yetu tukamuona mmoja wa walinzi akikatiza japo mwanza hakutuona lakini sauti ya viatu vya Sabra ilimtua na kujikuta amegeuka tulipo , papo hapo akaishikilia vizuri silaha yake na kuanza kutufuata..
"Sabra mpenzi huyo ulie mbeba mgongoni nani?"aliuliza mlinzi yule aliye onekana kijana wa makamo yangu huku akisogea aweze kuniona usoni vizuri, lakini kauli yake ili nifanya kujua ana mahusiano ya kimapenzi na Sabra.
"mpenzi huyu ndiye mnaye mtafuta na ni rafiki yangu wa muda mrefu nilisoma naye shule moja , kwahiyo nilivyo mkuta katika matatizo roho yangu haikuweza kutulia moyo uliniuma sana nikajikuta nashawishika kumsaidia, najua naenda kinyume na baba yangu mzazi pamoja na kiapo tuliacho weka , lakini tafadhali mpenzi wangu naomba uniache ni msaidie huyu ndugu yangu, nakuomba na kukuomba tena hii siri ubaki nayo peke yako mpenzi wangu na mpeleka mafichoni nitarejea baada ya muda kwa ajili yako nakupenda mpenzi naomba uaminifu wako"alisema Sabra na kumaliza kwa kumpiga busu jamaa yule ambaye alionekana kuridhishwa na maelezo ya mpenzi wake huyo pamoja na busu murua alilo pata lakini katika kutazamana naye usoni niligundua hakufurahia kitendo cha kuniona na mpenzi wake katika hali ile, yaani alikuwa na ka wivu fulani.
Tulitoka pale na kufika eneo la wazi lililokuwa na gari moja akanisaidia kuingia ndani ya gari ile kisha akashika usukani tukaanza kutoka nje ya ngome ile niliyo gundua ilikuwa ndani ya msitu mnene, nilimuuliza ana uhakika gani kama tungeweza kutoka katika ngome ile bila kujulikana akaniambia hata njia tuliyo tumia kutoka kule chumbani ilikuwa tofauti na iliyo zoeleka kupitiwa na watu ndani ya ngome ile na tungetumia njia ya kawaida tungekutana na makundi ya walinzi ambao bila shaka lazima wangetuweka chini ya ulinzi,pia nilimuuliza kuhusu kundi lile kuwa na uwepo wa watu wanaoonekana ni wakutoka mataifa mbalimbali duniani ,akaniambia ninacho takiwa kujua tu kuhusu mahali pale ni kwamba ile haikuwa ngome yao rasmi bali ni sehemu ya kupumzikia tu aliyo zoea kutumia baba yake ambayo aliweka vijana kadhaa kwa ulinzi wa eneo lile.
Gari ilizidi kukatiza msitu ule mnene huku nikiugulia maumivu makali hasa sehemu za shingoni kutokana mtikisiko wa gari lile hivyo Sabra akawa na kazi ya kunipa pole na kunitaka nivumilie. Hatimaye tulifika mwisho wa pori lile tukaingia kwenye barabara ya vumbi katika eneo ambalo pia hakukuwa na makazi ya watu bali ardhi kubwa na kavu ya tambarare ambapo tulishika barabara ile mpaka tukafika eneo lililokuwa na makazi ya watu katika eneo lililo kuwa na mji mdogo uliokuwa na watu nilio wafananisha na wasomali ikabidi nimuulize Sabra juu ya eneo tulilo kuwepo , akaniambia tulikuwa katika nchi ya Somalia katika mji wa kusini mashariki mwa nchi hiyo
Tulifika katika nyumba iliyokuwa tofauti na nyingine katika maeneo yale iliyokuwa imejegwa kisasa tofauti na nyingine zilizo jegwa kwa kuezekwa kwa udongo mpaka katika paa , tulipiga honi mara akatoka msichana wa makamo ya Sabra na kusalimiana na Sabra kwa lungha ya kisomali na kuzungumza kidogo , kisha wakasaidiana kunishusha gari wakanibeba na kunipeleka ndani ya nyumba ile ya kisasa ambapo msichana yule alibonyeza kitufe fulani ukutani , sehemu sakafu ya nyumba ile ikafunguka kukaonekana ngazi ambazo walishuka wakiwa bado wame nibeba tukafika sehemu ya chini ya nyumba ile iliyo kuwa na kila kitu ilicho takiwa kuwa nacho nyumba ya kisasa huku pia kukigawanywa vyumba tofauti na sebule.
Wasichana wale waliniweka kwenye kochi na kuanza kuni hudumia kwa kunipa chakula na vinywaji laini bapo sikuwa hata na nguvu ya kuinua kijiko hivyo walipata kazi ya kunilisha na kuni nywesha , baada ya kula walinibeba tena na kuniingiza katika chumba kingine kilicho onekana kama chumba cha kufanyia upasuaji ma hospitalini wanilaza juu ya kitanda kilicho zungukwa na mashine mbalimbali za kutibia na kunivua nguo nilizo kuwa nime zivaa na kuni visha mavazi kama wavaayo wagonjwa hospitalini kisha nao waka jitayarisha kidaktari
"Kaka huyu ni ndugu yangu anaitwa Shatya mtoto wa shangazi yangu , tunaishi wote hapa na tuna fanya kazi kama madaktari bingwa kwa baba yangu Mr.Erickson, hivyoo ondoa hofu hapa huko salama nia yetu nikukusaidia na kukurudisha katika nchi yako hapa tuna kufanyia operesheni kubwa ya kuondoa sumu iliyoingia mwilini mwako na pia tutaondoa makovu kwenye majeraha uliyo nayo sehemu mbalimbali na tutafanya jitihada kubadili mwonekano wa sura yako japo sio kufikia hatua ushindwe kutambuka kabisa , tutaongeza baadhi ya vitu katika uso wako ambavyo vitakufanya uwe tofauti kidogo na ulivyo sasa"alisema Sabra wakati huo msichana Shtya alinichoma sindano iliyo ulegeza mwili wangu nikajikuta napoteza nuru na sikuweza kutambua kilicho endelea..
Nilikuja kuzindika baada ya miezi miwili kweli nikiwa nime badilika kimuonekana katika sura ikiwa vigumu kunitambua kwa ambaye hatukuzoeana sana sio hilo tu hata afya yangu iliimarika sana na sikuwa na kovu la aina yeyote katika mwili wangu.
Niliwashukuru sana wasichana wale ambao nao walifurahishwa sana na kuamka kwangu huku nikiwa na afya tele, wakani tahadharisha kuwa Mr. Erickson ame kuwa akinitafuta kwa muda mrefu na ame fanya msako katika mji wote ule na kufikia hatua ya kuwa tuhumu baadhi ya walinzi wake na wao pia na kama sio hilo andaki la siri katika nyumba yao angesha nipata tangu muda mrefu, hivyo Sabra akaniambia alishanitafutia passport ya kusafiri pamoja na watu watakao nipeleka mpaka uwanja wa ndege Kenya nitakapo pata ndege ya kurudi Tanzania.
Nilimshukuru sana msichana yule nikiahidi kumlipia wema alio nitendea akanipa e. mail zake kama mawasiliano nika endelea kuishi pale nikisubiri siku ya kuondoka kweli ikafika siku ya kuondoka nikajiwa na wanaume wawili wa kisomali walio nisafirisha mpaka uwanja wa ndege wa kimataifa wa jomo kenyata ambapo nili panda ndege ili yonifikisha Tanzania katika jiji la Dar es salaam
Nili kwenda moja kwa moja katika hoteli niliyo kodiwa na mkuu wangu wa kazi na siku hiyo hiyo nikampigia simu na kumu eleza masaibu yote yaliyo nikuta huku nikimuomba ikiwezekana anitoe katika shughuli ile ambayo niliona tayari ili hatarisha maisha yangu nikimueleza kwamba upelelezi ule ulihitaji watu wengi maana ulihisisha vigogo wengi wakubwa ndani na nje ya nchi ambapo kwa Tanzania kiongozi wao alikuwa Mr.Erickson lakini nyuma yake kulikuwa na kundi kubwa linalo msapoti
Mkuu wa jeshi alifikiri kidogo na kuniambia ame kubaliana na ombi langu ata chagua kundi lingine lenye watu wengi ,lakini atahitaji niendelee kufanya upelelezi ule nikiwa kama mpelelezi binafsi huku akini tupia lawama kwa kuwa mzembe kiasi cha kushindwa kuwakabili watu wale wachache ukilinganisha na mafunzo niliyo kuwa nayo , sikuwa na jinsi nilikubaliana na uamuzi wa mkuu wangu huyo wa kazi niki omba ani wiye radhi kwa yaliyo tokea niki ahidi sasa kufanya kazi aliyo nipa kwa weledi..
Kesho yake jioni nilijiandaa vizuri na kwenda katika hoteli ile niliyo kutana na Mr. Erickson na kundi lake nikiwa na nia ya kutaka kujua kila kilicho endelea pale lakini hasa kuhusu msichana yule muhudumu aliye niingiza matatizoni siku ile na kupelekea kuharibika kwa kazi yangu..
Baada ya kufika nilikaa kwenye moja ya meza iliyokuwa tupu maeneo yale na kuagiza nyama choma na wine, nikaanza kula taratibu huku nikitazama tamthilia iliyo kuwa ikionyeshwa katika televisheni, mara kwa mbali kidogo nilimuona msichana yule akihudumia wateja vinyaji nili suburi amalize kisha nikamuita huku nikionyesha tabasamu pana usoni mwangu , kutokana na kubadilika kwa sura yangu kwa kiasi kikubwa hakuweza kunijua naye akatabasamu na kunifuata
Nilimsalimu na kumkaribisha mezani nikiweka tabasamu la bashasha , kwa kuwa wakati ule ndio alikuwa ame maliza mda wake kazini yaani alibadilishana na mwingine aliyeingia usiku , hakuwa na kipingamiza aliketi kwenye kiti na kutaka kujua nilicho hitaji kutoka kwake.
"nikusaidieje kaka yangu"aliniambia huku akiwa bize na simu yake aina ya Iphone
"samahani kwa usumbufu dada nacho hitaji kutoka kwako ni kampani yako tu kama hutojali, agiza kinywaji chochote utacho penda kutumia"nilimwambia huku nikiinua glasi na kupiga fundo moja la mvinyo
"hata usijali ndio natoka kazini , kama ni kampani tutakuwa pamoja"alinijibu na kuniaga anarudi ndani ya sekunde chache na baada ya nusu dakika alirejea akiwa na trey lililowekwa chupa mbili za mvinyo na glass ndogo za kioo
"mhhhh!!!!! vipi, unakunywa bila kula mbona haujachukua na chakula?"nilimuuliza
"usijali tayari nime shakula yani hapa nilipo niko full"alinijibu
"poa basi kwanza kabisa pole na kazi"nilimwambia huku nikifunga chupa ya mvinyo na kumimina kwenye glasi nikampatia
Tulianza kunywa taratibu huku nikimuuliza maswali yaliyo lenga kumuweka karibu na mimi na kutaka kujua undani kuhusu yeye naye alinijibu kulingana na jinsi nilivyo taka lakini pia akiniuliza maswali ambayo yalionesha kutokuwa na imani na mimi lakini niliyajibu kwa ufasaha hali iliyo mfanya aanze kuniamini na ndani ya muda mfupi tukajikuta tume zoeana kama watu waliofahamiana kwa muda mrefu
Kutokana na kilevi tulicho tumia tulijikuta tume wekeana ukaribu sana hivyo baada ya kumaliza pombe ile badala ya kila mmoja kurudi nyumbani kwake tulijikuta tunachukua chumba na kulala chumba kimoja usiku ule.
Asubuhi mida ya saa kumi na moja nilishtushwa na mlio wa ujumbe mfupi ulioingia katika simu ya msichana yule , nilijikuta nipo utupu pamoja na msichana yule katika kitanda kimoja ikiwa na maana tulivunja amri ya sita , nilivuta kumbukumbu na kukumbuka pombe kali tulio kunywa jana ndio iliyo tufanya tuwe katika hali ile lakini nilikumbuka pia nia yangu ya kukutana na msichana yule.
Niliiwasha simu yake nikakuta ime fungwa na inaweza kufunguliwa kwa kutumia (finger print) yaani alama za vidole, nilichekecha akili nikapata wazo la kumshikisha kidole chake ili niweze kufungua simu ile na kweli wazo lile lili fanikiwa bila yeye kutambua wakati wote huo akikoroma kwa usingizi mzito nazani pia ilichangiwa na mchezo tulio cheza usiku ule.
Niingia kwenye sehemu ya ujumbe ulio pokelewa (inbox) na kukuta messege kutoka kwa watu mbalimbali lakini kuna jina la mmoja wa watu aliotumiana nao ujumbe lilinifanya nifungue kutaka kusoma zaidi, hakuwa mwingine bali Mr. Erickson na alimsevu kwa jina hilo hilo hivyo niweza kupata wepesi wa kumtambua.
Nilianza kusoma message za tangu kipindi cha nyuma zilizo onyesha msichana yule alikuwa na tabia ya kuwa laghai wanaume na kuingia nao katika vyumba vya hoteli ile kwa ajili ya faragha lakini kuna kitu nyuma ya pazia walicho wafanyia watu hao
""tayari nimesha ingia Naye namdanganya naenda kuchukua kondomu halafu nyie mtaingia na kumkuta huko chumbani""ilikuwa ni moja kati ya jumbe zilizo tumwa kwa Mr. Erickson ambao ulijibiwa
""sawa vijana wamesha fika na vifaa pamoja na daktari"" nilibaki kujiuliza nini hasa sababu ya yeye kuingia na mwanaume na kumwacha ndani ya chumba na kisha majibu ya Mr .Erickson juu ya ujio wa vijana na daktari.
Niliachana na jumbe hizo nikashuka mpaka kwenye ujumbe ulio kuwa umenistua kutoka kwenye usingizi ule
"kama mawasiliano yanasumbua basi huyo achana naye ila uhakikishe siku nyingine una muweka mtegoni"ulisomeka ujumbe ule ambao sikuu elewa vizuri ikabidi nisome ujumbe uliotumwa kabla ya huo uliopokelewa.
"leo nime pata mmoja ila mawasiliano yana sumbua sijui kama tutaweza kuwasiliana vizuri" ulisomeka ujumbe ule ulioonesha ulitumwa saa sita usiku wakati nikiwa na msichana yule mezani tukipata vinywaji, nilijiuliza juu hasa ya alicho panga kunifanyia msichana yule na uhusiano wake na Mr. Erickson lakini sikuweza kupata majibu.
Niliufuta ujumbe ule uliokuwa umeingia nikausoma ili kuondoa uthibitisho kuwa nime chunguza simu yake nikatoka kwenye sehemu ya ujumbe mfupi na kuingia sehemu yenye picha , nikakuta picha mbalimbali za msichana yule mrembo huku nyingine akipiga na watu wa kundi la Mr. Erickson, lakini kuna faili la picha nililotaka kufungua lakini lika hitaji alama za vidole ili kufungua, nilichukua dole gumba la msichana yule ambaye bado alikuwa akikoroma kwa usingizi mzito na kugusisha katika sehemu iliyo hitaji kuwekwa kidole mara faili lile likafunguka
Nikaona picha za utupu na video za msichana yule akifanya uchafu na mwanaume fulani lakini wakati wakiendelea na tendo niliona mwanaume yule akianza kulegea na hatimaye kujilaza kama mlevi kitandani kisha msichana yule alijitoa akimuacha mwanaume yule akiwa mtupu na kuvaa nguo zake na kutoka nje ya chumba kile , mara waliingia vijana watano wakizungu wa nne na mwafrika mmoja wakiwa wame ambatana na mzee wa kizungu aliye valia mavazi ya kidaktari na kumsogelea mwanaume yule aliye kuwa kalala utupu kitandani na kuanza kutoa vifaa mbalimbali vya kidactari vyenye ncha kali lakini walicho mfanyia mwanaume yule kilinifanya nimuone msichana yule na kundi la Mr.Erickson katili zaidi ya wanyama wa porini na nikagundua kuwa mzee yule kuna mengi ya ajabu na ya kutisha aliyafanya bila kugundulika huku katika jamii akionekana moja kati ya wafanya biashara matajiri wema na walio tii sheria na amri za nchi.
Daktari yule haraka alichukua sindano na kuidunga kwenye kichupa kidogo cha dawa kisha akamdunga mwanaume yule shingoni ambaye alianza kurusharusha miguu na mikono kwa pupa huku akiyageuza macho yake mfano wa anaye kata roho hali iliyo wafanya wanaume waliofuatana na daktari yule wapate kazi ya kumshika kwa nguvu .
Baada ya dakika kadhaa mtu yule alitulia na tayari alisha yafumba macho yake na viungo vya mwili wake vilionekana legevu sana. Daktari yule akawaaagiza waovu wale wamlaze vizuri kitandani na kumbana na mikanda iliyo kuwa imeshikzwa kwenye kitanda sehemu za miguuni na kifuani jambo lililo fanyika ndani ya muda mfupi .
Kisha daktari yule pamoja na vijana wake wakavaa gloves mkononi na vifaa vya kufunika pua daktari aka chukua kisu kidogo chenye ncha kali na kuanza kumpasua kifuani mtu yule katika eneo la chembe ya moyo huku wote wame mzunguka nilishuhudia mtu yule akitolewa moyo wake uli chukuliwa katika utaalamu maalumu na kuhifadhiwa kwenye mashine maalumu kisha waka mtoa na figo zote mbili pamoja na ini ambavyo navyo vilihifadhiwa sehemu maalumu katika vifaa vya kitaalamu.
Baada ya kumaliza ukatili ule waliuchukua mwili ule uliobaki na matobo sehemu ya kifuani na tumboni ukivuja damu nyingi na kuutumbukiza katika begi kubwa la mizigo lililo wambwa kwa ngozi ya ngamia kisha wakachukua na zile mashine maalumu walizo hifadhia viungo vya mtu yule na kujiweka katika hali ya usafi huku wakipongezana kuimaliza kazi salama ambapo walipiga simu kumjulisha niliye hisi ni bosi wao kwamba kazi ilimalizika hivyo asiwe na hofu , walianza kucheka na kupasiana mikono huenda ni jibu zuri walilo pata kutoka kwa mkuu wao.
Baada ya yote hayo video ile ilikata kuonesha ime fika mwisho , nilijikuta nageuka upande wa pili kumtazama msichana aliye lala pembeni yangu hakika hakuwa na sura iliyoonesha uwepo wa roho mbaya na ya kikatili ndani yake , aliokuwa na sura ya kipole iliyo pambwa na muumba na nikiri alikuwa ni moja kati ya wasichana wazuri nilio wahi kukutana nao. Nilijiapia kuto muacha mpaka niujue ukweli kupitia yeye na kama ni mpango wa kuniangamiza nilijiza titi kuwa makini sana na kuepukana na mtego wowote watakao hitaji kuni fanyia.
Pia bado swali lilibaki kichwani mwangu juu ya nini hasa sababu ya kuchukua viungo vya mwanaume yule na kama ndio mchezo wao walivipeleka wapi ?, nikarudisha kumbukumbu zangu nyuma juu ya tukio la kupotea mara kwa mara kwa watu waliodhaniwa mara ya mwisho kuonekana walifika katika hoteli hiyo ikiwa ni matukio yalio tukia miaka miwili iliyo pita ikasadikika wali tekwa nikaona huenda msichana yule anajua mengi kuhusu mambo hayo niliamua taratibu kuendelea kumchunguza mpaka nitakapo ujua ukweli
Sikutaka kuona mengi zaidi katika simu ya msichana yule nilichukua e.mail yake kisha nikaizima simu yake na kuirudisha ilipokuwa bila yeye kutambua chochote
Taratibu nikaanza kuzichezea nywele zake nikiwa na nia ya kumuamsha ambapo nilifanikiwa kwani alishtuka na moja kwa moja akatupa macho kwenye saa ya ukutani iliyoonesha ilikuwa majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi , alinigeukia na kunitazama mfano wa anayetaka kukumbuka jambo fulani kisha akajitazama na yeye na kujikuta katika hali ya utupu.
"Khaaaaa!!! wewe kaka hivi tume fanya chochote usiku" aliniambia akionesha hofu huku amelishikilia shuka kifuani kujisitiri
"nikuulize wewe maana ndio uling'ang'ania"nilimwambia
"mungu wangu!!!!!! wekaka una niharibia maisha yangu yangu kwanini ulikubali kufanya hivyo wakati uliona kabisa nipo kwenye siku zangu??"aliongea kwa hamaki
"siku zakoo !! kwanini hukunieleza kabla sasa mimi ningejuaje"nilimjibu nami kwa mshangao ambapo alishuka pale kitandani na kuanza kuzunguka akitazama sehemu za pembeni ya kitanda ambapo kweli alitoa nguo ya ndani iliyokuwa imevaliwa na pedi iliyo kuwa imelowa damu
"hii hapa ona sasa ndoto zangu zote ume niharibia nitaenda wapi mimi na ujauzito huu kama sio kifo umeni tafutia"aliniambia huku akionesha masononeko.
Nilishindwa kujua cha kumsaidia zaidi ya kumuomba akapime ili kujua kama kweli ame nasa ujauzito na kumuahidi kama atakuwa na ujauzito nipo tayari kulipia gharama za kuitoa ile mimba. Alikubali shingo upande lakini akaniambia ange hitaji tupate muda wa kulizungumzia suala hilo mahali pengine akili zikiwa zime tulia na kama ni akigundua amenasa ujauzito hayupo tayari kutoa ni bora hata afe kuliko afanye hivyo kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na matakwa ya mwenyenzi mungu, nilishindwa kumuelewa msichana yule maana ukatili niliouona kwenye simu yake na maneno aliyo kuwa akiniambia wakati ule vilikuwa ni vitu viwili tofauti.
Nilikubaliana naye kuhusu suala la kukutana naye akachukua simu yake na kiuwasha lakini hakuweza kugundua kama ili tumika , nilitoka na kwenda bafuni kujimwagia maji kisha nikarejea na kuvaa nguo zangu na kuondoka nika mwomba tukutane baada ya siku tatu na aje na majibu ya daktari kuhusu suala la ujauzito alikubaliana nami lakini katika kumtazama niliona katawaliwa na msongo wa mawazo mengi kichwani.
Nilienda moja kwa moja mpaka hotelini nilipoishi na kuiwasha laptop yangu ambapo uliingia ujumbe kwa njia ya e.mail kutoka kwa mtu ambaye siku mtambua ukinitaka niende moja kwa moja katika hoteli moja ya kifahari iliyo julikana kwa jina la Vienna park kuna mauaji yalitakiwa kufanyika. Nilishtushwa na ujumbe ule ukizingatia siku mtambua mtumaji lakini nikaona niende kuona kama kuna ukweli..
Nilichukua bastola yangu ndogo iliyo kuwa ime wekewa kiwambo cha kuzuia sauti , sindano maalumu ya sumu inayo weza kuupoteza uhai ndani ya sekunde chache pamoja na miwani yangu yenye uwezo wa kupiga picha kwa kui elekeza kwa macho.
Nikachukua bajaji iliyo nifikisha mpaka nje ya eneo la hoteli hiyo hiyo kubwa iliyo tumiwa na watu walio kuwa na kipato cha juu nikaingia mpaka ndani ya eneo la hoteli hiyo lakini sasa nilibaki na mtihani wa kujua ni nani na ni mauaji gani yalihitaji kutekelezwa.
Niliingia mpaka kaunta na kukuta mhudumu ambaye baada ya kuniona alinipokea kwa uchangamfu na kuniambia kuwa nilikuwa mmoja kati ya washiriki wa mkutano ulio hitaji kufanyika katika eneo lile huku akinionesha kitambulisho kilicho kuwa na picha pamoja na majina yangu, nilishangazwa lakini ilinibidi kuamini maana hata taarifa yenyewe nilio tumiwa siku mjua aliye ituma.
Niliipokea kadi ile na kuongozana na msichana yule aliye niongoza mpaka katika chumba cha mkutano ambapo nilikuta watu mbalimbali wakiwemo baadhi ya viongozi wakubwa lakini wote walio kuwamo wakionekana ni watu walio kuwa na uwezo wa juu kifedha.
Pia nilimwona mkuu wangu wa kazi aliyeni salimu kwa tabasamu kutokana na umbali tulio kuwemo ,kisha katika kutazama nikamwona kijana aliye kuwa na umri makamo yangu aliye kuwa amevaa shati yenye kola iliyokuwa na nembo kama iliyokuwa kwenye shati yangu ambayo ilitumika kama utambulisho wa siri kuwakilisha wanajeshi waliofanya shughuli za kipelelezi aliponiona alinikonyeza na kuyarudisha macho yake mbele akiendelea kusikiliza yaliyo zungumzwa katika mkutano .
Mkutano ule ulikuwa ni wa wafanya biashara wakubwa nchini uliolenga kuimarisha uwekezaji na usalama wa mazingira rafiki kwa ajili ya wafanya biashara wote na mgeni rasmi alikuwa Mr.Erickson lakini hakuhudhuria hivyo aliwakilishwa na mfanya biashara mwenzake.
Niliweza pia kutambua uwepo wa vijana wa Mr. Erickson wawili ambao mmoja nakumbuka alikuwa kati ya nilio washambulia na kuwa uwa kwa risasi kipindi walipo nikamata .
Mkutano uliendelea huku nikiwa makini kutazama pande zote kuona iwapo kulikuwa na dalili ya kutendeka kwa ovu lolote , huku mpelelezi mwenzangu naye akiwa makini kufuatilia kila kina choendelea hata vijana wa Mr.Erickson nao walikuwa makini sana.
Ulifika wakati mkuu wa jeshi alitaka kwenda kujisaidia nikaona ameelekezwa na mhudumu mmoja chumba cha choo kilipo ni katupa macho upande walipo vijana wa mr.Erickson nikaona amebaki mmoja wakati mwanzo niliwaona wawili nikamtazama na mpelelezi mwenzangu naye kama kuna kitu aligungua akataka kunyanyuka nikamuonyesha ishara akae aniachie nami nikanyanyuka na kuelekea alipo mhudumu nikamuomba kujua vyumba vya kujisaidia vilipo mhudumu yule aliye nielekeza katika kile kile choo alicho ingia mkuu nikatembea mwendo wa haraka kusudi nimuwahi mkuu wangu maana kengele ya hatari tayari ilisha gonga kichwani mwangu
Nikaufungua mlango na kuingia kwa tahadhari
Niliingia na kuelekea moja kwa moja mpaka kwenye sehemu maalumu zilizo wekwa kwa ajili ya kujisaidia haja ndogo kwa wanaume na kukuta yule gaidi akiwa nyuma ya mkuu wa jeshi aliye kuwa bado akijisaidia huku huku gaidi yule akijifanya kujiweka vizuri ambapo niliona ameingiza mkono kwa tahadhari huku akitoa kitu lakini katika kuangaza macho akihakikisha hakuna aliye muona alikutana na sura yangu ikimtolea macho kama mjusi , haraka alirudisha kiunoni alichotaka kukitoa na kujiweka vizuri akitaka kuondoka lakini sura yake ilionesha mfadhaiko na chuki dhidi yangu.
Mkuu wangu wa kazi alipo maliza kujisaidia na kugeuka alikuta nimesimama mbele ya jamaa yule ambaye bado alikuwa akichomekea shati lake na kuweka koti lake la suti vizuri .
"vipi kijana kuna usalama mbona ume tusimamia kama unataka kututeka?"alisema mkuu wa jeshi lakini nazani tayari alijua hakuna usalama eneo lile na pia alijua dhumuni la uwepo wangu mahali pale
Sikumjibu chochote mkuu wangu nilicho fanya ni kuitoa bastola yangu kiunoni na kumnyooshea gaidi yule, ambaye alionesha kustuka haraka akamvamia mkuu wa jeshi na kumkaba shingoni kisha akatoa bastola yake na kumuwekea kichwani.
"try move i shoot him (jaribu kusogea nimpige risasi)"aliongea gaidi yule kwa lugha ya kiingereza huku ameikaza sura yake vilivyo, mkuu naye hakujigusa alitulia na kunikonyeza ambapo kwa haraka mkuu alijigeuza na kuishika kwa nguvu ile bastola ya gaidi na kumgeuzia ambapo yule gaidi kwa taharuki ajikuta akivuta kiwambo cha bastola kilicho fanya atoe ukelele wa maumivu baada ya risasi kadhaa kupenya ndani ya bega lake damu zikianza kumvuja bahati nzuri bastola ile ili kuwa na kiwambo cha kuzuia sauti, aliiachia bastola ile ambapo haraka mkuu wa jeshi aliiwahi na kuiokota wakati huo ilibidi niwe mtazamaji wa mtanange ule maana kulingana na sheria nilizo fundishwa haikuruhusiwa kuingilia wala kupinga kazi anayo ifanya mwanajeshi mwingine labda kama amezidiwa na ikitegemea yule alikuwa mkuu wangu ilibidi nimuwekee ulinzi kwa kutumia bastola tu endapo angezidiwa.
Gaidi yule haraka alirusha teke na kuipiga bastola ambapo mkuu aliiachia ikaanguka chini kisha akajiweka sawa ukaanza mpambano mkali kati ya mkuu wangu na jambazi aliyeonekana kuwa na ujuzi wa hali ya juu wa kivita japo tayari alikuwa majeruhi lakini aliweza kumpelekea mkuu wa jeshi makonde na ngumi nzito ambazo mkuu naye hakuwa nyuma alizipangua na kurudisha mapigo ya kipekee kabisa kwa gaidi yule ambaye kila alivyo zidi kupigwa naye ndivyo alivyo zidi kurusha mateke ya hewani ambayo baadhi yalimpata mkuu kifuani lakini mkuu alijiweka vizuri nayeye kuanzisha shambulizi .
Gaidi yule alianza kutumia staili mbalimbali ambazo baadhi nilikumbuka nilifundishwa kipindi nikiwa mafunzoni ughaibuni mapigo yaliyo mfanya mkuu ayumbe huku na kule kisha mkuu naye alikuja na aina mpya ya upambanaji ambapo alianza kumshambulia gaidi yule kwa kasi ya ajabu na ujuzi wa kipekee , gaidi yule alianza kuyumba huku akijitaidi kupangua baadhi ya mapigo .
Mkuu kuona hivyo alinitazama kisha akanikonyeza haraka na kujitoa karibu na gaidi nilimrushia bastola ile akaidaka na kumnyooshea kisha nikasogea alipokuwa gaidi yule haraka nikatumia staili ya kupigana kwa kutumia vidole viwili katika mikono yote nikivielekeza sehemu za machoni na shingoni kwa gaidi yule aliyeanza kuweweseka huku akijishika sehemu hizo ambapo damu zilianza kumtoka machoni hapo akanipa nafasi ya kurusha mateke matatu ya hewani yaliyo lenga katika sehemu iliyo lengwa na risasi nikelele za maumivu tu zilisikika ambapo gaidi yule alianguka chini akijaribu kujinyanyua lakini ilishindikana nilimsogelea na kuitoa sindano ya sumu kisha nikamdunga kiasi kidogo kabisa cha sumu ile ambacho niliamini kisinge weza kumuua zaidi ya kumpoteza fahamu kwa muda mrefu.
Baada ya hapo niligeuka na kumtazama mkuu wa jeshi aliye nipigia makofi huku akitabasamu na kunisifu juu ya uwezo na ujasiri wangu lakini nilimpa wazo la kumpeleka gaidi yule katika kikosi cha upelelezi jeshini wakamchunguze ili asaidie jeshi kujua mengi juu ya kundi lile haraka mkuu wa jeshi aliongea na mmoja wa makamanda wa jeshi akimueleza juu ya tukio zima na uamuzi tuliofanya ambapo ndani ya dakika tano liliingia kundi la wasichana watatu waliokuwa wamevalia kama wahudumu wa hoteli ile ambao baada ya kufika walimpa heshima mkuu wa jeshi kisha mimi halafu wakamchukua gaidi yule na kumuingiza ndani rambo kubwa nyeusi na kumuweka katika kifaa maalumu kilicho tumika kuwekea takataka kilichokuwa na matairi kisha wawili wakatoka akabaki mmoja wao akisafisha damu zilizo sambaa kwenye sakafu ambaye baada ya kumaliza alitoka nami pamoja na mkuu wa jeshi tulijiweka sawa na kurudi katika mkutano lakini uzuri ni kwamba katika tukio zima lililotokea hakuna aliye fika eneo la chooni japo hata mlinzi.
Hatimaye baada ya kikao kile kuisha watu walianza kutawanyika kila mmoja akirudi katika shughuli zake tukiwemo mimi, mkuu wa jeshi pamoja na wanajeshi wa kikosi cha upelelezi na walinzi wa mkuu wa jeshi waliokuwepo pale. Mr.Erickson na watu wake naye pia waliondoka eneo lile lakini baada ya kufika katika magari yao na kupanda waligundua kutokuwepo kwa mmoja wa wanajeshi wao aliye julikana kama Mkoma , waliulizana lakini hakuna aliye kuwa na taarifa zozote juu ya alipo kuwepo kwa wakati ule .
Ilibidi wambane mmoja wa magaidi aliye kuwa amekaa karibu na Mkoma katika mkutano ule ambaye alikiri kuondoka kwa Mkoma akidai anaelekea kujisaidia ambapo hakumuona tena mpaka wanatoka kwenye kikao kile, jambo hilo lilimchanganya sana Mr .Erickson aliye toa taarifa polisi na katika kundi lake huku akimtuhumu Mkoma kama mfanya kazi wake aliye toroka na kumuibia mamilioni ya shilingi na kushambulia kwa kutumia silaha yote hayo akiyafanya kama njia ya kummaliza Mkoma kwa kumchafulia jina na kumsababishia kesi ambayo inge weza kumweka ndani maana tayari alihisi huenda Mkoma ame wasaliti na hivyo kabla hajatoa siri akaona amchafue ili polisi wasiwe tayari kumsikiliza.
"niliwaambia muda mrefu huyu mnigeria si mtu mzuri ona sasa ana chotaka kutufanyia habari nimesha toa polisi nikimtuhumu kwa wizi wa kutumia silaha na pia kabla polisi hawaja mpata nataka mumtafute mmuuwe haraka"alisema Mr. Erickson akiwa katika gari yake ya kifahari .
Taarifa za kutafutwa kwa mhalifu mkubwa aliye muibia mamilioni bosi wake ambaye ni bilionea mkubwa nchini Mr.Erickson zilisambaa haraka nchini huku picha zake zikisambazwa mitaani na katika mitandao mbalimbali ya kijamii huku vijana wa Mr. Erickson nao wakifanya msako wa chini chini wakihitaji kuitoa roho ya mwenzao yule ambaye tayari alikuwa adui yao mkubwa ndani ya muda mfupi bila kujua sababu ya kutokea kwa yote hayo lakini hakuna hata mtu mmoja aliye jua alipo kuwa gaidi yule zaidi ya kikosi maalumu cha upelelezi cha jeshi nikiwemo mimi na mkuu wa jeshi.
Nilirudi hotelini nikiwa mchovu nika jimwagia maji na kuagiza chakula cha mchana ambapo simu yangu iliita nilipoitazama ilikuwa namba ya mkuu wa jeshi akinipongeza na kuelezea kuridhishwa na kazi yangu akahitaji kunipa nafasi ya kuwa mlinzi wake binafsi lakini sikuwa tayari nikamwomba anipe nafasi nifanye kazi kama mwanajeshi huru yaani niwe na uwezo wa kuishi nitakavyo lakini nihakikishe kazi ya kulimaliza kundi la Mr. Erickson inafanikiwa japo mwanzo alipinga lakini nilitumia ushawishi wangu baada ya muda akawa ame nielewana kukubaliana na maombi yangu, nilimshukuru na kumuomba aniongezee kiasi cha fedha katika akaunti yangu maana nilitaka kutafuta sehemu nyingine ya kuishi naye akafanya kulingana na ombi langu.
Mazoea kati yangu na msichana muhudumu wa hoteli yalizidi kukua tukawa tukikutana na kuzungumza mara kwa mara tukichukuana na kutoka jioni mara kwa mara msichana yule akajikuta ameangukia katika penzi langu , lakini ukweli sikuwa na hata chembe ya upendo juu yake bali nilifanya hivyo nikitaka kujua mengi juu ya uhusiano wake na kundi la Mr. Erickson na pia juu hasa mauaji ya kutisha yaliyo fanyika huku msichana yule akitumika kama chambo .
Nilimuhadaha kwa maneno matamu na vitendo vilivyoonyesha upendo juu yake akazidi kunipenda ikafikia hatua akawa hawezi kumaliza siku bila kuniona au kuisikia sauti yangu hakika kama ni mapenzi juu yangu yalizidi na kupilitiliza, lakini katika siku zote hizo sikutaka kukutana naye tena kimwili japo alinisumbua sana maana nilihisi huenda akaniambukizia magonjwa hatari kutokana na kazi aliyo kuwa akiifanya.
Alinipenda sana nami nikamuonyesha upendo wa kinafiki huku mara kwa mara nikitumia udhaifu wa mapenzi aliokuwa nao kwangu kumuuliza maswali kimtego yaliyo husu uhusiano wake na Mr. Erickson lakini siku zote hakuwahi kunieleza ukweli juu ya hilo ilibidi nianze kufuatilia mienendo yake
Nilisubiri mpaka wakati wa usiku ikiwa ni baada ya kuachana naye tukitoka kupata mlo wa pamoja akiniaga ana enda nyumbani . Nilimuaga nika igiza kama naondoka baada ya kufika mbali naye kidogo niligeuza na kuanza kumfuatilia wakati huo akitembea haraka akakatiza barabara iliyo elekea mtaa wa Vuai ilipokuwepo klabu kubwa ya usiku ya Serena nilimfuatilia nyuma taratibu na kwa umakini mkubwa mpaka alipo fika katika ile klabu ambapo aliingia ndani, sikukawia nami nikapiga hatua kumfuata kule ndani.
Kwakweli ndani ya klabu ile kulifanyika anasa za aina mbalimbali zikiwemo kamari , uasherati na ulevi bila kusahau mziki mnene uliokuwa ukichezwa na wadada waliovalia nusu uchi huku miili yao ikitomaswa vilivyo na wanaume wa rika la baba zao.
Msichana yule alipitiliza moja kwa moja mpaka kwenye moja ya vyumba katika hotel ile hivyo ikanibidi kukaa nisubiri kwa muda wakati huo nikaagiza bia baridi nikaanza kuinywa taratibu mara akaja msichana mmoja aliye kuwa ame vaa nusu uchi ikionesha moja kwa moja alifanya biashara ya kuuza mwili.
Alianza kuongea nami kwa uchangamfu huku wakati wote uso wake ume tawaliwa kwa tabasamu lenye bashasha lakini zaidi ya yote alijitahidi kukaa kimtego ili aweze kuninasa lakini wakati huo akili yangu haikuwa pale ili muwaza msichana mhudumu wa hoteli.
Baada ya muda kidogo msichana mhudumu wa hoteli alitoka ndani ya kile chumba alicho kuwa ameingia lakini wakati huu sasa alikuwa amebadilika kimuonekano kuanzia mavazi mpaka urembo wa sura naam alifanana na kinadada wale walio fanya biashara ya kuuza miili yao , kweli ilinishangaza lakini nikaona nitulie na kusubiri.
Msichana yule alitoka taratibu kwa mwendo wa madaha na kufika katika sehemu iliyo kuwa maalumu kwa mchezo wa kamari ambapo katika mwendo wake huo wa madaha , umbo na kivazi alicho kuwa amevaa vidume wengi walimkodolea macho ya matamanio, ali mtizama mmoja wa wachezaji wa mchezo ule aliyeonekana kuwa kijana aliye kuwa na mwili wenye afya ya mazoezi na kutabasamu . Tabasamu la msichana yule likawa mtego tosha wa kumnasa kijana yule ambaye aliwaaga wenzake taratibu akaanza kumfuata yule msichana , alipomfikia wakakaa meza moja na kuanza kuongea huku binti yule akikaa kimtego na kuyatanua mapaja yake hali iliyozidi kumchanganya kijana yule mbichi ambaye alijikuta akimshika mkono yule binti wakaondoka na kwenda kukodi chumba ndani ya hoteli ili.
Wakati huo tayari nilisha chukua picha za msichana yule pamoja na matukio yote ya ajabu nilio yaona pale,nilimaliza fundo la mwisho la bia yangu nikatoka na kulipia kisha likanijia wazo lakuchukua mmoja wa wasichana waliofanya biashara ile na kutoka naye nje ya eneo lile nikiwa na lengo la kumteka ikiwezekana anisaidie katika kufanikisha mambo yangu.
Nilipita taratibu nikiwa tizama mmoja mmoja machangudoa wale walio kuwa wa umri tofauti watoto hata wanawake watuwazima huku kila mmoja akijigeuza kimahaba ili mradi tu niweze kumchukua.Nilifika mpaka alipo kuwa binti mdogo aliyeonekana kama wa miaka kumi na tisa nikamshika kiuno na kutoka naye taratibu nikatafuta meza na kukaa ambapo alianza kuniwekea mitego kama ilivyo kawaida yao pia akinitajia bei ambapo ilikuwa shilingi laki mbili kwa usiku mmoja , nilikubaliana naye lakini kwa sharti moja kwamba nilitaka tuende nyumbani kwangu ambapo kama asinge jali ninge mlipa shilingi laki tano wakati huo tayari nilitoa bunda la fedha na kuliweka mezani , msichana yule baada ya kuona fedha zile akachanganyikiwa na kujikuta akitaka kuzichukua lakini nikamwambia anipe huduma kwanza pesa baadae ilibidi akubali japo kwa shingo upande lakini akaomba nitangulie kutoka nje yeye atafuata nilikubaliana naye na kutoka lakini kichwani likajijenga swali "kwanini iwe hivyo "?.
Kilipita kitambo naye akatoka nje nikatoka naye eneo lile tararibu tukitembea kwa miguu kwa kuwa gari nililiacha katika hoteli nilio kwenda kwa ajili ya mlo wa usiku.
Nilichukua gari tuka panda na kuelekea moja kwa moja nyumbani kwangu kimara ambapo tulikwenda moja kwa moja chumbani nikimuhakikishia usalama msichana yule aliyeonekana kuwa na hofu sana.
Nilimwambia azime simu yake nikiwa nahakikisha usalama wangu iwapo labda alijihusisha na kundi la Mr. Erickson lakini alikataa katu akasema hawezi kufanya hivyo na kama nina mlazimisha bora biashara ife, ikabidi nijishushe kidogo nikakubaliana naye tukaanza kuchezeana kuamsha hisia huku wakati huo nikiweka juhudi za kumlegeza msichana yule aliye kuwa mdogo wangu kiumri ambapo hilo nililifanikisha na haraka nilimkaba shingoni kwa nguvu huku sasa nime weka sura yangu katika hali ya kukasirika
"nataka uniambie kila kinacho endelea katika klabu ile pamoja na katika baadhi ya hoteli hapa mjini , kipi hasa huwa mnafanya ninyi machangudoa maana nimesikia kupotea kwa watu wengi wanao wachukua nyinyi, jibu haraka la sivyo na kumaliza"nilimwambia msichana yule aliye kuwa kalala chali na kuonyesha sintofahamu juu ya kinacho tukio wakati huo nimemkaba shingoni vilivyo
"Sijuuhh!!!!!iiii chochote"
"hujui sasa ngoja nikuoneshe" nilimwambia na kumshindilia konde zito usoni ambapo alitoa ukelele wa maumivu japo haukuweza kusikika kutokana na kumkaba kooni.
Akaanza kupambana kutaka kujinasua wakati huo sura yake ime anza kulowanishwa na machozi
"niambie mnacho fanya kule mwana haramu wewe ukileta utani na kumaliza"nilimwambia huku nikimnyanyua pale kitandani na kumuweka mkao wa kukaa tukawa tuna tazamana wakati huo alikuwa akilia na kuniomba nimuachie nilijikuta nimeingiwa na huruma na kuiachia shingo yake lakini nikimtaka anieleze bila kupindisha maneno.
Nilipo muachia tu ilikuwa kosa kubwa kwani haraka alinipiga kichwa kwa kikali katika paji langu la uso bapo niliweweseka kidogo akapata upenyo wa kurusha mateke ya juu yaliyo nipata kwa pamoja kifuani yakiniachia maumivu makali kutokana na visigino virefu vya viatu alivyo kuwa ame vaa.
Nilijiweka sawa haraka na kusubiri afanye shambulio ambapo alirusha tena mateke mawili kama alivyo fanya mwanzo niliyo yadaka kwa pamoja na kumzungusha hewani kwa nguvu kisha nikamrusha ukutani ambapo alipigiza mgongo nikazani hatoa mka tena lakini nilishangaa ameinuka na kukunja ngumi zake vizuri.
Ukweli ni kwamba sikutaka nitumie nguvu na uwezo nilio kuwa nao kwa msichana mdogo kama yule ambaye nilihitaji kupata mengi kutoka kwake,.
Alinifuata tena kwa kasi na kuanza kunirushia ngumi mfululizo huku pia akijitahidi kuyarusha mateke yake ambapo zote nilizipangua huku nikimpiga kwa nguvu katika viungo vya mikono na miguu yake ambapo niliona anajitahidi kujilazimisha kunirushia ngumi na mateke lakini mikono na miguu yake tayari vilimsaliti hivyo ika mbidi ajishushe japo alinitizama kwa hasira huku pia akitazama mlango wa chumba kile niliokuwa nimeufunga na kuzificha funguo.
"Nisikilize mdogo wangu sipo hapa kwa ajili ya utani wala kupigana na wewe nacho hitaji ni majibu ya maswali nilio kuuliza hapo mwanzo pia nataka kujua ni nani aliye kufundisha kupigana na pia kwanini huku takakuzima simu wakati nilipo kuambia"nilimwambia wakati huo nimesogea karibu na alipo nikimpa nguo zake avae lakini katika kumtazama kwa macho yangu mia moja ya kipelelezi niliona mkono wake mmoja ukitoa kisindano kidogo katika nguo ya ndani aliyo kuwa amevaa kish a kwa haraka akakirusha kuelekea nilipo, haraka nikakikwepa kikaenda moja kwa moja kulenga ukuta.
Nilijikuta hasira zime nipanda nikarusha ngumi nzito iliyo enda moja kwa moja katika paji la uso la msichana yule aliye anguka na kupoteza fahamu.
Niliifuata sindano ile sindano na kuichukua nikaichunguza na kugundua ni dawa iliyo kuwa na nguvu ya kumlevya mtu na kumfanya apoteze fahamu .
Nilimfunga msichana yule kwa kamba mikononi na miguuni nikasubiri mpaka alipo rejewa na fahamu kaanza kunisimulia mkasa mzima.
ITAENDELEA
Your Thoughts