RIWAYA: JESTINA
MTUNZI: Tariq Haji
CONTACT: +255624065911
SEHEMU YA TATU
ENDELEA.
Maisha yalisonga mbele huku walimu wakivutiwa sana na juhudi za wawili hao japo walikuwa magenius, hatimae walimaliza high school na kujiunga na college. Sasa Alwin alikuwa na umri wa miaka kumi na saba na Jestina alikuwa na umri wa miaka kumi na sita, uzuri wa Jestina ulizidi kunawiri huku ukitii kanuni za kibaolojia. Macho yake makubwa yalimpendeza yakisindikizwa na uso wa duara uliopambwa na pua ndogo nzuri pamoja na mdomo wenye lipsi ambazo muda wote ziling'aa. Hakuwa na kifua kikubwa lakini kilitosha kumueleza rijali yeyote kuwa tayari kifua hicho kilishamea vya kutosha, kiliambatana na mdidimio mkubwa kiunoni na hips zilitanuka vizuri sana huku zikiruhusu mwili huo uonekane kama nambari nane ambayo imeandikwa na fundi alieumba kila kitu. Kwa kweli uzuri wake ulipitiliza sasa na kuanza kuwachanganya walimu pamoja na wafaunzi na kila aliepishana nae njiani. Wapo waliojikwaa na kudondoka, wapo waliokosa kupata ajali kwa kumshangaa pindi anapopita, lakini kwa Alwin yote hayo yalikuwa yakawaida sana ukizingatia yeye amekua nae. Wakiwa college ukaribu wao ulimjengea uhasama mkubwa Alwin na kujikuta akipewa vitisho mara kwa mara. "Jestina na Alwin munaitwa ofisini" aliingia mwanafunzi darasani na kutoa tangazo hilo. Bila kuchelewa waliinuka na kuelekea ofisini walipoitwa.
"Vijana najua mtakuwa na maswali kwanini nimewaita" aliongea mwalimu mkuu huku akiwaangalia wawili hao kwa makini. "hivi punde tu nimepokea barua kutoka wizarani kuwa kumeandaliwa mashindano ya kielimu kwa ajili college zote hapa mjini na kwa kweli sisi tumekuwa wa mwisho kupata taarifa hiyo na mashindano yanatarajiwa kufanyika kesho kutwa" aliendelea kuongea mwalimu mkuu. "Maswali yanahusu nini" aliuliza Jestina,
"mengi yatakuwa ya kielimu hususan upande wa sayansi" alijibu mwalimu. "sawa sisi tumekubali kuiwakilisha shule" walijikuta wakiongea kwa pamoja kisha wakaangaliana na kutabasamu.
"sawa basi mnaweza kwenda tukutakane kesho kutwa asubuhi" mwalimu mkuu aliwaruhusu na wao wakaondoka na kuelekea darasani huku kila mmoja akiwaza itakuwaje siku hiyo ambayo hata maandalizi hawakuwa nayo.
Muda wa mapumziko ulifika na wanafunzi wote wakatika madarasani kuelekea sehemu tafauti. "Habari yako Jestina" ilikuwa ni sauti iliotokea nyuma ya Jestina, "safi" alijibu huku akigeuka na macho yake yakagongana na kijana Matt, kijana huyo ni mtanashati sana na wengi wamempa jina la HANDSOME.
"tunaweza kuongea kama utakuwa unanafasi" aliomba Matt, "sawa hamna shida" alijibu, hiyo ni sifa kubwa sana aliokuwa nayo Jestina, hakutumia uzuri wake kuwanyanyasa watu kama walivyo waschana wengi. Waliongea mengi lakini madhumuni ya kikao hicho ilikuwa ni kijana Matt kumueleza Jestina hisia zake juu yake, na alionekana ni bingwa katika tasnia hii ya kutongoza maana hakuwa na historia ya kukataliwa na mwanamke yeyote yule aliemfata. Basi Jestina aliomba muda ili atafakari ombi hilo na kijana Matt hakufanya makosa ya kukubaliana na ombi hilo.
**********************
"mwanangu sidhani kama kuna mtu atakaeweza kumtongoza Jestina", "ah lakini yule si ana bwana wake ". "yupi" ,"si yule genius mwenzake", kiliskika kiundi cha vijana kadhaa wakiongea na wengi walionekana kuwa na uchu wa kumvua nguo msichana huyo mrembo kuliko wote college hapo. "hakuna mkate mgumu mbele ya supu nyinyi" hapo ndipo ikaskika sauti ya Matt, "lakini mkate ule sidhani" mmoja aliongea. "ok, ikiwezekana je mtanipa nini" aliongea Matt kwa kujiamini. "we kama kweli unajiamini nenda kuhusu malipo ukishafanikiwa tutajua sisi tukupe nini" mmoja wao aliongea na wengine wakamuunga mkono. "basi siku mbili tu, ya tatu atakuwa kashakuwa wangu" aliongea Matt na kuondoka huku akijiapiza kuwa lazima ampate kwa njia yeyote ile hata kama haitakuwa nzuri.
"Alwin nishauri kitu" Jestina aliongea wakati akiwa rafiki yake kipenzi, "kitu gani hicho" Aliuliza. "si unakumbuka niliwahi kukwambia kuwa nampenda Matt", "ndio". "sasa leo muda wa mapumziko kanifata na kunambia ananipenda". Kwa kweli ulikuwa ni wakati mgumu sana kwa Alwin kumshauri Jestna hasa ukizingatia yeye pia alikuwa akimpenda sana lakini alipenda muda wote Jestina awe na furaha. "mimi nikushauri nini tena zaidi ya kukuona ukiwa na furaha" Alwin alijikaza na kuongea japo alielewa ndo kashamkosa tayari. Jestina alimkubatia Alwin kwa furaha bila kujua ni kwa jinsi gani Alwin ameumia, hii ndio inakuwa shida kwa magenius wengi wanashindwa kugundua kwa muonekano fulani basi mtu anakuwa yupo katika hali gani. Wao hujali furaha yao tu, na ndivyo ilivyotokea baada kumkumbatia aliinuka na kuenda kwao akiwa mwenye furaha sana na uzuri ulizidi mara dufu.
Alwin aliinuka na kuelekea kwao huku njia nzima akiwa ni mwenye mawazo kupita maelezo, usiku huo ndio ulikuwa usiku mrefu ambao hajawahi kuuona tokea azaliwe. Palikucha na kama kawaida wanafunzi wote alienda mashule, siku hiyo ilikuwa ni siku mpya kwa Jestina ambae alionekana kupebdeza kupita maelezo. Muda wa mapumziko ulipofika alimwita Matt na kumwambia kuwa amemkubalia ombi lake, Matt alijpongeza kwa ushindi ule japo moyoni hakumpenda hata kidogo na alifanya vile kuwaonesha kama yeye next level. Maisha mapya ya kimapenzi yalianza kwa Jestina lakini kwa Alwin yalikuwa ni magumu hayajawahi kutokea.
Siku ya mashindano ilifika, mapema asubuhi Alwin na Jestina walichukuliwa na kupelekwa katika ukumbi ambao ungefanyika mashindano hayo yaliokuwa yanatarajiwa kurushwa live kati runinga. Saa mbili mashindano yalianza na kweli yalipamba moto huku timu ya magenius hao ikiogoza kwa kupata alama nyingi sana na mpaka mashindano yanakwisha waliondoka na alama elfu moja bila kukosa swali hata moja. Walirudi shuleni na kupokewa kwa shangwe kubwa sana na kuambiwa wajiandae kwenda mashindano ya kitaifa ambayo ilikuwa ni hatua ya pili kuelekea mashindano ya kimataifa. Kwa muda mfupi tu alioingia katika wimbi la mapenzi Jestina, urafiki wake kwa Alwin ulianza kupungua kwa kasi. Japo Alwin alijitahidi kuwa karibu nae lakini yeye alionekana kumtenga na mapenzi yake yote aliyahamishia kwa Matt.
Unyonge na upweke ulianza kumtafuna Alwin,
"nikiruhusu hali hii ya upweke iendelee itaniathiri kisaikolojia, sasa ni muda kukubali kuwa Jestina nimeshanpoteza" alijisemea moyoni wakati akiwa peke yake. Baada ya kusema hivyo akili yake ilikubaliana nae na kuanza maisha mapya ambayo ndani yake hayakuwa na Jestina zaidi ya yule aliemzoea tokea udogoni kwake. Kuna wakati ilifikia hata salamu yake ikawa haiitikiwi na Jestina lakini wala hakushtka wala kuacha kumsalimia. Taratibu ubongo wa Jestina ukaanza kufanya kazi ndivo sivo, muda mwingi alimfikiria Matt badala ya kusoma hivyo kuanza kuathiri hata maendeleo yake ya kimasomo.
Alwin alijaribu kumueleza lakini sasa alionekana kama adui yake, kuna wakati alimtolea maneno ya kashfa kama vile
"achana na mimi sio wa aina yako",
"kwani we baba yangu mpaka unambie ninacho fanya ni kizuri au kibaya". Alwin hakuamini kama maneno hayo yalitoka kinywani mwa rafiki yake kipenzi
"ama kweli mapenzi ni ulemavu" alijikuta akijisemea maneno hayo baada kukaripiwa na Jestina mbele ya umati wa watu.
"hapa ni katika nyumba ya ibada usipokuja kwa kusali basi utakuja kwa dhiki au kuagwa lakini utakuja tu" Alwin aliongea maneno hayo kwa nguvu na kupenya sawa sawia katika masikio ya Jestina na alipogeuka alimuona Alwin akitokwa na machozi.
Bila kuongea neno jingine lolote aligeuka na kuelekea kwenye gari yake na safari ya kuelekea kwao ikaanza. Kwa mtu mwenye akili za kawaida alielewa maneno yale yalimaanisha nini lakini kwa Jestina kutokana uelewa wake mdogo juu ya kutambua hisia hakuyaelewa kabisa akabaki anacheka tu na kumfanya kila mtu kumshangaa.
Hata hivyo Jestina aliwapuuza watu waliokuwa wakimshangaa,
"hivi kweli Jestina wewe leo ni wa kumdhalilisha rafiki yako kipenzi tena mbele za watu" Miryam ambae ni rafiki mkubwa pia kwa Jestina alimuuliza. "na wewe usianze kuwa kama Alwin niache na maisha yangu
" alijibu kwa kejeli, "laiti ungeujua uzito wa maneno aliyoyasema wakati anaondoka basi ungemkimbilia na kumuomba msamaha" aliongea mwanamke huyo ambae alionekana kusikitishwa na mabadiliko ya Jestina.
"au wewe unamtaka Alwin, sema kama unamtaka nikuunganishie" Jestina aliendelea kujibu utumbo,
"kwa taarifa yako bibie kila mwanamke hapa shule anatamani kuwa na mwanaume kama Alwin, mwanaume ambae anajua thamani ya mwanamke, mwanaume ambae hakubali kuona mtu wake wa karibu anakunja uso, mwanaume ana utu na anajua kama mwanamke ni wa kuheshimiwa na sio kufanya kama mdoli" aliongea maneno hayo kwa ukali huku akimuangalia Jestina kwa macho makali
"halafu unasema kama namtaka Alwin uniunanishie, wewe mapenzi umeyajua juzi tu tena kwa taarifa yako kwa Matt umebugi step shosti, subiri akutanue miguu tu uone kama atakuthamini tena. Hebu zunguka uulize waschana wangapi walihadaika na uzuri wake lakini baada kuwavua chupi amewatupa. Kwa Matt mwanamke ni kama tishu tu, ukishaaitumia mara moja unaitupa na kwa taarifa yako sina haja ya wewe kuniunganisha mimi kwa Alwin. Nimeridhika na upendo wa kirafiki anaonionyesha tafauti na wewe. Mwanamke gani usie na fadhila, hustiriki kama harufu ya mavi au kwa sababu unaakili nyingi ndio unamuona kila mtu bwege. Pole kwa hilo na kama nimekukasirisha kunya boga" Miryam aliongea kwa hasira sana na alipomaliza hakusubiri jibu aligeuka na kuondoka maana alielewa kukaa pale kungezuwa matatizo.
Ukweli Miryam anampenda sana Alwin lakini baada kugundua kuwa Alwin ametokea kumpenda Jestina hakutaka aingilie kati na badala yake aliomba kuwa rafiki wa Alwin na Jestina ombi ambalo lilipokewa kwa mikono miwili na marafiki hao. Miryam ni mtoto wa tatu katika familia nambari moja kwa utajiri katika mji wa Mashvile, ni mschana mrefu mwenye asili ya kivenezuela na weupe wa kungaa. Kichwa chake kilipambwa na nywele za kimanga zilizonyooka kama nguo iliopigwa pasi, Kwa bahati mbaya yeye ndie mtoto pekee alieyepona katika ajali ya moto ulioteketeza nyumba yao akiwemo mama yake pamoja na kaka na dada yake. Kwa sasa anaishi na baba tu ambae kwake ndie baba na ndie mama.
Itaendelea...
Your Thoughts