NGOJA NILEWE 6

 NGOJA NILEWE 6




MTUNZI: Mbogo Edgar

WHATSAPP +255743632247


Ilipoishia 5


Saa kumi nambili za jioni, Sebastian alishuka toka kwenye dala dala, na kukutana na wakina Aedellah, hapo akajuwa tayari mambo yameshaanza kuwa mambo, na akuna kitu Daniel akutaka kuona kinacho mtokea, kama kurudi kwenye maisha ya kulala nje, “vipi jamani, kuna usalama kweli?” aliuliza Daniel kwa sauti yenye kihoro, “mambo yanazidi kuaribika huko, lazima tufanye kitu, vinginevyo mtarudi kwenye umasikini” alisema Sophia kwa sauti yenye uchochezi, “sasa tunafanyaje jamani” aliuliza Daniel, ambae kiukweli alianza kuona safari ya kurudi mbezi inanukia. ,…… . ENDELEA……..


Hapo Sophia akawaeleza anacho kifikilia, “huyu inabidi tufanye kitu ambacho kitasaidia nyie kupata malizake zote, lakini siyo kumuuwa, tutafungwa wote, sasa sijuwi ni itu ganikinaweza kufanyika kwa haraka, kabla ajaamua kwenda kumpima Adellah” alisema Sophia, na hapo Daniel akachukuwa nafasi yake, “ilo niachieni mimi, maana huyu dawa yake ni kwenda jela tu, akitoka huko sisi tumesha potea” alisema Daniel, na wao wakamwachia yeye mpango mzima.******


Siku ya pili Daniel alipanda gari la Seba kama ilivyo kawaida, lakini alishukiakivukoni, upande wa kigamboni, akidai kuwa kuna mtu anaenda kumwona, huku Seba akimweleza Daniel, kuwa baadae kuna kitu anataka waongee, kitu ambacho Daniel alihisi kuwa anaenda kusomewa mashtaka ya ujauzito wa Adellah, kitu ambacho Daniel akukijuwa ni kwamba, Sebastian alitaka amsimulie mashaka yake kwa mke wake, kuwa na ujauzito, lakini Daniel kwakuzania kuwa, amesha tiliwa mashaka, alia,ua luharakaisha mpango wake wa kutimiza angamizo la Sebastian.


Danel alienda moja kwa moja, kwenye vijiwe vya vijana wa pale ukweni, karibu na kivukoni, akachukuwa kete ishilini za bangi, akaziweka kwenye mfuko wa rambo, kisha akapanda dala dala na kwenda kushukia karibu na eneo la kiwanda, ambapo aliingia ndani ya kiwanda, akitumia njia ya panya, ambayo mala nyingi utumiwa na watu waliochelewa kuingia kazini, au wanao wai kutoka kazini, pasipo luksa ya mkuu wakitengo chake, japo alikutana na watu wawili watatu waliokuwa wanatoroka, lakini akuwajari, yeye alienda moja kwa moja mpaka idara ya uzalishaji, ambako alijibanza huko, huku mala kwa mala akichungulia upande wa ofisi ya mhasibu wa masoko, yani kwa bwana Sebastian, kuona kama anatoka, ili awai akafanye jambo lake.


Saa nne ndio mida ambayo Daniel alifanikiwa kumwona Sebastian akitoka ofisini kwake, na kuelekea canteen akipishana kidogo, na mhasibu mkuu, na hapo ndipo yeye alipo wai haraka na kwenda kuweka bangi kwenye moto wa meza ya Sebastian kishakapiga simu kituo cha polisi, kwa kitumia simu ya ofisini kwa Sebastian, akiwajulisha kuwa ndani ya ofisi ya mhasibu wa masoko wa FSC kuna mzigo wa bangi, ambayo inatumika kuwauzia wafanyakazi wa kiwanda hiki.


Dakika kumi baadae polisi toka kituo kongwe na kukibwa cha Kigamboni waliingia pale kiwandani na kuonana na meneja ambae aliwapeleka ofisini kwa mhasibu wa wa masoko, ambako baada ya kupekuwa kidogo wakakuta bangi kete ishilini, ndizo ambazo leo hii zilimpeleka Sebastian, kituo cha polisi, akiwaacha penda nao, wakiwa wanafurahia ushindi wao, wakisahau kabisa kule ambako Sebastian aliwatoa, walisahau kabisa kile ambacho Sebastian aliwafanyia, walisahau kabisa, kuwa kijana huyu aliitoka kwao songea Vijijini kuja dar es salaam kutafuta kazi imsaidie katika maisha yake, na pengine kuwasaidia wale wenye uitaji, awakujuwa shida ambazo Sebastian alizipitia, mpaka kufika pale, yani licha ya kuwasaidia wao na watoto wao, lakini bado wanakusudia kukomba kila alichonacho, na siyo kukomba alicho nacho, pia kumpoteza kabisa, na kumchukilia uhuru wake.*********


Naaaam, wakati Sebastian akiwa ndani ya chumba kidogo, cha mahabusu ya polisi, pamoja na wengine sita, aliwaza mambo mengi sana, kwanza nani alie mfanyia uovu kama ule, wakumwekea Bangi kwenye draw yake, akufikilia kabisa kuwa atakuwa Daniel, maana alichelewa kufika pale kiwandani, na huyu mtu alimkosea nini, mpaka afikie atua ile ya kumtegeshea bangi ofisini kwake.


Pia Sebastian aliwaza juu ya familia yake, yani mke wake na mtoto wake, wataishije wakati yeye akiwa ndani ya chumba cha mahabusu, na mwisho Sebastian aliwaza juu ya hatima yake, juu ya kosa lile la kukutwa na bangi ndani ya ofisi, japo kwa kipindi kile alikuwa kosa kubwa sana kwa bangi ambayo aijafika ata kilo moja, lakini kwa ugeni wakukukamatwa na polisi, Sebastian alijikuta katika wakati mgumu sana, kijana aliwaza jinsi atakavyoweza kumtazama mke wake akiwa amesimekuja kumtazama na mtoto huku analia.*******


Naaaam! Siku ya kwanza ikakatika akiwa ndan ya mahabusu, akuweza kumwona mke wake wala mtu alie mzania kuwa ni shemeji yake, zaidi alikuja bwana Ngimba, yani mhasibu mkuu, ambae alijaribu kumuuliza imekuwaje amepata tuhuma kama ile, katika kipindi kigumu kama hiki, ambacho amemshuku mke wake kuwa mjamzito, “mzee nazani una nifahamu ukweli mimi siusiki na ile bangi, na uhakika kuna mtu aliniwekea” alisema Sebastian, ambae mpaka sasa akujuwa ni kwanini mke wake na shemeji yake awajafika kumwona.


Siku yatatu, siyo Adellah, Sophia Philipo wala Daniel alie kuja kumwona, ila siku ya nne ambayo alifikishwa mahakamani, alikuja mzee Ngimba na meneja wao, ambao pia walimweleza kuwa shemeji yake Daniel akuwai kufika kazini, toka kukamatwa kwake.*******


Huku nyumbani pia, wanafamilia awa, wakishirikiana na Daniel wakakubaliana wauze nyumba, ili wapate kuondoka sehemu ile, sababu endapo Sebastian ata toka jela, ata ichukuwa nyumba yake na apata kuwa na siri tena, hivyo ataachana na Adellah, na wao kuwa wamekosa kila kitu, hivyo basi kwakuwa walikuwa na kila nyaraka inayo husu nyumba ile, na zile za manunuzi ya mwanzo, ndani ya mwezi mmoja tu, walifanikiwa kupata mteja na kuiuza, kwa tsh million saba, kisha wao waaenda kupanga kimara, wakaendele na maisha yao ya starehe, wakitumia gari la Sebastian lile escudo, ambalo pia awakuchukuwa muda mrefu wakaliuza kwa million tatu, na kuendelea kuponda raha, wakisahau kuwa kuna mtu yupo jela, na kwa upande wa Sophia alie pata mgao wa million moja, aliama na mume wake wakiamia chanika mwisho, ambako walifungua tena duka lao, na kuendelea na maisha yao.


Naaam akiwa ajuwi kinachoendelea nyumbani, siku zilienda, Sebastian aliendelea kusiliza kesi, ambayo ambayo ilikuwa inabadirishwa tarehe, huku akiamishiwa mahabusu ya Ukonga, atimae miezi mitatu ilikatika, bila hukumu kutoka, hii ni kutokana na ushaidi kukosekana, ata mwezi wa nne wa toka alipo kamatwa, siku moja Sebastian, ambae siyo tu kukosa amani juu ya ukimya wa mke wake, ambae mala ya mwisho walikuwa na mashaka juu ya dalili za ujauzito, pia alishangaa kuto tembelewa anata na shemeji yake mmoja, yani kati ya Sophia au Daniel.

Lakini siku hiyo ikiwa ni siku moja kabla ya siku ya hukumu, alitembelewa na bwana Ngimba, “kijana pole sana, inaonekana wazi kuwa kuna mtu alikufanyia njama za makusudi, nae ni bwana Daniel, ambae unamwita shemeji yako” alisema Ngimba, hiyo ilimshangaza kidogo bwana Seba, “ndio maana akutaka atakuja kunitembelea, kwani nyie mmejuwaje?” aliuliza Sebastian, “tumegundua jana wakati tunalipia bili ya simu, tumeikuta simu yako, siku ya tukio ilitumika kupiga simu kito cha polisi, ata tulipohoji watu kadhaa, wale wakiwandani wanasema walimwona Daniel akiwa amejibanda kule kiwandani muda mrefu, akiwa na mfuko, unao fanana  na ule uliokutwa ofisini kwako, pia hao tu, pia kuna yule kijana anaefanya usafai kwa meneja, nae alimwona Daniel anaingia  mapema tu, kwaile njia  ya uchochoroni, akiwa na mfuko huo huo, na kilisho watua vijana wa kiwandani ni kwamba, Daniel alikimbilia ofisini kwako mala tu baada ya wewe kuelekea canteen” alieleza mzee Ngimba, ambae alimweleza Sebastian kuwa, licha ya kuwa nafasi yake ilisha chukuliwa na mtu mwingine pale kiwandani, lakini meneja amepanga kumsaidia kumaliza kesi ile, sababu ata wao  walishaona kuwa kulikuwana njama zilitendeka zidi yake.


Hizo zilikuwa habari njema sana kwa Sebastian, “mzee kuhusu kazi siyo tatizo, maadamu ninanyumba na gari, naamini vita nisaidia kuanza upya, cha msingi nitoke tu humu ndani” alisema Sebastian kwa sauti yenye furaha ya matumaini mapya, hakika ilikuwa ni furaha kubwa kwake, ata alipokuwa kule lumande, aliona kuwa, siku inayofwata inachelewa, sababu alikuwa na maswali mengi sana, ambayo yalitakiwa yajibiwe na Daniel na Adellah, na pengine Sophia na Philipo, niwazi hao wote walikuwa wanajuwa kilikuwa kinaendelea.*******


Naaaam! Siku iliyofuata, ikiwa tayari kijana wetu ameshaka miezi minne ndani ya mahabusu, anaachiwa huru, na kuondoka zake, huku akiwa ayaamini macho yake, kwamba anatoka pale mahabusu, sehemu ambayo siku moja aliiona kama mwaka mzima, mfukoni kulikuwa na elfu moja pekee, fedhaambayo alipewa na mzee Ngimba, kwaajili ya nauri ya kufikia nyumbani, japo ingebakia nyingi sana, maana wakati huo nauri ta dala dala, ilikuwa ni shiingi mia hamsini, hiyo ni kwa umbali wa mwisho kabisa.


Akiwa ajuwo chochote kilicho tokea ndani ya miezi minne, ambayo akuwa mahabusu, Sebastian alie valia nguo yake ile ile, aliyo ivaa siku anakamatwa na polisi pale kiwandani, alishuka kwenye dala dala kituo cha kibamba kwa mangi, na kutembea taratibu mpaka nyumbani kwake, huku kila kitu akikiona kimebadirika, yani kama vile alikuwa mgeni kabisa jiji dar es salaam, ila kilichomshangaza ni namna watu walivyo kuwa wanamtazama, asa wale walio kuwa wanamfahamu, wakati anapita njia, kuelekea kule ambako kulikuwa na nyumba yake, ata alipowasalimu, waliitikia kwa sauti iliyopoa, huku wakimtazama kwa macho tofauti, wapo walio mtazama kwamacho ya huruma, na wapo walio mtazama kwa macho ya dharau, siunajuwa tena binadamu, licha ya kujuwa mkasa uliompata, lakini ungesikia jitu linasema “mwache apigike bwana, alikuwa anajidai sana” lakini katika kumbu kumbu zako, ukuwai kujidai ata siku moja, ulikuwa unawasalimia vizuri na wengine uliwaisaidia, ata akasiyo fedha au lift basi ata ushauri, Sebastian akuwajari walio mtazama kwa dharau, maana alijuwa fika juu ya matokeo ya mtu anae toka jela, ata kama ni kwa kusingiziwa, wao wangekuchukulia kama mtu mbaya na mwalifu.


Naam ile Sebastian anakaribia nyumbani kwake, anashangaa kuona nyumba imechangamka vibaya sana, watu kadhaa walionekana wakiwa katika pilika pilika zao za kila siku, tena sura ngeni kabisa, lakini akapiga moyo konde na kusogelea pale nyumbani, akimlenga dada mmoja aliekuwa anafuwa, “habari dada” alisalimia Sebastian kwa sauti tulivu yenye nidhamu, huku mapigo ya moyo wake yakianza kwenda kasi “salama habari” aliitikia yule dada, huku anaacha kufua na kumtazama Sebastian, ambae kiukweli alikuwa amepauka, kwa kukosa mafuta ya kujipaka, “salama tu dada yangu, samahani najuwa unifahamu, ila mimi ni baba Samuel” alisema Sebastian, na hapo yule dada, ambae kiumri nikama alimzidi Sebastian akamtazama Sebastian kwa macho ya tahadhari, “kwahiyo nakufahamu” aliuliza yule dada akionyesha dalili ya uoga, maana ni kwamba, ujio wa Seba na utambulisho wake, vilimfanya ahisi kuwa kuwa Seba alikuwa na matatizo ya hakiri, yani unafika tu sehemu na kujitambulisha mimi baba fulani, ili iweje.


Nikama Seba aliliona ilo, “hooo! Pengine unifahamu, labda niitie mama Samuel” alisema Sebastian, ambae mpaka hapo akuona dalili ya Adellah, wala Daniel, akamshangaza zaidi yule dada, “mbona hapa hakuna huyu mtu unae mtaja, hapa kuna familia tatu tu, zinakaa, na wote wanaishi na wanaume wao, na hakuna ata mmoja mwenye mtoto anaeitwa Samuel” alisema yule dada, na hapo Sebastian akaanza kujihisi kuvulugwa hakiri, akaitazama nyumba yake, na kuona ni pale pale, wala ajapotea.


Hapo sebastian akahisi kuwa Adellah, atakuwa ameamua kupangisha ile nyumba, na yeye kwenda kukaa sehemu nyingine, “kwahiyo nyie ni wapangaji?” aliuliza Sebastian, akijitaidi kuzuwia mshtuko wake, na yule dada akaitikia kwa kichwa, ikiwa ni ishara ya kukubari, “hooo sawa ndio maana numenishangaa nilipojitambulisha, sasa mama mwenye nyumba anaishi wapi kwa sasa?” aliuliza Sebastian akiwa na tumaini la kumpata Adellah akamjibu maswali yake.


Mpaka hapo yule dada kuna kitu akagundua, “sasa kaka nime kuelewa, labda nikueleweshe vizuri, ni kwamba, sisi siyo kama tumepanga kama unavyo zania kupanga kwa kawaida, hii nyumba imenunuliwa na mkurugenzi wa kiwanda cha mafuta ya alizeti cha V Sun OIL, na hapa amewaweka wafanyakazi wake” alisema yule dada, na hapo ilibakia kidogo Sebastian aanguke kwa kizungu zungu, lakini akajikaza, “unajuwa huyo alieuza anaishi wapi kwa sasa?” aliuliza Sebastian, kwa sauti ambayo ata kama ni wewe unangejuwa wazi kuwa, kuna kitu kizito kimempiga huyu jamaa, “hapana ata sijuwi kwani ata mtu mwenywe simjuwi na wala sijawai kumwona” alisema yule dada ambae alikuwa anamtazama Sebastian safari hii kwa macho ya huruma. 


Seba akiwa amesimama, aliinua uso wake taratibu akaitazama nyumba kushoto na kulia, juu na chini akatazama eneo lambele, huku yule dada anamtazama tu, nakuona macho ya kijana huyu, yakijawa na machozi, “aya dada yangu mimi naondoka” alisema Sebastian, kwa sauti ya kinyonge, huku anageuka na kuondoka zake, yule dada akimsindikiza kwa macho yenye mshangao na huruma, mpaka kijana yule alipotoweka, “mama Tedi yule mtu alikuwa anasemaje?” yule dada alishtuliwa na sauti ya kike, toka nyuma yake, yule dada anageuka na kutazama beseni lake, lwnye nguo, anashika na kuanza kifikicha, huku anaguna, “mh! yani mwenzangu, yule baba ata simuelewi, amekuja anajitambulisha kuwa nibaba Samuel, na kwamba ana itaji kumwona mama Samuel” alisema yule huyu alie itwa mama Tedi.


Na hapo unasikika mshangao wa bata, toka kwa huyu mwenzie, ambae alikuwa amesimama pembeni yake, “weeeeee! inamaana huyu kaka ameshatoka jela?” aliuliza yule mwingine kwa mshangao, na kumfanya mwenzie aache kufua na kumtazama kwa mshangao, “kwani unamfahamu huyu kaka?” aliuliza mama Tedi, “simfahamu, lakini baba John, aliwai kunisimulia habari zake” alisema yule mwanamke mwingine, huku akionekana kushangaa wazi wazi, huku huruma flani ikimjia usoni mwake, “ebu nipe story” alisema mama Tedi akiacha kabisa kufua.


“Huyu kaka kandie yeye, basi ndie alikuwa mwenye hii nyumba, na hapo mwanzo alikuwa anaishi mwenyewe, unaambiwa raha mustarehe, sindio akaja kujiingiza mwa huyu mama Samuel, tena pasipo kujuwa alikuwa ni mpenzi wa kaka mmoja hivi taperi, tena yule dada alivyo mshenzi, akamleta huyo mwanaume mpaka hapa, na akaishi humu humu, mwisho akashirikiana nae wakamtegeshea bangi ofisini akakamtwa na polisi, hivi unavyo muona ndio atakuwa ameachiwa, unaambiwa amekaa sana jela” alisimulia yule mke wa baba John, “weeee! Kwahiyo watakuwa wamauza nyumba wakati huyu baba yupo jela?” aliuliza kwa sauti yenye mshangao na masikitiko makubwa mama Tedi.*******


Naaaaam Sebastian alienda moja kwa moja, mpaka kwenye nyumba ambayo mala yamwisho, Sophia alikuwa anaishi na mume wake, alipouliza akaambiwa kwa Sophia alikuwa amesha hama muda mrefu sana, na akukuwa na ata mmoja aliejuwa anaishi wapi, hakika Sebastian alijihisi kuchanganyikiwa, ghafla maisha yalimgeuka na kurudi nyuma sana, zaidi ya kule alikotokea, alikuwa atika umskini mkubwa sana, ambao ata mama yake licha ya umskini aliokuwa nao hapo zamani, lakini akuwai kufikia hatua ya kukosa sehemu ya kuishi.


Sebastian alitembea taratibu kuelekea barabarani, lengo likiwa ni kwamba akatafute sehemu akae kidogo wakati anafikilia cha kufanya, maana akuwa na chochote alicho bakia nacho, siyo tu mke mtoto, nguo viatu na fedha, au nyumba na gari alivyopoteza, pia ata vyeti vyake vya shule, navyo akujuwa vipo wapi, na mbaya zaidi ata thamani ya utu wake pia ilisha potea, na kuwa zaidi ya wale ambao mwanzo walikuwa wananyenyekea na kumwona kuwa msaada kwao.


Mfano wakati anakatika maeneo ya magengeni, akashtuka mtu anamwita, “hoya, ni wewe bro?” Seba akageuka na kumtazama alie msemesha, ambae alikuwa karibu yake kabisa, akamwona kuwa alikuwa ni baraka, yule jamaa muuza genge, “nini kaka, mambo vipi baraka” alisalimia Sebastian, huku anachepuka kuingia kwenye genge la baraka, “pole sana bro, naona umetoka salama” alisema baraka huku anachukuwa ndizi mbivu, toka kwenye genge la jilani, na kumpatia Seba, “nashukuru nimetoka kaka, lakini nilicho kikuta nitofauti na nilivyoacha” alisema Sebastian kwa masikitiko, huku anapokea ndizi na kuimenya.


Waliongea mawili matatu, huku Sebastian akimsimulia baraka kilichotokea, mala akaja jamaa moja, wa genge la tatu toka kwa baraka, hapo ni sehumu ambayo Sebastian alikuwa ananunuaga sana mkaa, “hoya baraka jamaa yako ametoka jela” alisema yule jamaa maharufu kama Side mkaa, huku anapita kwa fujo pale alipokaa Sebastian, na kumkiumba kidogo, “hoya Side njia yote hiyo umpaka umsukume mshakaji?” aliuliza Baraka kwa sauti ya ukali kidogo, “mshakaji, weweeee, wakati ule sialikuwa anapita tu hapa, kwani alikuwa akaaga hapa kijiweni, akapande gari lake sasa” aliongea Side, akionyesha wazi kuwa, amefurahi kuona Sebastian akiwa katika hali kama ile, “Side angalia maneni yako akuna anaependa kukutwa na jambo kama ili” alisema Baraka, ambae wakati huo pia alikuwa anahudumia wateja wake, “achana nae bwana, kwani we ulikuwa uoni, anavyojifanya kununua ndizi hapa, eti hoo mambo ya week end” alisema Side huku anaendelea kutembea kuelekea alikokuwa anaelekea, ilionyesha wazi kuwa, Side alikuwa anachukizwa na kuumizwa sana, na maisha ya zamani ya Sebastian, licha ya kuwa alikuwa anamuungisha mkaa, lakini Side alikuwa na kinyongo moyoni, kuona kijana mdogo kama Sebastian anamtindo wa maisha ya kuburudika, anauo umudu.


Sebastian alitamani arudi kijijini kwa mama yake, lakini alishindwa kutokana na mambo mawili moja ni kwamba atamweleza nini mama yake ambae mpakasasa nikama ile ndoto yake aliyoiotaga wakati wakati ule imetokea kweli, ilila pili nalo lilikuwa inshu, yani nauri, japo kama ingekuwepo, basi ange enda ata kufikia songea mjini, afanye mpango wa kupata kazi, japo vyeti mpaka sasa akujuwa vipo wapi.


Naam Sebastian alishinda pale gengeni, akiongea ili na lile na baraka, ata chakula baraka ndie alie mnunulia, kuna mida Sebastian alienda chini ya mti mmoja mkubwa na kujilaza, ambapo alipitiwa na usingizi mkubwa sana, alilala saa saba mchana akashtuka saa kumi na mbili jioni tena baada ya kushtuliwa na baraka, “oya bro, umelele sana, njoo tutulie hapa gengeni” alisema barabara, nao wakaelekea gengeni, sehemu ambayo sasa ilikuwa nikama makazi ya Sebastian, ambae akuweza kwenda kulala kwa baraka, sababu nae tayari alikuwa na mke aliekuwa anaishi nae chumba kimoja cha kupanga, hivyo Seba alisubiri mpaka baraka alipofunga genge, na yeye angejiegesha hapo mpaka asubuhi, ambapo na wakati wa mchana angeenda chini ya mti na kulala usingizi mzito, lakini licha ya yote, masimango ya wakina Side na wenzake ayakukoma, yalimpa unyonge na kumyima laha, japo yalimpa somo na funzo kubwa sana, siyo kila mtu anapenda kile unacho kifanya, au unavyoishi, aya kwenye mafanikio.


Siku zilienda Seba akijitaidi kumtafuta Adellah, bila mafanikio, jioni angerudi na kulala pale gengeni, kuna wakati baraka, akaanza kumwachia genge Sebastian, pale anapokuwa na dharula, sasa ata jioni wakati wa usiku baraka akiwa anaondoka, alikuwa anamwachia sebastian genge aendelee kuuza mpaka muda ambao ataamua kulala, na pia kunapokucha tu, alikuwa anafungua mapema, hiyo ilisaidia sana, wao kuuza sana, na baraka alizidi kumsaidia na kumfadhiri Sebastian fedha ya chakula na nauri kila anapoitaji kwenda kumsaka Adellah.*******


Naaam maisha yalisonga hatimae miezi miwili ikakatika, toka Sebastian atoke jela, nakatika wakati huo Siku moja mida ya saa tano, baraka akiwa ametoka mabibo soko la matunda na mboga, akamweleza Sebastian kuwa amekutana na Philipo, shemeji yake Adellah, “sija mwambia kama nipo na wewe, ila nilimwuliza anakoishi, amenielekeza kuwa anaishi chanika mwisho kama unaenda masaki” alieleza Baraka, na hapo bila kuchelelewa, akamwelezza baraka ampatia elfu mbili, nae akampatia, na Sebastian akaondoka mala moja kuelekea Chanika.

Saa sita nanusu, tayari Baraka alikuwa kwenye mlango wa duka alilo elekezwa, hakuweza kuona ukubwa duka, maana lilikuwa limefungwa, sababu muuzaji ambae ni Philipo alikuwa ameenda mjini, lakini akapata watu ambao walimwelekeza anakoo mmiliki wa duka, nae akaelekea huko, huku akiwaaza aina majibu atakayopewa na Sophia.


Ukweli ni kwamba Sophia alishtuka sana, maana akutarajia kumwona Sebastian akifika hapa nyumbani kwake, maana ata kule kibamba walimkimbia yeye, nakuamia huku, ambako waliamini kuwa ataiweje, asingeweza kuwapata, “he! shemeji ni… niwewe ….. umepajuwaje hapa?” aliuliza Sophia alieonekana kushangaa na kushtuka sana, “shemeji sizani kama kuna umuhimu wakujuwa nimefikaje hapa, ni wazi kuwa ukutaka nipajuwe” alisema Sebastian ambae muda wote alikuwa anajizuwia hasira zake, maana chochote cha kipuuzi kingemrudisha ukonga, “aya sawa sasa umefwata nini kwangu?” aliuliza Sophia safari hii kwa sauti iliyojaa ujeuri, “nimekuja kwa mambo mawili, moja kukuambia asante sana kwa kunifundisha nini maana ya binadamu tupo tofauti, na pili nimekuja kuuliza mke wangu na mtoto wangu wapo wapi” alisema Sebastian, na hapo ni kama alipandisha mashetani ya Sophia, “hivi ulitumwa kujipendekeza kwa Adellah, si wewe mwenyewe na tamaa yako, alafu eti hooo mke wangu, kwa hiyo wewe unajiita mume wa mdogo wangu, nani alikuambia Adellah anamume muuza bangi” alisema kwa jeuri ya hali ya juu Sophia, kiasi kwamba baada ya kupatwa na hasira, Seba akajikuta anacheka.


Yani yule mwanamke mnyonge, alie kuwa anashinda na njaa kutwa nzima yeye anamwokoa pamoja na familia yake, leo hii anamtolea maneno machafu kama aya, “Sophia najuwa unajuwa mimi siyo muuza bangi, alafu pia aipendezi wewe kuongea maneno kama hayo, sababu nimesha juwa wewe ni nani hasa, sina deni wala ubaya na wewe, sababu wewe ndiyo wewe, na yoyote atakae kuwa na wewe akubari chochote kitakacho mtokea, naomba unijulishe Adellah yupo wapi, ata kama anitaki tena, nataka kwenda kumwona mtoto wangu” alisema Sebastian, kwa sauti tulivu ya upole.


Hapo ndiyo kwanza Sophia akaachia kicheko chakubeza, chenye dharau tani moja, “eti ndivyo nilivyo, aya naomba uondoke hapa, kabla sijakuitia mwizi, safari hii utauwawa hapa hapa, auto iona ataiyo segelea” alisema Sophia, huku anajifunga vizuri kitenge chake kiunoni, hapo Seba akaona kuwa ni kweli kabisa, anaenda kuitiwa mwizi, na kitakacho mtokea ni zaidi ya balaha, hivyo haraka sana akaamua kuondoka zake, kakirudi na njia aliyo jia, kichwani mwake, akishangazwa na tabia mpya ya Sophia, aliyo iona leo hii, akuamini kabisa kuwa yule ndie yule mwanamke ambae, wakati ule alikuwa anakaa kutwa nzima anabubujikwa na machozi kwa kuona watoto wake wanateseka kwa njaa, na yeye kuwa mkombozi wa tabasamu la mwanamke huyo.


Wakati Sebastian akiwa anatembea kwa unyonge kabisa, akakatiza pale dukani, kwa Sophia, na kwabahati nzuri, akaona lipo wazi, inamaana alipishana kidogo na muuzaji waduka lile, wakati alipokuja mala ya kwanza, Sebastiana akujiuliza mala mbili, akachepuka na kuingia pale dukani, “karibu…….” Alikaribisha philipo, huku anainua uso na kujikuta akuachia mdomo wazi kwa mshangao, “Seba, ni wewe kaka, umetokalini polisi?” aliuliza Philipokwa mshangao, huku anamtazama Sebastian kwa macho ya kustaajabu kama amemeuona mzimu mbele yake, “vipi uliambiwa sito kaa nitoke kule jela?” aliuliza Seba, ungesema alikuw anatania, Philipo ambae licha ya kusaidiwa sana na Seba, lakini awakuwa na mazoewea makubwa, alijichekesha kidogo, “nilisikia kesi yako ni ngumu, lazima ungefungwa kuanzia miaka miwili au mitatu” alisema Philipo huku anatoa kiti na kumpatia Seba akae, “hapana kaka, mimi siyo mkaaji, nilikuja kuwasalimia tu, pia nilitaka Nijuwe Adellah anaishi wapi kwasasa” alisema Sebastian, ambae aliona kidogo kuna utofauti kati ya Philipo na mke wake.


Ukweli nikama Phiipo aikuwa anasita kidogo kueleza Adellah anaishi wapi, ata Seba aliligudua ilo, “kaka na juwa kuwa huu mchezo mzima aliucheza Adellah, mke wako Sophia, na Daniel, mimi sina ugomvi nao, na juwa wamesha malizana na mimi, wameuza nyumba yangu wameondoka na gari langu, wameniaribia kazi yangu, nachotaka ni vyeti vyangu vya shule, nitafute kazi nyingine nianze upya, lakini kumbuka kuwa kama wameweza kunifanyia hivi mimi, kwa msaada wote nilio wapa, na wewe jiandae, pasipo kujari mna watoto au la” alisema Sebastian, kwa sauti tulivu kabisa, huku akikataa kukaa.


Nikama maneno yale yalimwingia sana Philipo, ambae alitulia kwa sekunde kadhaa, kabla ajafunguka, nikweli kaka, unachosema kinaweza kuni tokea inabidi niwe makini, na nichukuwe tahadhari mapema, Adellaha anaishi kimara mwisho, mtaa unaitwa kichungwani, ukifika njia panda unaingia mkono wa kulia, ukitembea kama hatia hamsini tu, unaulizia kwa mama Zawadi, au mama Peter, hapo ndipo walipo panga” alieleza Philipo ambae pia alipatia Sebastian shilingi miatano, ya kuongezea nauri, wakati anaondoka zake.


Ukweli baada ya Seba kuondoka zake, alimwacha pihilipo akiwa katika mawazo mengi sana, asa akiwaza endapo kitamtokea kile kilicho mtokea Sebastian, ambae siyo tu kumsaidia Adellah, kwa hali na mali katika kipindi kigumu alichokuwa nacho, lakini pia aliwasaidia wao na watoto wao, lakini bado mke wake akashirikiana na mdogowake na jambazi, kibaka, mwizi na taperi Daniel, kuzulumu na kumwaribia maisha yake Sebastian, ambae leo ukimwona uwezi amini kuwa, ni yule kijana aliekuwa anashinda nyumbani kwake, akinywa wine kila week end, “hapana lazima nifanye kitu mapema, vinginevyo watanigeuka ata mimi” alijisemea Philipo, huku analitazama ile duka.********


Naam saa kumi jioni ndio mida ambayo Sebastian alikuwa amesimama nje ya mlango wa chumba cha nje, alichoelekezwa kuwa, alikuwa anaishi mama Samuel, mapigo ya moyo yanamwenda kasi, huku anajiuliza atawezaje kumkabili Adellah, mwanamke ambae, alimwonyesha mapenzi ya hali ya juu, lakini leo kuna kila dalili ya kuwa siyo wake.


Baada ya kuwaza kwa sekunde kadhaa Sebastian anagonga mlango, “karibuuuuu” ilisikika sauti ya kike, ambayo mala moja Sebastian aliitambua kuwa ni sauti ya Adellah, iliyofwatiwa na vishindo vyepesi, vilivyo ufwata mlango, ambao aukuwa umefungwa kabisa, ila ulifunguliwa nusu.


Naam ile Adellah anaibuka tu, akakutana uso kwa macho na Seba, akashutuka kwa nguvu na kurudi ndani haraka, “baba Sam baba, amekuja, amekuja mwenyewe” alisema Adellah kwa sauti iliyojaa uoga wa hali ya juu, huku Seba akiwa ameshaona tumbo kubwa la Adellah, ambae sasa akukuwa na kificho kuwa ni mjamzito, “mwenyewe nani wewe mbona sikuelewei?” ilisikika sauti ya kiume toka ndani, sambamba na vishindo ilivyoingia sebuleni, “yupo nje, ni seba amekuja” alisema Adellah, kwa sauti ile ile ya uoga, huku Seba, ambae licha ya kujihakikishia kuwa Adellah ni kweli alikuwa na mimba, pia alitamani kumwona huyo alie itwa baba wa mtoto wake Samuel, “sasa Seba ndie mwenye nini, labda amefwata vitu vyake” alisikika huyu mwanaume mwenye kujiamini, huku anaibukia mlangoni, ni Daniel ambae alikuwa amevaa tauro na tumbo wazi, “Seba karibu ndani” anasema Daniel huku macho yakiwa makavu kabisa, kama vile akuna kilicho tokea kati yao, huku anaufungua zaidi mlango, na hapo Sebastian, anaweza kuona vitu vyake vya ndani, alivyo nunua kwa fedha yake mwenyewe, vikiwepo pale sebuleni.


Sebastian akiwa amesimama pale mlangoni, anatoa macho kwa mshangao, anamtazama Daniel kwa macho ya kuto kuamini, “inamaana wewe ndie mime wa Adellah, na siyo kaka yake kama mlivyo niambia, na wewe ndie ulie mpa ujauzito?” aliuliza Seba kwa sauti ya mshangao na kuto kuamini, “nazani umesha juwa, ila inabidi ufahamu kuwa ata Samuel pia siyo mtoto wako, aya sasa unaweza kueleza shida yako sasa” alisema Daniel kwa sauti yenye sanifu na dharau, “kwanini ukuniambia nikuachie mke wako, na ukaamua kuniwekea bangi ofisini kwangu?” aliuliza Sebastian, ambae kukweli alikuwa anatamanimvamie Daniel na kupiga vibaya sana, ikiwezekana kukaba mpaka kumuuwa, “kilicho kuponza ni kujifanya mjanja kama ungekubari kulala na Adellah, usingiziwe mimba, basi hayoyote yasinge kutokea” alisema Daniel kwa sauti ya dharau, yani usingejuwakama ndie huyu aliekuwa analalapale stendi ya mbezi, yani ile ya dala dala ya zamani, “kwa hiyo gharama yake ni kuchukuwa kila kilicho cha kwangu?” aliuliza Sebastian kwa sauti yenye hasira, “sikia we mpumbavu, usijifanye unahasira, safari hii nitakufanyia jambo na autoenda tena Ukonga, unaenda kuzikwa kabisa, nivyema kama ukaaeleza shida yako” alisema Daniel, ambae akuonyesha dalili ya utani.


Kuona hivyo Seba, akajuwa kuwa kuwa Daniel akuwa na mchezo katika kufanya mambo ya ajabu, asa njama zinazoweza kumwingiza yeye kwenye matatizo, “nime fwata vitu vyangu, kuna vyeti…” kabla ajamaliza kuongea tayari Daniel akapaza sauti, “mke wangu, ebu mletee hicho kifurushi chake atuondolee mikosi hapa” alisema Daniel kwa sauti yaenye mchanganyiko wa dharau na ubabe, zilipita sekunde ishili na saba, kabla ya kuibuka kwa Adellah alie shika mfuko wa rambo, ulio tuna kidogo, huku tumbo lake likiwa limetangulia mbele, hali ile ilimuumiza sana Sebastian ambae alimtazama Adellah, kuanzia chini mpaka juu, japo mwanamke huyu, alikuwa na wasi wasi kidogo, lakini akuonyesha kujutia chochote, japo kwasasa alionekana kuanza kupaka kidogo, Seba akujuwa kama ni ujauzito, au dalili ya ugumu wa maisha, 


 Adellah, ambae akuweza kumtazama Sebastian usoni, alimpatia Daniel ule mfuko, na kisha akarudi nyuma kidogo, na kusikilizia kinacho ongelewa, “Adellah, kwanini huku niambia kuwa wakati ule ulikuwa mjazito” aliuliza Sebastian wakati anapokea mfuko toka kwa Daniel, lakini Adellah akujibu kitu, kama vile akuulizwa yeye, alitulia tu, safari hii akitabasamu, “Adellah aukuwa na aja ya kujilahisi namna ile ili unisingizie ujauzito, ungenieleza shda yako ningekusaidia tu, mimi ndivyo nilivyo nimesha wasaidia watu wengi sana, ebu ona, kukusaidia kwangu, umeamua kunifanye nikose uwezo wa kuwa saidia wale ambao wanaitaji msaada wangu” alisema Sebastian, aliekuwa ameshikilia mfuko wake, ambao ulionyesha wazi kuwa licha ya kuwa na nguo chache sana, na pia kulikuwa na karatasi, ambazo zilimpamoyo Seba.


Adellah nikama akuingiwa na maneno ya Seba, maana alitulia tu, huku anatabasamu kama aangalia mchezo wa kuingiza wenye vichekesho, “ila siyo mbaya Adellah, ili nisomo kwangu, umenifundisha kuwa dunia ina watu wenye tabia za kila aina” alisema Sebastian, ambae kabla ya kuondka akakumbuka jambo, “alafu kuna kitu inabidi ujuwe, kwamba nimesha kusamehe, maana ili lilisha onekana muda mrefu sana ila nililipuuzia, kwa hiyo ilikuwa lazima itokee, nazani unakumbuka siku moja kabla atujaondoka kule kwa mama, alijifungia muda mrefu sana akiwa anasali, aliniambia kuwa, anahisi aukuwa sahihi kwangu, hiki kinacho tokea leo aliwai kuona usiku wa ile, lakini naamini kwa upande wangu, limeishia hapa, maana sito kuwa mjinga wakati wakurudi” alisema Sebastian, ambae aliukagua ule mfuko na kuona kuwa, kulikuwa na nguo mbili tu, tena ni kaptula ya kaki, na tisher jepesi la kijivu, pia kulikuwa na makaratasi kadhaa, ikiwepo mkataba wake na FSC, na vyeti vyake vya shule.********


Naaaam Sebastian akiwa amesha jihakikishia kwa macho yake, na kuujuwa ukweli wote, walirudi kibamba, na kumsimulia baraka kila kitu, huku akimweleza kuwa, kwa sasa mpango wake ni kutafuta kazi, “sikia Seba wewe ni mwanaume, cha msingi achana na yale yaliyopita, we fanya kama ayajatokea, anza kupambana upya, bahati nzuri elimu unayo, unaweza kupata kazi haraka” alisema Baraka, siku iliyofuata Sebastian akiwa na matumaini ya kupata kazi, akaanza kuzunguka kwenye maofisi kutafuta kazi, huku akitoa sifa zake kuwa alisha wai kufanya kazi ya uhasibu.


Itaendelea

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.