NGOJA NILEWE 5

 NGOJA NILEWE  5



MTUNZI: Mbogo Edgar


Naaam miezi miwili toka Daniel aanze kazi kwenye kiwanda cha FSC, mala dalili zakuporomoka kwa afya kwa mtoto Samuel, ilianza kuporomka, uku tatizo likiwa ni kuarisha, na homa za mala kwa mala, Sebastian alipo hoji kulikoni, akaambiwa kuwa ni swala la kawaida kwa mtoto anapoota meno, ilo lilithibitishwa na Sophia, japo zilipita siku kadhaa bila kuonekana kwa jino, wala dalili ya jino kwa mtoto mtoto wao. *****,…… . ENDELEA……..


Ata siku moja usiku, mida ambayo Sebastian akiwa na mke wake chumbani, akaona dalili ya mke wake kuanza kumchezea dudu, “mama Sam, siunajuwa mwezio nina hamu ya muda mrefu, alafu unashika hiyo kitu” alisema Sebastian kwa sauti ya kutoa tahadhari, “baba Sam mwenzio nimeshindwa kuvumilia, tufanje tu mala moja, nitaenda kuoga kabla sija mnyonyesha” alisema mama Samuel, na hapo wakakubariana wafanye hivyo, lakini kabla awajafanya lolote, ghafla mama Samuel yani Adellah, akachomoka mbio kuelekea bafuni, ambako akasikika akitapika vibaya sana, alitumia dakika kadhaa kutapika, kabla ya kurudi kitandani, “utakuwa na marelia, iinabidi ukatibiwe haraka kabla ujamwambukiza mtoto” alisema Sebastian, huku anajifunika shuka, “kwahiyo ndio umeghairi?” aliuliza Adellah, kwa sauti ambayo ilionyesha kama vile amekasirika, “sizani kama tuna haraka kiasi hicho, nenda ukatibiwe kwanza, aya mambo yapo tu” alisema Sebastian, ambae akuonyesha dalili ya kula kitumbua.


Ukweli ata leo ukimwiliza Seba kwa nini alikataa kula kitumbua, hakika awezi kueleza sababu ya mzingi, maana ukiachilie yeye mwenyewe kuwa na hamu kubwa ya kula kitumbua, ila pia Adellah, mwenyewe, mwenye kuijuwa afya yake, alisha sema kuwa anaweza kuendelea kuikabiri dudu, walilala bila kusemeshana mpaka siku ya pili Seba alipoenda kazini, ndiyo siku ambayo, Seba aliporudi nyumbani alikuta kuna udogo na limao, lililo lambwa kwa mdomo, hii ilionyesha wazi ni dalili ya ujauzito, ilimshtua sana Sebastian, ambae usiku ule alimshuhudia mke wake akitapika tena.


Ukweli kijana wetu asiku iliyofuata mida ya saa nne, alimuaga mhasibu mkuu, akimweleza juu ya matatizo aliyo yahisi kwa mke wake, kisha akatoka, na kuelekea kwenye ya kiwanda, ambako alifanikiwa kuongea na nurse mmoja, akimweleza juu ya alili za mke wake, ambae akumwingilia kwa muda mrefu sababu ya kunyonyesha, “aiwezi kuwa ujauzito, labda akapime maralia, maana kama ananyonyesha, mtoto mdogo, lazima ungeona dalili mapema tu, kamavile mtoto kuzorota kiafya, kuarisha na kupungua uzito” maelekezo ayo ya nurse, yali chemsha kichwa cha Sebastian, maana aligundua kuwa mke wake anadalili za ujauzito, na siyo kwamba alipata ujauzito, wakati mtoto mwingine akiwa mdogo, ila ni kwamba “mimba hii ameipata toka wapi, wakati sijamgusa kwa miezi nane sasa?” alijiuliza Sebastian, kwa sauti ya kunong’ona, na kumshangaza yule nurse, ambae akuweza kutia neno lolote, na kumwona kijana huyu, anatoka taratibu, nakuelekea ofisini kwake.


Seba akiwa ameshindwa kabisa kuelewa kilichotokea, alitamani kumweleza shemeji yake Daniel, lakini akaona aitakuwa vizuri kwa yeye kumweleza Daniel mambo yanayo muhusu Adella, hivyo nivyema kama ata enda kumweleza Sophia, hukweli Seba alishindwa kukaa ofisini, akaenda kwa mhasibu mkuu, na kumweleza kile anacho kabiliana nacho, kisha akamwomba luksa ya kuelekea nyumbani kwaajili ya kuweka sawa jambo ilo, akiwa kama amechanganyikiwa, muda wote aliganda kama sanamu, anawaza nakuwazuwa kama ni kweli mke wake atakuwa mjamzito, niwapi ametoa mimba hiyo, na kwanini amsaliti, na kama ni kweli achukuwe hatua gani, maana pasingekuwa na siri, kuwa mke wake amemsaliti, je amuache na mtoto wake aishi na yeye bila mama, au amwache na mama yake aishi bila yeye, hakika ilikuwa nimtiahani.


Siku ile seba aliondoka mapema kidogo, ata Daniel ilimlazimu kupanda daladala, wakati wakurudi nyumbani, wakati huo Seba alikuwa amepitia nyumbani kwa Sophia, na kumweleza mashaka yake juu ya ujauzito wa Adellah, “mh! shemeji, ni wasi wasi wako tu, atakuwa anaumwa homa, ukweli namfahamu Adellah, awezi kufanya hivyo ata siku moja, yani achilia kutembea na mwanaume mwingine wakati ananyonyesha, ile kukusariti tu awezi” alisema Sophia kwa kujiamini.


Hii kidogo ilipunguza wasi kwa Sebastian, ambae alirudi nyumbani na kukuta mke wake, akiwa amelala, akuwa amepika chochote, jikoni kulikuwa na juice ya malimao, hakika ilimwacha njia panda Sebastia, ambae alitamani kupata jibu haraka iwezekanavyo, japo sidhani kama alipata bahati hiyo.


Jioni ya saa kumi na mbili, Sophia nae alifika nyumbani kwa Sebastian, akidai alikuwa anatokea sehemu akaona nivyema kipita kuwasalimia, waliongea maili matatu, kisha Adellah akamsindikiza dada yake, japo alitumia muda mrefu, lakini aikizidi saa moja, akarudi akiwa ameongozana na kaka yake Daniel, aliekuwa anatoka kazini, lakini alionyesha utulivu wa hali ya juu, kama vile kunajambo amelisikia juu ya hiki kinachoendelea, Seba alihisi kuwa Sophia amesha msimulia mdogo wake, kwahiyo ata Adellah mwenye pia atakuwa amesha fahamu mashaka ya mume wake, lakini mpaka wanaingia kitandani, akuna alie mgusia mwenzie juu ya swala ilo. ******


Naaam siku ile Sebastian alilala akiwa na mawazo mengi sana, juu ya dalili za mke wake, japo alihakikishiwa na Sophia kuwa mdogo wake, kuwa akuwa na ujauzito, na asingeweza kufanya jambo ilo la kipumbavu, ata siku ya pili asubuhi alienda kazini pasipo kumweleza au kumwuliza chochote mke wake, ila alipanga kuwa jioni ya siku ile, angeongea na mke wake juu ya wasi wasi wake, ili wajuwe wanafanyaje, msikini Seba akujuwa kuwa, pengine huo ndio ungekuwa mwisho, wa yeye kuwa na Adellah, kama mke wake.


Yap! Sebastian akiwa na shemeji yake, walienda kimya kimya, huku wote wakionekana kuwa na mawazo mengi sana, ni wazi ata Daniel alisha fahamu kuhusu ujauzito wa dada yake, na alikuwa anasubiri kuelezwa kilichotokea, na ata walipovuka tu, Daniel akamwomba sehemeji yake amshushe, “samahani sehemeji, naomba uniache hapa, kuna mtu naonana nae, kazini nitakuja baadae kidogo” alisema Daniel, na Seba akasimamisha gari, Daniel akafungua mlango na kushuka, “alafu Dani kuna ishu tutaongea mida ya chai” alisema Sebastian, kabla ajaondoka, akujuwa huo ndio ulikuwa mwisho wa yeye kuongea na Daniel kama shemeji yake.


Ilikuwa hivi, Seba alikaa ofisini mpaka mida ya saa tatu kasoro, pasipo kumwona, Daniel at mida ya chai ilipofika akainuka na kuelekea canteen, ambako alikutana na yule mhasibu mkuu, “niambie Seba, swala lako linaendeleaje?” aliuliza mhasibu mkuu, ambae ni mtu mzima hivi, alie faha kika kwa jina la mzee Ngimba, “yani kaka atasijuwi nisemeje, ila dalili zinaonyesha wazi kuwa ni mjamzito, japo nimeongea na dada yake, ameniambia kuwa itakuwa ni homa tu, na kwamba mdogo wake awezi kutembea na mwanaume mwingine” alieleza Sebastian, “lakini dogo, kwanini kesho usimpeleke wewe mwenyewe hospital, ongea na madoctor kwamba wanampima maralia lakini wamchek ujauzito, nivyema kama utapata jibu, kuliko kukaa katikahali kama hii” alisema mzee Ngimba, na Sebastian akakubariana nae, “ilo wazo zuri, wacha niombe luksa ili kesho nifanye hivyo” alisema Sebastian ambae akujuwa kama amechelewa.

Maana wakati wanatoka pale canteen, akiwa namhasibu mkuu, mala wakashangaa kuona kuna gari la polisi, likiwa limesimama nje ya jengo kuu la ofisi, huku polisi kadhaa wakiwa nje ya yagari, pamoja na manager wa kiwanda, “yulepaleeee” alisema manager, huku anaonyesha kidole kule wanakotokea wao, ni wazi alikusudiwa mmoja wao, kati ya Seba na mzee Ngimba, nao wakashangaa, sababu awakuwa na kumbu kumbu ya kutenda kosa lolote.


Hapo wakawaona polisi wawili wakiwa na yule meneja wao, wanaanza kuja upande waliokuwa wanatokea wao, na walipo wafikia wakasimama mbele yao, “huyu hapa ndie mwenye ofisi, anaitwa Sebastian Samuel” alisema meneja, huku wote wakimtazama Sebastian, “bwana Sebastian hupo chini ya ulinzi kwa kosa la kupatikana kwa bangi ndani ya ofisi yako, kama auto leta ushirikiano nguvu itatumika kukufikisha kituoni” alisema mmoja kati ya wale polisi, na kuwaacha midomo wazi Sebastian na mzee ngimba, “jamani mimi, bangi ofisini kwangu, toka lini mimi naweka bangi ofisini kwangu” alisema Sebastian kwa kulalamika, lakini akuna alie alie msikiliza, zaidi ata meneja na mhasibu mkuu, pamoja na wafanyakazi wengine walionekana wakishangaa, juu ya tukio lile.


Seba akabebebwa na polisi, na wakati wanaondoka, akakumbuka jambo, “samahani mhasibu utampatia hii funguo Daniel akija, mweleze kilicho tokea” alisema Sebastian huku anakabidhi funguo yagari, kwa mhasibu mkuu, “mbona Daniel yupo muda mrefu tu” alisema mmoja kati ya wafanya kazi aliekuwepo eneo lile, Seba akuizingatia hiyo, wala kujiuliza kwanini kama Daniel alikuwepo muda mrefu akuonekana ofisini, sababu tayari alikuwa katika mkasa mzito.*******


Naaam saa moja narobo, adellah anasikia ngurumo ya gari ikiingia pale nyumbani, ana fungua mlango haraka na kukimbilia kwenye gari, anamwona Daniel anashuka toka kwenye seat ya Dereva, “usiniambie kama umefanikiwa” anasema Adellah, kwa sauti yenye kihoro, “wewe unazani mchezo, mipango ya watu wazima aishindwi” anasema Daniel kwa sauti ya majisifu, nakujimwambafai, huku anazunguka nyuma ya gari, na kufungua mlango wa nyuma kabisa, “weweeeee unasema kweli Dani” Adellah anashangangilia kwa nguvu, huku ana mrukia Dani mgongoni, katika hali ya furaha iliyo pitiliza“kwanini nikudanganye, mtu wako yupo mahabusu, anasubiri kuingia mahakamani” anasema Daniel, huku anashusha sanduku lenye kujaa bia, “kwahiyo leo kwaraha zetu” alisema Adellah, huku anasaidiana na Daniel kuingiza sanduku la bia ndani, ambako awakukaa sebuleni, waliacha sanduku na kuingia chumbani, moja kwa Sebastian moja kwa moja, kule chumbani ungesema ni wapenzi walio miana muda mrefu, walianza kunyonyana ndimi zao huku wakisaidiana kupembuana nguo, kisha wakaanza kupeana dudu.


Nusu saa baadae wakiwa wamesha toka chumbani, wanaendelea kunywa bia huku wamejawa na furaha, mala Sophia nae anakuja, na kuwa kuta Adellah na Daniel wakiwa katika hali ile ya furaha, na ulevi wa bia, “Adellah, kumbuka unaumimba, usinywe bia nyingi” alisema Sophia, huku anakaa pembeni na kuchukuwa chupa moja ya bia, “wacha ni burudike japo siku moja moja” alisema Adellah, mwenye furaha na shangwe kubwa, “hongereni kwa kushinda vita hii kubwa, maana kwa dalili hii nazani mpango umefanikiwa” alisema Sophia, huku anafungua bia kwa maneno, “mtoto mdogo yule awezi kunishinda mimi” alisema Daniel kwa kujiamini, sawa Shemeji, lakini ndio mfanye haraka mambo yenu, kila kitu kikae sawa, maana akitoka huko jela, ujuwe kila kitu kita kuwa wazi, atagungua ata Sam siyo wa kwake” alisema Sophia, ambae alinishangaza ata mimi, ambaesijuwi kinachoendelea. 

Jamani kwa hii imekaaje, mbona mambo yameenda kasi namna hii, hapa lazima tuujuwe ukweli, ladda tufahamu jambo ili toka mwanzo wake. ********


 Hipo hivi, Daniel na Adellah ni wapenzi wa muda mrefu sana, tena toka kijijini Lufilyo, na wala siyo mtoto wa baba mkubwa kama alivyo tambulishwa Danel, penzi lao lilianza wakiwa darasa la tano, mpaka walipomaliza Sule ya msingi, walikuwa wamesha achana mala kadhaa na kurudiana tena, sababu nyibgi zikiwa ni Daniel kupata mpenzi mwingine, ata anapoachana na mpenzi mpya, aukuwa kazi ngumu kurudiana na Adellah, ambae kwa kiasi kikubwa, alikuwa anampenda sana Daniel.


Naaam miaka minne, ya mapenzi na usaliti, toka wawili awa wamalize darasa la saba, Daniel aliondoka Mbeya kuelekea Dar, huku akiwa amepeana ahadi nyingi na mpenzi waka Adellah, kwamba baada ya kufanikisha kupata kazi huko dar, anakoenda kutafuta maisha, basi angetuma nauri na ili aende dar wakaanze maisha, hakika waliamini kuwa dar maisha ni malahisi sana, japo nikama msemo huo unaukweli ndani yake, maana maisha ya dar, utafanikiwa endepo utaitambua nafasi yako, mfano ukiwa wa kubeba mizigo, simama imara beba mizigo, utakula ulala utaoa na kuendelea kuishi, kama ni waofisini pambana na ofisi yako, maisha yaendelee, nakama ni mwizi pambana na wizi wako, maana kila siku watu wanazidi kujisahau, lakini ukikamatwa nazani unafahamu kinacho fwata.


Naaaam Daniel alifika dar es salaam na kumkuta mwenyeji wake, ambae alikuwa anaishi mbezi, maeneo ya kibanda cha mkaa, lakini mazingira ya makazi ya mwenyeji wake, ndiyo yalimshangaza Daniel, maana alikuwa anaishi na wenzake watano ndani ya chumba kimoja, ambacho siyo tu kuwa akikuwa na umeme, ila pia chumba hiki akikuwa na kitu chochote zaidi ya ndoo mbili zilizo fubaa kwa uchafu, na vipande vya mabox, vilivyo tandikwa sakafuni, vikiwa vime tandikwa vipande chakavu vya shuka, ambavyo ata ungepewa million kadhaa za fedha, usingeweza kutaja rangi yake, ni wazi ilikuwa ndio sehemu ya kulala.


Daniel alie tarajia maisha mazuri, akajikuta anaanza kusaka fedha ya kula mlo wa muda usika, yani kama ni asubuhi angesaka fedha ya chai, na baada ya hapo angeanza kusaka fedha ya chakula cha mchana, aijalishi kama ameipata au la, ila kuanzia mchana na kuendelea angesaka chakula cha jioni, na msako huo wa fedha, aukuchagua kazi, na mbaya zaidi bwana Daniel, alimkuta mwenyeji wake, akiwa anasaka fedha kwa njia isyo halari, kama vile kudokoa kwenye mifuko ya watu, kukaba na ata kutaperi, kwa njia mbali mbali, ikiwepo mchezo maarufu wa karata tatu, mchezo ambao Daniel kidogo aliona kuwa ndiyo sehemu salama, kwa yeye kuingiza fedha, kuliko ile michezo mingine ya kuiba na kukaba, huku fedha ya ziada wanayoipata wakiishia kunywa pombe, na vilevi vingine visivyo faa, akisahau ata kununua nguo nzuri.


Siku zilienda atimae miaka mitatu ikakatika, Daniel akiishia kupata fedha ya kula tu, japo tayari alishapata uwezo wa kujiamini, na kuanza kuiba na kukaba, tayari alisha kamatwa mala kadhaa na jeshi la polisi, ikiwa ni kwamakosa hayo na yale ya udhurulaji, ambapo alihishia kituo cha polisi na kuachiwa, lakini aikuishia hapo, mala mbili Daniel alisha wai kufungwa magereza ya ukonga, moja akisalia ukonga kwa miezi sita, na moja akipelekwa Mvuti kwa miezi saba,


 ni mala baada ya kukutwa na hatia ya kuiba kwenye duka la raia mmoja mbezi kwa msuguri.


Siku chache baada ya kumaliza kifungo chake, Daniel ambae sasa anaanza kazi ya kuita abiria pale stendi ya dala dala ya mbezi mwisho, ana kutana na dada yake Adellah, ambae anamjulisha ujio wa Adellah, ambae licha ya kuaga kijijini lufilyo, kwamba anakuja kutafuta kazi, lakini ukweli lengo lake ni kumfwata mpenzi wake, ambae ndie yeye Daniel, na kwa msaaada wa Sophia, wanafanikiwa kukutana nyumbani kwa Sophia, yani pale walipopanga, wote wanahamu ya kunyanduana, bahati nzuri, dada anawachukuwa watoto, na kuondoka nao, na kuwaachia nafasi wawili awa wapate kuongea, kuhusu maisha yao, na kwamba wataenda kuishi wapi na nilini Daniel angekuja kumchukuwa Adellah, maana tayari Adellah, alishakuwa mzigo kwa dada yake.


Ukweli Daniel akumficha kitu Adella, alimweleza ukweli, “Adella, kwanini umekurupuka kuja huku, wakati ujuwi mwenzio naishije, yani kula yangu nitabu, kuvaa ndio kama hivi, unazani nita kutunzaje, wakati ata sehemu ya kukaa na kaa na wakina Lusajo, kwenye kwenye chumba kimoja kibovu” alisema Daniel kwa sauti ya kulala mika, “sawa basi nigee nauri nirudi mbeya” aliitikia Adellah kwa roho shingo upande, huku sauti yake ikiwa imejawa na unyonge wa hali ya juu, “sawa nita kutafutia nauri, nikipata nitakuletea” alisema Daniel, ambae ukimtazama ata wewe ungetambua kuipata hiyo elfu kumi na mbili ingekiwa kazi ngumu, maana yeyemwenyewe mwonekano wake, ulionyesha wazi kuwa anaitaji fedha.


Naaam maongezi yao yaliisha kwa kupeana dudu, mle mle ndani ya chumba cha dada yake, kisha Adellah akamsindikiza mpenzi wake, huku njiani wakipeana matumaini ya kwamba, hipo siku watafanikiwa kimaisha, na kuishi pamoja katika nyumba yao, ndoto ambayo waliiota toka kipindi kile ambacho Daniel akiwa anatoka mbeya wilayani Lungwe, kijijini Lufilyo.


Kutokana na jinsi Sophia alivyo mwona Daniel, aliamini kuwa hapakuwa namaisha kati yao, zaidi Adellah angeingia katika maisha ya tabu, lakini akuwa na la kufanya, maana apakuwa na ubishi kuwa, mdogo wake alikuwa amesha mpenda sana Daniel na analifahamu ilo toka wawili awa wakiwa wadogo, ata sasa aliona wazi jinsi Adellah, alivyo pata tabu siku ambazo zinapita bila Daniel kuonekana, kuja kumtembelea, japo akuwai kupitisha siku tatu au nne bila kuonekana nyumbani kwa Sophia,  na alipokuja tu, Sophia angewapisha na kuwaachia nafasi ya kupeana dudu, japo ilikuwa ni mzigo kwao, maana Daniel ambae akuwai kuja na kitu chochote pale nyumbani, alihakikisha anakula milo yote miwili kama hipo, na mwisho Adellah angemsindikiza, mpaka stendi, ambako Daniel akazuga zuga na kupata lift, ya dala dala, akiwa kama mpiga debe mzoefu wa mbezi mwisho.


Ratiba hiyo iliendelea kwa muda wa mwenzi mmoja tu, ndipo Adellah alipojigundua kuwa ni mjamzito, akamweleza dada yake, ambae sasa aliona kuwa mdogo wake anaenda kutaabika, maana baba wa mtoto huyo, alikuwa ni Daniel ambae akuwa na A wala B, nay eye asingeweza kuishi na siku zote pale nyumbani, maana yeye mwenyewe na watoto wake tu, maisha yalikuwa magumu, mala kuongeza Adellah, na mtoto atakae zaliwa, siingekuwa balaha, “ebu mweleze ajuwe atafanya nini na huo ujauzito” alisema Sophia, na Adellah akafanya hivyo.


Naam Siku moja jioni wakati Adellah anamsindikiza Daniel, akamweleza juu ya ujauzito alionao, nae, “una uhakika kuwa hiyo mimba ni yangu, yani we ukakaa sijuwi mwezi mmoja na nus utu, unanieleza tayari umesha shika mimba” aling’aka Daniel, ambae akukata kukukubari ile mimba, licha ya kumsihi, huku anatokwa na machozi, lakini Daniel akutaka kabisa kukubariana na Adellah, ata safari ya kusindikizana ikaishia hapo, na kila mmoja akashika njia yake, Daniel akaelekea stend, huku Adellah anarudi nyumbani huku anatokwa na machozi.


Alipofika nyumbani Adellah, akamsimulia dada yake, na kumweleza kila kitu, kwamba Daniel amekataa kabisa kuwa mimba siyo yake, “jamani Adellah, na wewe umekubarije kubeba mimba ya Daniel, hali yake yenyewe, ndiyo kama unavyo ijuwa, yani mtu mwenywe wa ovyo kabisa, wenzio wakija dar wanabadirika, aya sasa tutafanyaje?” alisema Sophia, kwa sauti ya lawama na yenyekukata tamaa, “jamani dada sikujuwa kama itakuwa hivi” alisema Adellah, huku anaangua kilio cha chini chini, “hakuna ujanja inabidi tusaidiane kutafuta nauri urudi kijijini, wenyewe siunaona jinsi yalivyo magumu” alisema dada yake Adellah, yani Sophia.


Naam wawili awa walikubariana hivyo, kuwa Adellah, aende mbeya akalee ujauzito wake, lakini shida ilikuwa nivipi watapata hiyo nauri, wakati fedha ya kula yenyewe ilikuwa shida, na walikuwa wanamtegemea bwana Philipo peke yake, kutafuta fedha ya kula, kupitia kazi yake ya vibarua vya ujenzi, kama saidia fundi, kazi ambayo kuna siku alipata na kunasiku alikosa.


Njia rahisi ambayo ilionekana inafaa, ni kwa Adellah, kutafuta kazi ya ndani, ambayo kipindikile ilikuwa maafu kama yaya, sasa hivi watu wanaita kizungu, yani house Girl, kazi ambayo walipanga kama iipatikana afanye kwa muda wa miezi mitatu, ambapo mimba itakuwaimefikisha miezi minne, nae atakuwa ameshapata fedha ya nauri ya kurudia kwao Lufilyo huko wilayani Lungwe.


Lakini aikuwa lahisi kama walivyozania, kila nyumba waliyo enda awakuwa wanaitaji dada wakazi, na bahati mbaya iliyoje ni kwamba, ata Daniel akuonekana tena, kutembelea pale nyumbani kwakina Adellah, hiyo ilizidi kumkatisha tamaa Adellah, na kujuwa kuwa anaenda kulea mtoto yeye peke yake, aikuwa picha nzuri kwa wazazi wake wala kwa wanakijiji wengine, ambao wata toa safthiri ya kuwa alienda mjini kufanya tabia mbaya, ambayo ime msababishia mimba, ya mtoto ambae baba ajulikani, sababu tayari mwenye ujauzito alisha kataa, lakini bahati yake mmwenzi wapili kabla aujaisha akakutana na Sebastian, ambae alifanikisha kumwingiza mkenge, na kumkabidhi ujauzito ule, huku akifwata maelezo yadada yake, ya kumpa unyumba Sebastian kila siku, ili ionekane ile mimba ni yakwake

Kitu ambacho siyo Adellah, wala Sophia walicho kijuwa ni kwamba, siku mbili toka waonane na Daniel, Daniel alishawishiwa na Rusajo wakaibe kwenye duka moja la nguo pale mbezi, na walijipanga vyema kabisa kwenda kutekeleza wizi huo, katika duka ambalo awakujuwa kama linalindwa na mlinzi mmoja aliepitia mafunzo timamu ya mgambo, ambae alipo waona tu akapiga filimbi, iliyofwatiwa na kundi lla walinzi wa maduka ya jilani, walio wazingira wakina Daniel, na kuanza kuwashambulia.


Daniel aliweza kushuhudia Rusajo na wenzake wakiuwawa pale pale, huku yeye akiokolewa na polisi wa doria, waliowai kufika eneo la tukio, ambao walimfikisha kituoni na baadae akafunguliwa kesi ya wizi, ambapo kesi yake iliendeshwa kwa muda wa mwaka mmoja, siku zote akikaa mahabusu ya gereza la ukonga, ata mwisho ukakosekana ushaidi, baada ya yule mgambo alie mkamata kukosekana mahakamani, nayeye akaachiwa na kurudi mbezi, ambako alikuta chumba kile kimesha karabatiwa na kuna mtu amepangishwa, hivyo akaanza kulala pale stendi, huku akijaribu kutafuta fedha kwa kupiga debe, na kubeba mizigo maeneo ya soko la pale mbezi.


Naam wakati huo tayari Adellah, alikuwa amesha jifungua, na kitu ambacho dada yake alimsisitiza, ilikutunza afya ya mtoto, na kuepusha mume wake asije akagundua kuwa mtoto siyo wa kwake, sababu kuna vitu lazima vitokee endapo mwanaume ata tembea na mwanamke anae nyoonyesha mtoto ambae siyo wakwake (ifahamike ni maneno ya kwenye hadithi tu, sija ya thibitisha)******


Siku moja akiwa katika harakati zake, za upigaji wa Debe, ndipo alipopita Roida, huyu ni mwanamke mmoja ambae walisoma nae, shule ya msingi, ila yeye kwa bahati aliendelea na masomo ya kidato cha kwanza mpaka cha nne, na sasa ni mwalimu wa shule ya msingi Uyole, wakat huo alikuwa amekuja kwenye Semina, “samahani kaka, nakufananisha au ni wewe?” aliuliza Roida, kwasauti yenye mashaka, “hooo Roida ni wewe, ujanifanisha ni mimi Dany” alisema Daniel, kwa sauti yenye kujawa na uhakika kuwa yeye ndie mtu sahihi alie kusudiwa, “jamani zamasiku Dani?” alisalimia Roida, huku anamtazama Daniel kwamacho flani hivi, ambayo kwa mtu unaejitambua, ungejuwa kuwa yana ongaea kitu flani, “nzuri tu, vipi unaishi hapa dar au umekuja mala moja?” aliuliuliza Daniel ambae ukimwona, nguo alizo vaa, ungesema ametoka kijijini leo hii, “nimekuja mala moja, nimefikia tumbi, shirika la Elimu, kuna semina ya week moja” alisema Roida, ambae alishindwa kuficha duku duku lake, “hivi Dani imekuwaje mpaka ukaachana na Adellah, maana nilisikia alikuja huku, kwaajili yako?” aliuliza Roida, ambae sasa ni kama alisha sahau kuhusu mizunguko yake.


Kwanza kabisa, katika hali ya kujimwamba fai kirofa, Daniel akacheka kwa dharau, “mpuuzi yule yani anataka kunipakazia mimba mimi, usawa wenyewe huko wapi, vipi kwani alifanikiwa kurudi kijiji, maana ata nauri akuwa nayo” aliuliza Daniel, kwa sauti yenye kujiona mjanja kweli kweli, na hapo ikawa zamu ya Roida kucheka, “Dani acha uongo, hivi ukimwona Adellah wewe utamtambua kweli?” aliuliza Roida na hapo kidogo Daniel akacheka kidogo, akizania ni maneno ya utani ya Roida, yenye lengo la kumrusha roho, “amefanyaje, mpaka nisimtambue?” aliuliza Daniel huku akikunja mdomo kwa dharau, “kwani wewe unamuda gani ujamwona Adellah?” aliuliza Roida, “kitambo sana, yani alipo niambia tu, ana mimba nikaachana nae” alisema Daniel nasafari hii kidogo Rioda akashtuka, ni muda gani umepita?” aliuliza tena Roida, huku kengere ya tahadhari ikigonga kichwani mwake.


Hapo Dani akatulia kidogo akitafuta jibu, kwa kujumlisha muda alio kamatwa kwa kosa la wizi, na kuongeza muda alio kaa jela, mpaka kuachiwa, na miezi aliyokuwa katika msoto wa hapa mbezi, akakumbuka, “nikama mwaka na mwezi mmoja hivi” alisema Daniel na hapo Roida akaganda kwa mshangao, “vipi kwani kuna tatizo limetokea?” aliuliza Daniel kwa sauti yenye tahadhari, “inamaana yule mtoto ndio mimba unayosema?” aliuliza Roida, kwa sauti yenye mashangao wa masikitiko, “kumbe alisha jifungua, ebu niambie ni jike au dume?” aliuliza Daniel kwa sauti yenye furaha na majisifu, “wakiume, lakini mbona ameolewa na wanasema yule mtoto ni wa mwanaume alie muoa, na wanaishi huku huku dar?” aliuliza Roida ambae mshangao wake aukuweza kufichika, “eti nini ameolewa?” aliuliza Daniel kwa mshangao wenye wivu.


Na hapo Roida akaanza kumsimulia, jinsi Adellah, alipofika jijini kumtambulisha mume wake, ambae ni mtu mwenye fedha ya maana, “tena walikuja na gari lao, walikuja na Sophia, na watoto wake wawili, alileta mazawadi kibao kwa mama yake” alieleza Roida, hadithi ambayo ili mshtua sana, Daniel ambae japo akuwa na mpango wa kumtafuta Adellah, lakini akajikuta anatamani kukutana nae, ili ajuwe hatima ya mtoto wake, ambae sasa inasemekana ni mtoto wa mwanaume mwingine, “yani Adellah amependeza, sasa hivi ni mke wa Tajiri” alisema Roida, kabla ajaaga nakuondoka zake.


Hakika ulikuwa ni ujumbe wenye kuumiza sana, kwa Daniel, maumivu ambayo ukiyachukulia juu juu, ungesema ni sababu alikuwa anampenda sana Adellah, ila ukweli ulikuwa ni wivu, tena siyo wivu wakuona mwanaume mwingine anatembea na mpenzi wake wa toka utotoni, hapana, ni wivu wa kuona mwanamke ambae amekuja siku chache hapa mjini, mwanamke ambae alitegemea sasa atakuwa anaangaika kulea mtoto peke yake, eti sasa anasikia anaishi Maisha ya kitajiri, na walienda Lufilyo wakiwa na gari lao.


Ukweli siku hiyo, aikuweza kumalizika, kabla Daniel aja dandia dala dala, mida ya saa saba mchana na kuelekea kibamba kwa mangi, ambako alienda moja kwa moja mpaka kwenye nyumba zamani alikopanga Sophia, ambako alielekezwa nyumba anaishi sasa hivi, nae akafanikiwa kufika bila tabu yoyote.


Ujio wake ulimshtua sana Sophia, “wewe umeefwata nini huku, siulikimbia baada ya kusikia Adellah mjamzito, kwa taarifa yako amesha ondoka amerudi Mbeya” alisema Sophia ambae akutaka kabisa Daniel aingie katika Maisha ya Adellah kwamalanyingine, “Sophia siyo kwamba nilikimbia, mimi nilipatwa na matatizo, kuna mtu alinisingizia kesi, sababu anaela, nikakaa jela mwaka mzima, ndio nimetoka, nataka kumwona Adellah na mwanangu” alisema Daniel ambae kiukweli alitaka kufaidika kupitia Maisha ya sasa ya Adellah. 


Hadithi ya uongo ya Daniel akaingiwa na huruma, “lakini kwa sasa Adelah ameolewa, na anaishi Maisha mazuri tu na mume wake, sasa utafanyaje, labda nimtume mtoto akamwite, muongee wenyewe” alisema Sophia, ambae alikuwa anajuwa fika mapenzi ya Adellah kwa Daniel.


Lisaa limoja baadae Sophia alikuwa amefika nyumbani kwa Sophia, huku akiwa amembeba Samuel, moyoni hamu ya kumwona mpenzi wake Daniel, na alipofika tu, Daniel akuwa na aja ya kumwona mtoto, Sophia alimchukuwa mtoto, na kutoka nao akiwa ameongozana na watoto wake, akiwaachia nafasi wawili awa ya kunyanduana, walifanya hivyo kwa furaha kubwa, wakitumia msaa kadhaa, kisha wakaoga na kusindikizana stendi, ambapo Daniel alipanda dala dala, huku akiwa amepewa shilingi elfu tano.******


Naaaam huo ulikuwa niufufuo wa penzi ili la uthariti, ambalo siyo tu kufanyika kwenye nyumba ya Sophia, ambae akukumbuka msaada waliopewa na Sebastian, pia ulifanyika nyumbani kwa Adellah mwenyewe, huku dada wakazi akipewa luksa ya kwenda kytembea asione kinachoendelea, mapenzi yalikuwa moto moto, huku ata wakanogewa na kunogewa tena, kiasi cha kushirikiana na Sophia kupanga mbinu ya kumleta Daniel nyumbani kwa Sebastian, wakisingizia kuwa ni mtoto wa baba mkubwa wao.


Seba akiwa ajuwi ili wala lile akamkaribisha Daniel kama shimeji yake, na hapo ndipo alipo kuwa amekaribisha ndoa ya mitara, ya wanaume wawili ndani ya nyumba moja, Adellah akiwa amemfukuza dad wakazi, asije akafichuwa anacho kifanya, usiku alilala na mumewake, huku wakigeuziana migongo, kwa kisingizio cha kunyonyesha, huku nchana wakati wakitumia nafasi ya Sebastian kuwa kazini, walifanya walicho fanya kama wapo kwenye fungate.


Baada ya kukaa miezi kdhaa, na Sebastian kumtafuta kazi Daniel, ambae aliikubari kwa shingo upande, sababu alikuwa anapata kila anachokiitaji, alikula siku moja moja alitolewa matembezi na mume mwenzie, ambae walikuwa wanaitana shemeji, pia alikuwa ananunuliwa nguo, na kubwa zaidi alikuwa analelewa mke na mtoto wake, na pia alikuwa na uhakika wakula kitumbua kila anapotaka.******


Yap!, taarifa ya ujauzito mwingine iliwashtua wote watatu, yani Adellah Daniel na Sophia, nao wakaa kwa pamoja na kujadiri, wafanye nini, ili Sebastian aigundue, na kuachana na Adellah, ukizingatia toka mtoto alipozaliwa mpaka anatimiza miezi nane, akuwai kupitisha mwiko kwenye chungu cha mke wake, jibu lililopatikana kwenye kikao hiki cha watu watatu, ni kwamba, akukuwa na njia nyingine, lazima mimba hii asingiziwe tena Sebastian, maana siyo tu kubadirisha maisha yao, pia alikuwa msaada kwao na kwa wazazi wao kule kijijini.


Lakini sasa, kila pale Adellah. Alipojaribu kumshawishi Seba, kula kitumbua, ilishindikana, ata dalili za wazi zilipoanza kuonekana, na kilicho washtua zaidi, nisiku ambayo Sebastian alitoka kazini mapema na kwenda kuongea na Sophia, ambae alimhakikishia kuwa Adellah awezi kuwa na ujauzito, ambao utakuwa wanje, lakini hapo hapo mala baada ya Seba kuondoka, jioni Sophia akaenda nyumbani kwa Adellah, akijifanya alikuwa anapita njia na kuamua kuja kuwasalimia.


Lengo la Sophia lilikuwa ni kuongea na Adellah wakati anamsindikiza, na siyo tu kuongea na Adellah, ila pia ni kukutana na Daniel ili wajuwe la kufanya, kabla mambo ayaja aribika, maana akukuwa na namna, na kuna kitu uwaga akina siri, kama mimba, maana baada ya miezi kadhaa ingeonekana, hivyo wawali awa, yani mtu na mdogo wake, walio jiziuka kwa maisha ambayo walipewana Seba, walienda moja kwa moja mpaka kwenye kituo cha dala dala, na kumsubiri Daniel, huku wakiwa tayari wamesha panga mambo yao, japo kuna mambo walipanga mwanzo, lakini yalionekana kuwa yanaweza kuwaletea matatizo.


 Mfano, pale mwanzo, Adellah alisema kuwa ni vyema wakimwekea sumu Sebastian, ili afe na yeye abakie na kila kitu cha Seba, mwanaume ambae amemtoa katika umasikini mkubwa sana, “haapana Adellah, ukisema ufanye hivyo, lazima polisi watakukamata, alafu utanyoongwa, bola tukutane na Daniel tujuwe cha kufanya” alisema Sophia.


Saa kumi nambili za jioni, Sebastian alishuka toka kwenye dala dala, na kukutana na wakina Aedellah, hapo akajuwa tayari mambo yameshaanza kuwa mambo, na akuna kitu Daniel akutaka kuona kinacho mtokea, kama kurudi kwenye maisha ya kulala nje, “vipi jamani, kuna usalama kweli?” aliuliza Daniel kwa sauti yenye kihoro, “mambo yanazidi kuaribika huko, lazima tufanye kitu, vinginevyo mtarudi kwenye umasikini” alisema Sophia kwa sauti yenye uchochezi, “sasa tunafanyaje jamani” aliuliza Daniel, ambae kiukweli alianza kuona safari ya kurudi mbezi inanukia.


ITAENDELEA.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.