HOTUBA YA MWISHO YA MUAMMAR GADDAFI

JABA PLANET.

Leo katika historia tutaangazia hotuba ya mwisho ya aliyekuwa raisi wa Libya MUAMMAR GADDAFI
Hii hapa hotuba hiyo
   "Kwa jina la Mwenyezi Mungu
(Allah), Mungu mpaji, na mwenye
rehema,
   Kwa miaka takribani 40 ama ilikuwa zaidi sikumbuki, 
   Ninacho kumbuka ni kuwa nilifanya kila nilichoweza kuwapa watu wangu nyumba, hospitali na shule,
    Na kila walipo hisi njaa niliwapa chakula bure,
   Niliifanya Benghazi kutoka jangwa kuwa ardhi nzuri ya kilimo,
   Nilisimama imara dhidi ya Ronald
Regan (Rais wa zamani wa
Marekani),
   Pale ambapo alipo muua binti yangu niliyemuasili,
   Alikua anajaribu kuniua mimi lakini akamuua yule binti yatima masikini,
   Niliwasaidia kaka na dada zangu waafrika fedha kupitia AU,
  Nilifanya kila nililoweza kuwafanya
watu wangu waelewe maana halisi
ya demokrasia,
  Ambapo watu wa tabaka la chini niliwapa madaraka,
  Lakini hawakuridhika hata aliyekuwa na nyumba ya vyumba kumi, nguo mpya, na fanicha nzuri, hakuridhika alihitaji zaidi,
  Kwa jinsi walivyokuwa wabinafsi
walihitaji zaidi,
   Hivyo waka waambia Marekani kuwa wanataka demokrasia na uhuru,
   Hawakujua kuwa demokrasia waliyoitaka,
   IIikua ni mfumo wa unyonyaji ambapo mbwa mwenye nguvu zaidi huwala mbwa wadogo,
   Walikua hawasikii wala hawaoni
walitaka demokrasia,
  Wakasahau kuwa hata Marekani hakukuwa na huduma za afya za bure, dawa bure, elimu bure na chakula cha bure,
   Huduma hizi za bure zilipatikana nchini Libya tu,
   Nchini Marekani mtu masikini/fukara hana cha bure,
   Labda awe ombaomba au avuje jasho kuhemea,
  Haikujalisha nilifanya kwa kiasi gani
bado hawakuridhika,
   Lakini wapo waliojua mimi ni mtoto wa Gamal Abdel Nasser, 
  Mwarabu pekee halisi na kiongozi wa kiislamu tuliyewahi kuwa nae tangu enzi za Salah-al-Deen,
   Wakati Nasser anapigania mfereji wa Suez kwa watu wake,
   Nami nilikua naipigania Libya kwa watu wangu,
  Nilikua najaribu kufuata nyayo zake
ili kuwaweka watu wangu huru,
   Kutoka kwenye makucha ya wakoloni wanaotuibia,
   Lakini kwa sasa niko mateka katikati ya majeshi makubwa ya dunia katika historia,
   Mwanangu mpendwa mwenye asili ya Afrika Obama anataka kuniua,
  Ili achukue uhuru wetu achukue haki yetu ya huduma za bure za afya,
  Huduma za bure za elimu, na chakula chetu,
   Na kutuletea mfumo mpya wa
kimarekani wa kuiba uitwao Ubepari,
   Lakini wote katika dunia ya tatu
tunajua maana yake,
   Maana yake ni kuwa washirika wana tawala mataifa, 
   Wanatawala dunia, na watu wanaishia kuteseka,
  Kwahiyo hakuna mbadala kwangu lazima niwe na msimamo,
   Na kama Mungu atapenda nitakufa kwa mapenzi yake,
  Mapenzi yake yaliyofanya nchi yetu
kuwa na ardhi yenye rutuba, chakula
bora, na huduma bora za afya,
   Mapenzi ya Allah yaliyowezesha
tukawasaidia kaka na dada zetu
waafrika na waarabu waliokuwa na
shida,
   Sipendi kufa lakini kama nitakufa ili
kuiokoa ardhi hii, 
   Kuokoa watu wangu na wengine ambao ni kama wanangu ACHA NIFE,
  Acha sauti hii iwe agano langu kwa dunia kuwa nilisimama kupinga
uvamizi wa NATO,
  Nilisimama kishujaa kupinga usaliti wa nchi za magharibi na nia mbaya za kikoloni,
  Na hapa nimesimama na ndugu
zangu waafrika, 
  Kaka na dada zangu waislamu kama ngao yangu ya matumaini,
  Wakati wengine walipokuwa
wanajenga majumba ya kifahari,
   Mimi niliishi kwenye nyumba ya
kawaida na kwenye mahema,
   Siwezi kusahau maisha yangu ya utoto kule SIRTE,
  Sikutumia rasilimali za nchi yangu kipumbavu,
   Na kama alivyokua Salah-al-Deen kiongozi wetu katika uislamu, 
  Nilichukua kidogo sana kwa
ajili yangu na sehemu kubwa
niliwapa wananchi,
   Watu wa magharibi wameniita
kichaa na mwendawazimu,
   Lakini wanajua ukweli kuwa mimi si kichaa wala mwendawazimu,
   Ila waache waendelee kudanganya lakini wanajua hii ardhi ni huru na haipo kwenye himaya ya kikoloni,   
  Huu ndio msimamo wangu na dira yangu na imekuwa wazi kwa watu wangu,
   Nitapambana hadi pumzi yangu ya
mwisho ili watu wangu wawe huru,
   Mwenyezi Mungu atusaidie tubaki
waaminifu na tuwe huru" ... MUAMMAR GADDAFI
Hiyo ndio hotuba yake ya mwisho mwamba huyu.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Your Thoughts