SIRI YA MUUAJI EPISODE 1
NA.
K-FANI J.RUMAMBO.
Kwenye kituo cha polisi cha nchi ya china kulionekana
waandishi wa habari wa kila aina ya televisheni huku wakijitahidi kutaka
kuingia ndani ya kituo cha polisi ili kupata picha ikiwezekana na video pia
kuhusu kukamatwa kwa muuaji hatari sana aliyekuwa anasumbua serikali ya china na dunia kiujumla
kutokana na matukio yake aliyokuwa anayafanya kwenye kila nchi atakayoenda.
Walipata vikwazo kutoka kwa maaskari wa kituo kikuu cha shanghai, waliokuwa
wanawazuia kutoingia ndani kwa usalama wa mtuhumiwa kwani. Walijua kutakuwa na
watu wanaoshirikiana na muuaji huyo. Wanaweza kumuua ili kuondoa ushahidi na
kuepuka kutojulikana maficho yao.
Ndani ya chumba cha mahojiano, alionekana kijana mmoja
mwenye asili ya kiafrika akiwa kafungwa kwenye kiti na kamba ngumu ili kumzuia
kutojinasua kama atataka kufanya hivyo. Kijana yule aliyekuwa kapoteza fahamu
kutokana na kupigwa sana, haikujulikana ni kipi hasa kilichomfanya kuwa pale na
kwanini taarifa zake za kukamatwa zimesambaa kama mvua... Akiwa hana ufahamu wa
kujua sehemu alipo, mlango wa kuingilia ndani ya chumba cha mahojiano.
Ulifunguliwa na maafisa wa C.I.A.
wapatao watatu waliingia ndani wakiongozana na maaskari kutoka katika
jeshi la nchi ya china.
''Mfungueni hapo na mmpeleke kwenye gari. Atatakiwa
kuhukumiwa kwenye nchi ya marekani huyu''. Afisa mmoja wa C.I.A alitoa agizo na maaskari wawili wa china
wakishirikiana na wale wa C.I.A. Walimfuata yule kijana ambaye mpaka sasa bado
haijafahamika ni kwanini yupo pale. Walimfungua mtuhumiwa kwenye kiti na
kumbeba kwa kusaidizana, mmoja alimshika na kupitisha mkono wake wa kushoto
kwenye bega la kulia la mtuhumiwa..... Na yule mwingine akapitisha mkono wake
kwenye bega la kushoto la mtuhumiwa na kuanza kumtoa nnje huku nyuma wengine
wakiwasindikiza kwa silaha kama ulinzi.
Kutokana na kutokuwa na fahamu, ilimfanya yule kijana mwenye
asili ya kiafrika kushindwa kufanya jambo la kujitetea na kukubali kubebwa
msobemsobe kama gunia la taka, walitumia njia za chini kwa chini kumsafirisha
mtuhumiwa wakihofia kupita njia za juu kwaajili ya usalama zaidi, njia za chini
ziliwaraisishia kufika mpaka kwenye uwanja wa ndege wa nchi ya china ambapo
walimpakiza mtuhumiwa kwenye ndege tayari kwa safari.
''Agent Gibson, nadhani biashara baina ya nchi yako na yangu
itakuwa imeishia hapa. Mtuhumiwa wenu ndio huyo hapo na sisi kuanzia sasa
tutakuwa hatuhusiki kwa chochote kile kinachohusiana na huyu mtu.''. Kamanda wa
jeshi la polisi nchini china. Kamishna Wuen Lee, alizungumza hayo baada ya
kuwafikisha maafisa usalama kutoka kwenye kitengo maalumu cha C.I.A kwenye
uwanja wa ndege wa nchi ya china na kuongea juu ya nchi yao kujiangua kwenye
suala la muuaji yule aliyetakiwa akahukumiwe kwenye nchi yake ya marekani.
''Ahsante sana. Wuen Lee. Hakika wewe pamoja na nchi yako ni
marafiki wema sana, msaada mliotupatia unatosha sana na.... Mpaka hapa
tulipofika tunaweza kusema asanteni! Sana.''. Agent Gibson alizungumza hayo na
kupeana mikono kama ishara ya kushukuru kwa kile walichofanyiwa na nchi ya
china.
Baada ya makabidhiano ya mtuhumiwa na kuweka sign nyaraka
kadhaa. Maagent kutoka kwenye kituo kinachojishughulisha na maswala ya
kiupelelezi. C.I.A,walipanda kwenye ndege yao binafsi na kuiacha ardhi ya
china.
Ndani ya ndege kijana yule mwenye asili ya kiafrika au
unaweza kumuita mmarekani mweusi, alikuwa kafungwa kwenye cage maalumu yenye
nondo imara ili kutompa moyo wala mawazo kama anaweza kujinasua kwenye mikono
ya maagent wale. Taratiibu kijana yule akiwa ndani ya cage ambayo mara nyingi
hutumika kuhifadhia au kubebea wanyama kama, chui,simba na wengineo.
Fahamu zilimrejea na kuanza kuona nuru iliyohafifu kwenye
macho yake yaliyovimba kwa damu kuvilia ndani yake.
Alitikisa kichwa kulia na kushoto huku akilazimisha kufumbua
macho yake ili ajue yupo wapi.... Lakini ilishindikana kutokana na maumivu
kumzidi na kujikuta tena anapoteza fahamu akiwa ndani ya cage, baada ya safari
ndefu...... Hatimae ndege binafsi yenye nembo ya shirika la kijasusi la C.I.A.
Iliweza kuwasili nnje ya jengo kubwa la shirika hilo ambapo baada tu. Yakutua
juu ya ardhi, maaskari waliizunguka ndege hiyo wakiwa wameshika mitutu
iliyotayari kwa lolote lile. Kitanda maalumu cha kubebea wagonjwa. Alimaarufu
kama machela, kililetwa na mtuhumiwa akalazwa juu yake ili kumuwahisha kwanza
hospital kwaajili ya kuokoa maisha yake. Maana hali ya kiafya kwa upande wake
haikuwa nzuri sana kutokana na kupigwa sana.
Matibabu ya awali yalianza huku wauguzi wakipewa tahadhari
juu ya uzima wa kijana yule aliyeonekana ni wamuhimu sana kwenye mikono ya
maafisa wale wa C.I.A.
Taarifa za kijana yule kukamatwa nchini china na kurudishwa
kwenye nchi yake ya marekani. Ziliweza kuwafikia kikundi kimoja hatari sana
kilichokuwa kinamtafuta kijana huyo kwa udi na uvumba.
Kikundi cha kigaidi cha the brothers kinachomilikiwa na
mwanamama mmoja tajiri sana, kilikuwa kinamtafuta kijana huyo kwasababu zao
binafsi ambazo wanazijua wao na kijana yule.
Madam's Aretha Franklin ndio mmiliki wa kundi la the
brother's, kundi lenye kuhusika na wizi na unyang'anyi wa vito vya thamani.
''Vijana. Nadhani taarifa juu ya aliyekuwa ndugu yetu ila
kwasasa ni adui namba moja kwetu. Juu ya kukamatwa kwake zimewafikia... Huu
ndio mda wa kumrejesha nyumbani ili aje kuhumiwa huku maana tulishakula kiapo
kwamba tutazikwa sehemu moja, anatakiwa apatikane akiwa hai maana kuna nyaraka
muhimu sana anazo na zinatakiwa na boss. Hivyo jiandaeni ili jioni twende
tukamchukue kwenye hospital ya ST.MARCIA HOSPITAL.''. Miongoni mwa mwanachama
wa the brother's aliongea akiwa juu ya jukwaa kuwaambia vijana au wanajeshi wa
the brother's waliokuwa wamesimama kwa kupanga mstari kama wapo kwenye gwaride
wakimsikiliza kamanda wao.
Baada ya kutangaziwa taarifa ile. Kila kijana wa kundi la
the brothers alijiandaa na kujiweka sawa kwaajili ya kazi moja tu. Iliyopo
mbele yao ya kumkamata mwanakikundi mwenzao aliyeasi na kujitafutia uhuru wake,
''Nadhani hii ndio nafasi ya kipekee ya mimi kuonesha ubora
wangu, ALEXIS huu ndio mda wako wa kufa maana unajiona bora kushinda Mimi.''.
Kijana aliyetambulika kwa jina la LUCAS. Aliongea mwenyewe akiwa kwenye chumba
chake cha kubadirishia mavazi na kuchana
picha yake aliyopiga enzii hizo wakiwa watoto na ALEXIS.
Mdaa ulipofika. Vijana wapatao ishirini walipanda gari ya
ambulance kama vile wauguzi wanaoenda kumchukua mgonjwa sehemu na kuingia
barabarani kwaajili ya kufika kwenye hospital ya ST.MARCIA HOSPITAL anapotibiwa
kijana mwenzao aliyekimbia kikosi.
''Kumbukeni tunaeenda kumfuata ni zaidi ya hatari, kila
mmoja wetu hapa anautambua uwezo wake wa kutumia silaha pia wa kupigana jinsi
ulivyo.... Umakini unahitajika sana maana ni kiumbe mwenye kila aina ya mbinu
za kujinasua kwenye mikono hatari, inastaajabisha kukamatwa kizembe na maaskari
tena wa shanghai ambao uwezo wao ni robo ya uwezo wake.''. Kiongozi wa msafara
akiwa mbele kwenye kiti cha kushoto, aligeuka nyuma na kuwaangalia vijana wake
waliokuwa wamekaa nyuma kabisa huku wakiwa wamevalia mavazi ya kitabibu.
Aliongea na kurudisha kichwa chake mbele baada ya kuona vijana wake wamemuelewa
kwa kile alichokiongea.
******
Upande wa kijana ALEXIS akiwa hospital. Alikuwa kashamalizwa
kufanyiwa huduma ya kwanza na hapo alipo alikuwa juu ya kitanda akiwa kalazwa
juu huku madripu ya maji na damu yakiwa yamening'inia juu.
Akiwa kwenye usingizi wa kifo kijana ALEXIS... Alitokewa na
watu wawili wakiwa kwenye mavazi meupe huku kwenye nyuso zao wakiwa wamepambwa
kwa tabasamu lenye kusindikizwa kwa michirizi ya machozi kutoka kwenye macho
yao.
''Mama!!! Babaa.''. ALEXIS alijikuta anawaita wale watu
baada ya kuwafahamu ni wakina nani.
''Ni mda wa kuamka na kupambana na maumivu maana maadui wapo
mbele yako kijana wangu. Unatakiwa kuyashinda maumivu ili uipiganie ile haki
iliyopotea kwaajili ya faida za watu, wewe ni shujaa usiyeshindwa na kitu......
Amka uendeleze pale nilipopaacha. Amkaaaa ALEXIS... Amkaaaaaaa!!!!''".
''Babaaaaaaaaaaaa!!!!!!!'' Kijana ALEXIS alijikuta anaamka
kutoka kwenye usingizi wa kifo na kupiga ukunga kumuita baba ake ambaye
alimtokea ndotoni akiwa na mama ake.
Alishtuka na kujaribu kuinyanyua mikono yake ili aweze
kushika kichwa chake alichohisi kinamuuma. Lakini alishindwa kufanya hivyo
baada ya mikono kugoma kunyanyuka yote na kunyanyuka mmoja tu... Alizungusha
shingo yake kulia kwenye mkono ulioshindwa kunyanyuka, alishangaa baada ya
kuona kafungwa pingu kwenye chuma cha kitanda.
Akiwa bado anajiuliza na kukumbuka tukio la mwisho
lilomfanya kuwa pale , mara ghafla kwa mbali alianza kusikia sauti za viatu
vikitembea kuelekea upande kilipo chumba chake. Alijitupa kwenye kitanda na
kukaa kama alivyokuwa mwanzo, hatua zilizokuwa zinasikika kwenye masikio ya
kijana ALEXIS, ziliweza kufika tamati kwenye mlango wa chumba alichohifadhiwa.
Hawakuwa watu wabaya wala wazuri kwa upande wa kijana ALEXIS
maana kwenye maisha yake kila mtu ni mbaya. Walikuwa ni wale maafisa usalama
kutoka kwenye kitengo cha kipelelezi C.I.A wakiwa na mganga mkuu aliyehusika
kumfanyia matibabu ALEXIS, waliingia mpaka ndani ya chumba na kumkuta ALEXIS
akiwa kalala kana kwamba hajapata fahamu kumbe alikuwa kashazinduka mda sana
ila aliamua kufanya vile kuwaaminisha madaktari kwamba yeye bado hajazinduka.
Mganga mkuu alipofika kwenye kitanda alicholala ALEXIS.
Alianza kumpima mapigo yake ya moyo kisha akahamia kuchomoa dripu zilizokuwa
zimeisha na kuita manesi waje
kubadirisha dripu kwa mgonjwa, yote hayo yakiwa yanaendelea ALEXIS alikuwa
anasikilia kinachozungumzwa baina ya mganga mkuu na maafisa wa C.I.A lakini
alishindwa kuona kinachoendelea kutokana na kujifanya kama hana fahamu hivyo
aliishia kusikia sauti tu. Bila kuwaona wahusika wa zile sauti
''Hali ya mgonjwa ndo kama mnavyoiona.. Tumefanikisha kutoa
risasi iliyokuwa kwenye mwili wake baada ya masaa mawili anaweza kupata
fahamu.''. Mganga mkuu alizungumza baada ya kumpima ALEXIS na kuona maendeleo
yake. Aliwaambia maafisa wa C.I.A waliokuwa wamesimama pembeni ya kitanda alicholala
ALEXIS wakimuangalia kijana huyo ambae kwa macho yao na maelezo ya mganga
mkuu.. Waliamini kijana huyo atapata fahamu zake baada ya masaa yapatayo mawili bila kujua kama mwenzao alishapata
fahamu zake muda sio mrefu kabla ya wao kuingia.
Baada ya kukaa kwa kitambo kidogo kwenye chumba alicholazwa
ALEXIS, walitoka nnje ili kupisha manesi walioingia kumbadirisha dripu kijana
huyo. Waifanye kazi yao.
Agent GIBSON alikuwa wa mwisho kutoka kwenye kile chumba,
wakati akiwa anapishana na manesi wawili waliokuwa wanaingia mle na kimkokoteni
chenye dripu na mashuka... Kuna nesi mmoja aliyekuwa anasukuma kile
kimkokoteni, alimtilia mashaka baada ya kukutanisha mboni za macho yao.
Lakini alipotezea na kutoka nnje walipo wenzake wawili.
''Ulinzi unahitajika sana hapa. Nina mashaka na usalama
uliopo hapa, hakikisheni haingii mtu wala kukatiza maeneo haya bila ridhaa
yangu... Nahisi kuna watu wamejipandikiza humu na lengo lao sio zuri.'' Agent
GIBSON aliwaachia maagizo maaskari wake na yeye akashika njia ya kutokea nnje.
Alifika nnje na kuwapa ishara vijana wake wasogee upande alipo.
Vijana walijisogeza kwaajili ya kumsikiliza mkubwa wao ni
kipi anachotaka kuwaambia.
''Nahitaji umakini maeneo haya maana hatupo wenyewe kwenye
hii hospitali... Hakikisha hakuna mtu anaeweza kuingia ndani bila ruksa, mtu
yeyote mnaemwona haeleweki ruksa kumpiga risasi. Natoka mara moja kuna kitu
naenda kufuatilia..''. Agent GIBSON alitoa maagizo kwa vijana wake na kuingia
kwenye gari yake iliyoondoshwa kwa kasi maeneo ya hospital baada ya kuwashwa na
kutii amri ya dereva.
Vijana walijigawa kwa makundi kama walivyopewa maagizo na
mkubwa wao wa kazi... Wakati wao wakiwa wanapeana majukumu ya kulinda, kwenye
ghorofa ya pembeni iliyoumbali wa kilomita zipatazo hamsini. Kuna mtu alikuwa anawaangilia
kwa kutumia kifaa chake alimaarufu kama. Miwani ya shetani ambayo ni darubini
zenye uwezo wa kuangalia kwenye giza nene na mtumiaji akaona vizuri sana kama
aonavyo mchana.
Yule mtu akiwa kasimama juu kabisa ya ghorofa ile yenye rufu
zipatazo ishirini kwenda juu, alipeleka mkono wake wa kulia uliokuwa ndani ya
gropsi iliyokatwa kwenye vidole na kuacha uwazi upande wa vidole huku juu ya
kiganja kukiwa na nembo ya fuvu lenye bunduki zikiwa zimejiweka kwa mtindo wa
x.. Alipeleka juu ya sikio na kubonyeza kitu kilichokuwa ndani ya sikio lake
mfano wa earphone zinazotumikaga mara nyingi kusikilizia mziki kisha akaurudisha mkono wake kwenye miwani ya
shetani...
''Huku nnje naona sio salama kwa kumpitisha... Naona hawa
wapuuzi wa C.I.A wametapakaa kila sehemu... Embu ngoja kwanza naona kuna gari
ya wagonjwa inaingia hapa....... Ooooh shit. MONA LISA fanya haraka kidogo
naona the brothers na wao wameingia hapa na itakuwa ni hatari kama watakukuta
ndani..'' Baada ya kubonyeza kile kitu mfano wa earphone, kijana yule
alizungumza kumwambia mtu aliyemwita kwa jina la MONA LISSA afanye haraka baada
ya kuona gari ya ambulance ikiingia kwenye hospital ile na alipofuta taswira
kwenye darubini yake. Aliwaona na kuwatambua waliokuwa kwenye gari ile ya
kubebea wagonjwa ni wakina nani.
Upande wa ndani kwenye chumba alicholazwa kijana ALEXIS...
Wale manesi wawili walikuwa wanamfanyia mabadirisho ALEXIS lakini mmoja wapo
alipokea simu kutoka mahala, punde tu. Baada ya kupokea simu hiyo, alionekana kuchanganyikiwa
mpaka mwenzake akashangaa.
''The brothers wanakujaa.''. Yule nesi aliyepokea simu bila
shaka huyu ndie MONA LISA yule aliyepigiwa simu na yule kijana wa nnje aliyekaa
juu ya ghorofa iliyo jirani na hospital ya ST.MARICIA HOSPITAL.
Kitendo cha kutamka kwamba the brothers wanakuja...
Kilimfanya hata kijana ALEXIS kushtuka na kunyanyuka kutoka kwenye igizo lake
la kutopata fahamu, lakini alijikuta anarudi tena kwenye kitanda baada ya kitu
chenye ncha kali kikiwa cha baridi kupita kwenye mishipa yake ya mikono huku
baada kitu hicho kupita kwenye mishipa yake ya mikono... Ikafuatiwa na vitu vya
baridi kupenya kwenye mishipa yake ya damu na kuanza kusambaa kwa kasi.
ALEXIS alijaribu kukaza mishipa yake ili kitu alichochomwa
kisiendelee kuingia ndani zaidi ya mwili wake.. Alishindwa kuizuia dawa
iliyokuwa inasafiri kwenye mwili wake kwa kasi kubwa huku kila sehemu ya mwili
ikikosa nguvu baada ya dawa hiyo kupita, alijikuta anaanza kuweweseka kama
mgonjwa mwenye degedege huku mapovu yakimtoka mdomoni.
''Msaada jamani... Anakufaaaaa.''. MONA LISA baada ya
kuona mwenzake kashamchoma sindano
itakayomfanya ALEXIS kulala......
Alipiga kelele ili wale walinzi waliokuwa nnje ya wodi aliyolazwa kijana
ALEXIS waweze kuja ili adhma yao ya kumtoa ALEXIS itimie.
Maafisa wa C.I.A wawili walioachwa kama ulinzi kwenye chumba
alichomo ALEXIS... Waliposikia sauti za nesi akiomba msaada, bila kupoteza mda
waliingia ndani kichwa kichwa.. C.I.A wa mbele aliyetangulia, alikutana na teke
la shingo lilompeleka chini na kupoteza fahamu kwani mpigaji wa teke lile
alikuwa mtaalamu na anazifahamu vyema sehemu ambazo akikupiga lazima upoteze
fahamu... Yule mwingine nae katika harakati za kushtuka ni kitu gani
kilichomfanya mwenzake kuanguka kama mzigo, alijikuta na yeye anapigwa na
vidole laini katikati ya mfereji wa uti wa mgongo na kupoteza nae fahamu.
Baada ya mwili wake kuanguka, nyuma alionekana yule nesi
aliyekuja na MONA LISA akiwa kanyoosha mkono wake wa kulia huku mbele akiwa
kanyoosha vidole viwili kuonesha ndie aliyefanya tukio lile kwenye mwili wa
afisa yule aliyekuwa kageuka upande alipo MONA LISA aliyempiga teke la shingo
yule afisa mwingine aliyekuwa wa kwanza kuingia ndani kutaka kujua kunanii
lakini alizimishwa baada ya MONA LISA kuzunguka
kwa nyuma na kuachia teke la
nyuma lilompata vyema yule afisa huku kisigino cha kiatu alichovaa kikifanya
kazi ya kugusa sehemu yenye mshipa mkubwa wa fahamu.
Waliingiza ndani ya chumba wale maafisa na kufunga mlango
ili isijulikane kama kuna tukio limetokea, walimchukua kijana ALEXIS aliyekuwa
katepweta kutokana na kuchomwa na sindano yenye dawa za usingizi ndani yake...
Nesi yule aliyekuja na MONA LISA alimbeba kijana ALEXIS huku MONA LISA yeye
akiwa nyuma kwaajili ya ulinzi.
Kijana ALEXIS akiwa kwenye usingizi wa nusu kaputi, alianza
kukumbuka mambo kadhaa yaliyotokea nyuma.
‘’Wewe ni nani.?’’
‘’Mimi ni muaaji.’’
‘’Wewe ni nani.?’’
‘’Mimi ni muuaji’’
‘’Sheria na kanuni za muuaji ni ninii.?’’
‘’Kuua bila kuacha ushahidi,’’.
‘’Sheria na kanuni za muuaji ni nini.?''
’Kuua bila kuacha ushahidi,’’
‘’Msaliti yoyote atakejitokeza, adhabu yake nini.?’’
‘’Kuuwawa’’
‘’Sijasikia. Msaliti yoyote atakaejitokeza adhabu yake ni
nini.?’’
‘’Kuuwawa’’
‘’Sisi ni..?’’
‘’Familia moja’’
‘’Sisi ni..?’’
‘’Familia moja’’
‘’Kutengana kwetu..?’’
‘’Mwiko mpaka tunakufa’’
‘’Kila mmoja aweke akilini, hakuna uhuru kwenye hii dunia
ila uhuru uliopo kwenye dunia ya sasa ni
kuua ili uwe huru na maumivu kwenu mwiko, inatakiwa maumivu
yawaogope na sio nyinyi myaogope
na kudhihirisha kwamba sisi ni familia moja, kila mmoja wetu
atapita hapa na kuwekwa tatoo mbili
kiashirio cha sisi ni ndugu na ndugu milele hawatengani na
ikitokea mmoja wetu kajitenga na sisi.
Basi hukumu yake kifo, kwenye familia yetu hatuhitaji mtu
mlegevu. Familia yetu hakuna mtu
anaeshindwa’’
Yalikuwa ni moja ya matukio mengi anayoyakumbuka kijana
ALEXIS akiwa kabebwa juu ya mgongo... Alizidi kukumbuka mambo kadha wa kadha
yaliyopita...
''Nakufundisha hivi kwaajili ya maisha yako ya baadae na
ulinzi kwenye maisha yako... Najua kwasasa utachukulia kama nakutesa ila baadae utajua umuhimu wa haya mazoezi. Haya
ingiza mikono yako kwenye huo mchanga na upige vidole ndani yake huku
ukivizungusha kama unakoroga maji au kukanda ngano...''
''Lakini mwalimu kwanini mazoezi haya unanipa mimi tu.
Wenzangu huwapii...?''
''Utajua mbele
utakapokua mtu mzima na ukajua maana ya neno Uhuru.''.
Ni matukio ya nyuma kipindi angali mdogo.... Aliyakumbuka yote
akiwa kwenye usingizi mzito...
MONA LISA akiwa na
mwenzie wakiwa wamembeba kijana ALEXIS... Walipita njia za chini kwenye maji na
uchafu wote unaotupwa na hospital ile maana juu kulikuwa hakupitiki jinsi
ulinzi ulivyokuwa mkubwa na kikundi cha the brothers kilikuwa kimewasili nnje
ya hospital kikitaka kuingia ndani kwa kigezo cha kumleta mgonjwa.
''DENNY tupo underground way... Tukukute kwenye mataa.''.
MONA LISA aliongea kupitia simu maalumu iliyokuwa imepita kwenye sikio lake la
kulia na kuonekana kama earphone
''Usijali... Dakika kumi nitakuwa eneo husika.'' DENNY ambae
ndio yule kijana aliyopo juu ya ghorofa lililopo karibu na hospital ya ST.
MARCIA HOSPITAL.... Alizungumza hivyo baada ya kupokea simu kutoka kwa MONA
LISA...aliinama chini na kuirudisha silaha yake yenye uwezo wa kulenga masafa
marefu ndani ya begi lake...
Baada ya kufanya hivyo, alinyoosha mkono wake na kubofya
namba kadhaa kwenye saa aliyokuwa ameivaa mkononi, kuanzia mwanzo wa kiganja
mpaka yalipo makutano ya mkono na kuonekana kama mtu aliyefungwa bandeji au
kitambaa... Baada ya kubofya zile namba kwenye kioo cha saa, alivaa begi lake
mgongoni na kuliweka sawa kisha akageuka upande wa pili wa lile ghorofa na
kuanza kukimbia kuelekea ukingoni mwa lile ghorofa, alikimbia kwa spidi kama
yupo ardhini na alipofika kwenye engo za mwisho wa lile ghorofa... Aliibana
miguu yake na kudunda kwenye ncha za kuta na kujirusha juu kama samaki
aingiavyo kwenye maji, akiwa juu alijibetua na kutanguliza kichwa chini huku
miguu akiiacha juu tena ikiwa kaibana vilevile kama alivyoruka.
Lau kama ungebahatika kumuona jinsi alivyokuwa anashuka
kutoka kule juu ya ghorofa, ungeweza kusema na kumfananisha na spider man au
super man kama sio batman jinsi alivyokuwa anashuka kwa spidi kama ya roketi
huku akiwa hana parachuti lenye uwezo wa kumsaidia asije kutua chini vibaya.
Macho ya DENNY mara kwa mara yalikuwa yanaangalia saa
iliyokuwa inatoa sauti kama za alarm ikiwa inalia, alifika mpaka katikati ya
ghorofa na kubakiza rufu kadhaa tu. Afike chini,, aliangalia tena saa yake na
kutabasamu kisha akajibetua kwa kichwa chake kuangalia juu na ule mkono wenye
saa akiunyoosha juu.... Kuna kitu kilitoka kwa kasi kwenye vijitundu fulani
vilivyokuwa pembeni ya saa yake upande wa mbele na kwenda juu kwa kasi kama risasi
itokapo kwenye bunduki, kile kitu kilikuja kufika tamati baada ya kutoboa pembe
ya ukuta wa ile ghorofa na kutokea upande wa juu kabisa wa ile ghorofa.
Kilipofika juu kilijitanua na kuweka pembe tatu na kunata kwenye ukuta.
Mkono wa DENNY uliokuwa na ile saa, ulikaza na kufanya DENNY
ajivute chini kwa nguvu hali iliyofanya kutua kwa ustadi wa hali ya juu... Mguu
wake wa kulia ulipinda kidogo na kupiga goti huku ule wa kushoto ukiwa kama
kisaidizi cha mkono wa kushoto uliokuwa juu yake na ule wa kulia ulibaki ukiwa
umenyooka juu kutokana na ile kamba.
Alikaa style kama ya watu wa marathon wakiwa wanataka
kukimbia, alinyanyuka na kubonyeza batani iliyokuwa chini ya saa na ile kamba
kule juu ikajifungua na kurudi kwa kasi na kuingia ndani ya vitundu vilivyokuwa
kwenye saa ile... Alitabasamu na kutoka mbio kuelekea upande wa kushoto
kulipokuwa na njia za watu wa miguu na baiskeli, alikimbia mpaka akaja kutokea
sehemu moja kulipokuwa na gari aina ya hiace yenye nembo za mikate kuonesha ni
gari inayohusika na usambazaji wa mikate... Aliingia kwenye gari hiyo na kuitoa
kwa spidi kiasi cha tairi kulalama kwenye rami na kuacha moshi tu.
Upande wa pili kwenye njia za chini ambapo kulikuwepo na
watu watatu, MONA LISA na yule nesi ambae mpaka sasa hajatambulika jina ni nani
wakiwa na kijana ALEXIS... Walizidi kukata kona za Chemba zile za maji machafu
na kufanikiwa kufika sehemu moja walipoona kuna mwangaza unapenya kutoka juu
kuingia mle ndani, moja kwa moja bila kuchelewa walianza kusogezana sehemu ile
kwani ndio walikuwa wanaitafuta kwaajili ya kuwatoa nnje, MONA LISA alikuwa
mbele akiwa na toji huku nyuma yule nesi akija akiwa na ALEXIS.
MONA LISA alipofika pale , aliangalia juu na kuona mfuniko
wa chemba kuonesha wakiutoa mfuniko huo watakuwa wamepata njia ya kutokea
juu... Haraka aliibumba toji yake mdomoni na kuanza kupanda juu kutumia ngazi
zilizowekwa kwenye kila chemba, alipanda kwa kasi na kufanikiwa kufika juu
kiasi cha kichwa chake kugusa nondo za mfuniko.
Alitumia mikono yake kupitisha kwenye matundu ya mfuniko na
kufanikiwa kuusogeza pembeni huku yeye mwenyewe akijivuta juu kwa tahadhari
kubwa maana aliibukia kwenye mataa ya magari na ilikuwa ni katikati ya
barabara, alipofika juu aliangaza huku na kule kabla ya kuyatuliza macho yake
kwenye gari moja iliyokuwa inakuja upande alipo kwa kasi, alijikuta anaachia
tabasamu baada ya kujua ni nani anaekuja na ile gari. Hakuwa mwingine zaidi ya
kijana DENNY ndie aliyekuwa anakuja upande alipo MONA LISA na alipofika karibu
yake, alifunga breaki za ghafla na kufanya tairi kuburuzika kwenye rami.
Gari ilikuja kusimama kwenye miguu ya MONA LISA yaani
ilibakia kidogo tu kama angeachia breaki angemgonga, alishuka akiwa na kamba na
kuiviringa kwenye mkono wake.
Alifika mpaka pale kwenye ile chemba na kuirusha ile kamba
ndani ambapo yule nesi aliipokea na kumfunga kiunoni ALEXIS na kuivuta ishara
ya kuwataka walioko juu waivute. Kamba ilianza kuvutwa kwa watu wawili
kushirikiana huku wakipata msaada mwingine kutoka ndani kwa yule nesi Ambae nae
alikuwa anapanda juu.... Walifanikiwa kumtoa ALEXIS na yule nesi akatoka na
kuingia ndani ya gari iliyoondoka kwa kasi na kutokomea barabarani huku nyuma
wakiacha ushahidi wa moshi mdogo uliotokana na tairi kuburuzika kwenye rami.
Upande wa pili kwenye hospitali ya ST.MARCIA HOSPITAL... Hali
ya maaskari walioachwa kama ulinzi haikuwa nzuri baada ya kukutana na dhahama
kutoka kwa kundi la the brothers waloingia kwenye hospitali hiyo kwania ya
kumchukua kijana ALEXIS lakini wakakuta tayari ameshachukuliwa.... Kilichofuata
ni kuua kila mtu atakae wazuia na kujifanya anajua kuliko wao.
Miili iliyokuwa haina uhai ya maafisa wanaotoka kwenye
kitengo cha kipelelezi cha C.I.A ilikuwa imezagaa kila kona ya hospitali ile
ikiwa haina uhai tena huku wahusika waliofanya hivyo wakiwa wameshaondoka baada
ya kutimizia mauaji kwa maafisa hao.
Agent GIBSON alihisi kuchanganyikiwa baada ya kuona hali ile
kwa maafisa wake, breaki ya kwanza ilikuwa ni kwenye chumba alichomuacha kijana
ALEXIS akiwa kalazwa.... Alitahamaki baada ya kukuta kitanda kikiwa kitupu huku
pingu zikiwa zinaning’inia upande mmoja.
Aliangaza kwenye kila kona ya kile chumba na kubahatika
kuona miili ya maafisa wake wawili ikiwa imelala huku ikiwa na matundu ya
risasi kila sehemu ya mwili... Aliuma meno kwa hasira na kutoka nnje ambapo waandishi
wa habari walikuwa wameshajazana nnje kutaka kufahamu kipi kilichotokea.
*********
Wiki moja iliweza kukatika pasina taarifa zozote za
kupatikana au kuonekana kwa kijana ALEXIS.
Nnje ya ofisi moja iliyopo kwenye mitaa ya jiji la newYork,
kulionekana kuna gari moja ndogo yenye kutumika sana kwenye mbio za masafa
marefu ikiwa imepaki nnje ya ofisi hizo zenye kushughulika na utoaji huduma za
mikate na vyakula mbalimbali.... Tunamuona msichana mmoja akiwa counte
akihitaji huduma na baada ya dakika kadhaa kupita, akatoka nnje mkononi akiwa
na furushi la mikate..... Alienda kufungua buti ya gari na akahifadhi vitu
Vyake huko kisha yeye mwenyewe akaingia ndani ya gari hiyo na kutekenya funguo
ambapo bila ubishi engine ilitii amri na kuwaka.
Alitoa gari yake sehemu aliyopaki na kuingia barabara kubwa
ya jiji la NewYork,wakati akimalizia kuingia kwenye barabara kubwa... Kuna gari
nayo ilikuwa inamfuatilia kwa nyuma, ndani ya gari ile ya nyuma kulikuwa na
maafisa kutoka kwenye kitengo cha C.I.A .
Msichana akiwa hana hili wala lile, yeye alizidi kukanyaga
mafuta na kubadirisha gia bila kufahamu kama nyuma kuna watu wanamfuatilia....
maafisa wale walikuwa kwenye mwendo mdogo lakini hawakutaka kumpoteza mlengwa
wao aliyekuwa anazidi kukata mitaa ya jiji hilo.
‘’Kuna watu wanakufatilia nyuma... Kuwa makini sana.’’ .
Msichana yule akiwa kwenye gari yake yenye kioo kinachoonesha ramani ya jiji na
dunia kiujumla, alisikia sauti ikimweleza kipi kilichopo nyuma yake na yeye kwa
kuzibitisha, aligeuka nyuma na kuwaona maafisa wa C.I.A wakiwa kwenye mwendo wa
wastani.
Alitabasamu na kuvaa miwani kisha akajifunga mkanda vizuri
na kubadirisha gia kitendo kilichofanya gari yake kuongezeka mwendo na kuwaacha
maafisa wale nyuma kwa umbali kidogo ambapo nao baada ya kuona mlengwa wao
kaongeza mwendo ilibidi nao waongeze..... Patashika nguo kuchanika ikaanza
kwenye barabara ya NewYork baina ya yule msichana na maafisa wale. Mkimbizano
ulikuwa mkubwa lakini maafisa wale walikuwa hawaligusi wala kulisogelea gari la
binti yule liliokuwa linatembea kwa spidi kubwa, walifika sehemu ya mataa
ambapo magari yalisimamishwa na kuruhusiwa wavuka kwa miguu wapite... Yule
msichana alitabasamu na kuongeza mwendo kitu ambacho maafisa C.I.A nao
waliongeza mwendo bila kujua mbele kuna nini.
Kuna mwanamama mmoja alikuwa ndio wa mwisho kuvuka akiwa na
mwanae mchanga aliyemweka kwenye kigari kidogo chenye matairi nane, ile anafika
katikati ya barabara na yule msichana alikuwa ndo anafika na gari yake....
Binti yule alifanya kukanyaga breaki za nyuma huku mguu wake mwingine ukiwa
bado upo kwenye mafuta, gari yake iliseleleka kutumia tairi za nyuma na
kumzunguka yule mama aliyeishiwa nguvu na kubaki akiwa kasimama wima..
Alimzunguka karibia mara tatu kabla ya kuachia breaki na
kumpita kama upepo... Mama yule pamoja na mwanae waliwekwa katikati ya O
iliyochorwa na msichana yule huku moshi ukiwa umechukua nafasi... Maafisa C.I.A
walipofika pale walifunga breaki za ghafla ilihali gari yao ipo kwenye mwendo
kasi, walipinduka na kwenda kuangukia kwenye gari moja iliyokuwa imesimama
kusubiri wapita na miguu wamalize kupita.
Yule msichana aliachia tabasamu baada ya kuona tukio lile
kupitia kioo chake cha mbele.... Alikanyaga mafuta na kutokomea barabarani
Nnje ya jiji la New York city, tunaliona lile gari la yule msichana
likiingia kwenye moja ya mashamba ya mahindi huku ndani yake akionekana yule
msichana aliyekuwa anakimbizana na maafisa wa kipelelezi kutoka kwenye kitengo
cha C.I.A...... Alionekana ni mwenyeji kwenye mashamba yale maana alikuwa
anapita kwenye njia ambazo kwa mtu ambae hajui eneo lile anaweza kupata ajali.
Alitembea kwa mwendo kasi mpaka alipokuja kutokea kwenye
ukuta mrefu uliokuwa umetenganisha lile shamba na upande wa pili ambapo kuna
bahari... Alisimama kwa dakika kumi kabla ya kuruhusu gari yake kutembea
kuelekea sehemu moja iliyokuwa inajifungua kwenye ule ukuta, ulikuwa ni mlango
wa kuingia ndani au upande wa pili wa ule ukuta ambapo kuna bahari.. Aliingiza
gari ndani na ule mlango ukajifunga kama mwanzo na kufanya kutoonekana kama
kuna mlango wa siri maeneo yale, ndani ya ukuta ule.... Kulikuwa na barabara
kama nyingine ila isipokuwa barabara iliyokuwepo mle ndani ilikuwa
imetengenezwa kwa vitu maalumu vyenye uwezo wa kuzuia silaha ya aina yeyote
ile,
Binti yule alizidi kukanyaga mafuta mpaka alipofika kwenye
geti kubwa la kuingia ndani zaidi, alisimama na baada ya dakika tano akaendelea
kukanyaga mafuta na kuingia ndani zaidi ambapo kulikuwa na mji mdogo huku
kukionekana kuna kila aina ya dhana za jeshi.
Alisimamisha gari yake sehemu yenye magari kama yake na
kushuka...
‘’Naona umeivaa kwenye udereva.’’. Kuna mtu alikuwa anashuka
kutoka kwenye ndege moja ya kivita iliyokuwa ndio inapooza engine kuonesha
ilikuwa inafanya kazi muda sio mrefu.. Alizungumza vile na kusogea mpaka sehemu
alipo yule binti ambae anafanana na yule nesi aliyekuwa na MONA LISA kule
hospitalini walipoenda kumchukua kijana ALEXIS.
‘’Kawaida sana.’’. Yule binti alijibu na kutabasamu huku
akitoa vitu vyake alivyotoka navyo mjini.
‘’Naweza kukusaidia bibiye..?’’. Yule kijana aliyeshuka
kwenye ndege aina ya chopa, aliuliza swali kwa yule binti na kuweka mkono wake
wa kushoto chini ya buti huku ule wa kulia akishikilia mfuniko wa buti uliokuwa
juu.
‘’Ningehitaji msaada ningekwambia... Nipishe.’’. Yule binti
alijibu kwa sauti kidogo na kufunga buti kwa nguvu bila kujali kama yule kijana
kaweka mkono chini.
‘’Aaaaauuuuu!!! Shit..’’. Yule kijana alitoa mkono wake
baada ya kukandamizwa na buti.
Yule binti hakujali kama kamuumiza yule kijana... Alishika
njia mpaka kwenye rifti na kuiruhusu kupanda juu huku chini akimuacha kijana wa
watu akiugulia maumivu ya kidole.
‘’MIKEL... Pole sana ila usikate tamaa ipo siku CHRISTINA
atakuelewa na kuzikubali hisia zako, usife moyo.’’. Kuna kijana mwingine
alikuja na kumshika bega MIKEL aliyekuwa anamuangalia yule binti ambae ni yule
nesi aliyekuwepo kule hospitalini kipindi kile walichoenda kumtorosha kijana
ALEXIS.. Kumbe anaitwa CHRISTINA.
‘’Aaah!!! Sidhani kama ipo siku huyu binti atakuja kuzielewa
hisia zangu.. Ila poa twende ndani maana nasikia kuna vitu vimeharibika..’’.
MIKEL aliongea na kuongoza njia kwenda ndani zaidi ya kambi hiyo ambapo alidai
kuna vitu vimeharibika.
Ndani ya chumba kimoja hivi kwenye kambi hiyo, kulionekana
madaktari wakipishana huku mbele yao kukiwa na mwili wa mtu ukiwa umelala
kwenye incubator ambacho ni chombo cha kisayansi chenye kuhusika na kuhifadhia
watoto walioazaliwa kabla ya siku zao au mara nyingine hutumika kutengenezea
watoto wanaotokana na mbegu za mwanaume kuchukuliwa na za mwanamke kisha
zinachanganywa sehemu moja na kutengenezwa mtoto.
Nnje ya chumba kile kilichokuwa na vioo tu. Alionekana mtu
mmoja wa makamo akiwa kavaa suti huku pembeni yake kukiwa na watu wawili.. MONA
LISA na kijana DENNY, walikuwa makini sana kuangalia kile kinachoendelea ndani
ya maabara juu ya mwili wa kijana ALEXIS uliokuwa unafanyiwa vitu fulani vya
kutoa kumbukumbu za kijana huyo.
Madaktari waliokuwepo mle ndani baada ya kumaliza kumpachika
mirija fula kwenye mwili wa kijana ALEXIS... Walitoa alama ya dole gumba nnje
ya chumba kile upande wa kulia ambapo kulikuwa na makompyuta mengi yakiwa
yanaonesha mfumo mzima wa mwili wa kijana ALEXIS na mapigo yake ya moyo...
Madaktari waliokuwepo kwenye kompyuta zile baada ya kuona wenzao wa ndani
wamewapa taarifa, walianza kuchezea keyboard za computer zao huku wakiwa makini
kwa kile wakitendacho.
Walizidi kupoteza kumbukumbu za kijana yule mwenye asili ya
kiafrika.. Kadri muda ulivyokuwa unakwenda na ndio mwili wa ALEXIS ulivyoanza
kujitingisha kama anapinga kitu fulani .
Walizidi kuzipoteza kumbukumbu za kijana yule huku mhusika
mwenyewe akionekana kupingana na kitu fulani kisitoke kwenye mwili
wake...Walifanikiwa kiasi fulani lakini kuna kumbukumbu zilikataa kufutika
kwenye kichwa cha kijana ALEXIS.
‘’Kuna matukio kadhaa yamekataa kufutika kwenye ubongo wake
na tukilazimisha tunaweza kumpotezea uhai wake...’’. Kuna daktari aliongea
kuwaambia wakina MONA LISA na yule mtu aliyeonekana ni mkubwa wa kambi nzima.
Yule mtu alitoa ishara ya kuwataka waache maana alishajua ni
kumbukumbu gani hizo zilizokataa kufutika...
‘’Hapo inatosha najua kumbukumbu zilizokuwepo kwenye ubongo
wake zitazidisha chachu kwenye kazi... Mpelekeni chumbani tusubiri apate fahamu
zake..’’ Yule mtu alizungumza hivyo na kunyanyuka kutoka pale alipokaa na
kwenda nnje.
Walifanya kama walivyoambiwa, walimtoa kijana ALEXIS
aliyekuwa kalegea kutokana na shughuli aliyokuwa anafanyiwa na kumpeleka kwenye
chumba kimoja chenye rangi nyeupe kote mpaka kitanda... Walipofika walimlaza na
kutoka nnje.
Masaa yalizidi kukatika pasipo kijana ALEXIS kupata fahamu
zake.... Chumba alicholazwa kijana huyo, kilikuwa kimewekwa camera kila pembe
za ukuta lakini haikuwa kazi rahisi kwa mtu kugundua kama mle ndani kuna
camera.... Kutokana na rangi ya chumba kuwa nyeupe na camera zenyewe zilifungwa
kitaalamu.
ALEXIS akiwa kwenye usingizi wa madawa na kunyong’onyeshwa
ubongo wake baada ya kupotezewa kumbukumbu zake... Kuna ndoto aliweza kuota
akiwa pale kitandani.
Aliota yupo katikati ya pori lilofungamana huku yeye akiwa
katikati ya pori hilo...Mwili wake ulikuwa umetapakaa damu kuonesha kuna tukio
amelifanya nyuma, akiwa pale akijishangaa jinsi alivyo.. Ghafla kuna kitu
kilikuja na kumkumba pale alipo, alihangaika kujitoa kwenye mikono au himaya ya
kitu kikichomkumba, lakini ilimuwia ugumu kutokana na hali yake kuwa mbaya na
kukubali kuchanwa na kucha za yule kiumbe....
Kiumbe yule alikuwa ni aina mpya ya chui wapatikanao kwenye
nchi ya india.. Jinsi walivyo na wanavyoonekana hawakuwa na utofauti na wale
chui wa bengali lakini aina ya chui huyu ni wepesi na weredi kwenye kufanya
maamuzi dhidi ya adui.... ALEXIS alitupwa mbali na kujibamiza kwenye shina la
mti na kuanguka chini kama mzigo, akiwa pale chini akijaribu kujizoazoa...
Pembeni yake aliweza kuona kuna mtu akiwa kasimama akimuangalia kwa masikitiko
makubwa kuonesha hajapendezwa na tukio lile. ALEXIS alijaribu kunyanyua mkono
wake kutaka msaada kutoka kwa mtu yule, lakini alishindwa na kujikuta akianguka
chini na kupoteza fahamu.
‘’Mheshimiwa... Ameamka!!’’. Kwenye chumba kimoja
kinachotumika kuongozea camera.. Mlinzi aliyekuwa anaangalia camera za kambi
hiyo hususani ni camera zilizopo kwenye chumba alicholala kijana ALEXIS,
alizungumza hivyo kuwaambia watu waliokuwepo nyuma wakingojea kijana ALEXIS
apate fahamu zake.....
Baada ya taarifa ile, kuna mtu mmoja aliyeonekana ndio
kioongozi wa kambi ile... Alitoka sehemu alipokuwa ameketi na kwenda kwenye
luninga iliyokuwa inamuonesha kijana ALEXIS akiwa kakaa kwenye kitanda
akionekana kufikiri jambo.
‘’Hatimae amezinduka... Mpelekeeni nguo, nadhani
anajishangaa kujikuta hapo na hakumbuki tukio lolote hapo alipo... Huu ni muda
wetu wa kuifanya hii kazi juu ya ushenzi unaoendelea kwenye hii dunia na mtu
mwenye uwezo wa kumaliza mambo yote hayo ni huyu kijana..’’. Mtu yule aliongea
hayo na kuonesha furaha aliyokuwa nayo baada ya kijana ALEXIS kuzinduka.
Walitoka vijana wapatao watatu na kwenda kwenye chumba
alichopo ALEXIS.
*****
ALEXIS baada ya kuota ile ndoto ambayo kwa upande wake
ilikuwa yakutisha na wala hakuelewa nini maana ya ile ndoto.. Alizinduka na
kujikuta akiwa kwenye mazingira ambayo hakuyaelewa...
Alijaribu kuangaza macho yake kwenye kile chumba kama
anaweza kukijua. Lakini hakuweza kukumbuka kitu hata alipojaribu kushika kichwa
chake na kufumba macho kujaribu kukumbuka, hakuweza kukumbuka kitu zaidi ya
kusikia maumivu kwenye kichwa chake, alifunua shuka aliyokuwa kafunikwa na
kujishusha kutoka kwenye kile kitanda na kujaribu kukichunguza kile chumba....
Alikuwa na nguo ya ndani tuu. Alitembea huku na kule akijaribu kutafuta mlango
wa kutokea nnje lakini hakufanikiwa kuona dalili zozote za kumjulisha kama mle
ndani kuna mlango, ilibidi arudi na kukaa kwenye kitanda.. Akiwa anataka kukaa,
mara alianza kuhisi kuna sehemu zinafunguka kwenye ukuta... Ilibidi ageuke na
kukaa tayari kwa kukabiliana na kitu chochote kile ambacho ni kibaya kwa upande
wake, aliona mlango ukiwa unafunguka wenyewe na baada ya kumalizika....
Waliingia vijana watatu ambao kwenye macho yake walikuwa ni wageni, vijana wale
baada ya kuingia mle ndani... Wawili walikaa nyuma na mmoja aliyekuwa kabeba
nguo kwenye mikono yake, akaenda mbele ya ALEXIS na kumnyooshea mikono mbele
ikiwa na nguo juu yake ishara ya kumtaka azipokeee..
ALEXIS hakuelewa ni mambo gani yanajitokeza kwenye maisha
yake maana hakuwa na kumbukumbu kama watu waliopo mbele yake alishawahi kuwaona
kabla... Ilibidi azipokee zile nguo lakini kwa kusitasita...
‘’Karibu sana nyumbani.’’. Yule kijana ambae ni DENNY baada
ya kumpatia nguo ALEXIS... Alimkaribisha na kutabasamu kitu ambacho kijana
ALEXIS hakukielewa... Alilazimisha tabasamu usoni kuashiria kakubaliana na yale
aliyozungumza DENNY.
DENNY baada ya kuona vile... Alitoka nnje na wale wengine
wawili na kumuacha ALEXIS mwenyewe..
‘’Mbona sielewi mambo yanayotokea kwenye maisha yangu...
Mara ya mwisho nilikuwa wapiiiiiii!!!! Aaaaah. Hata sikumbuki alafu nimejikuta
nipo hapa na hawa watu wanaonesha tabasamu usoni mwao ilihali mimi siwatambui,
hii sinema gani sasa.’’. Alijiuluza maswali bila kupata majibu sahihi... Mwisho
akaamua kuvaa yale mavazi aliyoletewa na wale watu ambao kwake walikuwa ni
wageni.
‘’N.I.S.A.... Hii inamaana gani.?’’. Baada ya kuvaa na kuona
maneno yaliyoandikwa upande wa kushoto wa shati alilovaa, alijaribu kuyasoma na
kujiuliza nini maana ya neno N.I.S.A lakini hakupata jibu sahihi.
‘’Karibu sana nyumbani... DAMIAN, ni muda umepita
hatujaonana... Naitwa General JEFF ukiniita the ghost utakuwa hujakosea,
aaaah!!! Najua unajaribu kujiuliza kwanini upo hapa? Twende kwanza
nikakutembeze nnje ya hii kambi na nitakujulisha kidogo kidogo maana najua ni
muda mrefu sana hujafika hapa na ulishasahau mazingira ya hapa..’’. Akiwa
anajiuliza maana ya neno aliloliona kwenye t-shirt aliyoivaa... Ghafla kuna mtu
aliingia kwenye chumba alichokuwepo na kujitambulisha huku akimuomba watoke
nnje ili akamkumbushe vitu kadhaa ambavyo atakuwa amevisahamu na kumpachika
jina jipya badala ya lile la mwanzo.
‘’DAMIAN? Inamaana mimi naitwa DAMIAN.?’’. ALEXIS aliuliza
swali na kujishangaa kisha akamuangalia mtu aliyesimama mbele yake.
‘’Ndio.. Inamaana hata jina lako mwenyewe umelisahau!!
Aaaaaah. DAMIAN.. Embu acha masikhara yako najua lile tukio la kurushwa na bomu
ndio limekufanya usahau hata jina lako... Inamaana hata mimi hunikumbuki..’’.
General JEFF The Ghost alijibu na kumuuliza huku akimshangaa kijana ALEXIS kwa
kulisahau hata jina lake.
‘’Aaaanhaaa.!!! Ndomaana kichwa changu kinaniumaa aaah..
Basi kumbukumbu zimenitoka kidogo nadhani zitarejea polepole...’’. ALEXIS baada
ya kupewa maneno matamu na kuaminishwa na General JEFF The Ghost, alijikuta
anakubali na kuonesha kweli yeye ni DAMIAN ila alipitiwa tu.
Waliongea mengi kiasi cha kuzoeana kwa muda wa lisaa limoja
na dakika zake.. ALEXIS ambae kwasasa anatambulika kama DAMIAN... Alimzoea
General JEFF kama walishawahi kukutana kabla kumbe ni kutokana na kumbukumbu zake
kufutwa na kubaki na kumbukumbu chache ambazo nazo zitakuwa zinakuja kwenye
kichwa chake na kupotea..
Maisha mapya yalianza kwa kijana ALEXIS ambae kwenye ile
kambi ya siri anajulikana kama Leader DAMIAN.. Kambi ile iliyokuwa chini ya
General JEFF THE GHOST.. Ambae alishawahi kufanya mambo makubwa kwenye nchi ya
marekani na kupewa cheo cha the one and only kabla ya kupewa uongozi wa General
ambapo kwenye cheo hicho hakukaa sana kutokana na kuwa na maadui wengi sana...
Hivyo alitengeneza kifo cha bandia na kuwaaminisha watu kuwa amekufa lakini
ukweli aliujua yeye na kuamua kuanzisha kitengo chake mwenyewe kilichokuwa
kinatambulika na raisi wa nchi tu. Huku kambi yake akiitoa nnje kabisa ya mji
wa New York.
Huku wanajeshi wake akiwafunza kuua na sio kukamata maana
wasaliti wengi sana walikuwa serikalini.... Kitengo chake alichokipa jina la
NATIONAL INTELLEGENCY SECURITY AGENT (N.I.S.A).. Kilikuwa ni kitengo chenye
uwezo wa kivita kutokana na wengi wao kupitia mafunzo magumu sana... Walikuwa
wanajishughulisha na mambo ya kupambana na uharifu huku serikali kikitambua
kitengo kile ni moja ya makundi ya kigaidi na kuingia kwenye upelelezi.
General JEFF mara nyingi sana na kwa ungwe nyingi alikuwa
anatamani kufanya kazi na kijana ALEXIS ambae historia yake anaifahamu vyema na
uwezo aliokuwa nao pia na miongoni mwa kundi ambalo analitafuta ni kundi ambalo
ALEXIS analifahamu vyema kutokana na kukulia kwenye kundi hilo ambalo mmiliki
wake hajulikani kwa sura zaidi ya jina tu. Huku mtandano wake ukiwa mkubwa
duniani kutokana na washirika wake kuwa kwenye vyeo mbalimbali serikalini...
Hivyo iliwawia vigumu kuungamiza mtandano wasiojua hata chimbuko lake.
Waliitumia nafasi ya kumpata kijana ALEXIS ili awasaidie
kuuangamiza mtandao huo baada ya kuona ndio kijana wa pekee anaepigana kwaajili
ya kutafuta uhuru wake... Walitumia njia za kumtoa kumbukumbuku kijana huyo
kwasababu wanamfahamu vyema na wangeacha awe na kumbukumbu zake, ingewaletea
shida kutokana na kijana huyo kutoamini mtu mwingine awe mzuri au mbaya kwake
hakutaka kumuamini kiumbe wa aina yeyote ile zaidi yake mwenyewe.
‘’DAMIAN... Unajua hapa duniani kuna watu wanajifanya miungu
watu na kumkufuru mungu, biashara ya ushoga duniani imekuwa kubwa sana na
vijana wengi wanaharibika kupitia hii biashara... Wazazi wanalia kila siku kwa
kuwapoteza watoto ambao waliwazaa kwa kutumainia ni wakombozi wao wa baadae.
Lakini kuna watu wasiojua uchungu wa kuzaa wanawafanya mashoga na vijana wa
watu, wengine ni watu wazima na pesa zao ila nao wapo kwenye michezo hii ya
kufanya mapenzi jinsia moja.... Nimeangalia ni nani wa kumpatia hii kazi na
akaifanya vizuri, nimeona ni wewe kwasababu unauwezo na ni mzoefu kwenye
mapambano, naomba uifanye hii kazi kwaajili ya vizazi vijavyo..’’. General JEFF
aliongea hayo siku moja akiwa sehemu fulani kwenye kamgahawa kilichopo kwenye
mitaa fulani pale New York city....
DAMIAN alimsikiliza kwa umakini kabla ya kutua glass yake ya
juice na kumuangalia JEFF usoni kabla ya kupelekea tena glass kinywani.
‘’Aaa..Unajua watu wanaoiharibu dunia sio wakuishi sayari
moja na watu wema.. Hilo jambo ni zuri na nipo tayari kuipokea hiyo kazi ila
kwa sharti maalumu.’’
‘’Sharti gani tena..?’’.
‘’Sihitaji kuingiliwa kwenye kazi yangu..’’
‘’Wala usiwe na shaka juu ya suala hilo... Hakuna
atakaechumpa mipaka na kuinga kwenye tawala yako.! Jeff alimwambia Damian huku
akiruhusu koo lake kupita radha ya juice iliyotengenezwa kiustadi wa hali ya
juu..
‘’Kazi itaanza wiki ijayo, mtandao wa biashara hii haramu ni
mkubwa mno, yakupasa utulie na ufanye upekuzi kabla ya kutenda jambo!’’. Jeff
alimsisitiza na kumtaka kuweka umakini kwamaana mtandao anaoenda kuuchokoza ni
mpana sana na ni hatari endapo ataingia kichwa kichwa..
Walizungumza mambo kadha wa kadhaa kabla ya kujinyanyua
kutoka kwenye viti vya mgahawa huo na kutoka nnje.. Waliingia kwenye usafiri
wao waliokuja nao na kuuondoa kwa ustadi mkubwa sana, ndani ya gari ukimya ndio
ulitawala huku kila mmoja akionekana kutafakari jambo..
Umri wa General Jeff alimaarufu kama The Ghost, ulikuwa
umemtupa mkono na kutokuwa na makali yale ya enzi zake za ukamanda, walitembea
kila engo za jiji la NewYork city kama watalii lakini kuna mambo yao binafsi
walikuwa wanayafanya kwenye utembeaji wao.
Muda ulitamaraki na kusababisha majira kupinduka, usiku
walitafuta hotel yenye hadhi ili wajihifadhi ikiwa ni katika mikakati yao ya
kupembua jinsi watakavyoifanya kazi iliyombele yao.
Kutokana na Jeff kutambulika kama ni marehemu aliyekufa
kitambo kilichopita, ilifanya kutoingia ndani ya hoteli ile na kumpatia maelezo
pamoja na vifaa muhimu kwenye kazi kijana Damian ambae jina lake la awali ni
Alexis kisha yeye akaingia kwenye gari na kuliondoa maeneo yale akimuacha
Damian akimsindikiza kwa macho mpaka alipopotea kwenye upeo wake nd’o nae
akaingia ndani ya hoteli ambapo alipitiwa na kisachio ikiwa ni sehemu moja wapo
ya ulinzi uliopo kwenye hoteli ile yenye vyumba vya wageni ndani yake... Baada
ya kutambulika hana kitu chenye kuhatarisha usalama, alipatiwa ruksa ya kuingia
ndani mpaka sehemu ya mapokezi..
‘’Habari yako bibie! Naweza kupata chumba kinachoendana na
mimi?’’ Damian baada ya kufika mapokezi aliachia madaha yaliyomfanya mhudumu wa
pale kuachia tabasamu na kuonesha uzuri wake ulivyo, baada ya kuuliza suali
Damian alihitimisha mboni zake kwenye sura ya mrimbwende huyo ambae nae
alimtizama kijana aliyopo mbele yake kabla ya kujibu swali la kijana huyo.
‘’Vyumba vipo, unahitaji chumba cha aina gani labda? Kuna
vyumba vya V.I.P ambavyo ndani kuna kila kitu na ni salama kwa mambo yako
mbalimbali pia kuna vyumba vya kawaida..’’. Mrimbwende yule alijibu na kutazama
uso wa kijana mtanashati mwenye uchangamfu kupita maelezo.
‘’Nahitaji chumba cha V.I.P nadhani kitanifaa zaidi.’’.
Kijana Damian alitoa chaguzi yake na kuingiza mkono kwenye mfuko wake wa ndani
ya koti na kutoa mfuko mdogo wa kaki ambao Mara nyingi hutumika kuhifadhia
nyaraka na fedha pia, aliweka juu ya meza ambapo msichana yule aliuchukua na
kutoa noti za dola kadhaa na kuziweka kwenye mashine ya kuhesabia fedha.
‘’Ni kiasi cha miezi mitatu na wiki mbili, naomba pasipoti
yako tafadhali.’’. Msichana yule aliongea baada ya mashine yake ya kuhesabu
hundi kutoa takwimu za fedha ile iliyotolewa na kijana Damian. Bila hiyana
kijana Damian aliingiza mkono nyuma ya mfuko wa suruali aliyoiva siku hiyo na
kutoa waleti na kuifungua ambapo alichambua vitu kadhaa na kutoa pasipoti yake
iliyotengenezwa kwa masiku kadhaa yaliyopita nyuma na kumpatia yule kimwana
ambae aliipokea na kuiweka kwenye mashine maalum. Na baada ya dakika kadhaa
kukatika akaitoa na kuandika maelezo kwenye kompyuta yake na kuonesha sehemu
moja ya kuweka sahihi na kijana Damian bila kusita akaweka sahihi yake.
‘’Karibu sana bwana Damian Lewis kwenye hotel yetu, jisikie
huru kwa kila kitu utakacho utakipata, twende nikakuoneshe kilipo chumba
chako.... Wewe njoo mara moja ubebe mizigo ya mteja.!’’. Kimwana yule mwenye
sauti nyororo yenye kupendeza masikioni mwa kila amsikiae na kuwafanya watu
wengi kupenda kumsikia akiongea, alitoa maelezo kwa kijana Damian na kumuomba
aongozane nae akamuoneshe kilipo chumba chake na kuita mfanyakazi anaehusika na
ubebaji wa mabegi ama! Mizigo ya mteja na kumpelekea ndani.
‘’Aaah. Hapana usijali nitabeba mwenyewe nisikupe tabu..’’.
Damian aliomba asibebewe mizigo yake na kudai atabeba yeye, bila hiyana kijana
yule akarudi sehemu yake ya awali kungojea mtu mwingine wa kumbebea mzigo.
Walipanda lift na kutokea ghorofa ya juu kabisa ambapo nd'o
sehemu ya vyumba vya watu wenye heshma zao wanapokaa.
‘’Njia hii tafadhali..!!’’. Kigoli yule alimuonesha njia
kijana Damian baada ya kufika juu na kijana huyo akataka kupita kuliani kwake
kulipokuwa na watu wenye suti nyeusi wakiwa wamesimama kwenye milango kadhaa
kuonesha ni walindaji wanaomlinda mtu, alijiuliza upande ule kunani? Lakini
hakupata majibu sahihi kwenye kichwa chake na kuamua kupuuza na kuongoza kule
alipotakiwa kwenda.
‘’Chumba chako ni hiki, kama kutakuwa kuna vitu vingine
unahitaji usisite kutujuza kwa nambari zilizopo kwenye simu ya mkonge iliyopo
pale mezani. Nikutakie siku njema na upumzikaji mwema.’’. Msichana yule baada
ya kumfikisha sehemu husika kijana Damian alimkabidhi funguo na kumtakia
mapumziko mema na yeye akaondoka kwa mwendo wa maringo kama wa twiga, miguu
yake ya bia, mwendo wake wa kinyonga, shingo yake ya twiga, vilimvutia kijana
Damian na kutamani kumuita kimwana huyo lakini alikwisha chelewa maana bibie
alikuwa kashakata kona na kwenda sehemu ya lift na kuondoka akimuacha kijana
Damian akitumbua macho pima kama aliona kitu cha kustaajabisha mbele ya macho
yake.
Aliugeukia mlango wa chumba chake na kusoma namba za chumba
na kuufungua na kujitosa ndani yake, chumba kilikuwa ni kizuri na chenye
kupendeza kwenye macho ya kila mtu. Kijana Damian alitupia begi kwenye sofa
lililopo mule ndani na kupunguza uzito kwa kuvua koti lake na kulegeza tai
kisha akaanza kutalii kwenye kile chumba, alitembea kila sehemu na
kujihakikishia usalama na kurudi kwenye sebule ndogo na kutazama nnje kupitia
dirisha la kioo na kuona man’dhali ya jiji la New York city lilivyo.
Kwakua ilikuwa ni usiku na mchana kutwa hakupata nafasi ya
kujisafisha, ilibidi aingie maliwatoni kidogo kujifanyia usafi wa mwili, punde
baada ya kumaliza kujifanyia usafi allitoka maliwatoni akiwa kajifunga tauro
kiunoni huku jingine akijifutia maji. Alipofika sebuleni alifikia kwenye mkonga
wa simu na kubofya nambari kadhaa zilizoandikwa kwenye kikaratasi
kilichonatishwa juu ya simu ile na kuweka mkonga sikioni..
‘’Nahitaji chakula na wine moja, naomba viletwe chumba namba
291 muda huu.. Haya nashukuru..’’. Baada ya upande wa pili kupokea simu, kijana
Damian alitoa maagizo ya maang,’akuli na kurejesha mkonga sehemu husika baada
ya kumalizana na mtu aliyempa oda, aliendelea kujikausha maji na tauro dogo
kabla ya kushtushwa na mlango ukigongwa.
‘’Ngo! Ngo! Ngo! Ngo!’’. Mlango uligongwa kiustaarabu na
mgongaji na kufanya kijana Damian kunyanyuka alipokuwa ameketi na kuuendea
mlango maana alishajua ni nani anaegonga... Alizungusha kitasa na kikakubali na
mlango ukafunguka, alikuwa ni mhudumu akiwa na kimkokoteni chake cha kubebea
vyakuka na vinywaji alikaribishwa ndani na kijana Damian.
Alisukuma kimkokoteni chake mpaka mezani na kuweka vitu
alivyoagizwa juu ya meza kisha akaaga na kutoka. Baada ya mhudumu kutoka nyuma
kijana Damian alikaa mezani na kupata msosi na kushushia na wine kidogo na
baada ya kumaliza kupata chakula, alichukua begi lake na kutoa kompyuta ndogo
alimaarufu kama laptop na kuikunjua kisha akaiweka mezani na kuichomeka waya
wake kwenye soketi kwaajili ya kuilinda isije ikazima kwa kukosa chaji.
Alifungua na kutakiwa kuweka msimbo wa siri ili ifunguke,
alifanya hivyo na kuweka tarakimu kadhaa kisha akasubiri dakika kadhaa ili
mfumo mzima wa mashine ukae sawa, baada ya kuona umekaa sawa, alianza kuichezea
na kutoa kifaa kinachotumika kuhifadhia laini kwaajili ya kuingia mitandaoni na
kukiweka sehemu inayopaswa kuwekwa kisha akaingia kwenye mtandao na kuingiza
kitambulishi cha tovuti aliyoitaka na baada ya sekunde kadhaa tovuti ikafunguka
na yeye akaanza kufanya kile alichokusudia kukifanya ndani ya mtandao.
‘’Inamaana hii biashara inafanywa mpaka kwenye bara la
afrika? Mbona hawa watu ni waharibifu namna hii.? Kuna kitu natakiwa kukifanya
hapa ngoja niangalie maagent wao na ikiwezekana nitafute njia ya kuuvamia
mtandao wao ili nipate wepesi kwenye suala hili laasivyo nitakuwa natwanga maji
kwenye kinu.’’. Kijana Damian alijiuliza masuali mengi na kukosa majibu sahihi
baada ya kufungua moja ya tovuti na kuona takwimu za ushoga dunia na kuangalia
bara liloathirika ni bara la afrika ingawaje watu wa bara hilo wanaonekana
kipaombele kwenye kupinga mambo ya ushoga lakini ndio bara lenye uathirika
mkubwa sana wa biashara za ushoga.
Aliuma meno kwa hasira na misuri ya shingo na kifua kupanuka
na kutuna mithiri ya simba awapo hasirani, alichukia sana baada ya kuona vijana
wadogo wakijihusisha na biashara ya ngono za jinsia moja ilhali kwa umri wao na
maumbile yao hawakupaswa kufanya ujinga kama ule.
Alizidi kuchambua na kuandika maandiko kadha wa kadhaa
aliyoona yatampa muongozo kwenye upekuzi wake, masaa hayakuganda sehemu moja
yalizidi kukumbia mithiri ya barafu liwapo juani, kuja kutahamaki saa kumi
alfajiri ilimkutia kwenye laptop akifanya upembuzi wa mambo ya ushoga na
kutafuta mawakala wanaohusika na ununuzi na usambazaji wa biashara hiyo.
Usingizi ulikuwa unasumbua mboni zake za macho na kufanya
macho kumuomba yapumzike kwamaana yamechoka kusoma na kuangalia mwangaza wa
laptop lakini yeye hakutaka kuyasikia wala kulala angalau kidogo nd’o kwanza
alizidi kuingia ndani kabisa ya mtandao na kuchimba siri nzito za mashoga....
Kitu kilichomshangaza zaidi ni pale alipoona si. Vijana pekee wanaofanya kazi
hizo hata wazee nao walikuwa wanafanya kazi hizo kwa kuwanunua vijana mashababi
kwaajili ya kuwashughulikia kinyume na maumbile yao yanavyowataka wawe, alizidi
kupata hasira baada ya kuona orodha fupi ya viongozi wakubwa ambao nao ni
mashoga na wanawanunua vijana mashababi waliojazia kimazoezi kwaajili ya
kufanya nao mapenzi ya jinsia moja.
‘’Wanahidhaya wakubwa hawa, yaani hadi wazeee? Hii siwezi
kulifumbia macho lazima niikomeshe hii biashara kwa njia yeyote hata ikinibidi
kuutoa uhai wangu, naua kila mmoja si. Mnunuzi wa vijana kwaajili ya kufanya
nao ngono wala anaenunuliwa ni lazima wote wafe ili isitokee tena ushetani kama
huu.. Oooopsssss.’’. Kijana Damian alichoka hoi baada ya kuona mambo
yanayoendelea juu ya biashara iliyokithiri duniani... Aliiacha laptop yake on
na yeye akajitupa kwenye kitanda baada ya kuona kapata angalau kidogo kati ya
kingi alichokitaka.
******
‘’Bado hamjapata taarifa zozote kuhusu Alexis? Kwanini sasa
wakati mnatambua ni kijana pekee mwenye uwezo wa kuja na kuiangusha biashara
yetu..’’. Kuna mzee mmoja wa makamo alikuwa anazungumza na mtu kwenye simu huku
akifoka kweli juu ya uzembe walioufanya vijana wake.
Baada ya kuzungumza vile hakusubiri maelezo kutoka upande wa
pili wa ile simu, yeye alikata na kubofya nambari kadhaa na kuirudisha tena
sikioni ile simu.
‘’Madam's Aretha, kijana Alexis imekuwa ni ngumu kumpata
kutokana na kundi jingine kujitokeza na kumchukua kule hospitalini..’’. Mzee yule
alizungumza kwa adabu kuu na mtu wa upande wa pili wa simu aliyemtamka kwa jina
la Madam’s Aretha .
‘’Kwasasa inatakiwa kuangalia biashara jinsi inavyoenda
kuhusu huyo kijana achaneni nae.’’. Sauti ya kike ilisikika upande wa pili wa
simu ikizungumza na ukimya ukachukua nafasi kuonesha simu ilishakatwa.
Yule mzee alishusha pumzi ndefu na kuondoka sehemu alipokuwa
kasimama na kushuka mpaka chini, alikuwa kwenye hotel moja iliyopo Miami
Florida akifanya mambo ya biashara.
Ni miongoni mwa mawakala wa ushoga ambao ndio mashina
makubwa makubwa yanayotafutwa na kijana Damian.
Alitoka nnje ya hotel hiyo na kuingia kwenye gari moja ya
kifahari na kuamuru dereva aiondoshe pahala pale.... Alikuwa na msafara mkubwa
sana kama wa raisi ama mbuge zote hizo ni fedha wanazozichuma kiharamu kwa
kuuza na kusambaza mashoga duniani na kuua matajiri na kuwanyang’anya vito vyao
vya thamani, msafara wake ulikuja mpaka maeneo ya bandalini ambapo kwenye
bahari kulionekana kuna meri kubwa inaingizana sehemu ile tena kwenye usiku ule
wa manane.
Meri baada ya kutia nanga kwenye bandali ile wafanyakazi
walianza kushusha maboksi kadhaa yaliyomo mule ndani huku makontena yakishushwa
na kifaa maalumu. Baada ya nusu saa kukatika makontena yalikuwa yameshushwa kwa
wingi na yale maboksi yule mzee alishuka na kwenda kukagua vitu vilivyomo ndani
ya makontena yale na maboksi, lahaula!!! Kwenye makontena yapatayo kumi na moja
yalikuwa yamehifadhi ndani yake vijana wakike kwa waume waliokuwa chini ya
miaka kumi na minane huku wengi wao wakionekana kutokea kwenye bara la afrika.
Walikuwa wanatia huruma jinsi walivyokuwa wamefungwa kamba
kwa miguu na mikono huku wakionekana wamedhoofika kutokana na njaa, mzee yule
alitabasamu na kuwataka vijana wayaweke makontena hayo kwenye magari
yanayohusika kubeba makontena na wayasafirishe mpaka Las Vegas kwaajili ya
kuwafanyia biashara vijana wale huku yeye akitangulia uwanja wa ndege wa
kibinafsi na kukwea pipa kuelekea Las Vegas kuandaa soko.
Magari yaliyobeba makontena ambayo ndani yake kuna binadamu
yalianza kusafirishwa usiku huo wa manane huku maasikari wengi wakiliokuwemo
ndani ya bandali na kwengineko, wakikingia kifua biashara ile na kuyaruhusu
magari hayo kuvuka kwenye kila kizuizi, pesa nd’o iliongea kwa kipindi kile na
hakukuwa na askari wa kukataa kupokea mlungura mrefu ilhali kwa mwezi analipwa
kiasi cha hundi kidogo, viongozi wa nyanja za ulinzi wa nchi ya marekani
walikuwa chini ya mwanamama mwenye kuindesha biashara ile na hakukua na vikwazo
kwenye biashara yake hiyo ya haramu
ITAENDELEA
Your Thoughts