KOSA LANGU 2

KOSA LANGU 



MTUNZI: Emmanuel Kahindi

WhatsApp:+254796273110

Website: jabaplanet.blogspot.com


Sehemu ya Pili

Ilipoishia sehemu ya 1


"Baada ya somo hili Hezron nione tafadhali"

Atakuwa ashajua nimekopi huyu si bure muda wote simalizi kazi zake hajawahi niita hata mara moja mbona Leo au ana zawadi mmmh mbona asingenizawadia mbele ya wanafunzi wenzangu.


Somo lile lilikuwa la mwisho siku hiyo alhamisi katika shule hiyo ya Mtakatifu George

Somo lile lilienda mbio hata sikuelewa liliisha Vipi

"Hezron nifwate" nilishutushwa na sauti ya madam

Niliinuka kinyonge kufuata madam Nasra nili enjoy safari Ile fupi kutoka darasani kwetu Hadi ofisi ya Madam Nasra

"Ingia ndani!" aliniamrisha 


Endelea na sehemu ya 2


Niliingia ndani ya ofisi ya Madam Nasra, ofisi yake ilipangika vizuri.

Tofauti kubwa ya shule hii na shule niliyotoka ni kuwa huku kila mwalimu ana ofisi yake, ilihali Kule Kenya walimu husongamana pamoja kama wauza nyanya sokoni hata afadhali sokoni maana kelele huwa pale kwenye ofisi yao wee usiseme, haya fanya KOSA ndugu utaona moto.


Nilijikuta na kaa kitini kilichokuwa mbele ya meza yake Nasra

"Nani kakuruhusu ukae" alizungumza kwa ukali Nasra

Niliinuka haraka maana yeye hana masiara

Nasra alifungua moja ya kabati na kutoa kijiredio, kilichonishangaza ni kasi aliyotumia kufungua kabati ile na kutoa redio hio, kasi hiyo si ya mtu wa kawaida

Nilijikausha nini kinafuata.


"Unajikuta mjanja sio"

"Ujanja unatoka wapi" pia mimi nikauliza 

"Unajifanya hujui" Nasra alibonyeza batani ya redio hio 

'Duh ! nimeumbuka


**********

Msitu wa Kerugoya

"Unadhani watafanikiwa kweli"

"Tuombe Mungu misheni iishe vyema"

"Hayo ndio maombi yetu lakini ni mwaka wa pili sasa"

"Najua lakini uwepo wa Nasra utarahisisha kazi"

"Mmmh utazidisha ugumu wa kazi Kwa Abdul"

 

Hayo yalikuwa majibizano ya vijana wawili waliokuwa wameloa jasho mwili mzima licha ya kijibaridi cha eneo hili.

"Mbona useme uwepo wa Nasra utazidisha ugumu wa kazi ya Abdul"

"Sababu ni misheni bubu hawastahiki wajuane lakini mkuu alikosea sana kuwaweka mahali pamoja"

"Kwani walienda mahali pamoja basi hiyo sio misheni bubu"

"Mkuu alimwambia Nasra, asimpe nafasi Abdul amtambue"

"Master D, Acha hizo bana nadhani hujui misheni bubu"

"Lee si nakwambia ukweli mimi"

"Dah basi Nasra kashaliwa na Abdul tayari Yule mwamba hapimi Kwa totozi Yule" 

Kisha Lee aliachia kicheko hafifu


"Ni ngumu lakini" alisema master D

"Hakuna mkate mgumu mbele ya chai"

"Lee ndugu yangu inaonekana hujui hii misheni ipoje"

"Kabisa huwa sifuatilii misheni isonihusu"

"Haya basi nakutonya Abdul kaenda Tanzania kama mwanafunzi naye Nasra kaenda kama Mwalimu tena shule ni ile ile ya mtakatifu George mjini Arusha"

"Duh kweli lazima wajuane hilo nalo lipo wazi"


"Hebu tumalize ya huku Murang'a tuende zetu Voi bana"

"Kabisa ndugu" master D aliunga mkono

"Lakini ndugu Lee hivi ya REJECT KAYUMBA yaliishaje"

"Dah! Mwanangu yanasikitisha ya Yule mwamba"

"Mbona alikuwa mtu mweledi kwenye kikosi chetu hakuna wa kumfika lakini cha kushangaza wakamfukuza"

"Hujui ee Jeshi letu liligundua REJECT KAYUMBA ndiye Yule Yule aliyehusika katika mauaji ya Frankoo Sari na aliyetoboa siri ni huyo ambaye yuko Tanzania; Abdul" alieleza hayo kijana huyu anayeenda Kwa jina la Lee

"Lakini hakuna ushahidi kuwa Manu alimuua Frankoo Sari"

"Ndugu yangu REJECT KAYUMBA alikuwa ni anyongwe baada ya kugundulika kuwa ndiye Manu, lakini cha ajabu alitoweka siku ya hukumu"


"Lee, yote ulijulia wapi haya, na inamaana kuna mambo yanaenda kimya kimya jeshini mwetu"

"Unajifanya unajua mengi mbona hili hulijui" Kisha Lee aliachia kicheko kilichomkera master D

"Hadi hili la misheni ya Tanzania hulijui wewe"

"Dah! Kweli hata misheni hiyo sijui inahusu nini nachojua ni misheni bubu basi"

"Sasa unafanya nini jeshini tena katika kitengo nyeti kama hiki chetu"

"Kama ulivyosema awali misheni isiyo kuhusu haina haja ya kuifuatilia"

"Acha ni kuchanue kidogo, hata hili la Tanzania linamuhusu REJECT KAYUMBA"

Master D aliangua kicheko na kumtazama lee, inaonekana hakuamini alichosema Lee

"Huamini kama Hujui REJECT KAYUMBA na Abdul ni maadui hawali sahani moja wale"

"Lakini jeshini tunajua wale marafiki, hadi mafunzo Yao yote walijifunza vyuo vimoja kila walipoenda"

"Kuanzia leo jua Manu ndiye REJECT KAYUMBA na ndiye anasakwa na Abdul na Nasra huko Tanzania. Hebu tukaungane na wenzetu muda ndio huu"


Lee na Master D walitoka pale walipokuwa na kuanza mbio kuelekea kusini.


********

"Abdul" aliita

Duh nilihisi nimesikia Vibaya alivyoniita Madam Nasra jina Abdul linajulikana Kenya tena ndani ya kikosi nyeti ndani ya Jeshi letu upande wa usalama wa taifa iweje mtu huyu aniite Abdul

Nilijikausha kujifanya sijasikia kauli ile

"Abdul si na kuita ama umelisahau jina lako na kuliganda Hezron wazir"

Sikuamini, sikujua huyu ni rafiki ama adui hivyo nilijikausha tu

"Mbona madam sikuelewi unaongelea nini" nilijifanya simuelewi Nasra maana sikujua kama ni rafiki ama ni adui

"Ooh hunielewi"

Nasra alibonyeza batani ya kile kijiredio na sauti hiii ilisikika 

Ni sauti ninayo ijua vyema sana kijasho chembamba kilianza kunitoka

"Hey Abdul ni mwaka wa pili sasa unanitafuta, njoo kwenye Ile kambi ya Romeo nipo huku ndugu na Mrembo wangu Angel" kisha sauti ile ilimaliza Kwa kicheko

"Bado huelewi Abdul"

"Sikuelewi madam unaniita Abdul na ilihali wajua Jina langu ni Hezron, na haya yanahusiana vipi na masomo"

"REJECT KAYUMBA yupo mtaani na nipo hapa kukupa nguvu hivyo acha maaigizo"

Nasra muda huu alinikazia macho

"Sasa sauti hiyo umeitoa wapi"

"Makao makuu Nairobi kutoka Kwa Project Wendo"

"Sina taarifa ya uwepo wako, na hata kama kulikuwa na haja ya kuongeza nguvu inafaa iwe bubu mbona umejitambulisha"

"Jeshini kuna wasaliti ndio maana"

"Bila Shaka unaitambua kambi aliyosema"

"Yap naijua lakini hatuwezi kuenda maana hatuna vifaa hivyo na nligundua toka usiku ule alipotoroshwa"

"Alitoroshwa" Nasra alishangazwa na kauli hiyo


Nligundua KOSA langu, maana jeshini wanajua

 Manu alitoroka 'duh Abdul mie nimekuwa mzembe kiasi hiki dah ama ni uzuriwe unanichanganya'

ITAENDELEA 

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hadithi hizi zinmuingiliano hivyo kupata mtiririko wa KOSA LANGU ni uzisome hadithi zifuatazo pia
    Siku Isiyo Na Jina
    Reject Kayumba

    ReplyDelete
  2. Hadithi ipo vizuri aiseee

    ReplyDelete

Your Thoughts