RIWAYA: JESTINA
MTUNZI: Tariq Haji
CONTACT: +255624065911
SEHEMU YA PILI.
ENDELEA
Bila kuchelewa aliekea kwa Mr Hendrix na kumwambia kuwa Jestina na Alwin hawaonekani, wala hakushtuka sana "usijali ni watoto na hawajotoka ndani ya nyumba,we nenda kapumzike mi nitawatafuta" alisema na kumwambia Mr Kelvin amfuate.
Walizunguka nyumba nzima lakini hawakuwaona mpaka wasiwasi ukaanza kuwapata. Upande wa pili huko mpambao ulikuwa mkali kupita maelezo, kwa sababu ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Alwin kucheza mchezo ule ilikuwa ni vigumu sana kushinda lakini akili yake ilionekana kutokubaliana na kusindwa hivyo alienedele kuminyana na puzzle hio huku kijasho chemba kikimtoka. Wakati wakiendelea kutafuta, wazo lilimjia Mr Hendrix na kumwambia mwenzie waelekee varanda. Walipokaribia tu waliwaona wawili hao wakiwa katika mtanange huo na Mr kelvi alipotaka kuenda kuwashtua Mr Hendrix alimzuia na kutoa simu na kuanza kurikodi pambano hilo.
Kila mpambno ulivyokwenda ulizidi kuwa mkali huku kila mmoja akihakikisha anamaliza mwanzo kuliko mwenzake. Lakini bahati ilikuwa mbaya kwa Jestina baada kushindwa na Alwin ambae ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kupanga puzzle ile. Kwa kweli llilikuwa pigo kubwa kwa Jestina, alianza kulia baada kuona kuwa ameshindwa wakati yeye ndie aliezoea hasa kupanga vibox hivyo. Mr Hendrix alimsogelea na kumbeba mwanae "mbona unalia", "baba kanishinda yule" alijibu huku akimnyooshea kidole Alwin. "kushindwa ni kawaida katika maisha, lakini ipo siku na wewe utamshinda" aliongea huku akimfuta machozi mwanae ambae alianza kutabasamu.
"Alwin njoo" Mr kelvin alimuita mwanae na kumbeba, "Mr Kelvin" aliitwa na rafiki yake. "nishaalijua tatizo la mwanao la kushindwa kujichanganya" aliongea Mr Hendrix na kumshangaza rafiki yake, "Alwin ni genius" aliendelea kuongea. "acha utani wewe" alijibu Mr Kelvin huku akicheka akidhani rafiki yake anamtania. "unadhani nakutania, huyo mwanao ni genius na kama huamini kesho asubuhi njoo nae tuende hospitali akafanyiwe IQ test" aliongea Mr Hendrix akionyesha yuko serious sana. Basi walkubaliana kesho yake aje ili waende hospitali kwa ajili ya kazi ile. Baada ya hapo walirudi ukumbini na kuendelea kushereheka mpaka muda wa kuondoka ulipofika. Kila mtu aliaga na kurudi makwao, mawazo yalikiandama kichwa cha Mr Kelvin huku akijiuliza maswali kadhaa yaliokosa majibu. Alifika nyumbani kwake na kupumzika, siku ya pili mapema alimueleza mkewe kila kitu na kumwambia amuandae Alwin anataka kutoka nae. Baada ya nusu saa Alwin alikuwa tayari na safri ya kuelekea kwa Mr Hendrix ilianza, alimkuta rafiki yae huyo akimsubiri na hwakukaa sana waliondoka kuelekea hospitalini.
"habari za saa hizi dokta" Mr Hendrix aliongea baada kukaribishwa kwenye viti, "salama tu, niwasaidie nini". "ah tumemleta kijana wetu kwa ajili ya kupimwa uwezo wa akili", "ahaa basi haimna shida nifuateni". Dokta aliinuka na kuongoza njia mpaka alipofika katika chumba kilichoandikwa IQ test room na kuingia. Ndani ya chumba hicho kulikuwa na watu kumi ambao walionekana kama maprofesa "karibuni naomba mkae hapo,huyo mtoto nipeni mimi" aliwaonyesha sehemu ya kukaa na yeye akamchukua Alwin na kumpeleka kwenye kiti kilichokuwa katikati ya chumba hicho kisha yeye akarudi na kuungana na kina Mr Hendrix.
"jina lako nani" aliuliza mmoja kati ya wale watu kumi,
"jina langu ni Alwin Kelvin Alfred". "una miaka mingapi" aliuliza mwengine. "nina miaka mitano". "sasa Alwin tutakuuliza maswali kumi, matano ya kawaida matano ya hesabu" aliongea mwengine
"na kila swali utapewa sekunde kumi kulijibu",
"sawa" alijibu Alwin.
swali la kwanza: "umeingia kwenye banda la wanyama, chini kuna nyoka wawili, kwenye mti kuna nguchiro wanne na ndege watano wamekaa na wawili wanaruka, je kuna miguu mingapi iliokanyaga ardhi?"
Alwin: "kuna miguu miwili na hiyo miguu ni ya kwangu"
Swali la pili: "juu ya mti kuna mananasi nane, yakachumwa matatu. je yatabaki mangapi?"
Alwin: "mananasi hayaoti juu kwenye mti"
Swali la tatu: "ikiwa simba anauwezo wa kumuua swala kwa dakika mbili, je chui atakua na uwezo wa dakika ngapi kumuua swala huyo huyo?"
Alwin: "haiwezekani kwa sababu swala huyo kashakufa tayari, kauliwa na simba"
Swali la nne: " Clinton ana uraia wa nchi mbili wa Jamaica na wa Brazil, alizaliwa Jamaica lakini sasa anaishi Brazil, kwa sababu za kisheria Clinton hawezi kuzikwa Brazil. Je sentensi ya mwisho ni kweli ama uongo?"
Alwin: "ni kweli, kwa sababu Clinton bado hajafa"
Swali la tano: " kuna wakati kipindi cha christmas, Santa Claus hakuwapa watoto zawadi. Alikwenda North pole akiwa na chupa mbili za wiski, chupa tatu za wine na chupa nne za bia katika begi lake. Alikunywa zote mpaka tone la mwisho kisha akalala. Alikuja kuamka saa tatu asubuhi akiwa na chupa tisa ambazo zinakaribia kuwa tupu. Ikiwa sentensi tatu za mwanzo ni kweli basi sentensi ya mwisho ni kweli au uongo"
Alwin: "uongo, kwa sababu kumebakiwa na tone moja katika kila chupa, hata hivyo hakuna asubuhi wakati wa decmber katika north pole, kuna usiku tu".
Swali la sita: " kati ya namba hizi ipi haigawinyiki kwa tano. 786, 981 na 123"
Alwin: "zote zinagawanyika, ukichukua 786 gawa kwa tano unapata 157.2, 981 gawa kwa tano unapata 196.2 na 123 gawa kwa tano unapata24.6"
Maswali yaliendelea mpaka yote yalipoisha akawa amejibu yote kwa usahihi bila kukosea hata moja. Baada ya hapo alipelekwa katika chumba kingine lakini huko waliambiwa hawaruhusiwi kuingia ndani hivo walisubiri nje. Baada ya nusu saa daktari alitoka na Alwin na kuwaambia kuwa wasubiri muda si mrefu watapata majibu. Robo saa baadae daktari alitoka na ripoti kamili ya Alwin huku akitabasamu na kuwaomaba wamfuate. "kwanza niwape hongera kwa kuwa na kijana mwenye uwezo mkubwa sana wa akili, Akili ya Alwin inafanya kazi kwa kasi mara nne zaidi kuliko binadamu wengine, ninaposema hivyo namaanisha kuwa Alwina ana uwezo mkubwa sana wa kufikiri. Hii hapa ni ripoti yake kamili , ana IQ ya 170 . Hii ndio sababu ya yeye kupata ugumu katika kushirikiana na wenzake kwa sababu uwezo wake wa kupambanua mambo si wa kawaida, hivyo lolote utakalo mwambia basi yeye atalitafutia maana kwa undani zaidi"
Daktari aliendelea kuawafafanulia tabia za Alwin na kuwaambia kuwa wasipokuwa makini basi watamsababishia matatizo makubwa sana kwa sababu akili yake huwa haiko tayari kulazimishwa kufanya jambo ambalo halitaki. Baada ya kuelezwa kila kitu walifanya malipo na kuondoka zao kurudi nyumbani, wakiwa njiani
"Umejuaje kama Alwin ni genius" aliuliza Mr Kelvin.
"ni kwa sababu hata Jestina pia ni genius lakini yeye IQ yake ni 150, na ile puzzle waliokuwa wakishindana kuipanga nilipewa na daktari ili nimpe mwanangu wakati anaposhindwa kutatua jambo, ni watoto wachache sana ambao wana uwezo wa kupanga puzzle ile wakati mawazo yao yapo kwengine, wakati ule wakishindana mawazo yao yalikuwa ni kwa jinsi gani wangeweza wangeweza kukabiliana na umati mkubwa wa watu uliokuwepo ukumbini. We unadhani hawakutuona wakati tuna warikodi, walituona lakini kwa vile kimawazo hawakuwa pale basi hawakutushughulikia tu. Usiniulize nimejuaje yote haya, ni kwa sababu nimesomea saikoloji" alijibu Mr Hendrix na kumfafanulia rafiki yake kila kitu. Walifika nyumbani kwa Mr Hendrix na kuagana, Mr Kelvin aliekea kwake akiwa na furaha kubwa sana na alipofika alimueleza mkewe kila kitu.
********************
Akiwa na miaka mitano Jestina alimpoteza mtu muhimu sana katika familia yake, Bi Prisca aliaga dunia baada siku chache tokea kusheherekea mwaka wa tano tokea kuzaliwa kwa Jestina. Hili lilikuwa pigo kubwa sana hasa kwa Jestina kutokana na mapenzi makubwa aliokuwa nayo juu ya bibi huyo. Walifanya maziko na kuomboleza baada ya hapo kila mtu alirudi kwake, na kadri muda ulivyokwenda Jestina alikaa sawa na kuendelea na maisha kama kwaida kwa sababu alielewa hapa duniania tunapita tu na kila mtu ipo siku atakufa.
Kutokana na uwezo mkubwa wa akili Jestina na Alwin walipelekwa shule ya vipaji maalum, na huko moto uliwaka wanafunzi wengine waliisoma namba maana wawili hao walikuwa hawapitiki. Hiyo ilipelekea mpaka wanafunzi wengine kuwachukia lakini wao hawakujali hilo, kwao masomo yalikuwa wanayapa kipao mbele. Miaka ilisonga mbele huku kila siku uwezo wao akili ukizidi kuwa mkubwa, hatimae walimaliza shule ya msingi na kujiunga na high school kwa ajili ya kujiendeleza na masomo zaidi. Kwa wakati huo Alwin alikuwa na miaka kumi na tatu na Jestina alikuwa na kumi na mbili. Pamoja na umri mdogo lakini uzuri wa Jestina uliwavutia mapaka shume na kuanza kumtongoza. Lakini wengi waliambulia pakavu, lakini kwa Alwin ilikuwa tofauti japo yeye alimpenda alishindwa kumwambia. Lakini aliuonyesha dalili zote za upendo hata hivyo Jestina hakuonyesha dalili zozote za kumpenda zaidi ya upendo wa kirafiki tu.
Maisha yalisonga mbele huku walimu wakivutiwa sana na juhudi za wawili hao japo walikuwa magenius, hatimae walimaliza high school na kujiunga na college. Sasa Alwin alikuwa na umri wa miaka kumi na saba na Jestina alikuwa na umri wa miaka kumi na sita, uzuri wa Jestina ulizidi kunawiri huku ukitii kanuni za kibaolojia. Macho yake makubwa yalimpendeza yakisindikizwa na uso wa duara uliopambwa na pua ndogo nzuri pamoja na mdomo wenye lipsi ambazo muda wote ziling'aa.
Itaendelea
Your Thoughts