JESTINA 1

 RIWAYA: Jestina

MTUNZI: Tariq H. Haji

MAWASILIANO: +255624065911

SEHEMU YA 1

"Jestina....Jestina....Jestina...tafadhali usifunge macho eeeh mungu usimchukue Jestina wangu nitabaki na nani hapa duniani" hiyo ilikuwa ni sauti ya kijana Alwin akiwa amempakata katika mapaja yake mschana aliekuwa akimpenda zaidi kuliko kitu kingine chochote duniani. Wakati huo Jestina alikua akivuja damu maeneo kadhaa katika mwili wake. "Alwin kwanini unanipenda kiasi chote hicho na wakatii nilishaakwambia zamani kuwa sina hisia za kimapenzi juu yako" Jestina aliongea japo kwa tabu sana. "Jestina kukupenda mimi haikuwa na maana na wewe unipende, penzi la upande mmoja lilitosha kabisa kuishi na wewe" Alwin aliendelea kuongea huku machozi yakimchuruzika ka maji machoni mwake. 

 "Alwin nakuomba unyamaze na uniache nipumzike kwa amani, nakuahidi kuwa nitazaliwa tena kwa ajili yako iwe katika maisha haya au yoyote yale..... tafadhali niache niende kwa amani" alimaliza kuongea maneno hayo na kukaa kimya, Alwin alijaribu kumtingisha lakini hakushtuka, alipeleka kidole kwenye pua na hapo ndio akagundua kuwa tayari Jestina alishaamuacha peke yake duniani. "no...n.o...no ple...ase Jestina...Jestina... Jestinaaaaaa" alipiga kelele na papo hapoa akapoteza fahamu.

***********

 Mwaka 1993 katika mji wa Mashvile, iliskika sauti ya mwanamke akipiga kelele za uchungu. "sukuma..jitahidi mama mtoto kashafika mlangoni" hiyo ilikuwa ni sauti ya daktari aliekuwa akimzalisha mama huyo. Sekunde kadhaa baadae iliskika sauti ya kichanga kikilia, "hongera bwana Hendrix umepata mtoto wa kike" alitoka daktari na kumpasha habari hizo mume wa mama aliekua akijifungua. "naruhusiwa kuingia" aliuliza bwana Hendrix kwa furaha sana, "ndio" dokta alijibu na bila kuchelewa alipita na moja kwa moja alielekea kitandani alipokuwa mkewe. 

 "pole mke wangu" aliongea kwa bashasha na kumbusu mkewe katika paji la uso, "naweza kumbeba mwanangu" aliuliza bwana Hendrix, "ndio" alijibu nesi mmoja, basi nae bila kuchelewa alimchukua mtoto huyo kutoka mikoni mwa mkew na kumbeba. Kwa kweli siku hiyo ilikuwa ni siku nzuri sana kwa familia hiyo ya kitajiri. Hiyo imetokana na kuwa, ni miaka mingi sana wameishi katika ndoa bila kupata mtoto japo walipata misukosuko kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki lakini wao hawakujali waliamini siku zote mtoto ni riziki kutoka kwa Mungu. Basi baada kukamilika taratibu zote waliruhusiwa kurudi nyumbani, walitoka hospitalini na kuingia wene gari na kuondoka. Njia nzima kila mmoja alikuwa kimya akitafakari ni jina gani ampe mtoto wao, walikuja kushtuka baada dereva aliekuwa akiwaendesha kuwaambia kuwa tayari washafika nyumbani.

 Wafanya kazi wote walikuwa nje wakiwassubiri kwa hamu, waliposhuka tu kwenye gari watu walipiga vigelegele na kuwakaribisha ndani. Kwa vile walikuwa wamechoka sana waliekee chumbani kwao na kupumzika. Siku ya pili mapema asubuhi waliamka na kushuka chini, walishangaa kukuta kumebadilika sana, kwenye meza kulikuwa na keki kubwa ilioandikwa "Welcome to the world little princess". Ukweli nyumba hiyo ilijaa furaha kupita maelezo, na hiyo ilitokana pia na ukarimu wa matajiri hao kwa wafanya kazi. Kiufupi hawakuwachkulia kama ni wafanya kazi bali ni kama ndugu zao tu. 

 Siku kadhaa zilipita na muda wa kumpa jina ulifika, hapo sasa kukawa na mshikemshike maana wafanya kazi wa kike walikuwa wakimsapoti mama na wafanya kazi wa kiume walikuwa wakimsapoti baba. "Bora aitwe Jessey" huyo alikuwa ni bwana Hendrix, "bora tumuite Christina" na huyo alikuwa ni mke wake, mdahalo huo uliendelea kwa muda mrefu bila kupata jibu mpaka iliposkika sauti yenye kukwaruza ikisema "kwanini msimuite Jestina, Jes kutoka Jessey na Tina kutoka christina", "lakini kweli hapo itakuwa vizuri maana atakuwa na jina alilochaguliwa na baba yake na mama yake pia" wote walikubali na kumuita mtoto wao "JESTINA". 

 "Prisca mama yangu kwanini usiache tena kufanya kazi maana umri ushakwenda sana" Mr Hendrix alimuita na kumueleza hayo mfanya kazi huyo ambae alikuwa akimheshimu kama mama yake maana ndie aliemlea tokea wazazi wake wapo hai mpaka wamekufa na ndie anaejua ni kwa jinsi gani utajiri huo umepatikana "mwanangu Hendrix kama nitaacha kufanya kazi nitapata wapi pesa ya kula" aliongea mwanamke huyo alienekana kuzeeka na umri wake ulikuwa ni kati ya miaka sabini hadi sabini na tano. "Sijamaanisha uondoke hapa, hapa wewe ni kwako na mpaka mwisho wa maisha yako utaendelea kuishi hapa. Ninachomaanisha ni kwamba uache kufanya kazi tu kula utakula na mahitaji yako yote nitakupatia"Aliongea Hendrix na kumkumbatia bibi huyo ambae alimpenda kupita kiasi. "kama ni hivo sawa ila naomba kitu kimoja tu, niwe nacheza Jestina" aliongea bibi huyo huku machozi yakimtoka jambo ambalo Hendrix alilikubali kwa mikono miwili. Baada ya hapo aliamuru chumba cha Jestina kiongezwe kitanda kimoja kikubwa kwa ajili ya Prisca na kazi hiyo ilifanyika siku hiyohiyo kisha kila kitu cha bibi huyo kikahamishiwa chumbani huko. Ukweli bibi huyo alikuwa akimpenda sana Jestina na yeye ndie alieshauri kuwa mtoto huyo aitwe Jestina.


 Jestina alikuja na baraka ndani ya nyumba hio, maana mambo mengi yalikaa sawa huku bishara zikinawiri. Maka ilisogea na hatimae ilifika siku ya kusheherekea kuzaliwa kwa Jestina akiwa anatimiza miaka mitatu, watu wengi sana walialikwa katka sherehe hiyo. "mke wangu fanya haraka tushachelewa" mzee Kelvin alikua akimharakisha mkewe ili wawahi kwenye sherehe. "nishamaliza mume wangu nakuja" alijibu mkewe huku akitoka na mtoto mdogo wa kiume mwenye umri wa miaka minne akiwa amembeba. 

 Waliwasha gari na kuelekea katika sherehe, na kwasababu hakukuwa mbali,  walitumia dakika tano tu  mpaka kufika, walishuka kwebye gari na kuelekea ukumbini. "karibu Mr na Mrs Kelvin" aliongea Mr Hendrix baada kuwaona wakiingia, "asante lakini samahani kwa kuchelewa" alijibu Mr Kelvin ambae alionekana ni mwenye busara. "mbona kijana wenu anaonekana hajachangamka" Aliongea Mr Hendrix baada kumuandalia mtoto aliebebwa na mke wa Mr Kelvin. "ah ni kawaida yake huyo hawezi shangwe" alijibu Mr Kelvin huku akicheka, "anaitwa nani" aliuliza tena Mr Hendrix, "Alwin ndio Jina lake"alijibu Mr kelvin huku akimchukua Alwin kutoka mikononi mwa mkewe na kumshusha chini.

  "Alwin nenda kacheze na wa wenzako" alimwambia lakini Alwin wala hakusogea hata hatua moja, "mume wangu si unajua mtu mwenyewe huyo hawezi kujichanganya, acha tu nitakaa nae mimi" mkewe aliongea. "muache akacheze na wenzake na wewe nenda ukasalimiane na wanawake wenzako" alijibu Mr Kelvin akiwa amekunja sura. Bila kuuliza kitu mkewe aliondoka na kumuacha Alwin akiwa amesimama pembeni ya babaake. "unajua sikujali sana hii tabia ya mwanangu kutojichanganya kipindi ambacho nilikuwa naishi nje ya mji huu, lakini sasa hivi lazima ajifunze kwa sababu hapa ni kwao" aliongea Mr Kelvin, basi Mr Hendrix alimwita mfanya kazi mmoja na kumwambia ampeleke Alwin kwa watoto wenzake.

 Baada Alwin kuchukuliwa wao walianza kuongea mambo yao ya kibiashara huku wakisubiri muda ufike Jestina aletwe ukumbini. Baada ya nusu saa mlango ulifunguliwa na Jestina akaingia ukimbini huku aksindikizwa na mziki wa happy birthday mpaka kwenye meza ya keki. Alwin ni miongoni mwa watoto waliosimama mbele kabisa karibu na meza yenye keki lakini hakuimba, alinyamaza kimyaa na kutulia kama maji mtungini. Ni utamaduni wa mji huo katika kusheherekea mwaka wa tatu tokea kuzaliwa, yule ambae ndie mwenye sherehe huchagua mtoto mmoja na kucheza nae. "sasa tunamtaka Ms Jestina amchague mtoto mmoja wa kiume ili acheze nae kama sehemu ya kudumisha utamamduni wetu" MC aliongea na bi Prisca alimsogelea Jestina na kumnong'oneza jambo, Jestina alitabasamu kidogo na kutoka kwenye meza ya keki.

  Hakika kila mtoto mwenye umri wa miaka mitano kushuka chini alitamani iwe ni yeye ambae atapata bahati hiyo isipokuwa Alwin peke yake ,yeye aliomba asionekane haswaa lakini ni tafauti na alivotarajia. Jestina aliomsogelea na kumkabidhi uwa ikiwa ni kama ishara "njoo tucheze". Mama Alwin alijishika kichwa baada kuona mwanae ndie aliechaguliwa maana alielewa kuwa kungetokea vituko tu katika dance floor.

  Alwin hakuwa na la kufanya zaidi ya kukubali japo kuwa alikuwa katika wakati mgumu sana, maana akili yake ilikuwa haikubaliana haswaa na jambo hilo. DJ aliweka mziki laini unaojulikana kama slow germ, pamoja na kuwa Jestina alikuwa mdogo lakini yeye alishaafundishwa kucheza japo hakuwa akijua sana tafauti na Alwin ambae ilibidi amfuate Jestina anavyokwenda. Lakini maajabu yaliotokea baada dakika kidogo kupita, Alwin alionekana kuanza kuchanganya katika kucheza hata babaake na mamaake walishanga kuona mtoto wao anacheza huku ametabasamu.

 Mziki ulikwisha na sherehe ikawa imeanza rasmi, Jestina alikata keki na kuwalisha watoto wenzake wote. Baadae mziki ulifunguliwa tena na kila mtu akawa anashereheka kwa njia yake isipokuwa Alwin peke yake ambae aliondoka kabisa ukumbini na kuelekea varanda, "wewe mbona uko huku" ni sauti ya kitoto iliomuuliza. Alipogeuka alikutana na tabasamu liloipamba uso wa Jestina, "sijiskii kucheza" alijibu. "basi kama hutaki kucheza shika hichi kibox na ukipange mpaka rangi zinazofanana zikae pamoja" Jestina aliongea huku akimpa puzzle box Alwin na yeye alikuwa na kingine. Alwin alitabasamu kidogo na kumwambia "unaonaje tukashindana yupi atakae maliza mwanzo", "sawa" alijibu Jestina na wote wakakaa chini na kuanza mashindano. "jamani Jestina na Alwin wako wapi" bi Prisca alikuwa alikuwa akiwauliza wafanya kazi ambao hata wao walisema hawajui. 

Itaendelea 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.